2. Utangulizi
Katika mada za kidato cha kwanza
tumejifunza maana ya lugha.
Pia tumejifunza kuwa lugha ndio nyenzo
kuu ya mawasilianio.
Katika hayo tumeona pia kuwa lugha ina
uhusiano mkubwa sana na tamaduni za
jamii husika.
Leo tutaangalia jinsi lugha inavyotumika na
wasemaji wake wakizingitia mambo ya
msingi ya utumizi wa lugha.
Karibu.
3. Malengo
Kufikia mwisho wa somo
hili tunapaswa tuwe
tumejifunza mambo
yafuatayo;
Maana ya matumizi ya
lugha
Maana ya Muktadha
Mambo ya kuzingatia katika
matumizi ya lugha.
4. Maana ya Matumizi ya
Lugha
Matumizi ya lugha ni
hali ya kutumia lugha
kulingana na mila,
desturi na taratibu za
jamii husika.
Hii ina maana
kwamba lugha
hutumiwa na
watumiaji wake huku
wakizingatia tamaduni
za jamii yao.
5. Maana ya Muktadha
Neno muktadha lina
maana ya mazingira.
Katika matumiz ya
lugha, tunaposema
muktadha
tunamaanisha
mazingira ambapo
lugha hutumika.
Hii yuaweza kuwa;
shuleni, hospitalini au
mahakamani.
7. Uhusiano Baina ya
Wazungumzaji
Wazungumzaji huzingatia
uhusiano wao katika mazungumzo.
Kila mmoja huweka akilini mwake,
nani anazungumza naye.
Hii humsaidia mzungumzaji kuteua
misamiati mahususi na jinsi ya
kuongea.
Mfano; wewe mwanafunzi vile
unavyozungumza na mwalimu ni
tofauti na vile unavyozungumza
na mwanafunzi mwenzako.
Hapo huwa unazingatia uhusiano
baina yako na unayezungumza
naye.
Hivyo uhusiano baina ya
wazungumzaji huzingatiwa katika
matumizi ya lugha.
8. Muktadha/Mazingira
Mzungumzaji huzingatia
mazingira pale anapotumia
lugha.
Hii inamaana kuwa
mzungumzaji hujiuliza swali
kuwa niko wapi kabla hajatumia
lugha.
Wewe mwanafunzi kwa mfano,
jinsi unavyoongea unapokuwa
shuleni ni tofauti kabisa na jinsi
unavyoongea unapokuwa
kanisani au unapokuwa bwenini
au nyumbani.
Kwa hiyo; mazingira
humuelekeza mtu atumie lugha
namna gani.
9. Mada ya Mazungumzo
Mada ni jambo linalozungumziwa.
Mada ya mazungumzo
humuelekeza mtumiaji wa lugha
aina ya misamiati anayotakiwa
kutumia na namna ya kutumia
lugha.
Mfano kama mtu anazungumzia
masuala ya kisheria basi mtu
huyu hana budi kutumia misamiati
ya kisheria.
Kadharika yule anayezungumzia
,asuala ya kidini au kibiashara.
Hivyo matumizi ya lugha
huzingatia mada ya mazungumzo.
10. Lengo la Mzungumzaji/
Madhumuni
Mtu anapozungumza huwa
anakuwa na lengo fulani.
Mfano; anaweza
kuzungumza ili kuonya,
kufundisha, kufokea,
kufafanua au kusifia.
Lengo la mzungumzaji
ndilo hasa huwa
linamfanya achague aina
fulani ya misamiati na pia
jinsi atakavyoongea.
Hivyo lengo la
mzungumzaji huzingatiwa
katika matumizi ya lugha.
11. Kwa kuhitimisha
Hivyo, matumizi ya lugha hutawaliwa na ;
Mahusiano baina ya wazungumzaji (nani?)
Muktadha (wapi?)
Mada ya mazungumzo (nini?)
Madhumuni ya mazungumzo(kwa lengo
gani?)
Mambo haya yote ndio huzingatiwa katika
matumizi ya lugha kila siku.
12. Zoezi
Taja na fafanua mambo makuu manne
ambayo mzungumzaji huyazingatia
katika kuteuwa misamiati yake na
maumbo ya tungo zake.
Lugha ni kama bendera fuata upepo.
Fafanua kauli hii kwa kuonesha mambo
yanayotawala matumizi ya lugha.