UHURU WA MTUNZI
WA KAZI ZA FASIHI
MUSSA SHEKINYASHI
0714 807565
0743989829
Uhuru ni nini?
 Uhuru ni hali ya kutotawaliwa na mtu au nchi nyingine;
hali ya kufanya mambo bila kuingiliwa.
Uhuru wa mtunzi
 Ni hali ya mtunzi wa kazi ya fasihi kutunga au kuandika
kazi zake bila kushinikizwa na mtu, watu,au taasisi fulani
yenye nguvu kiuchumi, kisiasa au kiutawala.
 Profesa E.Kezilahabi(1993) anasema dhana ya uhuru wa
mwandishi wa kazi ya fasihi kifalsafa ni uwezo wa mtu
binafsi kufanya uamuzi,kujijua,kujiendesha na
kujirekebisha.
 Anaifafanua dhana ya uhuru kama ifuatavyo:
1.Uhuru wa mwandishi umo katika
utashi
 Mwandishi anayekosa utashi anakuwa mwoga na hukata
tamaa mapema au huyumbishwa kutokana na
makombora ya wahakiki na wanasiasa.
 Lakini mwandishi mwenye utashi, makombora ya
wahakiki watawala na wanasiasa humkomaza.
 Waandishi wa kiafrika wenye utashi ni Wole Soyinka wa
Nigeria na Ngugi wa Thiong’o wa Kenya.
2. Uhuru wa mwandishi upo katika
falsafa moja inayoeleweka
 Falsafa moja inayoeleweka huyafanya maandishi
yaonekane kama kazi moja yenye mwelekeo maalumu.
 Falsafa ndio kamba inayoyafanya maandishi yote ya
mwandishi yawe kazi moja na sio jina lake.
 Waandishi wa fasihi ya kiswahili waliosimama katika
falsafa moja ni Shabani Robert na E. Kezirahabi
3. Uhuru wa Mwandishi umo katika
Kuitawala Vema Sanaa Yake
 Mwandishi anayeandika aina fulani ya fasihi,kama vile
riwaya,tamthiliya au ushairi; ambayo hana ujuzi nayo hakika
kazi yake itatoka ikiwa hafifu.
 Kadhalika,mwandishi anayeshindwa kuunganisha vema
ubunifu na uhalisia kazi yake hupoteza ladha.
 Hivyo, uhuru wa mwandishi unategemea na uwezo wake wa
kushughulikia nyanja ya fasihi anayoimudu pia kuweza
kusimamia kipengele cha uhalisia na ubunifu katika viwango
sawa bila kuzidisha kimojawapo.
 Mfano wa waandishi wa kiswahili wanaozingatia haya ni
Ebrahim Husseni na Penina Muhando
4. Uhuru wa Mwandishi Umo katika
Kuitawala Lugha Anayoitumia
 Mwandishi au mtunzi wa kazi ya fasihi hawezi kuitawala
vema sanaa anayoitumia kama msingi wa lugha
anyoitumia ni mbovu.
 Lugha ndio kiungo maalum kati ya mtunzi na hadhira
anayoitungia au kuiandikia.
 Kukosekana kwa weledi katika lugha humkosesha uhuru
mwandishi au mtunzi wa kazi za kifasihi.
Historia Fupi ya Udhibiti wa Uhuru wa
Mwandishi
 Suala la udhibiti wa uhuru wa mwandishi ni la kitabaka
kwani lilianza pale tu jamii ilipogawanyika katika
matabaka mbalimbali ya watu.
 Hapa tunazungumzia jamii zilizofuata baada ya mfumo
wa kiujima; yaani utumwa,ukabaila na ubepari.
 Mara tu maandishi yalipogundulika,fasihi andishi ya
mwanzo ilikuwa ni teule kwa wachache wenye vyeo na
vyao.
 Walihakikisha kwamba kuna mbinu inatumika ikiwemo ya udhibiti wa
maandishi ili kulinda utawala wao.
 Ingawa tabaka la chini nalo lilikuwa na fasihi yao ambayo kimsingi ilikuwa
simulizi,iliyoelezea hisia zao,majonzi yao,hasira zao na matumaini yao.
 Fasihi hii pia ilishambuliwa na rungu la udhibiti hata ikakosa uhuru.
 Kutokana na maelezo hayo basi, kazi ya fasihi ni kulinda tabaka tawala.
 Tabaka tawala huhakikisha kwamba fasihi inatumiwa kueneza itikadi zake.
Mifano ya Kazi za Fasihi zilizokutana
na Udhibiti
 Mfano mzuri ni kazi za muamerika kusini Pablo Neruda
ambaye mwanzoni aliandika mashairi yake kusifia viumbe
na mazingira kwa ujumla.
 Baadae alibadilisha muelekeo akawa anaelezea dhiki za
watu wa tabaka la chini. Hapo alikutana na upinzani
mkubwa kutoka kwa wahakiki na tabaka tawala.
 Pia Ngugi wa Thion’go tamthiliya yake “I will Mary when I
want” “Nitaolewa Nitakapotaka”ilifungiwa kwa kuwa
ilikuwa inalikosoa tabaka tawala.
Uhuru wa Mwandishi wa Kazi za
Fasihi Nchini Tanzania
 Kabla ya Uhuru
 Kwa mujibu wa Senkoro (1993),hapa Tanzania udhibiti wa
uhuru wa mwandishi ulianza tangu enzi ya mkoloni.
 Udhibiti huu ulidhihirika kupitia vitabu walivyovitumia
kufundishia mashuleni ambavyo vyote vilitafsiriwa na vina
tukuza na kueneza utamaduni wao.
 Mfano wa vitabu hivyo ni kama: Mashimo ya Mfalme
Suleiman, Hadithi za Allan Quarterman ,Safari za Gulliver
na Robinson Kruso.
 Mbali ya kuwa fasihi hizo zilikuwa na lengo la kupumbaza
uwezo wa mwafrika kujitambua pia zilidhamiria
kupenyeza imani za kidini na kuua imani za dini za jadi za
watanganyika.
 Vitabu vya kihistoria vilivyotumika kufundishia mashuleni
vilikuwa vinapotosha uhalisia wa historia ya mtu mweusi
na kudai kuwa mwafrika hana historia kabisa
 Baada ya Uhuru
 Mapinduzi ya Zanzibar na Azimio la Arusha ni moja ya matukio
yaliyoshangiliwa sana nchini Tanzania baada ya uhuru.
 Fasihi andishi iliyojitokeza mara tu baada ya matukio haya ilijaa chereko
hoihoi na vifijo vya kuyashangilia.
 Kwa upande mwingine matukio hayo yalisaidia kuzichonga kalamu za
baadhi ya waandishi waliokuwa wakifuatilia utekelezaji au ukiukwaji wa
maadili ya matukio hayo kama ilivyotangazwa na wanasiasa.
 Zao la ufuatiliaji huo ni riwaya ya Rosa Mistika (1971) iliyoandikwa na
Profesa E. Kezilahabi.
 Riwaya hiyo ilipigwa marufuku isitumiwe mashuleni na isiuzwe madukani.
 Sababu,imekiuka miiko ya kijamii
 Pia, imedhalilisha kanisa katoliki kwa kutumia jina mistika
 Imewadhalilisha wanawake
 Mwaka 1974 na 1975 kamati kuu ya TANU ilifungia vitabu
vyote vya David G.Mailu wa Kenya.
 Vitabu hivyo ni;
 My Dear Bottle (1973)
 After4.30 (1973)
 Trouble (1974)
 Pia walifungia kitabu cha Mamuya “Jando na Unyago”
 Hivi vilielezwa kuwa ni vitabu vichafu havikuzingatia
maadili ya jamii.
Dhima ya uhuru wa Mwandishi
 Nia ya uhuru wa mwandishi ni kumfanya mwandishi
kuikosoa jamii au kulikosoa tabaka lolote lile
linalokwenda kinyume na utaratibu wa jamii bila matatizo.
 Mwandishi awe na falsafa inayoeleweka pamoja na utashi.
 Mwandishi awe huru kutoa mwongozo kwa jamii, kwa
kuikomboa jamii kutoka katika fikra gandamizi na za
unyonyaji.
 Kupunguza uandishi wa kikasuku
 Mwandishi awe huru kuielimisha jamii.
ASANTENI

Uhuru wa Mtunzi wa Kazi za Fasihi

  • 1.
    UHURU WA MTUNZI WAKAZI ZA FASIHI MUSSA SHEKINYASHI 0714 807565 0743989829
  • 2.
    Uhuru ni nini? Uhuru ni hali ya kutotawaliwa na mtu au nchi nyingine; hali ya kufanya mambo bila kuingiliwa.
  • 3.
    Uhuru wa mtunzi Ni hali ya mtunzi wa kazi ya fasihi kutunga au kuandika kazi zake bila kushinikizwa na mtu, watu,au taasisi fulani yenye nguvu kiuchumi, kisiasa au kiutawala.  Profesa E.Kezilahabi(1993) anasema dhana ya uhuru wa mwandishi wa kazi ya fasihi kifalsafa ni uwezo wa mtu binafsi kufanya uamuzi,kujijua,kujiendesha na kujirekebisha.  Anaifafanua dhana ya uhuru kama ifuatavyo:
  • 4.
    1.Uhuru wa mwandishiumo katika utashi  Mwandishi anayekosa utashi anakuwa mwoga na hukata tamaa mapema au huyumbishwa kutokana na makombora ya wahakiki na wanasiasa.  Lakini mwandishi mwenye utashi, makombora ya wahakiki watawala na wanasiasa humkomaza.  Waandishi wa kiafrika wenye utashi ni Wole Soyinka wa Nigeria na Ngugi wa Thiong’o wa Kenya.
  • 5.
    2. Uhuru wamwandishi upo katika falsafa moja inayoeleweka  Falsafa moja inayoeleweka huyafanya maandishi yaonekane kama kazi moja yenye mwelekeo maalumu.  Falsafa ndio kamba inayoyafanya maandishi yote ya mwandishi yawe kazi moja na sio jina lake.  Waandishi wa fasihi ya kiswahili waliosimama katika falsafa moja ni Shabani Robert na E. Kezirahabi
  • 6.
    3. Uhuru waMwandishi umo katika Kuitawala Vema Sanaa Yake  Mwandishi anayeandika aina fulani ya fasihi,kama vile riwaya,tamthiliya au ushairi; ambayo hana ujuzi nayo hakika kazi yake itatoka ikiwa hafifu.  Kadhalika,mwandishi anayeshindwa kuunganisha vema ubunifu na uhalisia kazi yake hupoteza ladha.  Hivyo, uhuru wa mwandishi unategemea na uwezo wake wa kushughulikia nyanja ya fasihi anayoimudu pia kuweza kusimamia kipengele cha uhalisia na ubunifu katika viwango sawa bila kuzidisha kimojawapo.  Mfano wa waandishi wa kiswahili wanaozingatia haya ni Ebrahim Husseni na Penina Muhando
  • 7.
    4. Uhuru waMwandishi Umo katika Kuitawala Lugha Anayoitumia  Mwandishi au mtunzi wa kazi ya fasihi hawezi kuitawala vema sanaa anayoitumia kama msingi wa lugha anyoitumia ni mbovu.  Lugha ndio kiungo maalum kati ya mtunzi na hadhira anayoitungia au kuiandikia.  Kukosekana kwa weledi katika lugha humkosesha uhuru mwandishi au mtunzi wa kazi za kifasihi.
  • 8.
    Historia Fupi yaUdhibiti wa Uhuru wa Mwandishi  Suala la udhibiti wa uhuru wa mwandishi ni la kitabaka kwani lilianza pale tu jamii ilipogawanyika katika matabaka mbalimbali ya watu.  Hapa tunazungumzia jamii zilizofuata baada ya mfumo wa kiujima; yaani utumwa,ukabaila na ubepari.  Mara tu maandishi yalipogundulika,fasihi andishi ya mwanzo ilikuwa ni teule kwa wachache wenye vyeo na vyao.
  • 9.
     Walihakikisha kwambakuna mbinu inatumika ikiwemo ya udhibiti wa maandishi ili kulinda utawala wao.  Ingawa tabaka la chini nalo lilikuwa na fasihi yao ambayo kimsingi ilikuwa simulizi,iliyoelezea hisia zao,majonzi yao,hasira zao na matumaini yao.  Fasihi hii pia ilishambuliwa na rungu la udhibiti hata ikakosa uhuru.  Kutokana na maelezo hayo basi, kazi ya fasihi ni kulinda tabaka tawala.  Tabaka tawala huhakikisha kwamba fasihi inatumiwa kueneza itikadi zake.
  • 10.
    Mifano ya Kaziza Fasihi zilizokutana na Udhibiti  Mfano mzuri ni kazi za muamerika kusini Pablo Neruda ambaye mwanzoni aliandika mashairi yake kusifia viumbe na mazingira kwa ujumla.  Baadae alibadilisha muelekeo akawa anaelezea dhiki za watu wa tabaka la chini. Hapo alikutana na upinzani mkubwa kutoka kwa wahakiki na tabaka tawala.  Pia Ngugi wa Thion’go tamthiliya yake “I will Mary when I want” “Nitaolewa Nitakapotaka”ilifungiwa kwa kuwa ilikuwa inalikosoa tabaka tawala.
  • 11.
    Uhuru wa Mwandishiwa Kazi za Fasihi Nchini Tanzania  Kabla ya Uhuru  Kwa mujibu wa Senkoro (1993),hapa Tanzania udhibiti wa uhuru wa mwandishi ulianza tangu enzi ya mkoloni.  Udhibiti huu ulidhihirika kupitia vitabu walivyovitumia kufundishia mashuleni ambavyo vyote vilitafsiriwa na vina tukuza na kueneza utamaduni wao.  Mfano wa vitabu hivyo ni kama: Mashimo ya Mfalme Suleiman, Hadithi za Allan Quarterman ,Safari za Gulliver na Robinson Kruso.
  • 12.
     Mbali yakuwa fasihi hizo zilikuwa na lengo la kupumbaza uwezo wa mwafrika kujitambua pia zilidhamiria kupenyeza imani za kidini na kuua imani za dini za jadi za watanganyika.  Vitabu vya kihistoria vilivyotumika kufundishia mashuleni vilikuwa vinapotosha uhalisia wa historia ya mtu mweusi na kudai kuwa mwafrika hana historia kabisa
  • 13.
     Baada yaUhuru  Mapinduzi ya Zanzibar na Azimio la Arusha ni moja ya matukio yaliyoshangiliwa sana nchini Tanzania baada ya uhuru.  Fasihi andishi iliyojitokeza mara tu baada ya matukio haya ilijaa chereko hoihoi na vifijo vya kuyashangilia.  Kwa upande mwingine matukio hayo yalisaidia kuzichonga kalamu za baadhi ya waandishi waliokuwa wakifuatilia utekelezaji au ukiukwaji wa maadili ya matukio hayo kama ilivyotangazwa na wanasiasa.
  • 14.
     Zao laufuatiliaji huo ni riwaya ya Rosa Mistika (1971) iliyoandikwa na Profesa E. Kezilahabi.  Riwaya hiyo ilipigwa marufuku isitumiwe mashuleni na isiuzwe madukani.  Sababu,imekiuka miiko ya kijamii  Pia, imedhalilisha kanisa katoliki kwa kutumia jina mistika  Imewadhalilisha wanawake
  • 15.
     Mwaka 1974na 1975 kamati kuu ya TANU ilifungia vitabu vyote vya David G.Mailu wa Kenya.  Vitabu hivyo ni;  My Dear Bottle (1973)  After4.30 (1973)  Trouble (1974)  Pia walifungia kitabu cha Mamuya “Jando na Unyago”  Hivi vilielezwa kuwa ni vitabu vichafu havikuzingatia maadili ya jamii.
  • 16.
    Dhima ya uhuruwa Mwandishi  Nia ya uhuru wa mwandishi ni kumfanya mwandishi kuikosoa jamii au kulikosoa tabaka lolote lile linalokwenda kinyume na utaratibu wa jamii bila matatizo.  Mwandishi awe na falsafa inayoeleweka pamoja na utashi.  Mwandishi awe huru kutoa mwongozo kwa jamii, kwa kuikomboa jamii kutoka katika fikra gandamizi na za unyonyaji.
  • 17.
     Kupunguza uandishiwa kikasuku  Mwandishi awe huru kuielimisha jamii.
  • 18.