Sarufi Matamshi (Fonolojia). Hii ni sehemu ya mada ndogo katika mada kuu ya Matumizi ya Sarufi kwa kidato cha Tano na Sita nchini Tanzania. Jisikie huru kutoa maoni yako na ushauri. Nitafurahi kama ukinipigia simu au ukinitumia barua pepe kunikosoa au kunirekebisha pale nilipokosea. Asante na karibu sana.
2. Fonolojia ni nini?
Ni tawi la sarufi linalojishughulisha na uchunguzi,
uchanganuzi na uanishaji wa sauti pambanuzi za
lugha .
Kwa maelezo mengine, fonolojia hujihusisha na
utaratibu wa mpangilio wa vitamkwa katika
maneno ya lugha.
Fonolojia kwa upana wake pia hujishughulisha na
vipengele kama: matamshi, kiimbo, mkazo,
lafudhi, toni, mfuatano wa sauti katika kuunda
mofimu, mfuatano katika kuunda neno na
otografia.
3. Sauti katika Lugha
Katika lugha ya kiswahili kuna sauti za aina
mbili. Ambazo ni;
Sauti Irabu
Sauti Konsonanti
4. Sauti Irabu
Ni sauti zinazotamkwa bila kuwepo kizuizi
katika mkondo wa hewa utokao mapafuni
kwenda nje kupitia chemba ya kinywa na
pua.
Kiswahili sanifu kina irabu tano (5)
Ambazo ni: /a/, /e/,/i/,/o/ na /u/
5. Vigezo vinavyotumika kuainisha
irabu
Irabu huweza kutofautishwa na kuanishwa
kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo:
Sehemu ya ulimi ya kutamkia
Mwinuko wa ulimi
Mkao wa mdomo
6.
7. Irabu za mbele
Irabu hizi hutamkwa katika sehemu ya mbele
ya ulimi.
9. Irabu za kati
Hizi hutamkiwa sehemu ya kati ya ulimi. Irabu
ya kati ni moja tu, /a/
10. 2. Mwinuko wa Ulimi
Katika kigezo hiki tunazingatia kiasi cha
kuinuka kwa ulimi wakati wa kuzitamka irabu.
Kwa kuzingatia kigezo hiki tuna:
Irabu za juu
Irabu za kati
Irabu za chini
12. Irabu za Kati
Hutamkwa ulimi ukiwa umeinuliwa wastani; si
chini wala juu). Irabu hizo ni /e/ na /o/.
13. Irabu ya Chini
Hutamkwa irabu ikiwa chini kinywani. Irabu ya
chini ni moja tu. /a/
14. 3. Mkao wa Mdomo
Hapa tunachunguza jinsi midomo ilivyo wakati
wa kuzitamka sauti.
Kwa kuzingatia kigezo hiki tunapata:
Irabu viringwa (mviringo)
Irabu tandazwa
19. Konsonanti
Ni sauti zinazo tamkwa kwa kuzuia mkondo
wa hewa katika sehemu mbalimbali kinywani
hasa kwa kutumia ulimi.
Konsonanti za kiswahili huainishwa kwa
kuzingatia vigezo vifuatavyo:
Mahala pa kutamkia
Namna ya kutamka
Mtetemo au mtikisiko wa nyuzi sauti
20. Mahala pa Kutamkia
Konsonanti za kiswahili hutamkwa katika
sehemu mbalimbali.
Sehemu hizo ni kama zifuatazo:
21. midomo
Sauti hizi hutamkwa mdomo wa juu
unapokutana na mdomo wa chini.
Sauti hizi ni:
/p/
/b/
/m/ na
/w/
22. Silabi
Ni sehemu ya neno ambayo hutamkwa mara moja au
kwa pamoja kama fungu moja la sauti.
Fungu hilo linaweza kuwa na sauti mbili au zaidi,
inategemea muundo wa lugha inayohusika
Muundo wa silabi wa lugha yoyote ile hutawaliwa na
kanuni za kifonolojia za lugha husika.
Kanuni za kifonolojia za lugha ndizo huelekeza:
Ni vipashio vipi vinavyoweza kujenga silabi
Kwa mfuatano au mpangilio wa namna gani
Ni vipashio vipi haviwezi kujenga silabi
23. Silabi ya kiswahili
Silabi ya kiswahili huundwa kwa kufuata
taratibu maalumu za lugha ya kiswahili
Mfuatano wa sauti za kiswahili unaruhusu tu
konsonanti za aina fulani kufuatana kwa idadi
na kwa mpangilio maalumu katika silabi.
Kila mzungumzaji wa lugha ya kuswahili
anaumilisi wa kuweza kutunga na kutumia
kanuni hizi kuunda maneno.
24. Aina za Silabi
Kuna aina mbili za silabi zakiswahili:
Silabi Huru (wazi)
Silabu Funge
25. Silabi Huru (wazi)
Ni silabi ambazo huishia na irabu, sauti
amabazo zina msikiko au mvumo wa juu.
Kutokana na kuishia na irabu, silabi huru
huwa zinakuwa na msikiko mkubwa zaidi.
Mfano: ba - ba
1 2
26. Konsonanti ng’ong’o
Konsonanti hizi ni kama vile /m/,/n/,/ng’/ na
/ny/.
Konsonanti hizi huweza kutamkwa katika
neno bila msaada wa irabu.
Konsonanti hizi huweza kusimama peke yake
kama silabi.
Mfano: neno mwanamke lina silabi nne:
Mwa-na-m-ke
27. Silabi Funge
Silabi funge ni salbi zinazoishia na
konsonanti,sauti ambazo kwa kawaida zinakuwa
na msikiko au mvumo hafifu.
Lugha ya kiswahili ikikopa maneno kutoka lugha
za kigeni kama vile kiarabu baadhi ya maneno
yake yanakuwa na silabi funge:
Mfano: maktaba,madrasa,
Kwenye kingereza neno kama: cut, car na push
28. Miundo ya Silabi Asilia ya
Kiswahili Sanifu
Tunaposema silabi asilia za kiswahili tuna
maana ya silabi zinazopatikana katika
maneno asiliaya lugha hiyo.
Lugha ya kiswahili ina miundo isiyopungua
mitano (5) ya irabu.
miundo hiyo ni kama ifuatayo:
29. 1. Irabu Pekee (I)
Kiswahili kina irabu tano (5) ambazo kila
moja huweza kuwa silabi katika miundo ya
maneno mbalimbali.
Mfano: ua:u-a
Oa : o-a
okoa: o-k-o-a
30. 2. Silabi ya Konsonanti pekee (k)
Hizi ni zile konsonanti ambazo huweza
kutamkwa bila msaada wa irabu.
Konsonanti hizi huweza kuwa silabi.
Hii ni kwa sababu konsonanti hizi zinausilabi
mkubwa kiasi cha kuweza kutamkika.
Konsonanti hizi ni ving’ong’o
Konsonanti hizi ni kama vile /m/,/n/,/ng’/ na
/ny/.
31. 3. Silabi za konsonati na irabu
(KI)
Huu ni muundo unaotumika sana katika lugha
sio tu ya kiswahili bali pia katika lugha
nyingine za kibantu.
Lugha nyingi ulimwenguni hutumia muundo
huu.
Mfano: kaka: ka-ka
lima : li-ma
32. 4. Siabi za konsonanti,konsonanti
na irabu (KKI)
Mafano
Pwani : pwa-ni
Kwisha : Kwi –sha
35. Lafudhi
Ni matamshi ya mseamji wa lugha fulani ambayo
yanatokana na athari za kimazingira.
Mazingira hayo yanaweza kuwa mahali alipotoka,
kiwango cha elimu na kadhalika.
Hii inamaana kwamba kutokanan na jinsi
mzungumzaji anavyoimudu sauti yake tunaweza
kujua kujua mahali atokako.
Lugha ya kwanza ya jamii atokayo mzungumzaji
inaweza kuathiri lafudhi ya mzungumzaji.
36. Mfano
Bwana wew, ntu alokanichilimisha aje
anchilimue…!
Nkuu wa nkoa wa ntwara n’jini kanipa
nchongo wa kusuka nkeka nipeleke nsanga
nkuu.
Ukisikia sauti ya mzungumzaji huyu utajua tu
anatokea mazingira gani au katika jamii gani.
37. Mkazo/ Shadda
Ni sifa ya kiarudhi ambapo sehemu Fulani ya
neno, aghalabu silabi hutamkwa kwa nguvu
au kwa kuvuta ili kwamba isikike au isistizwe
zaidi kuliko sehemu nyingine za neno au
sentensi.
Mfano:
Barabara (njia)
Barabara (sawasawa)
Mkazo hutumiwa kutofautisha maana za
maneno au kuonesha msisitizo wa jambo
katika sentensi.
38. Katika lugha ya Kiswahili mkazo huweza kuwekwa
katika kiwango cha neno au sentensi.
Mfano wa mkazo katika sentensi:
Walikuja kwa kasi ya ajabu.
Kazi waliyofanya ni kidogo sana.
Katika kiwango cha neno mkazo huwekwa katika
silabi ya pili kutoka mwisho:
Mfano: Watatu , walakini na walakini.
Mkazo katika sentensi huwekwa ili kudhihirisha
wazo linalotaka kusisitizwa.
Mkazo katika kiwango cha neno huwekwa kujenga
maana fulani.
39. Kiimbo
Ni hali ya kupanda na kushuka kwa sauti wakati
wa kutamka maneno mbalimbali katika sentensi.
Kiimbo pia kinaweza kufafanuliwa kama sauti
maalum inayojitokeza unapotamka maneno fulani.
Kiimbo husaidia kuleta maana kamili ya sentensi
iliyokusudiwa.
Katika uandishi, Viimbo husaidiwa na alama za
uakifishaji (uandishi) ili kumwelekeza msomaji
asome kwa kiimbo kilichokusudiwa.
40. Ruwaza za kiimbo
Hii ni mipangilio au mgawanyo wa viimbo
kulingana na maana vinazotoa.
Ruwaza hizi hubadilika kulingana na dhima ya
kauli za sentensi husika.
Katika sentensi ya taarifa, sauti huwa na kiimbo
sawa pasi na kupanda na kushuka.
Juma amekwenda
Katika sentensi ya swali, sauti huanzia chini kisha
hupanda na kufikia silabi pili kutoka mwisho.
Juma amekwenda?
Katika sentensi ya mshangao sauti huanzia chini
kisha hupanda na kufikia silabi ya mwisho.
Juma amekwenda?