Karibu
Huu ni uwasilishaji wa nadharia ya Pijini na Krioli. Kwa upande mwingine uwasilishaji huu unatathimini asili ya kiswahili katika mrejeo wa nadharia hii.
Mahususi kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita.
3. 1. pijini
Pijini ni zao la lugha mbili zilizokutana.
Pijini huweza kuzuka mahala ambapo kuna makundi
mawili au zaidi na kila kundi likiwa na lugha yake.
Ili kurahisisha mawasilano lugha hizi huchanganyika na
kuingiliana.
Jambo hili huweza kusababisha kuzuka kwa lugha ya
mchanganyiko ambayo inaeleweka na makundi yote
mawili.
Hivyo pijini huwapa watu uwezo wa kuwasiliana.
4. Sifa za Pijini
Huundwa baada ya muingiliano wa lugha mbili tofauti.
Haina mzungumzaji mzawa, kila mtu huwa na lugha
mama (lugha ya kwanza)
Huibuka kukidhi mahitaji maalum, kama biashara
Muundo wa maneno na tungo vimerahisishwa ili
kuwezesha mawasiliano.
Haina misamiati ya kutosha
Pijini ikikomaa na ikapata wazungumzaji wazawa huitwa
Krioli.
5. Aina za pijini
Loreto Todd anapambanua aina mbili za Pijini;
i.Pijini pana
ii.Pijini finyu
6. Pijinifinyu
Hii ni aina ya pijini ambayo huibuka katika muktadha wa
dharura sana baina ya jamii za watu wanaoongea lugha
mbili tofauti.
Huwa na miundo sahili, hasa ya kisintaksia. Aghalabu
huambatisha ishara za kimwili kama macho, mikono na
viungo vingine vya mwili.
Idadi kubwa ya misamiati hutoka kwenye lugha tawala.
Huhusisha lugha mbili tu, na uhusiano baina ya jamii
zenye lugha hizo unapokwisha, basi pijini hufa
7. pijinipana
Aina hii ya pijini huibuka kutokana na kudumishwa kwa
pijini.
Matumizi ya pijini finyu yanapoimarika na kupanuka
hujenga lugha ambayo si thabiti lakini ni bora zaidi ya
pijinifinyu.
Pijinipana ikipata wazungumzaji wazawa,basi huwa
krioli.
8. Wataalamu kama; Bishop Steere, Bwana Taylor na Dkt.R. Reusch
wanadai kuwa lugha ya kiswahili ilitokana na mchanganyiko wa
lugha za Kiarabu na lugha za pwani ya Afrika Mashariki.
Madai yanayotolewa na wataalamu hao ni kwamba kwa kipindi cha
karne nyingi wafanyabiashara wa kiarabu walikuwa wanakuja
Afrika Mashariki kufanya biashara.
Katika kuendesha biashara zao ilibidi wenyeji wa pwani na hao
waarabu waunde namna fulani ya lugha ili waweze kuwasiliana.
Lugha ambayo inajumuisha lugha zao zote; kiarabu na Lugha ya
kibantu.
Lugha hiyo ndio kiswahili.
9. Krioli
Ni Pijini iliyokomaa.
Watu wanaozungumza pijini wanaweza kuishi pamoja
wakazoeana na kuoana, kisha wakazaa watoto.
Watoto wakakuta pijini ikizungumzwa kama lugha ya
wazazi wao.
Kwao hao watoto hii itakuwa lugha ya kwanza.
Ikifika hatua hii, lugha hii huitwa krioli.
10. Sifa za krioli
Huwa na msamiati mipana.
Huwa na miundo mipana ya kisintaksia na kimofolojia.
Wakati mwingine fonolojia yake inaanza kuwa thabiti
kutokana na upanuzi wa matumizi yake na dhima yake
katika jamii.
Huwa na wasemaji wengi zaidi ya Pijini. Hii ni kwa
sababu krioli ina wasemaji wazawa.
Inakuwa imewekwa kwenye maandishi mbalimbali kama
vile vitabu na majarida.
Hufanyiwa uchambuzi katika luwaza zote; mofolojia,
fonolojia, sintaksia na semantiki.
11. Baadhi ya wataalamu hudai kuwa kiswahili ni lugha ya jamii ya
vizalia waliotokana na mwingiliano kati ya waarabu na wabantu.
Kutokana na mwingiliano huu kulizaliwa watoto ambao ni
mchanganyiko wa damu.
Watoto hao ndio waswahili,hawa hawakuwa waarabu wala
wabantu.
Wataalamu wanaounga mkono nadharia hii ni F. Johnson,
Freeman Genville,Hamo Sassoon na B. Krumm.
Wao wanadai kuwa kiswahili ni Pijini iliyopata kukomaa, ikapata
vizalia na kupindukia kuwa krioli.
12. Udhaifu/dosari ya mtazamo huu
Mtazamo huu umeshindwa kuitaja kinaganaga hiyo lugha ya
kibantu iliyochangamana na Kiarabu kuunda Kiswahili. Na kama ipo
ndio Kiswahili chenyewe.
Mtazamo huu umesisitiza zaidi juu ya msamiati wa kiswahili wenye
asili ya kiarabu kama kigezo chake na kutupilia mbali vipengele
kama vile matamshi,maumbo na miundo ya sentensi.
Kiswahili kingekuwa pijini au krioli inayotokana na lugha ya kibantu
na kiarabu, basi sintaksia yake ingefanana na ile ya kiarabu
13. Pia, kama Kiswahili kingekuwa ni zao la uchangamano wa Kiarabu
na lugha ya Kibantu basi asilimia hamsini ya misamiati ya kiswahili
ingekuwa na asili ya kiarabu.
Tofauti na ilivyo ambapo:
Msamiati wa kibantu- 60%
Msamiati wa Kiarabu-30%
Lugha nyingine -10%
Tukizingatia yote haya, tunaona kwamba hatuna sababu ya
kutushawishi kukubaliana na nadhariatete hii.
Kiswahili kinabaki kuwa ni lugha yenye asili ya Kibantu
14. Marejeleo
Massamba.D.P,Kihore et al (2012)Sarufi Miundo ya
Kiswahili Sanifu: Sekondari na Vyuo. TUKI. DUP. Dar es
Salaam
Masuko. C.S (2010)Kiswahili 1;Nadharia ya lugha kidato
cha tano na sita. STC publishers. Dar es Salaam.
Nyambari.N & Masebo .J.A (2012) Nadharia ya Lugha:
Kiswahili 1. Nyambari Nyangwine Publishers. Dar es
Salaam.
James.J &Mdunda F (2012)Kiswahili Kidatocha Tano na
Sita. Oxford University Press. Dar es salaam.