Mada ya Mjengo wa Tung ni moja kati kati ya mada yenye changamoto miongoni mwa wanfunzi wa kidato cha tatu.
Hapa mwanafunzi atapata fursa ya kujikumbusha aliyojifunza na mwalimu darasani.
asante.
2. Tungo
Neno tungo ni nomino ambayo hutokana na kitenzi tunga
ambacho kinamaana ya kushikanisha vitu.
Jambo la msingi hapa ni kufahamu kwamba tunapotunga
vitu huwatunapata kitu kinachoitwa utungo.
Katika taaluma ya sarufi neno tungo linamaana takribani
sawa na hiyo.
Ambapo tungo katika sarufi ni kuweka pamoja na kupanga
vipashio sahili ili kujenga vipashio vikubwa zaidi,
4. Tungo Neno
Tungo yoyote huundwa na vijenzi.
Vijenzi vya tungo neno katika lugha ya kiswahili ni
vitamkwa,silabi na mofimu.
Vitamkwa hujenga silabi, silabi hujenga mofimu na mofimu
hujenga tungo-neno.
Kwa mchakato huu tunapata aina nane za maneno, ambazo
ni:
Nomino,Vitenzi,Vielezi,Vivumishi,Viunganishi,Vihusishi,Viwak
ilishi na Viingizi.
5. Tungo-Kirai
Ni tungo isiyo na muundo wa kiima na kiarifu. AU
Ni neno au kundi la maneno katika mpangilio maalum
linalofanya kazi moja kisintaksia katika sentensi.
AU
Ni neno au maneno mawili au zaidi ambayo huwekwa
pamoja katika mpangilio maalum unaozingatia uhusiano
uliopo baina ya neno-kuu na maneno mengine.
6. Zingatia Mfano ufuatao…
Mtoto yule
Mtoto yule mzuri
Mtoto yule mnene kuliko wote
Mzee huyu mjanja
Mwalimu yule mwembamba
Mifano yote iliyotolewa hapo juu ni mifano ya tungo-virai ambazo zimekitwa
katika neno-kuu ambalo ni nomino.
Maneno yaliyoandikwa kwa hati ya kulala ndio chimbuko la kazi ya kirai
hicho katika sentensi
Hivyo tungo hizo ni Kirai-nomino
7. Sifa za kirai
Hikina muundo wa kiima na kiarifu
Lakini huweza kukaa katika upande wowote; wa kiima au
kiarifu.
Uainishaji (kujua aina ya kirai) unategemea mahusiano ya
maneno katika fungu hilo la maneno.
Kirai hujengwa na neno moja au zaidi ya moja.
8. Virai vya Kiswahili
Katika lugha ya kiswahili kuna aina za virai zifuatazo:
Kirai-nomino
Kirai –kielezi
Kirai-kitenzi
Kirai-kivumishi
Kirai –kiunganishi
9. Kirai Nomino
Tungo kirai nomino kinaweza kuwa na moja ya miundo
ifuatayo:
Nomino Pekee: Happy anasoma
Nomino zaidi ya moja: Hapy na Abriel wanasoma
Kiwakilishi Pekee: Sisi ni watanzania
Kiwakilishi na kivumishi: Sisi sote tumefaulu
Nomino moja na Kivumishi:Mtoto mzuri anaoga
Nomino na kishazi Tegemezi: Mbuzi aliyevunjia pembe
amechinjwa
10. Kirai Kielezi
Ni neno au fungu la maneno ambalo linatupatia taarifa zaidi
kuhusu tendo.
Kimsingi kirai kielezi kinajibu maswali kwamba tendo kwenye
sentensi:
Limefanyika wapi?
Limefanyikaje?
Limefanyika lini?
Mara ngapi?
Namna gani?
Kirai kielezi huweza kukaa mahala popote ingawa watumizi
wengi wa kiswahili hupenda kuweka kirai kielezi baada ya
kitenzi.
11. Mifano ya Kirai Kielezi
Abriel anacheza mpira vizuri sana
Babu husafiri kila siku
Mama atakuja kesho saa mbili
Happy anatembea haraka sana.
12. Kirai Kitenzi
Ni neno au kifungu cha maneno ambacho neno kuu ni kitenzi.
Kirai kitenzi huundwa na maneno yafuatayo:
Kitenzi Kikuu Pekee( T ):
Mfano; Abriel analia
Happy na Abby wanakimbia
Kitenzi Kisaidizi na Kitenzi Kikuu (Ts+T):
Mfano:Oscar alikuwa anaimba
Philemoni anapenda kuimba
13. Kitenzi kishirikishi (t):
Mara nyingi kitenzi kishirishi hufuatwa na KN cha pili katika
sentensi ambacho huitwa Shamirisho:
Mfano; Josia ni mwanafunzi
Asha alikuwa mgonjwa
Kalii yu mahututi
14. Kirai Kivumishi
Ni neno au kifungu cha maneno chenye kivumishi kama
neno kuu.
Mara nyingi kirai kivumishi huhusishwa kwenye kirai
nomino.
Chunguza mifano ifuatayo:
Beberu mwenye ndevu ndefu sana amerudi
Kibaka aliyekamatwa jana jioni ametoroka.
Katika mfano hiyo hapo juumaneno yalitokolezwa wino ndio
virai vivumishi.
15. Kirai Kiunganishi
Ni neno au kifungu cha maneno kinachohusisha tungo mbili
zenye hadhi sawa.
Baadhi ya maneno ambayo huunda kirai kiunganishi ni
pamoja na: kwa,na,pia,vilevile,lakini,ingawa,aidha n.k
Mfano:
16. Tungo-Kishazi
Ni aina ya tungo ambayo muundo wake unajumuisha kitenzi
ndani yake.
Kishazi ni tungo kubwa kuliko kirai na ndogo kuliko sentensi.
Kishazi kinaweza kutoa maana kamili au isiyokamili. Tazama
sentensi hii:
Ng’ombe aliyevunjika mguu amerudi zizini.
Maneno yaliyo katika hati ya kulaza ni kishazi, lakini yakisimama
pekee hayatoi maana kamili.
Maneno yaliyokolezwa wino ni kishazi na yanaweza kusimama
pekee na kutoa maana.
Hapo ndio tunapata aina za vishazi.
17. Aina za Vishazi
Kuna aina mbili za Vishazi
Vishazi Huru
Vishazi
Tegemezi
18. Kishazi Huru
Ni aina ya kishazi ambavyo hutoa taarifa kamili.
Aina hii ya vishazi hujengwa na kitenzi kinachojitosheleza
kimaana.
Kishazi huru huundwa na:
Kitenzi kikuu kimoja: mfano ;Amekuja
Kitenzi kisaidizi na kitenzi kikuu: mfano; Alikuwa
anaimba wimbo
Alikuwa anataka kuimba wimbo
Kitenzi Kishirishi: mfano; Juma ni mkulima
19. Kishazi Tegemezi
Hii ni aina ya vishazi ambavyo hutoa taarifa isiyokamili.
Ili vishazi hivi tegemezi viweze kutoa taarifa iliyo kamili
vinahitaji vishazi huru kukamilisha taarifa.
Mfano
Mwanafunzi aliyefaulu
Msichana aliyeolewa jana
Mzee aliyekuja jana
20. Sifa za kishazi tegemezi
Hakijitoshelezi kimaana
Kitenzi kisaidizi kilichomo kwenye kishazi tegemezi hubeba
viambishi virejeshi.
Mfano: aliyekimbia, walioimba, walichokikimbia.
Huweza kusimama kama kiima katika sentensi changamano
Kijana aliyekimbilia mjini mwaka jana
amerudi jana
Kitenzi kisaidizi kilichomo kwenye kishazi tegemezi hufanya
kazi ya kuvumisha nomino au kielezi.
21. Aina za vishazi tegemezi
Kishazi Tegemezi Vumishi (βV)
Hivi huvumisha jina lililoko katika tungo.
mfano: mtoto aliyekuja jana anaumwa.
Kishazi Tegemezi Kielezi (βE)
Hivi hutoa maelezo zaidi kwa kitenzi kilicho katika tungo.
Chakula kililiwa kilipoiva.