2. Dhana ya Tafsiri
Tafsiri ni mchakato wa uhawilishajiwa mawazo
katika maandishi kutoka lugha moja hadi
nyingine.
Kufasiri ni kuchukua mawazo yaliyo katika
maandishi kutoka lugha moja (lugha chanzi) na
kuweka badala yake mawazo yaliyolingana
kutoka lugha nyingine (lugha lengwa).
Mfasiri ni mtu anayefanya kazi ya kufasiri matini.
Tafsiri huzingatia mawazo kati ya lugha chanzi
na lugha lengwa kuwiana.
5. Mfasiri lazima azifahamu lugha zote mbili kwa
kina.
Mfasiri hana budi kufahamu kwa kina lugha zote mbili
anazozifanyia kazi.
Yaani lugha chanzi na lugha lengwa.
Umahiri huu anaotakiwa kuwa nao mfasiri
unajumuisha kuufahamu msamiati kwa kina na
kuzifahamu sheria za lugha zote mbili kwa kina.
Pia, mfasiri hana budi kuzifahamu mbinu mbalimbali
za matumizi ya lugha kulingana na mazingira au
muktadha.
6. Mfasiri ajue misingi ya kazi ya tafsiri
Ni sharti mtenda kazi yoyote ajue misingi ya kazi
ietendayo kabla hajaifanya.
Kadharika, mfasiri ni sharti ajue misingi ya kinadharia
ya kazi ya utafsiri.
Hii humpa nafasi mfasiri kujua ni aina gani ya fasiri
anaitumia kulingana na mahitaji ya hadhira yake.
Kukosekana kwa ufahamu juu ya misingi ya tafsiri
hupunguza mantiki ya matini iliyotafsiriwa.
7. Mfasiri awe mweledi
Mfasiri ili awe mahiri katika shughuli za utafsiri hana
budi kuwa na upeo mpana katika nyanja zote za
maisha: kiuchumi, kisiasa, tiba, sayansi na kijamii.
Ni vyema basi, akawa na tabia ya kuyafuatilia masuala
haya kwa jinsi yanavyotokea duniani.
Ujuzi huu utamwezesha mfasiri kuwa na msamiati wa
kutosha katika shughuli zake za kutafsiri.
8. Mfasiri afahamu kiwango cha uelewa cha
wasomaji anaowatafsiria
Kufahamu lugha zote mbili vizuri haitoshi kumfanya
mfasiri kuwa mahiri.
Pamoja na yote hayo ni sharti mfasiri awe na uwezo wa
kufahamu kiwango cha uelewa cha wasikilizaji na
wasomaji wake.
Hii itamwezesha kufasiri matini kutoka lugha chanzi
kuja lugha lengwa kwa kutumia msamiati wenye
uwiano na uelewa wa wasikilizaji.
9.
10. Kuisoma Matini Nzima
Jambo la msingi analopaswa kulizingatia mfasiri ni
kuisoma matini nzima kwa kina.
Kuisoma matini kutamuwezesha mfasiri, kwanza;
kuelewa maudhui ya matini chanzi.
Pia, humsaidia mfasiri kuandaa marejeleo
yatakayomwezesha mfasiri kuandaa kamusi
mahususi, orodha ya misamiati mipya na orodha ya
istilahi ghafi.
Hurahisisha pia, maafikiano baina ya wafasiri wawili
wanaofanyia kazi maini moja.
11. Kubaini Lengo la Matini
Kabla ya kuanza mchakato wa kufasiri matini ni
vyema mfasiri akafahamu lengo la matini chanzi.
Mara nyingine ufinyu wa uelewa wa lengo la matini
chanzi hupelekea kupotoshwa kwa lengo hilo katika
matini lengwa.
Kwa namna nyingine, mfasiri anapobaini lengo la
matini chanzi huweza kufasiri kwa namna aionayo ni
sahihi na kwa lengo analolipendekeza.
12. Kubaini Lengo la Mfasiri
Ni sharti mfasiri ajue lengo lake la msingi la katika
matini anayoifanyia kazi.
Je, lengo lake ni kuwapa wasomaji wake athari
inayolingana na ile ya matini chanzi?
Mara nyingine mfasiri hubali lengo la matini kwa
kunuia athari tofauti kwa wasomaji wake wa matini
lengwa.
Lengo la mfasiri huzingatia pia kiwango cha uelewa
cha wasomaji wa matini lengwa.
13. Kubaini Wasomaji wa Matini
Lengwa
Mfasiri anapaswa ajiulize maswali haya:
Hadhira ya matini chanzi ni ipi?
Je, msomaji wa matini yake lengwa ni yupi?
Ana elimu, umri na jinsia gani?
Haya ni baadhi ya maswali yambayo yatamsaidia
mfasiri kutafsiri matini huku akifahamu ni kwa kiasi
gani matini yake itapokelewa na kueleweka na
msomaji wa lugha lengwa.
14. Kubaini Mtindo wa Matini Chanzi
Kufahamu mtindo uliotumika kuiandika matini
chanzi ni muhimu kwa mfasiri.
Ni vyema afahamu kama matini chanzi imeandikwa
kifasihi, kirasmi au kitaaluma.
Kwa kufahamu hilo kutamsaidia kufahamu ni kwa
mtindo gani anatakiwa kuifasiri matini yake kwenda
lugha lengwa.
Kadharika, nadharia ya tafsiri inasisitiza kuwa mtindo
wa matini katika lugha chanzi uendane na ule wa
lugha lengwa.
15. Kubaini ubora na mamlaka ya
Matini
Ubora hubainika kwa kuzingatia lengo na na matarajio
ya mwandishi katika matini aliyoiandika.
Mmlaka ni hubainika kupitia umahiri na hadhi ya
mwandishi.
Mfasiri anajukumu la kujua haya ili kama matini
chanzi imeandikwa kwa ustadi wa hali ya juu na
mwandishi mwenye hadhi kubwa basi naye hana budi
kuhamisha hadhi na ubora huo katika matini yake
lengwa.
16. Kusoma Matini kwa mara ya
Mwisho
Ni vyema, baada ya kuyafahamu masuala hayo
yaliyojadiliwa hapo juu mfasiri akaisoma tena upya
matini chanzi ili aanze mchakato wa kutafsiri matini
hiyo.
Lakini pia si lazima vipengele hivyo apo juu vifuatwe
na mfasiri kama vilivyopangwa hapo, vinaweza kuwa
vinginevyo lakini jambo la msingi ni kwamba vyote
vizingatiwe kwa kina.
17.
18. Maandalizi
Hatua hii hujumuisha mambo ya msingi
yanayozingatiwa na mfasiri kabla ya kuanza kutafsiri.
Mambo hayo ni kama:
Kuisoma matini nzima, kubaini lengo la matini
chanzi, kubainisha lengo la mfasiri na kubaini mtindo
wa matini hiyo.
Mbali na hayo pia katika hatua hii mfasiri inampasa
kuchunguza taarifa kama; historia ya
mwandishi,mazingira yaliyomkuza na hadhi yake
katika jamii aliyoiandikia matini hiyo.
19. Uchambuzi
Katika hatua hii mfasiri anapaswa kuvitambua na
kuweka wazi visawe na maelezo yanayohitaji
ufafanuzi wa kina katika matini chanzi.
Hapa ndipo mfasiri hupitia marejeo mbalimbali ,kama
ensaiklopidia na kamusi ili kubaini visawe vya tafsiri
yake.
Hatua ya uchambuzi humpa nafasi mfasiri kurahisisha
kazi yake ya Tafsiri.
20. Uhawilishaji
Hapa mfasiri huamisha mawazo kutoka lugha chanzi
hadi lugha lengwa akitumia visawe alivyovibainisha
katika hatua ya uchambuzi.
Kimsingi katika hatua hii ndipo hasa zoezi la msingi la
tafsiri hufanyika
Mbali na hayo bado mfasiri ana nafasi ya kuongeza au
kupunguza visawe kwa mujibu wa mahitaji ya matini
lengwa na lengo la mfasiri.
21. Usawidi wa Rasimu ya Kwanza ya
Tafsiri
Usawidi wa rasimu ni kuiandika rasimu ya kwanza kwa
kadri ya ufasiri.
Mfasiri huzingatia umbo na mtindo wa matini chanzi
kuyapangilia mawazo katika matini lengwa .
Hatua hii hufuatwa baada ya hatua ya uhawilishaji,
Hapa ndio mfasiri huanza kuiona picha ya matini
lengwa katika mchakato mzima wa ufasiri.
22. Udurusu wa Rasimu ya Kwanza ya
Tafsiri
Baada mchakato wa usawidi ni wazi kwamba mfasiri
anapaswa kuisoma tafsiri aliyoifanya.
Wataalamu wanashauri mfasiri asome matini
aliyoitafsiri baada ya kuimaliza kuiandika.
Na ni vyema akaisoma kwa sauti ili kuweza kubaini
makosa mbalimbali kama vile; makosa ya kisarufi,
makosa ya kimatumizi ya lugha na pia kubaini uwiano
ulioo baina ya matini hiyo na matini chanzi.
23. Kusomwa kwa Rasimu na Mtu wa
Pili
Baada ya durusu ya mfasiri rasimu ya tafsiri inapaswa
isomwe na mtu mwingine.
Dhima kuu ni kubaini usahihi wa mtiririko wa
mawazo na ujumbe katika tafsiri hiyo.
Kwa kuisoma kwa makini msomaji wa pili ataweza
kubaini makosa na kuyawekea alama ili yasahihishwe.
Kama rasimu itasomwa vyema na msomaji wa pili na
kufanyiwa marekebisho basi rasimu hiyo itaondokea
kuwa nzuri.
24. Usawidi wa Rasimu ya Mwisho ya
Tafsiri
Hatua hii hujumuisha mchakato mzima wa kuyafanyia
kazi mawazo yaliyopendekezwa na msomaji wa pili wa
rasimu.
Usawidi huu ukipita basi matini lengwa hukamilika.
Tayari kutumiwa na hadhira lengwa.
25.
26. Nyenzo ya mawasiliano
Kueneza utamaduni wa jamii
Nyenzo ya kufundisha lugha za kigeni
Hupanua mawazo na fikra za wasomaji
Husaidia kuziba mapengo ya kimsamiati na kimaana
baina ya lugha.
28. Ukalimani ni nini?
Mshindo (2010) anasema ukalimani ni shughuli ya
kiakili inayowezesha kuwasiliana kwa maneno
yaliyosemwa au ishara zinazooonyeshwa baina ya watu
ambao hawasemi lugha moja au ambao hawatumii
ishara za aina moja.
Wanjara (2011) anasema ukalimani ni kuhawilisha
ujumbe ulioko katika mazungumzo, pamoja na
uamilifu wake, kutoka lugha chanzi kwenda lugha kwa
lengwa kwa kuzingatia isimu, utamaduni na
muktadha wa jamii husika.
29. Aina za Ukalimani
Kuna aina kuu mbili za ukalimani:
Ukalimani wa Papo kwa Papo
Ukalimani wa Ufuatizi
30. Ukalimani wa papo kwa papo
Aina hii ya ukalimani hutokea ambapo msemaji wa matini
chanzi na msemaji wa matini lenga hupishana kwa muda
kidogo sana .
Hapa si rahisi msikilizaji kuhisi kuwa mkalimani husikiliza
kabla hajakalimani kwa sabau sauti ya msemaji katika
lugha chanzi haipishani kabisa na sauti msemaji katika
lugha lengwa.
Kukalimani katika aina hii ya ukalimani inampasa
mkalimani awe na uwezo na ujuzi wa hali ya juu.
Aina hii ya ukalimani hutumika sana katika mikutano ya
kimataifa, mihadhara ya kidini na pia katika mahakama za
kimataifa.
31. maandalizi)
Hii ni aina ya ukalimani ambayo msemaji wa matini chanzi
na msemaji wa matini lenga hupishana kwa kipindi kirefu
katika kusema.
Hapa, hadhira hutambua wazi kwamba kuna watu
wanaozungumza kwa kupokezana.
Msemaji wa matini chanzi husema kwa kituo ili kumpa
nafasi msemaji wa lugha lengwa kuyafafanua kwa lugha ya
matini lengwa .
Kupokezana huko kunaweza kuwa kila baada ya sentensi,
aya au hata matini nzima alimuradi mkarimani anapewa
nafasi kujiandaa .
Aina hii hutumika katika mihadhara ya kidini na mara
nyingine katika mikutano ya kisiasa.
32. Sifa za Mkalimani
Uelewa wa kina juu ya lugha anazozitumia: hii
inajumuisha utajiri wa msamiati, kujua sheria na
taratibu za lugha na pia kuelewa matumizi ya lugha
katika miktadha mbalimbali.
Kuielewa kwa kina hadhira inayohusika:
kufahamu kiwango cha elimu, umri, mtazamo na
matarajio ya hadhira.
Kuelewa mbinu za kimawasiliano: hii inajumuisha
matumizi ya ishara na lugha za alama kusindikiza
ufafanuzi wa kikalimani. Sauti pia ni nyenzo nzuri ya
kimawasiliano inayovuta usikivu.
33. Umuhimu wa Mkalimani
Nyenzo ya mawasiliano
Nyenzo muhimu ya kujifunzia lugha
Nyenzo mahususi kudumisha amali za jamii
Nyenzo muhimu ya umoja baina ya jamii lugha tofauti
Nyenzo ya maendeleo
Kuenea kwa dini mbalimbali na tamaduni mbalimbali
duniani.
34. Swali…
1. Kwa mifano, fafanua sifa za mkalimani kwa
mujibu wa Wanjala (2011)
2. Jadili mambo ya msingi yanayozingatiwa na
mzungumzaji na mkalimani katika ukalimani.