Hii ni sehemu ndogo ya mada kuu ambayo ni matumizi ya lugha katika miktadha mbalimbali. Lengo la somo hili ni kumfafanulia mwanafunzi mtindo wa lugha unaotumika katika mazingira maalum.
2. Utangulizi
Katika somo lililopita tumeona jinsi
ambavyo lugha hutumika katika maisha
ya kila siku.
Tumeona mambo kadhaa ambayo
hutawala hayo ya utumizi wa lugha.
Sasa kutokana na mambo hayo
tunapata dhana ya rejesta.
Katika kipindi cha leo tutazingatia
matumizi ya lugha kimuktadha au
kimazingira.
3. Malengo
Kufikia mwisho wa
kipindi hiki tuwe
tumejifunza mambo
yafuatayo:
Maana ya rejesta
Aina za rejesta
Dhima za rejesta
4. Maana ya Rejesta
Rejesta ni mtindo wa lugha
unaotumika katika mazingira
maalum.
Mtindo huu hutumika pahali
fulani penye shughuli maalum,
agharabu huwa ni tofauti na
lugha ya kawaida.
Rejesta huwa na maneno na
muundo ambao lengo lake ni
kukidhi haja ya mawasiliano ya
sehemu husika.
Mfano wa sehemu ambazo
huwa na rejesta ni;
mahakamani, hospitali, hotelini
na sehemu nyingine mbalimbali.
6. Rejesta za Mtaani
Huu ni mtindo wa lugha
amabao huchipuka kutoka
katika kikundi kidogo cha
watu.
Agharabu watu hawa
huwa wanalingana rika na
huwa na utamaduni
mmoja.
Hususan vijana.
Lengo la kuibuka kwa
mtindo huu huwa ni
kujibainisha kiumri. Yaani
kuonesha ujana wao.
Mfano; manzi/shi –
msichana
Dingii – baba
Mazaa - mama
7. Rejesta za Hotelini
Huu ni mtindo ambao
hutumika hotelini au
migahawani.
Mtindo huu huwa na
lugha ya mkato kwa
lengo la kuokoa muda
katika kutoa huduma.
Mfano; walinyama
husemwa kama neno
moja badala ya
kusema wali kwa
nyama.
8. Rejesta za Hospitali
Mtindo huu wa lugha
hutumika mahospitalini.
Mara nyingi huwa ni
lugha ya mkato na
inakuwa na upole
mwingi. Lengo ni kumpa
tumaini mgonjwa.
Wakati mwingine huwa
wanatumia tafsidakwa
lengo la kupunguza
ukali wa maneno. Mfano
kalete Choo.
Mfano Dawa – 2 mara 3
9. Rejesta za
Mahakamani
Huu ni mtindo wa
lugha ambo hutumika
mahakani.
Lugha katika
muktadha huu
hutumiwa kwa
umakini mkubwa,
hivyo misamiati
maalumu hutumika
mara kwa mara.
Mfano; mheshimiwa
hakimu, kifungu,
ibara, kesi, shauri,
hukumu, upelelezi n.k
10. Rejesta za Kidini
Huu ni mtindo wa lugha
ambao haubadiliki.
Misamiati ambayo
hutumika katika mazingira
haya ni ile teule tu, yaani
ni ile ambayo imeteuliwa
na kukubaliwa kuwa
sehemu ya lugha ya
kiibada.
Mfano; Msikini maneno
kama – sheghe, sadaka,
lakaa, sunna n.k
Kanisani maneno kama:
Mtumishi, paroko,
madhabahu, ibada n. k
11. Dhima za Rejesta
Hutambulisha
mzungumzaji.
Hurahisisha
mawasiliano.
Hukuza lugha.
Hutumika kuweka
usiri au kuficha jambo
fulani.
Hupamba lugha.
Hutumika kupunguza
ukali wa meneno.
12. Zoezi
1. Eleza kwa kina
maana ya rejesta.
2. Kwa mifano
madhubuti fafanua
aina nne za rejesta
3. Toa dhima tano za
rejesta katika jamii