SlideShare a Scribd company logo
1 of 30
CHIMBUKO NA ASILI YA
KISWAHILI(kidato cha tatu)
Mussa Shekinyashi
+255 743 98 98 29
UTANGULIZI
• Lugha ya Kiswahili ni moja ya lugha zenye asili
ya Afrika ambazo zimefikia upeo wa kutumiwa
kama lugha za kiutandawazi ndani na nje ya bara
la Afrika.
• Kiswahili kinatumika kama lugha ya taifa katika
mataifa mawili ya Afrika Mashariki; Tanzania na
Kenya.
• Katika ulimwengu wa teknolojia pia Kiswahili
kinatumika kama lugha ya kiteknolojia.
• Kwa ujumla, Kiswahili kimepaa na kuwa lugha
yenye watumiaji wengi zaidi kuliko lugha
nyingine yenye asili ya kiafrika.
• Lakini tujiulize maswali ya msingi…
MASWALI YA MSINGI
Chimbuko
• Kiswahili kimeanzia wapi?
Asili
• Kiswahili kimeanzaje?
Chimbuko
• Chimbuko ni neno linalorejelea
mahala kitu kilipoanzia.
• Tunapoangazia chimbuko la Kiswahili
tunajikita kutaka kujua ni wapi hasa
(kijiografia) Kiswahili kimetokea.
Asili
• Neno asili lina maana ya jinsi au
namna kitu kilivyotokea.
• Tunapoangalia asili ya Kiswahili
tutakuwa tunazingatia namna Kiswahili
kilivyoanza.
KUNA NADHARIA NNE (4) ZA CHIMBUKO NA ASILI YA KISWAHILI
Kiswahili ni Kikongo
Kiswahili ni kiarabu
Kiswahli ni Pijini na Creoli
Kiswahili Kibantu
KISWAHILI NI KIKONGO
 Nadharia hii inafungamana na historia ya
wabantu.
 Wanahistoria wanasema wabantu walihama
kutoka katika misitu ya Kongo ambako ndio
chimbuko lao.
 Shughuli za kibiashara,ufugaji,kilimo na vita
ndio sababu za kuhama kwao.
 Wabantu kutoka Kongo walisambaa katika
sehemu mbalimbali za Afrika ikiwemo Afrika
Mashariki hadi wakatika pwani.
 Inasemekana kuwa walikuja na lugha yao
ambayo ndicho Kiswahili.
 Hivyo Kiswahili ni Kikongo.
UDHAIFU WA NADHARIA HII…
• Hakuna uthibitisho wa lini hasa wabantu hawa walihama kutoka Kongo kuja pwani
ya Afrika Mashariki.
• Lugha huwa imara na thabiti zaidi kule ilikoanzia kuliko kule ilikopelekwa. Kiswahili
cha Kongo ni dhaifu kimatamshi na kimsamiati ukilinganisha na kile cha pwani ya
Afrika Mashariki.
• Hii inathibitisha kuwa Kiswahili hakikuanzia Kongo bali kilipelekwa.
KISWAHILI NI KIARABU
• Wapo baadhi ya wataalamu
waliopendekeza kuwa Kiswahili ni
lugha ya kiarabu.
• Wao wanatoa hoja kwamba
maingiliano baina ya waarabu na
wabantu yalipelekea kufifia na kufa
kwa vijilugha vyote vilivyokuwako
katika upwa wa Afrika Mashariki na
kiarabu kikashika hatamu.
• Wanathibitisha hoja yao kwa uwepo
wa msamiati wenye asili ya Kiarabu
kwa asilimia 30 katika lugha ya
Kiswahili.
UDHAIFU WA NADHARIA HII
• Mtazamo huu umesisitiza zaidi juu ya msamiati wa kiswahili wenye asili ya kiarabu
kama kigezo chake na kutupilia mbali vipengele kama vile matamshi,maumbo na
miundo ya sentensi.
• Kiswahili kama lugha nyingine kimekopa msamiati kukidhi mawasiliano. Hiyo
haiwezi kuwa sababu ya chenyewe kuwa Kiarabu.
KISWAHILI NI PIJINI NA KREOLI
• Pijini ni lugha ya kati inayozuka baada ya
lugha mbili zenye asili tofauti zinapokutana
kimatumizi.
• Pijini huweza kuzuka mahala ambapo
kuna makundi mawili au zaidi na kila kundi
likiwa na lugha yake.
• Ili kurahisisha mawasilano lugha hizi
huchanganyika na kuingiliana.
• Jambo hili huweza kusababisha kuzuka
kwa lugha ya mchanganyiko ambayo
inaeleweka na makundi yote mawili.
• Hivyo pijini huwapa watu hao uwezo wa
kuwasiliana. Lugha AB
Lugha
B
Lugha
A
KREOLI
• Ni Pijini iliyokomaa.
• Watu wanaozungumza pijini wanaweza kuishi pamoja wakazoeana na kuoana, kisha
wakazaa watoto.
• Watoto wakakuta pijini ikizungumzwa kama lugha ya wazazi wao.
• Kwao hao watoto hii itakuwa lugha ya kwanza.
• Ikifika hatua hii, lugha hii huitwa krioli.
HIVYO…
• Wanaoshikilia nadharia hii wanadai kuwa Kiswahili ni Pijini ambayo ilikoma na kuwa
Kreoli.
• Wanasema, ujio wa Waarabu katika pwani ya Afrika Mashariki ulipelekea kuundwa
kwa lugha ya kati (pijini) ambayo ilichanganya Kiarabu na Kibantu.
• Baada ya maingiliano ya kiutamaduni ikiwemo kuoana baina ya waarabu na
wabantu vizazi vilivyofuata vilitumia pijini hiyo kama lugha yao ya kwanza.
• Ikawa Kreoli.
• Hivyo ndivyo Kiswahili kilivyoanza.
• Kwa hiyo Kiswahili na Pijini na Kreoli ya Kibantu na Kiarabu.
UDHAIFU WA NADHARIA HII
• Mtazamo huu umeshindwa kuitaja kinaganaga hiyo lugha ya kibantu iliyochangamana na
Kiarabu kuunda Kiswahili. Na kama ipo ndio Kiswahili chenyewe.
• Mtazamo huu umesisitiza zaidi juu ya msamiati wa kiswahili wenye asili ya kiarabu kama
kigezo chake na kutupilia mbali vipengele kama vile matamshi,maumbo na miundo ya
sentensi.
• Kiswahili kingekuwa pijini au krioli inayotokana na lugha ya kibantu na kiarabu, basi sintaksia
yake ingefanana na ile ya kiarabu
• Pia, kama Kiswahili kingekuwa ni zao la uchangamano wa Kiarabu na lugha ya Kibantu basi
asilimia hamsini ya misamiati ya kiswahili ingekuwa na asili ya kiarabu.
• Tofauti na ilivyo ambapo:
Msamiati wa kibantu- 60%
Msamiati wa Kiarabu-30%
Lugha nyingine -10%
KISWAHILI NI KIBANTU
• Nadharia hii inashikilia msimamo kuwa
Kiswahili si kiarabu, pijini au kreoli na
wala si Kikongo bali Kiswahili ni lugha
ya kibantu.
• Lugha za Kibantu ni lugha zenye asili
ya Kiafrika, hasa zile zinazopatikana
kusini mwa jangwa la sahala.
• Wataalamu wanoshikilia nadharia hii
wanasema Kiswahili ni moja ya lugha
hizo.
• Kuthibitisha hoja yao wanatoa ushaidi
wa Kihistoria na Kiisimu.
USHAHIDI WA KIHISTORIA
UGUNDUZI WA ALI – IDRISI
• Huyu ni mwana Jeografia aliyepata
kuzunguka sehemu kubwa ya Bahari ya
Hindi katika karne ya 10.
• Katika maandiko yake yaliyogunduliwa
huko Sicily, katika mahakama ya Mfalme
Roger II yanaonesha kuwa alipata kufika
katika upwa wa Afrika Mashariki.
• Amevielezea visiwa vya Zanzibar kwa jina la
“UNGUJA”
• Huu ni ushahidi kuwa kabla ya ujio wa
Waarabu walioleta neno Zanzibar, Visiwa
hivi vilikuwa na jina ‘Unguja’.
• Hii ni wazi kwamba wakazi wa visiwa hivi
walikuwa na lugha yao.
• Lugha hiyo ndicho Kiswahili.
• Kwa hiyo Kiswahili si Kiarabu wala si pijini
bali ni Kibantu
USHAHIDI WA MARCO-POLO
• Huyu ni mwanajeogarfia wa Kizungu
aliyepata kusafiri sehemu mbalimbali
duniani.
• Katika maandiko yake anaonesha kuwa
alipata kutembelea Afrika Mashariki katika
karne ya 10 na kuendelea.
• Katika maandishi yake anazungumzia asili
ya watu aliowakuta Afrika Mashariki, lugha,
dini na vyakula vyao.
• Maelezo ya Marco Polo yanakiri uwepo wa
lugha ya watu wa Afrika Mashariki.
• Hakusema kuwa lugha hiyo Kiarabu bali
lugha ya kibantu.
• Lugha hiyo ndicho Kiswahili.
• Hivyo Kiswahili ni Kibantu wala si kiarabu.
USHAHIDI WA AL-MASUDI
• Huyu ni mwanajeografia na historia wa
Kiarabu.
• Naye alipata nafasi ya kufika katika Pwani
ya Afrika Mashariki katika karne ya 10.
• Katika maandiko yake amefafanua majina
ya viongozi wa pwani ya Afrika Mashariki
kuwa ni Wakilimi.
• Pia, alistaajabishwa kusikia kuwa watu
Waafrika waliitwa Wazanji na nchi yao
Zanjibar.
• Ushahidi huu wa Al-Masudi
unatudhihirishia kuwa hata waarabu
wenyewe waliotembelea Afrika Mashariki
walikuta waafrika wakitumia lugha yao
ingawa ilikuwa na jina la Kiarabu.
• Hivyo Kiswahili si Kiarabu bali ni Kibantu.
HISTORIA YA MJI WA KILWA
• Katika historia, habari zinaeleza kuwepo
kwa masultani wa Kilwa waliopewa
majina kama Mkoma watu Nguo Nyingi
Hasha Hazifiki.
• Majina haya yanathibitisha kuwepo kwa
matumizi ya Kiswahili kabla ya ujio wa
utawala wa Mwarabu.
• Hivyo Kiswahili si Kiarabu wa Pijini bali
ni lugha yenye asili ya Kibantu.
UTENZI WA FUMO LIYONGO
• Kisa cha shujaa Lyongo kilikuwa
kikighaniwa kama ushairi kwa karne nyingi
kabla hakijarekodiwa kwenye maandishi
mnamo karne ya 13.
• Uwepo wa kisa hiki katika utenzi
kinadhihirisha kuwepo kwa lugha ya
Kiswahili kabla ya ujio wa waarabu.
• Mfano wa beti zake:
“Liyongo Kitamkali,
Akabalighi vijali,
Akawa mtu wa kweli,
Na hiba huongeya.”
• Utenzi huu unathibitisha kuwa Kiswahili ni
lugha yenye asili ya Kiafrika.
HIVYO…
• Kama tulivyoona hapo awali. Historia inathibitisha kuwa Kiswahili ni lugha yenye asili
ya Kibantu.
• Watu mashuhuri waliopata kuitembelea Afrika Mashariki wanaafiki katika maandishi
yao kuwa Kiswahili kilipata kuwapo na kuongelewa kabla ya ujio wa wageni.
• Hivyo Kiswahili ni Lugha yenye asili ya Kibantu.
USHAHIDI WA KIISIMU
MISAMIATI
• Msamiati ni sehemu ya msingi ya lugha.
• Sehemu kubwa ya msamiati wa Kiswahili unafanana na ule wa lugha za kibantu.
• Hii inamaana kwamba, misamiati katika lugha ya Kiswahili inaelekea kuwiana kimatamshi na
hata katika viambishi vichache.
• Mfano:
• Mifano hapo juu inaonesha knamna ambavyo misamiati katika lugha ya Kiswahili
inavyoelekea kufanana na mingine katika lugha nyingine za kibantu.
• Hivyo Kiswahili ni moja ya lugha za kibantu.
KISWAHILI KISAMBAA KIKURYA KIJITA
mtu mdhu omonto omontu
Maji mazi amanche amanji
Moto moto omoro omulilo
TUNGO ZA KISWAHILI
• Muundo wa tungo sentensi katika Kiswahili unafanana na muundo wa sentensi
katika lugha nyingine za kibantu.
• Sentensi katika Kiswahili zinazingatia muundo wa KIIMA na KIARIFU, kadharika
sentensi katika lugha nyingine za kibantu.
• Kufanana kwa muundo wa tungo kati ya Kiswahili na lugha nyingine za kibantu
kunathibitisha kuwa Kiswahili ni moja ya lugha zenye asili ya kibantu.
KIIMA KIARIFU
KISWAHILI Juma anakula ugali
KIZIGUA Juma adya ugali
KISUKUMA Juma alelya bugali
KINDALI Juma akulya ubhughali
UPATANISHO CHA KISARUFI
• Katika kigezo hiki tunazingatia uhusiano uliopo kati ya NOMINO(viwakilishi) na viambishi
awali vya nafsi katika vitenzi vya Kiswahili tukifananisha na lugha nyingine za kibantu.
• Ukichunguza kwa makini utagundua kuwa viambishi katika vitenzi vya Kiswahili hubadilika
kutokana na maumbo ya umoja na wingi wa nomino au kiwakilishi katika sentenis.
• Tabia hii pia inajidhihirisha katika lugha nyingine za kibantu.
• Mfano:
• Hii inathibitisha kuwa kiswahili ni moja ya lugha za kibantu.
UMOJA WINGI
KISWAHILI Baba analima Baba wanalima
KINDALI Utata akulima Abhatata bhakulima
KIKURYA Tata ararema Batata bararema
KISAMBAA Tate ataima Tate wataima
MPANGILIO WA VIAMBISHI
• Vitenzi katika lugha za kibantu huundwa na MZIZI ambao huambikwa viambishi ili
kukamilisha maana yake.
• Kiswahili pia hufuata utaratibu huu. Vitenzi vyake huundwa na mzizi kisha
kuambikwa viambishi.
• Mfano:
• Katika mfano hapo juu utagundua kuwa mbali na kuthibitisha kuwa vitenzi vya
Kiswahili na vile vya lugha za kibantu vinaundwa na mzizi na viambishi lakini pia
utagundua vyote vinampangilio sawa.
• Yaani viambishi vya nafsi huanza kisha vinafuata vya njeo kisha mzizi.
• Hii inathibitisha kuwa Kiswahili ni moja ya lugha za kibantu.
KISWAHILI analima a-na-lim-a
KISAMBAA ataima A-ta- im-a
KIKURYA arerema A-re-rem-a
IDADI YA IRABU
• Kiswahili na lugha nyingine za kibantu, zote zina irabu ambazo ni:
a , e , I , o , u
• Hii inathibitisha kuwa Kiswahili ni Kibantu na wala si Kiarabu.
HIVYO…
• Kama tulivyoona katika ushahidi wa kiisimu, Kiswahili kina sifa sawa za kiisimu na
lugha nyingine kusini mwa jangwa la sahara.
• Hii inathibitisha kuwa Kiswahili ni KIBANTU.
HITIMISHO
• Kiswahili kimepitia historia kubwa sana kimaendeleo.
• Katika makala yetu tumeona nadharia mbalimbali zinazojaribu kuangalia chimbuko
na asili ya Kiswahili.
• Kati ya nadharia zote imethibitika kuwa Kiswahili ni lugha ya kibantu.
• Hivyo; Kwa asili Kiswahili ni lugha ya kibantu na chimbuko lake ni katika pwani ya
Afrika Mashariki.
ASANTENI KWA KUNISIKILIZA

More Related Content

What's hot (20)

MATUMIZI YA SARUFI
MATUMIZI YA SARUFIMATUMIZI YA SARUFI
MATUMIZI YA SARUFI
 
Sarufi Matamshi (Fonolojia)
Sarufi Matamshi (Fonolojia)Sarufi Matamshi (Fonolojia)
Sarufi Matamshi (Fonolojia)
 
Tamthilia ni nini?
Tamthilia ni nini?Tamthilia ni nini?
Tamthilia ni nini?
 
TAFSIRI NA UKALIMANI
TAFSIRI NA UKALIMANITAFSIRI NA UKALIMANI
TAFSIRI NA UKALIMANI
 
CHIMBUKO LA FASIHI
CHIMBUKO LA FASIHICHIMBUKO LA FASIHI
CHIMBUKO LA FASIHI
 
FASIHI KWA UJUMLA
FASIHI KWA UJUMLAFASIHI KWA UJUMLA
FASIHI KWA UJUMLA
 
Kuongeza msamiati wa kiswahili
Kuongeza msamiati wa kiswahiliKuongeza msamiati wa kiswahili
Kuongeza msamiati wa kiswahili
 
Rejesta
RejestaRejesta
Rejesta
 
Mofolojia
MofolojiaMofolojia
Mofolojia
 
Umuhimu wa kujifunza nadharia za fonolojia
Umuhimu wa kujifunza nadharia za fonolojiaUmuhimu wa kujifunza nadharia za fonolojia
Umuhimu wa kujifunza nadharia za fonolojia
 
Uhakiki wa Tamthiliya ya Ngoswe penzi
Uhakiki wa Tamthiliya ya Ngoswe penziUhakiki wa Tamthiliya ya Ngoswe penzi
Uhakiki wa Tamthiliya ya Ngoswe penzi
 
Uhakiki wa kazi za fasihi andishi
Uhakiki wa kazi za fasihi andishiUhakiki wa kazi za fasihi andishi
Uhakiki wa kazi za fasihi andishi
 
Tafsiri na ukalimani
Tafsiri na ukalimaniTafsiri na ukalimani
Tafsiri na ukalimani
 
UHAKIKI WA FASIHI ANDISHI
UHAKIKI WA FASIHI ANDISHIUHAKIKI WA FASIHI ANDISHI
UHAKIKI WA FASIHI ANDISHI
 
UTUMIZI WA LUGHA
UTUMIZI WA LUGHAUTUMIZI WA LUGHA
UTUMIZI WA LUGHA
 
Maana ya maana!
Maana ya maana!Maana ya maana!
Maana ya maana!
 
UTUNGAJI
UTUNGAJIUTUNGAJI
UTUNGAJI
 
USHAIRI WA KISWAHILI
USHAIRI WA KISWAHILIUSHAIRI WA KISWAHILI
USHAIRI WA KISWAHILI
 
Matumizi ya Lugha Kimuktadha
Matumizi ya Lugha KimuktadhaMatumizi ya Lugha Kimuktadha
Matumizi ya Lugha Kimuktadha
 
Mjengo wa tungo 3
Mjengo wa tungo 3Mjengo wa tungo 3
Mjengo wa tungo 3
 

More from mussa Shekinyashi

More from mussa Shekinyashi (8)

Uhifadhi wa fasihi simulizi
Uhifadhi wa fasihi simuliziUhifadhi wa fasihi simulizi
Uhifadhi wa fasihi simulizi
 
Evolution of Man (form one)
Evolution of Man (form one)Evolution of Man (form one)
Evolution of Man (form one)
 
Public Speaking Tips
Public Speaking TipsPublic Speaking Tips
Public Speaking Tips
 
UHAKIKI WA TAMTHILIYA - ORODHA
UHAKIKI WA TAMTHILIYA - ORODHAUHAKIKI WA TAMTHILIYA - ORODHA
UHAKIKI WA TAMTHILIYA - ORODHA
 
Uhuru wa Mtunzi wa Kazi za Fasihi
Uhuru wa Mtunzi wa Kazi za FasihiUhuru wa Mtunzi wa Kazi za Fasihi
Uhuru wa Mtunzi wa Kazi za Fasihi
 
GENDER CONCEPTS - FORM TWO
GENDER CONCEPTS - FORM TWO GENDER CONCEPTS - FORM TWO
GENDER CONCEPTS - FORM TWO
 
UHAKIKI WA RIWAYA - USIKU UTAKAPOKWISHA
UHAKIKI WA RIWAYA - USIKU UTAKAPOKWISHAUHAKIKI WA RIWAYA - USIKU UTAKAPOKWISHA
UHAKIKI WA RIWAYA - USIKU UTAKAPOKWISHA
 
Semantiki
SemantikiSemantiki
Semantiki
 

Chimbuko na Asili ya Kiswahili

  • 1. CHIMBUKO NA ASILI YA KISWAHILI(kidato cha tatu) Mussa Shekinyashi +255 743 98 98 29
  • 2. UTANGULIZI • Lugha ya Kiswahili ni moja ya lugha zenye asili ya Afrika ambazo zimefikia upeo wa kutumiwa kama lugha za kiutandawazi ndani na nje ya bara la Afrika. • Kiswahili kinatumika kama lugha ya taifa katika mataifa mawili ya Afrika Mashariki; Tanzania na Kenya. • Katika ulimwengu wa teknolojia pia Kiswahili kinatumika kama lugha ya kiteknolojia. • Kwa ujumla, Kiswahili kimepaa na kuwa lugha yenye watumiaji wengi zaidi kuliko lugha nyingine yenye asili ya kiafrika. • Lakini tujiulize maswali ya msingi…
  • 3. MASWALI YA MSINGI Chimbuko • Kiswahili kimeanzia wapi? Asili • Kiswahili kimeanzaje?
  • 4. Chimbuko • Chimbuko ni neno linalorejelea mahala kitu kilipoanzia. • Tunapoangazia chimbuko la Kiswahili tunajikita kutaka kujua ni wapi hasa (kijiografia) Kiswahili kimetokea. Asili • Neno asili lina maana ya jinsi au namna kitu kilivyotokea. • Tunapoangalia asili ya Kiswahili tutakuwa tunazingatia namna Kiswahili kilivyoanza.
  • 5. KUNA NADHARIA NNE (4) ZA CHIMBUKO NA ASILI YA KISWAHILI Kiswahili ni Kikongo Kiswahili ni kiarabu Kiswahli ni Pijini na Creoli Kiswahili Kibantu
  • 6. KISWAHILI NI KIKONGO  Nadharia hii inafungamana na historia ya wabantu.  Wanahistoria wanasema wabantu walihama kutoka katika misitu ya Kongo ambako ndio chimbuko lao.  Shughuli za kibiashara,ufugaji,kilimo na vita ndio sababu za kuhama kwao.  Wabantu kutoka Kongo walisambaa katika sehemu mbalimbali za Afrika ikiwemo Afrika Mashariki hadi wakatika pwani.  Inasemekana kuwa walikuja na lugha yao ambayo ndicho Kiswahili.  Hivyo Kiswahili ni Kikongo.
  • 7. UDHAIFU WA NADHARIA HII… • Hakuna uthibitisho wa lini hasa wabantu hawa walihama kutoka Kongo kuja pwani ya Afrika Mashariki. • Lugha huwa imara na thabiti zaidi kule ilikoanzia kuliko kule ilikopelekwa. Kiswahili cha Kongo ni dhaifu kimatamshi na kimsamiati ukilinganisha na kile cha pwani ya Afrika Mashariki. • Hii inathibitisha kuwa Kiswahili hakikuanzia Kongo bali kilipelekwa.
  • 8. KISWAHILI NI KIARABU • Wapo baadhi ya wataalamu waliopendekeza kuwa Kiswahili ni lugha ya kiarabu. • Wao wanatoa hoja kwamba maingiliano baina ya waarabu na wabantu yalipelekea kufifia na kufa kwa vijilugha vyote vilivyokuwako katika upwa wa Afrika Mashariki na kiarabu kikashika hatamu. • Wanathibitisha hoja yao kwa uwepo wa msamiati wenye asili ya Kiarabu kwa asilimia 30 katika lugha ya Kiswahili.
  • 9. UDHAIFU WA NADHARIA HII • Mtazamo huu umesisitiza zaidi juu ya msamiati wa kiswahili wenye asili ya kiarabu kama kigezo chake na kutupilia mbali vipengele kama vile matamshi,maumbo na miundo ya sentensi. • Kiswahili kama lugha nyingine kimekopa msamiati kukidhi mawasiliano. Hiyo haiwezi kuwa sababu ya chenyewe kuwa Kiarabu.
  • 10. KISWAHILI NI PIJINI NA KREOLI • Pijini ni lugha ya kati inayozuka baada ya lugha mbili zenye asili tofauti zinapokutana kimatumizi. • Pijini huweza kuzuka mahala ambapo kuna makundi mawili au zaidi na kila kundi likiwa na lugha yake. • Ili kurahisisha mawasilano lugha hizi huchanganyika na kuingiliana. • Jambo hili huweza kusababisha kuzuka kwa lugha ya mchanganyiko ambayo inaeleweka na makundi yote mawili. • Hivyo pijini huwapa watu hao uwezo wa kuwasiliana. Lugha AB Lugha B Lugha A
  • 11. KREOLI • Ni Pijini iliyokomaa. • Watu wanaozungumza pijini wanaweza kuishi pamoja wakazoeana na kuoana, kisha wakazaa watoto. • Watoto wakakuta pijini ikizungumzwa kama lugha ya wazazi wao. • Kwao hao watoto hii itakuwa lugha ya kwanza. • Ikifika hatua hii, lugha hii huitwa krioli.
  • 12. HIVYO… • Wanaoshikilia nadharia hii wanadai kuwa Kiswahili ni Pijini ambayo ilikoma na kuwa Kreoli. • Wanasema, ujio wa Waarabu katika pwani ya Afrika Mashariki ulipelekea kuundwa kwa lugha ya kati (pijini) ambayo ilichanganya Kiarabu na Kibantu. • Baada ya maingiliano ya kiutamaduni ikiwemo kuoana baina ya waarabu na wabantu vizazi vilivyofuata vilitumia pijini hiyo kama lugha yao ya kwanza. • Ikawa Kreoli. • Hivyo ndivyo Kiswahili kilivyoanza. • Kwa hiyo Kiswahili na Pijini na Kreoli ya Kibantu na Kiarabu.
  • 13. UDHAIFU WA NADHARIA HII • Mtazamo huu umeshindwa kuitaja kinaganaga hiyo lugha ya kibantu iliyochangamana na Kiarabu kuunda Kiswahili. Na kama ipo ndio Kiswahili chenyewe. • Mtazamo huu umesisitiza zaidi juu ya msamiati wa kiswahili wenye asili ya kiarabu kama kigezo chake na kutupilia mbali vipengele kama vile matamshi,maumbo na miundo ya sentensi. • Kiswahili kingekuwa pijini au krioli inayotokana na lugha ya kibantu na kiarabu, basi sintaksia yake ingefanana na ile ya kiarabu • Pia, kama Kiswahili kingekuwa ni zao la uchangamano wa Kiarabu na lugha ya Kibantu basi asilimia hamsini ya misamiati ya kiswahili ingekuwa na asili ya kiarabu. • Tofauti na ilivyo ambapo: Msamiati wa kibantu- 60% Msamiati wa Kiarabu-30% Lugha nyingine -10%
  • 14. KISWAHILI NI KIBANTU • Nadharia hii inashikilia msimamo kuwa Kiswahili si kiarabu, pijini au kreoli na wala si Kikongo bali Kiswahili ni lugha ya kibantu. • Lugha za Kibantu ni lugha zenye asili ya Kiafrika, hasa zile zinazopatikana kusini mwa jangwa la sahala. • Wataalamu wanoshikilia nadharia hii wanasema Kiswahili ni moja ya lugha hizo. • Kuthibitisha hoja yao wanatoa ushaidi wa Kihistoria na Kiisimu.
  • 16. UGUNDUZI WA ALI – IDRISI • Huyu ni mwana Jeografia aliyepata kuzunguka sehemu kubwa ya Bahari ya Hindi katika karne ya 10. • Katika maandiko yake yaliyogunduliwa huko Sicily, katika mahakama ya Mfalme Roger II yanaonesha kuwa alipata kufika katika upwa wa Afrika Mashariki. • Amevielezea visiwa vya Zanzibar kwa jina la “UNGUJA” • Huu ni ushahidi kuwa kabla ya ujio wa Waarabu walioleta neno Zanzibar, Visiwa hivi vilikuwa na jina ‘Unguja’. • Hii ni wazi kwamba wakazi wa visiwa hivi walikuwa na lugha yao. • Lugha hiyo ndicho Kiswahili. • Kwa hiyo Kiswahili si Kiarabu wala si pijini bali ni Kibantu
  • 17. USHAHIDI WA MARCO-POLO • Huyu ni mwanajeogarfia wa Kizungu aliyepata kusafiri sehemu mbalimbali duniani. • Katika maandiko yake anaonesha kuwa alipata kutembelea Afrika Mashariki katika karne ya 10 na kuendelea. • Katika maandishi yake anazungumzia asili ya watu aliowakuta Afrika Mashariki, lugha, dini na vyakula vyao. • Maelezo ya Marco Polo yanakiri uwepo wa lugha ya watu wa Afrika Mashariki. • Hakusema kuwa lugha hiyo Kiarabu bali lugha ya kibantu. • Lugha hiyo ndicho Kiswahili. • Hivyo Kiswahili ni Kibantu wala si kiarabu.
  • 18. USHAHIDI WA AL-MASUDI • Huyu ni mwanajeografia na historia wa Kiarabu. • Naye alipata nafasi ya kufika katika Pwani ya Afrika Mashariki katika karne ya 10. • Katika maandiko yake amefafanua majina ya viongozi wa pwani ya Afrika Mashariki kuwa ni Wakilimi. • Pia, alistaajabishwa kusikia kuwa watu Waafrika waliitwa Wazanji na nchi yao Zanjibar. • Ushahidi huu wa Al-Masudi unatudhihirishia kuwa hata waarabu wenyewe waliotembelea Afrika Mashariki walikuta waafrika wakitumia lugha yao ingawa ilikuwa na jina la Kiarabu. • Hivyo Kiswahili si Kiarabu bali ni Kibantu.
  • 19. HISTORIA YA MJI WA KILWA • Katika historia, habari zinaeleza kuwepo kwa masultani wa Kilwa waliopewa majina kama Mkoma watu Nguo Nyingi Hasha Hazifiki. • Majina haya yanathibitisha kuwepo kwa matumizi ya Kiswahili kabla ya ujio wa utawala wa Mwarabu. • Hivyo Kiswahili si Kiarabu wa Pijini bali ni lugha yenye asili ya Kibantu.
  • 20. UTENZI WA FUMO LIYONGO • Kisa cha shujaa Lyongo kilikuwa kikighaniwa kama ushairi kwa karne nyingi kabla hakijarekodiwa kwenye maandishi mnamo karne ya 13. • Uwepo wa kisa hiki katika utenzi kinadhihirisha kuwepo kwa lugha ya Kiswahili kabla ya ujio wa waarabu. • Mfano wa beti zake: “Liyongo Kitamkali, Akabalighi vijali, Akawa mtu wa kweli, Na hiba huongeya.” • Utenzi huu unathibitisha kuwa Kiswahili ni lugha yenye asili ya Kiafrika.
  • 21. HIVYO… • Kama tulivyoona hapo awali. Historia inathibitisha kuwa Kiswahili ni lugha yenye asili ya Kibantu. • Watu mashuhuri waliopata kuitembelea Afrika Mashariki wanaafiki katika maandishi yao kuwa Kiswahili kilipata kuwapo na kuongelewa kabla ya ujio wa wageni. • Hivyo Kiswahili ni Lugha yenye asili ya Kibantu.
  • 23. MISAMIATI • Msamiati ni sehemu ya msingi ya lugha. • Sehemu kubwa ya msamiati wa Kiswahili unafanana na ule wa lugha za kibantu. • Hii inamaana kwamba, misamiati katika lugha ya Kiswahili inaelekea kuwiana kimatamshi na hata katika viambishi vichache. • Mfano: • Mifano hapo juu inaonesha knamna ambavyo misamiati katika lugha ya Kiswahili inavyoelekea kufanana na mingine katika lugha nyingine za kibantu. • Hivyo Kiswahili ni moja ya lugha za kibantu. KISWAHILI KISAMBAA KIKURYA KIJITA mtu mdhu omonto omontu Maji mazi amanche amanji Moto moto omoro omulilo
  • 24. TUNGO ZA KISWAHILI • Muundo wa tungo sentensi katika Kiswahili unafanana na muundo wa sentensi katika lugha nyingine za kibantu. • Sentensi katika Kiswahili zinazingatia muundo wa KIIMA na KIARIFU, kadharika sentensi katika lugha nyingine za kibantu. • Kufanana kwa muundo wa tungo kati ya Kiswahili na lugha nyingine za kibantu kunathibitisha kuwa Kiswahili ni moja ya lugha zenye asili ya kibantu. KIIMA KIARIFU KISWAHILI Juma anakula ugali KIZIGUA Juma adya ugali KISUKUMA Juma alelya bugali KINDALI Juma akulya ubhughali
  • 25. UPATANISHO CHA KISARUFI • Katika kigezo hiki tunazingatia uhusiano uliopo kati ya NOMINO(viwakilishi) na viambishi awali vya nafsi katika vitenzi vya Kiswahili tukifananisha na lugha nyingine za kibantu. • Ukichunguza kwa makini utagundua kuwa viambishi katika vitenzi vya Kiswahili hubadilika kutokana na maumbo ya umoja na wingi wa nomino au kiwakilishi katika sentenis. • Tabia hii pia inajidhihirisha katika lugha nyingine za kibantu. • Mfano: • Hii inathibitisha kuwa kiswahili ni moja ya lugha za kibantu. UMOJA WINGI KISWAHILI Baba analima Baba wanalima KINDALI Utata akulima Abhatata bhakulima KIKURYA Tata ararema Batata bararema KISAMBAA Tate ataima Tate wataima
  • 26. MPANGILIO WA VIAMBISHI • Vitenzi katika lugha za kibantu huundwa na MZIZI ambao huambikwa viambishi ili kukamilisha maana yake. • Kiswahili pia hufuata utaratibu huu. Vitenzi vyake huundwa na mzizi kisha kuambikwa viambishi. • Mfano: • Katika mfano hapo juu utagundua kuwa mbali na kuthibitisha kuwa vitenzi vya Kiswahili na vile vya lugha za kibantu vinaundwa na mzizi na viambishi lakini pia utagundua vyote vinampangilio sawa. • Yaani viambishi vya nafsi huanza kisha vinafuata vya njeo kisha mzizi. • Hii inathibitisha kuwa Kiswahili ni moja ya lugha za kibantu. KISWAHILI analima a-na-lim-a KISAMBAA ataima A-ta- im-a KIKURYA arerema A-re-rem-a
  • 27. IDADI YA IRABU • Kiswahili na lugha nyingine za kibantu, zote zina irabu ambazo ni: a , e , I , o , u • Hii inathibitisha kuwa Kiswahili ni Kibantu na wala si Kiarabu.
  • 28. HIVYO… • Kama tulivyoona katika ushahidi wa kiisimu, Kiswahili kina sifa sawa za kiisimu na lugha nyingine kusini mwa jangwa la sahara. • Hii inathibitisha kuwa Kiswahili ni KIBANTU.
  • 29. HITIMISHO • Kiswahili kimepitia historia kubwa sana kimaendeleo. • Katika makala yetu tumeona nadharia mbalimbali zinazojaribu kuangalia chimbuko na asili ya Kiswahili. • Kati ya nadharia zote imethibitika kuwa Kiswahili ni lugha ya kibantu. • Hivyo; Kwa asili Kiswahili ni lugha ya kibantu na chimbuko lake ni katika pwani ya Afrika Mashariki.