SlideShare a Scribd company logo
1 of 20
Download to read offline
http://www.poetrytranslation.org
POESIA SWAHILI
EUPHRASE KEZILAHABI
KITHAKA wa MBERIA
ALAMIN MAZRUI
INDICE
EUPHRASE KEZILAHABI
3 Upepo wa Wakati
4 Mafuriko
5 Mgomba
6 Chai ya Jioni
7 Fasihi
8 Kisima
KITHAKA wa MBERIA
9 Jumapili ya Damu
ALAMIN MAZRUI
12 Mlango
13 Mimi Ni Mimi
14 Nilivuka
15 Kifungoni
16 Kizuizini
17 Bega kwa bega
18 Sauti?
19 Mkata wa maneno
20 Niguse
EUPHRASE KEZILAHABI
Upepo wa Wakati
Juu ya mlima mdogo
Siku moja nilisimama.
Nikatazama chini ziwani, siku
Ya dhoruba. Halafu niliona mawimbi
Yakipanda na kushuka. Yakivimba,
Yakiviringika, yakigongana na kutoa povu
Kama fahari wehu katika bonde lisomajani.
Yalivyotengenezwa!
Yalivyofifia na kuanza tena!
Kamwe sikuona.
Lakini niliyaona yakishuka kwa nguvu
Na kupanda haraka, yakisukumwa
Na upepo wa Magharibi na Mashariki.
Hivyo ndivyo ulimwengu ulivyo.
Na hivyo maisha ya binadamu.
Wanapanda na kushuka
Wakisukumwa na upepo na wakati.
Tazama wanavyojinyakulia madaraka
Kama mzamaji, mguu wa rafikiye, ashikavyo!
Wanavyoshika pesa kama mtoto
Na picha ya bandia
Au asikari mwehu na bunduki yake
Na kutunyamazisha!
Watapanda na kushuka
Na wataanguka kweli!
Wakisukumwa na upepo wa wakati!
Mafuriko
Nitaandika wimbo juu ya mbawa za nzi
Utoe muziki arukapo wausikie walio wengi
Ushairi wa jalalani utaimbwa
Juu ya vidonda vya wakulima
Na usaha ulio jasho lao.
Nitaandika juu ya mbawa za wadudu
Wote warukao
Juu ya mistari ya pundamilia
Na masikio makubwa ya tembo.
Juu ya kuta vyooni, maofisini, madarasani,
Juu ya paa za nyumba, kuta za Ikulu,
Na juu ya khanga na tisheti.
Nitaandika wimbo huu:
Mafuriko ya mwaka huu
Yatishia nyumba kongwe bondeni.
Waliomo wameanza kuihama
Na miti ya umeme imeanguka.
Palipokuwa na mwanga, sasa giza.
Mafuriko ya mwaka huu!
Mti mkongwe umelalia upande
Wa nyumba zetu hafifu.
Upepo mkali uvumapo hatulali.
Kila kukicha twatazama mizizi yake
Na mkao wake, na kuta hafifu za nyumba.
Lazima ukatwe kuanzia matawi hadi shina
Mafuriko ya mwaka huu yaashiria...
Tutabaki kuwasimulia wajukuu:
Mwaka ule wa mafuriko
Miti mingi mikongwe ilianguka.
Mafuriko ya mwaka huu!
Wengi wataumbuka.
Mgomba
Mgomba umelala chini: hauna faida tena,
Baada ya kukatwa na wafanya kazi
Wa bustani kwa kusita.
Watoto, kwa wasiwasi wanasubiri wakati wao
Bustanini hakuna kitu
Isipokuwa upepo fulani wenye huzuni,
Unaotikisa majani na kutoa sauti ya kilio. 
Hivyo ndivyo ufalme wa mitara ulivyo.
Mti wa mji umelala chini: hauna faida tena,
Baada ya kukatwa na wafanya kazi
Wa bustani kwa kusita.
Chumbani hakuna kitu
Isipokuwa upepo fulani wenye huzuni utingishao
Wenye hila waliokizunguka kitanda na kulia.
Machozi yenye matumaini yapiga
Mbiu ya hatari ya magomvi nyumbani.
           Magomvi
Kati ya wanawake
           Magomvi
Kati ya watoto kwa ajili ya vitu na uongozi.
Ole! Milki ya 'Lexanda imekwisha!
 
Vidonda vya ukoma visofunikwa
Ambavyo kwa mda mrefu vilifichama
Sasa viko nje kufyonzwa na inzi wa kila aina
Na vinanuka vibaya.
Lakini inzi kila mara hufyonza wakifikiri
Nani watamwambukiza.
Chai ya Jioni
Wakati tunywapo chai hapa upenuni
Na kuwatazama watoto wetu
Wakicheza bembea kwa furaha
Tujue kamba ya bembea yetu
Imeshalika na imeanza kuoza
Na bado kidogo tutaporomoka.
Kulikuwa na wakati ulinisukuma juu
Nikaenda zaidi ya nusu duara;
Kulikuwa na wakati nilikudaka
Ulipokaribia kuanguka,
Na kulikuwa na wakati tulibebana kwa zamu
Mmoja wima akisukuma mwingine amekaa.
Wakati huo, japo tulipaa mbele na nyuma
Tulicheka kwa matumaini yaliyotiwa chumvi
Na kisha tukaongozana jikoni kupika chajio;
Ilikuwa adhuhuri yetu.
Sasa tukisubiri ndoto tusizoweza kutekeleza tena
Tumalizie machicha ya chai yetu ya jioni
Bila kutematema na kwa tabasamu.
Baada ya hapo tujilambelambe utamuutamu
Uliobakia kwenye midomo yetu,
Tukikumbuka siku ilee ya kwanza
Tulipokutana jioni chini ya mwembe
Tukitafuta tawi zuri gumu
La kufunga bembea yetu
Naye mbwa Simba akikusubiri.
Lakini kabla hatujaondoka kimyakimya
Kukamilika nusu duara iliyobakia.
Tuhakikishe vikombe vyetu ni safi.
Fasihi
Maneno yangu kumeza tena sasa siwezi.
Lakini kuonyesha ukweli na kuutafuta
Nitaendelea: mimi ni kama boga.
Nimepandwa katikati, bustanini,
Na kama boga nitatambaa chini
Zote pande, kuikwea miti ya hekima
Na yote magugu koo kuyakaba.
Bila woga, bila nyuma kurudi nitashambulia
Ya binadamu matendo bado yakihema.
            Halafu wakati
            Ujao utafika
            Matunda nitatoa
            Makubwa madogo
            Mazuri mabaya
Wakati utafika watakapokuja wajuzi
Kwa jembe la wino kunipalia.
Wala mboga za majani watanichuma.
Utafika, wa maboga kuwa mikata.
Machafu na safi yatachotwa
Na nitaingia mitungi ya kila mji-shamba.
Watoto mikononi mwao watanichezea.
Chini wataniangusha na kunipasua.
Lakini mbegu, mbegu zitabaki.
            Mimi ninajua
            Hatari sina
            Wajibu msomaji
            Mjini na shamba
            Vizuri kunichambua.
Halafu utafika ule wakati
Watumia vikombe dhahabu na glasi
Pembeni kwa chuki kunitupa,
Na nitakuwa nyuma ya wakati
Lakini wakisahau wahenga
Kata na mboga walitumia
Msingi wa wao utamaduni
Watakuwa wameutupa.
Kumbukeni, kumbukeni, kumbukeni.
Kisima
Kisima cha maji ya uzima ki wazi
Na vyura katika bonde la taaluma watuita
Tujongee kwa mahadhi yao
Yaongozayo pandikizi la mtu
Kwa hatua ndefu litembealo
Na sindano ya shaba kitovuni
Upinde na mishale mkononi
Kisha likapiga goti kisimani
Tayari kumfuma akaribiaye
Maana shujaa hafi miongoni mwa wezi
Bali kama simba mawindoni.
Hatuwezi tena kuteka maji
Na kalamu zetu zimekauka wino.
Nani atamsukuma kwa kalamu
Aitwe shujaa wa uwongo!
Aliyeitia kitovuni kwa hofu
Ingawa tegemeo hakulipata
Alifungua mlango uelekeao
Katikati ya ujuzi na urazini mpya
Mwanzo wa kizazi tukionacho.
KITHAKA wa MBERIA
Jumapili ya Damu
I 
Midundo ya Reggae
Inarindima hewani
Na kuchanganyika
Na macheo
 
Katika jiji
Vioo, madirisha
Na milango
Inasalimu amri
Kutoka kumbo kali
Za wenye njaa
Na matarajio
Ya miongo miwili.
 
Ndani ya maduka
Mawimbi ya watu
Yanapaa, kushuka
Na kupanda kwingineko
Huku rafu na kuta
Zikibadilika sura
Kama tanzu za miti
Kiangazi kinapojiri.
 
Vifaa vya kila ukoo
Nguo za kila rangi
Zinaketi vichwani
Kuninginia mikononi
Kulala migongoni
Au kubanwa kwapani
Zikibadili makazi
Na umiliki.
 
II
 
Risasi
Zinaanza kupiga miluzi
Na kwa ghadhabu
Kushtua kuta
Milingoti ya stima
Magari ya rangirangi
Na nyama na mifupa
 
Watu wanaterereka
Damu inatiririka
Uhai unaporomoka
 
III
 
Ghafla
Midundo ya Reggae
Inakauka
Na nyimbo za jana
Kurudi angani
Kama uvundo ambao
Umevamia pua tena
Baada ya kuangushwa
Na kumbo la upepo
 
Kutoka mwangu jikoni
Barabara ni dhahiri-
Magari ya rangirangi
Vifaru vya madoadoa
Vinatiririka kama mto,
Bunduki zinalenga kushoto
Kulia, nyuma na mbele
Nayo mizinga hatari
Inatega mbingu;
Huu mtiririko
Ni safari ya marejeo
Anarejea mungu-wa-kinamo
Kwenye ulingo.
 
IV
 
Katika fahamu
Mawazo mbalimbali
Yanapita kwa zamu
Kama vipepeo na nondo
Wakipita kwa makundi
Mbele ya macho;
Kwa tabasamu
Nakumbuka Obasanjo
Na uamuzi wake angavu
Bali pia
Kwa huzuni
Nakumbuka Bokassa na Amin,
Na Mobutu na Doe,
Na damu na mafuvu
Matita ya mafuvu!
Magurudumu ya mawazo
Yanafikia njia panda
Na kwa muda, kukwama
Kabla ya kuanza safari tena
Kwenye njia wazi
Ya serikali ya kiraia
Hata inapoongozwa
Na genge la mazimwi
ALAMIN MAZRUI
Alamin Mazrui
Mlango
Ama utapita
katika mlango huu
au hutapita.
Ukipita
kuna hatari
ya jinalo kulisahau.
Hayo ni matata
Mambo hukutizama mara mbili mbili
Nawe sharuti utazame kando
uwache yatendeke.
                Usitafute vita.
Usipopita
Huenda ukakuta
maisha mema ya kufuata
ukahifadhi mawazo yako
ukaendelea na kazi yako
ukafa kishujaa nchini mwako
lakini mengi huenda yakakupita
mengi yakakupofua, upofu ukakupata
kwa gharama gani? Sijui.
Mlango wenyewe
haumuahidi mtu kitu
Ni mlango tu!
Mimi Ni Mimi
Waniita mkomunisti
Waniita mkapitalisti
Waniita mnashinalisti
Na mimi ni binadamu tu,
Kwani hilo halitoshi?
 
Nchi zinajiwakia
Mamama wakiomboleza, wakilia
Tumbi ya watoto wakiumia
na maneno yote tunayotumia
            kuuana na kuangamia
 
Ewe mto
Tumesimama pambizoni mwako
machozi yakitudondoka
            yakichanganyika moyoni mwako.
Nilivuka
Nimevuka mabara kuja Afrika
Lakini siku katu haikufika
            ya milima kuwa vilima
            ya mito kuwa vijito
            vya kuweza kudakiika.
Sijakufikia mpenzi
kama kwamba u nyota ya mbali
kama kwamba umemea baina yetu
            ukuta wa usingizi.
Nikikushika, mikono huwa haishiki
ila maiti ilokufa bila haki
            kama kukumbatia damu yangu jiweni
            katika nyumba iloghariki kwa tufani
            ambayo usiku wake umesimama makini
            na asubuhi yake imekwama mbali
                                                                        ikisubiri njiani.
 
Miaka imenyumbuka baina yetu: damu na moto,
Daraja nikazikwea zilogeuka ukuta
Na wewe, ukazama chini baharini
                                                            nisiweze kukugusa.
Mashaza yakanichuna, yakikata mishipa
                                                            ya mikono yangu,
Nami nikaita:
            Ewe Afrika
            mpenzi wa roho yangu,
            mwenzi wa mabuu na giza,
            Nimezunguka miaka mingi kukutafuta
            na safari yangu bado haijakatika
            ewe maiti ulojifinika kwa yako maisha.
 
Nimevuka mabara kuja Afrika
lakini siku katu haikufika
ya daraja kuweza kuvukika.
Ewe ulalaye nami kitandani
U kama nyota ya mbali mbinguni
ulo milango ilofungwa kwa ndani
Nami nimesimama nje
                                    nasubiri baridini.
Kifungoni
Kwa kuangulia juu mbinguni
na kulia sana kwa matumaini
samawati imeingia
                              mwangu machoni.
Kwa kuota mahindi mashambani
na kulia sana kwa mahuzuni
manjano imeingia
                              mwangu machoni.
 
Waache majemadari waende vitani
Wapenzi waende bustanini
Na waalimu mwao darasani,
            Ama mimi, tasubihi nipeni
            Na kiti cha kale, za zamani
            Niwe vivi nilivyo duniani:
                        bawabu mlangoni
                        katika kingo ya maumivu ya ndani
            maadamu vitabu, sheria na zote dini
zitanihakikishia mauti
                                    nikiwa na njaa au kifungoni.
Kizuizini
Nikiwa na njaa na matambara mwilini
          nimehudumika kama hayawani
Kupigwa na kutukanwa
          kimya kama kupita kwa shetani.
Nafasi ya kupumzika hakuna
          ya kulala hakuna
          ya kuwaza hakuna.
Basi kwani hili kufanyika.
Ni kosa gani lilotendeka
Liloniletea adhabu hii isomalizika?
Ewe mwewe urukae juu mbinguni
          wajua lililomo mwangu moyoni.
Niambie: pale mipunga inapopepea
           ikitema miale ya jua
Mamaangu bado angali amesimama akinisubiri?
Je nadhari yake hujitokeza usoni
           ikielekea huku kizuizini?
Mpenzi mama, nitarudi nyumbani
Nitarudi kama hata ni kifoni
Hata kama maiti yangu imekatikakatika
           vipande elfu, elfu kumi
           Nitarudi nyumbani
Nikipenya kwenye ukuta huu
nikipitia mwingine kama shetani,
Nitarudi mpenzi mama ....
                                      hata kama ni kifoni.
Bega kwa bega
Baridi kutoka mlima mwa Kenya inaingia
Na upepo unavuma, misitu ya Nyandarua ukipasua
Lakini mimi ni mwanamke wa Kirinyaga
                baridi sitaisikia
                chochote sitakisikia
     isipokuwa sauti ya ardhi yetu
                                nchi yetu
                                polepole ikinililia.
Nyumbani...
                kuponda unga kunatusubiri
                kuchuna mboga kunatusubiri
                kuchanja kuni kunatusubiri
                na watoto
                                watoto si haba
                                                                nao pia wanatusubiri.
Lakini kumfuata mume wangu naendelea
                nchi yangu kuipigania
                utu wangu kujirudishia.
Lala mwanangu lala
                                        lala unono ukinisubiri.
Mwezi utakapoinama
                                           nitarudi, nikulinde nikuamiri
                Juu ya milima
                mwezi umejaa, umechotama
                kwa huruma ukitutazama.
Njia ni ndefu mno
Muda ni mfupi mno
                  lakini kumfuata mume wangu naendelea
                  bega kwa bega nasogea
                  utu kuukomboa.
Sauti?
Shingo zetu zimechongoka
            asubuhi kuilekea
lakini usiku wasogea
            ukichimba misingi ya nyumba,
                      na ukuta wa dakika nyumba
                      kuizunguka.
 
Kifo kimeadhimishwa
na ule wakati uliotandazika
                      mpaka
kila cha zamani kimesahaulika
isipokuwa majani makavu yalokauka
Mitini, mara kwa mara, yakitingisika
 
   Ati n'nani aliyesikia sauti?
   Kama kwamba kuna mtu huko mbinguni
wa kutulipia damu yetu iliyomwagwa
            na kumwagika
Mkata wa maneno
Zacheka nami zangu chekeo
               zacheka zafurahika
Sina mawazo    kichwani leo
               Bado hayajarauka ...
 
Nadhani ni asubuhi
               imeanza kuchipuka
Nayo ndiyo sababu
               ya moyo kuliwazika
na huu mdundo mtamu
               mwema ulotandazika
 
Najichekea ... kwani najua vyema
kwamba sijazoea hali hii tabasama
ijitembezayo kwa shairi na kwa ngoma
ikichezacheza nami ... ikininyegeza kama mke na mume
                                                          kama wapenzi daima
 
Najua sijaizoea hali hii ya furaha na shauku
                ijigambayo kwa mchana na usiku
                kufuata mtindo wa manju kila siku
                ... kufuata anasa za dunia
 
Ndipo nikawa mkata...
              mkata wa maneno ya furaha na amani
                                            ya mahaba au dini
maneno ya kufifisha kisasi cha mja
                juu ya maisha duniani
                maneno ya kushinda vita vya nyoyoni
                hivyo vita vya ndani kwa ndani.
 
Neno langu ni maumivu tu, ni mashaka
Ndipo kapendelea mwenendo wa kale ...
                                                                 fikira kutoziandika.
Niguse
Nitakapo kizuizini
Nitamwomba yoyote mwendani
            aniguse
                        taratibu
                        polepole
                                    lakini
                                    kwa yakini!
 
Niguse tena
Unijuze tena
Unifunze tena
                        maisha yalivyo
                        maisha yaonjavyo
                                                ladha yake ilivyo
 
Nipo hapa nimekukabili
Niguse tena tafadhali!
Niguse!
Niguse!
UNFO
Lanciato il 9/1/2016

More Related Content

Viewers also liked

Civiltá - Enciclopedia Einaudi [1982]
Civiltá - Enciclopedia Einaudi [1982]Civiltá - Enciclopedia Einaudi [1982]
Civiltá - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 
Cervello - Enciclopedia Einaudi [1982]
Cervello - Enciclopedia Einaudi [1982]Cervello - Enciclopedia Einaudi [1982]
Cervello - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 
Corpo - Enciclopedia Einaudi [1982]
Corpo - Enciclopedia Einaudi [1982]Corpo - Enciclopedia Einaudi [1982]
Corpo - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 
Teoria_modello - Enciclopedia Einaudi [1982]
Teoria_modello - Enciclopedia Einaudi [1982]Teoria_modello - Enciclopedia Einaudi [1982]
Teoria_modello - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 
Testo - Enciclopedia Einaudi [1982]
Testo - Enciclopedia Einaudi [1982]Testo - Enciclopedia Einaudi [1982]
Testo - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 
ARTI - Enciclopedia Einaudi [1982]
ARTI - Enciclopedia Einaudi [1982]ARTI - Enciclopedia Einaudi [1982]
ARTI - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 
ARGOMENTAZIONE - Enciclopedia Einaudi [1982]
ARGOMENTAZIONE - Enciclopedia Einaudi [1982]ARGOMENTAZIONE - Enciclopedia Einaudi [1982]
ARGOMENTAZIONE - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 
ANTHROPOS - Enciclopedia Einaudi [1982]
ANTHROPOS - Enciclopedia Einaudi [1982]ANTHROPOS - Enciclopedia Einaudi [1982]
ANTHROPOS - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 
Uomo - Enciclopedia Einaudi [1982]
Uomo - Enciclopedia Einaudi [1982]Uomo - Enciclopedia Einaudi [1982]
Uomo - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 
Universo - Enciclopedia Einaudi [1982]
Universo - Enciclopedia Einaudi [1982]Universo - Enciclopedia Einaudi [1982]
Universo - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 
Ereditá - Enciclopedia Einaudi [1982]
Ereditá - Enciclopedia Einaudi [1982]Ereditá - Enciclopedia Einaudi [1982]
Ereditá - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 
Concetto - Enciclopedia Einaudi [1982]
Concetto - Enciclopedia Einaudi [1982]Concetto - Enciclopedia Einaudi [1982]
Concetto - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 
Calcolo - Enciclopedia Einaudi [1982]
Calcolo -  Enciclopedia Einaudi [1982]Calcolo -  Enciclopedia Einaudi [1982]
Calcolo - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 
Classi - Enciclopedia Einaudi [1982]
Classi - Enciclopedia Einaudi [1982]Classi - Enciclopedia Einaudi [1982]
Classi - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 
Regione - Enciclopedia Einaudi [1982]
Regione - Enciclopedia Einaudi [1982]Regione - Enciclopedia Einaudi [1982]
Regione - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 
Mythos_Logos - Enciclopedia Einaudi [1982]
Mythos_Logos - Enciclopedia Einaudi [1982]Mythos_Logos - Enciclopedia Einaudi [1982]
Mythos_Logos - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 
Orale_scritto - Enciclopedia Einaudi [1982]
Orale_scritto - Enciclopedia Einaudi [1982]Orale_scritto - Enciclopedia Einaudi [1982]
Orale_scritto - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 
Religione - Enciclopedia Einaudi [1982]
Religione - Enciclopedia Einaudi [1982]Religione - Enciclopedia Einaudi [1982]
Religione - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 
Normale_anormale - Enciclopedia Einaudi [1982]
Normale_anormale - Enciclopedia Einaudi [1982]Normale_anormale - Enciclopedia Einaudi [1982]
Normale_anormale - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 
Conoscenza - Enciclopedia Einaudi [1982]
Conoscenza - Enciclopedia Einaudi [1982]Conoscenza - Enciclopedia Einaudi [1982]
Conoscenza - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 

Viewers also liked (20)

Civiltá - Enciclopedia Einaudi [1982]
Civiltá - Enciclopedia Einaudi [1982]Civiltá - Enciclopedia Einaudi [1982]
Civiltá - Enciclopedia Einaudi [1982]
 
Cervello - Enciclopedia Einaudi [1982]
Cervello - Enciclopedia Einaudi [1982]Cervello - Enciclopedia Einaudi [1982]
Cervello - Enciclopedia Einaudi [1982]
 
Corpo - Enciclopedia Einaudi [1982]
Corpo - Enciclopedia Einaudi [1982]Corpo - Enciclopedia Einaudi [1982]
Corpo - Enciclopedia Einaudi [1982]
 
Teoria_modello - Enciclopedia Einaudi [1982]
Teoria_modello - Enciclopedia Einaudi [1982]Teoria_modello - Enciclopedia Einaudi [1982]
Teoria_modello - Enciclopedia Einaudi [1982]
 
Testo - Enciclopedia Einaudi [1982]
Testo - Enciclopedia Einaudi [1982]Testo - Enciclopedia Einaudi [1982]
Testo - Enciclopedia Einaudi [1982]
 
ARTI - Enciclopedia Einaudi [1982]
ARTI - Enciclopedia Einaudi [1982]ARTI - Enciclopedia Einaudi [1982]
ARTI - Enciclopedia Einaudi [1982]
 
ARGOMENTAZIONE - Enciclopedia Einaudi [1982]
ARGOMENTAZIONE - Enciclopedia Einaudi [1982]ARGOMENTAZIONE - Enciclopedia Einaudi [1982]
ARGOMENTAZIONE - Enciclopedia Einaudi [1982]
 
ANTHROPOS - Enciclopedia Einaudi [1982]
ANTHROPOS - Enciclopedia Einaudi [1982]ANTHROPOS - Enciclopedia Einaudi [1982]
ANTHROPOS - Enciclopedia Einaudi [1982]
 
Uomo - Enciclopedia Einaudi [1982]
Uomo - Enciclopedia Einaudi [1982]Uomo - Enciclopedia Einaudi [1982]
Uomo - Enciclopedia Einaudi [1982]
 
Universo - Enciclopedia Einaudi [1982]
Universo - Enciclopedia Einaudi [1982]Universo - Enciclopedia Einaudi [1982]
Universo - Enciclopedia Einaudi [1982]
 
Ereditá - Enciclopedia Einaudi [1982]
Ereditá - Enciclopedia Einaudi [1982]Ereditá - Enciclopedia Einaudi [1982]
Ereditá - Enciclopedia Einaudi [1982]
 
Concetto - Enciclopedia Einaudi [1982]
Concetto - Enciclopedia Einaudi [1982]Concetto - Enciclopedia Einaudi [1982]
Concetto - Enciclopedia Einaudi [1982]
 
Calcolo - Enciclopedia Einaudi [1982]
Calcolo -  Enciclopedia Einaudi [1982]Calcolo -  Enciclopedia Einaudi [1982]
Calcolo - Enciclopedia Einaudi [1982]
 
Classi - Enciclopedia Einaudi [1982]
Classi - Enciclopedia Einaudi [1982]Classi - Enciclopedia Einaudi [1982]
Classi - Enciclopedia Einaudi [1982]
 
Regione - Enciclopedia Einaudi [1982]
Regione - Enciclopedia Einaudi [1982]Regione - Enciclopedia Einaudi [1982]
Regione - Enciclopedia Einaudi [1982]
 
Mythos_Logos - Enciclopedia Einaudi [1982]
Mythos_Logos - Enciclopedia Einaudi [1982]Mythos_Logos - Enciclopedia Einaudi [1982]
Mythos_Logos - Enciclopedia Einaudi [1982]
 
Orale_scritto - Enciclopedia Einaudi [1982]
Orale_scritto - Enciclopedia Einaudi [1982]Orale_scritto - Enciclopedia Einaudi [1982]
Orale_scritto - Enciclopedia Einaudi [1982]
 
Religione - Enciclopedia Einaudi [1982]
Religione - Enciclopedia Einaudi [1982]Religione - Enciclopedia Einaudi [1982]
Religione - Enciclopedia Einaudi [1982]
 
Normale_anormale - Enciclopedia Einaudi [1982]
Normale_anormale - Enciclopedia Einaudi [1982]Normale_anormale - Enciclopedia Einaudi [1982]
Normale_anormale - Enciclopedia Einaudi [1982]
 
Conoscenza - Enciclopedia Einaudi [1982]
Conoscenza - Enciclopedia Einaudi [1982]Conoscenza - Enciclopedia Einaudi [1982]
Conoscenza - Enciclopedia Einaudi [1982]
 

More from sabbioso

Catherine Douay_Daniel Roulland - Le mots de Gustave Guillaume [1990]
Catherine Douay_Daniel Roulland - Le mots de Gustave Guillaume [1990]Catherine Douay_Daniel Roulland - Le mots de Gustave Guillaume [1990]
Catherine Douay_Daniel Roulland - Le mots de Gustave Guillaume [1990]sabbioso
 
Appunti di ( Ki)swahili - CLASSI NOMINALI
Appunti di ( Ki)swahili - CLASSI NOMINALIAppunti di ( Ki)swahili - CLASSI NOMINALI
Appunti di ( Ki)swahili - CLASSI NOMINALIsabbioso
 
3di3 dizionario italiano_malgascio
3di3 dizionario italiano_malgascio3di3 dizionario italiano_malgascio
3di3 dizionario italiano_malgasciosabbioso
 
2di3 Dizionario Malgascio_italiano (M > Z)
2di3 Dizionario Malgascio_italiano (M > Z)2di3 Dizionario Malgascio_italiano (M > Z)
2di3 Dizionario Malgascio_italiano (M > Z)sabbioso
 
1di3 Dizionario malgascio_italiano (A > L)
1di3 Dizionario malgascio_italiano (A > L)1di3 Dizionario malgascio_italiano (A > L)
1di3 Dizionario malgascio_italiano (A > L)sabbioso
 
Appunti di ( ki)swahili il verbo 2 - unfo
Appunti di ( ki)swahili   il verbo 2 - unfoAppunti di ( ki)swahili   il verbo 2 - unfo
Appunti di ( ki)swahili il verbo 2 - unfosabbioso
 
Appunti di ( ki)swahili il verbo 1 - unfo
Appunti di ( ki)swahili   il verbo 1 - unfoAppunti di ( ki)swahili   il verbo 1 - unfo
Appunti di ( ki)swahili il verbo 1 - unfosabbioso
 
Appunti di ( ki)swahili corso - unfo
Appunti di ( ki)swahili   corso - unfoAppunti di ( ki)swahili   corso - unfo
Appunti di ( ki)swahili corso - unfosabbioso
 
Appunti di ( ki)swahili il locativo - unfo
Appunti di ( ki)swahili   il locativo - unfoAppunti di ( ki)swahili   il locativo - unfo
Appunti di ( ki)swahili il locativo - unfosabbioso
 
Appunti per un corso di malgascio unfo
Appunti per un corso di malgascio   unfoAppunti per un corso di malgascio   unfo
Appunti per un corso di malgascio unfosabbioso
 
Appunti di indonesiano (bahasa indonesia) unfo
Appunti di indonesiano (bahasa indonesia)   unfoAppunti di indonesiano (bahasa indonesia)   unfo
Appunti di indonesiano (bahasa indonesia) unfosabbioso
 
Come sette sarti andarono alla guerra coi turchi
Come sette sarti andarono alla guerra coi turchiCome sette sarti andarono alla guerra coi turchi
Come sette sarti andarono alla guerra coi turchisabbioso
 
Vita_morte - Enciclopedia Einaudi [1982]
Vita_morte - Enciclopedia Einaudi [1982]Vita_morte - Enciclopedia Einaudi [1982]
Vita_morte - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 
Visione - Enciclopedia Einaudi [1982]
Visione - Enciclopedia Einaudi [1982]Visione - Enciclopedia Einaudi [1982]
Visione - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 
Tradizioni - Enciclopedia Einaudi [1982]
Tradizioni - Enciclopedia Einaudi [1982]Tradizioni - Enciclopedia Einaudi [1982]
Tradizioni - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 
Tonale_atonale - Enciclopedia Einaudi [1982]
Tonale_atonale - Enciclopedia Einaudi [1982]Tonale_atonale - Enciclopedia Einaudi [1982]
Tonale_atonale - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 
Tolleranza_intolleranza - Enciclopedia Einaudi [1982]
Tolleranza_intolleranza - Enciclopedia Einaudi [1982]Tolleranza_intolleranza - Enciclopedia Einaudi [1982]
Tolleranza_intolleranza - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 
Tempo_temporalitá - Enciclopedia Einaudi [1982]
Tempo_temporalitá - Enciclopedia Einaudi [1982]Tempo_temporalitá - Enciclopedia Einaudi [1982]
Tempo_temporalitá - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 
Sviluppo_sottosviluppo - Enciclopedia Einaudi [1982]
Sviluppo_sottosviluppo - Enciclopedia Einaudi [1982]Sviluppo_sottosviluppo - Enciclopedia Einaudi [1982]
Sviluppo_sottosviluppo - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 
Strutture matematiche - Enciclopedia Einaudi [1982]
Strutture matematiche - Enciclopedia Einaudi [1982]Strutture matematiche - Enciclopedia Einaudi [1982]
Strutture matematiche - Enciclopedia Einaudi [1982]sabbioso
 

More from sabbioso (20)

Catherine Douay_Daniel Roulland - Le mots de Gustave Guillaume [1990]
Catherine Douay_Daniel Roulland - Le mots de Gustave Guillaume [1990]Catherine Douay_Daniel Roulland - Le mots de Gustave Guillaume [1990]
Catherine Douay_Daniel Roulland - Le mots de Gustave Guillaume [1990]
 
Appunti di ( Ki)swahili - CLASSI NOMINALI
Appunti di ( Ki)swahili - CLASSI NOMINALIAppunti di ( Ki)swahili - CLASSI NOMINALI
Appunti di ( Ki)swahili - CLASSI NOMINALI
 
3di3 dizionario italiano_malgascio
3di3 dizionario italiano_malgascio3di3 dizionario italiano_malgascio
3di3 dizionario italiano_malgascio
 
2di3 Dizionario Malgascio_italiano (M > Z)
2di3 Dizionario Malgascio_italiano (M > Z)2di3 Dizionario Malgascio_italiano (M > Z)
2di3 Dizionario Malgascio_italiano (M > Z)
 
1di3 Dizionario malgascio_italiano (A > L)
1di3 Dizionario malgascio_italiano (A > L)1di3 Dizionario malgascio_italiano (A > L)
1di3 Dizionario malgascio_italiano (A > L)
 
Appunti di ( ki)swahili il verbo 2 - unfo
Appunti di ( ki)swahili   il verbo 2 - unfoAppunti di ( ki)swahili   il verbo 2 - unfo
Appunti di ( ki)swahili il verbo 2 - unfo
 
Appunti di ( ki)swahili il verbo 1 - unfo
Appunti di ( ki)swahili   il verbo 1 - unfoAppunti di ( ki)swahili   il verbo 1 - unfo
Appunti di ( ki)swahili il verbo 1 - unfo
 
Appunti di ( ki)swahili corso - unfo
Appunti di ( ki)swahili   corso - unfoAppunti di ( ki)swahili   corso - unfo
Appunti di ( ki)swahili corso - unfo
 
Appunti di ( ki)swahili il locativo - unfo
Appunti di ( ki)swahili   il locativo - unfoAppunti di ( ki)swahili   il locativo - unfo
Appunti di ( ki)swahili il locativo - unfo
 
Appunti per un corso di malgascio unfo
Appunti per un corso di malgascio   unfoAppunti per un corso di malgascio   unfo
Appunti per un corso di malgascio unfo
 
Appunti di indonesiano (bahasa indonesia) unfo
Appunti di indonesiano (bahasa indonesia)   unfoAppunti di indonesiano (bahasa indonesia)   unfo
Appunti di indonesiano (bahasa indonesia) unfo
 
Come sette sarti andarono alla guerra coi turchi
Come sette sarti andarono alla guerra coi turchiCome sette sarti andarono alla guerra coi turchi
Come sette sarti andarono alla guerra coi turchi
 
Vita_morte - Enciclopedia Einaudi [1982]
Vita_morte - Enciclopedia Einaudi [1982]Vita_morte - Enciclopedia Einaudi [1982]
Vita_morte - Enciclopedia Einaudi [1982]
 
Visione - Enciclopedia Einaudi [1982]
Visione - Enciclopedia Einaudi [1982]Visione - Enciclopedia Einaudi [1982]
Visione - Enciclopedia Einaudi [1982]
 
Tradizioni - Enciclopedia Einaudi [1982]
Tradizioni - Enciclopedia Einaudi [1982]Tradizioni - Enciclopedia Einaudi [1982]
Tradizioni - Enciclopedia Einaudi [1982]
 
Tonale_atonale - Enciclopedia Einaudi [1982]
Tonale_atonale - Enciclopedia Einaudi [1982]Tonale_atonale - Enciclopedia Einaudi [1982]
Tonale_atonale - Enciclopedia Einaudi [1982]
 
Tolleranza_intolleranza - Enciclopedia Einaudi [1982]
Tolleranza_intolleranza - Enciclopedia Einaudi [1982]Tolleranza_intolleranza - Enciclopedia Einaudi [1982]
Tolleranza_intolleranza - Enciclopedia Einaudi [1982]
 
Tempo_temporalitá - Enciclopedia Einaudi [1982]
Tempo_temporalitá - Enciclopedia Einaudi [1982]Tempo_temporalitá - Enciclopedia Einaudi [1982]
Tempo_temporalitá - Enciclopedia Einaudi [1982]
 
Sviluppo_sottosviluppo - Enciclopedia Einaudi [1982]
Sviluppo_sottosviluppo - Enciclopedia Einaudi [1982]Sviluppo_sottosviluppo - Enciclopedia Einaudi [1982]
Sviluppo_sottosviluppo - Enciclopedia Einaudi [1982]
 
Strutture matematiche - Enciclopedia Einaudi [1982]
Strutture matematiche - Enciclopedia Einaudi [1982]Strutture matematiche - Enciclopedia Einaudi [1982]
Strutture matematiche - Enciclopedia Einaudi [1982]
 

Poesia Swahili [Euphrase Kezilahabi_Kithaka wa Mberia_Alamin Mazrui]

  • 2. INDICE EUPHRASE KEZILAHABI 3 Upepo wa Wakati 4 Mafuriko 5 Mgomba 6 Chai ya Jioni 7 Fasihi 8 Kisima KITHAKA wa MBERIA 9 Jumapili ya Damu ALAMIN MAZRUI 12 Mlango 13 Mimi Ni Mimi 14 Nilivuka 15 Kifungoni 16 Kizuizini 17 Bega kwa bega 18 Sauti? 19 Mkata wa maneno 20 Niguse
  • 3. EUPHRASE KEZILAHABI Upepo wa Wakati Juu ya mlima mdogo Siku moja nilisimama. Nikatazama chini ziwani, siku Ya dhoruba. Halafu niliona mawimbi Yakipanda na kushuka. Yakivimba, Yakiviringika, yakigongana na kutoa povu Kama fahari wehu katika bonde lisomajani. Yalivyotengenezwa! Yalivyofifia na kuanza tena! Kamwe sikuona. Lakini niliyaona yakishuka kwa nguvu Na kupanda haraka, yakisukumwa Na upepo wa Magharibi na Mashariki. Hivyo ndivyo ulimwengu ulivyo. Na hivyo maisha ya binadamu. Wanapanda na kushuka Wakisukumwa na upepo na wakati. Tazama wanavyojinyakulia madaraka Kama mzamaji, mguu wa rafikiye, ashikavyo! Wanavyoshika pesa kama mtoto Na picha ya bandia Au asikari mwehu na bunduki yake Na kutunyamazisha! Watapanda na kushuka Na wataanguka kweli! Wakisukumwa na upepo wa wakati!
  • 4. Mafuriko Nitaandika wimbo juu ya mbawa za nzi Utoe muziki arukapo wausikie walio wengi Ushairi wa jalalani utaimbwa Juu ya vidonda vya wakulima Na usaha ulio jasho lao. Nitaandika juu ya mbawa za wadudu Wote warukao Juu ya mistari ya pundamilia Na masikio makubwa ya tembo. Juu ya kuta vyooni, maofisini, madarasani, Juu ya paa za nyumba, kuta za Ikulu, Na juu ya khanga na tisheti. Nitaandika wimbo huu: Mafuriko ya mwaka huu Yatishia nyumba kongwe bondeni. Waliomo wameanza kuihama Na miti ya umeme imeanguka. Palipokuwa na mwanga, sasa giza. Mafuriko ya mwaka huu! Mti mkongwe umelalia upande Wa nyumba zetu hafifu. Upepo mkali uvumapo hatulali. Kila kukicha twatazama mizizi yake Na mkao wake, na kuta hafifu za nyumba. Lazima ukatwe kuanzia matawi hadi shina Mafuriko ya mwaka huu yaashiria... Tutabaki kuwasimulia wajukuu: Mwaka ule wa mafuriko Miti mingi mikongwe ilianguka. Mafuriko ya mwaka huu! Wengi wataumbuka.
  • 5. Mgomba Mgomba umelala chini: hauna faida tena, Baada ya kukatwa na wafanya kazi Wa bustani kwa kusita. Watoto, kwa wasiwasi wanasubiri wakati wao Bustanini hakuna kitu Isipokuwa upepo fulani wenye huzuni, Unaotikisa majani na kutoa sauti ya kilio.  Hivyo ndivyo ufalme wa mitara ulivyo. Mti wa mji umelala chini: hauna faida tena, Baada ya kukatwa na wafanya kazi Wa bustani kwa kusita. Chumbani hakuna kitu Isipokuwa upepo fulani wenye huzuni utingishao Wenye hila waliokizunguka kitanda na kulia. Machozi yenye matumaini yapiga Mbiu ya hatari ya magomvi nyumbani.            Magomvi Kati ya wanawake            Magomvi Kati ya watoto kwa ajili ya vitu na uongozi. Ole! Milki ya 'Lexanda imekwisha!   Vidonda vya ukoma visofunikwa Ambavyo kwa mda mrefu vilifichama Sasa viko nje kufyonzwa na inzi wa kila aina Na vinanuka vibaya. Lakini inzi kila mara hufyonza wakifikiri Nani watamwambukiza.
  • 6. Chai ya Jioni Wakati tunywapo chai hapa upenuni Na kuwatazama watoto wetu Wakicheza bembea kwa furaha Tujue kamba ya bembea yetu Imeshalika na imeanza kuoza Na bado kidogo tutaporomoka. Kulikuwa na wakati ulinisukuma juu Nikaenda zaidi ya nusu duara; Kulikuwa na wakati nilikudaka Ulipokaribia kuanguka, Na kulikuwa na wakati tulibebana kwa zamu Mmoja wima akisukuma mwingine amekaa. Wakati huo, japo tulipaa mbele na nyuma Tulicheka kwa matumaini yaliyotiwa chumvi Na kisha tukaongozana jikoni kupika chajio; Ilikuwa adhuhuri yetu. Sasa tukisubiri ndoto tusizoweza kutekeleza tena Tumalizie machicha ya chai yetu ya jioni Bila kutematema na kwa tabasamu. Baada ya hapo tujilambelambe utamuutamu Uliobakia kwenye midomo yetu, Tukikumbuka siku ilee ya kwanza Tulipokutana jioni chini ya mwembe Tukitafuta tawi zuri gumu La kufunga bembea yetu Naye mbwa Simba akikusubiri. Lakini kabla hatujaondoka kimyakimya Kukamilika nusu duara iliyobakia. Tuhakikishe vikombe vyetu ni safi.
  • 7. Fasihi Maneno yangu kumeza tena sasa siwezi. Lakini kuonyesha ukweli na kuutafuta Nitaendelea: mimi ni kama boga. Nimepandwa katikati, bustanini, Na kama boga nitatambaa chini Zote pande, kuikwea miti ya hekima Na yote magugu koo kuyakaba. Bila woga, bila nyuma kurudi nitashambulia Ya binadamu matendo bado yakihema.             Halafu wakati             Ujao utafika             Matunda nitatoa             Makubwa madogo             Mazuri mabaya Wakati utafika watakapokuja wajuzi Kwa jembe la wino kunipalia. Wala mboga za majani watanichuma. Utafika, wa maboga kuwa mikata. Machafu na safi yatachotwa Na nitaingia mitungi ya kila mji-shamba. Watoto mikononi mwao watanichezea. Chini wataniangusha na kunipasua. Lakini mbegu, mbegu zitabaki.             Mimi ninajua             Hatari sina             Wajibu msomaji             Mjini na shamba             Vizuri kunichambua. Halafu utafika ule wakati Watumia vikombe dhahabu na glasi Pembeni kwa chuki kunitupa, Na nitakuwa nyuma ya wakati Lakini wakisahau wahenga Kata na mboga walitumia Msingi wa wao utamaduni Watakuwa wameutupa. Kumbukeni, kumbukeni, kumbukeni.
  • 8. Kisima Kisima cha maji ya uzima ki wazi Na vyura katika bonde la taaluma watuita Tujongee kwa mahadhi yao Yaongozayo pandikizi la mtu Kwa hatua ndefu litembealo Na sindano ya shaba kitovuni Upinde na mishale mkononi Kisha likapiga goti kisimani Tayari kumfuma akaribiaye Maana shujaa hafi miongoni mwa wezi Bali kama simba mawindoni. Hatuwezi tena kuteka maji Na kalamu zetu zimekauka wino. Nani atamsukuma kwa kalamu Aitwe shujaa wa uwongo! Aliyeitia kitovuni kwa hofu Ingawa tegemeo hakulipata Alifungua mlango uelekeao Katikati ya ujuzi na urazini mpya Mwanzo wa kizazi tukionacho.
  • 9. KITHAKA wa MBERIA Jumapili ya Damu I  Midundo ya Reggae Inarindima hewani Na kuchanganyika Na macheo   Katika jiji Vioo, madirisha Na milango Inasalimu amri Kutoka kumbo kali Za wenye njaa Na matarajio Ya miongo miwili.   Ndani ya maduka Mawimbi ya watu Yanapaa, kushuka Na kupanda kwingineko Huku rafu na kuta Zikibadilika sura Kama tanzu za miti Kiangazi kinapojiri.   Vifaa vya kila ukoo Nguo za kila rangi Zinaketi vichwani Kuninginia mikononi Kulala migongoni Au kubanwa kwapani Zikibadili makazi Na umiliki.  
  • 10. II   Risasi Zinaanza kupiga miluzi Na kwa ghadhabu Kushtua kuta Milingoti ya stima Magari ya rangirangi Na nyama na mifupa   Watu wanaterereka Damu inatiririka Uhai unaporomoka   III   Ghafla Midundo ya Reggae Inakauka Na nyimbo za jana Kurudi angani Kama uvundo ambao Umevamia pua tena Baada ya kuangushwa Na kumbo la upepo   Kutoka mwangu jikoni Barabara ni dhahiri- Magari ya rangirangi Vifaru vya madoadoa Vinatiririka kama mto, Bunduki zinalenga kushoto Kulia, nyuma na mbele Nayo mizinga hatari Inatega mbingu; Huu mtiririko Ni safari ya marejeo Anarejea mungu-wa-kinamo Kwenye ulingo.  
  • 11. IV   Katika fahamu Mawazo mbalimbali Yanapita kwa zamu Kama vipepeo na nondo Wakipita kwa makundi Mbele ya macho; Kwa tabasamu Nakumbuka Obasanjo Na uamuzi wake angavu Bali pia Kwa huzuni Nakumbuka Bokassa na Amin, Na Mobutu na Doe, Na damu na mafuvu Matita ya mafuvu! Magurudumu ya mawazo Yanafikia njia panda Na kwa muda, kukwama Kabla ya kuanza safari tena Kwenye njia wazi Ya serikali ya kiraia Hata inapoongozwa Na genge la mazimwi
  • 12. ALAMIN MAZRUI Alamin Mazrui Mlango Ama utapita katika mlango huu au hutapita. Ukipita kuna hatari ya jinalo kulisahau. Hayo ni matata Mambo hukutizama mara mbili mbili Nawe sharuti utazame kando uwache yatendeke.                 Usitafute vita. Usipopita Huenda ukakuta maisha mema ya kufuata ukahifadhi mawazo yako ukaendelea na kazi yako ukafa kishujaa nchini mwako lakini mengi huenda yakakupita mengi yakakupofua, upofu ukakupata kwa gharama gani? Sijui. Mlango wenyewe haumuahidi mtu kitu Ni mlango tu!
  • 13. Mimi Ni Mimi Waniita mkomunisti Waniita mkapitalisti Waniita mnashinalisti Na mimi ni binadamu tu, Kwani hilo halitoshi?   Nchi zinajiwakia Mamama wakiomboleza, wakilia Tumbi ya watoto wakiumia na maneno yote tunayotumia             kuuana na kuangamia   Ewe mto Tumesimama pambizoni mwako machozi yakitudondoka             yakichanganyika moyoni mwako.
  • 14. Nilivuka Nimevuka mabara kuja Afrika Lakini siku katu haikufika             ya milima kuwa vilima             ya mito kuwa vijito             vya kuweza kudakiika. Sijakufikia mpenzi kama kwamba u nyota ya mbali kama kwamba umemea baina yetu             ukuta wa usingizi. Nikikushika, mikono huwa haishiki ila maiti ilokufa bila haki             kama kukumbatia damu yangu jiweni             katika nyumba iloghariki kwa tufani             ambayo usiku wake umesimama makini             na asubuhi yake imekwama mbali                                                                         ikisubiri njiani.   Miaka imenyumbuka baina yetu: damu na moto, Daraja nikazikwea zilogeuka ukuta Na wewe, ukazama chini baharini                                                             nisiweze kukugusa. Mashaza yakanichuna, yakikata mishipa                                                             ya mikono yangu, Nami nikaita:             Ewe Afrika             mpenzi wa roho yangu,             mwenzi wa mabuu na giza,             Nimezunguka miaka mingi kukutafuta             na safari yangu bado haijakatika             ewe maiti ulojifinika kwa yako maisha.   Nimevuka mabara kuja Afrika lakini siku katu haikufika ya daraja kuweza kuvukika. Ewe ulalaye nami kitandani U kama nyota ya mbali mbinguni ulo milango ilofungwa kwa ndani Nami nimesimama nje                                     nasubiri baridini.
  • 15. Kifungoni Kwa kuangulia juu mbinguni na kulia sana kwa matumaini samawati imeingia                               mwangu machoni. Kwa kuota mahindi mashambani na kulia sana kwa mahuzuni manjano imeingia                               mwangu machoni.   Waache majemadari waende vitani Wapenzi waende bustanini Na waalimu mwao darasani,             Ama mimi, tasubihi nipeni             Na kiti cha kale, za zamani             Niwe vivi nilivyo duniani:                         bawabu mlangoni                         katika kingo ya maumivu ya ndani             maadamu vitabu, sheria na zote dini zitanihakikishia mauti                                     nikiwa na njaa au kifungoni.
  • 16. Kizuizini Nikiwa na njaa na matambara mwilini           nimehudumika kama hayawani Kupigwa na kutukanwa           kimya kama kupita kwa shetani. Nafasi ya kupumzika hakuna           ya kulala hakuna           ya kuwaza hakuna. Basi kwani hili kufanyika. Ni kosa gani lilotendeka Liloniletea adhabu hii isomalizika? Ewe mwewe urukae juu mbinguni           wajua lililomo mwangu moyoni. Niambie: pale mipunga inapopepea            ikitema miale ya jua Mamaangu bado angali amesimama akinisubiri? Je nadhari yake hujitokeza usoni            ikielekea huku kizuizini? Mpenzi mama, nitarudi nyumbani Nitarudi kama hata ni kifoni Hata kama maiti yangu imekatikakatika            vipande elfu, elfu kumi            Nitarudi nyumbani Nikipenya kwenye ukuta huu nikipitia mwingine kama shetani, Nitarudi mpenzi mama ....                                       hata kama ni kifoni.
  • 17. Bega kwa bega Baridi kutoka mlima mwa Kenya inaingia Na upepo unavuma, misitu ya Nyandarua ukipasua Lakini mimi ni mwanamke wa Kirinyaga                 baridi sitaisikia                 chochote sitakisikia      isipokuwa sauti ya ardhi yetu                                 nchi yetu                                 polepole ikinililia. Nyumbani...                 kuponda unga kunatusubiri                 kuchuna mboga kunatusubiri                 kuchanja kuni kunatusubiri                 na watoto                                 watoto si haba                                                                 nao pia wanatusubiri. Lakini kumfuata mume wangu naendelea                 nchi yangu kuipigania                 utu wangu kujirudishia. Lala mwanangu lala                                         lala unono ukinisubiri. Mwezi utakapoinama                                            nitarudi, nikulinde nikuamiri                 Juu ya milima                 mwezi umejaa, umechotama                 kwa huruma ukitutazama. Njia ni ndefu mno Muda ni mfupi mno                   lakini kumfuata mume wangu naendelea                   bega kwa bega nasogea                   utu kuukomboa.
  • 18. Sauti? Shingo zetu zimechongoka             asubuhi kuilekea lakini usiku wasogea             ukichimba misingi ya nyumba,                       na ukuta wa dakika nyumba                       kuizunguka.   Kifo kimeadhimishwa na ule wakati uliotandazika                       mpaka kila cha zamani kimesahaulika isipokuwa majani makavu yalokauka Mitini, mara kwa mara, yakitingisika      Ati n'nani aliyesikia sauti?    Kama kwamba kuna mtu huko mbinguni wa kutulipia damu yetu iliyomwagwa             na kumwagika
  • 19. Mkata wa maneno Zacheka nami zangu chekeo                zacheka zafurahika Sina mawazo    kichwani leo                Bado hayajarauka ...   Nadhani ni asubuhi                imeanza kuchipuka Nayo ndiyo sababu                ya moyo kuliwazika na huu mdundo mtamu                mwema ulotandazika   Najichekea ... kwani najua vyema kwamba sijazoea hali hii tabasama ijitembezayo kwa shairi na kwa ngoma ikichezacheza nami ... ikininyegeza kama mke na mume                                                           kama wapenzi daima   Najua sijaizoea hali hii ya furaha na shauku                 ijigambayo kwa mchana na usiku                 kufuata mtindo wa manju kila siku                 ... kufuata anasa za dunia   Ndipo nikawa mkata...               mkata wa maneno ya furaha na amani                                             ya mahaba au dini maneno ya kufifisha kisasi cha mja                 juu ya maisha duniani                 maneno ya kushinda vita vya nyoyoni                 hivyo vita vya ndani kwa ndani.   Neno langu ni maumivu tu, ni mashaka Ndipo kapendelea mwenendo wa kale ...                                                                  fikira kutoziandika.
  • 20. Niguse Nitakapo kizuizini Nitamwomba yoyote mwendani             aniguse                         taratibu                         polepole                                     lakini                                     kwa yakini!   Niguse tena Unijuze tena Unifunze tena                         maisha yalivyo                         maisha yaonjavyo                                                 ladha yake ilivyo   Nipo hapa nimekukabili Niguse tena tafadhali! Niguse! Niguse! UNFO Lanciato il 9/1/2016