Successfully reported this slideshow.
We use your LinkedIn profile and activity data to personalize ads and to show you more relevant ads. You can change your ad preferences anytime.

0

Share

Download to read offline

Chuo kikuu cha mtakatifu agustino (autosaved)

Download to read offline

  • Be the first to like this

Chuo kikuu cha mtakatifu agustino (autosaved)

  1. 1. CHUO KIKUU CHA MTAKATIFU AGUSTINO CHA TANZANIA KITUO CHA BUKOBA KITOVU CHA ELIMU IDARA YA KISWAHILI. JINA LA KOZI: RIWAYA YA KISWAHILI. MSIMBO WA KOZI: SW 212 JINA LA MHADHIRI: MALUGU, A. JINA LA KIKUNDI: SCORPITON AINA YA KAZI: KAZI YA KIKUNDI. NAMBA JINA KAMILI NAMBA YA USAJILI SAHIHI 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. BENEDICTOR ADESA GODWINILENIDA KALIJA INNOCENT KERENGE MAAGE N. MHADISA ALFA P. MHILIMA LAURANCE MWITA MATWIGA E. NKOKO DOROFINA RANGSON RAPHAEL M SYLIVESTER BETNESS N BAED II 41464 BAED II 41499 BAED II 41538 BAED II 41544 BAED II 41606 BAED II 41607 BAED II 41640 BAED II 41648 BAED II 41659 BAED II 41683 Swali Bainisha ni vipi riwaya ya “kichwamaji” inastahili kuitwa riwaya ya Kifalsafa
  2. 2. Ama kuhusu maana ya riwaya, falsafa ya riwaya ya Kiswahili, wataalamu mbalimbali wamejaribu kufasili maana ya maneno hayo.Miongoni mwa wataalamu waliofasili dhana hizi ni pamoja na:- Wamitila(2003): 178), anasema kuwa riwaya ni kazi ya kinadharia au kibunilizi ambayohuwa na urefu wa kutosha,msukumo uliojengwa vizuri, wahusika wengi walioendelezwa kwa kina, yenye kuchukuwa muda mwingi katika maandalizi na kuhusisha madhari maalumu. Kamusi ya Kiswahili sanifu (2004) inafasili falsafa kuwa ni elimu ya asili, maana na sababu za mambo au vitu. Falsafa hujikita katika kutafuta ukweli juu ya mambo au vitu kupitia imani. Madumulla (2009:70), anasema kuwa riwaya ya kifalsafa ni riwaya ambayo inajadili migogoro ya maisha na kutafakari kwa mantiki na kwa kina kuhusu mambo ambayo urazini wake hauonekani kwa urahisi. Mwelekeo wa riwaya ya “Kichwa maji” Kichwa maji ni sawa na kusema debe tupu, hivyo dhana ya “kichwamaji” ni kufanya mambo ambayo hayaendani na upeo, umri au nafasi uliyonayo mtu katika jamii yake ambapo mtu huyo huwa anategemewa kuwa msaada mkubwa aidha kwa kutoa ushauri ama kuleta mabadiliko katika jamii yake kwa mfano katika riwaya hii ya” Kichwa maji” baadhi ya mhusika wamelinganishwa na dhana hii ya “Kichwamaji” ambapo mhusika kama Kazimoto katika (uk.194-195) anamwambia mke wake Sabina kwamba “hajui kwanini anaishi, pia anasema yeye hajijui na mke wake anamwambia kuwa “hakika sikufahamu kuwa wewe ni kichwa maji namna hiyo” Mara nyigine falsafa huchukuliwa kama njia pekee inayojaribu kueleza ulimwengu juu ya mafundisho pamoja na mambo mbalimbali ya kiimani ambayo yanafuatwa na mtu au kundi la watu kwa kutumia akili na mantiki dhabiti. “Kichwamaji”ni miongoni mwa riwaya ya kifalsafa, ni miongoni mwa kazi za kifalsafa iliyojikita na kuendana na mikondo ya nadharia ya kidhanaishi. Kwa hiyo basi tunakubaliana nakujadili ukweli kuwa riwaya ya “Kichwamaji”iliyoandikwa na E. Kezilahabi ni riwaya ya kifalsafa kwa kutumia riwaya hii tunajadili jinsi dhana mbalimbali zilivyojitokeza katika riwaya hii kama ifuatavyo: Dhana ya ukweli;katika kutafuta dhana hii yaani ukweli ni nini?tunaona mwandishi anajaribu kueleza falsafa yake ya kutaka kutafuta au kujua kukweli au mambo ambayo urazini wake hauonekani kirahisi. Kwa mfano katika riwaya hii ya “Kichwamaji”iliyoandikwa na E. Kazilahabi, tunaona mwandishi anapojaribu kujua ukweli wa mambo hasa anapomtumia mhusika Kazimoto ambaye anataka kujua ukweli juu ya mambo au matatizo yaliyo kuwa yakiwasibi ndugu zake. Kwa mfano katika (uk29-30)tunaona wanawake wanalia jikoni lakini hawakujua kilichokuwa kinawasibu, Rukia na mama yake pia wanamwagiwa mchanga juu ya vitanda vyao japokuwa ukweli wa mambo waliyokuwa wakifanyiwa hayakujulikana wazi kuwepo au kutokuwepo kwa wachawi, ingawa Kazimoto anaendelea kufikiri na kutafuta ukweli wa mambo hayo.
  3. 3. Dhana ya maisha ; Katika kujadili au kueleza dhana kuhusu maisha mwandishi anajaribu kuonesha mitazamo ya wahusika mbalimbali wanaojaribu kupambanua ukweli juu ya maisha yaani maisha ni nini? Kwa mfano katika (uk 84) Kazimoto anasema “maisha hayashibwi wala kuridhishwa,” pia katika (uk186) Manase anamwambia Kazimoto “maisha ni kifo cha polepole,kaburini hatua yetu ya mwisho tu, kwa hiyo kufa ni kuishi.”Kadharika mwandishi anamchora mhusika Rukia aliyekata tama ya maisha na baada ya kupata mimba ya kulazimishwa na manase, hivyo Rukia anaona maisha hayanamaana na ndiyo maana Kazimoto anaambiwa “ndugu yako mekufa akikulilia na aliomba umsamehe na amekuomba usisikitike sana hata yeye halikuwa haoni tena maana ya kuishi”. (uk83) kwa hiyo dhana ya maisha inatazwamwa katika mitazamo mbalimbali au tofauti tofauti. Dhana ya kifo;dhana hii imejitokeza na imejadiliwa katika riwaya hii “kichwamaji “ambapo mwandishi amejaribu kuchora wahusika mbalimbali namna wanavyokengeushwa na ukweli juu ya kifo. Kwa mfano mhusika Kazimoto anaamini kuwa kifo ni mstari usiokuwa na mwisho, katika (uk 123) anaposema “ninaamini kwamba kufa ni kugeuka hali, kama kufa ni kugeuka hali naamini kwamba kuna kugeuka kwingine kwa hali baada ya kufa, kugeuka na kugeuka. Ndiyo maana ya mstari usiokuwa na mwisho.”Pia mwandishi anamtumia mhusika Kazi motoanayesema kifo ni safari ya kwenda mbinguni kwani Kazimoto anasema “Lakini Kalia kabla ya kwenda mbinguni lazima nife,ndiyo Kalia anajibu” (uk 74).Kwa hiyo ukweli kuhusu kifo bado unaleta kukengeushi na katika falsafa ya watu kwani bado linachanguzwa katika namna tofautitofauti miongoni mwa watu. Dhana ya kuweko au kutokuwekokwa mungu au mambo fulani,dhana hii hujaribu kufafanua kuweko na kutokuweko mungu au mambo fulani. Dhana hii inajaribu kuthibitisha katika riwaya hii ya “kichwamaji” ambapo mwandishi anajaribu kuwatumia wahusika mbalimbali katika kukengeusha ukweli huu wa kuweko au kutokuweko kwa mungu na mambo mbalimbali.Kwa mfano katika (uk 180) Kazimoto haamini uwepo wa mungu baada ya kufiwa na mtoto wake anasema “Kama kweli mungu alikuwepo sikuweza kuona kwanini aliweza kufanya ukatiri mkubwa kama huu”. Pia Kazimoto hamwamini mungu pale alipokuwa anabishana na wazee alipokuwa akinywa pombe alipomtembelea Kamata(uk.51). Pia tunaona jinsi Kazimoto anavyomwoko Njuki aliyeanguka ndani ya maji(uk79) na hiyo inadhihirisha kuwa kila kitu au mtu ana mungu wake anayemsaidia. Dhana ya uzuri na ubaya ;Hii ni dhana inayojitokeza pia katika riwaya ya “Kichwamaji” kwani mwandishi anatumia wahusika wake mbalimbali wanaojaribu kutafuta ukweli juu ya uzuri na ubaya. Kwa mfano katika ( uk 128) kunamajibizano kati ya Manase na Salima juu ya uzuri na ubaya,wanasema “kwa hiyo wewe unaona kwamba mtu unaona kwamba mtu ana ubaya na mzuri? Nilimuuliza: Alinyamaza niliendelea kudadisi swaliililieleweki zaidi .Tuseme sisi hapa, wawili tunatazama picha ile moja pamoja, wewe unasema ni mzuri, mimi ninasema ni mbaya, Je, siyo kusema kwamba ile picha ina ubaya na uzuri? Nilimuuliza tena. Mimi ninaona kinyume alisema kwama wewe unaona ubaya, mimi nzuri ndiyo kuaema kwamba uzuri na ubaya umo mwetu sisi wenyewe na siyo ndani ya picha au kitu “ Dhana ya wema na ubaya ; katika kueleza falsafa kuhusumafundisho fulani katika jamii, mwandishi anajadili pia ukweli juu ya wema na ubaya hasa anapowatumia wahusika wake mbalimbali katika kupata ukweli juu ya dhana hii.Kwa mfano katika riwaya ya
  4. 4. “kichwamaji” mwandishi anamtumia mhusika mama na mtoto wake katika kueleza dhana ya wema na ubaya ambapo tunaona mama na mtoto wake peke yao wakizamishwa na kusukumiwa kisiwani na mtumbi waliokuwa wakisafiria, lakini kutokana na kukaa kwao kwa muda mrefu bila kupata chakula nawatu wa kuwaokoa ndipomwanamke anaamua kuchukuwa jiwe na kujiua ili mtoto apate chakula damu na mwili wake( uk 121 -122).Kwa hiyo katika kuelezea ukweli juu ya wema na ubaya, Mwandishi anaiacha dhana hii katika ukengeushi katika akiliza watu kwani huwaacha wakijiuliza maswali je huyu mama alitenda wema au ubaya? Kwa kuhitimisha; tunasema kuwa tofauti na dini au itikadi njia ya falsafa ni maantiki inayoelezea hatua zake ikiwa tayari kuchungulia upya kila hatua iliyochukua. Kwa hiyo falsafa ni nji ya maswali katika lugha ya kila siku kwani neno “falsafa” mara nyingi lina chukuliwa kutaja jumla ya mafundisho au imani ya mtu au kundi la watu. Kwa mfano “falsafa ya chama Fulani,”“falsafa ya maisha yangu” Lakini kwa ujumla fikra hizo hazistahili kuitwa “falsafa” ila tu kuna makundi ya wana”falsafa” wanopendelea mitazamo au mielekeo tofauti na kuhusu haya inawezekana kutumia neno”falsafa” ya fulani kwa kutaja matokeo ya kazi zake kwa mfano “falsafa”ya E. Kazilahabi katika kitabu chake cha “Kichwamaji” kinachojikuta katika mtazamo ulio katika mwelekeo wa kidhanaishi.
  5. 5. MAREJELEO Kamusi ya Kiswahili Sanifu, (2004). Oxford University Press, East Africa and Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Kenya. Kezilehabi, E. (2008), Kichwamaji, Vide~ Muwa Publishers Limited, Nairobi Kenya. Madumulla, J.S. (2009), Riwaya ya Kiswahili, Mture Education Publishers Limited, Dar es Salaam Tanzania Wamitila, K.W.(2003), Uhakiki wa Fasihi, Phoemix Publishers Limited, Nairobi- Kenya.

Views

Total views

11,249

On Slideshare

0

From embeds

0

Number of embeds

5

Actions

Downloads

14

Shares

0

Comments

0

Likes

0

×