SlideShare a Scribd company logo
1 of 6
SWALI: Hakiki uainishaji wa Ushairi wa Kiswahili kama ulivyofanywa na wataalamu
mbalimbali, na kisha kwa mtazamo wako bainisha mtazamo bora zaidi.
Kazi hii imegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni utangulizi, kiini na hitimisho.
Ambapo, katika utangulizi tumeonesha maana ya ushairi kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali
na kisha kuunganisha mawazo na kupata maana ya jumla, pia kwa ufupi sana tumeonesha
maaana ya uainishaji, katika kiini tumeonesha kwa kina uainishaji wa ushairi wa Kiswahili kwa
mujibu wa wataalamu mbalimbali na vigezo walivyovitumia, pia udhaifu kwa ufupi wa vigezo
vyao, na kisha kuonesha mtazamo wetu kuhusu uainishaji ulio bora zaidi. Na katika hitimisho
kutoa maoni kuhusu suala zima la uainishaji wa ushairi.
Maana ya ushairi imetolewa na wataalamu mbalimbali kama ifuatavyo;
Shaaban Robert (1958) “ Ushairi ni sanaa ya vina inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi, na
tenzi zaidi ya kuwa ni sanaa ya vina, ushairi una ufasaha wa maneno machache”.
Mathias Mnyampala (1970) “Ushairi ni wingi wa maneno, hekima tangu kale na kale ndicho kitu
kilicho bora sana katika mazingira ya dunia, kwa kutumia maneno ya mkato na lugha nzuri
yenye kunata iliyopangwa kwa urari wa vina na mizani maalumu”.
Abdilatifu Abdallah (1973) “ Ushairi ni utungo wowote ambao katika kila ubeti wake kuna
ulinganifu wa vina vitukufu vilivyopangwa kimoja baada ya chenzie, wenye vipande vilivyo na
ulinganifu wa mizani zisizo pungufu wala kuzidi, na vipande hivyo viwe vimetandwa na maneno
ya mkato maalumu na yenye lugha nyofu, tamu na laini, lugha ambayo ni telezi kwa ulimi na
kutamka, lugha ambayo ina uzito wa kifikra, tamu kusema au tambuzi kwa masikio na huathiri
moyo ilivyokusudiwa”.
Mulokozi (1989) “Ushairi ni sanaa ya vina inayopambanuluwa kama nyimbo, mashairi na tenzi,
zaidi ya kuwa na maneno machache au muhtasari, maneno ya ushairi huvuta moyo kwa namna
ya ajabu”
Wataalamu wote hao katika kufasili ushairi wamezingatia uzuri wa maneno au lugha ya kisanaa
itumikayo kifasaha, na usanaa wa vina na mizani katika ushairi. Hivyo, Kwa ujumla tunaweza
kusema kuwa; Ushairi ni utungo maalumu wa kisanaa,wenye kutumia lugha ya mkato yenye
kuvuta hisia, wazo, fikra nzito katika fani na maudhui. Jambo la msingi kutambua ni kwamba,
ushairi tofauti na nathari hauelezi tu, bali huonyesha hisi, wazo, hali au tukio na wakati huohuo
huathiri hisia zetu. Usawiri huo huweza kufanywa kijadi au kisasa.
Uainishaji kama ulivyofafanuliwa na Samwel Method (2013), Ni neno lililozaliwa kutoka katika
dhana ya “aina”, hivyo Uainishaji ni kupanga vitu katika aina, namna au makundi. Hivyo
tunaposema Uainishaji wa Ushairi tunamaanisha kutoa, kueleza, kutaja aina mbalimbali za
ushairi.
Wataalamu hutumia vigezo katika kuainisha Ushairi wa Kiswahili, na hivyo kila mtaalamu
kulingana na kigezo au vigezo vyake kuainisha ushairi katika aina mbalimbali. Vifuatavyo ni
baadhi ya vigezo vimevyotumiwa na wataalamu mbalimbali katika kuainisha Ushairi wa
Kiswahili:
Kigezo cha mafunzo na maongozi yabebwayo na shairi husika. Huu ni uainishaji wa awali
kabisa wa Ushairi wa Kiswahili uliofanywa na Mnyampala (1975) ambapo yeye anataja aina
tano za ushairi wa Kiswahili kwa kuzingatia kigezo hiki, aina hizo ni mashairi ya kusifu,
mashairi ya kuapiza, mashairi ya kutoa shukrani, mashairi ya kulaumu na kusimanga, na
mashairi ya kuomba dua. Pia El-Kaiim (1985:33-44) kwa kutumia kigezo hiki yeye anabainisha
aina sita za mashairi ambayo ni mashairi ya kusifu, mashairi ya kutukana, mashairi ya kuomba
dua, mashairi ya kuapiza, mashairi ya kutoa shukrani, na mashairi ya kulaumu na kusimanga.
Lakini Mnyampala anakosoa mashairi kutumia lugha ya utusi au matusi kwani mashairi yana
hekima ya pekee hivyo hayawezi kutumia matusi, hivyo anapinga kuwepo kwa mashairi ya
matusi lakini kukubaliana na aina nyingine za mashairi za El-Kaiim. Hata hivyo kigezo hiki cha
uainishaji hakina mashiko sana kwani kinajikita zaidi katika mafunzo na maongozi tu ya shairi
husika na kuitupilia mbali fani mbalimbali ya shairi husika, hivyo ni telezi mno.
Kigezo cha maudhui yanayobebwa na shairi lenyewe. Kwa mujibu wa Method, S. & Wenzake
(2013) anasema kigezo cha maudhui katika uainishaji wa ushairi wa Kiswahili kinazingatia zaidi
nyanja za maisha ya binadamu zilizoangaziwa na shairi hilo. Shairi laweza kubeba maudhui ya
kiuchumi, kisiasa, kijamii, na kiutamaduni, hivyo kwa kutumia kigezo hiki kuna aina nne za
mashairi ambazo ni mashairi ya kiuchumi, mashairi ya kisiasa, mashairi ya kijamii, na msahairi
ya kiutamaduni. Lakini kigezo hiki ni tepetepe mno, kwani kuna uwezekano wa shairi kubeba
maudhui zaidi ya moja ya nyanja za maisha, shairi laweza kuzungumzia mambo ya kiuchumi na
wakati huohuo kuzungumzia utamaduni na hata siasa, Mfano shairi la “Ulevi” la Mzale
(2009:74-78) ambapo shairi hili limebeba maudhui ya kiuchumi na kijamii kwa pamoja, hivyo
kigezo hiki bado kina legalega katika kuainisha ushairi wa Kiswahili.
Kigezo cha umbo la shairi husika, katika kigezo hiki kinachozingatiwa sana ni umbo la shairi
husika. Method, S & Wenzake (2013:111-112) wanasema kwamba shairi linaweza kutungwa na
kupewa umbo fulani ambalo laweza kuwa ni umbo la kinathari (kisimulizi), umbo la kitamthiliya
(kimajibizano), au umbo la kiwimbo. Mashairi ya kisimulizi ni yale yanayosimulia kitu au jambo
kwa jinsi au namna ya hadithi, mashairi haya ni kama tendi, ambazo hubeba hadithi fulani
inayosimuliwa. Mashairi ya kitamthiliya au kidrama ni yale ambayo huzingatia zaidi mbinu ya
kimajibizano baina ya wahusika. Ushairi wa kiwimbo huu huwa na beti na mistari katika urari
wa vina na mizani. Hata hivyo kigezo hiki ni rojorojo mno kisicho na ugumu wowote kwani
wataalamu wa kigezo hiki huchanganya dhana mbili tofauti, umbo la kitu na namna
kinavyoonekana na namna ya uwasilishaji wake ni dhana mbili tofauti, hivyo kigezo hiki si
toshelevu.
Kigezo cha mbinu za kisanaa zilizotumika katika shairi lenyewe, kigezo hiki huzingatia sana
mbinu za kisanaa zilizotumika. Mbinu za kisanaa zinazozungumzwa hasa katika kigezo hiki ni
vina na mizani. Shairi laweza kuzingatia vina na mizani au lisizingatie na bado likawa ni shairi.
Shaaban Robert (1958) na wengine husema kuwa iwapo shairi limezingatia urari wa vina na
mizani linakuwa shairi la kimapokeo. Mlokozi (1989) na wengine husema pia shairi
lisipozingatia urari wa vina na mizani hilo ni shairi la kisasa. Kwa hiyo wataalamu wa kigezo
hiki huainisha aina mbili za ushairi yaani ushairi wa kimapokeo na ushairi wa kisasa. Method, S.
& Wenzake (2013) wanaendelea kushadidia hoja hii kwa kusema kuwa wanamapokeo wao
hujikita katika ushairi usio wa Waswahili, bali wa kigeni (Kiarabu) kwani wao ndio
waliozingatia suala la urari wa vina na mizani, hivyo wanasahau ushairi wa asili wa asili
uliokuwepo kabla ya ujio wa wageni ambapo vina na mizani haikuwa ndio ushairi, ila kile
kinachoifikia jamii. Kigezo hiki sio makini sana kwani kuna mashairi katika ubeti fulani waweza
kufuata vina na mizani na ubeti mwingine ukafuata mizani tu au usifuate vina na mizani, hivyo
kukosa sifa ya kuwa katika aina mojawapo. Hivyo kigezo hiki pia hakijiwezi chenyewe katika
uainishaji wa ushairi wa Kiswahili.
Kigezo cha idadi ya mistari katika kila ubeti wa shairi husika, kwa kuzingatia kigezo hiki
mashairi hugawanywa katika makundi kulingana na idadi ya mistari katika kila ubeti wa shairi
husika. Baadhi ya wataalamu waliotumia kigezo hiki ni pamojo na Amri Abeid (1954), Kandoro
(1983) na Noor (1988). Huendelea kudai kuwa shairi laweza kuwa na msitari mmoja katika beti,
hadi misitari kumi katika beti la shairi, na kuendelea au zaidi ya kumi. Hudai pia kila shairi lina
jina lake kama walivyotaja; Tathmina lenye mstari mmoja, Tathnia lenye mistari miwili,
Tathlitha au Utatu lenye mistari mitatu, Tarbia au Unne lenye mistari nne, Takhmisa au Utano
lenye mistari mitano, Tasdia ua Usita lenye mistari sita, Tasadia au Usaba lenye mistari saba,
Naudia au unane lenye mistari nane, Telemani au Utisa lenye mistari tisa, na Ukumi lenye
mistari kumi. Kigezo hiki kinakuwa na ukata wa majina ya mashairi yenye mistari zaidi ya kumi,
na hivyo kinalegea katika uainishaji wake.
Kigezo cha uwasilishaji wa shairi husika, Kigezo hiki huzingatia namna shairi linavyotolewa na
mtunzi kuwafikia jamii husika, kama ni kwa maandishi au masimulizi, hivyo wataalamu hawa
huainisha aina mbili ambazo ni ushairi simuluzi na ushairi andishi. Method, S. & Wenzake
(2013) wanaendelea kushadidia kigezo hiki anasema ushairi simulizi ni ule unaowasilishwa kwa
njia ya masimulizi ya mdomo na ushairi andishi ni ushairi unaowasilishwa kwa hati ya
maandishi. Anaendelea kusema pia kuna uwezekano wa ushairi simulizi kuwekwa katika
maandishi, na ushairi andishi kusimuliwa. Hata hivyo kigezo hiki pia hakijitoshelezi kwani
kinajikita zaidi katika namna ya kuwasiliha na kusaha kuzingatia muundo wa shairi lenyewe na
kilichobebwa na shairi hilo, hivyo kuwa na upungufu kutumika kama kigezo cha kuainisha
Ushairi wa Kiswahili.
Kigezo cha Bahari ya shairi, Ibrahim Sharif (1988) akimnukuu Omboga (1963) anasema Bahari
ni umbo moja la kumbo ambalo huweza kuwa na mikondo tofautitofauti ndani yake, mfano
nyimbo na tenzi. Katika kigezo hiki kinachozingatiwa kwa ukaribu sana ni idadi ya mistari
katika beti na jinsi mistari hiyo ilivyogawanywa katika vipande katika beti husika. Amri Abeid
(1954) na Shaban Robert (1958) wameainisha aina tatu kwa kutumia kigezo hiki ambazo ni
Nyimbo, Tenzi na Shairi. Hichens (1942) yeye ametaja aina tano za bahari, lakini pia Ahmed
Sheikh na Nabhany katika kitabu chao cha “Tungo Zetu” wameainisha aina kumi na tatu za
bahari ambazo ni Shairi, Wimbo, Tenzi, Ink-Shafi au Duramandhuma, Ukawafi, Wajiwaji,
Hamziyya, Tiyani Fatiha, Utumbuizo, Wawe, Kimai, Zivindo na Sama. Akiendelea kukifafanua
kigezo hiki Samwel, M. & Wenzake (2013) wanasema kuwa wataalamu waliotumia kigezo hiki
wanakuwa na madhaifu kwani wao nao wanajikita zaidi katika ushairi wa kimapokeo na kusahau
mashairi ya usasa, na hivyo kukiboresha kigezo hiki kuwa kiitwe ‘Bahari za mashairi ya
kimapokeo na kisasa’. Anaendelea kueleza kuwa ndani ya kigezo hiki kuna vigezo kadhaa
vidogovidogo vinavyobebwa humo, na vigezo hivyo vidogovidogo hutupatia aina ya ushairi
kutokana na kigezo husika kama ifuatvyo;
Kigezo cha beti, mishororo na vipande. Hapa kinachoangaliwa ni idadi ya mishororo katika beti
na vipande vya mishororo hiyo, ambapo amepeta Shairi, Wimbo, Utenzi au Utendi, Tumbuizo,
Ukwafi au kawafi, Wajiwaji au Takhmisa, Gungu, Mathnawi, na Batundi.
Kigezo cha urari wa vina na mizani, ambapo anaangalia kuwapo au kutokuwapo kwa vina na
mizzani au vyote kwa pamoja, ambapo Mtaalamu Samwel Method ametaja kuwa kuna wajiwaji
au takhmisa, wawe au vave, kimai, ukara, ukuraguni, mtiririko, masivina, kisarambe, ghuni,
upeo na kikai.
Kigezo cha muundo, ambapo kwa kigezo hiki kidogo anaainisha kuwa kuna ngonjera, sarakani,
na mandhuma. Katika kigezo hiki kikubwa cha kuzingatia kwa mujibu wa Samwel ni umbo la
shairi husika.
Kigezo cha uradidi, uradidi ni hali ya kujirudiarudia kwa jambo, hasa neno au kifungu cha
maneno katika shairi, ambapo kwa kigezo hiki kuna aina mbili tu, yaani kikwamba na pindu.
Kigezo cha madhumuni ya utungaji, ambapo kulingana na dhumuni anataja aina tano za bahari
ambazo ni zivindo, tumbuizo, tiyani fatiha, Ink-shafi au dura mandhuma, na taabali.
Kigezo cha aina ya kiishilio, kiishilio ni kituo. Kinachoangaliwa hapa ni urefu, ufupi, au uwepo
wa kiishilio katika beti la shairi husika. Ikiwa kituo hakijirudiirudii huitwa kimalizio, Hivyo kwa
kigezo hiki kuna aina mbili za ushairi ambazo ni Msuko-kiishilio, ambapo kiishilio kinachokuwa
kifupi, na ya pili ni Sabilia panapokuwa na kimalizio.
Aidha, kutokana na kigezo cha bahari kama kilivyotumiwa na wataalamu waliotangulia
kinakuwa na sifa ya kujumuisha vipengele vingine vidogovidogo ndani yake, lakini pia kama
kinavyoboreshwa na Method,S. & Wenzake (2013) na kukiita bahari za ushairi wa kimapokeo na
kisasa.
Hivyo basi, kigezo kilicho bora zaidi ni kile cha “Bahari” kwa sababu kina sifa na sababu za
kimajumui za kuhusisha vigezo vingine vidogovidogo na vyote kumilikiwa na aina moja tu ya
kuainisha mashairi ya Kiswahili, na hivyo kubeba aina nyingi za ushairi sio hivyo tu pia
wataalamu wengi wameafikiana na aina hii ya uainishaji wa ushairi wa Kiswahili.
Kimsingi suala la uainishaji wa ushairi wa Kiswahili bado linaleta mkanganyiko katika taaluma
hii, kwani kuna maswali bado yanaweza kujitokeza kama kuhusu idadi ya bahari na ni kwa nini
tuainishe kwa kutumia bahari?. Jibu ni kwamba kuna umuhimu wa kuzingatia bahari kwa kuwa
hurahisisha usomaji na ufafanuzi wa ushairi wa Kiswahili. Hivyo taaluma hii inatoa mawanda
mapana zaidi kwa Wataalamu wengi zaidi kujikita katika kuainisha ushairi wa Kiswahili.
MAREJELEO
Abedi, K. A.(1954). Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri. Nairobi: Kenya Literature
Bereau.
Kahigi, K. K. & Mlokozi, M. M.(1973). Mashairi ya Kisasa. Dar es Salaam: Tanzania
Publishing House.
Kahigi, K. K. (1979). Kunga za Ushairi. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House.
Method, S. & Wenzake. (2013). Ushairi Wa Kiswahili. Dar es Salaam: Meveli Publisers (MVP).

More Related Content

What's hot

MAENDELEO YA KISWAHILI TANZANIA
MAENDELEO YA KISWAHILI TANZANIAMAENDELEO YA KISWAHILI TANZANIA
MAENDELEO YA KISWAHILI TANZANIAshahzadebaujiti
 
Mofolojia ya kiswahili
Mofolojia ya kiswahiliMofolojia ya kiswahili
Mofolojia ya kiswahiliGeophery sanga
 
Uhakiki wa kazi za fasihi andishi
Uhakiki wa kazi za fasihi andishiUhakiki wa kazi za fasihi andishi
Uhakiki wa kazi za fasihi andishiKAZEMBETVOnline
 
Chuo kikuu cha mtakatifu agustino (autosaved)
Chuo kikuu cha mtakatifu agustino (autosaved)Chuo kikuu cha mtakatifu agustino (autosaved)
Chuo kikuu cha mtakatifu agustino (autosaved)Mwl. Mapesa Nestory
 
Chimbuko na Asili ya Kiswahili
Chimbuko na Asili ya KiswahiliChimbuko na Asili ya Kiswahili
Chimbuko na Asili ya Kiswahilimussa Shekinyashi
 
MAENDELEO YA FASIHI SIMULIZI
MAENDELEO YA FASIHI SIMULIZIMAENDELEO YA FASIHI SIMULIZI
MAENDELEO YA FASIHI SIMULIZIshahzadebaujiti
 
Umuhimu wa kujifunza nadharia za fonolojia
Umuhimu wa kujifunza nadharia za fonolojiaUmuhimu wa kujifunza nadharia za fonolojia
Umuhimu wa kujifunza nadharia za fonolojiaHamad Khamis Juma
 
Uhakiki wa kazi za fasihi andishi
Uhakiki wa kazi za fasihi andishiUhakiki wa kazi za fasihi andishi
Uhakiki wa kazi za fasihi andishiMussaOmary3
 
KUKUA NA KUENEA KWA KISWAHILI
KUKUA NA KUENEA KWA KISWAHILIKUKUA NA KUENEA KWA KISWAHILI
KUKUA NA KUENEA KWA KISWAHILImussa Shekinyashi
 
Kiswahili ni Pijini au Krioli
Kiswahili ni Pijini au KrioliKiswahili ni Pijini au Krioli
Kiswahili ni Pijini au Kriolimussa Shekinyashi
 
UHAKIKI WA FASIHI ANDISHI
UHAKIKI WA FASIHI ANDISHIUHAKIKI WA FASIHI ANDISHI
UHAKIKI WA FASIHI ANDISHIshahzadebaujiti
 
Uhuru wa Mtunzi wa Kazi za Fasihi
Uhuru wa Mtunzi wa Kazi za FasihiUhuru wa Mtunzi wa Kazi za Fasihi
Uhuru wa Mtunzi wa Kazi za Fasihimussa Shekinyashi
 

What's hot (20)

CHIMBUKO LA FASIHI
CHIMBUKO LA FASIHICHIMBUKO LA FASIHI
CHIMBUKO LA FASIHI
 
MAENDELEO YA KISWAHILI TANZANIA
MAENDELEO YA KISWAHILI TANZANIAMAENDELEO YA KISWAHILI TANZANIA
MAENDELEO YA KISWAHILI TANZANIA
 
FASIHI KWA UJUMLA
FASIHI KWA UJUMLAFASIHI KWA UJUMLA
FASIHI KWA UJUMLA
 
TAFSIRI NA UKALIMANI
TAFSIRI NA UKALIMANITAFSIRI NA UKALIMANI
TAFSIRI NA UKALIMANI
 
Mofolojia ya kiswahili
Mofolojia ya kiswahiliMofolojia ya kiswahili
Mofolojia ya kiswahili
 
Semantiki
SemantikiSemantiki
Semantiki
 
Maana ya Hadithi
Maana ya HadithiMaana ya Hadithi
Maana ya Hadithi
 
Dhima za kamusi
Dhima za kamusiDhima za kamusi
Dhima za kamusi
 
Uhakiki wa kazi za fasihi andishi
Uhakiki wa kazi za fasihi andishiUhakiki wa kazi za fasihi andishi
Uhakiki wa kazi za fasihi andishi
 
Chuo kikuu cha mtakatifu agustino (autosaved)
Chuo kikuu cha mtakatifu agustino (autosaved)Chuo kikuu cha mtakatifu agustino (autosaved)
Chuo kikuu cha mtakatifu agustino (autosaved)
 
Chimbuko na Asili ya Kiswahili
Chimbuko na Asili ya KiswahiliChimbuko na Asili ya Kiswahili
Chimbuko na Asili ya Kiswahili
 
MAENDELEO YA FASIHI SIMULIZI
MAENDELEO YA FASIHI SIMULIZIMAENDELEO YA FASIHI SIMULIZI
MAENDELEO YA FASIHI SIMULIZI
 
MATUMIZI YA SARUFI
MATUMIZI YA SARUFIMATUMIZI YA SARUFI
MATUMIZI YA SARUFI
 
Umuhimu wa kujifunza nadharia za fonolojia
Umuhimu wa kujifunza nadharia za fonolojiaUmuhimu wa kujifunza nadharia za fonolojia
Umuhimu wa kujifunza nadharia za fonolojia
 
Mjengo wa tungo
Mjengo wa tungoMjengo wa tungo
Mjengo wa tungo
 
Uhakiki wa kazi za fasihi andishi
Uhakiki wa kazi za fasihi andishiUhakiki wa kazi za fasihi andishi
Uhakiki wa kazi za fasihi andishi
 
KUKUA NA KUENEA KWA KISWAHILI
KUKUA NA KUENEA KWA KISWAHILIKUKUA NA KUENEA KWA KISWAHILI
KUKUA NA KUENEA KWA KISWAHILI
 
Kiswahili ni Pijini au Krioli
Kiswahili ni Pijini au KrioliKiswahili ni Pijini au Krioli
Kiswahili ni Pijini au Krioli
 
UHAKIKI WA FASIHI ANDISHI
UHAKIKI WA FASIHI ANDISHIUHAKIKI WA FASIHI ANDISHI
UHAKIKI WA FASIHI ANDISHI
 
Uhuru wa Mtunzi wa Kazi za Fasihi
Uhuru wa Mtunzi wa Kazi za FasihiUhuru wa Mtunzi wa Kazi za Fasihi
Uhuru wa Mtunzi wa Kazi za Fasihi
 

USHAIRI WA KISWAHILI

  • 1. SWALI: Hakiki uainishaji wa Ushairi wa Kiswahili kama ulivyofanywa na wataalamu mbalimbali, na kisha kwa mtazamo wako bainisha mtazamo bora zaidi. Kazi hii imegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni utangulizi, kiini na hitimisho. Ambapo, katika utangulizi tumeonesha maana ya ushairi kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali na kisha kuunganisha mawazo na kupata maana ya jumla, pia kwa ufupi sana tumeonesha maaana ya uainishaji, katika kiini tumeonesha kwa kina uainishaji wa ushairi wa Kiswahili kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali na vigezo walivyovitumia, pia udhaifu kwa ufupi wa vigezo vyao, na kisha kuonesha mtazamo wetu kuhusu uainishaji ulio bora zaidi. Na katika hitimisho kutoa maoni kuhusu suala zima la uainishaji wa ushairi. Maana ya ushairi imetolewa na wataalamu mbalimbali kama ifuatavyo; Shaaban Robert (1958) “ Ushairi ni sanaa ya vina inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi, na tenzi zaidi ya kuwa ni sanaa ya vina, ushairi una ufasaha wa maneno machache”. Mathias Mnyampala (1970) “Ushairi ni wingi wa maneno, hekima tangu kale na kale ndicho kitu kilicho bora sana katika mazingira ya dunia, kwa kutumia maneno ya mkato na lugha nzuri yenye kunata iliyopangwa kwa urari wa vina na mizani maalumu”. Abdilatifu Abdallah (1973) “ Ushairi ni utungo wowote ambao katika kila ubeti wake kuna ulinganifu wa vina vitukufu vilivyopangwa kimoja baada ya chenzie, wenye vipande vilivyo na ulinganifu wa mizani zisizo pungufu wala kuzidi, na vipande hivyo viwe vimetandwa na maneno ya mkato maalumu na yenye lugha nyofu, tamu na laini, lugha ambayo ni telezi kwa ulimi na kutamka, lugha ambayo ina uzito wa kifikra, tamu kusema au tambuzi kwa masikio na huathiri moyo ilivyokusudiwa”. Mulokozi (1989) “Ushairi ni sanaa ya vina inayopambanuluwa kama nyimbo, mashairi na tenzi, zaidi ya kuwa na maneno machache au muhtasari, maneno ya ushairi huvuta moyo kwa namna ya ajabu” Wataalamu wote hao katika kufasili ushairi wamezingatia uzuri wa maneno au lugha ya kisanaa itumikayo kifasaha, na usanaa wa vina na mizani katika ushairi. Hivyo, Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa; Ushairi ni utungo maalumu wa kisanaa,wenye kutumia lugha ya mkato yenye kuvuta hisia, wazo, fikra nzito katika fani na maudhui. Jambo la msingi kutambua ni kwamba, ushairi tofauti na nathari hauelezi tu, bali huonyesha hisi, wazo, hali au tukio na wakati huohuo huathiri hisia zetu. Usawiri huo huweza kufanywa kijadi au kisasa. Uainishaji kama ulivyofafanuliwa na Samwel Method (2013), Ni neno lililozaliwa kutoka katika dhana ya “aina”, hivyo Uainishaji ni kupanga vitu katika aina, namna au makundi. Hivyo
  • 2. tunaposema Uainishaji wa Ushairi tunamaanisha kutoa, kueleza, kutaja aina mbalimbali za ushairi. Wataalamu hutumia vigezo katika kuainisha Ushairi wa Kiswahili, na hivyo kila mtaalamu kulingana na kigezo au vigezo vyake kuainisha ushairi katika aina mbalimbali. Vifuatavyo ni baadhi ya vigezo vimevyotumiwa na wataalamu mbalimbali katika kuainisha Ushairi wa Kiswahili: Kigezo cha mafunzo na maongozi yabebwayo na shairi husika. Huu ni uainishaji wa awali kabisa wa Ushairi wa Kiswahili uliofanywa na Mnyampala (1975) ambapo yeye anataja aina tano za ushairi wa Kiswahili kwa kuzingatia kigezo hiki, aina hizo ni mashairi ya kusifu, mashairi ya kuapiza, mashairi ya kutoa shukrani, mashairi ya kulaumu na kusimanga, na mashairi ya kuomba dua. Pia El-Kaiim (1985:33-44) kwa kutumia kigezo hiki yeye anabainisha aina sita za mashairi ambayo ni mashairi ya kusifu, mashairi ya kutukana, mashairi ya kuomba dua, mashairi ya kuapiza, mashairi ya kutoa shukrani, na mashairi ya kulaumu na kusimanga. Lakini Mnyampala anakosoa mashairi kutumia lugha ya utusi au matusi kwani mashairi yana hekima ya pekee hivyo hayawezi kutumia matusi, hivyo anapinga kuwepo kwa mashairi ya matusi lakini kukubaliana na aina nyingine za mashairi za El-Kaiim. Hata hivyo kigezo hiki cha uainishaji hakina mashiko sana kwani kinajikita zaidi katika mafunzo na maongozi tu ya shairi husika na kuitupilia mbali fani mbalimbali ya shairi husika, hivyo ni telezi mno. Kigezo cha maudhui yanayobebwa na shairi lenyewe. Kwa mujibu wa Method, S. & Wenzake (2013) anasema kigezo cha maudhui katika uainishaji wa ushairi wa Kiswahili kinazingatia zaidi nyanja za maisha ya binadamu zilizoangaziwa na shairi hilo. Shairi laweza kubeba maudhui ya kiuchumi, kisiasa, kijamii, na kiutamaduni, hivyo kwa kutumia kigezo hiki kuna aina nne za mashairi ambazo ni mashairi ya kiuchumi, mashairi ya kisiasa, mashairi ya kijamii, na msahairi ya kiutamaduni. Lakini kigezo hiki ni tepetepe mno, kwani kuna uwezekano wa shairi kubeba maudhui zaidi ya moja ya nyanja za maisha, shairi laweza kuzungumzia mambo ya kiuchumi na wakati huohuo kuzungumzia utamaduni na hata siasa, Mfano shairi la “Ulevi” la Mzale (2009:74-78) ambapo shairi hili limebeba maudhui ya kiuchumi na kijamii kwa pamoja, hivyo kigezo hiki bado kina legalega katika kuainisha ushairi wa Kiswahili. Kigezo cha umbo la shairi husika, katika kigezo hiki kinachozingatiwa sana ni umbo la shairi husika. Method, S & Wenzake (2013:111-112) wanasema kwamba shairi linaweza kutungwa na
  • 3. kupewa umbo fulani ambalo laweza kuwa ni umbo la kinathari (kisimulizi), umbo la kitamthiliya (kimajibizano), au umbo la kiwimbo. Mashairi ya kisimulizi ni yale yanayosimulia kitu au jambo kwa jinsi au namna ya hadithi, mashairi haya ni kama tendi, ambazo hubeba hadithi fulani inayosimuliwa. Mashairi ya kitamthiliya au kidrama ni yale ambayo huzingatia zaidi mbinu ya kimajibizano baina ya wahusika. Ushairi wa kiwimbo huu huwa na beti na mistari katika urari wa vina na mizani. Hata hivyo kigezo hiki ni rojorojo mno kisicho na ugumu wowote kwani wataalamu wa kigezo hiki huchanganya dhana mbili tofauti, umbo la kitu na namna kinavyoonekana na namna ya uwasilishaji wake ni dhana mbili tofauti, hivyo kigezo hiki si toshelevu. Kigezo cha mbinu za kisanaa zilizotumika katika shairi lenyewe, kigezo hiki huzingatia sana mbinu za kisanaa zilizotumika. Mbinu za kisanaa zinazozungumzwa hasa katika kigezo hiki ni vina na mizani. Shairi laweza kuzingatia vina na mizani au lisizingatie na bado likawa ni shairi. Shaaban Robert (1958) na wengine husema kuwa iwapo shairi limezingatia urari wa vina na mizani linakuwa shairi la kimapokeo. Mlokozi (1989) na wengine husema pia shairi lisipozingatia urari wa vina na mizani hilo ni shairi la kisasa. Kwa hiyo wataalamu wa kigezo hiki huainisha aina mbili za ushairi yaani ushairi wa kimapokeo na ushairi wa kisasa. Method, S. & Wenzake (2013) wanaendelea kushadidia hoja hii kwa kusema kuwa wanamapokeo wao hujikita katika ushairi usio wa Waswahili, bali wa kigeni (Kiarabu) kwani wao ndio waliozingatia suala la urari wa vina na mizani, hivyo wanasahau ushairi wa asili wa asili uliokuwepo kabla ya ujio wa wageni ambapo vina na mizani haikuwa ndio ushairi, ila kile kinachoifikia jamii. Kigezo hiki sio makini sana kwani kuna mashairi katika ubeti fulani waweza kufuata vina na mizani na ubeti mwingine ukafuata mizani tu au usifuate vina na mizani, hivyo kukosa sifa ya kuwa katika aina mojawapo. Hivyo kigezo hiki pia hakijiwezi chenyewe katika uainishaji wa ushairi wa Kiswahili. Kigezo cha idadi ya mistari katika kila ubeti wa shairi husika, kwa kuzingatia kigezo hiki mashairi hugawanywa katika makundi kulingana na idadi ya mistari katika kila ubeti wa shairi husika. Baadhi ya wataalamu waliotumia kigezo hiki ni pamojo na Amri Abeid (1954), Kandoro (1983) na Noor (1988). Huendelea kudai kuwa shairi laweza kuwa na msitari mmoja katika beti, hadi misitari kumi katika beti la shairi, na kuendelea au zaidi ya kumi. Hudai pia kila shairi lina jina lake kama walivyotaja; Tathmina lenye mstari mmoja, Tathnia lenye mistari miwili, Tathlitha au Utatu lenye mistari mitatu, Tarbia au Unne lenye mistari nne, Takhmisa au Utano
  • 4. lenye mistari mitano, Tasdia ua Usita lenye mistari sita, Tasadia au Usaba lenye mistari saba, Naudia au unane lenye mistari nane, Telemani au Utisa lenye mistari tisa, na Ukumi lenye mistari kumi. Kigezo hiki kinakuwa na ukata wa majina ya mashairi yenye mistari zaidi ya kumi, na hivyo kinalegea katika uainishaji wake. Kigezo cha uwasilishaji wa shairi husika, Kigezo hiki huzingatia namna shairi linavyotolewa na mtunzi kuwafikia jamii husika, kama ni kwa maandishi au masimulizi, hivyo wataalamu hawa huainisha aina mbili ambazo ni ushairi simuluzi na ushairi andishi. Method, S. & Wenzake (2013) wanaendelea kushadidia kigezo hiki anasema ushairi simulizi ni ule unaowasilishwa kwa njia ya masimulizi ya mdomo na ushairi andishi ni ushairi unaowasilishwa kwa hati ya maandishi. Anaendelea kusema pia kuna uwezekano wa ushairi simulizi kuwekwa katika maandishi, na ushairi andishi kusimuliwa. Hata hivyo kigezo hiki pia hakijitoshelezi kwani kinajikita zaidi katika namna ya kuwasiliha na kusaha kuzingatia muundo wa shairi lenyewe na kilichobebwa na shairi hilo, hivyo kuwa na upungufu kutumika kama kigezo cha kuainisha Ushairi wa Kiswahili. Kigezo cha Bahari ya shairi, Ibrahim Sharif (1988) akimnukuu Omboga (1963) anasema Bahari ni umbo moja la kumbo ambalo huweza kuwa na mikondo tofautitofauti ndani yake, mfano nyimbo na tenzi. Katika kigezo hiki kinachozingatiwa kwa ukaribu sana ni idadi ya mistari katika beti na jinsi mistari hiyo ilivyogawanywa katika vipande katika beti husika. Amri Abeid (1954) na Shaban Robert (1958) wameainisha aina tatu kwa kutumia kigezo hiki ambazo ni Nyimbo, Tenzi na Shairi. Hichens (1942) yeye ametaja aina tano za bahari, lakini pia Ahmed Sheikh na Nabhany katika kitabu chao cha “Tungo Zetu” wameainisha aina kumi na tatu za bahari ambazo ni Shairi, Wimbo, Tenzi, Ink-Shafi au Duramandhuma, Ukawafi, Wajiwaji, Hamziyya, Tiyani Fatiha, Utumbuizo, Wawe, Kimai, Zivindo na Sama. Akiendelea kukifafanua kigezo hiki Samwel, M. & Wenzake (2013) wanasema kuwa wataalamu waliotumia kigezo hiki wanakuwa na madhaifu kwani wao nao wanajikita zaidi katika ushairi wa kimapokeo na kusahau mashairi ya usasa, na hivyo kukiboresha kigezo hiki kuwa kiitwe ‘Bahari za mashairi ya kimapokeo na kisasa’. Anaendelea kueleza kuwa ndani ya kigezo hiki kuna vigezo kadhaa vidogovidogo vinavyobebwa humo, na vigezo hivyo vidogovidogo hutupatia aina ya ushairi kutokana na kigezo husika kama ifuatvyo;
  • 5. Kigezo cha beti, mishororo na vipande. Hapa kinachoangaliwa ni idadi ya mishororo katika beti na vipande vya mishororo hiyo, ambapo amepeta Shairi, Wimbo, Utenzi au Utendi, Tumbuizo, Ukwafi au kawafi, Wajiwaji au Takhmisa, Gungu, Mathnawi, na Batundi. Kigezo cha urari wa vina na mizani, ambapo anaangalia kuwapo au kutokuwapo kwa vina na mizzani au vyote kwa pamoja, ambapo Mtaalamu Samwel Method ametaja kuwa kuna wajiwaji au takhmisa, wawe au vave, kimai, ukara, ukuraguni, mtiririko, masivina, kisarambe, ghuni, upeo na kikai. Kigezo cha muundo, ambapo kwa kigezo hiki kidogo anaainisha kuwa kuna ngonjera, sarakani, na mandhuma. Katika kigezo hiki kikubwa cha kuzingatia kwa mujibu wa Samwel ni umbo la shairi husika. Kigezo cha uradidi, uradidi ni hali ya kujirudiarudia kwa jambo, hasa neno au kifungu cha maneno katika shairi, ambapo kwa kigezo hiki kuna aina mbili tu, yaani kikwamba na pindu. Kigezo cha madhumuni ya utungaji, ambapo kulingana na dhumuni anataja aina tano za bahari ambazo ni zivindo, tumbuizo, tiyani fatiha, Ink-shafi au dura mandhuma, na taabali. Kigezo cha aina ya kiishilio, kiishilio ni kituo. Kinachoangaliwa hapa ni urefu, ufupi, au uwepo wa kiishilio katika beti la shairi husika. Ikiwa kituo hakijirudiirudii huitwa kimalizio, Hivyo kwa kigezo hiki kuna aina mbili za ushairi ambazo ni Msuko-kiishilio, ambapo kiishilio kinachokuwa kifupi, na ya pili ni Sabilia panapokuwa na kimalizio. Aidha, kutokana na kigezo cha bahari kama kilivyotumiwa na wataalamu waliotangulia kinakuwa na sifa ya kujumuisha vipengele vingine vidogovidogo ndani yake, lakini pia kama kinavyoboreshwa na Method,S. & Wenzake (2013) na kukiita bahari za ushairi wa kimapokeo na kisasa. Hivyo basi, kigezo kilicho bora zaidi ni kile cha “Bahari” kwa sababu kina sifa na sababu za kimajumui za kuhusisha vigezo vingine vidogovidogo na vyote kumilikiwa na aina moja tu ya kuainisha mashairi ya Kiswahili, na hivyo kubeba aina nyingi za ushairi sio hivyo tu pia wataalamu wengi wameafikiana na aina hii ya uainishaji wa ushairi wa Kiswahili. Kimsingi suala la uainishaji wa ushairi wa Kiswahili bado linaleta mkanganyiko katika taaluma hii, kwani kuna maswali bado yanaweza kujitokeza kama kuhusu idadi ya bahari na ni kwa nini tuainishe kwa kutumia bahari?. Jibu ni kwamba kuna umuhimu wa kuzingatia bahari kwa kuwa
  • 6. hurahisisha usomaji na ufafanuzi wa ushairi wa Kiswahili. Hivyo taaluma hii inatoa mawanda mapana zaidi kwa Wataalamu wengi zaidi kujikita katika kuainisha ushairi wa Kiswahili. MAREJELEO Abedi, K. A.(1954). Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri. Nairobi: Kenya Literature Bereau. Kahigi, K. K. & Mlokozi, M. M.(1973). Mashairi ya Kisasa. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House. Kahigi, K. K. (1979). Kunga za Ushairi. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House. Method, S. & Wenzake. (2013). Ushairi Wa Kiswahili. Dar es Salaam: Meveli Publisers (MVP).