Mussa Shenyashi
mussashaky@gmail.com
+255 743 98 98 29
+255 714 80 75 65
MJENGO
WA
TUNGO
Tungo
 Neno tungo ni nomino ambayo hutokana na kitenzi tunga
ambacho kinamaana ya kushikanisha vitu.
 Jambo la msingi hapa ni kufahamu kwamba tunapotunga
vitu huwatunapata kitu kinachoitwa utungo.
 Katika taaluma ya sarufi neno tungo linamaana takribani
sawa na hiyo.
 Ambapo tungo katika sarufi ni kuweka pamoja na kupanga
vipashio sahili ili kujenga vipashio vikubwa zaidi,
Aina za Tungo
Tungo Neno
 Tungo yoyote huundwa na vijenzi.
 Vijenzi vya tungo neno katika lugha ya kiswahili ni
vitamkwa,silabi na mofimu.
 Vitamkwa hujenga silabi, silabi hujenga mofimu na mofimu
hujenga tungo-neno.
 Kwa mchakato huu tunapata aina nane za maneno, ambazo
ni:
Nomino,Vitenzi,Vielezi,Vivumishi,Viunganishi,Vihusishi,Viwak
ilishi na Viingizi.
Tungo-Kirai
 Ni tungo isiyo na muundo wa kiima na kiarifu. AU
 Ni neno au kundi la maneno katika mpangilio maalum
linalofanya kazi moja kisintaksia katika sentensi.
AU
 Ni neno au maneno mawili au zaidi ambayo huwekwa
pamoja katika mpangilio maalum unaozingatia uhusiano
uliopo baina ya neno-kuu na maneno mengine.
Zingatia Mfano ufuatao…
 Mtoto yule
 Mtoto yule mzuri
 Mtoto yule mnene kuliko wote
 Mzee huyu mjanja
 Mwalimu yule mwembamba
 Mifano yote iliyotolewa hapo juu ni mifano ya tungo-virai ambazo zimekitwa
katika neno-kuu ambalo ni nomino.
 Maneno yaliyoandikwa kwa hati ya kulala ndio chimbuko la kazi ya kirai
hicho katika sentensi
 Hivyo tungo hizo ni Kirai-nomino
Sifa za kirai
 Hikina muundo wa kiima na kiarifu
 Lakini huweza kukaa katika upande wowote; wa kiima au
kiarifu.
 Uainishaji (kujua aina ya kirai) unategemea mahusiano ya
maneno katika fungu hilo la maneno.
 Kirai hujengwa na neno moja au zaidi ya moja.
Virai vya Kiswahili
 Katika lugha ya kiswahili kuna aina za virai zifuatazo:
 Kirai-nomino
 Kirai –kielezi
 Kirai-kitenzi
 Kirai-kivumishi
 Kirai –kiunganishi
Kirai Nomino
 Tungo kirai nomino kinaweza kuwa na moja ya miundo
ifuatayo:
 Nomino Pekee: Happy anasoma
 Nomino zaidi ya moja: Hapy na Abriel wanasoma
 Kiwakilishi Pekee: Sisi ni watanzania
 Kiwakilishi na kivumishi: Sisi sote tumefaulu
 Nomino moja na Kivumishi:Mtoto mzuri anaoga
 Nomino na kishazi Tegemezi: Mbuzi aliyevunjia pembe
amechinjwa
Kirai Kielezi
 Ni neno au fungu la maneno ambalo linatupatia taarifa zaidi
kuhusu tendo.
 Kimsingi kirai kielezi kinajibu maswali kwamba tendo kwenye
sentensi:
 Limefanyika wapi?
 Limefanyikaje?
 Limefanyika lini?
 Mara ngapi?
 Namna gani?
 Kirai kielezi huweza kukaa mahala popote ingawa watumizi
wengi wa kiswahili hupenda kuweka kirai kielezi baada ya
kitenzi.
Mifano ya Kirai Kielezi
 Abriel anacheza mpira vizuri sana
 Babu husafiri kila siku
 Mama atakuja kesho saa mbili
 Happy anatembea haraka sana.
Kirai Kitenzi
 Ni neno au kifungu cha maneno ambacho neno kuu ni kitenzi.
 Kirai kitenzi huundwa na maneno yafuatayo:
 Kitenzi Kikuu Pekee( T ):
 Mfano; Abriel analia
Happy na Abby wanakimbia
 Kitenzi Kisaidizi na Kitenzi Kikuu (Ts+T):
 Mfano:Oscar alikuwa anaimba
Philemoni anapenda kuimba
 Kitenzi kishirikishi (t):
 Mara nyingi kitenzi kishirishi hufuatwa na KN cha pili katika
sentensi ambacho huitwa Shamirisho:
 Mfano; Josia ni mwanafunzi
Asha alikuwa mgonjwa
Kalii yu mahututi
Kirai Kivumishi
 Ni neno au kifungu cha maneno chenye kivumishi kama
neno kuu.
 Mara nyingi kirai kivumishi huhusishwa kwenye kirai
nomino.
 Chunguza mifano ifuatayo:
 Beberu mwenye ndevu ndefu sana amerudi
 Kibaka aliyekamatwa jana jioni ametoroka.
 Katika mfano hiyo hapo juumaneno yalitokolezwa wino ndio
virai vivumishi.
Kirai Kiunganishi
 Ni neno au kifungu cha maneno kinachohusisha tungo mbili
zenye hadhi sawa.
 Baadhi ya maneno ambayo huunda kirai kiunganishi ni
pamoja na: kwa,na,pia,vilevile,lakini,ingawa,aidha n.k
 Mfano:
Tungo-Kishazi
 Ni aina ya tungo ambayo muundo wake unajumuisha kitenzi
ndani yake.
 Kishazi ni tungo kubwa kuliko kirai na ndogo kuliko sentensi.
 Kishazi kinaweza kutoa maana kamili au isiyokamili. Tazama
sentensi hii:
 Ng’ombe aliyevunjika mguu amerudi zizini.
 Maneno yaliyo katika hati ya kulaza ni kishazi, lakini yakisimama
pekee hayatoi maana kamili.
 Maneno yaliyokolezwa wino ni kishazi na yanaweza kusimama
pekee na kutoa maana.
 Hapo ndio tunapata aina za vishazi.
Aina za Vishazi
 Kuna aina mbili za Vishazi
Vishazi Huru
Vishazi
Tegemezi
Kishazi Huru
 Ni aina ya kishazi ambavyo hutoa taarifa kamili.
 Aina hii ya vishazi hujengwa na kitenzi kinachojitosheleza
kimaana.
 Kishazi huru huundwa na:
 Kitenzi kikuu kimoja: mfano ;Amekuja
 Kitenzi kisaidizi na kitenzi kikuu: mfano; Alikuwa
anaimba wimbo
Alikuwa anataka kuimba wimbo
 Kitenzi Kishirishi: mfano; Juma ni mkulima
Kishazi Tegemezi
 Hii ni aina ya vishazi ambavyo hutoa taarifa isiyokamili.
 Ili vishazi hivi tegemezi viweze kutoa taarifa iliyo kamili
vinahitaji vishazi huru kukamilisha taarifa.
 Mfano
 Mwanafunzi aliyefaulu
 Msichana aliyeolewa jana
 Mzee aliyekuja jana
Sifa za kishazi tegemezi
 Hakijitoshelezi kimaana
 Kitenzi kisaidizi kilichomo kwenye kishazi tegemezi hubeba
viambishi virejeshi.
Mfano: aliyekimbia, walioimba, walichokikimbia.
 Huweza kusimama kama kiima katika sentensi changamano
Kijana aliyekimbilia mjini mwaka jana
amerudi jana
 Kitenzi kisaidizi kilichomo kwenye kishazi tegemezi hufanya
kazi ya kuvumisha nomino au kielezi.
Aina za vishazi tegemezi
 Kishazi Tegemezi Vumishi (βV)
 Hivi huvumisha jina lililoko katika tungo.
mfano: mtoto aliyekuja jana anaumwa.
 Kishazi Tegemezi Kielezi (βE)
 Hivi hutoa maelezo zaidi kwa kitenzi kilicho katika tungo.
 Chakula kililiwa kilipoiva.
Asanteni

Mjengo wa tungo 3

  • 1.
    Mussa Shenyashi mussashaky@gmail.com +255 74398 98 29 +255 714 80 75 65 MJENGO WA TUNGO
  • 2.
    Tungo  Neno tungoni nomino ambayo hutokana na kitenzi tunga ambacho kinamaana ya kushikanisha vitu.  Jambo la msingi hapa ni kufahamu kwamba tunapotunga vitu huwatunapata kitu kinachoitwa utungo.  Katika taaluma ya sarufi neno tungo linamaana takribani sawa na hiyo.  Ambapo tungo katika sarufi ni kuweka pamoja na kupanga vipashio sahili ili kujenga vipashio vikubwa zaidi,
  • 3.
  • 4.
    Tungo Neno  Tungoyoyote huundwa na vijenzi.  Vijenzi vya tungo neno katika lugha ya kiswahili ni vitamkwa,silabi na mofimu.  Vitamkwa hujenga silabi, silabi hujenga mofimu na mofimu hujenga tungo-neno.  Kwa mchakato huu tunapata aina nane za maneno, ambazo ni: Nomino,Vitenzi,Vielezi,Vivumishi,Viunganishi,Vihusishi,Viwak ilishi na Viingizi.
  • 5.
    Tungo-Kirai  Ni tungoisiyo na muundo wa kiima na kiarifu. AU  Ni neno au kundi la maneno katika mpangilio maalum linalofanya kazi moja kisintaksia katika sentensi. AU  Ni neno au maneno mawili au zaidi ambayo huwekwa pamoja katika mpangilio maalum unaozingatia uhusiano uliopo baina ya neno-kuu na maneno mengine.
  • 6.
    Zingatia Mfano ufuatao… Mtoto yule  Mtoto yule mzuri  Mtoto yule mnene kuliko wote  Mzee huyu mjanja  Mwalimu yule mwembamba  Mifano yote iliyotolewa hapo juu ni mifano ya tungo-virai ambazo zimekitwa katika neno-kuu ambalo ni nomino.  Maneno yaliyoandikwa kwa hati ya kulala ndio chimbuko la kazi ya kirai hicho katika sentensi  Hivyo tungo hizo ni Kirai-nomino
  • 7.
    Sifa za kirai Hikina muundo wa kiima na kiarifu  Lakini huweza kukaa katika upande wowote; wa kiima au kiarifu.  Uainishaji (kujua aina ya kirai) unategemea mahusiano ya maneno katika fungu hilo la maneno.  Kirai hujengwa na neno moja au zaidi ya moja.
  • 8.
    Virai vya Kiswahili Katika lugha ya kiswahili kuna aina za virai zifuatazo:  Kirai-nomino  Kirai –kielezi  Kirai-kitenzi  Kirai-kivumishi  Kirai –kiunganishi
  • 9.
    Kirai Nomino  Tungokirai nomino kinaweza kuwa na moja ya miundo ifuatayo:  Nomino Pekee: Happy anasoma  Nomino zaidi ya moja: Hapy na Abriel wanasoma  Kiwakilishi Pekee: Sisi ni watanzania  Kiwakilishi na kivumishi: Sisi sote tumefaulu  Nomino moja na Kivumishi:Mtoto mzuri anaoga  Nomino na kishazi Tegemezi: Mbuzi aliyevunjia pembe amechinjwa
  • 10.
    Kirai Kielezi  Nineno au fungu la maneno ambalo linatupatia taarifa zaidi kuhusu tendo.  Kimsingi kirai kielezi kinajibu maswali kwamba tendo kwenye sentensi:  Limefanyika wapi?  Limefanyikaje?  Limefanyika lini?  Mara ngapi?  Namna gani?  Kirai kielezi huweza kukaa mahala popote ingawa watumizi wengi wa kiswahili hupenda kuweka kirai kielezi baada ya kitenzi.
  • 11.
    Mifano ya KiraiKielezi  Abriel anacheza mpira vizuri sana  Babu husafiri kila siku  Mama atakuja kesho saa mbili  Happy anatembea haraka sana.
  • 12.
    Kirai Kitenzi  Nineno au kifungu cha maneno ambacho neno kuu ni kitenzi.  Kirai kitenzi huundwa na maneno yafuatayo:  Kitenzi Kikuu Pekee( T ):  Mfano; Abriel analia Happy na Abby wanakimbia  Kitenzi Kisaidizi na Kitenzi Kikuu (Ts+T):  Mfano:Oscar alikuwa anaimba Philemoni anapenda kuimba
  • 13.
     Kitenzi kishirikishi(t):  Mara nyingi kitenzi kishirishi hufuatwa na KN cha pili katika sentensi ambacho huitwa Shamirisho:  Mfano; Josia ni mwanafunzi Asha alikuwa mgonjwa Kalii yu mahututi
  • 14.
    Kirai Kivumishi  Nineno au kifungu cha maneno chenye kivumishi kama neno kuu.  Mara nyingi kirai kivumishi huhusishwa kwenye kirai nomino.  Chunguza mifano ifuatayo:  Beberu mwenye ndevu ndefu sana amerudi  Kibaka aliyekamatwa jana jioni ametoroka.  Katika mfano hiyo hapo juumaneno yalitokolezwa wino ndio virai vivumishi.
  • 15.
    Kirai Kiunganishi  Nineno au kifungu cha maneno kinachohusisha tungo mbili zenye hadhi sawa.  Baadhi ya maneno ambayo huunda kirai kiunganishi ni pamoja na: kwa,na,pia,vilevile,lakini,ingawa,aidha n.k  Mfano:
  • 16.
    Tungo-Kishazi  Ni ainaya tungo ambayo muundo wake unajumuisha kitenzi ndani yake.  Kishazi ni tungo kubwa kuliko kirai na ndogo kuliko sentensi.  Kishazi kinaweza kutoa maana kamili au isiyokamili. Tazama sentensi hii:  Ng’ombe aliyevunjika mguu amerudi zizini.  Maneno yaliyo katika hati ya kulaza ni kishazi, lakini yakisimama pekee hayatoi maana kamili.  Maneno yaliyokolezwa wino ni kishazi na yanaweza kusimama pekee na kutoa maana.  Hapo ndio tunapata aina za vishazi.
  • 17.
    Aina za Vishazi Kuna aina mbili za Vishazi Vishazi Huru Vishazi Tegemezi
  • 18.
    Kishazi Huru  Niaina ya kishazi ambavyo hutoa taarifa kamili.  Aina hii ya vishazi hujengwa na kitenzi kinachojitosheleza kimaana.  Kishazi huru huundwa na:  Kitenzi kikuu kimoja: mfano ;Amekuja  Kitenzi kisaidizi na kitenzi kikuu: mfano; Alikuwa anaimba wimbo Alikuwa anataka kuimba wimbo  Kitenzi Kishirishi: mfano; Juma ni mkulima
  • 19.
    Kishazi Tegemezi  Hiini aina ya vishazi ambavyo hutoa taarifa isiyokamili.  Ili vishazi hivi tegemezi viweze kutoa taarifa iliyo kamili vinahitaji vishazi huru kukamilisha taarifa.  Mfano  Mwanafunzi aliyefaulu  Msichana aliyeolewa jana  Mzee aliyekuja jana
  • 20.
    Sifa za kishazitegemezi  Hakijitoshelezi kimaana  Kitenzi kisaidizi kilichomo kwenye kishazi tegemezi hubeba viambishi virejeshi. Mfano: aliyekimbia, walioimba, walichokikimbia.  Huweza kusimama kama kiima katika sentensi changamano Kijana aliyekimbilia mjini mwaka jana amerudi jana  Kitenzi kisaidizi kilichomo kwenye kishazi tegemezi hufanya kazi ya kuvumisha nomino au kielezi.
  • 21.
    Aina za vishazitegemezi  Kishazi Tegemezi Vumishi (βV)  Hivi huvumisha jina lililoko katika tungo. mfano: mtoto aliyekuja jana anaumwa.  Kishazi Tegemezi Kielezi (βE)  Hivi hutoa maelezo zaidi kwa kitenzi kilicho katika tungo.  Chakula kililiwa kilipoiva.
  • 22.