Lahaja za Kiswahili zimekuwa zikichanganya watumiaji wengi na watu wengi wanaojifunza lugha ya Kiswahili, hivyo matini hii imekusudia kuondoa mkanganyiko huo.
Hii ni makala ya uwasilishaji wa mada ya kukua na kuenea kwa Kiswahili. Mada hii itawafaa sana wanafunzi wa kidato cha tatu na nne katika shule za sekondari nchini Tanzania.
Karibu
Huu ni uwasilishaji wa nadharia ya Pijini na Krioli. Kwa upande mwingine uwasilishaji huu unatathimini asili ya kiswahili katika mrejeo wa nadharia hii.
Mahususi kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita.
Uwasilishaji huu unajikita katika kufafanua chimbuko na asili ya Kiswahili. Umejitosheleza kwa mujibu wa mukhtasari wa Kiswahili kwa kidato cha tatu na nne.
Kwa maswali zaidi au kama unahitaji kujifunza na mimi usisite kunipigia kwa namba unazoziona hapo.
Mada ya Mjengo wa Tung ni moja kati kati ya mada yenye changamoto miongoni mwa wanfunzi wa kidato cha tatu.
Hapa mwanafunzi atapata fursa ya kujikumbusha aliyojifunza na mwalimu darasani.
asante.

UTUNGAJI WA MASHAIRI
- Mashairi ya kale yanajulikana kama mashairi ya kimapokeo mashairi haya hutungwa kwa kufuata kanuni zifuatazo: -
- Kutokana na kanuni hizo shairi la kimapokeo litakuwa na
KICHWA
Shairi lazima liwe na kichwa, kichwa cha shairi hutokana na jambo linalojadiliwa katika shairi. Kichwa hicho huandikwa kwa kutumia maneno machache yasiyozidi matano.
BETI
Hii ni sehemu ndogo ya mada kuu ambayo ni matumizi ya lugha katika miktadha mbalimbali. Lengo la somo hili ni kumfafanulia mwanafunzi mtindo wa lugha unaotumika katika mazingira maalum.
Sarufi Matamshi (Fonolojia). Hii ni sehemu ya mada ndogo katika mada kuu ya Matumizi ya Sarufi kwa kidato cha Tano na Sita nchini Tanzania. Jisikie huru kutoa maoni yako na ushauri. Nitafurahi kama ukinipigia simu au ukinitumia barua pepe kunikosoa au kunirekebisha pale nilipokosea. Asante na karibu sana.
Uwasilishaji huu ni juu ya uhuru wa mtunzi wa kazi za fasihi. Ni nukuu muhimu kwa ajili ya walimu na wanafunzi wa kidato cha tano na sita nchini Tanzania
KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI
UUNDAJI WA MANENO.
MANENO
Kwa kawaida hakuna lugha inayojitosheleza kimawasiliano na kimantiki hivyo hakuna lugha iliyo bora kuliko nyingine.

Uhakiki wa riwaya ya usiku utakapokwisha. Katika vipande-picha hivi utajifunza kuhakiki riwaya hii iliyoandikwa kwa ustadi wa juu na mwanishi Mbunda Msokile.
Maswali ya sayansi kwa wanafunzi wa darasa la sita Tanzania. Ni mkusanyiko wa maswali ya sayansi yaliyowahi kutoka kwenye mitihani mbalimbali ya darasa la sita.
1. LAHAJA ZA KISWAHILI
KWA UJUMLA
Wilson S. Pastory
8/7/2016
Matini hii imedhamiria kutoa uelewa wa jumla kuhusu lahaja za Kiswahili. Hii itasaidia kupunguza
mkanganyiko ambao umekuwepo kwa muda mrefu kuhusu dhana ya lahaja za kiswahili .
2. wilsonpastory@gmail.com
+255 769 526 281
2
LAHAJA ZA KISWAHILI KWA UJUMLA
Lahaja ni dhana changamani na hivyo ili iweze kueleweka vizuri hatuna budi kuchunguza vigezo
vikuu vitatu vinavyotumiwa na wataalamu mbalimbali katika kuelezea maana ya dhana hii.
Vigezo hivyo ni:
o Kigezo cha Isimu jamii
o Kigezo cha Kiisimu
o Kigezo cha Utengamano wa Kijiografia
Kigezo cha Isimu Jamii
Katika kigezo hiki mtafiti huwashirikisha wanajamii au wazungumzaji wa lahaja hiyo ili kupata
msimamo wao kuhusu lahaja husika. Hivyo kupitia mawazo na msimamo wa wazungumzaji au
wanajamii wa lahaja husika, mtafiti wa lugha huweza kuja na hitimisho lake kuhusu dhana ya
lahaja.
Kigezo cha Kiisimu
Hiki ni kigezo cha kutofautisha lugha na lahaja nyingine kwa kutumia vigezo vya msamiati wa
msingi, fonolojia, pamoja na mofolojia. Hapa mtafiti wa lugha huchunguza jinsi maneno
yanavyoundwa, tamkwa na jinsi yanavyofanana katika msamiati wake wa msingi.
Kigezo cha Utengano wa Kijiografia
Kigezo hiki hutazama lahaja Fulani inazungumzwa mahali Fulani na huzungumzwa na watu wa
kundi fulani. Mfano lahaja ya kitumbatu huzungumzwa sehemu ya kisiwa cha Tumbatu, vivyo
3. wilsonpastory@gmail.com
+255 769 526 281
3
hivyo lahaja ya kipemba huzungumzwa na watu wa pemba. Kwakifupi, mtafiti wa lugha hutumia
kigezo cha mahali lahaja fulani inapotumika kuelezea dhana ya lahaja husika.
Kutokana na vigezo vitatu tulivyoviona, kumeweza kushuhudiwa fasili mbalimbali za lahaja,
zifuatazo ni baadhi tu ya fasili za lahaja kama zinavyotolewa na Msanjila (2009) na Massamba
(2002).
Msanjila (2009) anasema kuwa Lahaja ni lugha mojawapo kati ya lugha ambazo kimsingi
uhesabiwa kuwa ni lugha moja isipokuwa zinatofautiana katika baadhi ya vipengele fulani fulani
kama vile lafudhi, fonolojia, msamiati usiokuwa wa msingi au muundo kutokana na eneo lugha
hiyo inapozungumzwa.
Massamba (2002) anasema kuwa Lahaja ni lugha mbalimbali za pwani zilizokuwa na uhusiano
wa karibu sana. Lugha hizo kama vile Kiamu, Kimvita, Kijomvu, Kimtang’ata, Kimakunduchi,
Kitumbatu, Kimgao, Kiunguja, na Ci-mbalazi.
Kwaujumla tunaweza kusema kuwa, Lahaja ni vilugha vidogo vidogo vya lugha moja ambavyo
hubainika kijamii au kijiografia. Au Lahaja ni lugha mojawapo kati ya lugha ambazo kimsingi
uhesabiwa kuwa ni lugha moja isipokuwa zinatofautiana katika baadhi ya vipengele fulani fulani
kama vile lafudhi, fonolojia, msamiati usiokuwa wa msingi au muundo kutokana na eneo lugha
hiyo inamozungumzwa.
IDADI YA LAHAJA ZA KISWAHILI NA JINSI ZILIVYOINUKA
Ilikubaini idadi kamili ya lahaja za Kiswahili, tafiti mbalimbali zimeweza kufanywa, na katika
tafiti hizo kila wataalamu walikuja na idadi tofauti na wataalamu wengine na ivyo kuleta utata
juu ya idadi kamili ya lahaja za Kiswahili. Hata hivyo utafiti wao kwa ujumla umeonesha kuwa
4. wilsonpastory@gmail.com
+255 769 526 281
4
idadi ya lahaja za Kiswahili hulenga kati ya 13 hadi 20. Baadhi ya wataalamu hao ni: Dalby
(1977) aliyepata lahaja 17, Heine (1970) aliyepata lahaja 16, Polome (1967) aliyepata lahaja 17,
Bryan (1959) aliyepata lahaja 18, Stigand (1915) aliyepata lahaja 13, na Chiraghdin (1977)
aliyepata lahaja 20.
Kwakuwa Chiraghdin(1977) ndiye anayeonekana kupata lahaja nyingi zaidi ya Wataalamu
wengine, si vibaya tukiangalia lahaja anazozitaja yeye. Lahaja zilizotajwa na Chiraghdini ni:
Kiunguja
Kimrima
Kimgao
Kimvita
Kihadimu
Kipemba
Kirumba
Kiamu
Kipate
Kisiu
Kitikuu
Kingazija
Kingozi
Kitumbatu
Kimtang’ata
Chichifundi
Chibalanzi
5. wilsonpastory@gmail.com
+255 769 526 281
5
Kingwana
Kinyare
Kijomvu.
MGAWANYO WA LAHAJA KIKANDA AU KIMAENEO
Tunaweza kuzigawa lahaja za Kiswahili katika makundi makuu manne (4) kama ifuatavyo:
Lahaja za kaskazini
Hizi ziko katika mwambao wa Somalia na Kenya. Kundi hili hujumuisha lahaja ndogondogo
kama vile:
i. Kiamu
ii. Kitukuu
iii. Kipate
iv. Kingozi
v. Kisiu
vi. Chimbalazi/Chimini
Lahaja za kusini
Hizi ziko pemba, Unguja na Comoro. Kundi hili hujumuisha lahaja ndogondogo kama vile:
i. Kiunguja
ii. Kihadimu
iii. Kipemba
iv. Kingazija
6. wilsonpastory@gmail.com
+255 769 526 281
6
v. Kitumbatu
Lahaja za katikati
Hizi ni lahaja ambazo hupatikana katika eneo la katikati. Kundi hili hujumuisha lahaja kama
vile:
i. Kivumba
ii. Kimtang’ata
iii. Kimrima
iv. Kimvita
v. Kingao (Kimgao)
Lahaja za Bara
Kundi hili la halaja hujumuisha lahaja za Kiungwana (Zaire) na misemo ya Wageni kama vile
Wazungu na Wahindi.
MAMBO YANAYOSABABISHA LAHAJA KUTOKEA AU CHANZO CHA LAHAJA
Lahaja nyingi zimeenea au zimetokea kutokana na mambo mbalimbali, baadhi ya mambo hayo
ni kama yafuatayo:
Umbali wa Kijiografia
Umbali wa Kijiografia kutoka eneo moja kwenda eneo jingine huweza kusababisha hutokeaji wa
lahaja.
Kutawanyika kwa watu
Kitendo cha watu kuhama hama huweza kusababisha kutokea kwa lahaja.
7. wilsonpastory@gmail.com
+255 769 526 281
7
Kuingiliana na kuoana kwa watu
Kitendo cha watu kuingiliana na kuoana huweza kuchangia hutokeaji wa lahaja, mwingiliano wa
tamaduni tofauti.
Biashara mbalimbali
Biashara mbalimbali pia zimechangia kutokea kwa lahaja, katika biashara mbalimbali baadhi ya
lahaja zimeweza kutokea.
Suala la dini
Suala la dini hususani dini ya Kiislamu limeweza kujangia hutokeaji wa lahaja.
Suala la Elimu na Siasa
Suala la Elimu na Siasa husababisha matabaka ya watu katika jamii, hivyo kutokana na
matabaka haya baadhi ya lahaja huweza kutokea.