Mada ya Mjengo wa Tung ni moja kati kati ya mada yenye changamoto miongoni mwa wanfunzi wa kidato cha tatu.
Hapa mwanafunzi atapata fursa ya kujikumbusha aliyojifunza na mwalimu darasani.
asante.
Lahaja za Kiswahili zimekuwa zikichanganya watumiaji wengi na watu wengi wanaojifunza lugha ya Kiswahili, hivyo matini hii imekusudia kuondoa mkanganyiko huo.

Ushairi wa Kiswahili kuanzia karne ya 16 mpaka karne ya 20Mathieu Roy
Ushairi wa Kiswahili kuanzia karne ya 16 mpaka karne ya 20: Nadharia kuhusu Arudhi na Bahari za Kishairi -
Poésie swahilie du XVième au XXème siècles; théorie sur la métrique et la versification (en kiswahili) -
Kiswahili poetry from the 16th to the 20th centuries: theory about the metrics and meters of kiswahili poems (in Kiswahili)
Sarufi Matamshi (Fonolojia). Hii ni sehemu ya mada ndogo katika mada kuu ya Matumizi ya Sarufi kwa kidato cha Tano na Sita nchini Tanzania. Jisikie huru kutoa maoni yako na ushauri. Nitafurahi kama ukinipigia simu au ukinitumia barua pepe kunikosoa au kunirekebisha pale nilipokosea. Asante na karibu sana.
Uwasilishaji huu ni juu ya uhuru wa mtunzi wa kazi za fasihi. Ni nukuu muhimu kwa ajili ya walimu na wanafunzi wa kidato cha tano na sita nchini Tanzania
Uwasilishaji huu unajikita katika kufafanua chimbuko na asili ya Kiswahili. Umejitosheleza kwa mujibu wa mukhtasari wa Kiswahili kwa kidato cha tatu na nne.
Kwa maswali zaidi au kama unahitaji kujifunza na mimi usisite kunipigia kwa namba unazoziona hapo.
According to Eggins (1994, p.7), systemic functional linguistics claims that language and context are interrelated. To understand how people use language, it need to consider the contexts of language use: the context of culture (Genre) and context of the situation (Register).
FEEL FREE TO USE IT!
This presentation answers some questions like: ''How are languages planned in multilingual countries?, What is the role of TDK in Turkish language reform?, What are the processes of Language Planning?'' Language planning in Switzerland, Canada, India and USA is mentioned in this presentation.
A Critical Discourse Analysis of Malaysian prime minister's speech in Copenh...Roozbeh Kardooni
This paper aim to analysis environmental speech given by Malaysian PM (Najib Tun Razak) during the U.N. CLIMATE CHANGE CONFERENCE 2009 in Copenhagen(cop15).
Maswali ya sayansi kwa wanafunzi wa darasa la sita Tanzania. Ni mkusanyiko wa maswali ya sayansi yaliyowahi kutoka kwenye mitihani mbalimbali ya darasa la sita.

Have you ever thought about starting your own business? Have you ever thought about turning your passion into a profit? A side business or what I like to call, a side hustle, is a great way to grow, make money and escape the 9 to 5.
Please Read and then contact me mapesanestory@yahoo.com/ kabaganga@gmail.com/ mapesanestory@outlook.com or +255752997756/+255684248202 For more readings
1. CHUO KIKUU CHA MTAKATIFU AGUSTINO CHA TANZANIA
KITUO CHA BUKOBA
KITOVU CHA ELIMU
IDARA YA KISWAHILI.
JINA LA KOZI: RIWAYA YA KISWAHILI.
MSIMBO WA KOZI: SW 212
JINA LA MHADHIRI: MALUGU, A.
JINA LA KIKUNDI: SCORPITON
AINA YA KAZI: KAZI YA KIKUNDI.
NAMBA JINA KAMILI NAMBA YA USAJILI SAHIHI
1.
2.
3.
4.
5.
6.
7.
8.
9.
10.
BENEDICTOR ADESA
GODWINILENIDA
KALIJA INNOCENT
KERENGE MAAGE N.
MHADISA ALFA P.
MHILIMA LAURANCE
MWITA MATWIGA E.
NKOKO DOROFINA
RANGSON RAPHAEL M
SYLIVESTER BETNESS N
BAED II 41464
BAED II 41499
BAED II 41538
BAED II 41544
BAED II 41606
BAED II 41607
BAED II 41640
BAED II 41648
BAED II 41659
BAED II 41683
Swali
Bainisha ni vipi riwaya ya “kichwamaji” inastahili kuitwa riwaya ya Kifalsafa
2. Ama kuhusu maana ya riwaya, falsafa ya riwaya ya Kiswahili, wataalamu mbalimbali
wamejaribu kufasili maana ya maneno hayo.Miongoni mwa wataalamu waliofasili dhana hizi
ni pamoja na:-
Wamitila(2003): 178), anasema kuwa riwaya ni kazi ya kinadharia au kibunilizi
ambayohuwa na urefu wa kutosha,msukumo uliojengwa vizuri, wahusika wengi
walioendelezwa kwa kina, yenye kuchukuwa muda mwingi katika maandalizi na kuhusisha
madhari maalumu.
Kamusi ya Kiswahili sanifu (2004) inafasili falsafa kuwa ni elimu ya asili, maana na
sababu za mambo au vitu. Falsafa hujikita katika kutafuta ukweli juu ya mambo au vitu
kupitia imani.
Madumulla (2009:70), anasema kuwa riwaya ya kifalsafa ni riwaya ambayo inajadili
migogoro ya maisha na kutafakari kwa mantiki na kwa kina kuhusu mambo ambayo urazini
wake hauonekani kwa urahisi.
Mwelekeo wa riwaya ya “Kichwa maji”
Kichwa maji ni sawa na kusema debe tupu, hivyo dhana ya “kichwamaji” ni kufanya
mambo ambayo hayaendani na upeo, umri au nafasi uliyonayo mtu katika jamii yake
ambapo mtu huyo huwa anategemewa kuwa msaada mkubwa aidha kwa kutoa ushauri ama
kuleta mabadiliko katika jamii yake kwa mfano katika riwaya hii ya” Kichwa maji” baadhi ya
mhusika wamelinganishwa na dhana hii ya “Kichwamaji” ambapo mhusika kama Kazimoto
katika (uk.194-195) anamwambia mke wake Sabina kwamba “hajui kwanini anaishi, pia
anasema yeye hajijui na mke wake anamwambia kuwa “hakika sikufahamu kuwa wewe ni
kichwa maji namna hiyo”
Mara nyigine falsafa huchukuliwa kama njia pekee inayojaribu kueleza ulimwengu
juu ya mafundisho pamoja na mambo mbalimbali ya kiimani ambayo yanafuatwa na mtu au
kundi la watu kwa kutumia akili na mantiki dhabiti.
“Kichwamaji”ni miongoni mwa riwaya ya kifalsafa, ni miongoni mwa kazi za kifalsafa
iliyojikita na kuendana na mikondo ya nadharia ya kidhanaishi. Kwa hiyo basi tunakubaliana
nakujadili ukweli kuwa riwaya ya “Kichwamaji”iliyoandikwa na E. Kezilahabi ni riwaya ya
kifalsafa kwa kutumia riwaya hii tunajadili jinsi dhana mbalimbali zilivyojitokeza katika riwaya
hii kama ifuatavyo:
Dhana ya ukweli;katika kutafuta dhana hii yaani ukweli ni nini?tunaona mwandishi
anajaribu kueleza falsafa yake ya kutaka kutafuta au kujua kukweli au mambo ambayo
urazini wake hauonekani kirahisi. Kwa mfano katika riwaya hii ya “Kichwamaji”iliyoandikwa
na E. Kazilahabi, tunaona mwandishi anapojaribu kujua ukweli wa mambo hasa
anapomtumia mhusika Kazimoto ambaye anataka kujua ukweli juu ya mambo au matatizo
yaliyo kuwa yakiwasibi ndugu zake. Kwa mfano katika (uk29-30)tunaona wanawake wanalia
jikoni lakini hawakujua kilichokuwa kinawasibu, Rukia na mama yake pia wanamwagiwa
mchanga juu ya vitanda vyao japokuwa ukweli wa mambo waliyokuwa wakifanyiwa
hayakujulikana wazi kuwepo au kutokuwepo kwa wachawi, ingawa Kazimoto anaendelea
kufikiri na kutafuta ukweli wa mambo hayo.
3. Dhana ya maisha ; Katika kujadili au kueleza dhana kuhusu maisha mwandishi
anajaribu kuonesha mitazamo ya wahusika mbalimbali wanaojaribu kupambanua ukweli juu
ya maisha yaani maisha ni nini? Kwa mfano katika (uk 84) Kazimoto anasema “maisha
hayashibwi wala kuridhishwa,” pia katika (uk186) Manase anamwambia Kazimoto “maisha ni
kifo cha polepole,kaburini hatua yetu ya mwisho tu, kwa hiyo kufa ni kuishi.”Kadharika
mwandishi anamchora mhusika Rukia aliyekata tama ya maisha na baada ya kupata mimba
ya kulazimishwa na manase, hivyo Rukia anaona maisha hayanamaana na ndiyo maana
Kazimoto anaambiwa “ndugu yako mekufa akikulilia na aliomba umsamehe na amekuomba
usisikitike sana hata yeye halikuwa haoni tena maana ya kuishi”. (uk83) kwa hiyo dhana ya
maisha inatazwamwa katika mitazamo mbalimbali au tofauti tofauti.
Dhana ya kifo;dhana hii imejitokeza na imejadiliwa katika riwaya hii “kichwamaji
“ambapo mwandishi amejaribu kuchora wahusika mbalimbali namna wanavyokengeushwa
na ukweli juu ya kifo. Kwa mfano mhusika Kazimoto anaamini kuwa kifo ni mstari usiokuwa
na mwisho, katika (uk 123) anaposema “ninaamini kwamba kufa ni kugeuka hali, kama kufa
ni kugeuka hali naamini kwamba kuna kugeuka kwingine kwa hali baada ya kufa, kugeuka
na kugeuka. Ndiyo maana ya mstari usiokuwa na mwisho.”Pia mwandishi anamtumia
mhusika Kazi motoanayesema kifo ni safari ya kwenda mbinguni kwani Kazimoto anasema
“Lakini Kalia kabla ya kwenda mbinguni lazima nife,ndiyo Kalia anajibu” (uk 74).Kwa hiyo
ukweli kuhusu kifo bado unaleta kukengeushi na katika falsafa ya watu kwani bado
linachanguzwa katika namna tofautitofauti miongoni mwa watu.
Dhana ya kuweko au kutokuwekokwa mungu au mambo fulani,dhana hii hujaribu
kufafanua kuweko na kutokuweko mungu au mambo fulani. Dhana hii inajaribu kuthibitisha
katika riwaya hii ya “kichwamaji” ambapo mwandishi anajaribu kuwatumia wahusika
mbalimbali katika kukengeusha ukweli huu wa kuweko au kutokuweko kwa mungu na
mambo mbalimbali.Kwa mfano katika (uk 180) Kazimoto haamini uwepo wa mungu baada
ya kufiwa na mtoto wake anasema “Kama kweli mungu alikuwepo sikuweza kuona kwanini
aliweza kufanya ukatiri mkubwa kama huu”. Pia Kazimoto hamwamini mungu pale
alipokuwa anabishana na wazee alipokuwa akinywa pombe alipomtembelea Kamata(uk.51).
Pia tunaona jinsi Kazimoto anavyomwoko Njuki aliyeanguka ndani ya maji(uk79) na hiyo
inadhihirisha kuwa kila kitu au mtu ana mungu wake anayemsaidia.
Dhana ya uzuri na ubaya ;Hii ni dhana inayojitokeza pia katika riwaya ya
“Kichwamaji” kwani mwandishi anatumia wahusika wake mbalimbali wanaojaribu kutafuta
ukweli juu ya uzuri na ubaya. Kwa mfano katika ( uk 128) kunamajibizano kati ya Manase na
Salima juu ya uzuri na ubaya,wanasema “kwa hiyo wewe unaona kwamba mtu unaona
kwamba mtu ana ubaya na mzuri? Nilimuuliza: Alinyamaza niliendelea kudadisi
swaliililieleweki zaidi .Tuseme sisi hapa, wawili tunatazama picha ile moja pamoja, wewe
unasema ni mzuri, mimi ninasema ni mbaya, Je, siyo kusema kwamba ile picha ina ubaya na
uzuri? Nilimuuliza tena. Mimi ninaona kinyume alisema kwama wewe unaona ubaya, mimi
nzuri ndiyo kuaema kwamba uzuri na ubaya umo mwetu sisi wenyewe na siyo ndani ya
picha au kitu “
Dhana ya wema na ubaya ; katika kueleza falsafa kuhusumafundisho fulani katika
jamii, mwandishi anajadili pia ukweli juu ya wema na ubaya hasa anapowatumia wahusika
wake mbalimbali katika kupata ukweli juu ya dhana hii.Kwa mfano katika riwaya ya
4. “kichwamaji” mwandishi anamtumia mhusika mama na mtoto wake katika kueleza dhana ya
wema na ubaya ambapo tunaona mama na mtoto wake peke yao wakizamishwa na
kusukumiwa kisiwani na mtumbi waliokuwa wakisafiria, lakini kutokana na kukaa kwao kwa
muda mrefu bila kupata chakula nawatu wa kuwaokoa ndipomwanamke anaamua
kuchukuwa jiwe na kujiua ili mtoto apate chakula damu na mwili wake( uk 121 -122).Kwa
hiyo katika kuelezea ukweli juu ya wema na ubaya, Mwandishi anaiacha dhana hii katika
ukengeushi katika akiliza watu kwani huwaacha wakijiuliza maswali je huyu mama alitenda
wema au ubaya?
Kwa kuhitimisha; tunasema kuwa tofauti na dini au itikadi njia ya falsafa ni maantiki
inayoelezea hatua zake ikiwa tayari kuchungulia upya kila hatua iliyochukua. Kwa hiyo
falsafa ni nji ya maswali katika lugha ya kila siku kwani neno “falsafa” mara nyingi lina
chukuliwa kutaja jumla ya mafundisho au imani ya mtu au kundi la watu. Kwa mfano
“falsafa ya chama Fulani,”“falsafa ya maisha yangu” Lakini kwa ujumla fikra hizo hazistahili
kuitwa “falsafa” ila tu kuna makundi ya wana”falsafa” wanopendelea mitazamo au mielekeo
tofauti na kuhusu haya inawezekana kutumia neno”falsafa” ya fulani kwa kutaja matokeo
ya kazi zake kwa mfano “falsafa”ya E. Kazilahabi katika kitabu chake cha “Kichwamaji”
kinachojikuta katika mtazamo ulio katika mwelekeo wa kidhanaishi.
5. MAREJELEO
Kamusi ya Kiswahili Sanifu, (2004). Oxford University Press, East Africa and Taasisi ya
Uchunguzi wa Kiswahili, Kenya.
Kezilehabi, E. (2008), Kichwamaji, Vide~ Muwa Publishers Limited, Nairobi Kenya.
Madumulla, J.S. (2009), Riwaya ya Kiswahili, Mture Education Publishers Limited, Dar es
Salaam Tanzania
Wamitila, K.W.(2003), Uhakiki wa Fasihi, Phoemix Publishers Limited, Nairobi- Kenya.