1. TAMTHILIA MAMA EE
Na ARI KATINI MWACHOFI
UTANGULIZI
Hii ni tamthilia iliyoandikwa na Ari Katini Mwachofi. Mchezo huu
unasawiri matatizo yaliyomo katika taasisi ya ndoa katika jamii.
Ari Katini Mwachofi katika tamthilia Mama Ee anashughulikia uhusiano
wa kijinsia katika taasisi ya ndoa katika jamii yenye taasubi za kiume.
Mtoto anapozaliwa bila shaka lazima alie. Anakua akinung’unika na
anpokuwa mtu mzima yamkini huaga dunia kabla hajatosheka.
Kwenye utangulizi wa Mama Ee tunapata wanawakewatatu.
Wa kwanza ni binti mwenye umri wa miaka kumi na sita, na ni
mjamzito, amevaa matambara na amejitwika mikono kichwani huku
akilia.
Picha tuliyoipata inadhihirisha mazingira ya kukosa tumaini na hali ya
umaskini.Mwanamke wa pili ilisemekana kuwa alikuwa amevalia vizuri,
amebeba mtoto mgongoni lakini pia alikuwa akilia kwa uchungu,
kuashiria kuwa ana mambo yanayomhangaisha kisaikolojia licha ya
kuwa na uwezo.
Mwanamke wa tatu alikuwa amebeba mtoto mgongoni, kitambaa kikuu
begani na tita la kuni kichwani. Hii ilituonyesha taswira ya mwanamke
miongoni mwa jamii nyingi zenye utamaduni wa Kiafrika.
Mama Ee ni tamthilia ya masaibu katika ndoa ya Mwavita na Kinaya.
Mwavita aliolewa kasha akatumbukia kwenye lindi la matatizo
yanayopatikana kwenye baadhi ya ndoa nyingi katika jamii zetu.
Pia ni kilio cha Tenge dadake Mwavita aliyekuwa amepachikwa mimba
na George, jambo lililosababisha kutimuliwa kwa Tenge kutoka
shuleni.
Mwandishi alitumia shairi la tarbia katika utangulizi wa kazi yake.
Shairi hili ni ngonjera na pia aliwatumia wanawake hawa watatu
akidhamiria kutuonyesha kuwa duniani kuna matabaka ya wenye
nguvu na wanyonge.
Tabaka la wanyonge linajipa moyo wa subira, kutia juhudi na kupinga
unyonyaji, kutafuta uhuru, kuungana kudai haki, kujitegemea na
kukataa kutwikwa majukumu kupita kiasi, kugandamizwa, kupuuzwa
na kupigwa.
2. Katika kazi yake mwanamke amechorwa kuwa mwenye nguvu na
mwanamapinduzi huku akipigania hadhi yake.
Mwanamke anapigania ; haki, hadhi, usawa wa jinsia, uwezo wa
kujiamulia na elimu ya kujikomboa. Kwa mfano Mwavita na Tenge
wanakataa kuonewa na mwanamume. Hii ni kwa sababu wanaishi
katika jamii ya nomoni inayoleta hali ya umme katika kiume kama njia
ya kuwaonea wanawake.
MAUDHUI KATIKA TAMTHILIA MAMA EE
• MATATIZO YA UNYUMBA (Marital Problems)
• UBAGUZI WA KIJANA WA JINSIA YA KIKE (DISCRIMINATION
ANGAIST THE FEMALE YOUTH)
• NAFASI YA MILA NA DESTURI KATIKA NDOA (ROLE OF
CULTURAL PRACTICES IN MARRIAGE)
• UMOJA WA WANAWAKE (THE UNITY OF WOMEN)
•