SlideShare a Scribd company logo
1 of 16
1
Biashara ya kuku wa asili
Mwongozo kwa mfugaji
Biashara ya kuku
wa asili
Mwongozo wa uuzaji wa kuku na mazao
yake kwa mfugaji
2
Biashara ya kuku wa asili
RLDC na Uboreshaji wa Maisha Vijijini
Shirika la Rural Livelihood Development Company (RLDC ni moja ya mafanikio
ya ushirikaiano kati ya Tanzania na Uswisi kwenye mchakato wa kupambana na
umaskini na kuboresha maisha ya jamii za vijijini. Hii ni taasisi isiyo ya kibiashara
ili yoanzishwa mwaka 2005 na mashirika ya Intercooperation na Swisscontact,
lengo kuu likiwa kutekeleza Programu ya kuendeleza maisha ya jamii za vijijini
(RLDP). Programu hii inasha bihiana na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupambana
na Umaskini (MKUKUTA). Dhamira kuu ya RLDC ni Kuendeleza/kuboresha mifu
mo ya masoko ili kuwawezesha wazalishaji wa vijijini kutumia
fursa zilipo kuboresha maisha yao.
Kwa sasa, RLDC inatelekeleza awamu ya pili ya mpango wake (2008-2011)
na inaweka msukumo zaidi kwenye uendelezaji wa mifumo ya masoko. RLDC
inafanya kazi katika mikoa sita ya Kanda ya kati-Dodoma, Singida, Morogoro,
Shinyanga, Tabora, na Manyara. Jamii nyingi maskini zinaishi katika ukanda huu
wenye sehemu kubwa yenye hali ya mvua chache na nusu jangwa inayostawisha
shughuli chache za kiuchumi.
Hata hivyo kuna fursa nyingi sana zinazoweza kutoa ajira na kuboresha ya
jamii zake. RLDC inafadhiliwa na Serikali ya Uswisi kupitia shirika la Uswisi la
maendeleo (SDC).
Kwa sasa RLDC inawezesha sekta za pamba, alizeti, maziwa, ufugaji wa kuku wa
kienyeji, mpunga na habari kupitia vipindi vya redio kwa ajili ya wazalishaji wa
vijijini.
“RLDC inaboresha mifumo ya masoko ili kuwezesha wazalishaji wa
vijijini kuinua maisha yao”
Biashara ya kuku
wa asili
Mwongozo wa uuzaji wa kuku na mazao
yake kwa mfugaji
4
Biashara ya kuku wa asili
YALIYOMO
Utangulizi 	 1
Mbinu tofauti za kupata masoko mazuri 	 2
Kufanya makubaliano 	 2
Kuandaa mazingira mazuri ya soko kijijini 	 2
Nini kifanyike ili soko la ndani/ kijijini liwe endelevu? 	 2
Kuandaa na kusafirisha mayai na kuku 	 2
Mbinu bora za kusafirisha kuku 	 2
1
Biashara ya kuku wa asili
Utangulizi
Kuendelea kwa mradi wa ufugagji kuku na kukua kwa kipato cha jamii zinazojihusisha na
ufugaji wa kuku vijijini kunategemea ubora wa kuku na mazao yanayozalishwa pamoja
na soko zuri. Mahitaji ya kuku na mayai ya asili yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku
kutokana na ladha nzuri ya nyama na mayai hayo pamoja na uhalisi wake. Hii ndiyo
sababu (au fursa) ya msingi inayoshawishi kuendelea kuzalisha mazao haya.
Pamoja na kuwepo kwa fursa hizi bado zipo changamoto nyingi katikati eneo la soko
la mazao ya kuku wa asili. Changamoto hizi zinafanya mfugaji asinufaike kiasi cha
kuridhisha kutokana na ufugaji wake.
Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na:
•	 Wafugaji kutokuwa na maamuzi katika kupanga bei ya mazao yao.
•	 Wafugaji kukosa taarifa za bei za kuku wa asili na mayai kwenye masoko mbalimbali.
•	 Kuna idadi kubwa ya wanufaikaji kabla bidhaa haijamfikia mlaji wa mwisho
(mlolongo mrefu wa soko).
•	 Gharama kubwa za usafiri na usafirishaji kwenda sokoni kutokana na hali mbaya
ya miundo mbinu.
Ili mfugaji aweze kupata faida inabidi awe na mbinu za kukabiliana na changamoto hizi
za soko. Katika mwongozo huu yanaelezwa mambo ya kusaidia uuzaji kwa faida baada
ya kuzalisha kuku na mayai.
Mbinu tofauti za kupata masoko mazuri
Kuwa na umoja/mtandao wa wazalishaji na wauzaji wa kuku wa asili
Umoja huu utasaidia kuwawezesha wafugaji kuwa na sauti ya pamoja kupanga na
kusimamia bei ya mazao yao. Upangaji wa bei utazingatia gharama zote za uzalishaji ili
mfugaji apate faida ya kuridhisha. Hii itawezekana kama kuku/mayai yanauzwa katika
sehemu mmoja watakayokubaliana wafugaji.
2
Biashara ya kuku wa asili
Vile vile mtandao utuwarahisishia wanachama kupatiwa huduma za ushauri na wa
kitaalam. Katika umoja huu, wanachama pia wanaweza kuanzisha utaratibu wa kufanya
shughuli ya kuweka na kukopeshana baina yao ili kukidhi mahitaji ya kufanya ufugaji
wao vizuri na hatimaye uwapatie faida wanayotarajia.
Mambo mengine yanayoweza kufanywa na mtandao ni:
kuhakikisha kwamba kuku na mayai ya kila mfugaji yanazalishwa katika viwango
vinavyokubalika na soko au walaji na hivyo kusaidia kupata bei nzuri katika soko.
Uratibu wa shughuli za masoko
Ndani ya kikundi au mtandao huo wa wafugaji, kuwe na kikundi kidogo kama kamati
yenye majukumu ya kuratibu mambo ya masoko ya mayai na kuku wa asili.
Baadhi ya majukumu ya Kamati hii ni kufanya yafuatayo:
A. Kukusanya na kutoa taarifa mbalimbali za masoko ya kuku na mayai kwa ajili
ya kuwahabarisha wafugaji
Muuzaji ana uhuru wa kuuza mazao yake kijijini anapozalishia au kwenye masoko ya
nje. Ili aweze kufanya maamuzi mazuri ya sehemu ya kuuzia, hana budi awe na taarifa
muhimu kuhusu masoko ya nje:
Taarifa muhimu za kukusanya ni:
•	 Bidhaa inahitajika wapi / soko lipo wapi?
•	 Aina gani ya bidhaa inahitajika? Mayai /Nyama
•	 Inanunuliwa kwa bei gani?
•	 Je kwa kipindi husika bidhaa hiyo ipo kwa wingi kiasi gani sokoni na je inakidhi
mahitaji ya soko
•	 Je, mtindo wa uuzaji sokoni uko vipi, ni kupitia madalali au waweza kuuza wewe
mwenyewe kwa mlaji
•	 Ushuru wa soko ukoje
3
Biashara ya kuku wa asili
•	 Upatikanaji wa usafiri na gharama za kusafirisha yaani nauli, vifaa vya kusafirishia
•	 Hali halisi ya wauzaji wa bidhaa kama yako walioko sokoni. Unapotoa uamuzi wa
mahali pa kuuzia jiulize pia kama una uwezo wa kushindana na wauzaji wengine
waliopo kwenye soko hilo
•	 Ratiba ya minada mbalimbali (lini na wapi)
•	 Anwani (simu) za wateja mbalimbali
Taarifa hizi zinaweza kukusanywa kwa njia ya simu, kusafiri ili kukutana na kujadili na
wanunuzi ana kwa ana. Taarifa zikipatikana walio na taarifa wazitoe kwa wanakikundi
wenzao mara kwa mara ili wafugaji wazitumie kufanya maamuzi ya mahali pa kuuzia
kuku na mayai.
Kamati ya kuratibu masoko ijiwekee utaratibu wa kutunza kumbukumbu muhimu za
masoko na kuziweka mahali ambapo wafugaji wanaweza kuzipata kwa urahisi kurejea
wanapozihitaji.
Kufanya makubaliano ya bei
Angalizo
Zinapotafutwa taarifa za sokoni inabidi kuwa
makini na uhakika wa taarifa zinazopatikana. Hii
ni kwa sababu mawasiliano yakifanywa na mtu
asiye wa uhakika kuna uwezekano wa mzalishaji
kubabaishwa na madalali baada ya kufikisha bidhaa
sokoni. Maana hapo wanajua kuwa hutakuwa na
uwezo wa kusimamia bei unayoitaka kutokana na
kuwa:
o	 Utakuwa ugenini hufahamiani na watu wengi.
o	 Haja yako ni kukamilisha mapema shughuli ya
kuuza na kuondoka ili usiingie gharama zaidi
za kuishi ugenini.
4
Biashara ya kuku wa asili
Ili kuepuka usumbufu wa madalali kwa wafugaji watakaoamua kuuzia bidhaa zao kwenye
masoko ya nje, watafutaji wa taarifa wajitahiidi wafanye makubaliano/mawasiliano na
watu wanaowafahamu fika au wakubaliane na mlaji wa mwisho.
Mfano Wa Jedwali La Taarifa Za Masoko	
Tarehe Jina la soko
mfanya
biashara
Anuani/Simu Bei
Kuku Mayai
Gharama
ya usafiri
kwenda na
kurudi
MengineyoGharama ya
kusafirisha
mizigo
					
B. Kutangaza bidhaa kwa walaji kwenye masoko mbalimbali
Hili ni jukumu jingine la waratibu wa mambo ya soko. Matangazo ya upatikanaji wa
bidhaa yatolewe kwa walaji / wateja. Elezea ubora wa bidhaa yako ili kuvutia wateja.
Lakini kabla ya kuitangaza bidhaa, kamati ihakikishe kuwa wafugaji wanao uwezo wa
kuzalisha bidhaa ya kutosheleza hitaji la walaji wanaotangaziwa.
Kama mahitaji ya walaji ya kuku wa asili na mayai ni kubwa, wafugaji wajipange kuzalisha
kuku wengi kwa wakati mmoja ili kukidhi mahitaji ya soko. Njia zifuatazo zizanaweza
kutumika kupata kuku wengi kwa mara moja.
-	 Kwa mtu mmoja mmoja ni kutotolesha vifaranga wengi kwa wakati mmoja.
	 Fanya hivi kwa kwa kutumia njia ya asili au kwa kutumia mashine.
-	 Njia nyingine ya kuwa na kuku wengi wa kuuza kwa wakati mmoja ni kwa wazalishaji
kukubaliana kuungana na kuuza sehemu moja na kwa wakati mmoja.
Mfugaji akijua hali halisi ya soko la nje na la kijijini, ataweza kujua ni wapi kuna faida
zaidi na atafanya maamuzi vema kabla hujapeleka bidhaa yako sokoni.
5
Biashara ya kuku wa asili
C. Pia kamati hii ifuatilie kupata eneo maalum la kuuzia kuku na mayai kijijini
Hii itasaidia kuwa na sauti ya pamoja katika kupanga bei na kuokoa muda wa wanunuzi
badala ya kuzunguka kutafuta kuku /mayai sehemu tofauti.
Kuandaa mazingira mazuri ya soko kijijini
Katika maelezo yaliyotolewa awali, tumeona kwamba mfugaji ana uwezo wa kuuza
kuku au mayai kijijini au kwenye masoko ya nje. Uamuzi wake utategemea ni wapi
patampatia faida zaidi baada ya kuondoa gharama zote za uzalishaji. Vile vile itabidi
azingatie changamoto zinazoendana na mahali anapotaka kuuzia (hasa masoko ya nje)
ajipime kama anaweza kukabiliana nazo na hatimaye kupata faida.
Iwapo wafugaji katika umoja wao wataamua kuuza bidhaa zao kijijini ,watatakiwa
kuzingatia yafuatayo:-
-	 Kuzalisha bidhaa bora ambazo zitawavutia wateja wa ndani na nje kuzifuata.
-	 Bidhaa bora utazipataje?
o	 Kwa kuzingatia kanuni za ufugaji bora ambazo ni –Kuwalisha kuku vyakula
vyenye virutubisho vyote muhimu (Protini, Vitamini, wanga, madini na maji).
Kuku wa asili akilishwa vizuri anafikia uzito wa kuuzika mapema. Hivi nyama
yake pamoja na kuwa na ladha nzuri inakuwa laini, tofauti na ilivyozoeleka
kuwa nyama ya kuku wa asili ni ngumu.
o	 Dhibiti na kutibu magonjwa ya kuku. Itasaidia kuwa na idadi kubwa ya kuku
kwa wakati mwingi.
o	 Dhibiti kuku wenye uhusiano wa damu wasizaliane wenyewe kwa wenyewe.
Ili wasidumae na wasichelewe kufikia uzito wa kuuza mapema.
Baada ya wafugaji kufanikiwa kuwavutia wateja kuja kununua kijijini (soko la ndani),
wanashauriwa wachukue hatua za makusudi kulifanya soko hilo liendelee kuwepo.
6
Biashara ya kuku wa asili
Nini kifanyike ili soko la ndani/ kijijini liwe endelevu?
Kama ilivyolezwa awali, wanunuzi kutoka nje ya kijiji watakuwa tayari kufuata bidhaa
bora (kuku / mayai) kijijini kama watahakikishiwa upatikanaji wake kwa wingi wa kutosha
kutoka sehemu moja. Pia kuku au mayai yapatikane kwa kipindi kirefu kama uzalishaji
wake hufungwi na tofauti za misimu.
Wanunuzi hupenda mazingira ya namna hii kwa sababu huwapunguzia adha ya
kuzunguka sehemu tofauti kutafuta bidhaa kwa muda mrefu. Kwao hii huwaokolea
gharama na katika hali hii wanaweza kununua kwa bei nzuri kutoka kwa mfugaji.
Wafugaji wanaweza kujipanga kufanya yafuatayo kudumisha soko lao la ndani:
•	 Wazalishe kuku wa umri mmoja kwa wingi (kwa mmoja mmoja au kwa kushirikiana.
•	 Kwa vile chanzo kikubwa cha vifo katika kuku ni magonjwa, wafugaji wazingatie
ratiba za chanjo muhimu katika eneo.
•	 Pia huduma za tiba na kwa magonjwa mbalimbali ya kuku yanayojitokeza ipatikane
kwa urahisi na mapema pale inapohitajika. Hii itawezesha wafugaji wengi kuwa
na idadi nzuri ya kuku kwa wakati mwingi katika mwaka. Hivyo mayai na kuku
watapatikana kwa wateja kwa kipindi kirefu.
•	 Haya yote yafanyike kwa kuzingatia/ kuoanisha vipindi ambapo uhitaji wa kuku/
mayai kwa wateja unakuwa mkubwa.
Licha ya kuhakikisha uzalishaji na upatikanaji wa bidhaa ya kutosha kwa wateja kila
wanapoihitaji kuna mambo ya ziada ya kufanya kudumisha uhai wa soko la ndani.
Mambo haya ni pamoja na:
o	 Kuzingatia kuwa na vikao vya mara kwa mara ndani kikundi cha wazalishaji ili
kujadili mafanikio na changamoto. Kisha tafakari namna ya kukabiliana na
changamoto kwa ajili ya uzalishaji kuweza kuendelea mbele.
o	 Wazalishaji walinde ubora wa bidhaa wanayozalisha kwa kuzingatia matakwa ya
soko.
7
Biashara ya kuku wa asili
o	 Kikundi kisitegemee mtu mmoja tu katika kufanya majukumu nyeti ndani ya
kikundi; mfano mawasiliano na wanunuzi kwa ajili ya kutafuta taarifa muhimu
kuhusu masoko yasiachwe mikononi mwa mtu mmoja. Utaalam huu washirikishwe
wengine wachache ili mmoja akipata shida kikundi kisikwame.
o	 Wazalishaji wahakikishe wanaendana na mabadiliko yanayotokea sokoni au kwa
wateja wao. Jitahidi kuzalisha kwa kulenga matakwa ya wateja.
Watafuta taarifa za soko wasifungwe na mazoea ya kuuza kwenye masoko machache
waliyoyazoea.Wadhubutukutafutawanunuzikutokasehemunyingitofautiiwezekanavyo.
Hii itatoa fursa pana ya kulinganisha bei zao na kuamua nani wa kumuuzia kwa faida
zaidi.
Kuandaa na kusafirisha mayai na
kuku
Kutunza mayai kabla ya kuyasafirisha
Ukiamua kufuga kuku wako wa asili kwa ajili
ya kupata mayai ya kuuza, kumbuka kuzingatia
mambo yafuatayo:
	 Usiyaache mayai ndani ya viota kutagia
kwa muda mrefu. Yaokote mayai mara
kwa mara kutegemeana na utagaji,
	 ili kuepuka kuharibiwa kwa mayai na
kuku wenyewe.
	 Mayai yasipohifadhiwa vizuri ni rahisi
kuharibika. Hivyo ni muhimu yahifadhiwe
vyema kabla hayajapelekwa sokoni.
Fanya yafuatayo ili mayai yawe salama:
•	 Yatenge mayai yenye nyufa,
yatumiwe nyumbani kwa kula.
Mayai kwenye chano tayari kwa kusafirisha
8
Biashara ya kuku wa asili
•	 Kama yamechafuka ondoa uchafu kwa mkono mikavu. Usiyaoshe kwa maji
yataharibika upesi, hutaweza kuyahiifadhi kwa muda mrefu.
•	 Yahifadhiwe sehemu isiyokuwa na joto.
Kusafirisha mayai
Mayai yanayosafirishwa yawekwe kwenye chano (tray) za kubebea mayai na kuwekwa
kwenye makasha (boksi) kwa utaratibu ufuatao:-
•	 Mayai yapangwe kwenye chano sehemu iliyochongoka ikiwa inaangalia chini.
•	 Chano zipangwe ndani ya kasha kwa mpango unaokubalika.
•	 Kasha liwe na ukubwa unaolingana na chano kuepusha mtikitisiko.
•	 Kasha liruhusu mzunguko wa hewa.
•	 Kasha liwe imara.
Kama hakuna chano ndani ya mazingira yako, yapakie mayai katika chombo imara kwa
kuyachanganya na pumba ya mpunga au kitu chochote laini kuzuia yasivujike.
Mbinu bora za kusafirisha kuku
Kuku wanaosafirishwa wawekwe kwenye matenga au chombo cha kubebea yenye sifa
zifuatazo:-
•	 Kiwe na nafasi ya kutosha kwa kuku wanaosafirishwa.
•	 Kihurusu mzunguko wa hewa safi.
•	 Kisiwe na uwezekano wa kuumiza kuku.
•	 Kiwe imara.
•	 Kiruhusu kinyesi kudondoka.
•	 Kiwe rahisi kusafisha.
•	 Kiwe na mlango/funiko unaoruhusu kuingiza na kutoa kuku wa urahisi.
•	 Kwa wale wanaosafirishwa mbali kiwe na nafasi ya kuweka chakula na maji.
9
Biashara ya kuku wa asili
Kifaa kama tenga kinafaa kwa kusafirishia kuku
Matenga yanayofaa kubebea kuku
Usiwasafirishe kuku kwa kuwaninginiza kichwa chini miguu juu kama wafanyabiashara
wengi wanavyofanya. Hii inawapatisha kuku shida na kinyume na sheria za haki za
wanyama.
10
Biashara ya kuku wa asili
Namna hii haifai
HITIMISHO
Kuku wa kienyeji wanayo nafasi kubwa ya kuchangia kipato cha mfugaji kama atajitahidi
kufanya haya wakati:
o	 Kabla ya kuuza zalisha bidhaa bora.
o	 Itangaze kwa kuisifia bidhaa yako.
o	 Tafuta taarifa za uhakika za soko.
o	 Zalisha kwa wingi kulingana na hitaji lililopo sokoni.
o	 Panga bei kwa kuzingatia gharama zote za uzalishaji.
11
Biashara ya kuku wa asili
12
Biashara ya kuku wa asili
Jengo la NBC
Ghorofa ya Pili, Mtaa wa Nyerere
S.L.P. 2978, Dodoma, Tanzania.
Simu +255 26 2321455, Faksi +255 26 2321457.
Barua pepe: info@rldc.co.tz.
Tovuti: www.rldc.co.tz.

More Related Content

What's hot

Pelaburan Perdagangan F4
Pelaburan Perdagangan F4Pelaburan Perdagangan F4
Pelaburan Perdagangan F4Miss Jia
 
Buku rekod keluar masuk pelawat
Buku rekod keluar masuk pelawatBuku rekod keluar masuk pelawat
Buku rekod keluar masuk pelawatHasniza Hassan
 
Perjanjian sewa rumah
Perjanjian sewa rumahPerjanjian sewa rumah
Perjanjian sewa rumahalisa1109
 
Topik 9.1 Insurans
Topik 9.1 InsuransTopik 9.1 Insurans
Topik 9.1 InsuransFiza Wahab
 
Sekolah Amanah
Sekolah AmanahSekolah Amanah
Sekolah AmanahVince Here
 
Microsoft word panduan pengelolaan sukan olahraga sekolah
Microsoft word   panduan pengelolaan sukan olahraga sekolahMicrosoft word   panduan pengelolaan sukan olahraga sekolah
Microsoft word panduan pengelolaan sukan olahraga sekolahnorlela zakariah
 
Garis Panduan Geran Agropelancongan pindaan 16 Februari 2021 (OFFICIAL UPLOAD...
Garis Panduan Geran Agropelancongan pindaan 16 Februari 2021 (OFFICIAL UPLOAD...Garis Panduan Geran Agropelancongan pindaan 16 Februari 2021 (OFFICIAL UPLOAD...
Garis Panduan Geran Agropelancongan pindaan 16 Februari 2021 (OFFICIAL UPLOAD...MRizzal
 
Kajian mengenai kesan penggunaan telefon bimbit di kalangan pelajar
Kajian mengenai kesan penggunaan telefon bimbit di kalangan pelajarKajian mengenai kesan penggunaan telefon bimbit di kalangan pelajar
Kajian mengenai kesan penggunaan telefon bimbit di kalangan pelajarZieya Ash
 
42129075 penyataan-sebelum-semasa-dan-slps-pbs-fasa-1
42129075 penyataan-sebelum-semasa-dan-slps-pbs-fasa-142129075 penyataan-sebelum-semasa-dan-slps-pbs-fasa-1
42129075 penyataan-sebelum-semasa-dan-slps-pbs-fasa-1Zhu Miqael
 
Rancangan pengajaran harian(berpusatkan pelajar)
Rancangan pengajaran harian(berpusatkan pelajar)Rancangan pengajaran harian(berpusatkan pelajar)
Rancangan pengajaran harian(berpusatkan pelajar)Fathdzelly Jaya
 
Rph kssr pergerakan berirama
Rph kssr pergerakan beriramaRph kssr pergerakan berirama
Rph kssr pergerakan beriramaGobi Krrish
 
surat aku janji.docx
surat aku janji.docxsurat aku janji.docx
surat aku janji.docxRoziYani1
 
Borang Sarana Peer Coaching
Borang Sarana Peer CoachingBorang Sarana Peer Coaching
Borang Sarana Peer CoachingMokhzani Fadir
 

What's hot (20)

Pelaburan Perdagangan F4
Pelaburan Perdagangan F4Pelaburan Perdagangan F4
Pelaburan Perdagangan F4
 
Pengurusan kewangan
Pengurusan kewanganPengurusan kewangan
Pengurusan kewangan
 
Buku rekod keluar masuk pelawat
Buku rekod keluar masuk pelawatBuku rekod keluar masuk pelawat
Buku rekod keluar masuk pelawat
 
Perjanjian sewa rumah
Perjanjian sewa rumahPerjanjian sewa rumah
Perjanjian sewa rumah
 
Topik 9.1 Insurans
Topik 9.1 InsuransTopik 9.1 Insurans
Topik 9.1 Insurans
 
Sekolah Amanah
Sekolah AmanahSekolah Amanah
Sekolah Amanah
 
Microsoft word panduan pengelolaan sukan olahraga sekolah
Microsoft word   panduan pengelolaan sukan olahraga sekolahMicrosoft word   panduan pengelolaan sukan olahraga sekolah
Microsoft word panduan pengelolaan sukan olahraga sekolah
 
Surat kebenaran murid
Surat kebenaran muridSurat kebenaran murid
Surat kebenaran murid
 
Buku log penggunaan makmal komputer
Buku log penggunaan makmal komputerBuku log penggunaan makmal komputer
Buku log penggunaan makmal komputer
 
Garis Panduan Geran Agropelancongan pindaan 16 Februari 2021 (OFFICIAL UPLOAD...
Garis Panduan Geran Agropelancongan pindaan 16 Februari 2021 (OFFICIAL UPLOAD...Garis Panduan Geran Agropelancongan pindaan 16 Februari 2021 (OFFICIAL UPLOAD...
Garis Panduan Geran Agropelancongan pindaan 16 Februari 2021 (OFFICIAL UPLOAD...
 
TAKLIMAT RMT DAN PSS 2022.pptx
TAKLIMAT RMT DAN PSS 2022.pptxTAKLIMAT RMT DAN PSS 2022.pptx
TAKLIMAT RMT DAN PSS 2022.pptx
 
Rumusan
RumusanRumusan
Rumusan
 
Kajian mengenai kesan penggunaan telefon bimbit di kalangan pelajar
Kajian mengenai kesan penggunaan telefon bimbit di kalangan pelajarKajian mengenai kesan penggunaan telefon bimbit di kalangan pelajar
Kajian mengenai kesan penggunaan telefon bimbit di kalangan pelajar
 
Aku janji 2
Aku janji 2Aku janji 2
Aku janji 2
 
42129075 penyataan-sebelum-semasa-dan-slps-pbs-fasa-1
42129075 penyataan-sebelum-semasa-dan-slps-pbs-fasa-142129075 penyataan-sebelum-semasa-dan-slps-pbs-fasa-1
42129075 penyataan-sebelum-semasa-dan-slps-pbs-fasa-1
 
Rancangan pengajaran harian(berpusatkan pelajar)
Rancangan pengajaran harian(berpusatkan pelajar)Rancangan pengajaran harian(berpusatkan pelajar)
Rancangan pengajaran harian(berpusatkan pelajar)
 
Rph kssr pergerakan berirama
Rph kssr pergerakan beriramaRph kssr pergerakan berirama
Rph kssr pergerakan berirama
 
Model personal
Model personalModel personal
Model personal
 
surat aku janji.docx
surat aku janji.docxsurat aku janji.docx
surat aku janji.docx
 
Borang Sarana Peer Coaching
Borang Sarana Peer CoachingBorang Sarana Peer Coaching
Borang Sarana Peer Coaching
 

More from FLYMAN TECHNOLOGY LIMITED

Flyman Technology Limited Introduction Presentation
Flyman Technology Limited Introduction PresentationFlyman Technology Limited Introduction Presentation
Flyman Technology Limited Introduction PresentationFLYMAN TECHNOLOGY LIMITED
 
Flyman Technology Limited (Mzumbe University Tanzania)
Flyman Technology Limited (Mzumbe University Tanzania)Flyman Technology Limited (Mzumbe University Tanzania)
Flyman Technology Limited (Mzumbe University Tanzania)FLYMAN TECHNOLOGY LIMITED
 
introduction to the document object model- Dom chapter5
introduction to the document object model- Dom chapter5introduction to the document object model- Dom chapter5
introduction to the document object model- Dom chapter5FLYMAN TECHNOLOGY LIMITED
 

More from FLYMAN TECHNOLOGY LIMITED (20)

Flyman Technology Limited Introduction Presentation
Flyman Technology Limited Introduction PresentationFlyman Technology Limited Introduction Presentation
Flyman Technology Limited Introduction Presentation
 
Flyman Technology Limited (Mzumbe University Tanzania)
Flyman Technology Limited (Mzumbe University Tanzania)Flyman Technology Limited (Mzumbe University Tanzania)
Flyman Technology Limited (Mzumbe University Tanzania)
 
Flyman Technology Limited Tanzania
Flyman Technology Limited TanzaniaFlyman Technology Limited Tanzania
Flyman Technology Limited Tanzania
 
Saadani national park 2015
Saadani national park 2015Saadani national park 2015
Saadani national park 2015
 
Entrepreneurship manual BIT
Entrepreneurship manual BITEntrepreneurship manual BIT
Entrepreneurship manual BIT
 
Security chapter6
Security chapter6Security chapter6
Security chapter6
 
introduction to the document object model- Dom chapter5
introduction to the document object model- Dom chapter5introduction to the document object model- Dom chapter5
introduction to the document object model- Dom chapter5
 
Dhtml chapter2
Dhtml chapter2Dhtml chapter2
Dhtml chapter2
 
internet intranet and extranet
internet intranet and extranetinternet intranet and extranet
internet intranet and extranet
 
introduction to web application development
introduction to web application developmentintroduction to web application development
introduction to web application development
 
Marketing management
Marketing managementMarketing management
Marketing management
 
Marketing communications
Marketing communicationsMarketing communications
Marketing communications
 
Marketing analysis
Marketing analysisMarketing analysis
Marketing analysis
 
Market segmentation
Market segmentationMarket segmentation
Market segmentation
 
Consumer markets
Consumer marketsConsumer markets
Consumer markets
 
ENTREPRENEURSHIP MANUAL
ENTREPRENEURSHIP MANUALENTREPRENEURSHIP MANUAL
ENTREPRENEURSHIP MANUAL
 
THINGS NOT TO DO IN A JOB INTERVIEW!
THINGS NOT TO DO IN A JOB INTERVIEW!THINGS NOT TO DO IN A JOB INTERVIEW!
THINGS NOT TO DO IN A JOB INTERVIEW!
 
TAXATION CONCEPTS
TAXATION CONCEPTSTAXATION CONCEPTS
TAXATION CONCEPTS
 
Html tutorial
Html tutorialHtml tutorial
Html tutorial
 
SYSTEM MODELLING
SYSTEM MODELLINGSYSTEM MODELLING
SYSTEM MODELLING
 

Uuzaji wa mazao ya kuku wa asili

  • 1. 1 Biashara ya kuku wa asili Mwongozo kwa mfugaji Biashara ya kuku wa asili Mwongozo wa uuzaji wa kuku na mazao yake kwa mfugaji
  • 2. 2 Biashara ya kuku wa asili RLDC na Uboreshaji wa Maisha Vijijini Shirika la Rural Livelihood Development Company (RLDC ni moja ya mafanikio ya ushirikaiano kati ya Tanzania na Uswisi kwenye mchakato wa kupambana na umaskini na kuboresha maisha ya jamii za vijijini. Hii ni taasisi isiyo ya kibiashara ili yoanzishwa mwaka 2005 na mashirika ya Intercooperation na Swisscontact, lengo kuu likiwa kutekeleza Programu ya kuendeleza maisha ya jamii za vijijini (RLDP). Programu hii inasha bihiana na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupambana na Umaskini (MKUKUTA). Dhamira kuu ya RLDC ni Kuendeleza/kuboresha mifu mo ya masoko ili kuwawezesha wazalishaji wa vijijini kutumia fursa zilipo kuboresha maisha yao. Kwa sasa, RLDC inatelekeleza awamu ya pili ya mpango wake (2008-2011) na inaweka msukumo zaidi kwenye uendelezaji wa mifumo ya masoko. RLDC inafanya kazi katika mikoa sita ya Kanda ya kati-Dodoma, Singida, Morogoro, Shinyanga, Tabora, na Manyara. Jamii nyingi maskini zinaishi katika ukanda huu wenye sehemu kubwa yenye hali ya mvua chache na nusu jangwa inayostawisha shughuli chache za kiuchumi. Hata hivyo kuna fursa nyingi sana zinazoweza kutoa ajira na kuboresha ya jamii zake. RLDC inafadhiliwa na Serikali ya Uswisi kupitia shirika la Uswisi la maendeleo (SDC). Kwa sasa RLDC inawezesha sekta za pamba, alizeti, maziwa, ufugaji wa kuku wa kienyeji, mpunga na habari kupitia vipindi vya redio kwa ajili ya wazalishaji wa vijijini. “RLDC inaboresha mifumo ya masoko ili kuwezesha wazalishaji wa vijijini kuinua maisha yao”
  • 3. Biashara ya kuku wa asili Mwongozo wa uuzaji wa kuku na mazao yake kwa mfugaji
  • 4. 4 Biashara ya kuku wa asili YALIYOMO Utangulizi 1 Mbinu tofauti za kupata masoko mazuri 2 Kufanya makubaliano 2 Kuandaa mazingira mazuri ya soko kijijini 2 Nini kifanyike ili soko la ndani/ kijijini liwe endelevu? 2 Kuandaa na kusafirisha mayai na kuku 2 Mbinu bora za kusafirisha kuku 2
  • 5. 1 Biashara ya kuku wa asili Utangulizi Kuendelea kwa mradi wa ufugagji kuku na kukua kwa kipato cha jamii zinazojihusisha na ufugaji wa kuku vijijini kunategemea ubora wa kuku na mazao yanayozalishwa pamoja na soko zuri. Mahitaji ya kuku na mayai ya asili yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku kutokana na ladha nzuri ya nyama na mayai hayo pamoja na uhalisi wake. Hii ndiyo sababu (au fursa) ya msingi inayoshawishi kuendelea kuzalisha mazao haya. Pamoja na kuwepo kwa fursa hizi bado zipo changamoto nyingi katikati eneo la soko la mazao ya kuku wa asili. Changamoto hizi zinafanya mfugaji asinufaike kiasi cha kuridhisha kutokana na ufugaji wake. Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na: • Wafugaji kutokuwa na maamuzi katika kupanga bei ya mazao yao. • Wafugaji kukosa taarifa za bei za kuku wa asili na mayai kwenye masoko mbalimbali. • Kuna idadi kubwa ya wanufaikaji kabla bidhaa haijamfikia mlaji wa mwisho (mlolongo mrefu wa soko). • Gharama kubwa za usafiri na usafirishaji kwenda sokoni kutokana na hali mbaya ya miundo mbinu. Ili mfugaji aweze kupata faida inabidi awe na mbinu za kukabiliana na changamoto hizi za soko. Katika mwongozo huu yanaelezwa mambo ya kusaidia uuzaji kwa faida baada ya kuzalisha kuku na mayai. Mbinu tofauti za kupata masoko mazuri Kuwa na umoja/mtandao wa wazalishaji na wauzaji wa kuku wa asili Umoja huu utasaidia kuwawezesha wafugaji kuwa na sauti ya pamoja kupanga na kusimamia bei ya mazao yao. Upangaji wa bei utazingatia gharama zote za uzalishaji ili mfugaji apate faida ya kuridhisha. Hii itawezekana kama kuku/mayai yanauzwa katika sehemu mmoja watakayokubaliana wafugaji.
  • 6. 2 Biashara ya kuku wa asili Vile vile mtandao utuwarahisishia wanachama kupatiwa huduma za ushauri na wa kitaalam. Katika umoja huu, wanachama pia wanaweza kuanzisha utaratibu wa kufanya shughuli ya kuweka na kukopeshana baina yao ili kukidhi mahitaji ya kufanya ufugaji wao vizuri na hatimaye uwapatie faida wanayotarajia. Mambo mengine yanayoweza kufanywa na mtandao ni: kuhakikisha kwamba kuku na mayai ya kila mfugaji yanazalishwa katika viwango vinavyokubalika na soko au walaji na hivyo kusaidia kupata bei nzuri katika soko. Uratibu wa shughuli za masoko Ndani ya kikundi au mtandao huo wa wafugaji, kuwe na kikundi kidogo kama kamati yenye majukumu ya kuratibu mambo ya masoko ya mayai na kuku wa asili. Baadhi ya majukumu ya Kamati hii ni kufanya yafuatayo: A. Kukusanya na kutoa taarifa mbalimbali za masoko ya kuku na mayai kwa ajili ya kuwahabarisha wafugaji Muuzaji ana uhuru wa kuuza mazao yake kijijini anapozalishia au kwenye masoko ya nje. Ili aweze kufanya maamuzi mazuri ya sehemu ya kuuzia, hana budi awe na taarifa muhimu kuhusu masoko ya nje: Taarifa muhimu za kukusanya ni: • Bidhaa inahitajika wapi / soko lipo wapi? • Aina gani ya bidhaa inahitajika? Mayai /Nyama • Inanunuliwa kwa bei gani? • Je kwa kipindi husika bidhaa hiyo ipo kwa wingi kiasi gani sokoni na je inakidhi mahitaji ya soko • Je, mtindo wa uuzaji sokoni uko vipi, ni kupitia madalali au waweza kuuza wewe mwenyewe kwa mlaji • Ushuru wa soko ukoje
  • 7. 3 Biashara ya kuku wa asili • Upatikanaji wa usafiri na gharama za kusafirisha yaani nauli, vifaa vya kusafirishia • Hali halisi ya wauzaji wa bidhaa kama yako walioko sokoni. Unapotoa uamuzi wa mahali pa kuuzia jiulize pia kama una uwezo wa kushindana na wauzaji wengine waliopo kwenye soko hilo • Ratiba ya minada mbalimbali (lini na wapi) • Anwani (simu) za wateja mbalimbali Taarifa hizi zinaweza kukusanywa kwa njia ya simu, kusafiri ili kukutana na kujadili na wanunuzi ana kwa ana. Taarifa zikipatikana walio na taarifa wazitoe kwa wanakikundi wenzao mara kwa mara ili wafugaji wazitumie kufanya maamuzi ya mahali pa kuuzia kuku na mayai. Kamati ya kuratibu masoko ijiwekee utaratibu wa kutunza kumbukumbu muhimu za masoko na kuziweka mahali ambapo wafugaji wanaweza kuzipata kwa urahisi kurejea wanapozihitaji. Kufanya makubaliano ya bei Angalizo Zinapotafutwa taarifa za sokoni inabidi kuwa makini na uhakika wa taarifa zinazopatikana. Hii ni kwa sababu mawasiliano yakifanywa na mtu asiye wa uhakika kuna uwezekano wa mzalishaji kubabaishwa na madalali baada ya kufikisha bidhaa sokoni. Maana hapo wanajua kuwa hutakuwa na uwezo wa kusimamia bei unayoitaka kutokana na kuwa: o Utakuwa ugenini hufahamiani na watu wengi. o Haja yako ni kukamilisha mapema shughuli ya kuuza na kuondoka ili usiingie gharama zaidi za kuishi ugenini.
  • 8. 4 Biashara ya kuku wa asili Ili kuepuka usumbufu wa madalali kwa wafugaji watakaoamua kuuzia bidhaa zao kwenye masoko ya nje, watafutaji wa taarifa wajitahiidi wafanye makubaliano/mawasiliano na watu wanaowafahamu fika au wakubaliane na mlaji wa mwisho. Mfano Wa Jedwali La Taarifa Za Masoko Tarehe Jina la soko mfanya biashara Anuani/Simu Bei Kuku Mayai Gharama ya usafiri kwenda na kurudi MengineyoGharama ya kusafirisha mizigo B. Kutangaza bidhaa kwa walaji kwenye masoko mbalimbali Hili ni jukumu jingine la waratibu wa mambo ya soko. Matangazo ya upatikanaji wa bidhaa yatolewe kwa walaji / wateja. Elezea ubora wa bidhaa yako ili kuvutia wateja. Lakini kabla ya kuitangaza bidhaa, kamati ihakikishe kuwa wafugaji wanao uwezo wa kuzalisha bidhaa ya kutosheleza hitaji la walaji wanaotangaziwa. Kama mahitaji ya walaji ya kuku wa asili na mayai ni kubwa, wafugaji wajipange kuzalisha kuku wengi kwa wakati mmoja ili kukidhi mahitaji ya soko. Njia zifuatazo zizanaweza kutumika kupata kuku wengi kwa mara moja. - Kwa mtu mmoja mmoja ni kutotolesha vifaranga wengi kwa wakati mmoja. Fanya hivi kwa kwa kutumia njia ya asili au kwa kutumia mashine. - Njia nyingine ya kuwa na kuku wengi wa kuuza kwa wakati mmoja ni kwa wazalishaji kukubaliana kuungana na kuuza sehemu moja na kwa wakati mmoja. Mfugaji akijua hali halisi ya soko la nje na la kijijini, ataweza kujua ni wapi kuna faida zaidi na atafanya maamuzi vema kabla hujapeleka bidhaa yako sokoni.
  • 9. 5 Biashara ya kuku wa asili C. Pia kamati hii ifuatilie kupata eneo maalum la kuuzia kuku na mayai kijijini Hii itasaidia kuwa na sauti ya pamoja katika kupanga bei na kuokoa muda wa wanunuzi badala ya kuzunguka kutafuta kuku /mayai sehemu tofauti. Kuandaa mazingira mazuri ya soko kijijini Katika maelezo yaliyotolewa awali, tumeona kwamba mfugaji ana uwezo wa kuuza kuku au mayai kijijini au kwenye masoko ya nje. Uamuzi wake utategemea ni wapi patampatia faida zaidi baada ya kuondoa gharama zote za uzalishaji. Vile vile itabidi azingatie changamoto zinazoendana na mahali anapotaka kuuzia (hasa masoko ya nje) ajipime kama anaweza kukabiliana nazo na hatimaye kupata faida. Iwapo wafugaji katika umoja wao wataamua kuuza bidhaa zao kijijini ,watatakiwa kuzingatia yafuatayo:- - Kuzalisha bidhaa bora ambazo zitawavutia wateja wa ndani na nje kuzifuata. - Bidhaa bora utazipataje? o Kwa kuzingatia kanuni za ufugaji bora ambazo ni –Kuwalisha kuku vyakula vyenye virutubisho vyote muhimu (Protini, Vitamini, wanga, madini na maji). Kuku wa asili akilishwa vizuri anafikia uzito wa kuuzika mapema. Hivi nyama yake pamoja na kuwa na ladha nzuri inakuwa laini, tofauti na ilivyozoeleka kuwa nyama ya kuku wa asili ni ngumu. o Dhibiti na kutibu magonjwa ya kuku. Itasaidia kuwa na idadi kubwa ya kuku kwa wakati mwingi. o Dhibiti kuku wenye uhusiano wa damu wasizaliane wenyewe kwa wenyewe. Ili wasidumae na wasichelewe kufikia uzito wa kuuza mapema. Baada ya wafugaji kufanikiwa kuwavutia wateja kuja kununua kijijini (soko la ndani), wanashauriwa wachukue hatua za makusudi kulifanya soko hilo liendelee kuwepo.
  • 10. 6 Biashara ya kuku wa asili Nini kifanyike ili soko la ndani/ kijijini liwe endelevu? Kama ilivyolezwa awali, wanunuzi kutoka nje ya kijiji watakuwa tayari kufuata bidhaa bora (kuku / mayai) kijijini kama watahakikishiwa upatikanaji wake kwa wingi wa kutosha kutoka sehemu moja. Pia kuku au mayai yapatikane kwa kipindi kirefu kama uzalishaji wake hufungwi na tofauti za misimu. Wanunuzi hupenda mazingira ya namna hii kwa sababu huwapunguzia adha ya kuzunguka sehemu tofauti kutafuta bidhaa kwa muda mrefu. Kwao hii huwaokolea gharama na katika hali hii wanaweza kununua kwa bei nzuri kutoka kwa mfugaji. Wafugaji wanaweza kujipanga kufanya yafuatayo kudumisha soko lao la ndani: • Wazalishe kuku wa umri mmoja kwa wingi (kwa mmoja mmoja au kwa kushirikiana. • Kwa vile chanzo kikubwa cha vifo katika kuku ni magonjwa, wafugaji wazingatie ratiba za chanjo muhimu katika eneo. • Pia huduma za tiba na kwa magonjwa mbalimbali ya kuku yanayojitokeza ipatikane kwa urahisi na mapema pale inapohitajika. Hii itawezesha wafugaji wengi kuwa na idadi nzuri ya kuku kwa wakati mwingi katika mwaka. Hivyo mayai na kuku watapatikana kwa wateja kwa kipindi kirefu. • Haya yote yafanyike kwa kuzingatia/ kuoanisha vipindi ambapo uhitaji wa kuku/ mayai kwa wateja unakuwa mkubwa. Licha ya kuhakikisha uzalishaji na upatikanaji wa bidhaa ya kutosha kwa wateja kila wanapoihitaji kuna mambo ya ziada ya kufanya kudumisha uhai wa soko la ndani. Mambo haya ni pamoja na: o Kuzingatia kuwa na vikao vya mara kwa mara ndani kikundi cha wazalishaji ili kujadili mafanikio na changamoto. Kisha tafakari namna ya kukabiliana na changamoto kwa ajili ya uzalishaji kuweza kuendelea mbele. o Wazalishaji walinde ubora wa bidhaa wanayozalisha kwa kuzingatia matakwa ya soko.
  • 11. 7 Biashara ya kuku wa asili o Kikundi kisitegemee mtu mmoja tu katika kufanya majukumu nyeti ndani ya kikundi; mfano mawasiliano na wanunuzi kwa ajili ya kutafuta taarifa muhimu kuhusu masoko yasiachwe mikononi mwa mtu mmoja. Utaalam huu washirikishwe wengine wachache ili mmoja akipata shida kikundi kisikwame. o Wazalishaji wahakikishe wanaendana na mabadiliko yanayotokea sokoni au kwa wateja wao. Jitahidi kuzalisha kwa kulenga matakwa ya wateja. Watafuta taarifa za soko wasifungwe na mazoea ya kuuza kwenye masoko machache waliyoyazoea.Wadhubutukutafutawanunuzikutokasehemunyingitofautiiwezekanavyo. Hii itatoa fursa pana ya kulinganisha bei zao na kuamua nani wa kumuuzia kwa faida zaidi. Kuandaa na kusafirisha mayai na kuku Kutunza mayai kabla ya kuyasafirisha Ukiamua kufuga kuku wako wa asili kwa ajili ya kupata mayai ya kuuza, kumbuka kuzingatia mambo yafuatayo: Usiyaache mayai ndani ya viota kutagia kwa muda mrefu. Yaokote mayai mara kwa mara kutegemeana na utagaji, ili kuepuka kuharibiwa kwa mayai na kuku wenyewe. Mayai yasipohifadhiwa vizuri ni rahisi kuharibika. Hivyo ni muhimu yahifadhiwe vyema kabla hayajapelekwa sokoni. Fanya yafuatayo ili mayai yawe salama: • Yatenge mayai yenye nyufa, yatumiwe nyumbani kwa kula. Mayai kwenye chano tayari kwa kusafirisha
  • 12. 8 Biashara ya kuku wa asili • Kama yamechafuka ondoa uchafu kwa mkono mikavu. Usiyaoshe kwa maji yataharibika upesi, hutaweza kuyahiifadhi kwa muda mrefu. • Yahifadhiwe sehemu isiyokuwa na joto. Kusafirisha mayai Mayai yanayosafirishwa yawekwe kwenye chano (tray) za kubebea mayai na kuwekwa kwenye makasha (boksi) kwa utaratibu ufuatao:- • Mayai yapangwe kwenye chano sehemu iliyochongoka ikiwa inaangalia chini. • Chano zipangwe ndani ya kasha kwa mpango unaokubalika. • Kasha liwe na ukubwa unaolingana na chano kuepusha mtikitisiko. • Kasha liruhusu mzunguko wa hewa. • Kasha liwe imara. Kama hakuna chano ndani ya mazingira yako, yapakie mayai katika chombo imara kwa kuyachanganya na pumba ya mpunga au kitu chochote laini kuzuia yasivujike. Mbinu bora za kusafirisha kuku Kuku wanaosafirishwa wawekwe kwenye matenga au chombo cha kubebea yenye sifa zifuatazo:- • Kiwe na nafasi ya kutosha kwa kuku wanaosafirishwa. • Kihurusu mzunguko wa hewa safi. • Kisiwe na uwezekano wa kuumiza kuku. • Kiwe imara. • Kiruhusu kinyesi kudondoka. • Kiwe rahisi kusafisha. • Kiwe na mlango/funiko unaoruhusu kuingiza na kutoa kuku wa urahisi. • Kwa wale wanaosafirishwa mbali kiwe na nafasi ya kuweka chakula na maji.
  • 13. 9 Biashara ya kuku wa asili Kifaa kama tenga kinafaa kwa kusafirishia kuku Matenga yanayofaa kubebea kuku Usiwasafirishe kuku kwa kuwaninginiza kichwa chini miguu juu kama wafanyabiashara wengi wanavyofanya. Hii inawapatisha kuku shida na kinyume na sheria za haki za wanyama.
  • 14. 10 Biashara ya kuku wa asili Namna hii haifai HITIMISHO Kuku wa kienyeji wanayo nafasi kubwa ya kuchangia kipato cha mfugaji kama atajitahidi kufanya haya wakati: o Kabla ya kuuza zalisha bidhaa bora. o Itangaze kwa kuisifia bidhaa yako. o Tafuta taarifa za uhakika za soko. o Zalisha kwa wingi kulingana na hitaji lililopo sokoni. o Panga bei kwa kuzingatia gharama zote za uzalishaji.
  • 16. 12 Biashara ya kuku wa asili Jengo la NBC Ghorofa ya Pili, Mtaa wa Nyerere S.L.P. 2978, Dodoma, Tanzania. Simu +255 26 2321455, Faksi +255 26 2321457. Barua pepe: info@rldc.co.tz. Tovuti: www.rldc.co.tz.