SlideShare a Scribd company logo
1 of 64
Download to read offline
¯ :




 Mimi ni
Mwislamu
     Authorship
Muhammed Ashraf Salah
Mimi ni Mwislamu
Mimi ni Mwislamu




Kwa jina la Mungu wa Rehema


hgfedc ba`_

             : ¯       kji

Na mtu anataka dini nyingine zaidi ya
Uislamu wala kukubali kuwa wakati ni
 mmoja wa wenye kukhasiri Akhera
                           Al-Imran: 85
Mimi ni Mwislamu




Copyright, distribution and translation are
       reserved for every Muslim

Legal Deposit No.          22274 / 2008

International Serial      977-6157-64-5


     For charitable distribution call:
            0020101459613
         For suggestions e-mail:
      anamuslim@windowslive.com
        WWW.Iam-Muslim.com
Mimi ni Mwislamu

   (1) KUMWAMINI MWENYEZI
           MUNGU
Mimi ni Mwislamu…
  • Ninamwamini          Mwenyezi       Mungu
     Pekee Asiye na mshirika na hakuna
     mola mwingine isipokuwa Yeye,
     Hakuzaa       wala     Hakuzaliwa,      na
     hakuna kamwe kifano chake.
  • Ameumba mbingu na ardhi, Naye
     Ndiye       Anayezimiliki.      Anayajua
     yaliyofichikana na yenye kuonekana.
     Yu Hai na Hafi, Anayasimamia
     mambo yote milele na Halali.
  • Ana Majina Mazuri Kabisa na Sifa za
     Juu. Kati yake ni Majina tisini na tisa,
     mwenye kuyajua na kuyadhibiti
     vyema na akamwomba Mwenyezi
     Mungu Kwayo, ataingia peponi.
  • Kati yake ni Sifa za Upweke, kwani Yeye
     Subhaanahu wa Taalaa ni Mmoja wa
     Dhati, Sifa na Vitendo, Aliyepwekeka, Aliye
     Pekee,      Mkusudiwa,       Mmiliki   wa
     ufalme.
Mimi ni Mwislamu
• Na Sifa za Utukufu, kwani Yeye ni
  Mwenye hekima, Mwenye habari ya
  kila jambo, Mwelekezaji wa manufaa,
  Haki, wa Mwanzo, wa Mwisho, wa
  Dhahiri, wa Siri, Mrithi, Mwenye
  Kubakia, Mkwasi, Mtakasifu, Mwenye
  Kushuhudia, Aliye Karibu, Mbora wa
  Kupangilia,    Mwadilifu,   Nuru   ya
  mbingu na ardhi, Mwenye Utukufu na
  Ukarimu.
• Na Sifa za Uadhama, kwani Yeye ni
  Mshindi Asiyeshindika, Mwenye Sifa
  zote Tukufu, Mwenye Uadhama,
  Mwenye Sifa za Utukuzo, Mwenye
  Kulazimisha, Mwenye Nguvu, Aliye
  Imara, Mteza nguvu, Mweza, Mwenye
  uwezo wa juu, Mwingi wa Kunusuru,
  Aliye Juu, Aliye Juu ya vyote.
• Na Sifa za Uwezo, kwani Yeye ni
  Mwingi wa Ujuzi, Mwenye Kusikia,
  Mwenye kuona, Yu Hai,
Mwenye Kukamata, Mwenye Kukunjua,
Mwenye         Kushusha,         Mwenye
Kupandisha,      Mwenye       Kutukuza,
Mwenye Kudhalilisha, Mwenye Kutoa,
Mwenye Kuzuia, Mwenye Kunufaisha,
Mimi ni Mwislamu
Mwenye Kudhuru, Mwenye Kuhuisha,
Mwenye Kufisha, Mwenye Kutanguliza
na Mwenye Kuchelewesha.
• Na Sifa za Uumbaji, kwani Yeye ni
   Muumbaji, Msanifu wa Maumbile,
   Mtiaji Sura, Hakimpiti au Kumshinda
   kitu, Mbunifu, Mwenye Kuanzisha,
   Mwenye Kurejesha, Mwenye Kufufua,
   Mwenye Kukusanya, Mpaji Mkuu,
   Mfunguzi wa kila jambo, Mwingi wa
   Kuruzuku,     Mwenye      Kutajirisha,
   Mdhibiti wa idadi, Mwenye Kudhibiti
   mambo, Mwenye Kuhifadhi, Mlinzi na
   Muumbaji wa mbingu na ardhi bila
   ruwaza.
• Sifa za Rehma, kwani Yeye ni Mwingi
   wa Rehma, Mwingi wa Kurehemu,
   Mwingi     wa    Huruma,      Mwenye
   Kuneemesha neema nzuri, Mwingi wa
   Penzi, Mtenda Wema, Mwingi wa
   Kughufiria, Mwenye Kusamehe, Mwingi
   wa Kukubali toba, Mwenye Amani,
   Mtoaji amani na imani, Mpole, Mwenye
   Kulipa vyema, Mkarimu, Mwenye
   Kuneemesha,    Mwingi    wa    Kutoa,
   Mwenye Kusaidia, Mwenye Kujibu,
Mimi ni Mwislamu
    Mkunjufu, Mwingi wa subira, Mvumilivu
    kwa Waja Wake, Latifu, Wakili, Mwenye
    Kutoa Misaada, Mwenye Kuombwa
    msaada na Mwenye Kukubali toba.
•   Amemneemesha mwanadamu neema
    nyingi zisizo na hesabu. Na hakuna
    neema yoyote anayoneemeka nayo
    mja ila hutoka kwa Mwenyezi Mungu
    Pekee, kwani Yeye Ndiye Aliyemuumba
    na Akampa uhai, Akamfanya asikie na
    aone, Akamkirimu, kisha Akamruzuku
    na Akamfanyia wema.
•   Kwa ajili hiyo, ni lazima mja
    amwabudu Mwenyezi Mungu Peke
    Yake – nako ni kufuata amri Yake na
    kuacha makatazo Yake – kwa kuwa
    hastahiki        yeyote   kuabudiwa
    isipokuwa Mwenyezi Mungu Peke
    Yake.
•   Vile vile, bila shaka Mwenyezi Mungu
    Anazijua hali zote za mja kati ya
    utiifu
Mimi ni Mwislamu

na uasi. Hivyo basi, ni wajibu moyo wa
mja ujae haiba kwa Mwenyezi Mungu
Mtukufu, utukuzo na mapenzi, na aone
haya kumwasi na aachane na maasi,
kwani Mwenyezi Mungu Humwona
wakati akiyafanya.
• Anafurahi kwa amali zake njema
  zinazomkurubisha kwenye radhi za
  Muumbaji wake Subhaanahuu wa
  Taala. Hivyo huzidi kufanya amali
  hizo hadi kufikia ngazi ya ihsani,
  kwani imani huzidi kwa matendo
  mema na hupungua kwa maasi.
• Asivutike kwenye matamanio, hawaa
  au bid'a, bali avutike kwa Mwenyezi
  Mungu      Pekee      huku    akifuata
  maamrisho ya Mtume Swalla Allaahu
  Alayhi    wa    Aalihii  wa    Sallam.
  Asitafute kwa amali yake starehe
  ndogo ya dunia bali atafute kwayo
  malipo toka kwa Mwenyezi Mungu tu.
• Aidha, hakika Mwenyezi Mungu Ana
  huruma mno kwa mwanadamu kuliko
  huruma ya mama kwa mwanaye. Na
  rehma Yake imekienea kila kitu.
Mimi ni Mwislamu
    Hivyo basi, ni wajibu kwa mja
    amwombe na anyenyekee Kwake
    katika haja zake za kidunia na za
    kiakhera, na wala asimwombe yeyote
    mwingine.
•   Kwa vile hakuna faida yoyote ya
    kumwomba asiye Mwenyezi Mungu,
    kwa kuwa hamiliki uwezo ulio kamili
    isipokuwa Mwenyezi Mungu, na
    hakuna     asikiaye    ya    siri    na
    minong'ono ila Mwenyezi Mungu, na
    hakuna      anayemiliki     makadirio
    isipokuwa Mwenyezi Mungu, basi
    kwa maana hiyo, hakuna wa kujibu
    dua isipokuwa Mwenyezi Mungu.
•   Na kwa ajili hiyo, haijuzu kwa
    Mwislamu     kuliomba     kaburi,    au
    kumwomba         aliyezikwa       humo
    vyovyote awavyo, kwa kuwa yeye
    hamsikii. Na kama hamsikii, basi ni
    vipi atamjibu au kumnufaisha? Hakika
    Mwenyezi     Mungu      Pekee     Ndiye
    Mwenye Kunufaisha na Mwenye
    Kudhuru. Na kwa ajili hiyo, ni wajibu
    kwa Mwislamu asijenge msikiti juu ya
    makaburi,    kwani    Mtume     Swalla
Mimi ni Mwislamu
    Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam
    amelikataza hilo.
•   Kadhalika, ni wajibu kwa mja
    alinganishe kati ya udhaifu wake na
    Nguvu za Mwenyezi Mungu Mtukufu,
    na kati ya umasikini wake na Utajiri
    wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kati
    ya ujinga wake na Elimu           ya
    Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kati ya
    unyonge wake na Utukufu wa
    Mwenyezi Mungu Mtukufu.
•   Na ajue kwamba utukufu ni wa
    Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na
    Waumini.
•   Hivyo yampasa awe ni miongoni mwa
    Waumini hawa ambao hawatawakali
    isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu
    Pekee,   wala     hawaombi   msaada
    isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu,
    wala hawaombi kinga na kujilinda
    isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu,
    wala hawaombi msaada wa dharura
    ila kwa Mwenyezi Mungu, wala
    hawamwogopi isipokuwa Mwenyezi
    Mungu, wala hawataraji isipokuwa
    kwa     Mwenyezi      Mungu,   wala
Mimi ni Mwislamu
      hawamwombi isipokuwa Mwenyezi
      Mungu, wala hawachinji isipokuwa
      kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wala
      hawaweki nadhiri isipokuwa kwa ajili
      ya Mwenyezi Mungu, wala hawaapi
      isipokuwa kwa Jina la Mwenyezi
      Mungu, wala hawaweki talasimu na
      hirizi   (amali),   wala     hawasadiki
      wasemayo        makuhani,      watabiri
      (wanajimu) na wachawi, na wala
      hawawaendei.
   • Na wao hawakosi rajua, na huwa na
      tahadhari ya mponyoko wa ndimi zao
      ili    wasije     kutelezea     motoni.
      Hawasemi: "Amependa Mwenyezi
      Mungu na amependa fulani", "lau si
      Mwenyezi       Mungu       na   wewe",
      "nimetawakali kwa Mwenyezi Mungu
      na      kwako".       Bali     waseme:
      "Nimetawakali kwa Mwenyezi Mungu
      Pekee",      "Amependa        Mwenyezi
      Mungu kisha amependa fulani".
     Maneno         haya      humsawazisha
Mwenyezi Mungu na waja Wake,            na ni
katika shirki ndogo.
Mimi ni Mwislamu
•   Na    kama    ilivyo   wajibu   kwetu
    kumwamini Mwenyezi Mungu, ni
    wajibu wetu vile vile tuwakatae
    mataghuti.
•   Na kigogo wa mataghuti ni shetani
    na kila yule aliyeabudiwa badala ya
    Mwenyezi Mungu naye akaridhia hilo.
•   Na kati ya mataghuti hawa ni yule
    aliyetunga sheria zinazoharamisha
    Aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu,
    au    kuhalalisha    Aliyoyaharamisha
    Mwenyezi Mungu.
•   Aidha,    taghuti     ni   kila  yule
    aliyelingania hilo, au akawaamuru
    watu hilo, au akahukumu kwa hilo,
    kwa vile ametaadi na akavuka mpaka
    wa kiumbe wa kusikia na kutii.
• Basi      Allaah    Pekee    Ndiye
    Aliyewaumba wanadamu, na Ndiye
    Anayejua yanayowafaa, na kwa
    hivyo,  hakuna   yeyote  awezaye
    kuwapangia sheria isipokuwa Yeye
    tu.
Mimi ni Mwislamu

    (2) KUWAAMINI MALAIKA

•   Ninaamini kuwepo malaika ambao
    Mwenyezi     Mungu      Amewaumba
    kutokana na nuru, na Akawafanya
    kuwa na mbawa mbili mbili, tatu
    tatu, na nne nne. Nao hawali,
    hawanywi, hawalali wala hawaoi.
    Amewaamuru      kufanya    kazi   na
    kusimamia majukumu mbalimbali,
    nao hutekeleza hayo.
•   Malaika siku zote humtii Mwenyezi
    Mungu bila kuchoka. Hawamwasi na
    humwogopa Mola wao toka juu yao.
    Kuna kati yao aliyesujudu toka siku
    Alipoziumba     Mwenyezi      Mungu
    mbingu na ardhi hadi siku ya Kiyama.
    Na atakaponyanyua kichwa chake
    atasema:                "Subhaanak!
    Hatujakuabudu        ukweli      wa
    kukuabudu".
•   Wao ni waja wa Mwenyezi Mungu na
    si wanawake, na wala si wasaidizi
    Wake, na wao watawaombea shifaa
Mimi ni Mwislamu
  Waumini – kwa idhini ya Mwenyezi
  Mungu – siku ya Kiyama.

Kati ya malaika hawa, wapo:
  • Walinzi ambao huwalinda viumbe
      na madhara.
  • Watukufu       waandishi    ambao
      huandika matendo ya wanadamu,
      mema yao na mabaya yao.
  • Wenye       kumsabihi    Mwenyezi
      Mungu.      Hawa       humsabihi
      Mwenyezi Mungu mchana na usiku
      na hawachoki mpaka siku ya
      Kiyama.
  • Wenye         kuvinjari     ambao
      huhudhuria vikao vya dhikri,
      kisomo cha Qura-aan na vikao vya
      elimu.
  • Wabebaji Arshi ambao idadi yao ni
      wanane. Ni viumbe wakubwa mno
      kati ya viumbe wa Mwenyezi
      Mungu. Ndege huruka toka ncha
      ya sikio la mmoja wao hadi
      shingoni kwa muda wa miaka mia
      tano.
Mimi ni Mwislamu
•   Malaika wa mauti anayezitoa roho
    za viumbe kwa Amri ya Mwenyezi
    Mungu. Huyu ana wasaidizi wake.
•   Israfil atakayelipuliza baragumu,
    kisha viumbe vyote vitakufa kabla
    ya     kutokea    Kiyama.    Kisha
    litapulizwa   jingine,  na   hapo
    watasimama viumbe wakiangalia.
•   Mikaili anayesimamia jukumu la
    mvua.
•   Ridhwaan ambaye ni mlinzi wa
    Pepo. Yeye ana wasaidizi wake
    walio     mbioni     kuwahudumia
    Waumini Peponi.
•   Maalik ambaye ni mlinzi wa moto.
    Ana     wasaidizi   wake    ambao
    viongozi wao ni kumi na tisa.
    Wana marungu ya chuma ya
    kuwaadhibu makafiri motoni -
    Mwenyezi Mungu Atuepushe na
    hayo.
•   Mkuu     wa    Malaika   ni  Jibril
    aliyewakilishwa kupeleka wahyi
    kwa Manabii na Mitume.
Mimi ni Mwislamu
•   Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa
    Aalihii wa Sallam alimwona katika
    umbile lake. Kutokana na ukubwa
    wake, alizifunika peo za mbingu.
    Ana mbawa mia sita, naye ndiye
    aliyekikamata kijiji cha Lut kwa
    ncha      ya     ubawa       wake,
    akakinyanyua hadi juu mbinguni,
    kisha akakipindua juu chini.
•   Kuna malaika wengineo wengi
    zaidi ya hawa, na hakuna ajuaye
    askari wa Mola wako isipokuwa
    Yeye tu.

            :¯   ´ ³ ²± °
•   Malaika   huwapenda   Waumini
    ambao      Mwenyezi     Mungu
    Huwapenda     na    huwaombea
    maghfira.
•   Malaika mbali na nguvu zao hizi
    hupigana pamoja na Waumini.
Mimi ni Mwislamu
    (3) KUVIAMINI VITABU

•   Ninaviamini Vitabu vya Mwenyezi
    Mungu Alivyoviteremsha kwa Mitume
    Wake, na kwamba katika asili ya
    kuteremshwa Kwake, ni Maneno ya
    Mwenyezi Mungu Aliyowafunulia ili
    waifikishe sheria na dini Yake. Vitabu
    vikubwa zaidi ni:
          Quraan Tukufu iliyoteremshwa
    kwa Mtume wetu           Muhammad
    Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa
    Sallam.
         Injili iliyoteremshwa kwa Iysa
    Alayhi Ssalaam.
         Taurat   iliyoteremshwa     kwa
    Musa Alayhi Ssalaam.
         Zaburi   iliyoteremshwa     kwa
    Daud Alayhi Ssalaam.
         Sahifa zilizoteremshwa      kwa
    Ibrahim Alayhi Ssalaam.
Mimi ni Mwislamu
•   Kati ya hivi, kuna vilivyopotolewa na
    kubadilishwa kabla ya kushuka Qur-
    aan.
•   Na Qur-aan ndiyo iliyo juu ya Vitabu
    hivi, na ndiyo yenye kuongoza sheria
    zote na hukumu zake, na yenye
    kuondosha yale yote yenye kwenda
    kinyume na hukumu zake baada tu
    ya kuteremka kwake.
•   Na     kwamba    Mwenyezi    Mungu
    Hatokubali siku ya Kiyama ila amali
    kupitia    uongofu   wa    Qur-aan.
    Hatokubali amali kwa kufuata Vitabu
    vilivyotangulia baada ya kuteremka
    Qur-aan kwa Mtume Muhammad
    Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa
    Sallam.
•   Na kwamba Qur-aan ni Maneno ya
    Mwenyezi Mungu ya miujiza. Maneno
    haya yana utukufu wake, na wala
    hayaingiliwi na batili kabla yake wala
    baada yake. Mwenye kuyasema,
    amesema      kweli,     na    mwenye
    kuhukumia       kwayo,       amefanya
    uadilifu, na mwenye kuyafanyia kazi
Mimi ni Mwislamu
    basi hakika ameongolewa katika njia
    iliyonyooka, mwenye kushikamana
    nayo amefuzu na kuokoka, na
    mwenye kuyakengeuka atakuwa ni
    katika wenye kuhiliki.
•   Ni kwamba watu wa Qur-aan, hao
    ndio watu wa Mwenyezi Mungu
    waliokurubishwa Kwake, na kwamba
    mbora zaidi wa watu ni yule
    aliyejifundisha      Qur-aan     na
    akawafundisha watu, kwani Qur-aan
    hii    itakuja  siku    ya   Kiyama
    ikimwombea shifaa kila aliyeisoma,
    akaihifadhi na akaifanyia kazi, na
    itawaombea watu wake Pepo.
•   Qur-aan     huzitwaharisha   nyoyo
    kutokana na shubha na matamanio
    yanayozichafua, huzikurubisha kwa
    Muumbaji Wake Subhaanahuu wa
    Ta'alaa, na huzihimiza kufanya kazi
    ili kufuzu na kupata neema za
    kudumu milele.
•   Kati ya adabu za kusoma Qur-aan ni:
          Kuwa twahara na wudhuu.
Mimi ni Mwislamu
  Kuelekea Kibla.
  Kukaa kwa adabu na heshima.
  Kutoisoma kwa haraka.
  Kuwa na unyenyekevu.
   Kuonyesha    huzuni   kwa
madhambi na kuvuka mipaka.
  Kulia kutokana na kumwogopa
Mwenyezi Mungu na Utukufu wa
Maneno Yake.
  Kusoma kwa sauti nzuri.
  Kusoma kwa sauti ya chini ili
kutowabughudhi wenye kuswali.
  Kuzingatia maana ya maneno.
  Kuhudhurisha moyo.
 Kutaamuli kwa kina Aayah za
Mwenyezi Mungu.
    Tuwe    na   yakini  kuwa
kusimamisha hukumu za Kitabu
hiki kwa watu ni moja kati ya
sababu za kumakinishwa katika
ardhi na kuwashinda maadui.
Mimi ni Mwislamu
Basi harakia ndugu yangu Mwislamu
kwenda kwa Mola wako, na kikamate
Kitabu hiki kwa hima. Kuwa na shime
asikutangulie yeyote kuelekea kwa
Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi
Mungu Hufurahi zaidi kwa kurejea
kwako Kwake kuliko wanavyofurahi
watu kwa kurejea mtu wao aliyekuwa
mbali.
Mimi ni Mwislamu

      (4) KUWAAMINI MITUME
•   Ninawaamini    Mitume     wa     Mwenyezi
    Mungu.    Hakika     Mwenyezi      Mungu
    Aliwateua Mitume kati ya wanadamu,
    Akawafunulia Sheria Yake kwa njia ya
    wahyi, na Akawaamuru kuifikisha kwa
    watu, na kwamba mwenye kuwatii
    ataingia peponi, na mwenye kuwaasi
    ataingia motoni.

•   Kisha Akawatilia nguvu kwa miujiza
    yenye    kuonyesha      ukweli    wao   ili
    iwasaidie mbele ya wakadhibishaji, na
    ili iwe ni hoja kwao.

•   Na kwamba Mtume wa mwanzo ni
    Nuhu,    na   wa     mwisho      wao    ni
    Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa
    Aalihii wa Sallam.
Mimi ni Mwislamu

•   Na     kuwa    Mitume      hawa     ni     watu;
    wanakula,                     wanakunywa,
    wanaoa,wanaugua na wanakufa. Wao
    ndio viumbe bora kabisa wa Mwenyezi
    Mungu na wamehifadhiwa na maasi.

•   Mitume wa Mwenyezi Mungu ni wengi.
    Mwenyezi Mungu Amewataja baadhi
    yao katika Qur-aan. Nao ni Muhammad
    Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa
    Sallam,       Ibrahim     Khalili     wa     Ar-
    Rahmaan,       Musa      aliyesemeshwa       na
    Allaah, Iysa Neno la Mwenyezi Mungu
    na Nuhu. Hawa ndio Mitume wenye
    azma ya juu Rehma na Amani ziwe juu
    yao.    Pia    Ismail,     Is-haaq,      Yakub,
    Harun,    Ayyub,         Yunus,     Sulayman,
    Daawud, Yahya, Zakariya, Hud, Saleh,
Mimi ni Mwislamu

    Yusuf, Shuayb, Ilyaas, Lut, Dhulkifl,
    Idris, na wengi wengineo. Kati yao
    kuna Aliowahadithia Mwenyezi Mungu
    katika         Qur-aan     na       wengineo
    Hakuwahadithia.

•   Jambo      la    kwanza     walilolilingania
    Mitume ni tawhid, na jambo kubwa
    zaidi walilolikataza ni shirki, na wote
    wamekuja na Uislamu na wito.

•   wa     tawhid.    Lakini   sheria    zao   na
    mifumo     ya     kumwabudu         Mwenyezi
    Mungu Mtukufu ilitofautiana kutokana
    na kutofautiana zama zao na nchi zao.

•   Na kwamba Mitume walitoa bishara ya
    kuja     kwa    Nabii    Muhammad     Swalla
    Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam na
Mimi ni Mwislamu

    wakawaamrisha                    kaumu          zao
    kumwamini Muhammad Swalla Allaahu
    Alayhi      wa         Aalihii      wa        Sallam
    atakapotumwa kwao.

•   Tofauti kati ya Rasuli (Mtume) na
    Nabii     ni      kuwa      Rasuli       ni     yule
    aliyefunuliwa           sheria       mpya        na
    akaamrishwa        kuifikisha        kwa      watu.
    Ama      Nabii,   ni    yule     aliyetumwa       ili
    kuithibitisha na kuipitisha sheria ya
    Rasuli aliyemtangulia.

•   Ninaamini kuwa mbora wa Mitume
    mbele ya Allaah ni Muhammad Swalla
    Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam
    toka     kwa      mwana        wa   Ismaili      bin
    Ibrahim        Alayhima      Ssalaam.         Allaah
    Amemtuma            kwa           watu        wote,
Mimi ni Mwislamu

    Akahitimisha Unabii kwa Unabii wake,
    na Utume kwa Utume wake.

•   Akamtilia      nguvu        kwa       miujiza,
    Akamfanya bora kuliko Mitume wote.
    Pia   Ameufanya       Utume    wake     kuwa
    bora kuliko Utume wote uliotangulia,
    na    sheria   yake     kuwa   bora    kuliko
    sheria zinginezo zilizopita, na Kitabu
    chake    Qur-aan       kuwa    bora    kuliko
    Vitabu    vyote,      na   umati    wake    –
    Waislamu – kuwa bora kuliko uma
    nyinginezo.

•   Na Mola wake Akampa mambo ambayo
    Hakumpa        yeyote      katika     Manabii
    waliomtangulia. Kati ya mambo hayo
    ni:
Mimi ni Mwislamu

(1) Al Wasiylah: Nayo ndiyo daraja ya
    juu     kabisa        Peponi     ambayo
    Mwenyezi       Mungu     Amemwandalia
    Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa
    Aalihii wa Sallam.

(2) Al Kawthar: Nao ni mto Peponi
    wenye kupita chini ya Arshi ya Ar
    Rahman.

(3) Al    Hawdh:     Ni   sehemu     ambayo
    Waislamu         peke      yao     ndio
    watakayokunywa siku ya Kiyama.
    Siku ambayo watu watapatwa na
    kiu kikali, na jasho litawafika hadi
    magotini, viunoni na mabegani –
    kila mmoja kwa mujibu wa amali
    yake – na Waislamu watakunywa
    hapo kwa vikombe atakavyowapa
Mimi ni Mwislamu

   Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa
   Aalihii wa Sallam kwa mikono yake
   mitukufu.          Baada        ya    hapo
   hawatapatwa na kiu milele.

(4) Shafaa: Ni makamu ya kuhimidiwa
   siku ya Kiyama. Hapo Mtume Swalla
   Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam
   ataomba         shifaa    kwa     Mwenyezi
   Mungu     ili    Waislamu       waliofanya
   maasi     watolewe          motoni,     na
   hatobakia ndani ya moto yeyote
   anayeshuhudia            kwamba      hapana
   Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu
   na Muhammad ni Mtume wa Allaah.
   Aliyefanya maasi hatosalia milele
   motoni,     bali    atatoka     baada    ya
   kutakaswa na maasi yake.
Mimi ni Mwislamu

   Aliyewaamini Manabii wote na wala
   hakumwamini      Muhammad         Swalla
   Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam,
   basi hatatoka motoni.

(5) Na kwamba Allaah Amemnusuru na
   Akawanusuru         askari   wake    na
   wafuasi wake hadi siku ya Kiyama
   kwa kuzagaza hofu ndani ya nyoyo
   za maadui umbali wa mwendo wa
   mwezi. Na hakuna Nabii           yeyote
   aliyepewa      hili      kabla      yake
   Muhammad Swalla Allaahu Alayhi
   wa Aalihii wa Sallam.

(6) Na   ardhi   imefanywa      kwake   na
   Waislamu kuwa msikiti (sehemu ya
   kuswalia)      na      twahara,      na
Mimi ni Mwislamu

       haikufanywa     hivyo   kwa   Manabii
       waliomtangulia.

  (7) Na Allaah Amemtuma kwa watu na
       majini wote, lakini Mitume wengine
       wametumwa maalumu kwa watu
       wao tu.

  (8) Na kuwa yeye ndiye wa mwanzo
       kaburi lake kufunguka, na ndiye
       mwombezi wa kwanza, na ndiye wa
       kwanza kupewa shifaa, na ndiye wa
       kwanza kugonga mlango wa Pepo.
       Atakapougonga, mlinzi

wa   Pepo   Ridhwaan     atamuuliza:   "Nani
wewe?" Atajibu: "Muhammad". Ridhwaan
atamwambia:      "Kwako        nimeamrishwa
nisimfungulie yeyote kabla yako".
Mimi ni Mwislamu

Na    kati   ya   miujiza    ya    Mtume      Swalla
Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam ni:

              Kupasuka mwezi.

              Alilirejesha     jicho    la    Qatada
     lilipopofuliwa siku ya Uhud, macho yake
     yakarudi yakawa mazima kabisa.

              Aliurejesha muundi wa Ibn Al
     Hakam kama ulivyokuwa ulipovunjwa
     siku ya Vita vya Badr.

              Aliutaka mti utamke shahada,
     nao ukatamka shahada mbili mara tatu
     mbele ya kafiri, naye akasilimu.

              Kigogo     cha      mti   alichokuwa
     akihutubia    juu   yake       kililia   wakati
     alipokiacha na hakikunyamaza mpaka
     alipoiweka mikono yake juu yake.
Mimi ni Mwislamu

          Alikifanya chakula kidogo kuwa
kingi baina ya mikono yake miwili, na
wakaweza kula na kushiba zaidi ya
watu 80 chakula cha kujaa viganja
viwili.

          Aliyafanya maji kidogo kuwa
mengi siku ya Hudaybiyah wakati jeshi
lilipobakiwa na bakuli moja tu ya maji.
Hapo Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa
Aalihii wa Sallam aliingiza mikono yake
ndani, maji yakaanza kububujika kati ya
vidole    vyake     kama     chemchemu,
wakanywa     maji   Waislamu     wote   na
wakatawadhia      maji   hayo.   Walikuwa
kiasi cha watu 1400.

          Alipelekwa usiku hadi Msikiti
wa Al Aqsa, na kisha alipandishwa hadi
Mimi ni Mwislamu

mbingu za juu na kukomea Sidrat Al
Muntahaa.

           Alielezea na kuhadithia habari
za umma zilizotangulia na Manabii wao
nailhali    yeye     hana     kisomo;         hajui
kusoma wala kuandika. Pia alielezea
matukio yatakayotokea siku za usoni
kwa    kufunguliwa       Fursi    na       Rome,
kusambaratishwa         ufalme        wa      Kisra
aliyechanachana barua ya Mtume Swalla
Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam
aliyomtumia,         pamoja      na        miujiza
mingineyo mingi.

           Muujiza     mkubwa         zaidi     wa
Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii
wa    Sallam    ni    Qur-aan     Tukufu.       Ni
Mimi ni Mwislamu

muujiza     utakaosalia     hadi   siku       ya
Kiyama.

          Kisha    Allaah    Ameunyanyua
utajo    wake,    Akaliandamisha       jina   la
Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii
wa Sallam na Jina Lake Subhaanahuu
wa Taalaa, na Akaifanya shahada ya
kuwa hapana mola isipokuwa Allaah na
kwamba      Muhammad        ni   Mtume        wa
Mwenyezi Mungu kuwa ndio jambo la
kwanza     analoingia     nalo   mja    katika
Uislamu,na jambo la mwisho analotoka
nalo duniani. Basi yeyote ambaye neno
lake la mwisho litakuwa ni "Laailaaha
illa Allaah", ataingia peponi.

•   Ni   wajibu   wetu    kwa    upande       wa
    Mtume wetu Swalla Allaahu Alayhi
Mimi ni Mwislamu

    wa Aalihii wa Sallam tusilitangulize
    neno la kiumbe yeyote juu ya neno
    lake, au rai ya yeyote hata kama ana
    sauti    kwa   watu.   Na   ikiwa   watu
    watakutangulia kuhamia kwake, basi
    hama wewe kwenda katika sunnah
    yake katika kila jambo lako na wala
    usimfuate mwingine zaidi yake. Ni
    wajibu    wetu      tushikamane     sote
    pembezoni mwa amri yake na tumtii,
    kwani mwenye kumtii Mtume, basi
    huwa amemtii Mwenyezi Mungu.

              :      GFEDCBA
•   Na tusimwiite ila kwa kusema Mtume
    wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu
    Alayhi    wa     Aalihii    wa   Sallam.
    Tusiseme (Muhammad) basi.
Mimi ni Mwislamu

•   Tujipambe      kwa     adabu    zake,    na
    tumwige katika hali zake zote; kulala
    kwake,    kula       kwake,      kutembea
    kwake,   kuswali       kwake,     kufunga
    kwake,   kutoa   kwake         sadaka,   na
    jihadi yake.

•   Na tumpende zaidi kuliko nafsi zetu,
    wana wetu, wazazi wetu na watu
    wote.

•   Na tumpende kila yule anayempenda
    Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla
    Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam
    na   kumfanya        kiigizo   chake,    na
    tumchukie kila yule anayemchukia
    Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla
    Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam
    na wala hawajibiki na sheria yake.
Mimi ni Mwislamu

•   Hivyo basi, ni lazima kwa Mwislamu
    awapende         Waumini,       awanusuru,
    ajifananishe         nao,      ashughulikie
    mambo yao, asaidiane nao katika
    mambo ya kheri, na awafanye kuwa
    marafiki zake wa dhati.

•   Ni     wajibu       kwake     awabughudhi
    makafiri na      ukafiri     wao,    asiwatii,
    asiungane nao dhidi ya Waislamu,
    wala asisaidiane nao katika ubatilifu
    wao,    na    wala    asishiriki       katika
    sikukuu      zao.    Ni     haramu     kwake
    kuwadhulumu,         na     linalotakiwa   ni
    kuwatendea haki.

•   Ni wajibu wetu tuwapende Mama wa
    Waumini;        Wakeze      Mtume     Swalla
    Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam,
Mimi ni Mwislamu

    na   tuwapende       Maswahaba      Wake
    Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa
    Sallam, kwani wao ndio bora wa
    watu baada ya Manabii.

•   Pia ni wajibu wetu tuihuishe Sunnah
    yake Mtume Swalla Allaahu Alayhi
    wa Aalihii wa Sallam, tuidhihirishe
    sheria      yake,     na     tubalighishe
    ulinganio    wake     kwa    watu   wote.
    Kisha    tusubiri     maudhi   na   kero
    zinazotupata        katika   kuyapigania
    hayo, kwani hayo hayaepukiki.

•   Kwa vile Mwenendo wa Mwenyezi
    Mungu uliopita kwa viumbe Vyake
    unahukumia kuwa hakuna Nabii au
    walii yeyote aliyelingania haki hii ila
    alifanyiwa uadui na kuudhiwa.
Mimi ni Mwislamu

•   Zindukana ndugu yangu Mwislamu!
    Maudhi   ya    makafiri     yasikufanye
    ukaiacha dini yako. Kwani Mtume wa
    Mwenyezi      Mungu      Swalla    Allaahu
    Alayhi   wa     Aalihii     wa      Sallam
    aliudhiwa       wakati       Maswahaba
    walipokuwa      wachache,         nao    pia
    waliudhiwa wakafanya subira.

•   Na wala usilegeze azma yako hata
    kama          watakwambia               kuwa
    unayoyazungumza       ni    upuuzi,      una
    misimamo migumu, au umepitwa na
    wakati. Au wakisema: "ashachezewa
    akili huyo". Kwani wewe una kiigizo
    chema    kwa   Mtume       wa   Mwenyezi
    Mungu, yeye ashaambiwa mshairi na
    hata mwendawazimu.
Mimi ni Mwislamu

•    Wala      usisononeke       ukiambiwa
     mpotevu mwenye siasa kali. Hii ndio
     tabia ya makafiri kwa Waumini.

     :

((Na wanapowaona, husema hakika
    hawa bila shaka ni wapotevu)).

•    Ikiwa watu wako makundi mawili, je
     haikutoshi    wewe    kuwepo     katika
     kundi     aliloko     Mtume      wako
     Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa
     Aalihii wa Sallam?!

•    Achana nao hao mpaka ifike siku
     ambayo    dhalimu     ataviuma   vidole
     vyake        aseme:     "Laiti    mimi
     ningeliifuata njia pamoja na Mtume".
Mimi ni Mwislamu

                                     
                            : ¯

•   Wala usibabaike au kuchanganyikiwa
    kama watakwambia kuwa wewe ni
    gaidi au mwovu, kwani hayo ndio
    madai    ya   madhalimu       dhidi   ya
    Waumini duniani na akhera. Ni kuwa
    pale    Malaika   watakapowaongoza
    kwenda     Jahannamu    wakisunukia,
    wataangalia humo kisha waseme:

     :     JIH GFEDCBA
              ((Na watasema: Mbona
            hatuwaoni watu tuliokuwa
           tukiwazingatia kuwa ni katika
              waovu?))
Mimi ni Mwislamu

•   Na hapa, Waumini (ambao makafiri
    wamewaita          kuwa         ni   waovu)
    watawaita toka kwenye magorofa ya
    juu kabisa ya Firdaws wakiwaambia:

                : ¯          LKJIHGF
         ٤٤ : ‫اف‬      ‫(( ا‬      ‫ر‬   ‫و‬    ‫و‬   ‫)) أن‬

           ((Hakika sisi tumeyakuta
        Aliyotuahidi Mola wetu kuwa ni
                             kweli))
Mimi ni Mwislamu
(5) KUAMINI SIKU YA MWISHO

•   Ninaiamini siku ya mwisho, nayo ni
    iku ambayo dunia (nyumba ya amali)
    itamalizika, na akhera (nyumba ya
    malipo) itasimama, wema wakalipwa
    Pepo, na waovu wakalipwa moto.

•   Katika   siku    ya   Kiyama,    mizani
    itawekwa,   na    kila   mja    atapewa
    kitabu chake. Atakayepokea kitabu
    chake kwa mkono wake wa kuume,
    basi Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa
    Aalihii wa Sallam atakuwa pamoja
    naye Peponi. Ama yule atakayepokea
    kitabu chake kwa mkono wake wa
    kushoto, basi atakuwa pamoja na
Mimi ni Mwislamu

    Firauni     –laana     ziwe     juu      yake–
    motoni.

•   Sirati     itawekwa,      atakayefanikiwa
    kuivuka     basi   atafikia    Peponi.    Ama
    ambaye kulabu zitamnyakua kutokana
    na       amali     zake       mbovu,      basi
    ataangukia motoni.

•   Siku ya Kiyama ina dalili, ina alama
    ndogo na ina alama kubwa.

•   Miongoni         mwa   alama     ndogo      ni
    kupotea uaminifu, kukithiri mauaji,
    madaraka kukamatwa kwa mabavu
    na mafasiki, na masuala muhimu
    kuzungumziwa na wasiojua kitu.

•   Na miongoni mwa alama kubwa ni
    kuibuka Al Mahdi, kusimama ukhalifa
Mimi ni Mwislamu

    wongofu        utakaokwenda        juu     ya
    misingi ya njia ya Utume kabla ya
    kutokea Kiyama, na kudhihiri masihi
    mwongo.

•   Pia kuteremka Iysa Alayhi Ssalaam ili
    awaongoze       Waislamu,       apigane    na
    makafiri, avunje vunje misalaba, aue
    nguruwe,       na    azikatae    dini     zote
    nyingine ila Uislamu tu.

•   Basi haitobakia nyumba yoyote ya
    mjini     au    ya     mashambani          ila
    Mwenyezi Mungu Ataiingiza dini hii,
    kwa heshima ya mwenye nguvu, au
    kwa udhalili wa mnyonge.

•   Vile vile kutoka Yaajuju na Maajuju.
    Pia            atatoka             mnyama
Mimi ni Mwislamu

    anayewasemesha       watu,    na    jua
    litachomoza toka magharibi, Qur-aan
    itaondoshwa na mambo mengineyo.

•   Basi yeyote atakayefanya amali ya
    uzito wa atomu ikiwa ni ya kheri au
    ni ya shari, ataiona siku ya Kiyama
    ndani ya kitabu chake.

•   Basi harakieni kwenye mambo ya
    kheri kabla haujamalizka muda wa
    kusajiliwa kwa kufa mja katika muda
    ambao haujui yeyote ila Mwenyezi
    Mungu Pekee.

•   Wakamwosha           jamaa         zake,
    wakamvisha     sanda,    wakamswalia,
    wakamzika. Kisha akajiwa na Malaika
    wawili;    Munkari       na    Nakiyr,
Mimi ni Mwislamu

    wakamkalisha kitako na kumwuuliza:
    "Nani Mola wako? Nini dini yako?
    Nani Nabii wako?"

•   Ikiwa atajibu kuwa: "Allaah ni Mola
    wangu, na Uislamu ndiyo dini yangu,
    na Muhammad Swalla Allaahu Alayhi
    wa Aalihii wa Sallam ndiye Nabii
    wangu na Mtume wangu" – na Allaah
    Akamwezesha         hilo      –       basi
    itafunguliwa    katika     kaburi     lake
    harufu   ya    rayhaan     hadi   peponi,
    akaona   mashukio    yake     huko,    na
    makasri yake na ufalme wake. Hapo
    atashangilia kwa furaha kubwa, na
    kaburi lake litapanuliwa upeo wa
    macho.
Mimi ni Mwislamu

•   Na ikiwa ni katika makafiri, basi
    hatoweza        kujibu    chochote,       kwani
    majibu wakati huo si kwa akili au
    werevu wa mtu.

•   Bali Mwenyezi Mungu Huwathibitisha
    na      kuwaimarisha      watu       wa   imani
    wakati           huo           kwa         yale
    waliyoyatanguliza          kati     ya    amali
    njema zilizosimamia juu ya tawhid,
    utekelezaji      wa      faradhi,     kushiriki
    jihadi,    kutenda       mema,      kuamrisha
    mema,         kukataza        mabaya,     kutoa
    sadaka, kusoma Qur-aan, kufunga
    siku     za    joto   kali,    na    kusimama
    kuswali muda mrefu usiku wa baridi
    kali.
Mimi ni Mwislamu

•   Ama akiwa ni katika makafiri, basi
    kaburi lake humbana hadi mbavu
    zake zikaingiana katika mwili wake,
    na kaburi lake huwa ni shimo katika
    mashimo ya motoni kwa sababu ya
    amali zake mbaya.

•   Basi jitahidi ndugu yangu Mwislamu,
    kwani leo ni amali na hakuna hisabu,
    lakini kesho ni hisabu na hakuna
    amali.

•   Na   siku   hiyo,   Waislamu   watiifu
    wataingia Peponi peke yao, kwa vile
    Mwenyezi    Mungu    Hatoikubali   dini
    yoyote siku ya Kiyama isipokuwa
    Uislamu.
Mimi ni Mwislamu

•   Ndani ya Pepo kuna neema ambazo
    hakuna sikio lililowahi kuzisikia, wala
    jicho lililowahi kuziona, wala hata
    kuwaziwa        katika     akili     ya
    mwanadamu. Neema zake zitasalia
    milele   wala     hazitomalizika,    na
    waliomo humo hawatakufa milele.
    Neema kubwa zaidi ya zote humo, ni
    kuuangalia Uso wa Mwenyezi Mungu
    Mola wa walimwengu wote.

•   Na   waasi,     waovu    na    makafiri
    wataingia motoni. Ndani ya moto,
    kuna adhabu zisizoweza kuvumilika
    Alizoziandaa Mwenyezi Mungu kwa
    ajili ya makafiri. Milima mirefu thabiti
    haiwezi kuzivumilia adhabu hizi, na
Mimi ni Mwislamu

    hao     wataadhibiwa        humo     bila
    kupumzishwa.

•   Na    humo,    wafuasi   wa   mataghuti
    wataomba           adhabu     iongezwe
    maradufu       kwa     wakubwa      wao
    waliowapoteza. Na hapo Mwenyezi
    Mungu Ataamuru adhabu iongezwe
    maradufu kwa wote.

•   Basi thibiti ndugu yangu Mwislamu
    juu ya haki hii, wala usidanganyike
    kabisa kuona kuwa wavunjaji sheria
    ni wengi zaidi, kwani ikiwa wewe
    utawatii      na   ukawafuata      wengi
    waliomo ardhini, basi watakupoteza
    njia ya Mwenyezi Mungu. Nawe pita
    pamoja na wenye kupita kuelekea
    kwa Mwenyezi Mungu.
Mimi ni Mwislamu

•   Kwani   kundi        katika        umma     wa
    Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa
    Aalihii wa Sallam litaendelea kuwa
    juu ya haki likiwa na nguvu, hawezi
    kuwadhuru yeyote aliyekwenda nao
    kinyume au aliyewasaliti mpaka siku
    ya Kiyama.

•   Basi ni mbinu zipi za kuzijua ngazi
    hizo za kupanda juu, na kuokoka na
    ngazi hizo za kuporomokea chini? Na
    ni   mbinu      zipi     za         kuwafikia
    waliotangulia wenye kukurubishwa,
    na   kujiweka    mbali        na    wapingaji
    wenye kuangamia? Bila shaka ni toba
    ya   kweli      ya     kusahihisha          na
    kurekebisha     yaliyopita,        na     amali
    njema    za     kuweka         sawa       umri
Mimi ni Mwislamu

    uliosalia, na kuweka nia ya kweli ya
    kunyooka na kutokengeuka.

•   Basi   kuwa   pamoja    na     watu   kwa
    kiwiliwili chako, ukiuza, ukinunua,
    ukioa na ukiiamirisha ardhi kwa yale
    Aliyokuhalalishia Mwenyezi Mungu.

• Wala moyo wako usifungamane na
    kitu chochote cha kidunia, bali nenda
    na     moyo      wako   pale     ambapo
    unatakikana uwe, huko chini ya Arshi
    ya Ar Rahmaan, na sujudu kwa moyo
    wako    sijdah    ambayo     utaendelea
    kuisujudu hadi siku ya Kiyama.
Mimi ni Mwislamu

(6) KUAMINI QADHAA NA QADARI


 •   Nako ni kuamini kwamba Mwenyezi
     Mungu     Anayajua       yote     yaliyomo
     ulimwenguni, yote yanayofanyika na
     yatakayotokea hadi siku ya Kiyama.
     Hata     chembe     ndogo    mno,    Yeye
     Hakosi    kuijua.   Na    kwamba     Yeye
     Anavijua vitendo vya waja, riziki zao,
     muda wao wa kuishi, na nani kati yao
     atakuwa wa peponi, na nani kati yao
     atakuwa       wa         motoni      kabla
     Hajawaumba.

 •   Na     kwamba       Mwenyezi        Mungu
     Ameyaandika makadirio haya katika
     Lawh     Al   Mahfuudh      kabla     hata
     Hajaziumba mbingu na ardhi kwa
     miaka elfu hamsini, na kwamba Lawh
Mimi ni Mwislamu

    Al Mahfuudh hii hakuna malaika wa
    karibu    au      hata    Nabii    aliyetumwa
    awezaye kuichungulia.

•   Hata     kijusi    kinapokuwa       ndani     ya
    tumbo      la     uzazi   la   mama         yake,
    Mwenyezi          Mungu        Huwaamrisha
    Malaika waandike kama ni cha kike
    au kiume, waandike na riziki yake,
    amali yake, muda wake wa kuishi na
    hatima yake (ima peponi au motoni).
    Pia    waandike      mazuri       na    mabaya
    atakayokabiliana nayo.

•   Kisha     unapoingia       usiku       wa   cheo
    (Laylatul          Qadr),          huteremka
    makadirio ya         mwaka mzima            toka
    Lawh al Mahfuudh kati ya ajali za
    watu, riziki zao, nani kati yao atahiji
    mwaka huo na mengineyo. Katika
Mimi ni Mwislamu

    usiku huo, hukadiriwa mambo ya
    mwaka mzima.

•   Kisha huteremka makadirio ya kila
    siku kwa nyakati zake na watu wake,
    hapo Mwenyezi Mungu Huwanyanyua
    watu na wengine Huwashusha.

•   Na   tuamini    kuwa     Mapendeleo    ya
    Mwenyezi       Mungu     ndiyo    yawayo,
    Alilolitaka huwa na Asilolitaka haliwi.
    Mwenyezi        Mungu       Hana      wa
    kumshinda, na Yeye Ndiye Mwenye
    kuzipindua      nyoyo.      Humwongoa
    Amtakaye kwa fadhila Zake na rehma
    Zake, na Humpoteza Amtakaye kwa
    Uadilifu   Wake    na    Hekima     Yake,
    kwani Yeye Ndiye Ajuaye zaidi nani
    anastahiki      uongofu      na      nani
    anastahiki upotevu.
Mimi ni Mwislamu

•   Na Mwenyezi Mungu Haulizwi yale
    Ayafanyayo lakini watu huulizwa.

•   Na tuamini kuwa Mwenyezi Mungu
    Amekiumba     kila    kitu,    na   hakuna
    chembe yoyote ndogo ulimwenguni
    isipokuwa         Mwenyezi             Mungu
    Ameiumba     na   Akaumba        kutikisika
    kwake na kutulia kwake.

•   `Na kwamba Yeye Amewaumba waja
    na vitendo vyao, na kwamba Yeye
    Amewaumbia         waja       uwezo       na
    mapendeleo      yao    ili    wajichagulie
    wenyewe vitendo vyao.

•   Na     kwamba        Mwenyezi          Mungu
    Mtukufu Amewaamuru viumbe Wake
    wamtii, na Akawaahidi kuwapa Pepo
    Yake      wakifanya           hivyo,      na
    Amewakataza       kumwasi       Yeye,     na
Mimi ni Mwislamu

    Akawapa onyo la kuwaingiza ndani
    ya moto Wake wakifanya hivyo, na
    wala Hakuwakalifisha kazi isipokuwa
    ile ambayo wanaweza kuifanya. Na
    hapo     wakagawanyika        makundi
    mawili: Waumini na makafiri; kwa
    hiari yao wenyewe, kwa mapendeleo
    yao wenyewe na kwa uwezo wao
    wenyewe, na yote hayo Mwenyezi
    Mungu Amewaumbia.

•   Na   kwamba    thawabu   na    adhabu
    hutokana na kuifuata sheria, si kwa
    kutangulia Elimu ya Mwenyezi Mungu
    kwao. Basi yeyote atakayefanya amali
    yoyote ya kheri ya uzito wa atomu,
    atalipwa kwayo. Na yeyote atakayefanya
    amali yoyote ya shari ya uzito wa
    atomu, basi ataadhibiwa kwayo.
Mimi ni Mwislamu

•   Na   kwamba       kinachozingatiwa     ni
    mwisho wa matendo, na kwamba kila
    mja ni mwenye kuendeshwa katika
    lile aliloumbiwa kati ya kufurahika
    Peponi au kupata shakawa motoni.

•   Na kwa ajili hiyo, ni wajibu kwa mja
    aogope mwisho mbaya, na aendelee
    daima kumwomba Mwenyezi Mungu
    na   amhitajie,   Amhidi   katika    njia
    iliyonyooka, na adumu kumwomba
    Amsaidie katika kumtii, na ajilinde
    Kwake na maasia, kwa vile mja hana
    hila wala nguvu zozote za kuyafanya
    hayo ila kwa Uwezo wa Mwenyezi
    Mungu.

•   Na    kwamba       Waumini     Huridhia
    Qadhaa    ya   Mwenyezi      Mungu    na
    Qadari Yake; ya kheri yake na ya
Mimi ni Mwislamu

      shari yake, katika misukosuko na
      katika furaha, na wana yakini kuwa
      hawezi      yeyote         kuwanufaisha
      isipokuwa kwa Qadari ya Mwenyezi
      Mungu,      na     wala      hawadhuru
      isipokuwa   liwe   lisha   andikwa   na
      Mwenyezi Mungu.

 •    Na mja hatopata utamu wa imani
      mpaka    pale    atakapojua    kwamba
      lililompata lisingekuwa la kumkosa,
      na   lililomkosa     lisingekuwa     la
      kumpata.

       Na mwisho naomba nikisema:
     "Ninamhimidi Mwenyezi Mungu, na
ninamwomba Aniingize Peponi mimi na
Waislamu wengine, na Anilinde na moto
 mimi na Waislamu wengine". Aamiyn.
Mimi ni Mwislamu
Mimi ni Mwislamu




   ed c b a ` _
         k j ih g f
[٨٥:‫ان‬    ‫]ل‬
                              Ù               
anamuslim@windowslive.com             Ø       ×       ª Ø
               WWW.Iam-Muslim.com



                     ٢٠١٠ J ١٤٣١
                 ‫و‬                ‫ق‬       ‫ا‬
               ٢٠٠٩L٢٢٢٧٤ W

         ٠١٢٠١٥٢٩٠٨ :ª                           W
Mimi ni Mwislamu

                    ª




                a


٠١٢٥٨٣٤٥٧٤          ٠١٠٦٧١٤٧٦٨

More Related Content

More from iam-muslim

Iam muslim persian
Iam muslim persianIam muslim persian
Iam muslim persianiam-muslim
 
Hokm almabtoor-shatem-alrasool ara
Hokm almabtoor-shatem-alrasool araHokm almabtoor-shatem-alrasool ara
Hokm almabtoor-shatem-alrasool araiam-muslim
 
Iam muslim eng
Iam muslim engIam muslim eng
Iam muslim engiam-muslim
 
Iam muslim greek
Iam muslim greekIam muslim greek
Iam muslim greekiam-muslim
 
Iam muslim french
Iam muslim frenchIam muslim french
Iam muslim frenchiam-muslim
 
Iam muslim ger
Iam muslim gerIam muslim ger
Iam muslim geriam-muslim
 
Iam muslim ara
Iam muslim araIam muslim ara
Iam muslim araiam-muslim
 
Iam muslim hausa
Iam muslim hausaIam muslim hausa
Iam muslim hausaiam-muslim
 
Iam muslim chin
Iam muslim chinIam muslim chin
Iam muslim chiniam-muslim
 
Abwab almagfera ara
Abwab almagfera araAbwab almagfera ara
Abwab almagfera araiam-muslim
 
Iam muslim ital
Iam muslim italIam muslim ital
Iam muslim italiam-muslim
 
Iam muslim fulani
Iam muslim fulaniIam muslim fulani
Iam muslim fulaniiam-muslim
 
Iam muslim amharic
Iam muslim amharicIam muslim amharic
Iam muslim amhariciam-muslim
 
Iam muslim malay
Iam muslim malayIam muslim malay
Iam muslim malayiam-muslim
 
العبادات القلبية
العبادات القلبية العبادات القلبية
العبادات القلبية iam-muslim
 

More from iam-muslim (15)

Iam muslim persian
Iam muslim persianIam muslim persian
Iam muslim persian
 
Hokm almabtoor-shatem-alrasool ara
Hokm almabtoor-shatem-alrasool araHokm almabtoor-shatem-alrasool ara
Hokm almabtoor-shatem-alrasool ara
 
Iam muslim eng
Iam muslim engIam muslim eng
Iam muslim eng
 
Iam muslim greek
Iam muslim greekIam muslim greek
Iam muslim greek
 
Iam muslim french
Iam muslim frenchIam muslim french
Iam muslim french
 
Iam muslim ger
Iam muslim gerIam muslim ger
Iam muslim ger
 
Iam muslim ara
Iam muslim araIam muslim ara
Iam muslim ara
 
Iam muslim hausa
Iam muslim hausaIam muslim hausa
Iam muslim hausa
 
Iam muslim chin
Iam muslim chinIam muslim chin
Iam muslim chin
 
Abwab almagfera ara
Abwab almagfera araAbwab almagfera ara
Abwab almagfera ara
 
Iam muslim ital
Iam muslim italIam muslim ital
Iam muslim ital
 
Iam muslim fulani
Iam muslim fulaniIam muslim fulani
Iam muslim fulani
 
Iam muslim amharic
Iam muslim amharicIam muslim amharic
Iam muslim amharic
 
Iam muslim malay
Iam muslim malayIam muslim malay
Iam muslim malay
 
العبادات القلبية
العبادات القلبية العبادات القلبية
العبادات القلبية
 

Iam muslim sawhilil

  • 1. ¯ : Mimi ni Mwislamu Authorship Muhammed Ashraf Salah
  • 3. Mimi ni Mwislamu Kwa jina la Mungu wa Rehema hgfedc ba`_ : ¯ kji Na mtu anataka dini nyingine zaidi ya Uislamu wala kukubali kuwa wakati ni mmoja wa wenye kukhasiri Akhera Al-Imran: 85
  • 4. Mimi ni Mwislamu Copyright, distribution and translation are reserved for every Muslim Legal Deposit No. 22274 / 2008 International Serial 977-6157-64-5 For charitable distribution call: 0020101459613 For suggestions e-mail: anamuslim@windowslive.com WWW.Iam-Muslim.com
  • 5. Mimi ni Mwislamu (1) KUMWAMINI MWENYEZI MUNGU Mimi ni Mwislamu… • Ninamwamini Mwenyezi Mungu Pekee Asiye na mshirika na hakuna mola mwingine isipokuwa Yeye, Hakuzaa wala Hakuzaliwa, na hakuna kamwe kifano chake. • Ameumba mbingu na ardhi, Naye Ndiye Anayezimiliki. Anayajua yaliyofichikana na yenye kuonekana. Yu Hai na Hafi, Anayasimamia mambo yote milele na Halali. • Ana Majina Mazuri Kabisa na Sifa za Juu. Kati yake ni Majina tisini na tisa, mwenye kuyajua na kuyadhibiti vyema na akamwomba Mwenyezi Mungu Kwayo, ataingia peponi. • Kati yake ni Sifa za Upweke, kwani Yeye Subhaanahu wa Taalaa ni Mmoja wa Dhati, Sifa na Vitendo, Aliyepwekeka, Aliye Pekee, Mkusudiwa, Mmiliki wa ufalme.
  • 6. Mimi ni Mwislamu • Na Sifa za Utukufu, kwani Yeye ni Mwenye hekima, Mwenye habari ya kila jambo, Mwelekezaji wa manufaa, Haki, wa Mwanzo, wa Mwisho, wa Dhahiri, wa Siri, Mrithi, Mwenye Kubakia, Mkwasi, Mtakasifu, Mwenye Kushuhudia, Aliye Karibu, Mbora wa Kupangilia, Mwadilifu, Nuru ya mbingu na ardhi, Mwenye Utukufu na Ukarimu. • Na Sifa za Uadhama, kwani Yeye ni Mshindi Asiyeshindika, Mwenye Sifa zote Tukufu, Mwenye Uadhama, Mwenye Sifa za Utukuzo, Mwenye Kulazimisha, Mwenye Nguvu, Aliye Imara, Mteza nguvu, Mweza, Mwenye uwezo wa juu, Mwingi wa Kunusuru, Aliye Juu, Aliye Juu ya vyote. • Na Sifa za Uwezo, kwani Yeye ni Mwingi wa Ujuzi, Mwenye Kusikia, Mwenye kuona, Yu Hai, Mwenye Kukamata, Mwenye Kukunjua, Mwenye Kushusha, Mwenye Kupandisha, Mwenye Kutukuza, Mwenye Kudhalilisha, Mwenye Kutoa, Mwenye Kuzuia, Mwenye Kunufaisha,
  • 7. Mimi ni Mwislamu Mwenye Kudhuru, Mwenye Kuhuisha, Mwenye Kufisha, Mwenye Kutanguliza na Mwenye Kuchelewesha. • Na Sifa za Uumbaji, kwani Yeye ni Muumbaji, Msanifu wa Maumbile, Mtiaji Sura, Hakimpiti au Kumshinda kitu, Mbunifu, Mwenye Kuanzisha, Mwenye Kurejesha, Mwenye Kufufua, Mwenye Kukusanya, Mpaji Mkuu, Mfunguzi wa kila jambo, Mwingi wa Kuruzuku, Mwenye Kutajirisha, Mdhibiti wa idadi, Mwenye Kudhibiti mambo, Mwenye Kuhifadhi, Mlinzi na Muumbaji wa mbingu na ardhi bila ruwaza. • Sifa za Rehma, kwani Yeye ni Mwingi wa Rehma, Mwingi wa Kurehemu, Mwingi wa Huruma, Mwenye Kuneemesha neema nzuri, Mwingi wa Penzi, Mtenda Wema, Mwingi wa Kughufiria, Mwenye Kusamehe, Mwingi wa Kukubali toba, Mwenye Amani, Mtoaji amani na imani, Mpole, Mwenye Kulipa vyema, Mkarimu, Mwenye Kuneemesha, Mwingi wa Kutoa, Mwenye Kusaidia, Mwenye Kujibu,
  • 8. Mimi ni Mwislamu Mkunjufu, Mwingi wa subira, Mvumilivu kwa Waja Wake, Latifu, Wakili, Mwenye Kutoa Misaada, Mwenye Kuombwa msaada na Mwenye Kukubali toba. • Amemneemesha mwanadamu neema nyingi zisizo na hesabu. Na hakuna neema yoyote anayoneemeka nayo mja ila hutoka kwa Mwenyezi Mungu Pekee, kwani Yeye Ndiye Aliyemuumba na Akampa uhai, Akamfanya asikie na aone, Akamkirimu, kisha Akamruzuku na Akamfanyia wema. • Kwa ajili hiyo, ni lazima mja amwabudu Mwenyezi Mungu Peke Yake – nako ni kufuata amri Yake na kuacha makatazo Yake – kwa kuwa hastahiki yeyote kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu Peke Yake. • Vile vile, bila shaka Mwenyezi Mungu Anazijua hali zote za mja kati ya utiifu
  • 9. Mimi ni Mwislamu na uasi. Hivyo basi, ni wajibu moyo wa mja ujae haiba kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, utukuzo na mapenzi, na aone haya kumwasi na aachane na maasi, kwani Mwenyezi Mungu Humwona wakati akiyafanya. • Anafurahi kwa amali zake njema zinazomkurubisha kwenye radhi za Muumbaji wake Subhaanahuu wa Taala. Hivyo huzidi kufanya amali hizo hadi kufikia ngazi ya ihsani, kwani imani huzidi kwa matendo mema na hupungua kwa maasi. • Asivutike kwenye matamanio, hawaa au bid'a, bali avutike kwa Mwenyezi Mungu Pekee huku akifuata maamrisho ya Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam. Asitafute kwa amali yake starehe ndogo ya dunia bali atafute kwayo malipo toka kwa Mwenyezi Mungu tu. • Aidha, hakika Mwenyezi Mungu Ana huruma mno kwa mwanadamu kuliko huruma ya mama kwa mwanaye. Na rehma Yake imekienea kila kitu.
  • 10. Mimi ni Mwislamu Hivyo basi, ni wajibu kwa mja amwombe na anyenyekee Kwake katika haja zake za kidunia na za kiakhera, na wala asimwombe yeyote mwingine. • Kwa vile hakuna faida yoyote ya kumwomba asiye Mwenyezi Mungu, kwa kuwa hamiliki uwezo ulio kamili isipokuwa Mwenyezi Mungu, na hakuna asikiaye ya siri na minong'ono ila Mwenyezi Mungu, na hakuna anayemiliki makadirio isipokuwa Mwenyezi Mungu, basi kwa maana hiyo, hakuna wa kujibu dua isipokuwa Mwenyezi Mungu. • Na kwa ajili hiyo, haijuzu kwa Mwislamu kuliomba kaburi, au kumwomba aliyezikwa humo vyovyote awavyo, kwa kuwa yeye hamsikii. Na kama hamsikii, basi ni vipi atamjibu au kumnufaisha? Hakika Mwenyezi Mungu Pekee Ndiye Mwenye Kunufaisha na Mwenye Kudhuru. Na kwa ajili hiyo, ni wajibu kwa Mwislamu asijenge msikiti juu ya makaburi, kwani Mtume Swalla
  • 11. Mimi ni Mwislamu Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam amelikataza hilo. • Kadhalika, ni wajibu kwa mja alinganishe kati ya udhaifu wake na Nguvu za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kati ya umasikini wake na Utajiri wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kati ya ujinga wake na Elimu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kati ya unyonge wake na Utukufu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. • Na ajue kwamba utukufu ni wa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na Waumini. • Hivyo yampasa awe ni miongoni mwa Waumini hawa ambao hawatawakali isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu Pekee, wala hawaombi msaada isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, wala hawaombi kinga na kujilinda isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, wala hawaombi msaada wa dharura ila kwa Mwenyezi Mungu, wala hawamwogopi isipokuwa Mwenyezi Mungu, wala hawataraji isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, wala
  • 12. Mimi ni Mwislamu hawamwombi isipokuwa Mwenyezi Mungu, wala hawachinji isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wala hawaweki nadhiri isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wala hawaapi isipokuwa kwa Jina la Mwenyezi Mungu, wala hawaweki talasimu na hirizi (amali), wala hawasadiki wasemayo makuhani, watabiri (wanajimu) na wachawi, na wala hawawaendei. • Na wao hawakosi rajua, na huwa na tahadhari ya mponyoko wa ndimi zao ili wasije kutelezea motoni. Hawasemi: "Amependa Mwenyezi Mungu na amependa fulani", "lau si Mwenyezi Mungu na wewe", "nimetawakali kwa Mwenyezi Mungu na kwako". Bali waseme: "Nimetawakali kwa Mwenyezi Mungu Pekee", "Amependa Mwenyezi Mungu kisha amependa fulani". Maneno haya humsawazisha Mwenyezi Mungu na waja Wake, na ni katika shirki ndogo.
  • 13. Mimi ni Mwislamu • Na kama ilivyo wajibu kwetu kumwamini Mwenyezi Mungu, ni wajibu wetu vile vile tuwakatae mataghuti. • Na kigogo wa mataghuti ni shetani na kila yule aliyeabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu naye akaridhia hilo. • Na kati ya mataghuti hawa ni yule aliyetunga sheria zinazoharamisha Aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu, au kuhalalisha Aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu. • Aidha, taghuti ni kila yule aliyelingania hilo, au akawaamuru watu hilo, au akahukumu kwa hilo, kwa vile ametaadi na akavuka mpaka wa kiumbe wa kusikia na kutii. • Basi Allaah Pekee Ndiye Aliyewaumba wanadamu, na Ndiye Anayejua yanayowafaa, na kwa hivyo, hakuna yeyote awezaye kuwapangia sheria isipokuwa Yeye tu.
  • 14. Mimi ni Mwislamu (2) KUWAAMINI MALAIKA • Ninaamini kuwepo malaika ambao Mwenyezi Mungu Amewaumba kutokana na nuru, na Akawafanya kuwa na mbawa mbili mbili, tatu tatu, na nne nne. Nao hawali, hawanywi, hawalali wala hawaoi. Amewaamuru kufanya kazi na kusimamia majukumu mbalimbali, nao hutekeleza hayo. • Malaika siku zote humtii Mwenyezi Mungu bila kuchoka. Hawamwasi na humwogopa Mola wao toka juu yao. Kuna kati yao aliyesujudu toka siku Alipoziumba Mwenyezi Mungu mbingu na ardhi hadi siku ya Kiyama. Na atakaponyanyua kichwa chake atasema: "Subhaanak! Hatujakuabudu ukweli wa kukuabudu". • Wao ni waja wa Mwenyezi Mungu na si wanawake, na wala si wasaidizi Wake, na wao watawaombea shifaa
  • 15. Mimi ni Mwislamu Waumini – kwa idhini ya Mwenyezi Mungu – siku ya Kiyama. Kati ya malaika hawa, wapo: • Walinzi ambao huwalinda viumbe na madhara. • Watukufu waandishi ambao huandika matendo ya wanadamu, mema yao na mabaya yao. • Wenye kumsabihi Mwenyezi Mungu. Hawa humsabihi Mwenyezi Mungu mchana na usiku na hawachoki mpaka siku ya Kiyama. • Wenye kuvinjari ambao huhudhuria vikao vya dhikri, kisomo cha Qura-aan na vikao vya elimu. • Wabebaji Arshi ambao idadi yao ni wanane. Ni viumbe wakubwa mno kati ya viumbe wa Mwenyezi Mungu. Ndege huruka toka ncha ya sikio la mmoja wao hadi shingoni kwa muda wa miaka mia tano.
  • 16. Mimi ni Mwislamu • Malaika wa mauti anayezitoa roho za viumbe kwa Amri ya Mwenyezi Mungu. Huyu ana wasaidizi wake. • Israfil atakayelipuliza baragumu, kisha viumbe vyote vitakufa kabla ya kutokea Kiyama. Kisha litapulizwa jingine, na hapo watasimama viumbe wakiangalia. • Mikaili anayesimamia jukumu la mvua. • Ridhwaan ambaye ni mlinzi wa Pepo. Yeye ana wasaidizi wake walio mbioni kuwahudumia Waumini Peponi. • Maalik ambaye ni mlinzi wa moto. Ana wasaidizi wake ambao viongozi wao ni kumi na tisa. Wana marungu ya chuma ya kuwaadhibu makafiri motoni - Mwenyezi Mungu Atuepushe na hayo. • Mkuu wa Malaika ni Jibril aliyewakilishwa kupeleka wahyi kwa Manabii na Mitume.
  • 17. Mimi ni Mwislamu • Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam alimwona katika umbile lake. Kutokana na ukubwa wake, alizifunika peo za mbingu. Ana mbawa mia sita, naye ndiye aliyekikamata kijiji cha Lut kwa ncha ya ubawa wake, akakinyanyua hadi juu mbinguni, kisha akakipindua juu chini. • Kuna malaika wengineo wengi zaidi ya hawa, na hakuna ajuaye askari wa Mola wako isipokuwa Yeye tu. :¯ ´ ³ ²± ° • Malaika huwapenda Waumini ambao Mwenyezi Mungu Huwapenda na huwaombea maghfira. • Malaika mbali na nguvu zao hizi hupigana pamoja na Waumini.
  • 18. Mimi ni Mwislamu (3) KUVIAMINI VITABU • Ninaviamini Vitabu vya Mwenyezi Mungu Alivyoviteremsha kwa Mitume Wake, na kwamba katika asili ya kuteremshwa Kwake, ni Maneno ya Mwenyezi Mungu Aliyowafunulia ili waifikishe sheria na dini Yake. Vitabu vikubwa zaidi ni: Quraan Tukufu iliyoteremshwa kwa Mtume wetu Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam. Injili iliyoteremshwa kwa Iysa Alayhi Ssalaam. Taurat iliyoteremshwa kwa Musa Alayhi Ssalaam. Zaburi iliyoteremshwa kwa Daud Alayhi Ssalaam. Sahifa zilizoteremshwa kwa Ibrahim Alayhi Ssalaam.
  • 19. Mimi ni Mwislamu • Kati ya hivi, kuna vilivyopotolewa na kubadilishwa kabla ya kushuka Qur- aan. • Na Qur-aan ndiyo iliyo juu ya Vitabu hivi, na ndiyo yenye kuongoza sheria zote na hukumu zake, na yenye kuondosha yale yote yenye kwenda kinyume na hukumu zake baada tu ya kuteremka kwake. • Na kwamba Mwenyezi Mungu Hatokubali siku ya Kiyama ila amali kupitia uongofu wa Qur-aan. Hatokubali amali kwa kufuata Vitabu vilivyotangulia baada ya kuteremka Qur-aan kwa Mtume Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam. • Na kwamba Qur-aan ni Maneno ya Mwenyezi Mungu ya miujiza. Maneno haya yana utukufu wake, na wala hayaingiliwi na batili kabla yake wala baada yake. Mwenye kuyasema, amesema kweli, na mwenye kuhukumia kwayo, amefanya uadilifu, na mwenye kuyafanyia kazi
  • 20. Mimi ni Mwislamu basi hakika ameongolewa katika njia iliyonyooka, mwenye kushikamana nayo amefuzu na kuokoka, na mwenye kuyakengeuka atakuwa ni katika wenye kuhiliki. • Ni kwamba watu wa Qur-aan, hao ndio watu wa Mwenyezi Mungu waliokurubishwa Kwake, na kwamba mbora zaidi wa watu ni yule aliyejifundisha Qur-aan na akawafundisha watu, kwani Qur-aan hii itakuja siku ya Kiyama ikimwombea shifaa kila aliyeisoma, akaihifadhi na akaifanyia kazi, na itawaombea watu wake Pepo. • Qur-aan huzitwaharisha nyoyo kutokana na shubha na matamanio yanayozichafua, huzikurubisha kwa Muumbaji Wake Subhaanahuu wa Ta'alaa, na huzihimiza kufanya kazi ili kufuzu na kupata neema za kudumu milele. • Kati ya adabu za kusoma Qur-aan ni: Kuwa twahara na wudhuu.
  • 21. Mimi ni Mwislamu Kuelekea Kibla. Kukaa kwa adabu na heshima. Kutoisoma kwa haraka. Kuwa na unyenyekevu. Kuonyesha huzuni kwa madhambi na kuvuka mipaka. Kulia kutokana na kumwogopa Mwenyezi Mungu na Utukufu wa Maneno Yake. Kusoma kwa sauti nzuri. Kusoma kwa sauti ya chini ili kutowabughudhi wenye kuswali. Kuzingatia maana ya maneno. Kuhudhurisha moyo. Kutaamuli kwa kina Aayah za Mwenyezi Mungu. Tuwe na yakini kuwa kusimamisha hukumu za Kitabu hiki kwa watu ni moja kati ya sababu za kumakinishwa katika ardhi na kuwashinda maadui.
  • 22. Mimi ni Mwislamu Basi harakia ndugu yangu Mwislamu kwenda kwa Mola wako, na kikamate Kitabu hiki kwa hima. Kuwa na shime asikutangulie yeyote kuelekea kwa Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu Hufurahi zaidi kwa kurejea kwako Kwake kuliko wanavyofurahi watu kwa kurejea mtu wao aliyekuwa mbali.
  • 23. Mimi ni Mwislamu (4) KUWAAMINI MITUME • Ninawaamini Mitume wa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu Aliwateua Mitume kati ya wanadamu, Akawafunulia Sheria Yake kwa njia ya wahyi, na Akawaamuru kuifikisha kwa watu, na kwamba mwenye kuwatii ataingia peponi, na mwenye kuwaasi ataingia motoni. • Kisha Akawatilia nguvu kwa miujiza yenye kuonyesha ukweli wao ili iwasaidie mbele ya wakadhibishaji, na ili iwe ni hoja kwao. • Na kwamba Mtume wa mwanzo ni Nuhu, na wa mwisho wao ni Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam.
  • 24. Mimi ni Mwislamu • Na kuwa Mitume hawa ni watu; wanakula, wanakunywa, wanaoa,wanaugua na wanakufa. Wao ndio viumbe bora kabisa wa Mwenyezi Mungu na wamehifadhiwa na maasi. • Mitume wa Mwenyezi Mungu ni wengi. Mwenyezi Mungu Amewataja baadhi yao katika Qur-aan. Nao ni Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam, Ibrahim Khalili wa Ar- Rahmaan, Musa aliyesemeshwa na Allaah, Iysa Neno la Mwenyezi Mungu na Nuhu. Hawa ndio Mitume wenye azma ya juu Rehma na Amani ziwe juu yao. Pia Ismail, Is-haaq, Yakub, Harun, Ayyub, Yunus, Sulayman, Daawud, Yahya, Zakariya, Hud, Saleh,
  • 25. Mimi ni Mwislamu Yusuf, Shuayb, Ilyaas, Lut, Dhulkifl, Idris, na wengi wengineo. Kati yao kuna Aliowahadithia Mwenyezi Mungu katika Qur-aan na wengineo Hakuwahadithia. • Jambo la kwanza walilolilingania Mitume ni tawhid, na jambo kubwa zaidi walilolikataza ni shirki, na wote wamekuja na Uislamu na wito. • wa tawhid. Lakini sheria zao na mifumo ya kumwabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu ilitofautiana kutokana na kutofautiana zama zao na nchi zao. • Na kwamba Mitume walitoa bishara ya kuja kwa Nabii Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam na
  • 26. Mimi ni Mwislamu wakawaamrisha kaumu zao kumwamini Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam atakapotumwa kwao. • Tofauti kati ya Rasuli (Mtume) na Nabii ni kuwa Rasuli ni yule aliyefunuliwa sheria mpya na akaamrishwa kuifikisha kwa watu. Ama Nabii, ni yule aliyetumwa ili kuithibitisha na kuipitisha sheria ya Rasuli aliyemtangulia. • Ninaamini kuwa mbora wa Mitume mbele ya Allaah ni Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam toka kwa mwana wa Ismaili bin Ibrahim Alayhima Ssalaam. Allaah Amemtuma kwa watu wote,
  • 27. Mimi ni Mwislamu Akahitimisha Unabii kwa Unabii wake, na Utume kwa Utume wake. • Akamtilia nguvu kwa miujiza, Akamfanya bora kuliko Mitume wote. Pia Ameufanya Utume wake kuwa bora kuliko Utume wote uliotangulia, na sheria yake kuwa bora kuliko sheria zinginezo zilizopita, na Kitabu chake Qur-aan kuwa bora kuliko Vitabu vyote, na umati wake – Waislamu – kuwa bora kuliko uma nyinginezo. • Na Mola wake Akampa mambo ambayo Hakumpa yeyote katika Manabii waliomtangulia. Kati ya mambo hayo ni:
  • 28. Mimi ni Mwislamu (1) Al Wasiylah: Nayo ndiyo daraja ya juu kabisa Peponi ambayo Mwenyezi Mungu Amemwandalia Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam. (2) Al Kawthar: Nao ni mto Peponi wenye kupita chini ya Arshi ya Ar Rahman. (3) Al Hawdh: Ni sehemu ambayo Waislamu peke yao ndio watakayokunywa siku ya Kiyama. Siku ambayo watu watapatwa na kiu kikali, na jasho litawafika hadi magotini, viunoni na mabegani – kila mmoja kwa mujibu wa amali yake – na Waislamu watakunywa hapo kwa vikombe atakavyowapa
  • 29. Mimi ni Mwislamu Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam kwa mikono yake mitukufu. Baada ya hapo hawatapatwa na kiu milele. (4) Shafaa: Ni makamu ya kuhimidiwa siku ya Kiyama. Hapo Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam ataomba shifaa kwa Mwenyezi Mungu ili Waislamu waliofanya maasi watolewe motoni, na hatobakia ndani ya moto yeyote anayeshuhudia kwamba hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Allaah. Aliyefanya maasi hatosalia milele motoni, bali atatoka baada ya kutakaswa na maasi yake.
  • 30. Mimi ni Mwislamu Aliyewaamini Manabii wote na wala hakumwamini Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam, basi hatatoka motoni. (5) Na kwamba Allaah Amemnusuru na Akawanusuru askari wake na wafuasi wake hadi siku ya Kiyama kwa kuzagaza hofu ndani ya nyoyo za maadui umbali wa mwendo wa mwezi. Na hakuna Nabii yeyote aliyepewa hili kabla yake Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam. (6) Na ardhi imefanywa kwake na Waislamu kuwa msikiti (sehemu ya kuswalia) na twahara, na
  • 31. Mimi ni Mwislamu haikufanywa hivyo kwa Manabii waliomtangulia. (7) Na Allaah Amemtuma kwa watu na majini wote, lakini Mitume wengine wametumwa maalumu kwa watu wao tu. (8) Na kuwa yeye ndiye wa mwanzo kaburi lake kufunguka, na ndiye mwombezi wa kwanza, na ndiye wa kwanza kupewa shifaa, na ndiye wa kwanza kugonga mlango wa Pepo. Atakapougonga, mlinzi wa Pepo Ridhwaan atamuuliza: "Nani wewe?" Atajibu: "Muhammad". Ridhwaan atamwambia: "Kwako nimeamrishwa nisimfungulie yeyote kabla yako".
  • 32. Mimi ni Mwislamu Na kati ya miujiza ya Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam ni: Kupasuka mwezi. Alilirejesha jicho la Qatada lilipopofuliwa siku ya Uhud, macho yake yakarudi yakawa mazima kabisa. Aliurejesha muundi wa Ibn Al Hakam kama ulivyokuwa ulipovunjwa siku ya Vita vya Badr. Aliutaka mti utamke shahada, nao ukatamka shahada mbili mara tatu mbele ya kafiri, naye akasilimu. Kigogo cha mti alichokuwa akihutubia juu yake kililia wakati alipokiacha na hakikunyamaza mpaka alipoiweka mikono yake juu yake.
  • 33. Mimi ni Mwislamu Alikifanya chakula kidogo kuwa kingi baina ya mikono yake miwili, na wakaweza kula na kushiba zaidi ya watu 80 chakula cha kujaa viganja viwili. Aliyafanya maji kidogo kuwa mengi siku ya Hudaybiyah wakati jeshi lilipobakiwa na bakuli moja tu ya maji. Hapo Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam aliingiza mikono yake ndani, maji yakaanza kububujika kati ya vidole vyake kama chemchemu, wakanywa maji Waislamu wote na wakatawadhia maji hayo. Walikuwa kiasi cha watu 1400. Alipelekwa usiku hadi Msikiti wa Al Aqsa, na kisha alipandishwa hadi
  • 34. Mimi ni Mwislamu mbingu za juu na kukomea Sidrat Al Muntahaa. Alielezea na kuhadithia habari za umma zilizotangulia na Manabii wao nailhali yeye hana kisomo; hajui kusoma wala kuandika. Pia alielezea matukio yatakayotokea siku za usoni kwa kufunguliwa Fursi na Rome, kusambaratishwa ufalme wa Kisra aliyechanachana barua ya Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam aliyomtumia, pamoja na miujiza mingineyo mingi. Muujiza mkubwa zaidi wa Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam ni Qur-aan Tukufu. Ni
  • 35. Mimi ni Mwislamu muujiza utakaosalia hadi siku ya Kiyama. Kisha Allaah Ameunyanyua utajo wake, Akaliandamisha jina la Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam na Jina Lake Subhaanahuu wa Taalaa, na Akaifanya shahada ya kuwa hapana mola isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kuwa ndio jambo la kwanza analoingia nalo mja katika Uislamu,na jambo la mwisho analotoka nalo duniani. Basi yeyote ambaye neno lake la mwisho litakuwa ni "Laailaaha illa Allaah", ataingia peponi. • Ni wajibu wetu kwa upande wa Mtume wetu Swalla Allaahu Alayhi
  • 36. Mimi ni Mwislamu wa Aalihii wa Sallam tusilitangulize neno la kiumbe yeyote juu ya neno lake, au rai ya yeyote hata kama ana sauti kwa watu. Na ikiwa watu watakutangulia kuhamia kwake, basi hama wewe kwenda katika sunnah yake katika kila jambo lako na wala usimfuate mwingine zaidi yake. Ni wajibu wetu tushikamane sote pembezoni mwa amri yake na tumtii, kwani mwenye kumtii Mtume, basi huwa amemtii Mwenyezi Mungu. : GFEDCBA • Na tusimwiite ila kwa kusema Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam. Tusiseme (Muhammad) basi.
  • 37. Mimi ni Mwislamu • Tujipambe kwa adabu zake, na tumwige katika hali zake zote; kulala kwake, kula kwake, kutembea kwake, kuswali kwake, kufunga kwake, kutoa kwake sadaka, na jihadi yake. • Na tumpende zaidi kuliko nafsi zetu, wana wetu, wazazi wetu na watu wote. • Na tumpende kila yule anayempenda Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam na kumfanya kiigizo chake, na tumchukie kila yule anayemchukia Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam na wala hawajibiki na sheria yake.
  • 38. Mimi ni Mwislamu • Hivyo basi, ni lazima kwa Mwislamu awapende Waumini, awanusuru, ajifananishe nao, ashughulikie mambo yao, asaidiane nao katika mambo ya kheri, na awafanye kuwa marafiki zake wa dhati. • Ni wajibu kwake awabughudhi makafiri na ukafiri wao, asiwatii, asiungane nao dhidi ya Waislamu, wala asisaidiane nao katika ubatilifu wao, na wala asishiriki katika sikukuu zao. Ni haramu kwake kuwadhulumu, na linalotakiwa ni kuwatendea haki. • Ni wajibu wetu tuwapende Mama wa Waumini; Wakeze Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam,
  • 39. Mimi ni Mwislamu na tuwapende Maswahaba Wake Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam, kwani wao ndio bora wa watu baada ya Manabii. • Pia ni wajibu wetu tuihuishe Sunnah yake Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam, tuidhihirishe sheria yake, na tubalighishe ulinganio wake kwa watu wote. Kisha tusubiri maudhi na kero zinazotupata katika kuyapigania hayo, kwani hayo hayaepukiki. • Kwa vile Mwenendo wa Mwenyezi Mungu uliopita kwa viumbe Vyake unahukumia kuwa hakuna Nabii au walii yeyote aliyelingania haki hii ila alifanyiwa uadui na kuudhiwa.
  • 40. Mimi ni Mwislamu • Zindukana ndugu yangu Mwislamu! Maudhi ya makafiri yasikufanye ukaiacha dini yako. Kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam aliudhiwa wakati Maswahaba walipokuwa wachache, nao pia waliudhiwa wakafanya subira. • Na wala usilegeze azma yako hata kama watakwambia kuwa unayoyazungumza ni upuuzi, una misimamo migumu, au umepitwa na wakati. Au wakisema: "ashachezewa akili huyo". Kwani wewe una kiigizo chema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, yeye ashaambiwa mshairi na hata mwendawazimu.
  • 41. Mimi ni Mwislamu • Wala usisononeke ukiambiwa mpotevu mwenye siasa kali. Hii ndio tabia ya makafiri kwa Waumini. : ((Na wanapowaona, husema hakika hawa bila shaka ni wapotevu)). • Ikiwa watu wako makundi mawili, je haikutoshi wewe kuwepo katika kundi aliloko Mtume wako Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam?! • Achana nao hao mpaka ifike siku ambayo dhalimu ataviuma vidole vyake aseme: "Laiti mimi ningeliifuata njia pamoja na Mtume".
  • 42. Mimi ni Mwislamu : ¯ • Wala usibabaike au kuchanganyikiwa kama watakwambia kuwa wewe ni gaidi au mwovu, kwani hayo ndio madai ya madhalimu dhidi ya Waumini duniani na akhera. Ni kuwa pale Malaika watakapowaongoza kwenda Jahannamu wakisunukia, wataangalia humo kisha waseme: : JIH GFEDCBA ((Na watasema: Mbona hatuwaoni watu tuliokuwa tukiwazingatia kuwa ni katika waovu?))
  • 43. Mimi ni Mwislamu • Na hapa, Waumini (ambao makafiri wamewaita kuwa ni waovu) watawaita toka kwenye magorofa ya juu kabisa ya Firdaws wakiwaambia: : ¯ LKJIHGF ٤٤ : ‫اف‬ ‫(( ا‬ ‫ر‬ ‫و‬ ‫و‬ ‫)) أن‬ ((Hakika sisi tumeyakuta Aliyotuahidi Mola wetu kuwa ni kweli))
  • 44. Mimi ni Mwislamu (5) KUAMINI SIKU YA MWISHO • Ninaiamini siku ya mwisho, nayo ni iku ambayo dunia (nyumba ya amali) itamalizika, na akhera (nyumba ya malipo) itasimama, wema wakalipwa Pepo, na waovu wakalipwa moto. • Katika siku ya Kiyama, mizani itawekwa, na kila mja atapewa kitabu chake. Atakayepokea kitabu chake kwa mkono wake wa kuume, basi Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam atakuwa pamoja naye Peponi. Ama yule atakayepokea kitabu chake kwa mkono wake wa kushoto, basi atakuwa pamoja na
  • 45. Mimi ni Mwislamu Firauni –laana ziwe juu yake– motoni. • Sirati itawekwa, atakayefanikiwa kuivuka basi atafikia Peponi. Ama ambaye kulabu zitamnyakua kutokana na amali zake mbovu, basi ataangukia motoni. • Siku ya Kiyama ina dalili, ina alama ndogo na ina alama kubwa. • Miongoni mwa alama ndogo ni kupotea uaminifu, kukithiri mauaji, madaraka kukamatwa kwa mabavu na mafasiki, na masuala muhimu kuzungumziwa na wasiojua kitu. • Na miongoni mwa alama kubwa ni kuibuka Al Mahdi, kusimama ukhalifa
  • 46. Mimi ni Mwislamu wongofu utakaokwenda juu ya misingi ya njia ya Utume kabla ya kutokea Kiyama, na kudhihiri masihi mwongo. • Pia kuteremka Iysa Alayhi Ssalaam ili awaongoze Waislamu, apigane na makafiri, avunje vunje misalaba, aue nguruwe, na azikatae dini zote nyingine ila Uislamu tu. • Basi haitobakia nyumba yoyote ya mjini au ya mashambani ila Mwenyezi Mungu Ataiingiza dini hii, kwa heshima ya mwenye nguvu, au kwa udhalili wa mnyonge. • Vile vile kutoka Yaajuju na Maajuju. Pia atatoka mnyama
  • 47. Mimi ni Mwislamu anayewasemesha watu, na jua litachomoza toka magharibi, Qur-aan itaondoshwa na mambo mengineyo. • Basi yeyote atakayefanya amali ya uzito wa atomu ikiwa ni ya kheri au ni ya shari, ataiona siku ya Kiyama ndani ya kitabu chake. • Basi harakieni kwenye mambo ya kheri kabla haujamalizka muda wa kusajiliwa kwa kufa mja katika muda ambao haujui yeyote ila Mwenyezi Mungu Pekee. • Wakamwosha jamaa zake, wakamvisha sanda, wakamswalia, wakamzika. Kisha akajiwa na Malaika wawili; Munkari na Nakiyr,
  • 48. Mimi ni Mwislamu wakamkalisha kitako na kumwuuliza: "Nani Mola wako? Nini dini yako? Nani Nabii wako?" • Ikiwa atajibu kuwa: "Allaah ni Mola wangu, na Uislamu ndiyo dini yangu, na Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam ndiye Nabii wangu na Mtume wangu" – na Allaah Akamwezesha hilo – basi itafunguliwa katika kaburi lake harufu ya rayhaan hadi peponi, akaona mashukio yake huko, na makasri yake na ufalme wake. Hapo atashangilia kwa furaha kubwa, na kaburi lake litapanuliwa upeo wa macho.
  • 49. Mimi ni Mwislamu • Na ikiwa ni katika makafiri, basi hatoweza kujibu chochote, kwani majibu wakati huo si kwa akili au werevu wa mtu. • Bali Mwenyezi Mungu Huwathibitisha na kuwaimarisha watu wa imani wakati huo kwa yale waliyoyatanguliza kati ya amali njema zilizosimamia juu ya tawhid, utekelezaji wa faradhi, kushiriki jihadi, kutenda mema, kuamrisha mema, kukataza mabaya, kutoa sadaka, kusoma Qur-aan, kufunga siku za joto kali, na kusimama kuswali muda mrefu usiku wa baridi kali.
  • 50. Mimi ni Mwislamu • Ama akiwa ni katika makafiri, basi kaburi lake humbana hadi mbavu zake zikaingiana katika mwili wake, na kaburi lake huwa ni shimo katika mashimo ya motoni kwa sababu ya amali zake mbaya. • Basi jitahidi ndugu yangu Mwislamu, kwani leo ni amali na hakuna hisabu, lakini kesho ni hisabu na hakuna amali. • Na siku hiyo, Waislamu watiifu wataingia Peponi peke yao, kwa vile Mwenyezi Mungu Hatoikubali dini yoyote siku ya Kiyama isipokuwa Uislamu.
  • 51. Mimi ni Mwislamu • Ndani ya Pepo kuna neema ambazo hakuna sikio lililowahi kuzisikia, wala jicho lililowahi kuziona, wala hata kuwaziwa katika akili ya mwanadamu. Neema zake zitasalia milele wala hazitomalizika, na waliomo humo hawatakufa milele. Neema kubwa zaidi ya zote humo, ni kuuangalia Uso wa Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu wote. • Na waasi, waovu na makafiri wataingia motoni. Ndani ya moto, kuna adhabu zisizoweza kuvumilika Alizoziandaa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya makafiri. Milima mirefu thabiti haiwezi kuzivumilia adhabu hizi, na
  • 52. Mimi ni Mwislamu hao wataadhibiwa humo bila kupumzishwa. • Na humo, wafuasi wa mataghuti wataomba adhabu iongezwe maradufu kwa wakubwa wao waliowapoteza. Na hapo Mwenyezi Mungu Ataamuru adhabu iongezwe maradufu kwa wote. • Basi thibiti ndugu yangu Mwislamu juu ya haki hii, wala usidanganyike kabisa kuona kuwa wavunjaji sheria ni wengi zaidi, kwani ikiwa wewe utawatii na ukawafuata wengi waliomo ardhini, basi watakupoteza njia ya Mwenyezi Mungu. Nawe pita pamoja na wenye kupita kuelekea kwa Mwenyezi Mungu.
  • 53. Mimi ni Mwislamu • Kwani kundi katika umma wa Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam litaendelea kuwa juu ya haki likiwa na nguvu, hawezi kuwadhuru yeyote aliyekwenda nao kinyume au aliyewasaliti mpaka siku ya Kiyama. • Basi ni mbinu zipi za kuzijua ngazi hizo za kupanda juu, na kuokoka na ngazi hizo za kuporomokea chini? Na ni mbinu zipi za kuwafikia waliotangulia wenye kukurubishwa, na kujiweka mbali na wapingaji wenye kuangamia? Bila shaka ni toba ya kweli ya kusahihisha na kurekebisha yaliyopita, na amali njema za kuweka sawa umri
  • 54. Mimi ni Mwislamu uliosalia, na kuweka nia ya kweli ya kunyooka na kutokengeuka. • Basi kuwa pamoja na watu kwa kiwiliwili chako, ukiuza, ukinunua, ukioa na ukiiamirisha ardhi kwa yale Aliyokuhalalishia Mwenyezi Mungu. • Wala moyo wako usifungamane na kitu chochote cha kidunia, bali nenda na moyo wako pale ambapo unatakikana uwe, huko chini ya Arshi ya Ar Rahmaan, na sujudu kwa moyo wako sijdah ambayo utaendelea kuisujudu hadi siku ya Kiyama.
  • 55. Mimi ni Mwislamu (6) KUAMINI QADHAA NA QADARI • Nako ni kuamini kwamba Mwenyezi Mungu Anayajua yote yaliyomo ulimwenguni, yote yanayofanyika na yatakayotokea hadi siku ya Kiyama. Hata chembe ndogo mno, Yeye Hakosi kuijua. Na kwamba Yeye Anavijua vitendo vya waja, riziki zao, muda wao wa kuishi, na nani kati yao atakuwa wa peponi, na nani kati yao atakuwa wa motoni kabla Hajawaumba. • Na kwamba Mwenyezi Mungu Ameyaandika makadirio haya katika Lawh Al Mahfuudh kabla hata Hajaziumba mbingu na ardhi kwa miaka elfu hamsini, na kwamba Lawh
  • 56. Mimi ni Mwislamu Al Mahfuudh hii hakuna malaika wa karibu au hata Nabii aliyetumwa awezaye kuichungulia. • Hata kijusi kinapokuwa ndani ya tumbo la uzazi la mama yake, Mwenyezi Mungu Huwaamrisha Malaika waandike kama ni cha kike au kiume, waandike na riziki yake, amali yake, muda wake wa kuishi na hatima yake (ima peponi au motoni). Pia waandike mazuri na mabaya atakayokabiliana nayo. • Kisha unapoingia usiku wa cheo (Laylatul Qadr), huteremka makadirio ya mwaka mzima toka Lawh al Mahfuudh kati ya ajali za watu, riziki zao, nani kati yao atahiji mwaka huo na mengineyo. Katika
  • 57. Mimi ni Mwislamu usiku huo, hukadiriwa mambo ya mwaka mzima. • Kisha huteremka makadirio ya kila siku kwa nyakati zake na watu wake, hapo Mwenyezi Mungu Huwanyanyua watu na wengine Huwashusha. • Na tuamini kuwa Mapendeleo ya Mwenyezi Mungu ndiyo yawayo, Alilolitaka huwa na Asilolitaka haliwi. Mwenyezi Mungu Hana wa kumshinda, na Yeye Ndiye Mwenye kuzipindua nyoyo. Humwongoa Amtakaye kwa fadhila Zake na rehma Zake, na Humpoteza Amtakaye kwa Uadilifu Wake na Hekima Yake, kwani Yeye Ndiye Ajuaye zaidi nani anastahiki uongofu na nani anastahiki upotevu.
  • 58. Mimi ni Mwislamu • Na Mwenyezi Mungu Haulizwi yale Ayafanyayo lakini watu huulizwa. • Na tuamini kuwa Mwenyezi Mungu Amekiumba kila kitu, na hakuna chembe yoyote ndogo ulimwenguni isipokuwa Mwenyezi Mungu Ameiumba na Akaumba kutikisika kwake na kutulia kwake. • `Na kwamba Yeye Amewaumba waja na vitendo vyao, na kwamba Yeye Amewaumbia waja uwezo na mapendeleo yao ili wajichagulie wenyewe vitendo vyao. • Na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu Amewaamuru viumbe Wake wamtii, na Akawaahidi kuwapa Pepo Yake wakifanya hivyo, na Amewakataza kumwasi Yeye, na
  • 59. Mimi ni Mwislamu Akawapa onyo la kuwaingiza ndani ya moto Wake wakifanya hivyo, na wala Hakuwakalifisha kazi isipokuwa ile ambayo wanaweza kuifanya. Na hapo wakagawanyika makundi mawili: Waumini na makafiri; kwa hiari yao wenyewe, kwa mapendeleo yao wenyewe na kwa uwezo wao wenyewe, na yote hayo Mwenyezi Mungu Amewaumbia. • Na kwamba thawabu na adhabu hutokana na kuifuata sheria, si kwa kutangulia Elimu ya Mwenyezi Mungu kwao. Basi yeyote atakayefanya amali yoyote ya kheri ya uzito wa atomu, atalipwa kwayo. Na yeyote atakayefanya amali yoyote ya shari ya uzito wa atomu, basi ataadhibiwa kwayo.
  • 60. Mimi ni Mwislamu • Na kwamba kinachozingatiwa ni mwisho wa matendo, na kwamba kila mja ni mwenye kuendeshwa katika lile aliloumbiwa kati ya kufurahika Peponi au kupata shakawa motoni. • Na kwa ajili hiyo, ni wajibu kwa mja aogope mwisho mbaya, na aendelee daima kumwomba Mwenyezi Mungu na amhitajie, Amhidi katika njia iliyonyooka, na adumu kumwomba Amsaidie katika kumtii, na ajilinde Kwake na maasia, kwa vile mja hana hila wala nguvu zozote za kuyafanya hayo ila kwa Uwezo wa Mwenyezi Mungu. • Na kwamba Waumini Huridhia Qadhaa ya Mwenyezi Mungu na Qadari Yake; ya kheri yake na ya
  • 61. Mimi ni Mwislamu shari yake, katika misukosuko na katika furaha, na wana yakini kuwa hawezi yeyote kuwanufaisha isipokuwa kwa Qadari ya Mwenyezi Mungu, na wala hawadhuru isipokuwa liwe lisha andikwa na Mwenyezi Mungu. • Na mja hatopata utamu wa imani mpaka pale atakapojua kwamba lililompata lisingekuwa la kumkosa, na lililomkosa lisingekuwa la kumpata. Na mwisho naomba nikisema: "Ninamhimidi Mwenyezi Mungu, na ninamwomba Aniingize Peponi mimi na Waislamu wengine, na Anilinde na moto mimi na Waislamu wengine". Aamiyn.
  • 63. Mimi ni Mwislamu ed c b a ` _ k j ih g f [٨٥:‫ان‬ ‫]ل‬ Ù anamuslim@windowslive.com Ø × ª Ø WWW.Iam-Muslim.com ٢٠١٠ J ١٤٣١ ‫و‬ ‫ق‬ ‫ا‬ ٢٠٠٩L٢٢٢٧٤ W ٠١٢٠١٥٢٩٠٨ :ª W
  • 64. Mimi ni Mwislamu ª a ٠١٢٥٨٣٤٥٧٤ ٠١٠٦٧١٤٧٦٨