SlideShare a Scribd company logo
1 of 83
Download to read offline
Umefika wakati tuyazungumzie mambo kadhaa ya
msingi waziwazi ili Wakristo watambue ya kwamba
Bwana ana mambo mazuri zaidi kwa ajili yao!
Miki Hardy
LINAHITAJI
KUJUA
KANISA
Kanisa Linahitaji Kujua
10
Hakimiliki © 2013 na Church Team Ministries International (CTMI)
Kanisa Linahitaji Kujua na Miki Hardy.
Imechapishwa na Church Team Ministries International (CTMI)
Toleo la kwanza: Julai 2015
Jalada limebuniwa na: Idara ya Habari ya CTMI
Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu ya chapisho hili inayoweza kunakiliwa,
kusambazwa,au kutolewa kwa namna yo yote ile isipokuwa kwa ruhusa ya
mchapishaji.
Vifungu vya Biblia vimetolewa katika Biblia, Swahili – Union Version, 1962.
Machapisho mengi ya Church Team Ministries International yanapatikana kwa
gharama nafuu ikiwa yananunuliwa kwa jumla kwa ajili ya kutangaza, kuchangisha
fedha, kugawa bure, na kwa kuelimishia.
Kwa maelezo zaidi, tuandikie: Media Dept., CTMI, Trianon, Mauritius;
au tuma baruapepe kwa: media@ctmi.org
Tembelea tovuti yetu: www.ctmi.org
ISBN 978-99949-0-181-4
Yaliyomo
I. Moyo wa Mungu Juu ya Ndoa na Talaka 5
II. Je, Wakristo Wanaweza Kupagawa Mapepo? 15
III. Mkristo na Pesa 23
IV. Mungu na Muziki 31
V. Vita ya Rohoni 39
VI. Mahusiano Kabla ya Ndoa 47
VII. Barabara ni Nyembamba 55
VIII. Kanisa Litakabiliwa 65
IX. Yesu Anaita Tena 75
...................................
..........................
.......................................................................
......................................................................
...........................................................................
.......................................................
........................................................
................................................................
.....................................................................
3
Kanisa Linahitaji Kujua
4
Sura ya I
Moyo wa Mungu
Juu ya Ndoa na Talaka
5
Kanisa Linahitaji Kujua
Wakristo wengi leo wanaweza kukumbuka wakati ambapo suala
la talaka kwa mchungaji au kiongozi wa Kanisa lilikuwa ni jambo la
aibu isiyoneneka. Hapakuwepo na uwezekano kwa mtu wa jinsi hiyo
kuendelea katika utumishi. Zaidi na zaidi, leo tunaona wachungaji
wakitoa talaka, wakioa upya na kuendelea na huduma kana kwamba
hakuna jambo zito lililofanyika. Ninaamini haya ni matokeo ya anguko
na udini ambavyo vimechukua nafasi ya fundisho la uzima na Kweli
ya Kibiblia ndani ya Kanisa. Hili ndilo chimbuko la hii hali ya mambo.
Sasa, ikiwa mchungaji anaweza kumpa mkewe talaka na akaendelea
kuwaongoza watu wa Mungu, je! waumini wanapata mfano wa jinsi
gani wa kuiga?
Labda maswali tunayopaswa kujiuliza ni, “Ni kwa nini Wakristo wawili
waliojazwa Roho Mtakatifu washindwe kutatua tofauti zao” na, “Je!
kuna uhalali wo wote kwa haya matatizo kutotatulika, au kwa wawili
hawa kuachana?” Ama liwe linamhusu mchungaji, au mshirika wa
kanisa, ninaamini suala la kutengana, kutoa talaka, na kufunga ndoa
mara ya pili hufanyika kwa sababu hawa watu hawajui wajibu wao
kamili mmoja kwa mwingine katika ndoa. Tunaona kwenye Maandiko
ya kuwa mume ana wajibu mkubwa mno: kumpenda mkewe kama
Kristo anavyolipenda Kanisa. Vivyo hivyo, mke naye ameitwa amtii
mumewe. Kama wawili hawa wasipouchukua msalaba wao, na
kumruhusu Roho wa Mungu awavunje na kuwabadilisha, hilo kamwe
halitakuja kutokea… Mungu peke yake ndiye anayeweza kulifanya hili
mioyoni mwao. Hakuna mbinu inayoweza kulifanya hili… ni matokeo
ya kazi ya Msalaba maishani mwao!
6
Sijaona popote kwenye Maandiko kinachonielekeza kuamini ya
kuwa ni mapenzi ya Mungu kwa wanandoa Wakristo, achilia mbali
mchungaji, kutoa talaka. Hii ni kwa sababu Mungu, kwa njia ya
Msalaba, ameleta njia ya kurejesha upendo na umoja kati yao. Hebu
sasa tuangalie Neno la Mungu linavyotufunulia kuhusu suala la ndoa
na talaka…
Siku hizi, watu wengi hawaoni shida kwa Wakristo wanandoa
kuachana kwa sababu tu mmoja wao hapatani na mwenzake; au
kwa kuwa tu hawana mtazamo mmoja kuhusu mambo mbalimbali au
hawana tena maono mamoja!
Hakika hili ni eneo ambalo Kanisa limekubali kuathiriwa si tu na njia
za ulimwengu usioamini, bali pia na viongozi wa Kikristo ambao
wameandika vitabu, wakihalalisha matendo yao ya kibinafsi sana na
ambao, kwa kuamua kuchukua njia ya talaka wamefungua mlango
kwa waumini kufanya vile vile. Ninaamini ya kwamba badala yake,
tunapaswa tuuangalie mtazamo wa Mungu juu ya suala hili.
Ndoa Kwenye Agano Jipya
Kwenye kitabu cha Mwanzo, Mungu aliianzisha ndoa. Baada ya yale
Yesu aliyokamilisha Msalabani, ndoa ya kwenye Agano la Kale, yenye
wake wengi na hati za talaka, haiwezi tena kulinganishwa na ndoa
chini ya Agano Jipya.
Sura ya I - Moyo wa Mungu Juu ya Ndoa na Talaka
7
Kanisa Linahitaji Kujua
Mpango wa Mungu kwetu sisi, kama Wakristo tuliozaliwa mara ya pili,
ni kuishi na waume zetu na wake zetu hadi ‘kifo kitakapotutenganisha’.
Katika Marko 10:2, kwa kuwa Yesu alikuwa akiwahoji Mafarisayo
juu ya mtazamo wao wa kisheria katika masuala mengi, walimjaribu
kwa kumwuuliza: “Je, ni halali kwa mtu kumwacha mkewe?” Yesu
akawaonyesha ya kuwa, chini ya Musa na Torati, Mungu ‘aliruhusu’
talaka kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao (Marko 10:5); lakini
katika Agano Jipya, mambo yangekuwa tofauti. Katika Mathayo 5:32,
anazungumzia waziwazi juu ya kile kinachotarajiwa kwa waamini
wote wa Agano Jipya: “Lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye
mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi;
na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.” ‘Isipokuwa kwa habari ya
uasherati’ bila shaka haimaanishi pale mwenzi mmoja anapoanguka
katika dhambi na kufanya tendo moja la uasherati au la kukosa
uaminifu. Inazungumzia mtu ambaye amerudi nyuma na anaishi
katika dhambi, na aliyedhamiria kuendelea kuishi katika dhambi. Kwa
kuiruhusu talaka katika mazingira hayo maalum, Yesu hajaondoa
ukweli kwamba yule aliyekosewa bado anatakiwa kunyenyekea na
kusamehe. Hili linaweza kufanyika kwa dhati pale tu tunapoikubali njia
ya Msalaba. Kwa hivyo, Biblia iko wazi: kwenye Agano Jipya, hakuna
uhalali wowote wa kutoa talaka isipokuwa katika maeneo maalum
sana… vinginevyo itapunguza kile Yesu alichokifanya Kalvari!
8
Injili Zisizokuwa Na Uweza
Nina hakika utakuwa umegundua ya kuwa Kanisa limepoteza
mwelekeo katika hili eneo, na linaenenda kama vile Injili ni kitu
kinachobadilika kwa kutegemea nyakati. Katika miongo michache
iliyopita, Kanisa, kwa kujumuisha wachungaji na viongozi, kwa usahihi
kabisa, halikukubaliana na talaka, lakini leo hii talaka imekubalika
makanisani. Ni nini kilichofanyika? Bila shaka ni kwa sababu injili
inayohubiriwa leo hii imebadilika na haina uwezo wa kushughulika
na mambo ya jinsi hiyo. Haina nguvu tena ya kuihakiki dhambi kama
mwanzoni. Mfano mzuri ni injili ya ‘Mafanikio’ inayovuta mioyo ya
watu kuyaandamia mambo ya mwilini badala ya kutafuta makuzi ya
rohoni. Haijengi, na hakika haina uwezo wa kukabiliana na mambo
ya ndani ambayo Wakristo wanapambana nayo leo. Hii ndio maana
ni muhimu turejee kwenye injili ya ufunuo wa Msalaba ikiwa tutataka
kuona familia za Kikristo zenye umoja pamoja na kupungua kwa
kiwango cha talaka Kanisani.
Siku hizi Wakristo mara nyingi wanataka njia rahisi ya kutatua matatizo
yao ya ndoa, mlango rahisi wa kutokea. Wanaachana kwa sababu
nyepesi kama vile: “Mke wangu hanitii”; “Mume wangu si mtu wa
rohoni,” au mbaya zaidi, “Hatupatani tena, maono yetu na matarajio
yetu yamebadilika…” Watu wa jinsi hii bila shaka hawajaisikia injili
sahihi, kwani injili sahihi itawaongoza katika kuwajibika kila mmoja
kwa mwenzake.
Sura ya I - Moyo wa Mungu Juu ya Ndoa na Talaka
9
Kanisa Linahitaji Kujua
Nafasi Ya Mume
Niruhusu nifafanue juu ya ufunuo wa ajabu Paulo aliopewa kuhusu
ndoa kwenye Waefeso 5. Uhusiano wa mume na mke ndio tu
uliolinganishwa katika Agano Jipya na uhusiano Yesu alio nao na
Kanisa lake. Paulo anatamka kwa ujasiri ya kuwa, “KAMA Kristo naye
alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake VIVYO HIVYO mume naye
anapaswa kumpenda mke wake.” Yesu alijinyenyekeza, akachukua
sura ya mwanadamu, akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
Hiyo ndiyo hali ya moyo Yesu anayoagiza mume awe nayo kwa mke
wake. Huo ndio wajibu wa mume: kama Yesu, yeye naye anaitwa
apoteze haki zake na autoe uhai wake kwa ajili ya mke wake. Huu
ndio ufunguo wa ndoa yenye mafanikio.
Utaratibu Wa Mungu Kwenye Ndoa
Nafasi ya mke imefananishwa na ile ya Kanisa. Paulo anatamka ya
kuwa “KAMA vile Kanisa limtiivyo Kristo, VIVYO HIVYO mke naye
anapaswa kumtii mumewe.” Kwa hivyo, Kanisa – wewe na mimi –
linapoelewa kile Yesu alichofanya msalabani kwa ajili yetu; kwa
manenomengine,upendoaliouonyesha,sisinasitunawezakumpenda
pia. Isingewezekana tumpende Yeye kabla ya kuujua upendo wake
kwetu. Je, unaweza ukaona utaratibu wa mambo hapa?
10
Ni wazi, basi, kwamba mume ana wajibu mkubwa zaidi kuliko mke
katika ndoa, kwani huduma yake inalinganishwa na ya Kristo, ilhali
ya mke imefananishwa na ya Kanisa. Ikiwa mume atakuwa tayari
kuchukua hatua ya kwanza, katika kuutii wito wake, kama Kristo
alivyofanya, moja kwa moja atavuna hali ya utii kutoka kwa mke
wake. Katika mazingira ya kawaida, hatutarajii kwamba utii wa
mwanamke kwa mumewe utakuwa wa moja kwa moja; lakini msingi
sahihi unapokuwepo, mume anaweza akatarajia ya kuwa mkewe
atamnyenyekea. Hata hivyo, hata kama mke hatafanya vile, mume
anapaswa aendelee kuyatoa maisha yake kwake, na amtegemee
Mungu kufanya muujiza moyoni mwa mkewe. Mwishoni mwa kifungu
hiki, Paulo ananukuu andiko kutoka katika Agano la Kale, “Kwa sababu
hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na
mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.” Moyo wa Mungu kwa
ajili ya ndoa ni mume na mke wadumu katika umoja maisha yao yote.
Tunapozitii amri za Mungu, yeye ni mwaminifu na hutenda miujiza.
Mume Wa Mke Mmoja…
Yapo mambo mengi sana yahusuyo ndoa ambayo hayajatajwa katika
Biblia. Kanisani mwetu penyewe tumeshuhudia matukio mengi
tofauti katika miaka hii mingi, na tumejifunza kuyatatua kila moja kwa
namna yake, katika neema na kweli. Mahali ndugu wa kiume au wa
kike alipoichukua njia ya Msalaba, na kuiruhusu toba kufanya kazi
11
Sura ya I - Moyo wa Mungu Juu ya Ndoa na Talaka
Kanisa Linahitaji Kujua
moyoni mwake, tumeshuhudia urejesho na ushindi maishani mwao
na katika utumishi wao kwa Bwana. Na hebu niongeze kusema
ya kwamba Mungu si Mungu anayetoa nafasi ya pili au ya tatu ya
kujaribisha mambo. Mpango wake sikuzote ni kwa mume kuwa na
mke mmoja, na ametuwezesha katika hilo kwa kumtuma Yesu katika
mfano wa mwanadamu, afe Msalabani na kuishinda dhambi katika
mwili. Ni juu yetu kuyatoa maisha yetu yawe dhabihu ili miili yetu
isulubiwe. Mwanamume anayemwacha mkewe halafu akaendelea
katika utumishi kana kwamba hakuna kilichofanyika, hawezi kutarajia
kuendelea kubeba upako ule ule katika utumishi wake kwa Bwana, na
hasa ikiwa ameoa tena, hadi atakapoacha kuhalalisha uamuzi wake
huo na kutubu.
Ufunguo Unaoleta Matengenezo
Si mpango wa Mungu kwa mtu yeyote kumwacha mwenzi wake.
Mungu anachukia talaka; lakini hawakatai wale walioachana – au
waliooa ama kuolewa mara ya pili – ikiwa watatubu. Ikiwa nimegusa
eneo linalokuhusu, hujachelewa. Mungu anaweza kukurejesha,
pamoja na utumishi wako kama uko kwenye huduma, ikiwa utakuwa
tayari kukiri ya kuwa haukuenenda sawasawa na moyo wala Neno la
Mungu, bali ulifuata tamaa za mwili wako; na ya kuwa, inawezekana
ulijiingiza katika mahusiano yasiyo sahihi.
12
Ikiwa ni hivyo, ni lazima umrudie Bwana kwa toba ya kweli; kulingana
na maongozi ya Roho Mtakatifu, na ukiwa na utayari wa kufanya lolote
atakalokuagiza kufanya... hata kama itakulazimu kumrudia mwenzi
wako wa mwanzo. Kumbuka ya kwamba Bwana hahitaji sababu au
maelezo kuhusu mwenzi wako, au kuhusu yale aliyoyafanya. Yeye
huuangalia moyo wa mtu.
Katika kila jambo, Mungu anatamani tuwe na moyo safi, mnyenyekevu,
uliojaa msamaha, na ulio na toba. Inawezekana yakawepo
mahusiano ambayo pengine hayawezi kurekebishika; ila, mengi zaidi
yanarekebishika, ikiwa tuko tayari kujikana nafsi zetu na kuuchukua
msalaba wetu. Msalaba ndilo suluhisho la Mungu kwa ndoa yenye
mafanikio!
13
Sura ya I - Moyo wa Mungu Juu ya Ndoa na Talaka
Kanisa Linahitaji Kujua
14
Sura ya II
Je, Wakristo Wanaweza
Kupagawa Mapepo?
15
Kanisa Linahitaji Kujua
Katika safari zangu barani Afrika katika miaka 25 iliyopita, swali moja
limekuwa likijitokeza mara kwa mara: “Je, inawezekana kwa Mkristo
aliyezaliwa mara ya pili kupagawa mapepo?” Hili jambo mara nyingi
huhusishwa na maisha aliyoishi mhusika huko nyuma, au kibaya
zaidi, linahusishwa na mambo waliyoyafanya mababu zake.
Inanihuzunisha kuona kwamba kuna Wakristo wengi wanaoamini
ya kwamba wao, au ndugu zao wa kiume na wa kike katika Kristo
wanaweza kupagawa mapepo baada ya kupokea wokovu. Sote
tunakubali ya kuwa kazi za mapepo na roho chafu zipo. Lakini je!
inawezekana kwa mtu aliyezaliwa mara ya pili kuhitaji kufunguliwa
kutokana na nguvu za mapepo? Ninaposoma Maandiko, jibu langu
kwa swali hili ni “Hapana!” yenye nguvu. Biblia iko wazi kuhusu hili
suala: tunapozaliwa mara ya pili, tunaokolewa kutoka katika nguvu
za giza na kuingizwa katika Ufalme wa Yesu Kristo. Roho Mtakatifu
anakuja kuishi ndani yetu na nuru haiwezi kukaa pamoja na giza.
Hakuna jinsi kabisa ambapo pepo anaweza akaishi ki-kwelikweli
ndani ya Mkristo aliyezaliwa mara ya pili, aliyeyatoa maisha yake kwa
Bwana Yesu Kristo na anayetamani kumtumikia. Haiwezekani kabisa!
Tunapaswa tuhoji wokovu wa watu waliojitokeza kwenye mikutano
na kuungama sala ya toba, halafu wakaendelea kudhihirisha dalili za
kupagawa mapepo. Katika hali kama hizo, labda tungepaswa kuuliza
swali: ‘Je, toba ya kweli imefanyika mioyoni mwao?’
Lakini cha muhimu zaidi, ni kwamba ninaamini matatizo mengi
yanayosingiziwa pepo ni madhihirisho tu ya mwili. Kwa bahati mbaya,
16
Wakristo wengi wameaminishwa ya kwamba haya madhihirisho ya
mwili ni kazi za Shetani. Jambo ambalo Kanisa linapaswa kujua ni
kwamba, katika hali kama hizi, maombezi ya ‘ukombozi’ sio jawabu.
Maisha yetu yanapooana na mfano wa Yesu Kristo, na tunapouchukua
Msalaba wetu kila siku, na kuifisha miili yetu na kumfuata yeye, suala
la ‘kupagawa pepo’ halitakuwa tatizo maishani mwetu, au kwa Kanisa.
Ulimwengu wa roho upo na unaweza kuwa na nguvu kuliko
tunavyofikiri. Ndio maana Mungu anapogusa maisha yetu tunaweza
kubadilishwa mara moja. Kwa msingi huo huo kuna watu ambao
maisha yao yameathiriwa na mapepo pamoja na roho za kishetani.
Katika vitabu vya injili, Yesu mwenyewe alitoa pepo na kuwaweka watu
huru. Ukweli kwamba watu wanapagawa mapepo upo na hauwezi
kupingwa. Hata hivyo, katika Mathayo 12, Yesu anapozungumza
juu ya kutoa pepo, alizungumza kabla ya Msalaba na alikuwa
akizungumzia kizazi kikaidi, sio Kanisa. Kwa hivyo, swali langu ni hili:
Wakristo waliozaliwa mara ya pili, waliotubu dhambi zao za kale, na
kuyasalimisha maisha yao kwa Yesu, je! bado wanahitaji kufunguliwa
kutoka katika nguvu za mapepo?
Kuzaliwa Mara Ya Pili Au Kutokuzaliwa Kabisa
Sijaona mahali popote kwenye Biblia Wakristo katika Kanisa la
mwanzo wakitolewa mapepo. Ama umezaliwa mara ya pili au la;
17
Sura ya II - Je, Wakristo Wanaweza Kupagawa Mapepo?
Kanisa Linahitaji Kujua
hakuna zaidi! Kabla ya kumjua Yesu tulikuwa chini ya mamlaka
ya Shetani. Hatukumjua Mungu; na sisi sote pia tulikuwa chini ya
ushawishi wa roho za kishetani au tulitawaliwa nazo (Waefeso 2:1-5).
Mtu asiyeamini anapotubu dhambi zake na kuamini katika dhabihu
ya Yesu msalabani, Mwenyezi Mungu mwenyewe huja na kuishi
moyoni mwake. Wakolosai 1:13 inaelezea hivi: “Naye alituokoa katika
nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana
wa pendo lake.” Baada ya sisi kuzaliwa upya na Roho Mtakatifu, asili
ya Mungu inachukua nafasi ya asili ya dhambi iliyotutawala mioyoni
mwetu hapo kabla.
Mara nyingi sio lazima hata kuomba ili mtu afunguliwe. Yule
asiyeamini tayari yuko chini ya hukumu kubwa sana na yuko tayari
kuyasalimisha maisha yake kwa Kristo, kiasi kwamba anawekwa
huru kwa wepesi sana kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Mara nyingine
anahitajika kufanyiwa maombi ili afunguliwe. Kutokana na hayo
unaweza ukauliza je, maana yake nini haya madhihirisho ya nguvu
za giza leo hii makanisani? Jawabu ni kwamba watu wengi huja tu
kwa ajili ya kupokea uponyaji na kufunguliwa kutokana na nguvu za
giza, kubarikiwa, na si kumtafuta Mungu kwanza. Na kwa sababu
hawajazaliwa mara ya pili, nguvu za giza huendelea kuyatawala
maisha yao. Lakini haiwezekani kwa Wakristo waliozaliwa mara ya
pili kuendelea kuwa chini ya nguvu za mapepo, isipokuwa wamerudi
nyuma hadi kuvunja kabisa uhusiano wao na Kristo, wamemkataa
Bwana na kuzifungulia mlango kazi za mapepo mioyoni mwao na
18
maishani mwao. Kwa sababu, inawezekanaje Roho Mtakatifu kuishi
kwenye mwili mmoja na pepo?
Shida nyingi na mambo mengi yanayohusishwa na mapepo yana
mizizi yake kwingineko. Kama hatupo kwenye msingi wa Msalaba
tunajikuta tukipokea kila aina ya mafundisho ya uongo na imani za
kigeni. Kwa kila jambo linaloharibika tunatupia pepo lawama.
Ni Mwili!
Ni lazima ieleweke kwamba ikiwa mimi kama Mkristo nina shida na
mwili wangu, haina maana kwamba kuna pepo ndani yangu… ila ni
kwamba tu nimeziruhusu tamaa za mwili wangu zinitawale.
Ni kweli twaweza kujaribiwa, lakini ni lazima tutofautishe kati ya
kujaribiwa na kumilikiwa na roho chafu. Ni pale tu nitakapojikana
nafsi yangu, kuwa tayari kuziachilia haki zangu na kuyapoteza maisha
yangu kwa kuuchukua msalaba wangu, ndipo nitakapopata ushindi
katika eneo husika. Sihitaji kabisa kukemewa pepo yeyote atoke,
maana tayari niko huru na mapepo!
19
Sura ya II - Je, Wakristo Wanaweza Kupagawa Mapepo?
Kanisa Linahitaji Kujua
Maombi ya Kufunguliwa Sio Jawabu
Mungu ametufungulia njia ya kutokushindwa na miili yetu, au
kuzisikiliza tamaa zake. Ni Msalaba. Ndio maana maisha yetu
hayana uhusiano wowote na mapepo. Roho wa Mungu anaishi ndani
yetu. Yeye anatuombea na kutuwezesha, kwa neema ya Mungu,
kuusulubisha huu mwili. Kile Mungu anachotaka kufanya maishani
mwako kwa njia ya utakaso hakiwezi kupatikana kupitia maombezi
ya kutoa pepo.
Usimruhusu mtu yeyote ajaribu kukemea ndani yako pepo wa hasira,
uvivu, wivu na kadhalika. Vivyo hivyo huwezi kutatua tofauti zilizopo
kati yako na mwenzi wako, watoto wako au Mkristo mwenzako kwa
kukemewa pepo... Haya ni madhihirisho ya mwili wako, matokeo ya
maisha ambayo hayajasalimishwa kwa Bwana. Wakristo wengi leo
wamekata tamaa kwa sababu wanafahamu ni aina gani ya watu
wanaopaswa kuwa, lakini wanapoitazama hali halisi ya maisha yao,
wanahisi tu kushindwa na kukata tamaa. Hivyo wanakimbilia kwenye
kutolewa pepo. Ushindi upo katika Msalaba. Hebu kuwa na utayari
wa kuyapoteza maisha yako na utaona matokeo yake... Tunaweza
kuwa dhaifu katika maeneo mengi, lakini bado tukaudhihirisha uzima
wa Kristo. Tumewekwa huru mbali na mapepo na tunaitembelea
hiyo njia ya kuuelekea ukamilifu; Bwana apewe sifa! Kwa maelezo
kuhusiana na kazi za mwili, angalia orodha iliyoko Wagalatia 5:19-21.
Na hebu nikuambie, huhitaji kutolewa pepo ili uweze kutembea katika
ushindi dhidi ya mambo haya. Chukua tu msalaba wako.
20
Kujifananisha Na Kristo
Ni muhimu tuweze kuelewa kusudi la ujumbe wa Msalaba kwa
maisha yetu. Ni lazima tuwe tayari kujifananisha na mauti ya Kristo
ili tuweze kuubeba uzima wake na kuwa huru. Mara tu tunapouweka
msalaba kando, tunatafuta njia za mkato, au jambo mbadala kama vile
kukemewa pepo, yaani, aina ya Ukristo wa kubonyeza kitufe. Lakini
katika Wagalatia 2:20, maneno ya Paulo, “Nimesulibiwa pamoja na
Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu;
na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa
Mungu…” ni tamko la ajabu linalodhihirisha aina ya maisha aliyoishi.
Kupitia ufunuo alioupokea, Paulo alijifunza ya kwamba alihitajika
ayafananishe maisha yake na maisha ya Kristo, ajikane nafsi yake,
ausulubishe mwili wake. Aliuishi huo ufunuo na akaweza kuuhubiri;
maisha yake yalikuwa ni ushuhuda wa mabadiliko yanayoletwa na
kazi ya Msalaba. Ujumbe wa Msalaba ni onyo la mara kwa mara na
kumbukumbu inayoufunua udhaifu wa miili yetu, na kutuwezesha
kuona hali halisi ya maisha yetu. Inatuleta kwenye toba, kujikana nafsi
na kurejea Msalabani.
21
Sura ya II - Je, Wakristo Wanaweza Kupagawa Mapepo?
Kanisa Linahitaji Kujua
Huru Kweli Kweli!
Kwa hivyo, ndugu au dada mpendwa, ikiwa kutoka katika vina vya
moyo wako umeyasalimisha maisha yako kwa Kristo, tofautisha kati
ya udhaifu wa mwili wako na kupagawa mapepo. Unaweza ukawa
ni Mkristo dhaifu, ila tambua umewekwa huru mbali na mapepo.
Haleluya! Ndio sababu Mtume Paulo alinena sana juu ya hatari za
mwili. Alifahamu fika udhaifu wa mwili. Kumbuka, “Mwana akiwaweka
huru, mtakuwa huru kweli kweli!”
22
23
Sura ya III
Mkristo na Pesa
Kanisa Linahitaji Kujua
24
Kama kuna eneo ambalo Wakristo leo hii wamelaghaiwa na
kufundishwa mafundisho yenye udanganyifu, hakika ni katika eneo
la fedha na utoaji. Ni aibu kubwa kwa Kanisa kuona wachungaji
wengi wakilikosesha kundi la Mungu kwa kuwapa ahadi za uongo
za mafanikio na baraka; wakiwapotosha kwa kutumia sheria
zinazowashurutisha kutoa.
Mara nyingi nimelishutumu fundisho la mafanikio lililolivamia Kanisa,
kwenye nchi tajiri na nchi maskini. Jumbe zangu zimeelezewa kuwa
zenye utata kwa sababu nimepinga kuhubiriwa fundisho hili la uongo.
Sina tatizo kabisa Wakristo wanapotajirika kwa mali za ulimwengu
huu, na wanapobarikiwa. Lakini ninapingana vikali na mafundisho
ya kwamba ni mapenzi ya Mungu ya kuwa Wakristo wote wameitwa
kuwa matajiri. Hili linapatikana wapi kwenye Biblia? Hata Kanisa la
Mwanzo lilikuwa na Wakristo maskini. Kwa hivyo, ninaamini ni uzushi
kuwaaminisha Wakristo wote ya kwamba ni mapenzi ya Mungu wote
wawe matajiri, wote wamiliki majumba makubwa, magari ya kifahari,
n.k., au ya kwamba wanapoendelea kubaki maskini ni kwa sababu
hawana imani… uzushi kabisa! Katika maeneo kama Afrika na India,
Wakristo wengi wanaishi katika umaskini wa kutisha. Hakuna aibu
katika hilo, na haimaanishi hawana imani. Zaidi ya hilo, katika mahubiri
mengi ya siku hizi, pesa inapewa umuhimu kupita kiasi!
25
Si kwamba ninalishambulia fundisho la mafanikio, lakini ninaamini
tunahitajika tuangalie Neno la Mungu kuhusu hili suala katika mtazamo
sahihi – katika kuutafuta moyo wa Mungu kwa hili. Kinachonisikitisha
zaidi ni kwamba waumini katika makanisa ambapo injili ya jinsi hii
inahubiriwa, na ambao wengi wao ni maskini, hawafiki mahali pa
kuelewa ya kwamba Mungu ana haja na aina ya moyo tulionao katika
kumtolea. Mungu humpenda mtu anayetoa kwa moyo mkunjufu, si
mtoaji tajiri!
Katika makanisa mengi sana, linapokuja suala la utoaji, watu wanaleta
sadaka zao wakitaraji kurudishiwa kwa wingi ‘walichopanda’, au
kutokana na shinikizo na hofu ya kuonekana wanaenda kinyume na
‘kile Biblia inachosema’! Ila, tunapolitazama Neno la Mungu, je! ni
wapi tunapomuona Yesu au Mitume wakizungumzia mafanikio kwa
mtazamo wa jinsi hii? Jambo lililo wazi ni kwamba Mungu ameahidi
kuyashughulikia maisha yetu (Mathayo 6:25-26); ni udhihirisho wa
moyo wa Mungu kwa watu wake na maono yake kwa ajili ya Ufalme.
Biblia sio kitabu chenye mbinu na kanuni kwa wahubiri kutumia ili
kuwaomba ninyi muwape pesa ili Mungu aweze kuwabariki.
Sura ya III - Mkristo na Pesa
Kanisa Linahitaji Kujua
26
Kumpenda Yesu, Kuupenda Ufalme Wake
Mpango wa Mungu kwa Kanisa lake ni kwamba Wakristo wabebe
moyo wake uwe ushuhuda kwa ulimwengu usioamini. Kwa Mkristo
mwenye shukrani anayejua kuwa Yesu alitoa kila kitu kwa ajili yake,
ambaye moyo wake unamilikiwa na Mungu na ambaye maisha yake
yamebadilishwa na Kristo, kutamani kumtolea Mungu ni asili yake.
Si mtu anayeleta matoleo yake kwa sababu analazimika kufanya
hivyo, au kwa sababu mtu fulani amemwambia atoe kiasi fulani, au
kwa kuwa amefundishwa jinsi ya kumtolea Mungu. Na hakika hatoi
ili abarikiwe. Anatoa kwa sababu anampenda Yesu na Ufalme wa
Mungu; ana shukrani kwa ajili ya wokovu.
Maisha yake yamefananishwa kikamilifu na ya Kristo, na moyo
wake umetolewa kikamilifu katika kuyatumikia maono ya Mungu
kwa Kanisa lake. Hapa yupo mtu mwenye uwezo wa kutoa vyote,
juu sana kuliko asilimia yoyote iliyopangwa au kiwango chochote
kilichowekwa. Yeye hupanda kwa furaha katika Ufalme wa Mungu
kwa kadiri anavyoongozwa na Roho Mtakatifu. Mkristo wa aina hii
anaweza kutoa kwa ukarimu hata katika nyakati za uhitaji mkubwa,
kama tunavyoona Kanisa la Makedonia likifanya katika 2 Wakorintho
8. Anatenda huku akiamini ya kuwa Mungu atashughulikia mahitaji
yake binafsi, kwa sababu anajua moyo wake ni kwa ajili ya Ufalme.
27
Mungu Anataka Tufanikiwe
Kuna vifungu viwili vya Maandiko ambavyo karibu kila Mkristo
anavijua; kwani, katika nyakati fulani, wengi wetu huenda tumesikia
vikifundishwa kuhusiana na utoaji na mafanikio. Katika maeneo
yote mawili, mafundisho ya uongo yamepenyezwa Kanisani ikiwa ni
matokeo ya wahubiri kuichukua mistari hii kwa maana nyingine…
Katika 3 Yohana 1-8 tunasoma, “Mpenzi, naomba ufanikiwe katika
mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.”
Sote tunafahamu kuwa Mtume Yohana anamsifu Gayo kwa moyo,
upendo, jinsi anavyoujali Ufalme, na ukarimu wake kwa watu wa
Mungu. Je, si ni jambo la kawaida kabisa kwa Yohana kumtaka
Mungu ambariki mtu wa jinsi hii?
Mtume anataka Gayo afanikiwe katika mambo yake yote, kwa sababu
anajua chochote anachopewa na Bwana kitatumika kuwabariki ndugu
wengine na kitakuwa na manufaa katika Ufalme. Sasa, tunarukaje
kutoka kwenye kweli hii hadi kutangaza kuwa ni mapenzi ya Mungu -
ni kusudi lake na mpango wake - kwamba Wakristo wote wafanikiwe
kifedha; kwamba Wakristo wote wanapaswa watarajie kupokea
mara mia kama malipo, endapo watatoa kwa ajili ya mhubiri huyu au
mradi ule? Hili ni kinyume na Maandiko! Tunachoweza kusema bila
shaka yo yote ni kwamba Mungu angependa kumbariki kila Mkristo,
ambaye, kama Gayo, ana moyo kwa ajili ya Ufalme, na ni mkarimu
kwa watu wa Mungu.
Sura ya III - Mkristo na Pesa
Kanisa Linahitaji Kujua
28
Maono Ya Agano Jipya
Tunaposoma maneno ya Yesu katika Luka 6, tunaona roho ile ile na
moyo ule ule aliokuwa nao Yohana na mitume wengine wote. Hapa
(mistari 27-46) Yesu anazungumza na makutano kuhusu kuwa na
moyo mwingine na maono mengine... moyo na maono ya Ufalme.
Anawasihi watu kutoa maisha yao na kumruhusu Mungu awabadilishe
ili waishi sawasawa na Agano Jipya.
Kwamba, katika mtazamo huu anasema katika msitari wa 38: “Wapeni
watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na
kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani
mwenu.Kwakuwakipimokilekilempimachondichomtakachopimiwa”,
si sababu ya mtu kutafsiri kuwa alikuwa akizungumzia utoaji na
mafanikio. Hiki kifungu kinahusu aina ya moyo anaopaswa kuwa nao
Mkristo ambaye daima anashughulishwa na Ufalme wa Mungu. Kwa
msingi huo Yesu anamalizia, katika msitari wa 46 kwa kusema, “Na
kwa nini mnaniita Bwana, Bwana, walakini hamyatendi nisemayo?”
Kwa hiyo, hapaswi mtu yeyote kutumia andiko hilo kushawishi watu
ya kuwa wakitoa, bila kujali hali za mioyo yao au nia wanayotoa nayo,
ya kwamba Mungu bado anawajibika kuwabariki. Hii ndiyo maana leo
hii kuna mamilioni ya Wakristo ambao bado wanasubiri baraka zao!
29
Kwa Kadri Ya Uhuru Wa Moyo Wako
Niruhusu niseme ya kwamba ikiwa bado unaamini kuwa unalazimika
kumtolea Mungu, hujaelewa undani wa kile ambacho Yesu Kristo
alifanya pale msalabani; ukombozi aliotupatia Mwana wa Mungu.
Ametuweka huru. Leo hii tuko huru kutoa kutoka katika ndani ya
mioyo yetu, kwa kadiri tunavyoongozwa na Roho Mtakatifu.
Je, unafahamu ya kuwa kama nitamtegemea mtu au sheria yoyote
katika Agano la Kale iliyo chini ya ukuhani wa ki-Lawi kuniambia ni
kiasi gani ninachotakiwa kutoa, ninaweza nikajikuta nikitoa chini zaidi
ya kiwango nilichodhamiria moyoni kutoa? Sasa katika mtazamo
halisi tunaona moyo wa Mkristo wa Agano Jipya katika tamko la
Mtume Paulo katika 2 Wakorintho 9:7 “Kila mtu na atende kama
alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima;
maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.” Hapa
hatuoni Mkristo mwenye hofu, na mnyimivu, anayelazimika kutoa
kwa sababu anawajibika kutoa, au kwa sababu kila mtu atafahamu
kiasi alichotoa.
Kutumika Katika Uhuru
Makanisa ya Makedonia yalikuwa na uwezo wa kutoa licha ya
umaskini wao mkubwa, ikiwa ni matokeo ya Injili iliyowafanya kukubali
Sura ya III - Mkristo na Pesa
Kanisa Linahitaji Kujua
30
kupoteza maisha yao, kujikana nafsi zao, kuuchukua msalaba kila
siku na kumfuata Yesu. Ukarimu wao ulikuwa ni matunda ya kazi ya
injili, si matokeo ya kulaghaiwa kihisia. Walitamani kutoa kutoka katika
vina vya mioyo yao, na wakasisitiza kutaka kushiriki katika mradi wa
kiroho na wenye manufaa kwa Ufalme na kwa watakatifu wengine.
Tafadhali elewa kuwa sitaki kukufanya uangalie nyuma na uanze
kuhoji ni kwa jinsi gani au ni kwa lipi ulilotolea pesa zako huko nyuma.
Lakini ninaamini kuna Wakristo wengi wanaotafuta kuujua ukweli.
Nami ninachotaka ni kwa Kanisa kuujua moyo wa Mungu kwenye
suala la pesa; fundisho la kweli ni lipi kulingana na Neno lake ili, kwa
neema yake na kwa kuongozwa na Roho wake Mtakatifu, tuweze
kuwa huru kumtumikia Mungu kwa pesa zetu.
31
Sura ya IV
Mungu na Muziki
Kanisa Linahitaji Kujua
32
Sitakuwa ninatia chumvi nikisema ya kwamba uzi unaotenganisha
muziki wa kidunia na kile kinachoitwa ‘Muziki wa Kikristo wa Kizazi
Kipya’, ni mwembamba kwelikweli. Inasikitisha, lakini uimbaji mwingi
tunaousikia Kanisani siku hizi ni muziki wa kidunia wenye maneno
ya Kikristo.
Kwa kadiri roho wa dunia hii inavyozidi kujipenyeza Kanisani, si ajabu
kuuona muziki wake pia ukiingia Kanisani. Tunapotazama muziki na
uimbaji wa ‘Kikristo’ ulioko sasa hivi, tunapata kuona ni kwa kiasi gani
roho ya ulimwengu ilivyolivamia Kanisa. Kwa kadiri uimbaji Kanisani
unavyozidi kuchukua sura ya kidunia tunaona jinsi hili linavyoleta
kuchanganyikiwa na kumenyana, hasa kwa vijana.
Swali ninalotaka kuuliza ni: ‘Je, kuabudu halisi kuna uhusiano gani na
muziki wa kidunia?’ Ninashindwa kuelewa ni kwa nini tutake na hata
tujaribu kuyachanganya, haya mawili – kumsifu Bwana kwa mdundo
wa kidunia… kwa kweli, haiwezekani! Tunapokuwa tumezaliwa mara
ya pili, tunapaswa tutamani kuabudu kwa mioyo yetu, katika Roho na
Kweli. Jambo lolote nje ya hilo ni kuuburudisha mwili.
Kwa mara nyingine tena, ninaamini ya kwamba katika kuliangalia Neno
la Mungu tutapata ufahamu na ufunuo mpya juu ya moyo wa Mungu
katika suala la sifa na kuabudu. Hebu tuwe makini tusikaribishe kila kitu
kinachobeba nembo ‘Kristo’ ya kwamba kinampatia Mungu utukufu.
Hakuna maelekezo ya wazi katika Biblia kuhusu namna tunavyo-
paswa kumuabudu Mungu. Katika Agano la Kale kuna maagizo
33
yanayohusiana na muziki, kuabudu, na vyombo vya muziki, pamoja
na mifano ya watu wa Mungu wakimsifu Mungu kwa shangwe na
kucheza; lakini katika Kanisa la Agano Jipya hakuna maelekezo juu
ya aina ya maneno, mapigo, au midundo tunayoweza kutumia; au
hata namna ya kucheza. Kuna sababu nzuri juu ya hili... kumbuka
kuwa sisi ni watu wa Agano Jipya! Kwamba ni weusi au weupe, tajiri
au maskini, wasomi au wasio wasomi, sote tuna vitu viwili vinavyof-
anana: mioyo yetu na Roho Mtakatifu aliyeko ndani yetu. Yeye ni
mwalimu wetu, anatuongoza na kutushuhudia mioyoni mwetu juu ya
nini kinachotokana na Mungu Baba na nini kisichokuwa cha Mungu.
Roho Mtakatifu Ni Mwangalizi Wetu
Katika Yohana 16:13-14, tunasoma, “Lakini yeye atakapokuja, huyo
Roho wa kweli atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana
hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia
atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. Yeye
atanitukuza mimi; kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha
habari.” Hakuna kuchanganya hapa: Ni wazi kwamba Roho Mtakatifu
ndiye anayetuelekeza, kutufundisha na kutuongoza katika namna
Yesu anavyonena na namna anavyotenda. Sote tutakubaliana kuwa
kulikuwa na harufu nzuri ya manukato katika yote Yesu aliyosema na
kufanya. Vivyo hivyo, harufu ya manukato ya kumjua Kristo inapaswa
iambatane na yote tunayosema na kufanya. Cho chote kinachotokana
Sura ya IV - Mungu na Muziki
Kanisa Linahitaji Kujua
34
na dunia kina roho nyingine; lakini kwa sababu Mungu ametupa sisi
(Wakristo tuliozaliwa mara ya pili) Roho Mtakatifu kuishi ndani ya
mioyo yetu, tunaweza kupambanua roho ya ulimwengu huu ulioko
chini ya milki ya Shetani.
Mambo Ya Ajabu Yanafanyika
Ninaamini watu wanaelewa ya kuwa hata katika Ukristo kuna mambo
ya misisimko na ya kimwili yanayoendelea. Kwa bahati mbaya si kila
kitu chenye nembo ya ‘Ukristo’ ni kizuri kwa moyo wako au roho
yako. Kama ilivyo kwamba kuna aina ya uimbaji na muziki ambavyo
tunashuhudiwa mioyoni mwetu ya kuwa vinatokana na Bwana, vivyo
hivyo kuna aina ya muziki, uimbaji na kucheza ambavyo vinatoa
harufu kali ya kidunia na ya mwili. Tuwe makini tusibebe Neno la
Mungu katika hali ya maandiko tu. Neno linaposema ‘Msifuni Bwana
kwa vinanda’ au ‘Msifuni kwa kucheza na shangwe’, haina maana
kwamba tunaweza kuleta roho ya dunia Kanisani, kwa kucheza
kwa namna yoyote tunayojisikia, au kwa kutumia vyombo kucheza
midundo au mitindo ambayo huwezi kutofautisha na ile inayochezwa
katika kumbi za muziki.
Kwa kuangalia mifano michache tu ya kucheza na kushangilia katika
Biblia, ninaamini tunaweza kuona tofauti kati ya muziki na kuabudu
kunakompendeza Mungu kwa kuashiria kile kilichomo ndani ya
35
mioyo yetu, na muziki unaotumbuiza tu na kulisha miili yetu, ambao
mwisho wake ni kutupeleka katika kutenda dhambi. Katika Kitabu cha
2 Samweli 6:12-15, kuhusiana na wakati ambapo Daudi aliporejesha
sanduku la agano, lililowakilisha uwepo wa Mungu katika Yerusalemu,
mistari ya 14-15 inaeleza, “Daudi akacheza mbele za BWANA kwa
nguvu zake zote; na Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani. Basi
Daudi na nyumba yote ya Israeli wakalileta sanduku la BWANA kwa
shangwe, na kwa sauti ya tarumbeta.” Daudi pamoja na watu wa
Israeli walikuwa wanasherehekea ushindi mkubwa. Kicho chake
kwa Mungu, unyenyekevu wake, pamoja na furaha ya kweli vilizidi
sana ndani yake kiasi cha kumfanya acheze, licha ya kuwa tendo
lile lilionekana kama la kipuuzi mbele ya mke wake. Watu walifurahia
kile ambacho Mungu alikuwa amefanya, walijua hii haikuwa kazi ya
mwanadamu. Daudi alipomuua Goliathi, watu wale wale waliokuwa
wakitetemeka kwa hofu ghafla walijawa ujasiri wakatoka kwenda
kuwashambulia Wafilisti. Baada ya kuwa wametoka kwenye vita
kama hiyo, tunasoma katika 1 Samweli 18:6-7 kwamba, “wanawake
wakatoka katika miji yote ya Israeli, kwa kuimba na kucheza, ili kumlaki
Mfalme Sauli; wakatoka na matari, na shangwe, na vinanda. Nao
wanawake wakaitikiana wakicheza.” Katika Agano Jipya (Matendo
ya Mitume 3) Petro na Yohana walienda hekaluni siku moja, na mtu
mmoja aliyekuwa kiwete tangu kuzaliwa akaponywa. Mtu huyu
alishangilia kwa furaha kuu na kucheza ndani ya hekalu akimsifu
Mungu kwa muujiza wake. Hakuweza kujizuia katika furaha yake.
Sura ya IV - Mungu na Muziki
Kanisa Linahitaji Kujua
36
Shangwe Itokayo Moyoni
Katika mifano yote mitatu, tunaona mlipuko wa shukrani na shangwe,
vilivyotokana na moyo wa shukrani uliosababisha kuimba, kucheza
na muziki. Ni suala la Mungu, wala si muziki. Tunaponyenyekezwa
na kile ambacho Mungu ametufanyia, tuko huru kufurahia kwa
kadiri mioyo yetu itakavyotuongoza. Hakuna tatizo juu ya kuimba na
kucheza katika mazingira kama hayo.
Lakini viongozi wa sifa wanapoamua Jumapili asubuhi kwamba
‘sasa’ ni wakati wa kuanza kumsifu Bwana kwa kucheza, au kuabudu
kwa kushawishi hisia za watu, kwa uimbaji ambao si kingine bali
ni maneno ya Kikristo yaliyoambatana na midundo ya kidunia na
yanayotupelekea katika kuigiza, ni lazima tuanze kujiuliza maswali.
Na ni vivyo hivyo kwa ‘Matamasha ya Injili’.
Je, ni nini kinachotokea kwa hawa vijana wa kike na wa kiume ambao
hisia zao na miili yao inakuwa imeamshwa kwa hali ya juu na waimbaji
walioko jukwaani? Yesu anapewaje heshima na utukufu katika
mazingira haya? Wengine wanaweza kusema hiyo ndiyo namna
vijana wa kisasa wanavyoabudu na ni njia ya kuwavuta marafiki zao
kuja kusikiliza habari za Bwana Yesu. Lakini mimi naweza kuuliza
je! ni wangapi katika hawa marafiki wanaofikia kwenye kuzaliwa
mara ya pili kwenye haya matamasha? Na, cha muhimu zaidi, je! ni
idadi gani ya hawa Wakristo vijana wanaojikuta sasa wakiwa katika
barabara ya kurudi nyuma kiroho ikiwa ni matokeo ya kuwasha tamaa
37
za miili yao kupitia haya matamasha? Mimi binafsi ninapoyasikiliza
au kuyatazama matamasha kama haya, Roho Mtakatifu hushuhudia
ndani yangu kuwa kuna kitu hakiko sawa. Na sote tunajua ni nani
na ni nini kilichoko nyuma ya kila kitu ambacho hakitokani na Roho!
Hatuwezi kujificha nyuma ya ‘muziki wa injili’ unaofurahisha hisia zetu
na kuamsha miili yetu. Mwili hauwezi kutoa uzima wa rohoni, kwa
hiyo, mara tu mwili unaposisimkia aina fulani ya muziki tuko hatarini.
Sisi kama watu wa rohoni ni lazima tuweze kupambanua kati ya
muziki utokanao na Mungu - ibada ya moyoni inayojenga - na muziki
wa kidunia unaoamsha tu miili na hisia zetu.
Muziki Una Vyanzo Viwili
Kama tunavyojua, muziki unatokana na mmojawapo ya vyanzo viwili
tu. Chanzo cha kwanza ni katika moyo wa Mungu - ambapo wanaume
na wanawake, mara nyingi kutokana na kazi ya Mungu waliyoishuhudia
maishani mwao, huongozwa na Roho Mtakatifu kutunga sauti au
kuandika wimbo. Nyingi za tenzi kuu za Kikristo tulizonazo leo hii
zinalishuhudia hili. Mungu ndiye anayeumba huu muziki moyoni mwa
mwanadamu ili amwabudu na kumsifu Yeye, kumpa utukufu wote,
heshima na uweza. Upako wa Mungu unapokuwepo, mioyo yetu
inayeyuka na tunamezwa katika uwepo wake. Chanzo cha pili cha
muziki ni roho inayoutawala ulimwengu - ambapo midundo, vionjo na
miondoko ni ya kimwili na ya kidunia.
Sura ya IV - Mungu na Muziki
Kanisa Linahitaji Kujua
38
Muziki ni eneo lingine la hatari sana kwa Kanisa tunapouweka
kando msingi, yaani, Injili ya Msalaba, ambayo mara zote inatupa
changamoto na kutuleta kwenye utu uzima. Tukikaa kwenye huo
msingi, kwa kadiri tunavyozidi kukua na kufanana zaidi na Kristo,
tutafahamu pasipo na shaka yo yote ni lipi tufanye, wapi pa kwenda,
na kipi cha kusikiliza. Na tutajikuta hatuvutiwi tena na muziki ambao
hauifaidi roho kwa namna yoyote.
Ninataraji ya kuwa maneno haya machache yameleta mwanga na
ufafanuzi zaidi kuhusiana na somo hili; ya kwamba kwa namna fulani
Mungu ameyafungua macho yako na umetiwa moyo
39
Sura ya V
Vita ya Rohoni
Kanisa Linahitaji Kujua
40
Fundisho lingine ambalo limejipenyeza Kanisani ni lile la ‘vita vya
kiroho’. Wakristo kila mahali wanatilia mkazo katika kutoa pepo na
kudhibiti roho chafu kila mahali wanakokwenda. Ikiwa tunataka kuishi
sawasawa na fundisho la uzima la Kristo, tunapaswa tuyachunguze
Maandiko tuone ni nini kilichomo moyoni mwa Mungu, na katika
mioyo ya Mitume walioandika Nyaraka.
Leo hii katika mengi ya makanisa, kuna lugha nyingi na shughuli nyingi
linapokuja suala la vita ya rohoni, na kifungu cha Biblia kinachotumika
katika hili suala ni Waefeso 6. Hata hivyo, ninapokitazama hiki kifungu,
sioni jambo lolote linazungumzia kuanzisha mapambano dhidi ya
roho wachafu. Ninachoona ni wito halisi wa Mungu juu ya maisha
ya muumini. Mtume Paulo anatuhimiza tujitie nguvu katika Bwana,
ili tuweze kusimama siku ya uovu. Mahali pengine, Mtume Yakobo
anatuagiza ya kwamba adui ashambuliapo: “Mpingeni Shetani naye
atawakimbia.”
Sehemu kubwa ya kile Kanisa linachokiita ‘vita vya kiroho’ si kingine
zaidi ya kupigana na mapepo. Wakristo wanaona hiyo kuwa ndiyo njia
ya kupata ushindi maishani mwao. Lakini, Biblia inasema waziwazi
ya kuwa ikiwa tuko ndani ya Kristo, Shetani hawezi kutugusa. Ikiwa
maisha yetu yako sawa mbele za Mungu , na mioyo yetu ni safi, ni
kwa nini tuyaogope mapepo? Tunapaswa tu kuyapinga. Tumeitwa
tuishi maisha yenye ushindi, na tutaupata huo ushindi na kupinga
mashambulizi ya Shetani tutakapoyafuata maagizo ya Yesu katika
Mathayo 16:24: “Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe,
ajitwike msalaba wake, anifuate.”
41
TunapoyaangaliaMaandikokatikamtazamosahihi,nakupataufahamu
sahihi wa kile kilichofanyika Msalabani, tutaanza kuona nafasi yetu
na msimamo wetu katika Kristo na katika Neno lake. Ninaamini wale
wanaojishughulisha na ‘vita vya kiroho’ wanapaswa wajiulize maswali
matatu… “Vita vya kiroho ni nini hasa?” “Hili limetajwa wapi kwenye
Agano Jipya?” Na, “Je, dhabihu ya Yesu Msalabani haikutosha?”
Katika Waefeso 6, ninaamini Mtume Paulo anazungumzia maisha
ya ushindi pamoja na Bwana, maisha yenye ushindi katika haki na
maisha matakatifu yanayompendeza Mungu. Kwa namna fulani, hii
mistari imetafsiriwa kwa namna isiyo sahihi kuleta maana ya kwamba
vita ya rohoni ni sehemu ya wito wetu. Leo hii, Kanisani kumeingia
uelewa fulani ya kwamba, ikiwa tunataka ushindi, tunahitajika muda
wote kuwa vitani tukipigana na mapepo, roho chafu, na kila nguvu na
mamlaka; kufunga na kufungua roho kila tupatapo nafasi kwa sababu
wametuzunguka kila mahali.
Hebu tuangalie mistari ya 10-11: “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika
Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu,
mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana
kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka,
n.k...” Kusudi la hili andiko sio kutufundisha jinsi ya kupigana vita
ya rohoni. Wito uliopo hapa ni kwamba tuimarike, kwa sababu
adui atashambulia! Paulo anasema, ‘Muimarike katika Kristo kwa
sababu siku ya uovu imewadia.’ Mtume anaelewa fika ya kuwa vita
au mapambano yo yote maishani mwetu hakika ni ya rohoni, na
Sura ya V - Vita ya Rohoni
Kanisa Linahitaji Kujua
42
wala si kitu cha kimwili au cha asili. Anatuonya mapema ya kwamba
tunapaswa kuwa hodari katika Bwana. Kwa maana nyingine, ikiwa tu
imara rohoni hatutashindwa na hila za adui.
Ufunguo wa hili ni shauku yetu ya kutaka kukua, na utayari wa
kuyasalimisha maisha yetu kikamilifu kwa Kristo. Hapo Bwana atatupa
neema ya kusimama, hata kama tu wachanga kiroho, tunapozidi
kumpinga Shetani. Mungu hatamruhusu adui avuke mpaka kwani
yeye ndiye mlinzi wetu; yeye ni ngao na mwokozi wetu. Shauku kuu
ya Paulo ni kwamba tumtumikie Bwana katika hali zote na ya kwamba
adui ashambuliapo, tuwe hodari katika imani ili tuweze kusimama
imara na kuupata ushindi.
Kumtii Mungu
Mtume Yakobo anasema katika waraka wake (4:7-8): “Basi mtiini
Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu,
naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi...”
Roho iliyoko nyuma ya mistari hii ni sawa na ile iliyo kwenye Waefeso
6; mwito ule ule, maisha yale yale, mamlaka ile ile! Anaposema
tuyatiishe maisha yetu kwa Mungu, anamaanisha kujikana nafsi zetu,
kuuchukua msalaba wetu, na hatimaye, kumpinga Shetani.
43
Tutawezaje kubaki mwilini halafu tuende vitani dhidi ya mapepo, na
falme, na kudai na kufundisha ya kuwa tutapata ushindi dhidi yao?
Huku ni kuyatumia Maandiko kama mbinu, na inakwepa ukweli ya
kwamba Ukristo ni maisha tunayoishi katika roho.
Silaha Zote Za Mungu
Ni vigumu kumshinda Shetani ikiwa hautembei kwenye barabara ya
Msalaba na kumruhusu Mungu akutakase na ashughulike na mwili
wako. Unaweza ukanukuu kila Andiko, ukafunga kila pepo, ukakiri
kila msitari, ukachukua mamlaka dhidi ya kila jambo, na kufunga
na kufungua kwa kadiri upendavyo. Ikiwa maisha yako ya rohoni
yamevurugika, na hayako juu ya msingi wa Kristo aliyesulubiwa,
adui hatakimbia utakapojaribu kumpinga; badala yake, atakuingiza
dhambini na kukushinda.
Jumbe nyingi zimehubiriwa, na vitabu vimeandikwa, juu ya ‘kuvaa
silaha zote za Mungu’. Hakika hii haiwezekani iwe ni kanuni ya kimwili;
wala haihusikani na kuyanukuu Maandiko, kufunga mapepo, n.k. Si
suala la maneno hata kidogo. Silaha yetu ya rohoni inapatikana katika
hali za mioyo yetu, maisha yetu matakatifu, na roho wa maombi.
Mamlaka yetu inapatikana katika utakatifu wa maisha yetu ya rohoni.
Ushindi unapatikana kwenye barabara ya Msalaba!
Sura ya V - Vita ya Rohoni
Kanisa Linahitaji Kujua
44
Kwa hivyo, je! ‘kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu
zake’ inamaanisha nini hasa kwa maisha yetu ya siku kwa siku?
Tukiunganisha yale wanayoyasema Paulo na Yakobo, ni kwamba ni
wakati tunapoyaweka maisha yetu katika mkono hodari wa Bwana.
Ni wakati tunapoifungua mioyo yetu kwa ajili ya kuupokea ufunuo wa
injili na kumruhusu Mungu kutenda kazi ndani yetu, inayotupeleka
kwenye maisha ya imani, haki, maombi, n.k. – kwa maana nyingine,
tunazivaa silaha zote za Mungu. Kwa jinsi hiyo tunaupata ushindi bila
kumenyana na mapepo mchana kutwa.
Na, Shetani anapokuja, tunahitajika tu kumpinga bila kufanya jambo
lingine zaidi. Huo ndio wito, ndugu na dada zangu. Si kuingia kwenye
mapambano ya kiroho dhidi ya mapepo…
Maisha yetu yanapokuwa juu ya msingi sahihi, tunakuwa na mamlaka
ya Mungu katika kumpinga Shetani. Kila anaposhambulia na sisi
kumpinga, Shetani hana budi kukimbia. Sote tunakubali ya kuwa
mapepo na roho chafu wapo, ila Yesu Kristo amewashinda wote
(Wakolosai 2:15). Ndio maana, maisha yetu yanapokuwa yametiishwa
kwa Mungu, hatutaogopa mapepo, wala kuyatafuta kila mahali.
Mamlaka Ya Mungu
Hebu sasa tuangalie Mathayo 16:18-19. Yesu anasema, “Nami
nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga
45
kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa
wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani
litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utalolifungua duniani,
litakuwa limefunguliwa mbinguni.” Bwana wetu alimpa Petro mamlaka
kuliongoza Kanisa lake. Anamwambia, ‘Lo lote utakaloamua na
kutamka duniani kulingana na mpango wangu na mapenzi yangu, kwa
manufaa ya Ufalme, nitakutetea nikiwa mbinguni na nitalifanikisha.’
Mfano wa hii mamlaka ikitenda kazi unaonekana katika Matendo 5.
Akiwa mtu wa imani na maombi, aliyeishi maisha matakatifu na ya
haki, Petro alivaa silaha za Mungu, na akaongozwa na Roho Mtakatifu
kunena sawasawa na mapenzi ya Mungu. Akafahamu kile Anania
na Safira walichokuwa wamekifanya, na akanena kwa mamlaka ya
Mungu. Alichofunga duniani kikafungwa na mbinguni. Ninamwona
Petro akitekeleza jukumu lake la uongozi, pamoja na mamlaka
aliyopewa na Bwana.
Kumpinga Shetani
Mara nyingine tunahitajika kumpinga Shetani, na kumzuia na
kumsimamisha katika kazi zake. Lakini hii haiwezi kuwa mbinu
tutakayotumia katika maisha yetu ya siku kwa siku. Paulo na Sila
walipowekwa gerezani, hawakuanzisha kipindi cha vita ya rohoni;
Biblia inasema walianza kumtukuza Mungu.
Sura ya V - Vita ya Rohoni
Kanisa Linahitaji Kujua
46
Hawakuhitaji kufunga mapepo au roho yo yote ili wafunguliwe.
Mioyo yao ilikuwa sawa, maisha yao yalikuwa kwenye utaratibu wa
roho na walimwabudu Mungu, huku wakifahamu ya kuwa ukombozi
wao ulikuwa karibu. Muda si mrefu, Mungu akalitikisa gereza na
kuwaokoa. Paulo alipofika Athene, Biblia inasema alichukizwa
na sanamu na miungu waliyoiabudu. Je, Mtume alianza kufunga
mapepo? Hapana! Alinena waziwazi, akiwaambia ya kuwa waliabudu
kila aina ya miungu, ila yeye angewaambia habari za Yule waliyepaswa
kumwabudu. Akanena habari za Mungu wake, na akawahubiria habari
za Yesu Kristo.
Tunaposoma kitabu cha Matendo ya Mitume, tunaona wanafunzi
walitumia muda wao wakiihubiri Injili. Walipokutana na mazingira
ya kuhitaji kumpinga adui, walifanya hivyo na kuendelea na kazi ya
huduma. Hebu tusitekwe akili na kutumia muda mwingi tukishughulika
na mapepo, badala ya kuiishi na kuishiriki Injili, na kumtumikia Kristo
kwa mioyo yetu yote.
47
Sura ya VI
Mahusiano Kabla ya Ndoa
Kanisa Linahitaji Kujua
48
Kama kuna eneo Kanisani leo ambapo kuna mkanganyiko mwingi,
na ambapo kuna ushahidi ya kwamba mfumo wa ulimwengu
umejipenyeza tena na kuathiri namna Wakristo wanavyofikiri na
kuenenda, ni katika mahusiano kabla ya ndoa. Ingawa hili somo
linaweza kuonekana kama linawahusu tu vijana wanaotaraji kufunga
ndoa, ukweli ni kwamba ni jambo linalohusika na Wakristo wote.
Katika hili suala, Kanisa linaonekana kuamua kuchukua mitazamo
miwili inayokinzana kabisa. Leo hii tunaona ama sheria au uhuru
usiokuwa na mipaka. Katika baadhi ya makanisa kuna sheria kuhusu
kile watu wanachoruhusiwa kufanya au kutokufanya, ilhali katika
mengine, hilo suala halizungumziwi kabisa. Hakuna mmojawapo ya
hii misimamo ulio sahihi!
Ninaamini kwa dhati ya kwamba Kanisa limeutelekeza wajibu wake
kwa kutokuchukua msimamo wa wazi wa Kibiblia kuhusu namna
Wakristo, na hasa vijana, wanavyopaswa kuishi maisha halisi ya
Ukristo, iwe ni kabla ya au baada ya kufunga ndoa. Katika kukaa kimya
na kuruhusu viwango na fikra za kidunia kuingia Kanisani, tumeacha
kuisimamia Kweli ya Injili, na tumejichanganya. Matokeo yake ni
kwamba Wakristo wanajiingiza kwenye mahusiano yasiyokuwa ya
rohoni na ambayo hayawasaidii kukua na kumtumikia Bwana katika
njia sahihi na mara nyingi yakiwapelekea katika kutenda dhambi na
kuwaondoa mbali na mpango wa Mungu kwa maisha yao.
49
Kwa ujuzi nilionao ninafahamu ya kwamba Injili inapoyakamata
maisha ya vijana, hawamenyani, au kuhisi kusukumwa au
kuchanganyikiwa juu ya kile kinachoruhusiwa katika mahusiano yao,
au ni wapi wanapaswa kuchora msitari. Kinyume chake, hawahitaji
sheria za kuwaambia ni lipi wafanye na lipi wasifanye. Wanafahamu
waziwazi mpango wa Mungu ni upi juu ya maisha yao na wanatamani
kutenda mapenzi ya Mungu, kubaki wasafi, na kuenenda katika njia
inayompendeza Mungu.
TunapoliangaliaNenolaMungukatikamtazamowake,ninashawishiwa
kufikiri ya kwamba dhana zetu kuhusu kuchumbiana, kuwa na marafiki
wa kike na marafiki wa kiume, na mahusiano kwa ujumla zitabadilika!
Ulimwenguni, mahusiano ya karibu ya kimwili kabla na nje ya ndoa
yanakubalika, na hata kushabikiwa. Vipindi vya uchumba vinahesabika
kama nyakati za wahusika hao wawili kuona kama ‘wanafaana’. Hili
mara nyingi linawapelekea katika kuwa na mahusiano ya kimwili kabla
ya ndoa.
Inasikitisha kwamba katika makanisa mengi vijana wanauiga mtindo
huu huu, na wale walio katika nafasi za mamlaka – viongozi wa kanisa,
wazazi, n.k., hawashughuliki na hili suala kwa umakini unaohitajika.
Vijana wanaachiwa kujiamulia wenyewe mipaka katika hili suala nyeti,
badala ya kupewa miongozo ya Kibiblia iliyo wazi.
Hebu tuwe wazi tokea mwanzo ya kwamba Mungu hachanganyikani;
Neno lake halijaficha jambo. Ndani mwake, tunaona maono na
Sura ya VI - Mahusiano Kabla ya Ndoa
Kanisa Linahitaji Kujua
50
mpango wake ulio dhahiri, kwa watu wake na kwa Kanisa lake. Ni
wazi kwamba hataki tujichanganye na ulimwengu na njia zake. Na
wala Mungu hataki sheria na kuhukumiana Kanisani mwake, ambavyo
havina nguvu yoyote ya kumbadilisha mtu. Anachotaka ni Wakristo
wote wahakikishiwe na Roho Mtakatifu kuhusu dhambi kupitia Injili
ya Yesu Kristo ambayo inaweka mpaka ulio wazi na kutuonyesha
tunapaswa tusimame juu ya msingi upi. Hii ndiyo maana ninaamini
tunapaswa kurejea kwenye msingi – Neno la Mungu – ili tuone Mungu
anasemaje juu ya hili suala.
Miili Yetu Ni Viungo Vya Kristo
Hebu tuangalie Mungu anavyoiona ndoa na mahusiano nje ya ndoa,
na tutafahamu ya kwamba uhusiano wowote wa kimwili nje ya ndoa,
uwe wa aina yo yote ile, unahesabika kuwa ni dhambi machoni pa
Mungu. Si suala la ‘Tuweke wapi mipaka?’ kwa sababu tukijaribu
kuweka mipaka ya aina yoyote, tutaivuka tu. Ni kama lile tangazo
la breki za magari lisemalo, “Usianzishe jambo ambalo hutaweza
kulizuilia!”
1 Wakorintho 6:15 inasema: “Je, hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo
vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya
kahaba? Hasha!” Kwa hivyo, si roho zetu tu zilizounganika na Kristo;
nafsi yetu yote ni moja naye. Mistari ya 16 – 17 inasema, “Au hamjui
51
ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana
asema, ‘Wale wawili watakuwa mwili mmoja.’ Lakini yeye aliyeungwa
na Bwana ni roho moja naye.”
Paulo hapa anasema waziwazi ya kwamba ni lile tendo la ndoa
linalowaunga watu wawili kuwa mwili mmoja, na hili linapaswa
kuchukuliwa kwa uzito. Katu hatupaswi kusahau ya kuwa roho zetu,
nafsi zetu na miili yetu imeungwa pamoja na Kristo. Siku hizi Wakristo
wengi wanafanya wanavyopenda na miili yao, pasipo kutambua
madhara ya rohoni yanayotokana na matendo yao. Kwenye kifungu
hiki Paulo anaweka utofauti kati ya dhambi ya mwili na dhambi
nyingine; katika zinaa unatenda dhambi dhidi ya mwili wako kwa
sababu unafanyika kuwa mmoja na yule mnayeunganika naye
kimwili. Uzinzi ni uhusiano wowote wa kimwili nje ya ndoa. Uongo,
wizi, hasira, n.k., ni tofauti; haya ni matunda ya tamaa zetu za kimwili.
Ikiwa Mungu aliamua kuweka utofauti kati ya dhambi ya mwili na
dhambi nyingine, tunapaswa kuwa makini sana, na kuufahamu moyo
wake katika hili suala. Msitari wa 18 unasema, “Kila dhambi aitendayo
mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda
dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.” Hatupaswi kusahau ya kuwa
miili yetu pamoja na roho zetu vimeungwa na Kristo, na tunapotenda
zinaa ni jambo zito sana machoni pa Mungu. Mistari ya 19-20
inatukumbusha ya kuwa mwili wetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, na
tunahimizwa, “mtukuzeni Mungu katika miili yenu.”
Sura ya VI - Mahusiano Kabla ya Ndoa
Kanisa Linahitaji Kujua
52
Mwili Unapaswa Kusulubiwa
Katika Wagalatia 5:24-25, Paulo anasema, “Na hao walio wa Kristo
wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.
Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.” Kila Mkristo ana uelewa
fulani wa maana ya haya Maandiko. Lakini kwa wale wanaotamani
kutembea rohoni, na walio tayari kuoa au kuolewa, yana maana zaidi
maishani mwao.
Tumeitwa kuisulubisha miili yetu na tamaa zake. Hii ndio maana
tunahitajika kuusikia ujumbe wa Msalaba kila wakati kwa sababu
unatukumbusha kujikana nafsi zetu na kuyapoteza maisha. Hakuna
nafasi ya kudanganyana, wala kujaribisha mambo… Sisi ni watu
waliochaguliwa ambao miili yetu ni mali ya Bwana Yesu Kristo.
Iweje, basi, tuwaze ya kuwa ni sahihi kwa watu wawili waliochumbiana
rasmi au vinginevyo, kufanya mambo wanayoruhusiwa kufanya tu
mume na mke, eti kwa kuwa wamefikia uamuzi wa kuwa wenza?
Uamuziwawatuwawiliwakuoanahukombeleniunapaswaumaanishe
ya kwamba wataheshiminiana kwa utimilifu mbele za Bwana. Hadi
siku ya kuoana, Bwana anawataka waishi maisha safi na matakatifu.
Vijana, sikilizeni... isipokuwa una uhakika moyoni mwako ya kuwa
uhusiano unaoingia umeanzishwa na Mungu, usithubutu kuuingia.
Ukitaka kuufahamu mpango wake kwako, na mtu aliyekuandalia
kuwa mwenza wako, fahamu ya kuwa atakufunulia.
53
Mkishafahamu ya kuwa ni mpango wa Mungu muoane, na ikiwa
mnafahamu maisha ya utakatifu mnayopaswa kuishi kabla ya harusi,
hakuna hatari. Mnaweza mkachumbiana na kutiana moyo katika
kuheshimiana, kwa sababu mmehakikishiwa mioyoni mwenu ya
kuwa mnapaswa kuishi maisha matakatifu mbele za Bwana hadi
mtakapooana. Utakuwa na kicho kitakatifu cha uwepo wa Mungu
katika maisha ya mwenza wako na kufanyika kielelezo kwa wengine.
Ndio maana unapaswa uthibitike katika kile Mungu anachosema,
ili pasiwepo na kubahatisha. Je, kuna mahusiano ya aina yoyote ya
kimwili kabla ya ndoa yanayokubalika? Hasha! Neno la Mungu liko
wazi sana juu ya suala hili.
Manukato Ya Uhusiano Safi Na Mtakatifu
Labda tayari uko katika uhusiano wa kimwili nje au kabla ya ndoa, na
Bwana anakunenea ya kwamba si sahihi. Ushauri wangu ni kwamba
utubu na ufanye uamuzi imara wa kuacha mahusiano yote ya
kimwili mara moja; na usigeuke nyuma. Si jambo ambalo linafanyika
kwa awamu, wala si jambo la kuchukulia kwa wepesi. Neema ya
Mungu ipo kukusaidia. Na ikiwa ninyi wawili mnafahamu mioyoni
mwenu ya kuwa mmeandaliwa kuoana, basi jitunzeni hadi siku hiyo,
mheshimiane kama vile ndugu wa kiume anavyomheshimu ndugu
wa kike kanisani, na katika kufanya hivyo muishi maisha matakatifu
Sura ya VI - Mahusiano Kabla ya Ndoa
Kanisa Linahitaji Kujua
54
na safi. Injili ya Msalaba wa Yesu Kristo inaleta jawabu, na kuchora
msitari ulio wazi katika kila jambo tunalokabiliana nalo maishani
mwetu. Inatusaidia kuenenda katika uhakikisho, na kwa maana
hiyo tunatembea katika ushindi. Wakristo wa kila rika, walio kwenye
ndoa na walio bado, wanahitajika wasikilize kwa umakini kile Mungu
anachosema katika Neno lake ili waweze kuishi maisha matakatifu
na kufanyika vielelezo kwa wengine. Je! si ni jambo la utukufu moyo
wako unapokushuhudia ya kuwa kuna hali ya usafi katika uhusiano
wa ndugu wanaotaraji kufunga ndoa? Hili linaleta harufu nzuri ya
manukato inayopendeza. Ni ushuhuda mkuu kiasi gani wa nguvu ya
Injili watu wawili wanapooana juu ya msingi huu!
Ninaamini huu ndio mpango wa Mungu kwa Kanisa lake na kwa
watoto wake. Hakuna haja ya kukata tamaa. Mungu yu hai; anaweza
kuleta watu wawili pamoja. Anajua ya mbeleni. Anajua kila kitu kuhusu
maisha yetu, na shauku yake ni sisi tuishi maisha safi na matakatifu.
Ndio maana ni heri kusubiri, kuliko kujaribisha mambo. Fungua moyo
wako; mwache Mungu azungumze na wewe na akushawishi. Kwa
Yesu Kristo hakuna kuchelewa. Leo inaweza ikawa siku yako ya
kumtangazia Bwana ya kuwa unaenda kuishi maisha yako ya Ukristo
kabla ya ndoa kwa kulifuata Neno lake..
55
Sura ya VII
Barabara ni Nyembamba
Kanisa Linahitaji Kujua
56
Ni kweli kwamba nimeshutumiwa mara nyingi ya kuwa ninaweka
mkazo kupita kiasi juu ya ujumbe wa Msalaba, na ya kwamba sihubiri
kingine zaidi, wakati ambapo leo hii huu ujumbe unahubiriwa kidogo
sana Kanisani. Lakini, mimi nami ningejibu hili kwa kuuliza swali: “Ni
kwa nini ujumbe wa msingi wa Yesu Kristo – kile mitume wa mwanzo
walichohubiri, na tunachosoma katika nyaraka za Paulo, Yakobo,
Yohana na Petro – ni kwa nini hicho kisihubiriwe katika kila kanisa kila
wakati?” Ujumbe wa Msalaba ndio ujumbe wa msingi wa Ukristo!
Ninaamini kwa moyo wangu wote ya kuwa kila mchungaji angepaswa
atamani kuuleta moyo wa kila Mkristo mahali ambapo ataona hitaji la
kufanyiwa kazi na Bwana moyoni mwake na maishani mwake, na pia
anamruhusu Mungu amfinyange. Kupitia hilo, huyo mtu atakua katika
sura ya Kristo na katika kuyabeba maisha ya Kristo. Hii ndio maana
kuna umuhimu kabisa wa kuuhubiri ujumbe wa Msalaba, ujumbe
wa msingi wa maisha ya Ukristo. Kutokana na kile nilichopitia mimi
mwenyewe ninaamini huwezi kuuhubiri huu ujumbe vya kutosha; kwa
sababu sisi sote kama waamini tunahitaji kukabiliwa kunakoletwa na
hii kweli, kila siku ya maisha yetu.
57
Kuna Wakristo wengi mno wanaoiacha imani yao kwa kuwa tu
hawaisikii injili sahihi. Kwa kuuangalia mfano wa Kanisa la Mwanzo
katika Neno la Mungu, tunaweza tukaona ya kwamba uwepo wa
Mitume halisi waliokuwa wakihubiri Injili ya kweli kulilifanya Kanisa
liendelee kusimama kwenye msingi sahihi na katika fundisho lenye
uzima. Yesu mwenyewe alitoa tamko lisilokuwa na shaka juu ya
maisha ya Ukristo aliponena kuhusu njia nyembamba. Ni kwa nini
ujumbe wa Msalaba hauhubiriwi Kanisani leo?
“Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni
mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa
mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo
uzimani, nao waionao ni wachache.…” Mathayo 7:13.
Maisha ambayo Yesu anazungumzia katika hiki kifungu ni maisha
ya rohoni. Wakristo wote, basi, wanapaswa wasikilize kwa umakini
mkubwa anachokisema. Bwana wetu anatuonyesha barabara
tunayopaswa kuichukua ikiwa tunataka kuukwepa ‘upotevu’ pamoja
na madhara yote ya kutokumtii. Ikiwa wewe unaamini ya kuwa
maisha ya Ukristo ni ya baraka za mwilini na mafanikio – Ukristo
usiokuwa na maumivu – basi hujayaelewa maneno ya Yesu, na
ushuhuda wa maisha yake. Kitabu cha Matendo na nyaraka za
mitume zinashuhudia Wakristo wa Kanisa la mwanzo wakipita katika
nyakati ngumu, mitihani, majaribu, mateso na adha katika barabara
hii ngumu na nyembamba.
Sura ya VII - Barabara ni Nyembamba
Kanisa Linahitaji Kujua
58
Kuteseka Kwa Ajili Ya Kukua
Ikiwa tunatamani kuyaishi maisha ya ufufuo, maisha ya Kristo, maisha
ya Roho, hatuna budi kukubali ya kwamba tumeitwa tuitembee
barabara inayojumuisha shida; barabara inayojumuisha mateso na
maumivu. Sisemi ya kwamba ni lazima tuyapitie maumivu ya mwilini,
bali nazungumzia maumivu yanayokuja pale Mungu anapoyachukua
maisha yetu na kuanza kuyashughulikia – tabia zetu, miili yetu,
tamaa zetu za kibinafsi na nia zetu – na tunakubali kuvunjwa na
kunyenyekezwa katika ujumla wa maisha yetu; ili, kwa neema yake,
tuanze kukua taratibu na kufananishwa na sura ya Kristo. Katika
Wakolosai 1:24, Mtume Paulo anatudokezea ni kwa nini alikuwa tayari
kulipa gharama ya kuteseka: “Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa
ajili yenu; tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya
mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake…” Mkristo
anayeikimbia changamoto hii na asiyeikubali kazi ya Kristo maishani
mwake, hawezi kutaraji kukua katika maisha yake ya rohoni. Katika
jinsi ya roho, atabakia kuwa mtoto mchanga.
Kazi Ya Utakaso
Mungu anatusihi tuipitie hii barabara nyembamba kwa sababu hapa
ndipo kazi yake ya utakaso itakapotimilika maishani mwetu. Mateso
tunayoyapata mikononi mwake si kwa ajili ya kutukandamiza au
59
kutuangamiza. Tukijaribu kuyakwepa maumivu na mateso, matokeo
yake tunaweza kuishia kuangamizwa na hali ile ile tunayojaribu
kuikwepa. Wengi wetu tunataka kumfanyia Mungu mambo makubwa,
ila tunapata shida kukubali ya kwamba, Mungu alilazimika kwanza
kufanya kazi ya ndani na nzito maishani mwa wengi wa wale
aliowatumia kwa namna ya kipekee. Hebu tafakari watu mashuhuri
wa Mungu katika Agano la Kale waliotajwa katika Waebrania 11.
Wote walikabiliwa, walipita katika majaribu, mateso, adha, pamoja
na kurudiwa na Mungu: yaani, kujaribiwa kwa imani yao. Na, je!
matokeo yake yalikuwaje? Walifanyika watu mashuhuri wa rohoni,
mashujaa wa imani. Mungu yule yule anatuita tuipitie barabara ile ile
nyembamba katika siku za leo.
Kulipa Gharama
Je! unaamini ya kuwa Ibrahimu alijawa na furaha alipoamua
kumwamini Mungu na kumtoa mwanawe dhabihu? Atakuwa aliteseka
sana alipokuwa njiani wakielekea mahali pa kutolea dhabihu pamoja
na Isaka; ila aliamua kuutii mpango Mungu aliokuwa nao kwa maisha
yake, na Mungu akamzawadia. Je! Musa alilipa gharama alipoamua
kubeba shutuma ya Kristo na kuteseka pamoja na watu wa Mungu,
badala ya kuzifurahia hazina za Misri? Je! Habili alikuwa na huzuni
alipoelewa ya kuwa alipaswa kumtolea Bwana wazao wake wa kwanza
wa mifugo? Mtafakari Nuhu, je! alikata tamaa kwa sababu hakuna mtu
Sura ya VII - Barabara ni Nyembamba
Kanisa Linahitaji Kujua
60
aliyemjali na wote walimdhihaki? Hapana! Watu hawa walimtii Mungu,
walipita katika mitihani na majaribu; walilipa gharama. Mioyoni mwao,
walikuwa tayari kuipitia barabara nyembamba; imani yao iliimarishwa,
na walipata kibali kwa Bwana. Leo hii, tunayafananisha maisha yetu
na mateso na kifo cha Kristo, kwa sababu tumeitwa kuipita njia hiyo
hiyo ngumu, na hatuwezi kuikwepa.
Mitihani Na Majaribu
Ninaamini hakuna maelezo sahihi kuhusu wito huu kuliko yaliyo
katika Wafilipi 1:29 ambapo Paulo anasema: “Maana mmepewa
kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake…”
Katika 2 Wakorintho 4:8-9, anasema “… Pande zote twadhikika,
bali hatusongwi; twaona shaka, bali hatukati tamaa; twaudhiwa,
bali hatuachwi; twatupwa chini, bali hatuangamizwi.” Kwingineko,
Mtume Yakobo ananena juu ya mitihani na majaribu ya imani
yetu. Hayo ndiyo mambo tunayopaswa kutarajia kwenye barabara
nyembamba. Kama Paulo, sisi pia tunajikuta tumesongwa pande
zote lakini tunasonga mbele; tukitatizwa, lakini tukimtumainia Mungu;
tukikataliwa kwa ajili ya Yesu, lakini tungali wenye furaha. Sisi pia
tunafahamu ya kuwa hatuna budi kuyapitia mambo hayo kama Yesu,
Mitume, na Wakristo wa Kanisa la Mwanzo walivyopitia; hili ndilo
fungu letu. Huu ndio Ukristo halisi! Mara tunapoamua kumfuata Yesu,
tunaitwa tuyafananishe maisha yetu na mateso yake. Yesu alituonya
61
mapema ya kuwa mambo yangekuwa hivyo. Lakini, wakati kila jambo
linapoonekana kugubikwa na giza na hali inakuwa ya kukatisha tamaa,
hebu tukumbuke ya kuwa kuna kusudi katika hayo yote. Katika hayo
tutauona ukombozi wa Mungu wetu na katika hayo tutakua rohoni.
Kusudi La Mateso
Waebrania 12:4 inasema: “Hamjafanya vita hata kumwagika damu,
mkishindana na dhambi.” Kwa maana nyingine, mioyoni mwenu
hamjafika mahali pa kuchukizwa na dhambi kabisa kabisa. Katika 1
Petro 4:1 tunasoma: “Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake,
ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliyeteswa katika
mwili ameachana na dhambi.” Ili kuelewa kinachozungumziwa katika
hii mistari, ni lazima tuikamate roho wa Injili. Vinginevyo, haitakuwa
rahisi kwetu kuelewa ni kwa nini tunaitwa kushiriki katika mateso ya
Kristo. Hakika Yesu hakutaka tu tupite katika mateso na shida bila
sababu.
Ni lazima kutakuwepo na kusudi, lengo, katika haya mambo. Nalo ni
nini? Matunda ya maisha ya jinsi hii ni uzima wa Kristo ndani yetu; ili
tuweze kufanana naye. Paulo anasema katika Wafilipi 2:5, “Iweni na
nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo…”; kwa
maana nyingine, iweni na nia aliyokuwa nayo Yesu, alipojinyenyekeza
na kuonja kifo cha Msalaba. Matokeo yake ni kwamba Mungu
alimwadhimisha mno.
Sura ya VII - Barabara ni Nyembamba
Kanisa Linahitaji Kujua
62
Kufanyika Kielelezo
Hatimaye, hebu tuangalie Waebrania 12:5-6, ambapo tunahimizwa
kutoyadharau marudia ya Bwana, kwani anatutendea kama wana,
wa kike na wa kiume... Ikiwa tunatamani kuhesabika kama wana
nyumbani mwa Mungu Baba yetu na kupata kibali kwake, ni lazima
tumruhusu atufinyange na kuturudi. Mwandishi anamalizia hiyo
sura kwa kuzungumzia maumivu yatokanayo na marudia; si wakati
wa furaha, tunateseka Mungu anapotuvunja na kutufinyanga,
anapofanya kazi maishani mwetu, lakini hili huleta matunda ya haki,
maisha matakatifu; matunda ya utakaso. Katika kuichukua barabara
nyembamba, hatuna budi kukubali ya kuwa ni jambo ambalo Mungu
ametuandalia, ili tuwe mifano, na vielelezo kwa ulimwengu.
Barabara Ya Utakaso
Hii ndiyo barabara ya utakaso. Tunatakaswa, na kufanyika zaidi na
zaidi kama Kristo. Kwenye hii barabara nyembamba, pamoja na
makemeo, marudia na maonyo yake – yanayoelezewa kuwa ni ‘kwa
faida yenu’ – ndipo tunapoandaliwa “tuushiriki utukufu wake”, na
kuleta “matunda ya haki yenye amani” Waebrania 12:10-11.
Hakuna njia nyingine ya kushughulika na dhambi yetu isipokuwa ni
kuyafananisha maisha yetu na mateso ya Kristo. Tunaweza kuwa na
63
uhakika wa kukua katika Ukristo wetu na kufanyika watu wa rohoni
pale tu tutakapoichukua barabara nyembamba, na kudumu juu yake.
Hii ndiyo siri ya maisha yenye ushindi.
Sisi watu wa Kanisa tunapaswa kubadili mtazamo wetu, na tuache
kuendelea kuikwepa barabara nyembamba. Ni sehemu ya mpango
maridadi kabisa Mungu alionao kwa ajili yetu. Na hapo, kama wale
mashujaa wa imani waliotajwa katika Waebrania 11, tutakuwa na
uhakika wa kusimama imara, na kuzikamilisha mbio zetu. Kamwe
tusisahau ya kwamba barabara nyembamba ndiyo iendayo uzimani!
Sura ya VII - Barabara ni Nyembamba
Kanisa Linahitaji Kujua
64
65
Sura ya VIII
Kanisa Litakabiliwa
Kanisa Linahitaji Kujua
66
Ninapoiangalia hali ya Kanisa la leo, nina hakika Wakristo wengi
wanahuzunishwa na kile wanachokiona. Kwa namna nyingi hakuna
utofauti kati ya mwenendo wa Wakristo wa karne ya 21 na maisha
waliyoishi wana wa Israeli enzi za Yeremia na manabii wengine wa
Agano la Kale. Katika siku za leo inaonekana ya kwamba, mara
nyingine tena, watu wa Mungu wanaelekezwa katika kufukuzia
mambo yasiyowafaidi.
Siku hizo, kutokana na upendo wake kwa watu wake, Mungu alituma
watu kuwaonya juu ya hatari za yale waliyokuwa wakifanya na athari
za kuendelea kumpinga. Leo tumebarikiwa kwa kuwa na Neno la
Mungu, Biblia, inayotuonya, kutuhimiza na kututia moyo. Zaidi ya
hayo, tunayo mifano ya Yesu Kristo, pamoja na Kanisa la Mwanzo,
inayotutia nguvu kubaki kwenye hiyo ‘barabara nyembamba’.
Zaidi ya hayo pia, tuna ujumbe wa Msalaba – nguvu ya Mungu –
unaotuwezesha kuishi maisha yenye ushindi na kulinda fundisho
la uzima. Kutokana na hilo, hakika inasikitisha kuona Wakristo
wakitafuta baraka ‘zinazopita’ ilhali ‘nguvu ya Mungu’ ipo kwa ajili
yao. Ushuhuda wa Kanisa dhaifu, na lililojaa migawanyiko, hakika
hauwezi kumfurahisha Mungu. Isipokuwa Kanisa liurudie ujumbe wa
msingi wa Ukristo, litaendelea kupeperushwa na kila upepo wa elimu
unaojitokeza.
Nina hakika ya kwamba Mungu anataka kutuonya juu ya baadhi
ya mambo yanayoendelea Kanisani katika siku za leo. Katika siku
67
tunazoishi Kanisa litakabiliwa: katika mwenendo wake, katika mahubiri
na mafundisho yake, na katika namna Wakristo wanavyohimizwa
kuyaishi maisha yao. Imani yangu ni kwamba kupitia kuhubiriwa kwa
ujumbe wa Msalaba, watu wa Mungu watakabiliwa.
Katika siku zake, nabii Yeremia, kupitia maagizo aliopewa na Mungu,
hakuacha kuwaonya Waisraeli juu ya kile ambacho kingewapata
kama wangeendelea katika njia zao zenye uovu. Wakati ule walikuwa
wakifukuzia vitu vingine vingi badala ya Mungu. Yeremia 1:9-10
inasema, “...Tazama, nimetia maneno yangu kinywani mwako;
angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung’oa,
na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.”
Sote tutakubaliana ya kuwa mara nyingi maonyo huja wakati mambo
yanahitajika kubadilika. Katika siku hizi za mwisho, ninaamini Kanisa
litakabiliwa katika namna linavyomtumikia Mungu, na katika mambo
yanayoivuta mioyo ya watu wa Mungu!
Neno la Mungu linasema ya kuwa mambo yaliyofanyika katika vizazi
vya nyuma yalikuwa ni mifano kuvionya vizazi vya mbeleni. Kwa mfano,
katika 1 Wakorintho 10:11 tunamwoma Mtume Paulo akitamka ya
kuwa mambo yote yaliyowapata Waisraeli jangwani yaliandikwa kwa
ajili yetu, sisi waamini wa Agano Jipya; “Basi mambo hayo yaliwapata
kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na
miisho ya zamani.” Tunaishi katika nyakati ambapo maisha ya juu juu,
au ya kurushwa huku na huku na kila aina ya upepo, hayana nafasi
tena. Vinginevyo tutajikuta tukivutwa na ulimwengu haraka sana,
Sura ya VIII - Kanisa Litakabiliwa
Kanisa Linahitaji Kujua
68
pamoja na mafundisho ya uongo, na hatimaye kunaswa katika mtego
wa adui.
Tunafahamu kilichowapata wana wa Israeli kutokana na kutotii kwao
na uasi wao. Lakini hata hivyo wao, pamoja na viongozi wao wa
kiroho, walipewa onyo baada ya jingine. Katika Yeremia 2:8 Mungu
anawakemea waziwazi kwa kutafuta mambo ambayo hayatawafaidia:
“Makuhani hawakusema, Yuko wapi BWANA? Wala wana-sheria
hawakunijua; wachungaji nao waliniasi, nao manabii walitoa unabii
kwa Baali, wakafuata mambo yasiyofaidia kitu.” Mungu anarudia tena
kemeo lake katika msitari wa 11, “Je! taifa wamebadili miungu yao,
ingawa si miungu? lakini watu wangu wameubadili utukufu wao kwa
ajili ya kitu kisichofaidia.” Nina hakika unatambua ya kuwa mali ya
kidunia haiwezi kutuletea badiliko la rohoni, au kutuleta katika utu
uzima rohoni na ukamilifu katika Kristo! Ndio maana wakati umefika
Kanisa likabiliwe na ujumbe wa Msalaba wa Yesu Kristo; injili pekee
inayoshughulika na mwili, inayokabili maisha yetu na hali za mioyo
yetu; na inayotupa kuyatamani mambo ya Roho yatakayotufaidia.
Katika msitari wa 13 Mungu anawakemea watu wake: “Kwa maana
watu wangu hawa wametenda maovu mawili; wameniacha mimi,
niliye chemichemi ya maji ya uzima, wamejichimbia mabirika,
mabirika yavujayo, yasiyoweza kuweka maji.” Birika linalovuja halina
kazi yoyote. Vivyo hivyo na sisi leo, tunajenga maisha ya ubatili kwa
kutafuta vitu ambavyo tumeaminishwa Kristo atatupatia, badala
ya kuutafuta uzima wake; uzima wa ufufuo, uzima wa Roho. Mimi
69
sina neno na wale Mungu mwenyewe anaoamua kuwabariki na
kuwafanikisha, hasa ninapofahamu ya kuwa shauku ya mioyo yao
ni kuubariki Ufalme. Lakini, ninapata shida Wakristo wanapohimizwa
kutafuta mali ya ulimwengu huu badala ya uzima wa Roho. Hata hivyo,
hakuna mahali kwenye Biblia tunapohimizwa kutafuta mali ya dunia;
kinyume chake, katika Wakolosai 3:1-2 Paulo anatuagiza waziwazi,
“Basi ikiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo
aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo
yaliyo katika nchi.”
Kukemewa Na Kukabiliwa
Ni wazi kwamba si kila mtu atakayepokea makemeo kwa moyo wa
toba. Mungu alimtahadharisha Yeremia kwamba ujumbe aliokuwa
awaletee watu ungezua upinzani mkubwa. Yeremia 1:19 inasema,
“Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo
pamojanawe,asemaBWANA,ilinikuokoe.”Waisraeliwalikujakinyume
na kile alichokuwa akisema; hasa kauli yake ya kuwa alichokuwa
akisema kilitoka kwa Mungu. Kwa sababu mioyo yao ilikuwa mbali
na Mungu, Waisraeli walikataa kusikiliza; walifurahia kukimbizana na
mambo yaliyoiridhisha miili yao. Matokeo yake ni kwamba walimpinga
Yeremia kwa muda wa miaka 40! Kanisa la Yesu Kristo la mwaka 2010
lina hali inayofanana na hiyo: watu wa Mungu wanahimizwa kutafuta
vitu visivyoweza kuwatosheleza kiroho. Wakati huo huo, Msalaba wa
Sura ya VIII - Kanisa Litakabiliwa
Kanisa Linahitaji Kujua
70
Yesu unapohubiriwa leo hii, unaleta mwanga Kanisani; unakemea; na
ndio maana, si ajabu, watu wengi hawaupendi.
Msalaba Ndio Msingi
Wahubiri wanapounda fundisho kutokana na vitu vya juujuu,
wanaondoa hamu ya kukua kiroho mioyoni mwa Wakristo.
Msalaba wa Yesu Kristo unapaswa uwe sehemu ya maisha ya wale
wanaosimama madhabahuni. Na Wakristo wanapaswa kulishuhudia
hilo; ya kwamba hawa watu wamevunjwa, na wanaendelea kuvunjwa
na Mungu; ya kwamba wamefanyika mifano, vielelezo; na ya kwamba
hawaneni tu elimu ya kibiblia. Hii ndio maana ujumbe wa Msalaba
unapaswa kurudi Kanisani sasa, ili mioyo ya Wakristo irejeshwe kwa
Kristo; hadi kuyafananisha maisha yao naye katika kuteswa kwake na
kifo chake. Hii ndiyo njia pekee ya kuushiriki uzima wa ufufuo, ambao
ni maisha ya Kristo anayoyaishi ndani yako na ndani yangu… tumaini
la utukufu!
Kuna hicho kipengele cha mateso na kifo ambacho kwa kiasi kikubwa
kimepotea Kanisani; huo ndio ujumbe wa Msalaba. Hatuwezi
kuukimbia. Ukristo unaotosheka tu na kuja kanisani, kubarikiwa, na
‘kuwa na wakati mzuri’ na wenzako kabla ya kutoa sadaka yako, kwa
kweli hii ni dini tu! Inanihuzunisha, ila ninaamini ya kuwa mengi ya
mambo yanayoendelea Kanisani leo hii ni dini tu; mikakati, kanuni,
71
mbinu, vyote vikiwa vimetokana na hekima ya mwanadamu…
kinachosikitisha zaidi ni kwamba katika mengi ya makanisa, pesa
ndio msingi wa kila kitu. Biblia inatamka waziwazi ya kwamba ujumbe
wa Msalaba ndio msingi wa maisha yetu ya Ukristo. Neno la Mungu
lina mengi zaidi kwa ajili ya roho zetu badala ya kuhubiri mfululizo
kuhusu mafanikio, pesa, kutoa na baraka.
Waalimu Kumi Elfu…
Katika 1 Wakorintho 4:14-15 Paulo ananena na Wakorintho wa mwilini
waliokuwa wamerudi nyuma katika kuwakumbusha na kuwaonya:
“Siyaandiki hayo ili kuwatahayarisha; bali kuwaonya kama watoto
niwapendao. Kwa maana ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika
Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndiye niliyewazaa
katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili.” Kila mahali alikokwenda aliweka
msingi mmoja tu na alihubiri injili moja katika makanisa yote: Injili ya
Msalaba. Hawa Wakorintho walifahamu fika kile Mungu alichotaraji
kutoka kwao, na kazi aliyohitaji kufanya ndani yao, ili wafanyike
wanafunzi, watumishi, na vielelezo kwa ulimwengu uliowazunguka.
Msalaba unapokosekana, mlango unakuwa wazi kwa mioyo yetu
kuvutwa na mambo yasiyokuwa na faida. Hilo ndilo lililowapata
Wakorintho. Walisikiliza injili nyingi. “Mnaweza kuwa na waalimu kumi
elfu.” Katika msitari wa 15 Paulo alikuwa anamaanisha: ‘Mmesikiliza
wahubiri wengi, mmesikiliza imani nyingi, mmejifunza mbinu nyingi;
Sura ya VIII - Kanisa Litakabiliwa
Kanisa Linahitaji Kujua
72
lakini angalieni hali yenu… kuna vita, wivu, na zinaa kati yenu!’
Mara tu unapouondoa msingi wa msalaba, matokeo ni Wakristo
wanaoenenda mwilini; waliorudi nyuma na walioshindwa!
Ikiwa hujazaliwa katika Injili ya Msalaba, utaitafsiri Biblia kwa manufaa
yako binafsi. Hautataka kusikia juu ya mitihani na majaribu, adha, na
mateso; juu ya kukemewa, kuonywa na kutubu; juu ya kuifia nafsi.
Mfano mzuri wa hili ni wakati Wakristo wanaponukuu Wafilipi 4:13,
“Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.” Wanachokazia
tu ni ile sehemu ya kwanza ya hili andiko: ‘Nayaweza mambo
yote.’ Lakini hebu tuangalie andiko zima tukianzia msitari wa 10…
”Nalifurahi sana katika Bwana, kwa kuwa sasa mwisho mmehuisha
tena fikra zenu kwa ajili yangu, kama vile mlivyokuwa mkinifikiri hali
yangu; lakini hamkupata nafasi. Si kwamba nasema haya kwa kuwa
nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo
nayo. Najua kudhiliwa tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na
katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa
na vingi na kupungukiwa. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye
nguvu.” Katika kuliangalia kwa ukaribu, tunaona kitu tofauti kabisa,
linazungumza habari za Paulo alivyoubeba msalaba wake. Mazingira
yo yote kwake – wingi au uchache – na kwa moyo mnyenyekevu,
neema ya Mungu na nguvu za Mungu vilimpitisha katika hayo yote.
Hii neema itakuwepo katika hali zote, nzuri au mbaya. Hiyo ndiyo
roho, ndio moyo, ambao Paulo anawasilisha hapa; huu ndio moyo wa
Kristo, roho wa Injili.
73
Kumfahamu Kristo
Usipozaliwa katika Injili ya kweli, utapata shida kukubali kile Mungu
anachotaka kwako. Mwili wako utang’ang’ania vitu vya mwilini, na
utakuzuia katika kuyafananisha maisha yako kikamilifu na Kristo.
Katika Wafilipi 3:10-11 Paulo anasema, “…ili nimjue yeye, na uweza
wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa
na kufa kwake; ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu.”
Tunawezaje kusema, sisi kama Wakristo, ya kuwa tunataka kumjua
Kristo pasipo kuwa tayari kuyafananisha maisha yetu na maisha
yake? Kama ilivyokuwa kwa Paulo, vivyo hivyo na sisi pia, tunaitwa
katika ushirika wa mateso yake, ili tuweze kuushiriki uzima wa ufufuo.
Vinginevyo, tutakuwa tunanena tu juu ya kule kuzaliwa mara ya pili.
Lakini, hatuwezi kuishia tu hapo… kwani katika msitari wa 15 Paulo
ananena zaidi ya kuzaliwa mara ya pili. Anatuhimiza kuwa na hali ya
moyo ambapo, hata kama hatuelewi sana au kukubaliana na ufunuo
wa Kristo na namna tulivyoitwa kujifananisha na yeye katika mateso
yake, kifo chake na kufufuka kwake, bado tunaweza kumwamini
Mungu kwamba atatufunulia anachohitaji kutufunulia.
Sura ya VIII - Kanisa Litakabiliwa
Kanisa Linahitaji Kujua
74
Msalaba Ndio Uzima Wako
Ninakutia moyo, mpe Mungu nafasi, kwa njia ya Yesu Kristo,
aidhihirishe nafasi stahili ya Msalaba wake maishani mwako, kama
anavyosema katika Mathayo 16:24: “Mtu yeyote akitaka kunifuata,
na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.” Maisha yetu
ya Ukristo yanapaswa kuwa na msingi mmoja tu: “Yesu Kristo naye
amesulubiwa!”
75
Sura ya IX
Yesu Anaita Tena
Kanisa Linahitaji Kujua
76
Ni jambo la kawaida kwa mwanadamu kutaka starehe na utoshelevu,
na kutotaka mabadiliko. Sisi kama Wakristo tunaweza tukawa na hali
iyo hiyo kuhusu mwenendo wetu na Mungu; watu waliotosheka na
wanaoishi maisha mepesi katika mfumo wa Ukristo uliozoeleka.
Ninaamini kwa dhati kabisa ya kuwa wimbi lingine la Mungu linakuja
hivi karibuni na ya kwamba Wakristo wanapaswa wafahamu mambo
yaliyoko mbeleni. Ni lazima tuelewe pia ya kuwa kila wimbi la Mungu
huambatana na kutetemeshwa. Mwanzoni miili yetu itataka kulipinga
jambo hili. Lakini wale wanaotamani kwa dhati kumtumikia Mungu na
kumfuata, watakuwa tayari kukubali chochote atakachotaka kwao.
Ni lazima tuhakikishe ya kuwa kwamba tu wachungaji, viongozi au
Wakristo ‘wa kawaida’, tunamtafuta Bwana na kutaka kujua kile Roho
Mtakatifu anacholiambia Kanisa leo.
Bila shaka, Mungu anatuita tulete ujumbe utakaowalisha watu wake;
utakaowafikisha katika utu uzima na uhuru katika Kristo. Ikiwa Yesu
anarudi hivi punde, hatakuja kulichukua Kanisa lisilokuwa na nguvu
wala utakatifu. Ujumbe wa Msalaba ndiyo Injili pekee yenye nguvu
ya kulibadilisha Kanisa na maisha ya Wakristo; na kuwaleta katika
kuichukua sura ya Kristo.
Katika historia ya Kanisa, zimekuwepo nyakati na majira ambapo
Mungu aliwaita wanaume na wanawake kwa makusudi mbalimbali
ili kutekeleza mapenzi yake hapa duniani. Nina hakika ya kwamba
huu sasa ni wakati ambapo Yesu anawaita wanaume na wanawake
kuupokea ujumbe mahsusi, ufunuo: injili ya Msalaba, fundisho la
msingi la Ukristo.
77
Yesu ana mpango na maono kwa Kanisa lake, na anataka yatimizwe.
Kwa bahati mbaya, anapoita, si kila mtu anayesikiliza au kujali…
Lakini hili halimzuilii, kwa sababu mipango yake ni lazima itekelezwe.
Haiyumkiniki kwamba Yesu atalijia Kanisa butu lisilokuwa na
uhai; na, zaidi ya hapo, Kanisa lililostarehe, lililojitosheleza, lililojaa
udini. Atachagua wanaume na wanawake; atawaita, na kuwapa
changamoto, vile vile kama alivyowachagua wanafunzi 12 waanzishe
Kanisa. Alimwita pia Mtume Paulo kwa kusudi maalum: “Lakini
Mungu…akaniita kwa neema yake…ili niwahubiri Mataifa habari
zake…” Tazama Wagalatia 1:15.
Muda wa Mungu wa kufanya jambo unapowadia, hulifanya. Katika
miaka 40 au 50 iliyopita, Mungu alileta ufunuo mpya kwa Kanisa;
ulikuwa mzuri nasi tunamsifu kwa huo. Lakini, je! tunaona nini leo?
Tunaona Kanisa lililopoteza nguvu yake, utakatifu, na kutengwa
kwake na ulimwengu. Ni nini kilichochukua nafasi? Kuchanganyikana,
dhambi, mafundisho ya uongo, na misisimko! Lakini, tena, Yesu
anawaita wanaume na wanawake ambao atawafunulia ujumbe wa
kweli wa Msalaba, ili waweze kuishi maisha halisi yenye ushindi, na
watakaoihubiri hiyo injili na kuitetea. Si kwa bahati mbaya, basi, ikiwa
wewe binafsi unahisi ya kwamba maisha ya Ukristo si tu kustarehe na
kukubaliana na kila jambo linalofanyika Kanisani siku hizi.
Sura ya IX - Yesu Anaita Tena
Kanisa Linahitaji Kujua
78
Jambo Jipya
Roho Mtakatifu anabisha kwenye mioyo ya Wakristo wengi; viongozi
wa makanisa, wanaume na wanawake, duniani kote; watu waliochoka
na ambao hawakubali ya kuwa Kanisa la Yesu Kristo halina zaidi ya
hiki wanachokiona. Ninaamini kwa moyo wangu wote ya kuwa kuna
jambo jipya, jambo zuri, ambalo Roho Mtakatifu anajiandaa kuinenea
mioyo ya hawa Wakristo. Tayari yuko kazini, akiandaa mioyo kuipokea
Injili ya Msalaba wa Yesu Kristo, hata kama tunaweza tusiione hiyo
kazi. Nina hakika ya kuwa Wakristo wengi wanahisi mioyoni mwao ya
kuwa kuna jambo jipya, jambo tofauti, linalokuja.
Wengine wenu mnaweza kuwa hata mmewaza ya kuwa haya mawazo
yanatokananauasindaniyenu,auyakwambamnauhurubinafsikatika
kutokukubaliana na mengi ya yale yanayohubiriwa madhabahuni leo
hii. Unajiuliza maswali... juu ya maisha yako ya Ukristo, na hali ya
moyo wako. Huyu ni Yesu anayeita! Hapa hatuzungumzii wito kwa
ajili ya huduma, bali ni Yesu anayekuita kama Mkristo uishi maisha ya
injili ya kweli, umruhusu Mungu kuikamilisha kazi ile njema aliyoianza
ndani yako.
79
Adui Za Msalaba
Lakini, kama ilivyokuwa siku za Mtume Paulo, wengi watasikia na
kupinga mahubiri ya ujumbe huu na watakuwa ni adui za Msalaba;
tazama Wafilipi 3:18: “Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni
mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi kuwa
ni adui za msalaba wa Kristo…” Inasikitisha kwamba si wahubiri
au Wakristo wote walio tayari kuupokea ujumbe wa Msalaba na
changamoto inayoletwa na maisha ya Ukristo.
Daima kutakuwepo na watu ndani ya Kanisa watakaoinuka na
kupingana na kile Mungu anachotaka kufanya. Kuanzia enzi za
Luther wakati wa Matengenezo hadi leo upinzani umekuwepo ndani
ya Kanisa; maadui wamepingana na kile Mungu anachotaka kufanya
Kanisani mwake. Matokeo yake, tutakutana na wale wanaoamini ni
jukumu lao ki-imani kuyapinga mahubiri ya injili ya Msalaba.
Msalaba Pekee
Paulo anasema katika 1 Wakorintho 2:2, “Maana naliazimu nisijue
neno lo lote kwenu, ila Yesu Kristo, naye amesulubiwa.” Injili ya
Msalaba ndio msingi wa Ukristo; hii Injili ndiyo iliyowapa changamoto
Wakristo katika Kitabu cha Matendo. Leo, Yesu anaita tena. Vile
vile kama Paulo anavyonena katika Wagalatia 1:11 jinsi alivyopokea
Sura ya IX - Yesu Anaita Tena
Kanisa Linahitaji Kujua
80
ufunuo moja kwa moja kutoka kwa Yesu Kristo, ninaamini Bwana
anachagua wanaume na wanawake, anawatenga, anaiandaa mioyo
yao na kuwafunulia ujumbe wa Msalaba.
Huu ujumbe ndio ufunuo ule ule uliokuwepo katika Kanisa la
Mwanzo; unawaalika Wakristo kuitika na kujisalimisha; kujihesabu ya
kuwa wamepoteza maisha yao na kutoshikilia kitu cho chote. Huu
ushawishi wa moyoni unatokana tu na injili ya Msalaba. Wanaume
na wanawake wataanza kusoma Maandiko na kuyafananisha maisha
yao na kile wanachokisoma. Viongozi wa makanisa watayadhihirisha
maisha yao madhabahuni, na kuikiri kazi ambayo Mungu anahitaji
kufanya maishani mwao. Wakristo kutoka kila rika na kabila wataanza
kufahamu ya kuwa Ukristo wa kweli unahusu kupoteza maisha yetu
ili Yesu aishi ndani yetu. Zaidi na zaidi wachungaji na washirika
watakubali ya kwamba injili hii ndiyo iliyokosekana Kanisani leo hii.
Si Ujumbe Mpya
Yesu alifundisha ya kwamba barabara ni nyembamba na ya kwamba
kuna gharama katika kumfuata, inayojumuisha kujikana nafsi, mateso,
adha, na kuyapoteza maisha yako. Wakristo wanapoanza kufahamu
ya kwamba Mungu anataka kuwaumba katika sura ya Mwanawe
watakuwa tayari kuikubali kazi anayotaka kufanya maishani mwao.
Kama Kanisa tutatambua ya kuwa mwenendo wetu hauna uhusiano
81
na sisi, bali yeye – Yesu akiishi ndani yetu; ni kujifananisha na yeye
kikamilifu. Katika Warumi 6:3-4, Paulo anasema ya kuwa tulizikwa
pamoja na Kristo kwa njia ya ubatizo, na ya kwamba tunapaswa
tuenende katika upya wa uzima, kama Kristo alivyofufuliwa kutoka
kwa wafu. Tunaposhiriki mauti yake, tunashiriki pia katika uzima
wake. Huu ndio upya wa uzima; huu ndio uzima wa Kristo! Haya ndiyo
maisha ya ushindi ambayo Yesu anatuitia… utimilifu wa Kristo ndani
yetu! Huu ndio ujumbe waliohubiri Mitume wa kwanza, na ambao ndio
Kanisa la Kwanza lililouishi. Ujumbe huu si mgeni; utaukuta kwenye
kila tafsiri ya Biblia.
Kufanya Uamuzi
Watu wengi wataanza kuusikia wito na watakabiliwa na uamuzi.
Wengine watasikia na kuupinga wito, lakini wengi watasikia na
kuuitikia.Kwahaoataifunuainjiliyakwelinahitajilaolakujifananishana
Kristo. Pamoja na upinzani na adha zitakazowakabili, watakapoanza
kuhisi Yesu akiita, watajawa na shauku ya kuyaishi hayo maisha.
Fahamu zao zinaweza zikataka kujadiliana, lakini mioyo yao itasema,
‘Ndiyo, Bwana. Niko tayari kulipa gharama ya kukufuata, kuiishi hii
injili; kufanyika udongo mikononi mwa mfinyanzi; kubadilishwa,
kutetemeshwa, kugeuzwa; kufanyika kama wewe, Bwana Yesu.’
Watawatafuta wale wanaoishi na kuihubiri Injili. Wataona utofauti ulio
Sura ya IX - Yesu Anaita Tena
Kanisa Linahitaji Kujua
82
wazi kati ya injili ya kweli ya Yesu Kristo na injili nyingine zote watu
wanazohubiri na kuziishi.
Katika Wafilipi 1, Mtume Paulo anasema aliitwa aitetee injili. Katika
kuuitikia wito wa Yesu, wewe pia utalazimika kuweka msimamo
na kusema: ‘Hiki si sahihi; yale siyo mafundisho yenye uzima!’
Utakabiliana na watesi na upinzani, lakini kwa neema ya Mungu
utashinda. Hivyo ndivyo Paulo alivyoweza kusema: “Lakini kwa neema
ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo… bali nalizidi sana kufanya kazi kupita
wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami.”
Kuuitikia Wito Wake
Yesu anaita tena leo. Anabisha kwenye mlango wa moyo wako na
anakuandaa uwe tayari kuuitikia huo wito. Ni upendeleo wa jinsi gani
huo, ni heshima kuu kiasi gani! Je! uko tayari kuitikia wito wake?
KanisaLinahitajiKujuaMikiHardy
Kanisa Linahitaji Kujua
Hebu sote tukubaliane ya kwamba kwa namna moja au nyingine Kanisa
limeliacha fundisho la uzima, na matokeo yake yanaonekana katika
maisha ya watu wa Mungu.
Viongozi wengi wameathiriwa na mafundisho ya mafanikio ya miaka ya
hivi karibuni, na wanatafuta kujinufaisha wenyewe. Wengine hawatambui
ya kwamba injili ya Msalaba ndiyo nguvu ya Mungu itakayowafikisha
Wakristo katika utu uzima rohoni.
Umefika wakati tuyazungumzie mambo fulani ya msingi waziwazi, ili
Wakristo watambue ya kwamba Bwana ana mambo mazuri zaidi kwa ajili
yao, makusudi watembee katika uhuru na katika ushindi!
9 789994 901814
ISBN 978-99949-0-181-4
Church Team Ministries International | Trianon, Mauritius
(230) 403 4500 | info@ctmi.org | www.ctmi.org
CTMI ni mtandao wa Kikristo usio rasmi ulioanzishwa mwaka
2001 na timu ya viongozi kutoka nchi mbalimbali barani Afrika
waliounganishwa pamoja na ujumbe wa msalaba na kazi ya Mungu
maishani mwao.

More Related Content

What's hot

Christian Fellowship
Christian FellowshipChristian Fellowship
Christian FellowshipGeorge Reala
 
THE MYSTERIOUS BABYLON - The Three Angels' Messages 4 of 8
THE MYSTERIOUS BABYLON - The Three Angels' Messages 4 of 8THE MYSTERIOUS BABYLON - The Three Angels' Messages 4 of 8
THE MYSTERIOUS BABYLON - The Three Angels' Messages 4 of 8Sarpong Boateng Josiah
 
ESTUDIO DE GUERRA ESPIRITUAL
ESTUDIO DE GUERRA ESPIRITUALESTUDIO DE GUERRA ESPIRITUAL
ESTUDIO DE GUERRA ESPIRITUALRaquel Bertañan
 
7 Letters: The Church of Sardis
7 Letters: The Church of Sardis7 Letters: The Church of Sardis
7 Letters: The Church of SardisStephen Palm
 
¿Cuerpo y alma son lo mismo? ¿muere el alma cuando muere el cuerpo? ¿Hay dife...
¿Cuerpo y alma son lo mismo? ¿muere el alma cuando muere el cuerpo? ¿Hay dife...¿Cuerpo y alma son lo mismo? ¿muere el alma cuando muere el cuerpo? ¿Hay dife...
¿Cuerpo y alma son lo mismo? ¿muere el alma cuando muere el cuerpo? ¿Hay dife...manu2002
 
Revelation 2 & 3 the seven churches
Revelation 2 & 3 the seven churchesRevelation 2 & 3 the seven churches
Revelation 2 & 3 the seven churchesEMMANUEL EMEH™
 
25. salmo 25 comunión íntima
25.  salmo 25 comunión íntima25.  salmo 25 comunión íntima
25. salmo 25 comunión íntimaComparte la Biblia
 
¿Qué pasó en la cruz? Néstor Martínez
¿Qué pasó en la cruz? Néstor Martínez¿Qué pasó en la cruz? Néstor Martínez
¿Qué pasó en la cruz? Néstor MartínezEberto Mejia
 
Spiritual warfare training: Battlefield of the Mind Part 3 (Pastor Ameerah)
Spiritual warfare training: Battlefield of the Mind Part 3 (Pastor Ameerah)Spiritual warfare training: Battlefield of the Mind Part 3 (Pastor Ameerah)
Spiritual warfare training: Battlefield of the Mind Part 3 (Pastor Ameerah)Ameerah Lewis
 
Overcoming the world
Overcoming the worldOvercoming the world
Overcoming the worldElleb Saj
 
EL PODER CREATIVO DE LA PALABRA
EL PODER CREATIVO DE LA PALABRA EL PODER CREATIVO DE LA PALABRA
EL PODER CREATIVO DE LA PALABRA Valentin Moraleja
 
Revelation 3:1-6 Sardis—Distinguished Yet Dead
Revelation 3:1-6 Sardis—Distinguished Yet DeadRevelation 3:1-6 Sardis—Distinguished Yet Dead
Revelation 3:1-6 Sardis—Distinguished Yet DeadDr. Rick Griffith
 
Armor of God
Armor of GodArmor of God
Armor of Godflutem3
 

What's hot (20)

Christian Fellowship
Christian FellowshipChristian Fellowship
Christian Fellowship
 
THE MYSTERIOUS BABYLON - The Three Angels' Messages 4 of 8
THE MYSTERIOUS BABYLON - The Three Angels' Messages 4 of 8THE MYSTERIOUS BABYLON - The Three Angels' Messages 4 of 8
THE MYSTERIOUS BABYLON - The Three Angels' Messages 4 of 8
 
ESTUDIO DE GUERRA ESPIRITUAL
ESTUDIO DE GUERRA ESPIRITUALESTUDIO DE GUERRA ESPIRITUAL
ESTUDIO DE GUERRA ESPIRITUAL
 
7 Letters: The Church of Sardis
7 Letters: The Church of Sardis7 Letters: The Church of Sardis
7 Letters: The Church of Sardis
 
03. What isnt the Gospel?
03. What isnt the Gospel?03. What isnt the Gospel?
03. What isnt the Gospel?
 
¿Cuerpo y alma son lo mismo? ¿muere el alma cuando muere el cuerpo? ¿Hay dife...
¿Cuerpo y alma son lo mismo? ¿muere el alma cuando muere el cuerpo? ¿Hay dife...¿Cuerpo y alma son lo mismo? ¿muere el alma cuando muere el cuerpo? ¿Hay dife...
¿Cuerpo y alma son lo mismo? ¿muere el alma cuando muere el cuerpo? ¿Hay dife...
 
Power in Prayer Together
Power in Prayer TogetherPower in Prayer Together
Power in Prayer Together
 
Revelation 2 & 3 the seven churches
Revelation 2 & 3 the seven churchesRevelation 2 & 3 the seven churches
Revelation 2 & 3 the seven churches
 
La Verdadera Amistad
La Verdadera AmistadLa Verdadera Amistad
La Verdadera Amistad
 
La sanacion a través del perdon
La sanacion a través del perdonLa sanacion a través del perdon
La sanacion a través del perdon
 
25. salmo 25 comunión íntima
25.  salmo 25 comunión íntima25.  salmo 25 comunión íntima
25. salmo 25 comunión íntima
 
¿Qué pasó en la cruz? Néstor Martínez
¿Qué pasó en la cruz? Néstor Martínez¿Qué pasó en la cruz? Néstor Martínez
¿Qué pasó en la cruz? Néstor Martínez
 
Spiritual warfare training: Battlefield of the Mind Part 3 (Pastor Ameerah)
Spiritual warfare training: Battlefield of the Mind Part 3 (Pastor Ameerah)Spiritual warfare training: Battlefield of the Mind Part 3 (Pastor Ameerah)
Spiritual warfare training: Battlefield of the Mind Part 3 (Pastor Ameerah)
 
Overcoming the world
Overcoming the worldOvercoming the world
Overcoming the world
 
How Do I Communicate with God?
How Do I Communicate with God?How Do I Communicate with God?
How Do I Communicate with God?
 
EL PODER CREATIVO DE LA PALABRA
EL PODER CREATIVO DE LA PALABRA EL PODER CREATIVO DE LA PALABRA
EL PODER CREATIVO DE LA PALABRA
 
Tu eres lo que piensas
Tu eres lo que piensasTu eres lo que piensas
Tu eres lo que piensas
 
Revelation 3:1-6 Sardis—Distinguished Yet Dead
Revelation 3:1-6 Sardis—Distinguished Yet DeadRevelation 3:1-6 Sardis—Distinguished Yet Dead
Revelation 3:1-6 Sardis—Distinguished Yet Dead
 
Armor of God
Armor of GodArmor of God
Armor of God
 
Unidad de la iglesia
Unidad de la iglesiaUnidad de la iglesia
Unidad de la iglesia
 

More from CTMI - Church Team Ministries International (9)

Le défi de la Croix
Le défi de la CroixLe défi de la Croix
Le défi de la Croix
 
The Five-fold Ministry (english)
The Five-fold Ministry (english)The Five-fold Ministry (english)
The Five-fold Ministry (english)
 
A Igreja Precisa De Saber (Portuguese)
A Igreja Precisa De Saber (Portuguese)A Igreja Precisa De Saber (Portuguese)
A Igreja Precisa De Saber (Portuguese)
 
Les cinq ministères (French)
Les cinq ministères (French)Les cinq ministères (French)
Les cinq ministères (French)
 
L'Eglise doit savoir (French)
L'Eglise doit savoir (French)L'Eglise doit savoir (French)
L'Eglise doit savoir (French)
 
Chrétien, tu es libre ! (French)
Chrétien, tu es libre ! (French)Chrétien, tu es libre ! (French)
Chrétien, tu es libre ! (French)
 
The Church Needs to Know (English)
The Church Needs to Know (English)The Church Needs to Know (English)
The Church Needs to Know (English)
 
Une famille unie, c'est possible ! (French)
Une famille unie, c'est possible ! (French)Une famille unie, c'est possible ! (French)
Une famille unie, c'est possible ! (French)
 
The New Covenant (English)
The New Covenant (English)The New Covenant (English)
The New Covenant (English)
 

Kanisa Linahitaji Kujua (Swahili)

  • 1. Umefika wakati tuyazungumzie mambo kadhaa ya msingi waziwazi ili Wakristo watambue ya kwamba Bwana ana mambo mazuri zaidi kwa ajili yao! Miki Hardy LINAHITAJI KUJUA KANISA
  • 2. Kanisa Linahitaji Kujua 10 Hakimiliki © 2013 na Church Team Ministries International (CTMI) Kanisa Linahitaji Kujua na Miki Hardy. Imechapishwa na Church Team Ministries International (CTMI) Toleo la kwanza: Julai 2015 Jalada limebuniwa na: Idara ya Habari ya CTMI Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu ya chapisho hili inayoweza kunakiliwa, kusambazwa,au kutolewa kwa namna yo yote ile isipokuwa kwa ruhusa ya mchapishaji. Vifungu vya Biblia vimetolewa katika Biblia, Swahili – Union Version, 1962. Machapisho mengi ya Church Team Ministries International yanapatikana kwa gharama nafuu ikiwa yananunuliwa kwa jumla kwa ajili ya kutangaza, kuchangisha fedha, kugawa bure, na kwa kuelimishia. Kwa maelezo zaidi, tuandikie: Media Dept., CTMI, Trianon, Mauritius; au tuma baruapepe kwa: media@ctmi.org Tembelea tovuti yetu: www.ctmi.org ISBN 978-99949-0-181-4
  • 3. Yaliyomo I. Moyo wa Mungu Juu ya Ndoa na Talaka 5 II. Je, Wakristo Wanaweza Kupagawa Mapepo? 15 III. Mkristo na Pesa 23 IV. Mungu na Muziki 31 V. Vita ya Rohoni 39 VI. Mahusiano Kabla ya Ndoa 47 VII. Barabara ni Nyembamba 55 VIII. Kanisa Litakabiliwa 65 IX. Yesu Anaita Tena 75 ................................... .......................... ....................................................................... ...................................................................... ........................................................................... ....................................................... ........................................................ ................................................................ ..................................................................... 3
  • 5. Sura ya I Moyo wa Mungu Juu ya Ndoa na Talaka 5
  • 6. Kanisa Linahitaji Kujua Wakristo wengi leo wanaweza kukumbuka wakati ambapo suala la talaka kwa mchungaji au kiongozi wa Kanisa lilikuwa ni jambo la aibu isiyoneneka. Hapakuwepo na uwezekano kwa mtu wa jinsi hiyo kuendelea katika utumishi. Zaidi na zaidi, leo tunaona wachungaji wakitoa talaka, wakioa upya na kuendelea na huduma kana kwamba hakuna jambo zito lililofanyika. Ninaamini haya ni matokeo ya anguko na udini ambavyo vimechukua nafasi ya fundisho la uzima na Kweli ya Kibiblia ndani ya Kanisa. Hili ndilo chimbuko la hii hali ya mambo. Sasa, ikiwa mchungaji anaweza kumpa mkewe talaka na akaendelea kuwaongoza watu wa Mungu, je! waumini wanapata mfano wa jinsi gani wa kuiga? Labda maswali tunayopaswa kujiuliza ni, “Ni kwa nini Wakristo wawili waliojazwa Roho Mtakatifu washindwe kutatua tofauti zao” na, “Je! kuna uhalali wo wote kwa haya matatizo kutotatulika, au kwa wawili hawa kuachana?” Ama liwe linamhusu mchungaji, au mshirika wa kanisa, ninaamini suala la kutengana, kutoa talaka, na kufunga ndoa mara ya pili hufanyika kwa sababu hawa watu hawajui wajibu wao kamili mmoja kwa mwingine katika ndoa. Tunaona kwenye Maandiko ya kuwa mume ana wajibu mkubwa mno: kumpenda mkewe kama Kristo anavyolipenda Kanisa. Vivyo hivyo, mke naye ameitwa amtii mumewe. Kama wawili hawa wasipouchukua msalaba wao, na kumruhusu Roho wa Mungu awavunje na kuwabadilisha, hilo kamwe halitakuja kutokea… Mungu peke yake ndiye anayeweza kulifanya hili mioyoni mwao. Hakuna mbinu inayoweza kulifanya hili… ni matokeo ya kazi ya Msalaba maishani mwao! 6
  • 7. Sijaona popote kwenye Maandiko kinachonielekeza kuamini ya kuwa ni mapenzi ya Mungu kwa wanandoa Wakristo, achilia mbali mchungaji, kutoa talaka. Hii ni kwa sababu Mungu, kwa njia ya Msalaba, ameleta njia ya kurejesha upendo na umoja kati yao. Hebu sasa tuangalie Neno la Mungu linavyotufunulia kuhusu suala la ndoa na talaka… Siku hizi, watu wengi hawaoni shida kwa Wakristo wanandoa kuachana kwa sababu tu mmoja wao hapatani na mwenzake; au kwa kuwa tu hawana mtazamo mmoja kuhusu mambo mbalimbali au hawana tena maono mamoja! Hakika hili ni eneo ambalo Kanisa limekubali kuathiriwa si tu na njia za ulimwengu usioamini, bali pia na viongozi wa Kikristo ambao wameandika vitabu, wakihalalisha matendo yao ya kibinafsi sana na ambao, kwa kuamua kuchukua njia ya talaka wamefungua mlango kwa waumini kufanya vile vile. Ninaamini ya kwamba badala yake, tunapaswa tuuangalie mtazamo wa Mungu juu ya suala hili. Ndoa Kwenye Agano Jipya Kwenye kitabu cha Mwanzo, Mungu aliianzisha ndoa. Baada ya yale Yesu aliyokamilisha Msalabani, ndoa ya kwenye Agano la Kale, yenye wake wengi na hati za talaka, haiwezi tena kulinganishwa na ndoa chini ya Agano Jipya. Sura ya I - Moyo wa Mungu Juu ya Ndoa na Talaka 7
  • 8. Kanisa Linahitaji Kujua Mpango wa Mungu kwetu sisi, kama Wakristo tuliozaliwa mara ya pili, ni kuishi na waume zetu na wake zetu hadi ‘kifo kitakapotutenganisha’. Katika Marko 10:2, kwa kuwa Yesu alikuwa akiwahoji Mafarisayo juu ya mtazamo wao wa kisheria katika masuala mengi, walimjaribu kwa kumwuuliza: “Je, ni halali kwa mtu kumwacha mkewe?” Yesu akawaonyesha ya kuwa, chini ya Musa na Torati, Mungu ‘aliruhusu’ talaka kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao (Marko 10:5); lakini katika Agano Jipya, mambo yangekuwa tofauti. Katika Mathayo 5:32, anazungumzia waziwazi juu ya kile kinachotarajiwa kwa waamini wote wa Agano Jipya: “Lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.” ‘Isipokuwa kwa habari ya uasherati’ bila shaka haimaanishi pale mwenzi mmoja anapoanguka katika dhambi na kufanya tendo moja la uasherati au la kukosa uaminifu. Inazungumzia mtu ambaye amerudi nyuma na anaishi katika dhambi, na aliyedhamiria kuendelea kuishi katika dhambi. Kwa kuiruhusu talaka katika mazingira hayo maalum, Yesu hajaondoa ukweli kwamba yule aliyekosewa bado anatakiwa kunyenyekea na kusamehe. Hili linaweza kufanyika kwa dhati pale tu tunapoikubali njia ya Msalaba. Kwa hivyo, Biblia iko wazi: kwenye Agano Jipya, hakuna uhalali wowote wa kutoa talaka isipokuwa katika maeneo maalum sana… vinginevyo itapunguza kile Yesu alichokifanya Kalvari! 8
  • 9. Injili Zisizokuwa Na Uweza Nina hakika utakuwa umegundua ya kuwa Kanisa limepoteza mwelekeo katika hili eneo, na linaenenda kama vile Injili ni kitu kinachobadilika kwa kutegemea nyakati. Katika miongo michache iliyopita, Kanisa, kwa kujumuisha wachungaji na viongozi, kwa usahihi kabisa, halikukubaliana na talaka, lakini leo hii talaka imekubalika makanisani. Ni nini kilichofanyika? Bila shaka ni kwa sababu injili inayohubiriwa leo hii imebadilika na haina uwezo wa kushughulika na mambo ya jinsi hiyo. Haina nguvu tena ya kuihakiki dhambi kama mwanzoni. Mfano mzuri ni injili ya ‘Mafanikio’ inayovuta mioyo ya watu kuyaandamia mambo ya mwilini badala ya kutafuta makuzi ya rohoni. Haijengi, na hakika haina uwezo wa kukabiliana na mambo ya ndani ambayo Wakristo wanapambana nayo leo. Hii ndio maana ni muhimu turejee kwenye injili ya ufunuo wa Msalaba ikiwa tutataka kuona familia za Kikristo zenye umoja pamoja na kupungua kwa kiwango cha talaka Kanisani. Siku hizi Wakristo mara nyingi wanataka njia rahisi ya kutatua matatizo yao ya ndoa, mlango rahisi wa kutokea. Wanaachana kwa sababu nyepesi kama vile: “Mke wangu hanitii”; “Mume wangu si mtu wa rohoni,” au mbaya zaidi, “Hatupatani tena, maono yetu na matarajio yetu yamebadilika…” Watu wa jinsi hii bila shaka hawajaisikia injili sahihi, kwani injili sahihi itawaongoza katika kuwajibika kila mmoja kwa mwenzake. Sura ya I - Moyo wa Mungu Juu ya Ndoa na Talaka 9
  • 10. Kanisa Linahitaji Kujua Nafasi Ya Mume Niruhusu nifafanue juu ya ufunuo wa ajabu Paulo aliopewa kuhusu ndoa kwenye Waefeso 5. Uhusiano wa mume na mke ndio tu uliolinganishwa katika Agano Jipya na uhusiano Yesu alio nao na Kanisa lake. Paulo anatamka kwa ujasiri ya kuwa, “KAMA Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake VIVYO HIVYO mume naye anapaswa kumpenda mke wake.” Yesu alijinyenyekeza, akachukua sura ya mwanadamu, akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Hiyo ndiyo hali ya moyo Yesu anayoagiza mume awe nayo kwa mke wake. Huo ndio wajibu wa mume: kama Yesu, yeye naye anaitwa apoteze haki zake na autoe uhai wake kwa ajili ya mke wake. Huu ndio ufunguo wa ndoa yenye mafanikio. Utaratibu Wa Mungu Kwenye Ndoa Nafasi ya mke imefananishwa na ile ya Kanisa. Paulo anatamka ya kuwa “KAMA vile Kanisa limtiivyo Kristo, VIVYO HIVYO mke naye anapaswa kumtii mumewe.” Kwa hivyo, Kanisa – wewe na mimi – linapoelewa kile Yesu alichofanya msalabani kwa ajili yetu; kwa manenomengine,upendoaliouonyesha,sisinasitunawezakumpenda pia. Isingewezekana tumpende Yeye kabla ya kuujua upendo wake kwetu. Je, unaweza ukaona utaratibu wa mambo hapa? 10
  • 11. Ni wazi, basi, kwamba mume ana wajibu mkubwa zaidi kuliko mke katika ndoa, kwani huduma yake inalinganishwa na ya Kristo, ilhali ya mke imefananishwa na ya Kanisa. Ikiwa mume atakuwa tayari kuchukua hatua ya kwanza, katika kuutii wito wake, kama Kristo alivyofanya, moja kwa moja atavuna hali ya utii kutoka kwa mke wake. Katika mazingira ya kawaida, hatutarajii kwamba utii wa mwanamke kwa mumewe utakuwa wa moja kwa moja; lakini msingi sahihi unapokuwepo, mume anaweza akatarajia ya kuwa mkewe atamnyenyekea. Hata hivyo, hata kama mke hatafanya vile, mume anapaswa aendelee kuyatoa maisha yake kwake, na amtegemee Mungu kufanya muujiza moyoni mwa mkewe. Mwishoni mwa kifungu hiki, Paulo ananukuu andiko kutoka katika Agano la Kale, “Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.” Moyo wa Mungu kwa ajili ya ndoa ni mume na mke wadumu katika umoja maisha yao yote. Tunapozitii amri za Mungu, yeye ni mwaminifu na hutenda miujiza. Mume Wa Mke Mmoja… Yapo mambo mengi sana yahusuyo ndoa ambayo hayajatajwa katika Biblia. Kanisani mwetu penyewe tumeshuhudia matukio mengi tofauti katika miaka hii mingi, na tumejifunza kuyatatua kila moja kwa namna yake, katika neema na kweli. Mahali ndugu wa kiume au wa kike alipoichukua njia ya Msalaba, na kuiruhusu toba kufanya kazi 11 Sura ya I - Moyo wa Mungu Juu ya Ndoa na Talaka
  • 12. Kanisa Linahitaji Kujua moyoni mwake, tumeshuhudia urejesho na ushindi maishani mwao na katika utumishi wao kwa Bwana. Na hebu niongeze kusema ya kwamba Mungu si Mungu anayetoa nafasi ya pili au ya tatu ya kujaribisha mambo. Mpango wake sikuzote ni kwa mume kuwa na mke mmoja, na ametuwezesha katika hilo kwa kumtuma Yesu katika mfano wa mwanadamu, afe Msalabani na kuishinda dhambi katika mwili. Ni juu yetu kuyatoa maisha yetu yawe dhabihu ili miili yetu isulubiwe. Mwanamume anayemwacha mkewe halafu akaendelea katika utumishi kana kwamba hakuna kilichofanyika, hawezi kutarajia kuendelea kubeba upako ule ule katika utumishi wake kwa Bwana, na hasa ikiwa ameoa tena, hadi atakapoacha kuhalalisha uamuzi wake huo na kutubu. Ufunguo Unaoleta Matengenezo Si mpango wa Mungu kwa mtu yeyote kumwacha mwenzi wake. Mungu anachukia talaka; lakini hawakatai wale walioachana – au waliooa ama kuolewa mara ya pili – ikiwa watatubu. Ikiwa nimegusa eneo linalokuhusu, hujachelewa. Mungu anaweza kukurejesha, pamoja na utumishi wako kama uko kwenye huduma, ikiwa utakuwa tayari kukiri ya kuwa haukuenenda sawasawa na moyo wala Neno la Mungu, bali ulifuata tamaa za mwili wako; na ya kuwa, inawezekana ulijiingiza katika mahusiano yasiyo sahihi. 12
  • 13. Ikiwa ni hivyo, ni lazima umrudie Bwana kwa toba ya kweli; kulingana na maongozi ya Roho Mtakatifu, na ukiwa na utayari wa kufanya lolote atakalokuagiza kufanya... hata kama itakulazimu kumrudia mwenzi wako wa mwanzo. Kumbuka ya kwamba Bwana hahitaji sababu au maelezo kuhusu mwenzi wako, au kuhusu yale aliyoyafanya. Yeye huuangalia moyo wa mtu. Katika kila jambo, Mungu anatamani tuwe na moyo safi, mnyenyekevu, uliojaa msamaha, na ulio na toba. Inawezekana yakawepo mahusiano ambayo pengine hayawezi kurekebishika; ila, mengi zaidi yanarekebishika, ikiwa tuko tayari kujikana nafsi zetu na kuuchukua msalaba wetu. Msalaba ndilo suluhisho la Mungu kwa ndoa yenye mafanikio! 13 Sura ya I - Moyo wa Mungu Juu ya Ndoa na Talaka
  • 15. Sura ya II Je, Wakristo Wanaweza Kupagawa Mapepo? 15
  • 16. Kanisa Linahitaji Kujua Katika safari zangu barani Afrika katika miaka 25 iliyopita, swali moja limekuwa likijitokeza mara kwa mara: “Je, inawezekana kwa Mkristo aliyezaliwa mara ya pili kupagawa mapepo?” Hili jambo mara nyingi huhusishwa na maisha aliyoishi mhusika huko nyuma, au kibaya zaidi, linahusishwa na mambo waliyoyafanya mababu zake. Inanihuzunisha kuona kwamba kuna Wakristo wengi wanaoamini ya kwamba wao, au ndugu zao wa kiume na wa kike katika Kristo wanaweza kupagawa mapepo baada ya kupokea wokovu. Sote tunakubali ya kuwa kazi za mapepo na roho chafu zipo. Lakini je! inawezekana kwa mtu aliyezaliwa mara ya pili kuhitaji kufunguliwa kutokana na nguvu za mapepo? Ninaposoma Maandiko, jibu langu kwa swali hili ni “Hapana!” yenye nguvu. Biblia iko wazi kuhusu hili suala: tunapozaliwa mara ya pili, tunaokolewa kutoka katika nguvu za giza na kuingizwa katika Ufalme wa Yesu Kristo. Roho Mtakatifu anakuja kuishi ndani yetu na nuru haiwezi kukaa pamoja na giza. Hakuna jinsi kabisa ambapo pepo anaweza akaishi ki-kwelikweli ndani ya Mkristo aliyezaliwa mara ya pili, aliyeyatoa maisha yake kwa Bwana Yesu Kristo na anayetamani kumtumikia. Haiwezekani kabisa! Tunapaswa tuhoji wokovu wa watu waliojitokeza kwenye mikutano na kuungama sala ya toba, halafu wakaendelea kudhihirisha dalili za kupagawa mapepo. Katika hali kama hizo, labda tungepaswa kuuliza swali: ‘Je, toba ya kweli imefanyika mioyoni mwao?’ Lakini cha muhimu zaidi, ni kwamba ninaamini matatizo mengi yanayosingiziwa pepo ni madhihirisho tu ya mwili. Kwa bahati mbaya, 16
  • 17. Wakristo wengi wameaminishwa ya kwamba haya madhihirisho ya mwili ni kazi za Shetani. Jambo ambalo Kanisa linapaswa kujua ni kwamba, katika hali kama hizi, maombezi ya ‘ukombozi’ sio jawabu. Maisha yetu yanapooana na mfano wa Yesu Kristo, na tunapouchukua Msalaba wetu kila siku, na kuifisha miili yetu na kumfuata yeye, suala la ‘kupagawa pepo’ halitakuwa tatizo maishani mwetu, au kwa Kanisa. Ulimwengu wa roho upo na unaweza kuwa na nguvu kuliko tunavyofikiri. Ndio maana Mungu anapogusa maisha yetu tunaweza kubadilishwa mara moja. Kwa msingi huo huo kuna watu ambao maisha yao yameathiriwa na mapepo pamoja na roho za kishetani. Katika vitabu vya injili, Yesu mwenyewe alitoa pepo na kuwaweka watu huru. Ukweli kwamba watu wanapagawa mapepo upo na hauwezi kupingwa. Hata hivyo, katika Mathayo 12, Yesu anapozungumza juu ya kutoa pepo, alizungumza kabla ya Msalaba na alikuwa akizungumzia kizazi kikaidi, sio Kanisa. Kwa hivyo, swali langu ni hili: Wakristo waliozaliwa mara ya pili, waliotubu dhambi zao za kale, na kuyasalimisha maisha yao kwa Yesu, je! bado wanahitaji kufunguliwa kutoka katika nguvu za mapepo? Kuzaliwa Mara Ya Pili Au Kutokuzaliwa Kabisa Sijaona mahali popote kwenye Biblia Wakristo katika Kanisa la mwanzo wakitolewa mapepo. Ama umezaliwa mara ya pili au la; 17 Sura ya II - Je, Wakristo Wanaweza Kupagawa Mapepo?
  • 18. Kanisa Linahitaji Kujua hakuna zaidi! Kabla ya kumjua Yesu tulikuwa chini ya mamlaka ya Shetani. Hatukumjua Mungu; na sisi sote pia tulikuwa chini ya ushawishi wa roho za kishetani au tulitawaliwa nazo (Waefeso 2:1-5). Mtu asiyeamini anapotubu dhambi zake na kuamini katika dhabihu ya Yesu msalabani, Mwenyezi Mungu mwenyewe huja na kuishi moyoni mwake. Wakolosai 1:13 inaelezea hivi: “Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake.” Baada ya sisi kuzaliwa upya na Roho Mtakatifu, asili ya Mungu inachukua nafasi ya asili ya dhambi iliyotutawala mioyoni mwetu hapo kabla. Mara nyingi sio lazima hata kuomba ili mtu afunguliwe. Yule asiyeamini tayari yuko chini ya hukumu kubwa sana na yuko tayari kuyasalimisha maisha yake kwa Kristo, kiasi kwamba anawekwa huru kwa wepesi sana kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Mara nyingine anahitajika kufanyiwa maombi ili afunguliwe. Kutokana na hayo unaweza ukauliza je, maana yake nini haya madhihirisho ya nguvu za giza leo hii makanisani? Jawabu ni kwamba watu wengi huja tu kwa ajili ya kupokea uponyaji na kufunguliwa kutokana na nguvu za giza, kubarikiwa, na si kumtafuta Mungu kwanza. Na kwa sababu hawajazaliwa mara ya pili, nguvu za giza huendelea kuyatawala maisha yao. Lakini haiwezekani kwa Wakristo waliozaliwa mara ya pili kuendelea kuwa chini ya nguvu za mapepo, isipokuwa wamerudi nyuma hadi kuvunja kabisa uhusiano wao na Kristo, wamemkataa Bwana na kuzifungulia mlango kazi za mapepo mioyoni mwao na 18
  • 19. maishani mwao. Kwa sababu, inawezekanaje Roho Mtakatifu kuishi kwenye mwili mmoja na pepo? Shida nyingi na mambo mengi yanayohusishwa na mapepo yana mizizi yake kwingineko. Kama hatupo kwenye msingi wa Msalaba tunajikuta tukipokea kila aina ya mafundisho ya uongo na imani za kigeni. Kwa kila jambo linaloharibika tunatupia pepo lawama. Ni Mwili! Ni lazima ieleweke kwamba ikiwa mimi kama Mkristo nina shida na mwili wangu, haina maana kwamba kuna pepo ndani yangu… ila ni kwamba tu nimeziruhusu tamaa za mwili wangu zinitawale. Ni kweli twaweza kujaribiwa, lakini ni lazima tutofautishe kati ya kujaribiwa na kumilikiwa na roho chafu. Ni pale tu nitakapojikana nafsi yangu, kuwa tayari kuziachilia haki zangu na kuyapoteza maisha yangu kwa kuuchukua msalaba wangu, ndipo nitakapopata ushindi katika eneo husika. Sihitaji kabisa kukemewa pepo yeyote atoke, maana tayari niko huru na mapepo! 19 Sura ya II - Je, Wakristo Wanaweza Kupagawa Mapepo?
  • 20. Kanisa Linahitaji Kujua Maombi ya Kufunguliwa Sio Jawabu Mungu ametufungulia njia ya kutokushindwa na miili yetu, au kuzisikiliza tamaa zake. Ni Msalaba. Ndio maana maisha yetu hayana uhusiano wowote na mapepo. Roho wa Mungu anaishi ndani yetu. Yeye anatuombea na kutuwezesha, kwa neema ya Mungu, kuusulubisha huu mwili. Kile Mungu anachotaka kufanya maishani mwako kwa njia ya utakaso hakiwezi kupatikana kupitia maombezi ya kutoa pepo. Usimruhusu mtu yeyote ajaribu kukemea ndani yako pepo wa hasira, uvivu, wivu na kadhalika. Vivyo hivyo huwezi kutatua tofauti zilizopo kati yako na mwenzi wako, watoto wako au Mkristo mwenzako kwa kukemewa pepo... Haya ni madhihirisho ya mwili wako, matokeo ya maisha ambayo hayajasalimishwa kwa Bwana. Wakristo wengi leo wamekata tamaa kwa sababu wanafahamu ni aina gani ya watu wanaopaswa kuwa, lakini wanapoitazama hali halisi ya maisha yao, wanahisi tu kushindwa na kukata tamaa. Hivyo wanakimbilia kwenye kutolewa pepo. Ushindi upo katika Msalaba. Hebu kuwa na utayari wa kuyapoteza maisha yako na utaona matokeo yake... Tunaweza kuwa dhaifu katika maeneo mengi, lakini bado tukaudhihirisha uzima wa Kristo. Tumewekwa huru mbali na mapepo na tunaitembelea hiyo njia ya kuuelekea ukamilifu; Bwana apewe sifa! Kwa maelezo kuhusiana na kazi za mwili, angalia orodha iliyoko Wagalatia 5:19-21. Na hebu nikuambie, huhitaji kutolewa pepo ili uweze kutembea katika ushindi dhidi ya mambo haya. Chukua tu msalaba wako. 20
  • 21. Kujifananisha Na Kristo Ni muhimu tuweze kuelewa kusudi la ujumbe wa Msalaba kwa maisha yetu. Ni lazima tuwe tayari kujifananisha na mauti ya Kristo ili tuweze kuubeba uzima wake na kuwa huru. Mara tu tunapouweka msalaba kando, tunatafuta njia za mkato, au jambo mbadala kama vile kukemewa pepo, yaani, aina ya Ukristo wa kubonyeza kitufe. Lakini katika Wagalatia 2:20, maneno ya Paulo, “Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu…” ni tamko la ajabu linalodhihirisha aina ya maisha aliyoishi. Kupitia ufunuo alioupokea, Paulo alijifunza ya kwamba alihitajika ayafananishe maisha yake na maisha ya Kristo, ajikane nafsi yake, ausulubishe mwili wake. Aliuishi huo ufunuo na akaweza kuuhubiri; maisha yake yalikuwa ni ushuhuda wa mabadiliko yanayoletwa na kazi ya Msalaba. Ujumbe wa Msalaba ni onyo la mara kwa mara na kumbukumbu inayoufunua udhaifu wa miili yetu, na kutuwezesha kuona hali halisi ya maisha yetu. Inatuleta kwenye toba, kujikana nafsi na kurejea Msalabani. 21 Sura ya II - Je, Wakristo Wanaweza Kupagawa Mapepo?
  • 22. Kanisa Linahitaji Kujua Huru Kweli Kweli! Kwa hivyo, ndugu au dada mpendwa, ikiwa kutoka katika vina vya moyo wako umeyasalimisha maisha yako kwa Kristo, tofautisha kati ya udhaifu wa mwili wako na kupagawa mapepo. Unaweza ukawa ni Mkristo dhaifu, ila tambua umewekwa huru mbali na mapepo. Haleluya! Ndio sababu Mtume Paulo alinena sana juu ya hatari za mwili. Alifahamu fika udhaifu wa mwili. Kumbuka, “Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli!” 22
  • 24. Kanisa Linahitaji Kujua 24 Kama kuna eneo ambalo Wakristo leo hii wamelaghaiwa na kufundishwa mafundisho yenye udanganyifu, hakika ni katika eneo la fedha na utoaji. Ni aibu kubwa kwa Kanisa kuona wachungaji wengi wakilikosesha kundi la Mungu kwa kuwapa ahadi za uongo za mafanikio na baraka; wakiwapotosha kwa kutumia sheria zinazowashurutisha kutoa. Mara nyingi nimelishutumu fundisho la mafanikio lililolivamia Kanisa, kwenye nchi tajiri na nchi maskini. Jumbe zangu zimeelezewa kuwa zenye utata kwa sababu nimepinga kuhubiriwa fundisho hili la uongo. Sina tatizo kabisa Wakristo wanapotajirika kwa mali za ulimwengu huu, na wanapobarikiwa. Lakini ninapingana vikali na mafundisho ya kwamba ni mapenzi ya Mungu ya kuwa Wakristo wote wameitwa kuwa matajiri. Hili linapatikana wapi kwenye Biblia? Hata Kanisa la Mwanzo lilikuwa na Wakristo maskini. Kwa hivyo, ninaamini ni uzushi kuwaaminisha Wakristo wote ya kwamba ni mapenzi ya Mungu wote wawe matajiri, wote wamiliki majumba makubwa, magari ya kifahari, n.k., au ya kwamba wanapoendelea kubaki maskini ni kwa sababu hawana imani… uzushi kabisa! Katika maeneo kama Afrika na India, Wakristo wengi wanaishi katika umaskini wa kutisha. Hakuna aibu katika hilo, na haimaanishi hawana imani. Zaidi ya hilo, katika mahubiri mengi ya siku hizi, pesa inapewa umuhimu kupita kiasi!
  • 25. 25 Si kwamba ninalishambulia fundisho la mafanikio, lakini ninaamini tunahitajika tuangalie Neno la Mungu kuhusu hili suala katika mtazamo sahihi – katika kuutafuta moyo wa Mungu kwa hili. Kinachonisikitisha zaidi ni kwamba waumini katika makanisa ambapo injili ya jinsi hii inahubiriwa, na ambao wengi wao ni maskini, hawafiki mahali pa kuelewa ya kwamba Mungu ana haja na aina ya moyo tulionao katika kumtolea. Mungu humpenda mtu anayetoa kwa moyo mkunjufu, si mtoaji tajiri! Katika makanisa mengi sana, linapokuja suala la utoaji, watu wanaleta sadaka zao wakitaraji kurudishiwa kwa wingi ‘walichopanda’, au kutokana na shinikizo na hofu ya kuonekana wanaenda kinyume na ‘kile Biblia inachosema’! Ila, tunapolitazama Neno la Mungu, je! ni wapi tunapomuona Yesu au Mitume wakizungumzia mafanikio kwa mtazamo wa jinsi hii? Jambo lililo wazi ni kwamba Mungu ameahidi kuyashughulikia maisha yetu (Mathayo 6:25-26); ni udhihirisho wa moyo wa Mungu kwa watu wake na maono yake kwa ajili ya Ufalme. Biblia sio kitabu chenye mbinu na kanuni kwa wahubiri kutumia ili kuwaomba ninyi muwape pesa ili Mungu aweze kuwabariki. Sura ya III - Mkristo na Pesa
  • 26. Kanisa Linahitaji Kujua 26 Kumpenda Yesu, Kuupenda Ufalme Wake Mpango wa Mungu kwa Kanisa lake ni kwamba Wakristo wabebe moyo wake uwe ushuhuda kwa ulimwengu usioamini. Kwa Mkristo mwenye shukrani anayejua kuwa Yesu alitoa kila kitu kwa ajili yake, ambaye moyo wake unamilikiwa na Mungu na ambaye maisha yake yamebadilishwa na Kristo, kutamani kumtolea Mungu ni asili yake. Si mtu anayeleta matoleo yake kwa sababu analazimika kufanya hivyo, au kwa sababu mtu fulani amemwambia atoe kiasi fulani, au kwa kuwa amefundishwa jinsi ya kumtolea Mungu. Na hakika hatoi ili abarikiwe. Anatoa kwa sababu anampenda Yesu na Ufalme wa Mungu; ana shukrani kwa ajili ya wokovu. Maisha yake yamefananishwa kikamilifu na ya Kristo, na moyo wake umetolewa kikamilifu katika kuyatumikia maono ya Mungu kwa Kanisa lake. Hapa yupo mtu mwenye uwezo wa kutoa vyote, juu sana kuliko asilimia yoyote iliyopangwa au kiwango chochote kilichowekwa. Yeye hupanda kwa furaha katika Ufalme wa Mungu kwa kadiri anavyoongozwa na Roho Mtakatifu. Mkristo wa aina hii anaweza kutoa kwa ukarimu hata katika nyakati za uhitaji mkubwa, kama tunavyoona Kanisa la Makedonia likifanya katika 2 Wakorintho 8. Anatenda huku akiamini ya kuwa Mungu atashughulikia mahitaji yake binafsi, kwa sababu anajua moyo wake ni kwa ajili ya Ufalme.
  • 27. 27 Mungu Anataka Tufanikiwe Kuna vifungu viwili vya Maandiko ambavyo karibu kila Mkristo anavijua; kwani, katika nyakati fulani, wengi wetu huenda tumesikia vikifundishwa kuhusiana na utoaji na mafanikio. Katika maeneo yote mawili, mafundisho ya uongo yamepenyezwa Kanisani ikiwa ni matokeo ya wahubiri kuichukua mistari hii kwa maana nyingine… Katika 3 Yohana 1-8 tunasoma, “Mpenzi, naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.” Sote tunafahamu kuwa Mtume Yohana anamsifu Gayo kwa moyo, upendo, jinsi anavyoujali Ufalme, na ukarimu wake kwa watu wa Mungu. Je, si ni jambo la kawaida kabisa kwa Yohana kumtaka Mungu ambariki mtu wa jinsi hii? Mtume anataka Gayo afanikiwe katika mambo yake yote, kwa sababu anajua chochote anachopewa na Bwana kitatumika kuwabariki ndugu wengine na kitakuwa na manufaa katika Ufalme. Sasa, tunarukaje kutoka kwenye kweli hii hadi kutangaza kuwa ni mapenzi ya Mungu - ni kusudi lake na mpango wake - kwamba Wakristo wote wafanikiwe kifedha; kwamba Wakristo wote wanapaswa watarajie kupokea mara mia kama malipo, endapo watatoa kwa ajili ya mhubiri huyu au mradi ule? Hili ni kinyume na Maandiko! Tunachoweza kusema bila shaka yo yote ni kwamba Mungu angependa kumbariki kila Mkristo, ambaye, kama Gayo, ana moyo kwa ajili ya Ufalme, na ni mkarimu kwa watu wa Mungu. Sura ya III - Mkristo na Pesa
  • 28. Kanisa Linahitaji Kujua 28 Maono Ya Agano Jipya Tunaposoma maneno ya Yesu katika Luka 6, tunaona roho ile ile na moyo ule ule aliokuwa nao Yohana na mitume wengine wote. Hapa (mistari 27-46) Yesu anazungumza na makutano kuhusu kuwa na moyo mwingine na maono mengine... moyo na maono ya Ufalme. Anawasihi watu kutoa maisha yao na kumruhusu Mungu awabadilishe ili waishi sawasawa na Agano Jipya. Kwamba, katika mtazamo huu anasema katika msitari wa 38: “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu.Kwakuwakipimokilekilempimachondichomtakachopimiwa”, si sababu ya mtu kutafsiri kuwa alikuwa akizungumzia utoaji na mafanikio. Hiki kifungu kinahusu aina ya moyo anaopaswa kuwa nao Mkristo ambaye daima anashughulishwa na Ufalme wa Mungu. Kwa msingi huo Yesu anamalizia, katika msitari wa 46 kwa kusema, “Na kwa nini mnaniita Bwana, Bwana, walakini hamyatendi nisemayo?” Kwa hiyo, hapaswi mtu yeyote kutumia andiko hilo kushawishi watu ya kuwa wakitoa, bila kujali hali za mioyo yao au nia wanayotoa nayo, ya kwamba Mungu bado anawajibika kuwabariki. Hii ndiyo maana leo hii kuna mamilioni ya Wakristo ambao bado wanasubiri baraka zao!
  • 29. 29 Kwa Kadri Ya Uhuru Wa Moyo Wako Niruhusu niseme ya kwamba ikiwa bado unaamini kuwa unalazimika kumtolea Mungu, hujaelewa undani wa kile ambacho Yesu Kristo alifanya pale msalabani; ukombozi aliotupatia Mwana wa Mungu. Ametuweka huru. Leo hii tuko huru kutoa kutoka katika ndani ya mioyo yetu, kwa kadiri tunavyoongozwa na Roho Mtakatifu. Je, unafahamu ya kuwa kama nitamtegemea mtu au sheria yoyote katika Agano la Kale iliyo chini ya ukuhani wa ki-Lawi kuniambia ni kiasi gani ninachotakiwa kutoa, ninaweza nikajikuta nikitoa chini zaidi ya kiwango nilichodhamiria moyoni kutoa? Sasa katika mtazamo halisi tunaona moyo wa Mkristo wa Agano Jipya katika tamko la Mtume Paulo katika 2 Wakorintho 9:7 “Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.” Hapa hatuoni Mkristo mwenye hofu, na mnyimivu, anayelazimika kutoa kwa sababu anawajibika kutoa, au kwa sababu kila mtu atafahamu kiasi alichotoa. Kutumika Katika Uhuru Makanisa ya Makedonia yalikuwa na uwezo wa kutoa licha ya umaskini wao mkubwa, ikiwa ni matokeo ya Injili iliyowafanya kukubali Sura ya III - Mkristo na Pesa
  • 30. Kanisa Linahitaji Kujua 30 kupoteza maisha yao, kujikana nafsi zao, kuuchukua msalaba kila siku na kumfuata Yesu. Ukarimu wao ulikuwa ni matunda ya kazi ya injili, si matokeo ya kulaghaiwa kihisia. Walitamani kutoa kutoka katika vina vya mioyo yao, na wakasisitiza kutaka kushiriki katika mradi wa kiroho na wenye manufaa kwa Ufalme na kwa watakatifu wengine. Tafadhali elewa kuwa sitaki kukufanya uangalie nyuma na uanze kuhoji ni kwa jinsi gani au ni kwa lipi ulilotolea pesa zako huko nyuma. Lakini ninaamini kuna Wakristo wengi wanaotafuta kuujua ukweli. Nami ninachotaka ni kwa Kanisa kuujua moyo wa Mungu kwenye suala la pesa; fundisho la kweli ni lipi kulingana na Neno lake ili, kwa neema yake na kwa kuongozwa na Roho wake Mtakatifu, tuweze kuwa huru kumtumikia Mungu kwa pesa zetu.
  • 31. 31 Sura ya IV Mungu na Muziki
  • 32. Kanisa Linahitaji Kujua 32 Sitakuwa ninatia chumvi nikisema ya kwamba uzi unaotenganisha muziki wa kidunia na kile kinachoitwa ‘Muziki wa Kikristo wa Kizazi Kipya’, ni mwembamba kwelikweli. Inasikitisha, lakini uimbaji mwingi tunaousikia Kanisani siku hizi ni muziki wa kidunia wenye maneno ya Kikristo. Kwa kadiri roho wa dunia hii inavyozidi kujipenyeza Kanisani, si ajabu kuuona muziki wake pia ukiingia Kanisani. Tunapotazama muziki na uimbaji wa ‘Kikristo’ ulioko sasa hivi, tunapata kuona ni kwa kiasi gani roho ya ulimwengu ilivyolivamia Kanisa. Kwa kadiri uimbaji Kanisani unavyozidi kuchukua sura ya kidunia tunaona jinsi hili linavyoleta kuchanganyikiwa na kumenyana, hasa kwa vijana. Swali ninalotaka kuuliza ni: ‘Je, kuabudu halisi kuna uhusiano gani na muziki wa kidunia?’ Ninashindwa kuelewa ni kwa nini tutake na hata tujaribu kuyachanganya, haya mawili – kumsifu Bwana kwa mdundo wa kidunia… kwa kweli, haiwezekani! Tunapokuwa tumezaliwa mara ya pili, tunapaswa tutamani kuabudu kwa mioyo yetu, katika Roho na Kweli. Jambo lolote nje ya hilo ni kuuburudisha mwili. Kwa mara nyingine tena, ninaamini ya kwamba katika kuliangalia Neno la Mungu tutapata ufahamu na ufunuo mpya juu ya moyo wa Mungu katika suala la sifa na kuabudu. Hebu tuwe makini tusikaribishe kila kitu kinachobeba nembo ‘Kristo’ ya kwamba kinampatia Mungu utukufu. Hakuna maelekezo ya wazi katika Biblia kuhusu namna tunavyo- paswa kumuabudu Mungu. Katika Agano la Kale kuna maagizo
  • 33. 33 yanayohusiana na muziki, kuabudu, na vyombo vya muziki, pamoja na mifano ya watu wa Mungu wakimsifu Mungu kwa shangwe na kucheza; lakini katika Kanisa la Agano Jipya hakuna maelekezo juu ya aina ya maneno, mapigo, au midundo tunayoweza kutumia; au hata namna ya kucheza. Kuna sababu nzuri juu ya hili... kumbuka kuwa sisi ni watu wa Agano Jipya! Kwamba ni weusi au weupe, tajiri au maskini, wasomi au wasio wasomi, sote tuna vitu viwili vinavyof- anana: mioyo yetu na Roho Mtakatifu aliyeko ndani yetu. Yeye ni mwalimu wetu, anatuongoza na kutushuhudia mioyoni mwetu juu ya nini kinachotokana na Mungu Baba na nini kisichokuwa cha Mungu. Roho Mtakatifu Ni Mwangalizi Wetu Katika Yohana 16:13-14, tunasoma, “Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. Yeye atanitukuza mimi; kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.” Hakuna kuchanganya hapa: Ni wazi kwamba Roho Mtakatifu ndiye anayetuelekeza, kutufundisha na kutuongoza katika namna Yesu anavyonena na namna anavyotenda. Sote tutakubaliana kuwa kulikuwa na harufu nzuri ya manukato katika yote Yesu aliyosema na kufanya. Vivyo hivyo, harufu ya manukato ya kumjua Kristo inapaswa iambatane na yote tunayosema na kufanya. Cho chote kinachotokana Sura ya IV - Mungu na Muziki
  • 34. Kanisa Linahitaji Kujua 34 na dunia kina roho nyingine; lakini kwa sababu Mungu ametupa sisi (Wakristo tuliozaliwa mara ya pili) Roho Mtakatifu kuishi ndani ya mioyo yetu, tunaweza kupambanua roho ya ulimwengu huu ulioko chini ya milki ya Shetani. Mambo Ya Ajabu Yanafanyika Ninaamini watu wanaelewa ya kuwa hata katika Ukristo kuna mambo ya misisimko na ya kimwili yanayoendelea. Kwa bahati mbaya si kila kitu chenye nembo ya ‘Ukristo’ ni kizuri kwa moyo wako au roho yako. Kama ilivyo kwamba kuna aina ya uimbaji na muziki ambavyo tunashuhudiwa mioyoni mwetu ya kuwa vinatokana na Bwana, vivyo hivyo kuna aina ya muziki, uimbaji na kucheza ambavyo vinatoa harufu kali ya kidunia na ya mwili. Tuwe makini tusibebe Neno la Mungu katika hali ya maandiko tu. Neno linaposema ‘Msifuni Bwana kwa vinanda’ au ‘Msifuni kwa kucheza na shangwe’, haina maana kwamba tunaweza kuleta roho ya dunia Kanisani, kwa kucheza kwa namna yoyote tunayojisikia, au kwa kutumia vyombo kucheza midundo au mitindo ambayo huwezi kutofautisha na ile inayochezwa katika kumbi za muziki. Kwa kuangalia mifano michache tu ya kucheza na kushangilia katika Biblia, ninaamini tunaweza kuona tofauti kati ya muziki na kuabudu kunakompendeza Mungu kwa kuashiria kile kilichomo ndani ya
  • 35. 35 mioyo yetu, na muziki unaotumbuiza tu na kulisha miili yetu, ambao mwisho wake ni kutupeleka katika kutenda dhambi. Katika Kitabu cha 2 Samweli 6:12-15, kuhusiana na wakati ambapo Daudi aliporejesha sanduku la agano, lililowakilisha uwepo wa Mungu katika Yerusalemu, mistari ya 14-15 inaeleza, “Daudi akacheza mbele za BWANA kwa nguvu zake zote; na Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani. Basi Daudi na nyumba yote ya Israeli wakalileta sanduku la BWANA kwa shangwe, na kwa sauti ya tarumbeta.” Daudi pamoja na watu wa Israeli walikuwa wanasherehekea ushindi mkubwa. Kicho chake kwa Mungu, unyenyekevu wake, pamoja na furaha ya kweli vilizidi sana ndani yake kiasi cha kumfanya acheze, licha ya kuwa tendo lile lilionekana kama la kipuuzi mbele ya mke wake. Watu walifurahia kile ambacho Mungu alikuwa amefanya, walijua hii haikuwa kazi ya mwanadamu. Daudi alipomuua Goliathi, watu wale wale waliokuwa wakitetemeka kwa hofu ghafla walijawa ujasiri wakatoka kwenda kuwashambulia Wafilisti. Baada ya kuwa wametoka kwenye vita kama hiyo, tunasoma katika 1 Samweli 18:6-7 kwamba, “wanawake wakatoka katika miji yote ya Israeli, kwa kuimba na kucheza, ili kumlaki Mfalme Sauli; wakatoka na matari, na shangwe, na vinanda. Nao wanawake wakaitikiana wakicheza.” Katika Agano Jipya (Matendo ya Mitume 3) Petro na Yohana walienda hekaluni siku moja, na mtu mmoja aliyekuwa kiwete tangu kuzaliwa akaponywa. Mtu huyu alishangilia kwa furaha kuu na kucheza ndani ya hekalu akimsifu Mungu kwa muujiza wake. Hakuweza kujizuia katika furaha yake. Sura ya IV - Mungu na Muziki
  • 36. Kanisa Linahitaji Kujua 36 Shangwe Itokayo Moyoni Katika mifano yote mitatu, tunaona mlipuko wa shukrani na shangwe, vilivyotokana na moyo wa shukrani uliosababisha kuimba, kucheza na muziki. Ni suala la Mungu, wala si muziki. Tunaponyenyekezwa na kile ambacho Mungu ametufanyia, tuko huru kufurahia kwa kadiri mioyo yetu itakavyotuongoza. Hakuna tatizo juu ya kuimba na kucheza katika mazingira kama hayo. Lakini viongozi wa sifa wanapoamua Jumapili asubuhi kwamba ‘sasa’ ni wakati wa kuanza kumsifu Bwana kwa kucheza, au kuabudu kwa kushawishi hisia za watu, kwa uimbaji ambao si kingine bali ni maneno ya Kikristo yaliyoambatana na midundo ya kidunia na yanayotupelekea katika kuigiza, ni lazima tuanze kujiuliza maswali. Na ni vivyo hivyo kwa ‘Matamasha ya Injili’. Je, ni nini kinachotokea kwa hawa vijana wa kike na wa kiume ambao hisia zao na miili yao inakuwa imeamshwa kwa hali ya juu na waimbaji walioko jukwaani? Yesu anapewaje heshima na utukufu katika mazingira haya? Wengine wanaweza kusema hiyo ndiyo namna vijana wa kisasa wanavyoabudu na ni njia ya kuwavuta marafiki zao kuja kusikiliza habari za Bwana Yesu. Lakini mimi naweza kuuliza je! ni wangapi katika hawa marafiki wanaofikia kwenye kuzaliwa mara ya pili kwenye haya matamasha? Na, cha muhimu zaidi, je! ni idadi gani ya hawa Wakristo vijana wanaojikuta sasa wakiwa katika barabara ya kurudi nyuma kiroho ikiwa ni matokeo ya kuwasha tamaa
  • 37. 37 za miili yao kupitia haya matamasha? Mimi binafsi ninapoyasikiliza au kuyatazama matamasha kama haya, Roho Mtakatifu hushuhudia ndani yangu kuwa kuna kitu hakiko sawa. Na sote tunajua ni nani na ni nini kilichoko nyuma ya kila kitu ambacho hakitokani na Roho! Hatuwezi kujificha nyuma ya ‘muziki wa injili’ unaofurahisha hisia zetu na kuamsha miili yetu. Mwili hauwezi kutoa uzima wa rohoni, kwa hiyo, mara tu mwili unaposisimkia aina fulani ya muziki tuko hatarini. Sisi kama watu wa rohoni ni lazima tuweze kupambanua kati ya muziki utokanao na Mungu - ibada ya moyoni inayojenga - na muziki wa kidunia unaoamsha tu miili na hisia zetu. Muziki Una Vyanzo Viwili Kama tunavyojua, muziki unatokana na mmojawapo ya vyanzo viwili tu. Chanzo cha kwanza ni katika moyo wa Mungu - ambapo wanaume na wanawake, mara nyingi kutokana na kazi ya Mungu waliyoishuhudia maishani mwao, huongozwa na Roho Mtakatifu kutunga sauti au kuandika wimbo. Nyingi za tenzi kuu za Kikristo tulizonazo leo hii zinalishuhudia hili. Mungu ndiye anayeumba huu muziki moyoni mwa mwanadamu ili amwabudu na kumsifu Yeye, kumpa utukufu wote, heshima na uweza. Upako wa Mungu unapokuwepo, mioyo yetu inayeyuka na tunamezwa katika uwepo wake. Chanzo cha pili cha muziki ni roho inayoutawala ulimwengu - ambapo midundo, vionjo na miondoko ni ya kimwili na ya kidunia. Sura ya IV - Mungu na Muziki
  • 38. Kanisa Linahitaji Kujua 38 Muziki ni eneo lingine la hatari sana kwa Kanisa tunapouweka kando msingi, yaani, Injili ya Msalaba, ambayo mara zote inatupa changamoto na kutuleta kwenye utu uzima. Tukikaa kwenye huo msingi, kwa kadiri tunavyozidi kukua na kufanana zaidi na Kristo, tutafahamu pasipo na shaka yo yote ni lipi tufanye, wapi pa kwenda, na kipi cha kusikiliza. Na tutajikuta hatuvutiwi tena na muziki ambao hauifaidi roho kwa namna yoyote. Ninataraji ya kuwa maneno haya machache yameleta mwanga na ufafanuzi zaidi kuhusiana na somo hili; ya kwamba kwa namna fulani Mungu ameyafungua macho yako na umetiwa moyo
  • 39. 39 Sura ya V Vita ya Rohoni
  • 40. Kanisa Linahitaji Kujua 40 Fundisho lingine ambalo limejipenyeza Kanisani ni lile la ‘vita vya kiroho’. Wakristo kila mahali wanatilia mkazo katika kutoa pepo na kudhibiti roho chafu kila mahali wanakokwenda. Ikiwa tunataka kuishi sawasawa na fundisho la uzima la Kristo, tunapaswa tuyachunguze Maandiko tuone ni nini kilichomo moyoni mwa Mungu, na katika mioyo ya Mitume walioandika Nyaraka. Leo hii katika mengi ya makanisa, kuna lugha nyingi na shughuli nyingi linapokuja suala la vita ya rohoni, na kifungu cha Biblia kinachotumika katika hili suala ni Waefeso 6. Hata hivyo, ninapokitazama hiki kifungu, sioni jambo lolote linazungumzia kuanzisha mapambano dhidi ya roho wachafu. Ninachoona ni wito halisi wa Mungu juu ya maisha ya muumini. Mtume Paulo anatuhimiza tujitie nguvu katika Bwana, ili tuweze kusimama siku ya uovu. Mahali pengine, Mtume Yakobo anatuagiza ya kwamba adui ashambuliapo: “Mpingeni Shetani naye atawakimbia.” Sehemu kubwa ya kile Kanisa linachokiita ‘vita vya kiroho’ si kingine zaidi ya kupigana na mapepo. Wakristo wanaona hiyo kuwa ndiyo njia ya kupata ushindi maishani mwao. Lakini, Biblia inasema waziwazi ya kuwa ikiwa tuko ndani ya Kristo, Shetani hawezi kutugusa. Ikiwa maisha yetu yako sawa mbele za Mungu , na mioyo yetu ni safi, ni kwa nini tuyaogope mapepo? Tunapaswa tu kuyapinga. Tumeitwa tuishi maisha yenye ushindi, na tutaupata huo ushindi na kupinga mashambulizi ya Shetani tutakapoyafuata maagizo ya Yesu katika Mathayo 16:24: “Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.”
  • 41. 41 TunapoyaangaliaMaandikokatikamtazamosahihi,nakupataufahamu sahihi wa kile kilichofanyika Msalabani, tutaanza kuona nafasi yetu na msimamo wetu katika Kristo na katika Neno lake. Ninaamini wale wanaojishughulisha na ‘vita vya kiroho’ wanapaswa wajiulize maswali matatu… “Vita vya kiroho ni nini hasa?” “Hili limetajwa wapi kwenye Agano Jipya?” Na, “Je, dhabihu ya Yesu Msalabani haikutosha?” Katika Waefeso 6, ninaamini Mtume Paulo anazungumzia maisha ya ushindi pamoja na Bwana, maisha yenye ushindi katika haki na maisha matakatifu yanayompendeza Mungu. Kwa namna fulani, hii mistari imetafsiriwa kwa namna isiyo sahihi kuleta maana ya kwamba vita ya rohoni ni sehemu ya wito wetu. Leo hii, Kanisani kumeingia uelewa fulani ya kwamba, ikiwa tunataka ushindi, tunahitajika muda wote kuwa vitani tukipigana na mapepo, roho chafu, na kila nguvu na mamlaka; kufunga na kufungua roho kila tupatapo nafasi kwa sababu wametuzunguka kila mahali. Hebu tuangalie mistari ya 10-11: “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, n.k...” Kusudi la hili andiko sio kutufundisha jinsi ya kupigana vita ya rohoni. Wito uliopo hapa ni kwamba tuimarike, kwa sababu adui atashambulia! Paulo anasema, ‘Muimarike katika Kristo kwa sababu siku ya uovu imewadia.’ Mtume anaelewa fika ya kuwa vita au mapambano yo yote maishani mwetu hakika ni ya rohoni, na Sura ya V - Vita ya Rohoni
  • 42. Kanisa Linahitaji Kujua 42 wala si kitu cha kimwili au cha asili. Anatuonya mapema ya kwamba tunapaswa kuwa hodari katika Bwana. Kwa maana nyingine, ikiwa tu imara rohoni hatutashindwa na hila za adui. Ufunguo wa hili ni shauku yetu ya kutaka kukua, na utayari wa kuyasalimisha maisha yetu kikamilifu kwa Kristo. Hapo Bwana atatupa neema ya kusimama, hata kama tu wachanga kiroho, tunapozidi kumpinga Shetani. Mungu hatamruhusu adui avuke mpaka kwani yeye ndiye mlinzi wetu; yeye ni ngao na mwokozi wetu. Shauku kuu ya Paulo ni kwamba tumtumikie Bwana katika hali zote na ya kwamba adui ashambuliapo, tuwe hodari katika imani ili tuweze kusimama imara na kuupata ushindi. Kumtii Mungu Mtume Yakobo anasema katika waraka wake (4:7-8): “Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi...” Roho iliyoko nyuma ya mistari hii ni sawa na ile iliyo kwenye Waefeso 6; mwito ule ule, maisha yale yale, mamlaka ile ile! Anaposema tuyatiishe maisha yetu kwa Mungu, anamaanisha kujikana nafsi zetu, kuuchukua msalaba wetu, na hatimaye, kumpinga Shetani.
  • 43. 43 Tutawezaje kubaki mwilini halafu tuende vitani dhidi ya mapepo, na falme, na kudai na kufundisha ya kuwa tutapata ushindi dhidi yao? Huku ni kuyatumia Maandiko kama mbinu, na inakwepa ukweli ya kwamba Ukristo ni maisha tunayoishi katika roho. Silaha Zote Za Mungu Ni vigumu kumshinda Shetani ikiwa hautembei kwenye barabara ya Msalaba na kumruhusu Mungu akutakase na ashughulike na mwili wako. Unaweza ukanukuu kila Andiko, ukafunga kila pepo, ukakiri kila msitari, ukachukua mamlaka dhidi ya kila jambo, na kufunga na kufungua kwa kadiri upendavyo. Ikiwa maisha yako ya rohoni yamevurugika, na hayako juu ya msingi wa Kristo aliyesulubiwa, adui hatakimbia utakapojaribu kumpinga; badala yake, atakuingiza dhambini na kukushinda. Jumbe nyingi zimehubiriwa, na vitabu vimeandikwa, juu ya ‘kuvaa silaha zote za Mungu’. Hakika hii haiwezekani iwe ni kanuni ya kimwili; wala haihusikani na kuyanukuu Maandiko, kufunga mapepo, n.k. Si suala la maneno hata kidogo. Silaha yetu ya rohoni inapatikana katika hali za mioyo yetu, maisha yetu matakatifu, na roho wa maombi. Mamlaka yetu inapatikana katika utakatifu wa maisha yetu ya rohoni. Ushindi unapatikana kwenye barabara ya Msalaba! Sura ya V - Vita ya Rohoni
  • 44. Kanisa Linahitaji Kujua 44 Kwa hivyo, je! ‘kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake’ inamaanisha nini hasa kwa maisha yetu ya siku kwa siku? Tukiunganisha yale wanayoyasema Paulo na Yakobo, ni kwamba ni wakati tunapoyaweka maisha yetu katika mkono hodari wa Bwana. Ni wakati tunapoifungua mioyo yetu kwa ajili ya kuupokea ufunuo wa injili na kumruhusu Mungu kutenda kazi ndani yetu, inayotupeleka kwenye maisha ya imani, haki, maombi, n.k. – kwa maana nyingine, tunazivaa silaha zote za Mungu. Kwa jinsi hiyo tunaupata ushindi bila kumenyana na mapepo mchana kutwa. Na, Shetani anapokuja, tunahitajika tu kumpinga bila kufanya jambo lingine zaidi. Huo ndio wito, ndugu na dada zangu. Si kuingia kwenye mapambano ya kiroho dhidi ya mapepo… Maisha yetu yanapokuwa juu ya msingi sahihi, tunakuwa na mamlaka ya Mungu katika kumpinga Shetani. Kila anaposhambulia na sisi kumpinga, Shetani hana budi kukimbia. Sote tunakubali ya kuwa mapepo na roho chafu wapo, ila Yesu Kristo amewashinda wote (Wakolosai 2:15). Ndio maana, maisha yetu yanapokuwa yametiishwa kwa Mungu, hatutaogopa mapepo, wala kuyatafuta kila mahali. Mamlaka Ya Mungu Hebu sasa tuangalie Mathayo 16:18-19. Yesu anasema, “Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga
  • 45. 45 kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.” Bwana wetu alimpa Petro mamlaka kuliongoza Kanisa lake. Anamwambia, ‘Lo lote utakaloamua na kutamka duniani kulingana na mpango wangu na mapenzi yangu, kwa manufaa ya Ufalme, nitakutetea nikiwa mbinguni na nitalifanikisha.’ Mfano wa hii mamlaka ikitenda kazi unaonekana katika Matendo 5. Akiwa mtu wa imani na maombi, aliyeishi maisha matakatifu na ya haki, Petro alivaa silaha za Mungu, na akaongozwa na Roho Mtakatifu kunena sawasawa na mapenzi ya Mungu. Akafahamu kile Anania na Safira walichokuwa wamekifanya, na akanena kwa mamlaka ya Mungu. Alichofunga duniani kikafungwa na mbinguni. Ninamwona Petro akitekeleza jukumu lake la uongozi, pamoja na mamlaka aliyopewa na Bwana. Kumpinga Shetani Mara nyingine tunahitajika kumpinga Shetani, na kumzuia na kumsimamisha katika kazi zake. Lakini hii haiwezi kuwa mbinu tutakayotumia katika maisha yetu ya siku kwa siku. Paulo na Sila walipowekwa gerezani, hawakuanzisha kipindi cha vita ya rohoni; Biblia inasema walianza kumtukuza Mungu. Sura ya V - Vita ya Rohoni
  • 46. Kanisa Linahitaji Kujua 46 Hawakuhitaji kufunga mapepo au roho yo yote ili wafunguliwe. Mioyo yao ilikuwa sawa, maisha yao yalikuwa kwenye utaratibu wa roho na walimwabudu Mungu, huku wakifahamu ya kuwa ukombozi wao ulikuwa karibu. Muda si mrefu, Mungu akalitikisa gereza na kuwaokoa. Paulo alipofika Athene, Biblia inasema alichukizwa na sanamu na miungu waliyoiabudu. Je, Mtume alianza kufunga mapepo? Hapana! Alinena waziwazi, akiwaambia ya kuwa waliabudu kila aina ya miungu, ila yeye angewaambia habari za Yule waliyepaswa kumwabudu. Akanena habari za Mungu wake, na akawahubiria habari za Yesu Kristo. Tunaposoma kitabu cha Matendo ya Mitume, tunaona wanafunzi walitumia muda wao wakiihubiri Injili. Walipokutana na mazingira ya kuhitaji kumpinga adui, walifanya hivyo na kuendelea na kazi ya huduma. Hebu tusitekwe akili na kutumia muda mwingi tukishughulika na mapepo, badala ya kuiishi na kuishiriki Injili, na kumtumikia Kristo kwa mioyo yetu yote.
  • 47. 47 Sura ya VI Mahusiano Kabla ya Ndoa
  • 48. Kanisa Linahitaji Kujua 48 Kama kuna eneo Kanisani leo ambapo kuna mkanganyiko mwingi, na ambapo kuna ushahidi ya kwamba mfumo wa ulimwengu umejipenyeza tena na kuathiri namna Wakristo wanavyofikiri na kuenenda, ni katika mahusiano kabla ya ndoa. Ingawa hili somo linaweza kuonekana kama linawahusu tu vijana wanaotaraji kufunga ndoa, ukweli ni kwamba ni jambo linalohusika na Wakristo wote. Katika hili suala, Kanisa linaonekana kuamua kuchukua mitazamo miwili inayokinzana kabisa. Leo hii tunaona ama sheria au uhuru usiokuwa na mipaka. Katika baadhi ya makanisa kuna sheria kuhusu kile watu wanachoruhusiwa kufanya au kutokufanya, ilhali katika mengine, hilo suala halizungumziwi kabisa. Hakuna mmojawapo ya hii misimamo ulio sahihi! Ninaamini kwa dhati ya kwamba Kanisa limeutelekeza wajibu wake kwa kutokuchukua msimamo wa wazi wa Kibiblia kuhusu namna Wakristo, na hasa vijana, wanavyopaswa kuishi maisha halisi ya Ukristo, iwe ni kabla ya au baada ya kufunga ndoa. Katika kukaa kimya na kuruhusu viwango na fikra za kidunia kuingia Kanisani, tumeacha kuisimamia Kweli ya Injili, na tumejichanganya. Matokeo yake ni kwamba Wakristo wanajiingiza kwenye mahusiano yasiyokuwa ya rohoni na ambayo hayawasaidii kukua na kumtumikia Bwana katika njia sahihi na mara nyingi yakiwapelekea katika kutenda dhambi na kuwaondoa mbali na mpango wa Mungu kwa maisha yao.
  • 49. 49 Kwa ujuzi nilionao ninafahamu ya kwamba Injili inapoyakamata maisha ya vijana, hawamenyani, au kuhisi kusukumwa au kuchanganyikiwa juu ya kile kinachoruhusiwa katika mahusiano yao, au ni wapi wanapaswa kuchora msitari. Kinyume chake, hawahitaji sheria za kuwaambia ni lipi wafanye na lipi wasifanye. Wanafahamu waziwazi mpango wa Mungu ni upi juu ya maisha yao na wanatamani kutenda mapenzi ya Mungu, kubaki wasafi, na kuenenda katika njia inayompendeza Mungu. TunapoliangaliaNenolaMungukatikamtazamowake,ninashawishiwa kufikiri ya kwamba dhana zetu kuhusu kuchumbiana, kuwa na marafiki wa kike na marafiki wa kiume, na mahusiano kwa ujumla zitabadilika! Ulimwenguni, mahusiano ya karibu ya kimwili kabla na nje ya ndoa yanakubalika, na hata kushabikiwa. Vipindi vya uchumba vinahesabika kama nyakati za wahusika hao wawili kuona kama ‘wanafaana’. Hili mara nyingi linawapelekea katika kuwa na mahusiano ya kimwili kabla ya ndoa. Inasikitisha kwamba katika makanisa mengi vijana wanauiga mtindo huu huu, na wale walio katika nafasi za mamlaka – viongozi wa kanisa, wazazi, n.k., hawashughuliki na hili suala kwa umakini unaohitajika. Vijana wanaachiwa kujiamulia wenyewe mipaka katika hili suala nyeti, badala ya kupewa miongozo ya Kibiblia iliyo wazi. Hebu tuwe wazi tokea mwanzo ya kwamba Mungu hachanganyikani; Neno lake halijaficha jambo. Ndani mwake, tunaona maono na Sura ya VI - Mahusiano Kabla ya Ndoa
  • 50. Kanisa Linahitaji Kujua 50 mpango wake ulio dhahiri, kwa watu wake na kwa Kanisa lake. Ni wazi kwamba hataki tujichanganye na ulimwengu na njia zake. Na wala Mungu hataki sheria na kuhukumiana Kanisani mwake, ambavyo havina nguvu yoyote ya kumbadilisha mtu. Anachotaka ni Wakristo wote wahakikishiwe na Roho Mtakatifu kuhusu dhambi kupitia Injili ya Yesu Kristo ambayo inaweka mpaka ulio wazi na kutuonyesha tunapaswa tusimame juu ya msingi upi. Hii ndiyo maana ninaamini tunapaswa kurejea kwenye msingi – Neno la Mungu – ili tuone Mungu anasemaje juu ya hili suala. Miili Yetu Ni Viungo Vya Kristo Hebu tuangalie Mungu anavyoiona ndoa na mahusiano nje ya ndoa, na tutafahamu ya kwamba uhusiano wowote wa kimwili nje ya ndoa, uwe wa aina yo yote ile, unahesabika kuwa ni dhambi machoni pa Mungu. Si suala la ‘Tuweke wapi mipaka?’ kwa sababu tukijaribu kuweka mipaka ya aina yoyote, tutaivuka tu. Ni kama lile tangazo la breki za magari lisemalo, “Usianzishe jambo ambalo hutaweza kulizuilia!” 1 Wakorintho 6:15 inasema: “Je, hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!” Kwa hivyo, si roho zetu tu zilizounganika na Kristo; nafsi yetu yote ni moja naye. Mistari ya 16 – 17 inasema, “Au hamjui
  • 51. 51 ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, ‘Wale wawili watakuwa mwili mmoja.’ Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.” Paulo hapa anasema waziwazi ya kwamba ni lile tendo la ndoa linalowaunga watu wawili kuwa mwili mmoja, na hili linapaswa kuchukuliwa kwa uzito. Katu hatupaswi kusahau ya kuwa roho zetu, nafsi zetu na miili yetu imeungwa pamoja na Kristo. Siku hizi Wakristo wengi wanafanya wanavyopenda na miili yao, pasipo kutambua madhara ya rohoni yanayotokana na matendo yao. Kwenye kifungu hiki Paulo anaweka utofauti kati ya dhambi ya mwili na dhambi nyingine; katika zinaa unatenda dhambi dhidi ya mwili wako kwa sababu unafanyika kuwa mmoja na yule mnayeunganika naye kimwili. Uzinzi ni uhusiano wowote wa kimwili nje ya ndoa. Uongo, wizi, hasira, n.k., ni tofauti; haya ni matunda ya tamaa zetu za kimwili. Ikiwa Mungu aliamua kuweka utofauti kati ya dhambi ya mwili na dhambi nyingine, tunapaswa kuwa makini sana, na kuufahamu moyo wake katika hili suala. Msitari wa 18 unasema, “Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.” Hatupaswi kusahau ya kuwa miili yetu pamoja na roho zetu vimeungwa na Kristo, na tunapotenda zinaa ni jambo zito sana machoni pa Mungu. Mistari ya 19-20 inatukumbusha ya kuwa mwili wetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, na tunahimizwa, “mtukuzeni Mungu katika miili yenu.” Sura ya VI - Mahusiano Kabla ya Ndoa
  • 52. Kanisa Linahitaji Kujua 52 Mwili Unapaswa Kusulubiwa Katika Wagalatia 5:24-25, Paulo anasema, “Na hao walio wa Kristo wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.” Kila Mkristo ana uelewa fulani wa maana ya haya Maandiko. Lakini kwa wale wanaotamani kutembea rohoni, na walio tayari kuoa au kuolewa, yana maana zaidi maishani mwao. Tumeitwa kuisulubisha miili yetu na tamaa zake. Hii ndio maana tunahitajika kuusikia ujumbe wa Msalaba kila wakati kwa sababu unatukumbusha kujikana nafsi zetu na kuyapoteza maisha. Hakuna nafasi ya kudanganyana, wala kujaribisha mambo… Sisi ni watu waliochaguliwa ambao miili yetu ni mali ya Bwana Yesu Kristo. Iweje, basi, tuwaze ya kuwa ni sahihi kwa watu wawili waliochumbiana rasmi au vinginevyo, kufanya mambo wanayoruhusiwa kufanya tu mume na mke, eti kwa kuwa wamefikia uamuzi wa kuwa wenza? Uamuziwawatuwawiliwakuoanahukombeleniunapaswaumaanishe ya kwamba wataheshiminiana kwa utimilifu mbele za Bwana. Hadi siku ya kuoana, Bwana anawataka waishi maisha safi na matakatifu. Vijana, sikilizeni... isipokuwa una uhakika moyoni mwako ya kuwa uhusiano unaoingia umeanzishwa na Mungu, usithubutu kuuingia. Ukitaka kuufahamu mpango wake kwako, na mtu aliyekuandalia kuwa mwenza wako, fahamu ya kuwa atakufunulia.
  • 53. 53 Mkishafahamu ya kuwa ni mpango wa Mungu muoane, na ikiwa mnafahamu maisha ya utakatifu mnayopaswa kuishi kabla ya harusi, hakuna hatari. Mnaweza mkachumbiana na kutiana moyo katika kuheshimiana, kwa sababu mmehakikishiwa mioyoni mwenu ya kuwa mnapaswa kuishi maisha matakatifu mbele za Bwana hadi mtakapooana. Utakuwa na kicho kitakatifu cha uwepo wa Mungu katika maisha ya mwenza wako na kufanyika kielelezo kwa wengine. Ndio maana unapaswa uthibitike katika kile Mungu anachosema, ili pasiwepo na kubahatisha. Je, kuna mahusiano ya aina yoyote ya kimwili kabla ya ndoa yanayokubalika? Hasha! Neno la Mungu liko wazi sana juu ya suala hili. Manukato Ya Uhusiano Safi Na Mtakatifu Labda tayari uko katika uhusiano wa kimwili nje au kabla ya ndoa, na Bwana anakunenea ya kwamba si sahihi. Ushauri wangu ni kwamba utubu na ufanye uamuzi imara wa kuacha mahusiano yote ya kimwili mara moja; na usigeuke nyuma. Si jambo ambalo linafanyika kwa awamu, wala si jambo la kuchukulia kwa wepesi. Neema ya Mungu ipo kukusaidia. Na ikiwa ninyi wawili mnafahamu mioyoni mwenu ya kuwa mmeandaliwa kuoana, basi jitunzeni hadi siku hiyo, mheshimiane kama vile ndugu wa kiume anavyomheshimu ndugu wa kike kanisani, na katika kufanya hivyo muishi maisha matakatifu Sura ya VI - Mahusiano Kabla ya Ndoa
  • 54. Kanisa Linahitaji Kujua 54 na safi. Injili ya Msalaba wa Yesu Kristo inaleta jawabu, na kuchora msitari ulio wazi katika kila jambo tunalokabiliana nalo maishani mwetu. Inatusaidia kuenenda katika uhakikisho, na kwa maana hiyo tunatembea katika ushindi. Wakristo wa kila rika, walio kwenye ndoa na walio bado, wanahitajika wasikilize kwa umakini kile Mungu anachosema katika Neno lake ili waweze kuishi maisha matakatifu na kufanyika vielelezo kwa wengine. Je! si ni jambo la utukufu moyo wako unapokushuhudia ya kuwa kuna hali ya usafi katika uhusiano wa ndugu wanaotaraji kufunga ndoa? Hili linaleta harufu nzuri ya manukato inayopendeza. Ni ushuhuda mkuu kiasi gani wa nguvu ya Injili watu wawili wanapooana juu ya msingi huu! Ninaamini huu ndio mpango wa Mungu kwa Kanisa lake na kwa watoto wake. Hakuna haja ya kukata tamaa. Mungu yu hai; anaweza kuleta watu wawili pamoja. Anajua ya mbeleni. Anajua kila kitu kuhusu maisha yetu, na shauku yake ni sisi tuishi maisha safi na matakatifu. Ndio maana ni heri kusubiri, kuliko kujaribisha mambo. Fungua moyo wako; mwache Mungu azungumze na wewe na akushawishi. Kwa Yesu Kristo hakuna kuchelewa. Leo inaweza ikawa siku yako ya kumtangazia Bwana ya kuwa unaenda kuishi maisha yako ya Ukristo kabla ya ndoa kwa kulifuata Neno lake..
  • 55. 55 Sura ya VII Barabara ni Nyembamba
  • 56. Kanisa Linahitaji Kujua 56 Ni kweli kwamba nimeshutumiwa mara nyingi ya kuwa ninaweka mkazo kupita kiasi juu ya ujumbe wa Msalaba, na ya kwamba sihubiri kingine zaidi, wakati ambapo leo hii huu ujumbe unahubiriwa kidogo sana Kanisani. Lakini, mimi nami ningejibu hili kwa kuuliza swali: “Ni kwa nini ujumbe wa msingi wa Yesu Kristo – kile mitume wa mwanzo walichohubiri, na tunachosoma katika nyaraka za Paulo, Yakobo, Yohana na Petro – ni kwa nini hicho kisihubiriwe katika kila kanisa kila wakati?” Ujumbe wa Msalaba ndio ujumbe wa msingi wa Ukristo! Ninaamini kwa moyo wangu wote ya kuwa kila mchungaji angepaswa atamani kuuleta moyo wa kila Mkristo mahali ambapo ataona hitaji la kufanyiwa kazi na Bwana moyoni mwake na maishani mwake, na pia anamruhusu Mungu amfinyange. Kupitia hilo, huyo mtu atakua katika sura ya Kristo na katika kuyabeba maisha ya Kristo. Hii ndio maana kuna umuhimu kabisa wa kuuhubiri ujumbe wa Msalaba, ujumbe wa msingi wa maisha ya Ukristo. Kutokana na kile nilichopitia mimi mwenyewe ninaamini huwezi kuuhubiri huu ujumbe vya kutosha; kwa sababu sisi sote kama waamini tunahitaji kukabiliwa kunakoletwa na hii kweli, kila siku ya maisha yetu.
  • 57. 57 Kuna Wakristo wengi mno wanaoiacha imani yao kwa kuwa tu hawaisikii injili sahihi. Kwa kuuangalia mfano wa Kanisa la Mwanzo katika Neno la Mungu, tunaweza tukaona ya kwamba uwepo wa Mitume halisi waliokuwa wakihubiri Injili ya kweli kulilifanya Kanisa liendelee kusimama kwenye msingi sahihi na katika fundisho lenye uzima. Yesu mwenyewe alitoa tamko lisilokuwa na shaka juu ya maisha ya Ukristo aliponena kuhusu njia nyembamba. Ni kwa nini ujumbe wa Msalaba hauhubiriwi Kanisani leo? “Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.…” Mathayo 7:13. Maisha ambayo Yesu anazungumzia katika hiki kifungu ni maisha ya rohoni. Wakristo wote, basi, wanapaswa wasikilize kwa umakini mkubwa anachokisema. Bwana wetu anatuonyesha barabara tunayopaswa kuichukua ikiwa tunataka kuukwepa ‘upotevu’ pamoja na madhara yote ya kutokumtii. Ikiwa wewe unaamini ya kuwa maisha ya Ukristo ni ya baraka za mwilini na mafanikio – Ukristo usiokuwa na maumivu – basi hujayaelewa maneno ya Yesu, na ushuhuda wa maisha yake. Kitabu cha Matendo na nyaraka za mitume zinashuhudia Wakristo wa Kanisa la mwanzo wakipita katika nyakati ngumu, mitihani, majaribu, mateso na adha katika barabara hii ngumu na nyembamba. Sura ya VII - Barabara ni Nyembamba
  • 58. Kanisa Linahitaji Kujua 58 Kuteseka Kwa Ajili Ya Kukua Ikiwa tunatamani kuyaishi maisha ya ufufuo, maisha ya Kristo, maisha ya Roho, hatuna budi kukubali ya kwamba tumeitwa tuitembee barabara inayojumuisha shida; barabara inayojumuisha mateso na maumivu. Sisemi ya kwamba ni lazima tuyapitie maumivu ya mwilini, bali nazungumzia maumivu yanayokuja pale Mungu anapoyachukua maisha yetu na kuanza kuyashughulikia – tabia zetu, miili yetu, tamaa zetu za kibinafsi na nia zetu – na tunakubali kuvunjwa na kunyenyekezwa katika ujumla wa maisha yetu; ili, kwa neema yake, tuanze kukua taratibu na kufananishwa na sura ya Kristo. Katika Wakolosai 1:24, Mtume Paulo anatudokezea ni kwa nini alikuwa tayari kulipa gharama ya kuteseka: “Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake…” Mkristo anayeikimbia changamoto hii na asiyeikubali kazi ya Kristo maishani mwake, hawezi kutaraji kukua katika maisha yake ya rohoni. Katika jinsi ya roho, atabakia kuwa mtoto mchanga. Kazi Ya Utakaso Mungu anatusihi tuipitie hii barabara nyembamba kwa sababu hapa ndipo kazi yake ya utakaso itakapotimilika maishani mwetu. Mateso tunayoyapata mikononi mwake si kwa ajili ya kutukandamiza au
  • 59. 59 kutuangamiza. Tukijaribu kuyakwepa maumivu na mateso, matokeo yake tunaweza kuishia kuangamizwa na hali ile ile tunayojaribu kuikwepa. Wengi wetu tunataka kumfanyia Mungu mambo makubwa, ila tunapata shida kukubali ya kwamba, Mungu alilazimika kwanza kufanya kazi ya ndani na nzito maishani mwa wengi wa wale aliowatumia kwa namna ya kipekee. Hebu tafakari watu mashuhuri wa Mungu katika Agano la Kale waliotajwa katika Waebrania 11. Wote walikabiliwa, walipita katika majaribu, mateso, adha, pamoja na kurudiwa na Mungu: yaani, kujaribiwa kwa imani yao. Na, je! matokeo yake yalikuwaje? Walifanyika watu mashuhuri wa rohoni, mashujaa wa imani. Mungu yule yule anatuita tuipitie barabara ile ile nyembamba katika siku za leo. Kulipa Gharama Je! unaamini ya kuwa Ibrahimu alijawa na furaha alipoamua kumwamini Mungu na kumtoa mwanawe dhabihu? Atakuwa aliteseka sana alipokuwa njiani wakielekea mahali pa kutolea dhabihu pamoja na Isaka; ila aliamua kuutii mpango Mungu aliokuwa nao kwa maisha yake, na Mungu akamzawadia. Je! Musa alilipa gharama alipoamua kubeba shutuma ya Kristo na kuteseka pamoja na watu wa Mungu, badala ya kuzifurahia hazina za Misri? Je! Habili alikuwa na huzuni alipoelewa ya kuwa alipaswa kumtolea Bwana wazao wake wa kwanza wa mifugo? Mtafakari Nuhu, je! alikata tamaa kwa sababu hakuna mtu Sura ya VII - Barabara ni Nyembamba
  • 60. Kanisa Linahitaji Kujua 60 aliyemjali na wote walimdhihaki? Hapana! Watu hawa walimtii Mungu, walipita katika mitihani na majaribu; walilipa gharama. Mioyoni mwao, walikuwa tayari kuipitia barabara nyembamba; imani yao iliimarishwa, na walipata kibali kwa Bwana. Leo hii, tunayafananisha maisha yetu na mateso na kifo cha Kristo, kwa sababu tumeitwa kuipita njia hiyo hiyo ngumu, na hatuwezi kuikwepa. Mitihani Na Majaribu Ninaamini hakuna maelezo sahihi kuhusu wito huu kuliko yaliyo katika Wafilipi 1:29 ambapo Paulo anasema: “Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake…” Katika 2 Wakorintho 4:8-9, anasema “… Pande zote twadhikika, bali hatusongwi; twaona shaka, bali hatukati tamaa; twaudhiwa, bali hatuachwi; twatupwa chini, bali hatuangamizwi.” Kwingineko, Mtume Yakobo ananena juu ya mitihani na majaribu ya imani yetu. Hayo ndiyo mambo tunayopaswa kutarajia kwenye barabara nyembamba. Kama Paulo, sisi pia tunajikuta tumesongwa pande zote lakini tunasonga mbele; tukitatizwa, lakini tukimtumainia Mungu; tukikataliwa kwa ajili ya Yesu, lakini tungali wenye furaha. Sisi pia tunafahamu ya kuwa hatuna budi kuyapitia mambo hayo kama Yesu, Mitume, na Wakristo wa Kanisa la Mwanzo walivyopitia; hili ndilo fungu letu. Huu ndio Ukristo halisi! Mara tunapoamua kumfuata Yesu, tunaitwa tuyafananishe maisha yetu na mateso yake. Yesu alituonya
  • 61. 61 mapema ya kuwa mambo yangekuwa hivyo. Lakini, wakati kila jambo linapoonekana kugubikwa na giza na hali inakuwa ya kukatisha tamaa, hebu tukumbuke ya kuwa kuna kusudi katika hayo yote. Katika hayo tutauona ukombozi wa Mungu wetu na katika hayo tutakua rohoni. Kusudi La Mateso Waebrania 12:4 inasema: “Hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi.” Kwa maana nyingine, mioyoni mwenu hamjafika mahali pa kuchukizwa na dhambi kabisa kabisa. Katika 1 Petro 4:1 tunasoma: “Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi.” Ili kuelewa kinachozungumziwa katika hii mistari, ni lazima tuikamate roho wa Injili. Vinginevyo, haitakuwa rahisi kwetu kuelewa ni kwa nini tunaitwa kushiriki katika mateso ya Kristo. Hakika Yesu hakutaka tu tupite katika mateso na shida bila sababu. Ni lazima kutakuwepo na kusudi, lengo, katika haya mambo. Nalo ni nini? Matunda ya maisha ya jinsi hii ni uzima wa Kristo ndani yetu; ili tuweze kufanana naye. Paulo anasema katika Wafilipi 2:5, “Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo…”; kwa maana nyingine, iweni na nia aliyokuwa nayo Yesu, alipojinyenyekeza na kuonja kifo cha Msalaba. Matokeo yake ni kwamba Mungu alimwadhimisha mno. Sura ya VII - Barabara ni Nyembamba
  • 62. Kanisa Linahitaji Kujua 62 Kufanyika Kielelezo Hatimaye, hebu tuangalie Waebrania 12:5-6, ambapo tunahimizwa kutoyadharau marudia ya Bwana, kwani anatutendea kama wana, wa kike na wa kiume... Ikiwa tunatamani kuhesabika kama wana nyumbani mwa Mungu Baba yetu na kupata kibali kwake, ni lazima tumruhusu atufinyange na kuturudi. Mwandishi anamalizia hiyo sura kwa kuzungumzia maumivu yatokanayo na marudia; si wakati wa furaha, tunateseka Mungu anapotuvunja na kutufinyanga, anapofanya kazi maishani mwetu, lakini hili huleta matunda ya haki, maisha matakatifu; matunda ya utakaso. Katika kuichukua barabara nyembamba, hatuna budi kukubali ya kuwa ni jambo ambalo Mungu ametuandalia, ili tuwe mifano, na vielelezo kwa ulimwengu. Barabara Ya Utakaso Hii ndiyo barabara ya utakaso. Tunatakaswa, na kufanyika zaidi na zaidi kama Kristo. Kwenye hii barabara nyembamba, pamoja na makemeo, marudia na maonyo yake – yanayoelezewa kuwa ni ‘kwa faida yenu’ – ndipo tunapoandaliwa “tuushiriki utukufu wake”, na kuleta “matunda ya haki yenye amani” Waebrania 12:10-11. Hakuna njia nyingine ya kushughulika na dhambi yetu isipokuwa ni kuyafananisha maisha yetu na mateso ya Kristo. Tunaweza kuwa na
  • 63. 63 uhakika wa kukua katika Ukristo wetu na kufanyika watu wa rohoni pale tu tutakapoichukua barabara nyembamba, na kudumu juu yake. Hii ndiyo siri ya maisha yenye ushindi. Sisi watu wa Kanisa tunapaswa kubadili mtazamo wetu, na tuache kuendelea kuikwepa barabara nyembamba. Ni sehemu ya mpango maridadi kabisa Mungu alionao kwa ajili yetu. Na hapo, kama wale mashujaa wa imani waliotajwa katika Waebrania 11, tutakuwa na uhakika wa kusimama imara, na kuzikamilisha mbio zetu. Kamwe tusisahau ya kwamba barabara nyembamba ndiyo iendayo uzimani! Sura ya VII - Barabara ni Nyembamba
  • 65. 65 Sura ya VIII Kanisa Litakabiliwa
  • 66. Kanisa Linahitaji Kujua 66 Ninapoiangalia hali ya Kanisa la leo, nina hakika Wakristo wengi wanahuzunishwa na kile wanachokiona. Kwa namna nyingi hakuna utofauti kati ya mwenendo wa Wakristo wa karne ya 21 na maisha waliyoishi wana wa Israeli enzi za Yeremia na manabii wengine wa Agano la Kale. Katika siku za leo inaonekana ya kwamba, mara nyingine tena, watu wa Mungu wanaelekezwa katika kufukuzia mambo yasiyowafaidi. Siku hizo, kutokana na upendo wake kwa watu wake, Mungu alituma watu kuwaonya juu ya hatari za yale waliyokuwa wakifanya na athari za kuendelea kumpinga. Leo tumebarikiwa kwa kuwa na Neno la Mungu, Biblia, inayotuonya, kutuhimiza na kututia moyo. Zaidi ya hayo, tunayo mifano ya Yesu Kristo, pamoja na Kanisa la Mwanzo, inayotutia nguvu kubaki kwenye hiyo ‘barabara nyembamba’. Zaidi ya hayo pia, tuna ujumbe wa Msalaba – nguvu ya Mungu – unaotuwezesha kuishi maisha yenye ushindi na kulinda fundisho la uzima. Kutokana na hilo, hakika inasikitisha kuona Wakristo wakitafuta baraka ‘zinazopita’ ilhali ‘nguvu ya Mungu’ ipo kwa ajili yao. Ushuhuda wa Kanisa dhaifu, na lililojaa migawanyiko, hakika hauwezi kumfurahisha Mungu. Isipokuwa Kanisa liurudie ujumbe wa msingi wa Ukristo, litaendelea kupeperushwa na kila upepo wa elimu unaojitokeza. Nina hakika ya kwamba Mungu anataka kutuonya juu ya baadhi ya mambo yanayoendelea Kanisani katika siku za leo. Katika siku
  • 67. 67 tunazoishi Kanisa litakabiliwa: katika mwenendo wake, katika mahubiri na mafundisho yake, na katika namna Wakristo wanavyohimizwa kuyaishi maisha yao. Imani yangu ni kwamba kupitia kuhubiriwa kwa ujumbe wa Msalaba, watu wa Mungu watakabiliwa. Katika siku zake, nabii Yeremia, kupitia maagizo aliopewa na Mungu, hakuacha kuwaonya Waisraeli juu ya kile ambacho kingewapata kama wangeendelea katika njia zao zenye uovu. Wakati ule walikuwa wakifukuzia vitu vingine vingi badala ya Mungu. Yeremia 1:9-10 inasema, “...Tazama, nimetia maneno yangu kinywani mwako; angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung’oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.” Sote tutakubaliana ya kuwa mara nyingi maonyo huja wakati mambo yanahitajika kubadilika. Katika siku hizi za mwisho, ninaamini Kanisa litakabiliwa katika namna linavyomtumikia Mungu, na katika mambo yanayoivuta mioyo ya watu wa Mungu! Neno la Mungu linasema ya kuwa mambo yaliyofanyika katika vizazi vya nyuma yalikuwa ni mifano kuvionya vizazi vya mbeleni. Kwa mfano, katika 1 Wakorintho 10:11 tunamwoma Mtume Paulo akitamka ya kuwa mambo yote yaliyowapata Waisraeli jangwani yaliandikwa kwa ajili yetu, sisi waamini wa Agano Jipya; “Basi mambo hayo yaliwapata kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.” Tunaishi katika nyakati ambapo maisha ya juu juu, au ya kurushwa huku na huku na kila aina ya upepo, hayana nafasi tena. Vinginevyo tutajikuta tukivutwa na ulimwengu haraka sana, Sura ya VIII - Kanisa Litakabiliwa
  • 68. Kanisa Linahitaji Kujua 68 pamoja na mafundisho ya uongo, na hatimaye kunaswa katika mtego wa adui. Tunafahamu kilichowapata wana wa Israeli kutokana na kutotii kwao na uasi wao. Lakini hata hivyo wao, pamoja na viongozi wao wa kiroho, walipewa onyo baada ya jingine. Katika Yeremia 2:8 Mungu anawakemea waziwazi kwa kutafuta mambo ambayo hayatawafaidia: “Makuhani hawakusema, Yuko wapi BWANA? Wala wana-sheria hawakunijua; wachungaji nao waliniasi, nao manabii walitoa unabii kwa Baali, wakafuata mambo yasiyofaidia kitu.” Mungu anarudia tena kemeo lake katika msitari wa 11, “Je! taifa wamebadili miungu yao, ingawa si miungu? lakini watu wangu wameubadili utukufu wao kwa ajili ya kitu kisichofaidia.” Nina hakika unatambua ya kuwa mali ya kidunia haiwezi kutuletea badiliko la rohoni, au kutuleta katika utu uzima rohoni na ukamilifu katika Kristo! Ndio maana wakati umefika Kanisa likabiliwe na ujumbe wa Msalaba wa Yesu Kristo; injili pekee inayoshughulika na mwili, inayokabili maisha yetu na hali za mioyo yetu; na inayotupa kuyatamani mambo ya Roho yatakayotufaidia. Katika msitari wa 13 Mungu anawakemea watu wake: “Kwa maana watu wangu hawa wametenda maovu mawili; wameniacha mimi, niliye chemichemi ya maji ya uzima, wamejichimbia mabirika, mabirika yavujayo, yasiyoweza kuweka maji.” Birika linalovuja halina kazi yoyote. Vivyo hivyo na sisi leo, tunajenga maisha ya ubatili kwa kutafuta vitu ambavyo tumeaminishwa Kristo atatupatia, badala ya kuutafuta uzima wake; uzima wa ufufuo, uzima wa Roho. Mimi
  • 69. 69 sina neno na wale Mungu mwenyewe anaoamua kuwabariki na kuwafanikisha, hasa ninapofahamu ya kuwa shauku ya mioyo yao ni kuubariki Ufalme. Lakini, ninapata shida Wakristo wanapohimizwa kutafuta mali ya ulimwengu huu badala ya uzima wa Roho. Hata hivyo, hakuna mahali kwenye Biblia tunapohimizwa kutafuta mali ya dunia; kinyume chake, katika Wakolosai 3:1-2 Paulo anatuagiza waziwazi, “Basi ikiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.” Kukemewa Na Kukabiliwa Ni wazi kwamba si kila mtu atakayepokea makemeo kwa moyo wa toba. Mungu alimtahadharisha Yeremia kwamba ujumbe aliokuwa awaletee watu ungezua upinzani mkubwa. Yeremia 1:19 inasema, “Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamojanawe,asemaBWANA,ilinikuokoe.”Waisraeliwalikujakinyume na kile alichokuwa akisema; hasa kauli yake ya kuwa alichokuwa akisema kilitoka kwa Mungu. Kwa sababu mioyo yao ilikuwa mbali na Mungu, Waisraeli walikataa kusikiliza; walifurahia kukimbizana na mambo yaliyoiridhisha miili yao. Matokeo yake ni kwamba walimpinga Yeremia kwa muda wa miaka 40! Kanisa la Yesu Kristo la mwaka 2010 lina hali inayofanana na hiyo: watu wa Mungu wanahimizwa kutafuta vitu visivyoweza kuwatosheleza kiroho. Wakati huo huo, Msalaba wa Sura ya VIII - Kanisa Litakabiliwa
  • 70. Kanisa Linahitaji Kujua 70 Yesu unapohubiriwa leo hii, unaleta mwanga Kanisani; unakemea; na ndio maana, si ajabu, watu wengi hawaupendi. Msalaba Ndio Msingi Wahubiri wanapounda fundisho kutokana na vitu vya juujuu, wanaondoa hamu ya kukua kiroho mioyoni mwa Wakristo. Msalaba wa Yesu Kristo unapaswa uwe sehemu ya maisha ya wale wanaosimama madhabahuni. Na Wakristo wanapaswa kulishuhudia hilo; ya kwamba hawa watu wamevunjwa, na wanaendelea kuvunjwa na Mungu; ya kwamba wamefanyika mifano, vielelezo; na ya kwamba hawaneni tu elimu ya kibiblia. Hii ndio maana ujumbe wa Msalaba unapaswa kurudi Kanisani sasa, ili mioyo ya Wakristo irejeshwe kwa Kristo; hadi kuyafananisha maisha yao naye katika kuteswa kwake na kifo chake. Hii ndiyo njia pekee ya kuushiriki uzima wa ufufuo, ambao ni maisha ya Kristo anayoyaishi ndani yako na ndani yangu… tumaini la utukufu! Kuna hicho kipengele cha mateso na kifo ambacho kwa kiasi kikubwa kimepotea Kanisani; huo ndio ujumbe wa Msalaba. Hatuwezi kuukimbia. Ukristo unaotosheka tu na kuja kanisani, kubarikiwa, na ‘kuwa na wakati mzuri’ na wenzako kabla ya kutoa sadaka yako, kwa kweli hii ni dini tu! Inanihuzunisha, ila ninaamini ya kuwa mengi ya mambo yanayoendelea Kanisani leo hii ni dini tu; mikakati, kanuni,
  • 71. 71 mbinu, vyote vikiwa vimetokana na hekima ya mwanadamu… kinachosikitisha zaidi ni kwamba katika mengi ya makanisa, pesa ndio msingi wa kila kitu. Biblia inatamka waziwazi ya kwamba ujumbe wa Msalaba ndio msingi wa maisha yetu ya Ukristo. Neno la Mungu lina mengi zaidi kwa ajili ya roho zetu badala ya kuhubiri mfululizo kuhusu mafanikio, pesa, kutoa na baraka. Waalimu Kumi Elfu… Katika 1 Wakorintho 4:14-15 Paulo ananena na Wakorintho wa mwilini waliokuwa wamerudi nyuma katika kuwakumbusha na kuwaonya: “Siyaandiki hayo ili kuwatahayarisha; bali kuwaonya kama watoto niwapendao. Kwa maana ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndiye niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili.” Kila mahali alikokwenda aliweka msingi mmoja tu na alihubiri injili moja katika makanisa yote: Injili ya Msalaba. Hawa Wakorintho walifahamu fika kile Mungu alichotaraji kutoka kwao, na kazi aliyohitaji kufanya ndani yao, ili wafanyike wanafunzi, watumishi, na vielelezo kwa ulimwengu uliowazunguka. Msalaba unapokosekana, mlango unakuwa wazi kwa mioyo yetu kuvutwa na mambo yasiyokuwa na faida. Hilo ndilo lililowapata Wakorintho. Walisikiliza injili nyingi. “Mnaweza kuwa na waalimu kumi elfu.” Katika msitari wa 15 Paulo alikuwa anamaanisha: ‘Mmesikiliza wahubiri wengi, mmesikiliza imani nyingi, mmejifunza mbinu nyingi; Sura ya VIII - Kanisa Litakabiliwa
  • 72. Kanisa Linahitaji Kujua 72 lakini angalieni hali yenu… kuna vita, wivu, na zinaa kati yenu!’ Mara tu unapouondoa msingi wa msalaba, matokeo ni Wakristo wanaoenenda mwilini; waliorudi nyuma na walioshindwa! Ikiwa hujazaliwa katika Injili ya Msalaba, utaitafsiri Biblia kwa manufaa yako binafsi. Hautataka kusikia juu ya mitihani na majaribu, adha, na mateso; juu ya kukemewa, kuonywa na kutubu; juu ya kuifia nafsi. Mfano mzuri wa hili ni wakati Wakristo wanaponukuu Wafilipi 4:13, “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.” Wanachokazia tu ni ile sehemu ya kwanza ya hili andiko: ‘Nayaweza mambo yote.’ Lakini hebu tuangalie andiko zima tukianzia msitari wa 10… ”Nalifurahi sana katika Bwana, kwa kuwa sasa mwisho mmehuisha tena fikra zenu kwa ajili yangu, kama vile mlivyokuwa mkinifikiri hali yangu; lakini hamkupata nafasi. Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo nayo. Najua kudhiliwa tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.” Katika kuliangalia kwa ukaribu, tunaona kitu tofauti kabisa, linazungumza habari za Paulo alivyoubeba msalaba wake. Mazingira yo yote kwake – wingi au uchache – na kwa moyo mnyenyekevu, neema ya Mungu na nguvu za Mungu vilimpitisha katika hayo yote. Hii neema itakuwepo katika hali zote, nzuri au mbaya. Hiyo ndiyo roho, ndio moyo, ambao Paulo anawasilisha hapa; huu ndio moyo wa Kristo, roho wa Injili.
  • 73. 73 Kumfahamu Kristo Usipozaliwa katika Injili ya kweli, utapata shida kukubali kile Mungu anachotaka kwako. Mwili wako utang’ang’ania vitu vya mwilini, na utakuzuia katika kuyafananisha maisha yako kikamilifu na Kristo. Katika Wafilipi 3:10-11 Paulo anasema, “…ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake; ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu.” Tunawezaje kusema, sisi kama Wakristo, ya kuwa tunataka kumjua Kristo pasipo kuwa tayari kuyafananisha maisha yetu na maisha yake? Kama ilivyokuwa kwa Paulo, vivyo hivyo na sisi pia, tunaitwa katika ushirika wa mateso yake, ili tuweze kuushiriki uzima wa ufufuo. Vinginevyo, tutakuwa tunanena tu juu ya kule kuzaliwa mara ya pili. Lakini, hatuwezi kuishia tu hapo… kwani katika msitari wa 15 Paulo ananena zaidi ya kuzaliwa mara ya pili. Anatuhimiza kuwa na hali ya moyo ambapo, hata kama hatuelewi sana au kukubaliana na ufunuo wa Kristo na namna tulivyoitwa kujifananisha na yeye katika mateso yake, kifo chake na kufufuka kwake, bado tunaweza kumwamini Mungu kwamba atatufunulia anachohitaji kutufunulia. Sura ya VIII - Kanisa Litakabiliwa
  • 74. Kanisa Linahitaji Kujua 74 Msalaba Ndio Uzima Wako Ninakutia moyo, mpe Mungu nafasi, kwa njia ya Yesu Kristo, aidhihirishe nafasi stahili ya Msalaba wake maishani mwako, kama anavyosema katika Mathayo 16:24: “Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.” Maisha yetu ya Ukristo yanapaswa kuwa na msingi mmoja tu: “Yesu Kristo naye amesulubiwa!”
  • 75. 75 Sura ya IX Yesu Anaita Tena
  • 76. Kanisa Linahitaji Kujua 76 Ni jambo la kawaida kwa mwanadamu kutaka starehe na utoshelevu, na kutotaka mabadiliko. Sisi kama Wakristo tunaweza tukawa na hali iyo hiyo kuhusu mwenendo wetu na Mungu; watu waliotosheka na wanaoishi maisha mepesi katika mfumo wa Ukristo uliozoeleka. Ninaamini kwa dhati kabisa ya kuwa wimbi lingine la Mungu linakuja hivi karibuni na ya kwamba Wakristo wanapaswa wafahamu mambo yaliyoko mbeleni. Ni lazima tuelewe pia ya kuwa kila wimbi la Mungu huambatana na kutetemeshwa. Mwanzoni miili yetu itataka kulipinga jambo hili. Lakini wale wanaotamani kwa dhati kumtumikia Mungu na kumfuata, watakuwa tayari kukubali chochote atakachotaka kwao. Ni lazima tuhakikishe ya kuwa kwamba tu wachungaji, viongozi au Wakristo ‘wa kawaida’, tunamtafuta Bwana na kutaka kujua kile Roho Mtakatifu anacholiambia Kanisa leo. Bila shaka, Mungu anatuita tulete ujumbe utakaowalisha watu wake; utakaowafikisha katika utu uzima na uhuru katika Kristo. Ikiwa Yesu anarudi hivi punde, hatakuja kulichukua Kanisa lisilokuwa na nguvu wala utakatifu. Ujumbe wa Msalaba ndiyo Injili pekee yenye nguvu ya kulibadilisha Kanisa na maisha ya Wakristo; na kuwaleta katika kuichukua sura ya Kristo. Katika historia ya Kanisa, zimekuwepo nyakati na majira ambapo Mungu aliwaita wanaume na wanawake kwa makusudi mbalimbali ili kutekeleza mapenzi yake hapa duniani. Nina hakika ya kwamba huu sasa ni wakati ambapo Yesu anawaita wanaume na wanawake kuupokea ujumbe mahsusi, ufunuo: injili ya Msalaba, fundisho la msingi la Ukristo.
  • 77. 77 Yesu ana mpango na maono kwa Kanisa lake, na anataka yatimizwe. Kwa bahati mbaya, anapoita, si kila mtu anayesikiliza au kujali… Lakini hili halimzuilii, kwa sababu mipango yake ni lazima itekelezwe. Haiyumkiniki kwamba Yesu atalijia Kanisa butu lisilokuwa na uhai; na, zaidi ya hapo, Kanisa lililostarehe, lililojitosheleza, lililojaa udini. Atachagua wanaume na wanawake; atawaita, na kuwapa changamoto, vile vile kama alivyowachagua wanafunzi 12 waanzishe Kanisa. Alimwita pia Mtume Paulo kwa kusudi maalum: “Lakini Mungu…akaniita kwa neema yake…ili niwahubiri Mataifa habari zake…” Tazama Wagalatia 1:15. Muda wa Mungu wa kufanya jambo unapowadia, hulifanya. Katika miaka 40 au 50 iliyopita, Mungu alileta ufunuo mpya kwa Kanisa; ulikuwa mzuri nasi tunamsifu kwa huo. Lakini, je! tunaona nini leo? Tunaona Kanisa lililopoteza nguvu yake, utakatifu, na kutengwa kwake na ulimwengu. Ni nini kilichochukua nafasi? Kuchanganyikana, dhambi, mafundisho ya uongo, na misisimko! Lakini, tena, Yesu anawaita wanaume na wanawake ambao atawafunulia ujumbe wa kweli wa Msalaba, ili waweze kuishi maisha halisi yenye ushindi, na watakaoihubiri hiyo injili na kuitetea. Si kwa bahati mbaya, basi, ikiwa wewe binafsi unahisi ya kwamba maisha ya Ukristo si tu kustarehe na kukubaliana na kila jambo linalofanyika Kanisani siku hizi. Sura ya IX - Yesu Anaita Tena
  • 78. Kanisa Linahitaji Kujua 78 Jambo Jipya Roho Mtakatifu anabisha kwenye mioyo ya Wakristo wengi; viongozi wa makanisa, wanaume na wanawake, duniani kote; watu waliochoka na ambao hawakubali ya kuwa Kanisa la Yesu Kristo halina zaidi ya hiki wanachokiona. Ninaamini kwa moyo wangu wote ya kuwa kuna jambo jipya, jambo zuri, ambalo Roho Mtakatifu anajiandaa kuinenea mioyo ya hawa Wakristo. Tayari yuko kazini, akiandaa mioyo kuipokea Injili ya Msalaba wa Yesu Kristo, hata kama tunaweza tusiione hiyo kazi. Nina hakika ya kuwa Wakristo wengi wanahisi mioyoni mwao ya kuwa kuna jambo jipya, jambo tofauti, linalokuja. Wengine wenu mnaweza kuwa hata mmewaza ya kuwa haya mawazo yanatokananauasindaniyenu,auyakwambamnauhurubinafsikatika kutokukubaliana na mengi ya yale yanayohubiriwa madhabahuni leo hii. Unajiuliza maswali... juu ya maisha yako ya Ukristo, na hali ya moyo wako. Huyu ni Yesu anayeita! Hapa hatuzungumzii wito kwa ajili ya huduma, bali ni Yesu anayekuita kama Mkristo uishi maisha ya injili ya kweli, umruhusu Mungu kuikamilisha kazi ile njema aliyoianza ndani yako.
  • 79. 79 Adui Za Msalaba Lakini, kama ilivyokuwa siku za Mtume Paulo, wengi watasikia na kupinga mahubiri ya ujumbe huu na watakuwa ni adui za Msalaba; tazama Wafilipi 3:18: “Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi kuwa ni adui za msalaba wa Kristo…” Inasikitisha kwamba si wahubiri au Wakristo wote walio tayari kuupokea ujumbe wa Msalaba na changamoto inayoletwa na maisha ya Ukristo. Daima kutakuwepo na watu ndani ya Kanisa watakaoinuka na kupingana na kile Mungu anachotaka kufanya. Kuanzia enzi za Luther wakati wa Matengenezo hadi leo upinzani umekuwepo ndani ya Kanisa; maadui wamepingana na kile Mungu anachotaka kufanya Kanisani mwake. Matokeo yake, tutakutana na wale wanaoamini ni jukumu lao ki-imani kuyapinga mahubiri ya injili ya Msalaba. Msalaba Pekee Paulo anasema katika 1 Wakorintho 2:2, “Maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu, ila Yesu Kristo, naye amesulubiwa.” Injili ya Msalaba ndio msingi wa Ukristo; hii Injili ndiyo iliyowapa changamoto Wakristo katika Kitabu cha Matendo. Leo, Yesu anaita tena. Vile vile kama Paulo anavyonena katika Wagalatia 1:11 jinsi alivyopokea Sura ya IX - Yesu Anaita Tena
  • 80. Kanisa Linahitaji Kujua 80 ufunuo moja kwa moja kutoka kwa Yesu Kristo, ninaamini Bwana anachagua wanaume na wanawake, anawatenga, anaiandaa mioyo yao na kuwafunulia ujumbe wa Msalaba. Huu ujumbe ndio ufunuo ule ule uliokuwepo katika Kanisa la Mwanzo; unawaalika Wakristo kuitika na kujisalimisha; kujihesabu ya kuwa wamepoteza maisha yao na kutoshikilia kitu cho chote. Huu ushawishi wa moyoni unatokana tu na injili ya Msalaba. Wanaume na wanawake wataanza kusoma Maandiko na kuyafananisha maisha yao na kile wanachokisoma. Viongozi wa makanisa watayadhihirisha maisha yao madhabahuni, na kuikiri kazi ambayo Mungu anahitaji kufanya maishani mwao. Wakristo kutoka kila rika na kabila wataanza kufahamu ya kuwa Ukristo wa kweli unahusu kupoteza maisha yetu ili Yesu aishi ndani yetu. Zaidi na zaidi wachungaji na washirika watakubali ya kwamba injili hii ndiyo iliyokosekana Kanisani leo hii. Si Ujumbe Mpya Yesu alifundisha ya kwamba barabara ni nyembamba na ya kwamba kuna gharama katika kumfuata, inayojumuisha kujikana nafsi, mateso, adha, na kuyapoteza maisha yako. Wakristo wanapoanza kufahamu ya kwamba Mungu anataka kuwaumba katika sura ya Mwanawe watakuwa tayari kuikubali kazi anayotaka kufanya maishani mwao. Kama Kanisa tutatambua ya kuwa mwenendo wetu hauna uhusiano
  • 81. 81 na sisi, bali yeye – Yesu akiishi ndani yetu; ni kujifananisha na yeye kikamilifu. Katika Warumi 6:3-4, Paulo anasema ya kuwa tulizikwa pamoja na Kristo kwa njia ya ubatizo, na ya kwamba tunapaswa tuenende katika upya wa uzima, kama Kristo alivyofufuliwa kutoka kwa wafu. Tunaposhiriki mauti yake, tunashiriki pia katika uzima wake. Huu ndio upya wa uzima; huu ndio uzima wa Kristo! Haya ndiyo maisha ya ushindi ambayo Yesu anatuitia… utimilifu wa Kristo ndani yetu! Huu ndio ujumbe waliohubiri Mitume wa kwanza, na ambao ndio Kanisa la Kwanza lililouishi. Ujumbe huu si mgeni; utaukuta kwenye kila tafsiri ya Biblia. Kufanya Uamuzi Watu wengi wataanza kuusikia wito na watakabiliwa na uamuzi. Wengine watasikia na kuupinga wito, lakini wengi watasikia na kuuitikia.Kwahaoataifunuainjiliyakwelinahitajilaolakujifananishana Kristo. Pamoja na upinzani na adha zitakazowakabili, watakapoanza kuhisi Yesu akiita, watajawa na shauku ya kuyaishi hayo maisha. Fahamu zao zinaweza zikataka kujadiliana, lakini mioyo yao itasema, ‘Ndiyo, Bwana. Niko tayari kulipa gharama ya kukufuata, kuiishi hii injili; kufanyika udongo mikononi mwa mfinyanzi; kubadilishwa, kutetemeshwa, kugeuzwa; kufanyika kama wewe, Bwana Yesu.’ Watawatafuta wale wanaoishi na kuihubiri Injili. Wataona utofauti ulio Sura ya IX - Yesu Anaita Tena
  • 82. Kanisa Linahitaji Kujua 82 wazi kati ya injili ya kweli ya Yesu Kristo na injili nyingine zote watu wanazohubiri na kuziishi. Katika Wafilipi 1, Mtume Paulo anasema aliitwa aitetee injili. Katika kuuitikia wito wa Yesu, wewe pia utalazimika kuweka msimamo na kusema: ‘Hiki si sahihi; yale siyo mafundisho yenye uzima!’ Utakabiliana na watesi na upinzani, lakini kwa neema ya Mungu utashinda. Hivyo ndivyo Paulo alivyoweza kusema: “Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo… bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami.” Kuuitikia Wito Wake Yesu anaita tena leo. Anabisha kwenye mlango wa moyo wako na anakuandaa uwe tayari kuuitikia huo wito. Ni upendeleo wa jinsi gani huo, ni heshima kuu kiasi gani! Je! uko tayari kuitikia wito wake?
  • 83. KanisaLinahitajiKujuaMikiHardy Kanisa Linahitaji Kujua Hebu sote tukubaliane ya kwamba kwa namna moja au nyingine Kanisa limeliacha fundisho la uzima, na matokeo yake yanaonekana katika maisha ya watu wa Mungu. Viongozi wengi wameathiriwa na mafundisho ya mafanikio ya miaka ya hivi karibuni, na wanatafuta kujinufaisha wenyewe. Wengine hawatambui ya kwamba injili ya Msalaba ndiyo nguvu ya Mungu itakayowafikisha Wakristo katika utu uzima rohoni. Umefika wakati tuyazungumzie mambo fulani ya msingi waziwazi, ili Wakristo watambue ya kwamba Bwana ana mambo mazuri zaidi kwa ajili yao, makusudi watembee katika uhuru na katika ushindi! 9 789994 901814 ISBN 978-99949-0-181-4 Church Team Ministries International | Trianon, Mauritius (230) 403 4500 | info@ctmi.org | www.ctmi.org CTMI ni mtandao wa Kikristo usio rasmi ulioanzishwa mwaka 2001 na timu ya viongozi kutoka nchi mbalimbali barani Afrika waliounganishwa pamoja na ujumbe wa msalaba na kazi ya Mungu maishani mwao.