Tanzania orphans street children and widows foundation(Towsf).ni taasisi isiyo ya kiserikali (NGO) yenye usajili no.00NGO/00006168 inayoshughulikia ustawi wa watoto yatima na wajane. Taasisi inahamasisha jamii ya watanzania kuona umuhimu wa kutoa misaada ya kielimu kwa watoto hawa.Taasisi imezindua mfuko maalumu wa kushughulikia masuala yote ya elimu kwa watoto yatima. mfuko unaitwa Towsf yatima education fund. kupitia mfuko huu watoto yatima wataweza kulipiwa ada,kununuliwa sare za shule pamoja na vitabu na madaftari. Kampeni ya kuchangia mfuko huu itadumu kwa miezi mitatu kuanzia tarehe01.07.2013 hadi tarehe31.09.2013. kampeni inashawishi kila mwenye uchungu na kundi hili achangie sh.30000.na kampeni imetazamia kuwafikia watanzania 1000.Ukiwa rafiki yangu wa karibu nakukaribisha kuchangia kwa manufaa yako hapa duniani na kesho kwa Mungu muumba. Njia za uchangiaji ni tigo pesa 0659996900.au kwenye akaunti no.0066001792.barclays bank. jina la account ni Tanzania Orphans, Street Children And Widows Foundation.unaweza changia 2500 kwa wiki au 10000 kwa mwezi au 30000 yote kwa pamoja.karibu sana. Mr.Imani Matabula M/kiti Towsf Taifa.
Good Stuff Happens in 1:1 Meetings: Why you need them and how to do them well
TOWSF YATIMA EDUCATION FUND
1. Ndugu…………………………………
YAH: MWALIKO WA KUCHANGIA ELIMU YA WATOTO YATIMA WAKITANZANIA.
UTANGULIZI.
Tanzania Orphans Street Children and Widows Foundation (TOWSF) ni taasisi isiyo ya
kiserikali (NGO) yenye Usajili No. 00NGO/00006168 inayoshughulikia mustakabali wa
watoto yatima, watoto waishio katika mazingira hatarishi (mitaani) na wajane. Taasisi hii
inahamasisha jamii ya Tanzania kuona umuhimu wa kutoa misaada ya kielimu, na
malezi kwa makundi haya na kuhakikisha kuwa watoto yatima wote wanasoma mpaka
wanahitimu masomo yao ili waweze kuja kulisaidia taifa lao na kuepuka kuja kuwa kizazi
tegemezi.
Taasisi imezindua mfuko maalumu wa taasisi hii unaoshughulikia masuala yote ya elimu
kwa watoto yatima. Mfuko huu unaitwa (TOWSF YATIMA EDUCATION FUND ). Kupitia
mfuko huu watoto yatima wataweza kulipiwa ada, kununuliwa sare za shule, vitabu na
madaftari kwa muda wa mwaka mzima.
Hivyo kutokana na umuhimu wako katika jamii yetu tunakuomba uwe sehemu ya
kuchangia mfuko kwa kutoa Tsh.30,000/ tu (elfu thelathini). Kampeni hii ni ya miezi mitatu
ambayo imelenga kufikia watanzania takribani elfu moja. Ikiwa utakuwa na uwezo
unaweza kutoa yote kwa awamu moja au unaweza kutoa shilingi elfu kumi(10,000/=)
kila mwezi ndani ya miezi mitatu.
Tunaamini kuwa utaunga mkono jitihada hizi za kuwakomboa watoto yatima kwani ni
sadaka kubwa sana mbele za Mungu.
OFISI YETU : Ofisi yetu ipo Mtaa wa matokeo Kata ya Mabibo wilaya ya Kinondoni Dar-
es- Salaam nyumba namba MTK/408.
NJIA ZA KUTOA MCHANGO WAKO
1. Unaweza kutoa pesa tasilimu na kumkabidhi aliyekukabidhi barua hii.
2. Unaweza tuma moja kwa moja ofisini kwetu kwa njia ya simu ifuatayo:
Tigo pesa namba 0659 996900.
3. Unaweza kupeleka kwenye Account yetu iliyopo katika bank ya Barclays A/C
0066001792. Jina la account ni TANZANIA ORPHANS STREET CHILDREN AND WIDOWS
FOUNDATION.
Uchangiaji huu umeanza tarehe 01/07/2013 hadi 31/09/2013 karibu sana TOWSF.
Watoto yatima na wajane wanastahiki kusaidiwa.
Muumba wetu ametusisitiza, tujitoe kwa hali na mali zetu tuwasaidie. Usiidharau pesa
utakayoitoa kuwa ni ndogo bali ina msaada mkubwa sana.
Natanguliza shukrani.
___________________
MR. IMANI MATABULA
MWENYEKITI TOWSF TAIFA
Tanzania Orphans, Street Children and Widows Foundation
P.O.Box 67620
Dar es Salaam
Tanzania
Phone: +255 652 600700,
+255 763 261711,
E-mail: info@towsf.or.tz
Website: www.towsf.or.tz