2. Kutokana na kwamba roho
pamoja na akili hufanya
kazi pamoja, nguvu ya
vitu hivyo viwili
hutegemea katika afya ya
mwili.
Hii hutwambia kuwa,
nguvu ya akili na ile ya
kiroho hutegemea sana
afya ya mwili ambayo
hupelekea hali njema
katika mifumo ya mwili.
3. Hivyo unapaswa kuhakikisha kwamba, jukumu ni lako kuboresha
afya yako, Katika viwango stahiki.
4. Wale ambao wangependa kuwa wabeba injili na pamoja na Mungu,
imewapasa kuwa tayari kufikia ukamilifu wa kila kiungo cha mwili na
kile cha akili.
5. Tabia zetu, nia zetu na
mitazamo yetu inapaswa
kuelekezwa sawia na
kanuni za afya. Kupitia
njia hii tunaweza kuwa na
afya iliyokubalika,
ambayo itasaidia
kufahamu, kufanya na
kuishi vyema angali
tukitofautisha wema na
uovu.
6. Katika hukumu, watu hawatahukumiwa kwa sababu waliamini uongo, bali kwa
sababu hawakuamini ukweli, na kwa sababu walipuuza kujifunza kile ambacho ni
kweli.
7.
8. Matokeo ya mwili katika akili na yale ya akili
katika mwili, hayapaswi kupuuzwa.
9. Kuna nguvu ya ajabu inayoongeza
afya ya mwili katika tabia kama zile
ambazo Yesu alikuwa nazo, kama vile
furaha, kujikana nafsi, kutokuwa
mbinafsi na kutoa shukrani.
Wakati ile nishati kama ya umeme
inapoamshwa katika bongo zetu
kupitia akili zetu, huupa mwili wote
nguvu, ambao unahusika na
kupambana dhidi ya magonjwa, na
kujenga ushindi katika tabia, katika
mambo ya kiroho, na katika maisha
ya kawaida.
10.
11. Ni mapenzi ya Mungu
kwamba watu wake
wawe na mafanikio
katika nyanja za kiroho
na Nyanja zingine za
maisha, ili waweze
kuishi kwa furaha na
asili. Hivyo wataweza
kuhamisha uzuri wa
asili katika uhusiano wa
upendo Mungu na watu
wake.
12. Wapendwa, hakuna njia ambayo
twaweza kumtumikia Bwana na
huku tukiacha afya ya mwili na
akili kando, badala yake kila
mmoja na aongeze bidii ili
kuhakikisha kuna furaha katika
Nyanja zote, kiakili, kimwili na
kiroho pia.