SlideShare a Scribd company logo
1 of 1
Download to read offline
TANGAZO MWANANCHI.CO.TZ JUMATATU, SEPTEMBA 14, 2020MWANANCHI18
1. Utangulizi
Mamlaka ya Elimu Tanzania (Tanzania Education Authority-TEA) ni Taasisi ya Umma iliyoanzishwa chini ya
kifungu cha (5)1 cha Sheria ya Mfuko wa Elimu Namba 8 ya Mwaka 2001, ili kusimamia Mfuko wa Elimu wa
Taifa ulioanzishwa chini ya Sheria hiyo. TEA inatekeleza majukumu yake chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia.
Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatekeleza Mradi wa Kukuza Ujuzi na Stadi za Kazi
(Education and Skills for Productive Jobs-ESPJ) ambao unapata ufadhili wa Benki ya Dunia na Serikali ya Jam-
huri ya Muungano wa Tanzania. Mradi wa ESPJ umekuwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa
Kuendeleza Ujuzi (National Skills Development Strategy – NSDS: 2016-2021). Aidha, Maeneo muhimu yanay-
olengwa katika utekelezaji wa Mkakati huu ni kuongeza ufanisi katika uzalishaji na pia kuongeza uwiano wa
wataalam wa fani mbalimbali katika Sekta sita (Kilimo Biashara, Utalii na Ukarimu, Nishati, Ujenzi, Uchukuzi
na TEHAMA) zenye mchango mkubwa wa kiuchumi nchini.
Mnamo mwaka 2017, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia iliipatia TEA jukumu la kuratibu na kusimamia
shughuli zote zinazohusu utekelezaji wa Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (Skills Development Fund-SDF) ambao
ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Kukuza Ujuzi na Stadi za Kazi (Education and Skills for Productive
Jobs-ESPJ).
Ili kuwafikia watanzania wengi zaidi hasa wenye mahitaji ya ujuzi, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania imeanzisha mpango wa Ufadhili (Bursary Scheme) ambao ni sehemu ya
utekelezaji wa Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi. Mpango huu utasaidia kuwezesha mafunzo ya ujuzi kwa vijana
kutoka makundi maalum na wanaoishi katika mazingira magumu ili wapate uwezo wa kujishughulisha katika
shughuli mbalimbali za uzalishaji wenye tija.
2. Muda wa Utekelezaji wa Mpango wa Ufadhili
Mpango wa ufadhili utatekelezwa kwa muda wa miaka miwili (2) kuanzia mwaka wa fedha 2020/2021 hadi
2021/2022 kwa kuzingatia programu zilizolengwa.
3. Muda wa Mafunzo
Mpango huu unafadhili mafunzo ya muda mfupi ya miezi mitatu na miezi sita; na mafunzo ya muda mrefu ya
miezi kumi na mbili. Mpango huu hautafadhili mafunzo zaidi ya muda uliotajwa.
Ufadhili huu utakuwa katika mfumo wa ruzuku; hivyo, watakaonufaika na mpango hawatafanya marejesho. Waji-
bu wa TEA ni kuhakikisha ufadhili unawafikia walengwa na kutumika kwa mujibu wa kanuni na miongozo husika.
4. Programu au Kozi za Mafunzo za Kipaumbele
Mafunzo yatajikita katika kuendeleza Ujuzi unaohitajika na soko la ajira katika Sekta sita za kipaumbele am-
bazo ni: Kilimo na kilimo-biashara, Usafirishaji na uchukuzi, Ujenzi, Nishati, Teknolojia ya Habari na Mawasilia-
no (TEHAMA) na Utalii na huduma za ukarimu. Hivyo basi, Makundi ya programu yafuatayo yatapewa kipa-
umbele:
5. Sifa za Mwombaji wa Ufadhili
Ili kupata ufadhili, mwombaji mwenye uhitaji wa ufadhili ni lazima atimize vigezo vifuatavyo;
(i) Awe miongoni mwa wasajiliwa wanaotoka katika Mpango wa kunusuru kaya maskini.
(ii) Awe mwenye umri kati ya miaka 15 hadi 35. Aidha, kwa walemavu umri unaweza kuongezeka
hadi miaka 40.
(iii) Asiwe amedahiliwa kwenye chuo kingine.
(iv) Asiwe mnufaika wa ruzuku nyingine katika mafunzo.
(v) Awe na nia ya kupata mafunzo.
(vi) Awe na uwezo wa kumaliza mafunzo.
(vii) Awe tayari kushirikiana na TEA katika ufuatiliaji wa maendeleo ya mafunzo yake.
(viii) Aidha, waombaji wa kike wanaweza kuwa miongoni mwa wasichana waliokatisha masomo katika
Vyuo vya Maendeleo ya Jamii (FDCs) kutokana na kushindwa kumudu gharama za masomo na mahi-
taji muhimu chuoni. Waombaji katika kundi hili wawe ni wale ambao wanaishi katika mazingira
mgumu na kutoka katika kaya maskini.
(ix) Awe hajawahi kuwa mnufaika wa mfuko wa SDF hapo awali ambaye alipata ufadhili lakini alikatisha
masomo bila sababu za msingi zinazokubalika.
(x) Awe Mtanzania, mwenye kitambulisho kinachotambulika au barua ya utambulisho ya Serikali ya kijiji/
mtaa.
ANGALIZO: Kipaumbele kitatolewa kwa Wanawake na Vijana wenye Ulemavu.
6. Vipengele vitakavyofadhiliwa kwa mwanafunzi mnufaika
Mpango wa Ufadhili utamgharamia Mwanafunzi mnufaika katika maeneo yafuatayo:
(i) Kulipia ada za mafunzo ya mwanafunzi kulingana na aina na muda wa mafunzo atakayoomba. Mafunzo
yasizidi kipindi cha miezi 12.
(ii) Mafunzo ya vitendo.
(iii) Bima ya Afya (NHIF).
(iv) Chakula, malazi na usafiri vitatolewa kulingana na viwango vya TEA.
(v) Hela ya tahadhari kuanzia shillingi 20,000/= hadi 50,000/=.
(vi) Vifaa muhimu vitakavyohitajika katika mafunzo.
(vii) Ada za uandikishaji na mahitaji mengine ya msingi yatakayohitajika chuoni.
(viii) Kugharamia vifaa kwa watu wenye mahitaji maalum kwa ajili ya kuwezesha mafunzo.
ANGALIZO: Mpango wa ufadhili hautagharamia kitu chochote ambacho kitakuwa nje ya gharama zilizoain-
ishwa hapo juu.
7. Taasisi zitakazotoa Mafunzo
Mafunzo yatatolewa na Taasisi zifuatazo:
(i) Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs);
(ii) Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA); na
(iii) Vituo vya Mafunzo ya Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo vidogo (SIDO).
Hivyo, waombaji watapangiwa vyuo vilivyo karibu na maeneo wanayoishi kulingana na programu walizoomba.
8. Jinsi ya Kuomba Ufadhili wa Masomo
(i) Maombi yote ya ufadhili yatafanyika kwa kuchukua fomu katika Halmashauri, kata au kwa Ofisa
wa TASAF katika ngazi ya Halmashauri, kuzijaza kwa usahihi na kuzirudisha tena kwa Ofisa wa TASAF
kwa ajili ya uhakiki na kuidhinishwa iwapo mwombaji anatoka katika Kaya ambazo zipo chini ya Mpan-
go wa ufadhili wa TASAF.
(ii) Fomu zote zitakazojazwa ni lazima zisainiwe na kugongwa muhuri na Mwenyekiti wa Kijiji/Mtendaji wa
kata na Ofisa wa TASAF.
(iii) Fomu zilizoidhinishwa ziwasilishwe Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri husika au kwa Ofisa wa
TASAF kwa ajili ya kuwasilishwa TEA kwa ajili ya mchakato wa uchambuzi na uchaguzi.
(iv) Hakuna ada yoyote inayotozwa wakati wa kufanya maombi ya ufadhili huu.
9. Mambo Muhimu ya Kuzingatia kwa Waombaji Wote Wa Ufadhili
Waombaji wote wa ufadhili wa masomo kupitia Mpango huu wa ufadhili wanaombwa kuzingatia mambo
yafuatayo:
(i) Waombaji wajaze fomu zao kwa usahihi kulingana na maelekezo kabla ya kuziwasilisha;
(ii) Maombi ya ufadhili yanapaswa kuwa na taarifa sahihi na za kweli;
(iii) Fomu zote lazima zihakikiwe na Ofisa wa TASAF kwa ajili ya uthibitisho wa usajili wa kaya ya mwombaji
na kumbukumbu zake;
(iv) Waombaji wa kike kutoka kaya maskini ambao waliacha au kukatisha mafunzo katika Vyuo vya
Maendeleo ya Wananchi (FDCs) kutokana na kushindwa kumudu gharama za masomo watapaswa
kuthibitishwa na Mkuu wa Chuo na Mkurugenzi wa Halmashauri husika kwa barua.
(v) Waombaji wote wanatakiwa kutunza nakala ya fomu ya maombi ya ufadhili waliyowasilisha TEA kwa
matumizi mengine (kama itahitajika);
(vi) Waombaji wote wanakumbushwa kuzingatia muda wa mwisho wa kutuma maombi ambao ni tarehe 25
Septemba 2020; na
(vii) Fomu ya maombi iambatanishwe na nakala ya Kitambulisho au barua ya utambulisho yenye picha
kutoka kwa Serikali ya kijiji/mtaa.
10. Mwisho wa Kupokea Maombi
Maombi haya ya ufadhili yatafanyika kuanzia tarehe 14 Septemba 2020 hadi tarehe 25 Septemba 2020.
11. Orodha ya Waombaji watakaopatiwa ufadhili
Orodha ya waombaji watakaofanikiwa kupatiwa ufadhili yatatangazwa kwenye magazeti mbalimbali, tovuti
ya TEA, TASAF na Ofisi za Halmashauri zote nchini.
12. Maulizo na Malalamiko
Waombaji au wanufaika wa ufadhili kama watakuwa na maswali au malalamiko yoyote kuhusu ufadhili huu
watapaswa wayawasilishe kwa Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Elimu Tanzania kwa anwani iliyoonyeshwa
hapo chini.
13. Mawasiliano
Kwa ufafanuzi au maelezo zaidi wasiliana na: Mratibu wa Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi kwa Namba ya simu:
0789304181 au Ofisa wa Mpango wa Ufadhili kwa Namba ya simu: 0718744385 au tuma barua pepe kwa:
sdf@tea.or.tz.
Imetolewa na:
MKURUGENZI MKUU
na MSIMAMIZI WA MFUKO WA KUENDELEZA UJUZI (SDF Fund Manager),
MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA,
S.L.P 34578,
DAR ES SALAAM.
Barua pepe:info@tea.or.tz,
sdf@tea.or,tz | dg@tea.or.tz
TANGAZO LA UFADHILI WA MAFUNZO YA KUENDELEZA UJUZI KWA MAKUNDI MAALUMU NA
VIJANA WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA
(Tanzania Education Authority - TEA)
MFUKO WA KUENDELEZA UJUZI
(Skills Development Fund-SDF)
SN SEKTA PROGRAMU
1. Kilimo na Kilimo-biashara
Usindikaji mazao ya kilimo/ vyakula, kuongezea thamani mazao ya kilimo/vyakula,
kuongeza thamani Ngozi, kilimo na ufugaji, ufugaji wa nyuki na mengineyo.
2. Usafirishaji na uchukuzi
Ufundi umeme wa magari, Udereva, ufundi magari, uendeshaji wa mashine, ukarabati
wa pikipiki na bajaji na mengineyo.
3. Ujenzi
Ufundi umeme wa majumbani, useremala, uashi, upakaji wa rangi nyumba, upambaji
wa nyumba (interior decorations), uboreshaji wa mazingira ya nje ya nyumba ikiwemo
utunzaji bustani za maua na miti, ufundi bomba, ujenzi na ukarabati wa barabara,
Uchomeleaji wa vyuma, uchakataji wa mbao (timber processing), uandishi wa
matangazo (sign writing), ukarabati wa vifaa vya upozaji (majokofu na viyoyozi) na
mengineyo.
4. Nishati
Ufundi wa umeme jua (solar energy), umeme wa upepo, matumizi ya bio gesi,
utengenezaji wa mishumaa, utengenezaji na uboreshaji wa chumvi, uchakataji wa
madini na mengineyo.
5. Teknolojia ya Habari na mawasiliano Ufundi simu, kompyuta na ufundi redio.
6.
Utalii na huduma za ukarimu
Uongozaji watalii, utalii wa mazingira na utamaduni (Eco and Culture Tourism), upishi,
upambaji, ufumaji (embroidery) ususi, ubunifu wa mavazi (dress design), uchongaji wa
vinyago, utengenezaji wa batiki, ushonaji, hifadhi ya mazingira, ukarabati wa mashine
za kushonea nguo (sewing machine repair), utengenezaji wa sabuni na vitakasio
(sanitisers), sanaa na ubunifu ikiwemo uandishi wa matangazo (sign writing), utunzaji
wa vyumba hotelini (housekeeping), mapokezi ya wageni katika hoteli (Front office
operations), mafunzo kwa Watumishi wa nyumbani, Usimamizi wa migahawa ya
chakula (management of restaurants), mafunzo ya upishi kwa mama na baba lishe.

More Related Content

Featured

2024 State of Marketing Report – by Hubspot
2024 State of Marketing Report – by Hubspot2024 State of Marketing Report – by Hubspot
2024 State of Marketing Report – by HubspotMarius Sescu
 
Everything You Need To Know About ChatGPT
Everything You Need To Know About ChatGPTEverything You Need To Know About ChatGPT
Everything You Need To Know About ChatGPTExpeed Software
 
Product Design Trends in 2024 | Teenage Engineerings
Product Design Trends in 2024 | Teenage EngineeringsProduct Design Trends in 2024 | Teenage Engineerings
Product Design Trends in 2024 | Teenage EngineeringsPixeldarts
 
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental Health
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental HealthHow Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental Health
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental HealthThinkNow
 
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdfAI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdfmarketingartwork
 
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024Neil Kimberley
 
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)contently
 
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024Albert Qian
 
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie InsightsSocial Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie InsightsKurio // The Social Media Age(ncy)
 
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024Search Engine Journal
 
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summarySpeakerHub
 
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd Clark Boyd
 
Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next Tessa Mero
 
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search IntentGoogle's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search IntentLily Ray
 
Time Management & Productivity - Best Practices
Time Management & Productivity -  Best PracticesTime Management & Productivity -  Best Practices
Time Management & Productivity - Best PracticesVit Horky
 
The six step guide to practical project management
The six step guide to practical project managementThe six step guide to practical project management
The six step guide to practical project managementMindGenius
 
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...RachelPearson36
 

Featured (20)

2024 State of Marketing Report – by Hubspot
2024 State of Marketing Report – by Hubspot2024 State of Marketing Report – by Hubspot
2024 State of Marketing Report – by Hubspot
 
Everything You Need To Know About ChatGPT
Everything You Need To Know About ChatGPTEverything You Need To Know About ChatGPT
Everything You Need To Know About ChatGPT
 
Product Design Trends in 2024 | Teenage Engineerings
Product Design Trends in 2024 | Teenage EngineeringsProduct Design Trends in 2024 | Teenage Engineerings
Product Design Trends in 2024 | Teenage Engineerings
 
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental Health
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental HealthHow Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental Health
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental Health
 
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdfAI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
 
Skeleton Culture Code
Skeleton Culture CodeSkeleton Culture Code
Skeleton Culture Code
 
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
 
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
 
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
 
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie InsightsSocial Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
 
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
 
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
 
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
 
Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next
 
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search IntentGoogle's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
 
How to have difficult conversations
How to have difficult conversations How to have difficult conversations
How to have difficult conversations
 
Introduction to Data Science
Introduction to Data ScienceIntroduction to Data Science
Introduction to Data Science
 
Time Management & Productivity - Best Practices
Time Management & Productivity -  Best PracticesTime Management & Productivity -  Best Practices
Time Management & Productivity - Best Practices
 
The six step guide to practical project management
The six step guide to practical project managementThe six step guide to practical project management
The six step guide to practical project management
 
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
 

018 mw140920

  • 1. TANGAZO MWANANCHI.CO.TZ JUMATATU, SEPTEMBA 14, 2020MWANANCHI18 1. Utangulizi Mamlaka ya Elimu Tanzania (Tanzania Education Authority-TEA) ni Taasisi ya Umma iliyoanzishwa chini ya kifungu cha (5)1 cha Sheria ya Mfuko wa Elimu Namba 8 ya Mwaka 2001, ili kusimamia Mfuko wa Elimu wa Taifa ulioanzishwa chini ya Sheria hiyo. TEA inatekeleza majukumu yake chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatekeleza Mradi wa Kukuza Ujuzi na Stadi za Kazi (Education and Skills for Productive Jobs-ESPJ) ambao unapata ufadhili wa Benki ya Dunia na Serikali ya Jam- huri ya Muungano wa Tanzania. Mradi wa ESPJ umekuwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Kuendeleza Ujuzi (National Skills Development Strategy – NSDS: 2016-2021). Aidha, Maeneo muhimu yanay- olengwa katika utekelezaji wa Mkakati huu ni kuongeza ufanisi katika uzalishaji na pia kuongeza uwiano wa wataalam wa fani mbalimbali katika Sekta sita (Kilimo Biashara, Utalii na Ukarimu, Nishati, Ujenzi, Uchukuzi na TEHAMA) zenye mchango mkubwa wa kiuchumi nchini. Mnamo mwaka 2017, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia iliipatia TEA jukumu la kuratibu na kusimamia shughuli zote zinazohusu utekelezaji wa Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (Skills Development Fund-SDF) ambao ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Kukuza Ujuzi na Stadi za Kazi (Education and Skills for Productive Jobs-ESPJ). Ili kuwafikia watanzania wengi zaidi hasa wenye mahitaji ya ujuzi, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania imeanzisha mpango wa Ufadhili (Bursary Scheme) ambao ni sehemu ya utekelezaji wa Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi. Mpango huu utasaidia kuwezesha mafunzo ya ujuzi kwa vijana kutoka makundi maalum na wanaoishi katika mazingira magumu ili wapate uwezo wa kujishughulisha katika shughuli mbalimbali za uzalishaji wenye tija. 2. Muda wa Utekelezaji wa Mpango wa Ufadhili Mpango wa ufadhili utatekelezwa kwa muda wa miaka miwili (2) kuanzia mwaka wa fedha 2020/2021 hadi 2021/2022 kwa kuzingatia programu zilizolengwa. 3. Muda wa Mafunzo Mpango huu unafadhili mafunzo ya muda mfupi ya miezi mitatu na miezi sita; na mafunzo ya muda mrefu ya miezi kumi na mbili. Mpango huu hautafadhili mafunzo zaidi ya muda uliotajwa. Ufadhili huu utakuwa katika mfumo wa ruzuku; hivyo, watakaonufaika na mpango hawatafanya marejesho. Waji- bu wa TEA ni kuhakikisha ufadhili unawafikia walengwa na kutumika kwa mujibu wa kanuni na miongozo husika. 4. Programu au Kozi za Mafunzo za Kipaumbele Mafunzo yatajikita katika kuendeleza Ujuzi unaohitajika na soko la ajira katika Sekta sita za kipaumbele am- bazo ni: Kilimo na kilimo-biashara, Usafirishaji na uchukuzi, Ujenzi, Nishati, Teknolojia ya Habari na Mawasilia- no (TEHAMA) na Utalii na huduma za ukarimu. Hivyo basi, Makundi ya programu yafuatayo yatapewa kipa- umbele: 5. Sifa za Mwombaji wa Ufadhili Ili kupata ufadhili, mwombaji mwenye uhitaji wa ufadhili ni lazima atimize vigezo vifuatavyo; (i) Awe miongoni mwa wasajiliwa wanaotoka katika Mpango wa kunusuru kaya maskini. (ii) Awe mwenye umri kati ya miaka 15 hadi 35. Aidha, kwa walemavu umri unaweza kuongezeka hadi miaka 40. (iii) Asiwe amedahiliwa kwenye chuo kingine. (iv) Asiwe mnufaika wa ruzuku nyingine katika mafunzo. (v) Awe na nia ya kupata mafunzo. (vi) Awe na uwezo wa kumaliza mafunzo. (vii) Awe tayari kushirikiana na TEA katika ufuatiliaji wa maendeleo ya mafunzo yake. (viii) Aidha, waombaji wa kike wanaweza kuwa miongoni mwa wasichana waliokatisha masomo katika Vyuo vya Maendeleo ya Jamii (FDCs) kutokana na kushindwa kumudu gharama za masomo na mahi- taji muhimu chuoni. Waombaji katika kundi hili wawe ni wale ambao wanaishi katika mazingira mgumu na kutoka katika kaya maskini. (ix) Awe hajawahi kuwa mnufaika wa mfuko wa SDF hapo awali ambaye alipata ufadhili lakini alikatisha masomo bila sababu za msingi zinazokubalika. (x) Awe Mtanzania, mwenye kitambulisho kinachotambulika au barua ya utambulisho ya Serikali ya kijiji/ mtaa. ANGALIZO: Kipaumbele kitatolewa kwa Wanawake na Vijana wenye Ulemavu. 6. Vipengele vitakavyofadhiliwa kwa mwanafunzi mnufaika Mpango wa Ufadhili utamgharamia Mwanafunzi mnufaika katika maeneo yafuatayo: (i) Kulipia ada za mafunzo ya mwanafunzi kulingana na aina na muda wa mafunzo atakayoomba. Mafunzo yasizidi kipindi cha miezi 12. (ii) Mafunzo ya vitendo. (iii) Bima ya Afya (NHIF). (iv) Chakula, malazi na usafiri vitatolewa kulingana na viwango vya TEA. (v) Hela ya tahadhari kuanzia shillingi 20,000/= hadi 50,000/=. (vi) Vifaa muhimu vitakavyohitajika katika mafunzo. (vii) Ada za uandikishaji na mahitaji mengine ya msingi yatakayohitajika chuoni. (viii) Kugharamia vifaa kwa watu wenye mahitaji maalum kwa ajili ya kuwezesha mafunzo. ANGALIZO: Mpango wa ufadhili hautagharamia kitu chochote ambacho kitakuwa nje ya gharama zilizoain- ishwa hapo juu. 7. Taasisi zitakazotoa Mafunzo Mafunzo yatatolewa na Taasisi zifuatazo: (i) Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs); (ii) Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA); na (iii) Vituo vya Mafunzo ya Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo vidogo (SIDO). Hivyo, waombaji watapangiwa vyuo vilivyo karibu na maeneo wanayoishi kulingana na programu walizoomba. 8. Jinsi ya Kuomba Ufadhili wa Masomo (i) Maombi yote ya ufadhili yatafanyika kwa kuchukua fomu katika Halmashauri, kata au kwa Ofisa wa TASAF katika ngazi ya Halmashauri, kuzijaza kwa usahihi na kuzirudisha tena kwa Ofisa wa TASAF kwa ajili ya uhakiki na kuidhinishwa iwapo mwombaji anatoka katika Kaya ambazo zipo chini ya Mpan- go wa ufadhili wa TASAF. (ii) Fomu zote zitakazojazwa ni lazima zisainiwe na kugongwa muhuri na Mwenyekiti wa Kijiji/Mtendaji wa kata na Ofisa wa TASAF. (iii) Fomu zilizoidhinishwa ziwasilishwe Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri husika au kwa Ofisa wa TASAF kwa ajili ya kuwasilishwa TEA kwa ajili ya mchakato wa uchambuzi na uchaguzi. (iv) Hakuna ada yoyote inayotozwa wakati wa kufanya maombi ya ufadhili huu. 9. Mambo Muhimu ya Kuzingatia kwa Waombaji Wote Wa Ufadhili Waombaji wote wa ufadhili wa masomo kupitia Mpango huu wa ufadhili wanaombwa kuzingatia mambo yafuatayo: (i) Waombaji wajaze fomu zao kwa usahihi kulingana na maelekezo kabla ya kuziwasilisha; (ii) Maombi ya ufadhili yanapaswa kuwa na taarifa sahihi na za kweli; (iii) Fomu zote lazima zihakikiwe na Ofisa wa TASAF kwa ajili ya uthibitisho wa usajili wa kaya ya mwombaji na kumbukumbu zake; (iv) Waombaji wa kike kutoka kaya maskini ambao waliacha au kukatisha mafunzo katika Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs) kutokana na kushindwa kumudu gharama za masomo watapaswa kuthibitishwa na Mkuu wa Chuo na Mkurugenzi wa Halmashauri husika kwa barua. (v) Waombaji wote wanatakiwa kutunza nakala ya fomu ya maombi ya ufadhili waliyowasilisha TEA kwa matumizi mengine (kama itahitajika); (vi) Waombaji wote wanakumbushwa kuzingatia muda wa mwisho wa kutuma maombi ambao ni tarehe 25 Septemba 2020; na (vii) Fomu ya maombi iambatanishwe na nakala ya Kitambulisho au barua ya utambulisho yenye picha kutoka kwa Serikali ya kijiji/mtaa. 10. Mwisho wa Kupokea Maombi Maombi haya ya ufadhili yatafanyika kuanzia tarehe 14 Septemba 2020 hadi tarehe 25 Septemba 2020. 11. Orodha ya Waombaji watakaopatiwa ufadhili Orodha ya waombaji watakaofanikiwa kupatiwa ufadhili yatatangazwa kwenye magazeti mbalimbali, tovuti ya TEA, TASAF na Ofisi za Halmashauri zote nchini. 12. Maulizo na Malalamiko Waombaji au wanufaika wa ufadhili kama watakuwa na maswali au malalamiko yoyote kuhusu ufadhili huu watapaswa wayawasilishe kwa Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Elimu Tanzania kwa anwani iliyoonyeshwa hapo chini. 13. Mawasiliano Kwa ufafanuzi au maelezo zaidi wasiliana na: Mratibu wa Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi kwa Namba ya simu: 0789304181 au Ofisa wa Mpango wa Ufadhili kwa Namba ya simu: 0718744385 au tuma barua pepe kwa: sdf@tea.or.tz. Imetolewa na: MKURUGENZI MKUU na MSIMAMIZI WA MFUKO WA KUENDELEZA UJUZI (SDF Fund Manager), MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA, S.L.P 34578, DAR ES SALAAM. Barua pepe:info@tea.or.tz, sdf@tea.or,tz | dg@tea.or.tz TANGAZO LA UFADHILI WA MAFUNZO YA KUENDELEZA UJUZI KWA MAKUNDI MAALUMU NA VIJANA WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU UNITED REPUBLIC OF TANZANIA MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA (Tanzania Education Authority - TEA) MFUKO WA KUENDELEZA UJUZI (Skills Development Fund-SDF) SN SEKTA PROGRAMU 1. Kilimo na Kilimo-biashara Usindikaji mazao ya kilimo/ vyakula, kuongezea thamani mazao ya kilimo/vyakula, kuongeza thamani Ngozi, kilimo na ufugaji, ufugaji wa nyuki na mengineyo. 2. Usafirishaji na uchukuzi Ufundi umeme wa magari, Udereva, ufundi magari, uendeshaji wa mashine, ukarabati wa pikipiki na bajaji na mengineyo. 3. Ujenzi Ufundi umeme wa majumbani, useremala, uashi, upakaji wa rangi nyumba, upambaji wa nyumba (interior decorations), uboreshaji wa mazingira ya nje ya nyumba ikiwemo utunzaji bustani za maua na miti, ufundi bomba, ujenzi na ukarabati wa barabara, Uchomeleaji wa vyuma, uchakataji wa mbao (timber processing), uandishi wa matangazo (sign writing), ukarabati wa vifaa vya upozaji (majokofu na viyoyozi) na mengineyo. 4. Nishati Ufundi wa umeme jua (solar energy), umeme wa upepo, matumizi ya bio gesi, utengenezaji wa mishumaa, utengenezaji na uboreshaji wa chumvi, uchakataji wa madini na mengineyo. 5. Teknolojia ya Habari na mawasiliano Ufundi simu, kompyuta na ufundi redio. 6. Utalii na huduma za ukarimu Uongozaji watalii, utalii wa mazingira na utamaduni (Eco and Culture Tourism), upishi, upambaji, ufumaji (embroidery) ususi, ubunifu wa mavazi (dress design), uchongaji wa vinyago, utengenezaji wa batiki, ushonaji, hifadhi ya mazingira, ukarabati wa mashine za kushonea nguo (sewing machine repair), utengenezaji wa sabuni na vitakasio (sanitisers), sanaa na ubunifu ikiwemo uandishi wa matangazo (sign writing), utunzaji wa vyumba hotelini (housekeeping), mapokezi ya wageni katika hoteli (Front office operations), mafunzo kwa Watumishi wa nyumbani, Usimamizi wa migahawa ya chakula (management of restaurants), mafunzo ya upishi kwa mama na baba lishe.