Good Stuff Happens in 1:1 Meetings: Why you need them and how to do them well
Kushukuru
1. Date: 14th April 2010
KUTOA SHUKURANI
UTANGULIZI.
Siku ya leo ni siku kubwa sana, siku ya mothering Sunday.
Ni siku ya kumshukuru Mungu kwa sababu ya akina mama na hasa
wazazi wetu.
Basi ni vizuri kujifundisha kuhusu kutoa shukurani na tutatumia Luka
17:11- 19
NENO: Luka 17:11-19
Yesu alipokuwa hapa ulimwenguni alienda akitenda mema kama jinsi
anavyofanya hata sasa.
Wakati huu aliwatendea wema wanaume kumi waliokuwa na ugonjwa wa
ukoma. Ugonjwa huu ulikuwa mbaya sana kwa sababu watu wengine
hawakutaka kuwakaribia. Lakini Yesu anatupenda hata jinsi tulivyo.
Wagonjwa hawa walipomuona Yesu walisimama mbali. Pengine
walifikiri Yesu atawapuuza kama wale watu wengine lakini Mungu wetu
sio hivyo.
Wagonjwa hawa walipaaza sauti zao kwa sababu ni vizuri kumwambia
Bwana mahitaji yetu. Walimwambia awahurumie.
Yesu alipowaona aliwahurumia na kuwaambia waende wajionnyeshe
kwa makuhani nao wakatii sauti ya Bwana. Ni vizuri kuitii sauti ya
Bwana kila wakati.
Hawa walipokuwa wakienda waliponywa kwa sababu hakuna lolote
linalomshinda Mungu wetu.
Mmoja wao peke yake ndiye aliyerudi kumshukuru Yesu. Naye alikuwa
msamaria. Aliona hakustahili kubarikiwa na Yesu hadi akarudi
kumshukuru.
Jambo hili likamshangaza Yesu kwa sababu ingawaje wote waliponywa
ni mmoja tu alirudi kushukuru.
Yesu akamwambia ya kwamba imani yake ndiyo ilimuokoa.
2. MAFUNDISHO:
Katika hadithi hii twaweza kujifundisha mambo yafuatayo:
1. Hata sasa Yesu yuko hapa na anaenda akitenda mema. Hata hapo mbeleni
ameenda akitenda mema. Ametupa wazazi wetu. Ametupa watoto.
Ametupa waume na wake. Ametuponya magonjwa na kutukinga na hatari
zote. Hakika ametupa mambo mengi kiasi cha kwamba hatuwezi
kuelezea yote.
2. Tunapaswa kila wakati kumwendea Yesu kwa maombi. Tupaaze sauti
zetu tumwite Bwana kama vile wale wanaume kumi walivyofanya.
Tuombe bila kukoma ili nyumba zetu zisimame na kanisa letu lizidi pia
kusimama wima. Naye Yesu ataturehemu.
3. Ni vizuri kuitii sauti ya Mungu. Wenye ukoma hawa walitii walipoambia
waende wakajionyeshe kwa makuhani. Basi hata nasi tunaposikia sauti ya
Bwana tusifanye mioyo yetu kuwa migumu.
4. Jambo kubwa sana ni kumshukuru Mungu kwa yote aliotutendea. Ni
mara ngapi umemshukuru Mungu kwa yale yote aliokutendea?
5. Siku ya mothering Sunday ilianzishwa miaka mingi liyopita ili
kuwashukuru akina mama wazazi wetu. Siku hii inaadhimishwa jumapili
ya nne wakati wa saumu. Watoto huwashukuru wazazi wao kwa sababu
ya kuwazaa na kuwatunza miaka yote.
6. Leo tunashukuru Mungu kwa sababu ya akina mama. Na hatuwezi
kwenda mbele ya Mungu mikono mitupu. Kwa hivyo tuliwapa bahasha
ili tuweze kumshukuru Mungu. Lakini ningewaomba baada ya service
tukawashukuru wazazi wetu kwa njia yoyote. Pengine tuwatembelee na
kupelekea kitu. Nanyi waume wetu tufanyieni kitu leo.
7. Jambo la mwisho tunaloona hapa katika somo hili ni kwamba imani ni
kitu cha maana sana. Wenye ukoma walipona kwa sababu ya imani. Hata
nasi tutatendewa mambo makubwa na Mungu kwa sababu ya imani yetu.
Basi nikimaliza nawaomba tumshukuru Mungu na hata akina mama kwa
yote waliotutendea.