1. Kila sifa njema zinamstahiki Allah (SW)
Bwana na Mlezi wa Viumbe vyote.
Rehma na Amani zimuendee Mtume
(s.a.w) na Maswahaba zake na Wale
Wote wanaofanya jitihada za makusudi
za kulingania na hatimae kusimamisha
Uislamu katika jamii bila kujali chuki za
Washirikina.
6. Lengo kuu la Mada hii ni
kuwapa waalimu Waislamu ari
na hamasa ya kujifunza na
kufundisha elimu ya Mazingira
na Muongozo pamoja na
kusimamia maadili ya watoto
wa Kiislamu mashuleni.
7 Machi 2024
9. 7 Machi 2024
i. Kueleza nafasi na Umuhimu wa
Elimu katika jamii.
ii. Kueleza kwanini elimu imepewa
umuhimu na nafasi hiyo.
iii. Kuanisha maana ya Ualimu na
Mwalimu.
iv. Kuainisha wajibu wa Mwalimu
Muislamu katika jamii.
10. 7 Machi 2024
iv. Kuainisha sifa za Mwalimu wa
Kiislamu.
v. Kuchambua hali ya Waislamu wasomi
hivi leo.
vi. Kuainisha changamoto zinazowakabili
walimu katika mashule na vyuo.
vii.Kuazimia kuwa Mwalimu wa
Kiislamu.
15. 7 Machi 2024
• Elimu ni ujuzi na Maarifa
yanayomuwezesha yule
aliyeipata kuishi kwa ufanisi zaidi.
• Kwa maana nyingine Elimu ni
nyenzo ya kuboresha maisha ya
Mwanadamu na kukabiliana na
Changamoto zinazomkabili.
16. 7 Machi 2024
• Elimu ni nyenzo muhimu sana ya
maisha yetu na kwa hiyo ni muhimu
kila Mmoja awe nayo.
• Kukosa Elimu ni ugonjwa na ni jambo
ambalo halifai kabisa.
• Elimu inasaidia jamii ya Mwanadamu
kukua kimaendeleo, hivyo ni nyenzo
muhimu ya kuleta mabadiliko.
18. 7 Machi 2024
Elimu yenye Manufaa ni ile
ambayo:
i.Humuwezesha mja kufikia lengo
la kuumbwa kwake; ambalo ni
kumuabudu Allah (s.w), ipasavyo
katika kila kipengele cha maisha
yake. (Qur-an 51:56).
19. 7 Machi 2024
Abu Hurairah amesimulia kuwa
Mtume (s.a.w) amesema:
“Anayetafuta elimu isiyokuwa kwa ajili
ya kutafuta radhi za Allah (s.w), hasomi
kwa lengo lolote lile ila la kupata
maslahi ya hapa duniani tu. Hivyo siku
ya kiyama hatapata hata harufu ya
Pepo.” (Ahmad, Abu Daud, Ibn majah).
20. 7 Machi 2024
Pia Mtume(s.a.w) ametuasa
kuwa mwenye kutafuta elimu ili
awazidi wasomi wengine au ili
kuitumia katika biashara za
kijahili au ili kujionesha kwa watu
kuwa naye ni msomi, Mwenyezi
Mungu atamuingiza motoni.
(Tirmidh).
21. 7 Machi 2024
ii.Elimu yenye manufaa kwa
Binaadamu hapa ulimwenguni na
huko akhera ni ile ambayo pamoja
na mtu binafsi kuitumia katika
kumuabudu Allah(s.w) ipasavyo
katika maisha yake ya kila siku,
huifundisha au huifikisha kwa
wengine pia kwa ajili ya kutafuta
radhi za Allah(s.w).
22. 7 Machi 2024
“Abu Hurairah amesimulia kuwa
Mtume (s.a.w) amesema:
“Atakayeulizwa juu ya jambo
alilojifunza kisha akaficha
(akakataa kutoa elimu ile)
atavalishwa mshipi wa moto
katika siku ya Kiyama”. (Ahmad,
Ibn Majah, Tirmidh na Abu Daud).
23. 7 Machi 2024
Katika hadith nyingine
iliyosimuliwa na Abu Hurairah
Mtume wa Allah (s.a.w) amesema:
“Mfano wa elimu isiyonufaisha ni
sawa na mfano wa mali
iliyokusanywa bila ya kutumiwa
katika njia ya Allah”. (Ahmad,
Darini).
24. 7 Machi 2024
Kutokana na hadith hizi tunajifunza
kuwa elimu yenye kunufaisha ni ile
iliyofundishwa na wengine
kinadharia na matendo. Kwa
kufundisha watu unachokijua bila
ya wewe mwenyewe kutenda ni
mfano mbaya mno kwa wale
wanaofundisha na chukizo kubwa
mno mbele ya Allah (s.a.w):
25. 7 Machi 2024
Enyi mlio amini! Kwa nini mnasema
msiyo yatenda?
Yanachukiza vikubwa mno kwa Mwenyezi
Mungu kuwa mnasema msiyo yatenda.
27. i. Elimu ndio takrima ya
kwanza aliyotunukiwa
mwanaadamu na Mola
wake.
Mara tu baada ya kuumbwa Adam (a.s),
alitunukiwa elimu – Qur'an (2:31).
7 Machi 2024
28. “Na Mwenyezi Mungu akamfundisha Adam
majina ya vitu vyote, kisha akaviweka mbele ya
Malaika, na akasema: Niambieni majina ya hivi
ikiwa mnasema kweli.” (2:31)
“Majina ya vitu vyote” inaashiria fani zote za
elimu anazohitajia mwanaadamu ili aweze
kuutawala ulimwengu (awe Khalifa).
7 Machi 2024
29. 7 Machi 2024
ii. Kutafuta Elimu ni faradh
ya kwanza kwa
Waislamu.
Jambo la kwanza kuamrishwa
Mtume (s.a.w) na kwahiyo
Waislamu wote ni “kusoma”
(kutafuta elimu).
30. 7 Machi 2024
“Soma kwa Jina la Mola wako aliyeumba.
Amemuumba mwanaadamu kwa pande la damu.
31. 7 Machi 2024
Soma, na Mola wako ni Karimu sana.
Ambaye amemfundisha (binaadamu
ilimu zote hizi) kwa wasita (msaada)
wa kalamu; (zilizoandika vitabu, watu
wakapata ilimu.
34. Elimu imepewa umuhimu na
nafasi ya kwanza kwa
sababu zifuatazo:
i. Elimu ndio nyenzo pekee
inayomuwezesha mwanaadamu
kumtambua Mola wake na
kumuabudu inavyostahiki.
7 Machi 2024
35. 7 Machi 2024
Na katika watu, na wanyama, na mifugo, pia
rangi zao zinakhitalifiana. Kwa hakika wanao
mcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja
wake ni wale wataalamu”. Hakika Mwenyezi
Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe.
36. Kwa bahati mbaya sana Elimu
tunayoitoa inafundisha
namna Mwanadamu
atakavyojipatia mahitaji yake
muhimu (basic needs of
Man); Ikasababisha kuzalisha
Mafisadi.
37. 7 Machi 2024
ii. Elimu iliyosomwa kwa mrengo
wa Qur'an; ndiyo nyenzo pekee
inayomuwezesha muunini
kuwa Khalifa wa Allah (s.w)
hapa duniani – Qur'an (2:30-
31, 38).
38. 7 Machi 2024
iii. Elimu hupandisha hadhi na daraja ya waumini.
“… Mwenyezi Mungu atawainua (daraja) wale
walioamini miongoni mwenu, na waliopewa
elimu watapata daraja zaidi. Na Mwenyezi
Mungu anazo habari za mnayoyatenda yote”
(58:11).
Mabadiliko na maendeleo ya jamii huletwa na
wataalamu waliobobea katika fani zao.
Jamii isiyo wasikiliza kuwaenzi wataalamu
haiwezi kuendelea.
39. iv. Elimu hupandisha hadhi na
daraja ya Waumini.
“…Mwenyezi Mungu atawainua walio
amini miongoni mwenu, na walio pewa
ilimu daraja za juu…”(58:11)
40. iv. Elimu ndiyo iliyomtukuza Adamu;
Malaika wakaamriwa wamsujudie
isipokuwa ibilisi yeye alikataa kwa
kuangalia umbile la Adamu na sio
Elimu, akalaaniwa.
v. Kupitia Elimu tunapata
Wataalamu mbalimbali, bila Elimu
hata ya Mazingira huwezi
kuwaongoza Watu.
42. 7 Machi 2024
“.............Sema, Je, wanaweza kuwa
sawa wale wanaojua na wale
wasiojua? Wanaotanabahi ni wale
wenye akili tu.” (39:9)
43. 7 Machi 2024
• Jibu la swali hili ni wazi. Mjuzi na asiyejua
hawawezi kuwa sawa kiutendaji na kitabia.
• Tunaweza kumtambua Daktari kwa kupata
matibabu na sio kwa kumuona kwa Macho
• Tunaweza kumjua Mpishi mzuri wa Pilau
kwa kula pilau aliyoipika na Sio kwa
kumuona n.k.
Hivyo Aliyeelimika ni Yule mwenye ujuzi
unaomuwezesha kutenda inavyotakikana.
44. 7 Machi 2024
“Mfano wa wale waliopewa Taurati kisha
hawakuichukua (kwa kuitia katika matendo)
ni kama punda aliyebeba (mzigo) wa vitabu
vikubwa (bila ya kufaidika kwavyo) ni mbaya
kabisa mfano wa watu waliokadhibisha aya
za Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu
hawaongoi watu madhalimu.” (62:5).
45. 7 Machi 2024
• Kwa hiyo kwa mtazamo wa Qur’ani
mtu aliyeelimika ni yule
anayetenda inavyotakikana na kwa
ufanisi zaidi.
• Kwa mantiki hiyo mjuzi wa Qur’ani
na Sunnah ni yule anayeendesha
maisha yake yote kwa mujibu wa
Qur’ani na Sunnah.
47. • Ualimu ni fani inayojihusisha na mchakato
mzima wa kuingiza ujuzi, maarifa na
ufahamu kwenye akili ya mtu kwa lengo la
kumuwezesha kufikia lengo husika.
• Kwa mtazamo wa Uislamu ni fani
inayojishughulisha na mchakato mzima wa
kumuelimisha mwanaadamu ili achukue
hadhi (nafasi) yake ya Ukhalifa (Qur'an
2:30) ili aweze kufikia lengo la kuumbwa
kwake (ur’an 51:56).
7 Machi 2024
48. 7 Machi 2024
• Kwa maana nyingine Ualimu ni fani
inayojihusha na utayarishaji watu
(rasilimali watu) ambao ndio
mawakala (agents) wakuu wa
mabadiliko ya jamii katika kuendea
lengo husika.
• Kwa Waislamu lengo husika ni lile
aliloletewa Mtume (s.a.w) la
kuutawalisha Uislamu katika jamii.
49. 7 Machi 2024
“Yeye ndiye Aliyemleta Mtume wake kwa
uongofu na Dini ya haki ili Aijaalie kushinda
(Dini hii) dini zote; ijapokuwa watachukia hao
washirikina” (9:33).
“Yeye ndiye Aliyemtuma (Aliymleta) Mtume wake
(Nabii Muhammad) kwa uwongofu na kwa Dini
ya haki ili kifanya ishinde Dini zote, ijapokuwa
washirikina watachuiwa” (61:9).
51. • Kwa kuzingatia maana ya Ualimu, Mwalimu
ni yule awezeshaye muendelezo wa
mchakato wa kuingiza ujuzi, maarifa na
ufahamu kwenye akili ya binaadamu kwa
kutumia utaalamu na nyenzo husika ili
kufikia lengo husika.
• Kwa ufupi Mwalimu ndiye muhusika mkuu
wa kwezesha mabadiliko ya kielimu,
kimtazamo na hatimaye kimaadili ya jamii
husika.
7 Machi 2024
52. 7 Machi 2024
• Mwalimu Mkuu ni Allah(SW)
Qur’ani(2:31) “Na(Mwenyezi Mungu
akamfundisha majina ya Vitu vyote…”
“Ambaye amemfundisha mwanaadamu kwa
kalamu. Amemfundisha mwanaadamu (chungu ya)
mambo aliyokuwa hayajui” (96:4-5).
Waalimu Wakuu Wasaidizi wa binaadamu ni
Mitume wa Allah (s.w) ambao wamekuja
kuwafundisha binaadamu vitabu vya Allah (s.w)
pamoja na mbinu (hekima) za ufundishaji.
53. 7 Machi 2024
“Yeye ndiye Aliyemleta Mtume katika watu
wasiojua kusoma (wasio na elimu),
anayetokana na wao, awasomee aya zake
na kuwatakasa na kuwafunza kitabu na
hikima (mbinu za kujifunzia na
kufundishia). Na kabla ya haya walikuwa
katika upotevu uliodhahiri” (62:2).
54. 7 Machi 2024
• Walimu wote wa Kiislamu
ni Walimu Wasaidizi wa
Mitume wa Allah (s.w).
Qur'an imetumia mbinu zaidi ya
hamsini (50) za kufikishia
ujumbe kwa binaadamu.
56. Ili tuelewe jukumu na nafasi ya
Mwalimu katika jamii ni vema tuzingatie
hakika ya kimaumbile kuwa:-
• Allah (s.w) ndiye muumbaji wa kila kitu.
• Pamoja na vipawa vikubwa vya akili na elimu
alivyotunukiwa mwanaadamu, hanauwezo wa
kuumba bali hutengeneza maumbile ya Allah
(s.w) kwa kuyatoa katika asili yake (yaliyoumbiwa)
na kuyabadilisha katika hali ambayo
yatamnufaisha (mwanaadamu).
7 Machi 2024
57. 7 Machi 2024
Kwa mfano:
• Allah (s.w) anaumba mti ambao mwanaadamu huukata
na kuupasua kupta mbao za kutengenezea viti,
madawati, meza, milango, n.k.
• Mwanaadamu (mtaalamu) anayefanya kazi hii huitwa
Seremala.
• Allah (s.w) ameumba madini ambayo mwanaadamu
huyayeyusha na kutengeneza hereni, mikufu, bangili,
pete, n.k.
• Mwanaadamu (mtaalamu) anayefanya kazi hii huitwa
Sonara.
• Allah (s.w) ameumba chuma ambacho mwanaadamu
hukifua na kutengeneza silaha, magari, ndege, n.k.
• Mtaalamu wa kufua chuma huitwa Mhunzi.
58. 7 Machi 2024
Allah (s.w) amemuumba
mwanaadamu katika
umbile lake la asili (fitra)
kama alivyoumba miti,
madini, chuma, n.k.
59. 7 Machi 2024
“Basi uelekeze uso wako katika Dini iliyo
sawasawa – ndilo umbile Mwenyezi Mungu
alilowaumbia watu; (yaani Dini hii ya Kiislamu
inawafikia na barabara na umbo la binaadamu).
Hakuna mabadiliko katika maumbile ya viumbe
vya Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo Dini iliyo haki,
lakini watu wengi hawajui” (30:30).
60. 7 Machi 2024
Pia Mtume (s.a.w) amesema:
“Kila kinachozaliwa (mwanaadamu) huzaliwa
katika fitra (Uislamu), ni wazazi wake (jamii na
walimu wake) ndio hukibadilisha (kikatoka kwnye
fitra) na kukifanya kuwa Mkristo, Myahudi au
Mmajusi”.
• Kutokana na Hadithi hii tunajifunza kuwa:-
–Wanaadamu wote katika asili yao ni
Waislamu.
i. Mtaalamu wa kumbakisha mwanaadamu
katika fitra yake (Uislamu) ni Mwalimu
(Muumini).
61. 7 Machi 2024
ii. Kwa njia mbali mbali mwanaadamu
hubadilishwa kutoka kwenye Uislamu na
kuingizwa kwenye mifumo mingine ya maisha
inayomuangamiza (mwanaadamu).
• Mtaalamu wa kubadilisha fitra ya
mwanaadamu na kuipelekea kwenye
maangamizi ni Mwalimu.
• Wataalamu wa kubadilisha umbile asili la
mwanaadamu (fitra) kama walivyo seremala,
masonara, wahunzi, n.k. ni walimu.
62. 7 Machi 2024
• Mwalimu ndiye msingi mkuu au chimbuko
kuu la mabadiliko ya jamii yoyote ile
kitaaluma na kimaadili.
• Fani yoyote aliyonayo mwanaadamu huyu, iwe
ya manufaa au ya maangamizi muhusika
mkuu ni Mwalimu.
• Mwalimu kwa kutumia mtaala husika
huibadilisha jamii kwa namna apendavyo.
• Mwalimu ndiye “Seremala, Sonara, Mhunzi,
n.k”. wa jamii.
63. 7 Machi 2024
WAALIMU KATIKA
KUIBADILISHA
(TRANSFORM) JAMII
HUTUMIA NJIA MBILI:
i. Isiyorasmi (Informal)
ii. Rasmi (Formal)
64. 7 Machi 2024
i.Kwa kutumia Njia
Isiyorasmi (informal)
hutumika vifaa kama:
Tv
Magazeti
Video
Internet
Electronics, n.k.
83. 7 Machi 2024
HUMAN RIGHTS
Virginia Nzamwita and Joseph
Shija, Longman Tanzania, 2011,
Civics Forms 1 & 2 (PB).
Collective rights
The right to raise a family page 26.
89. 7 Machi 2024
Kwa kuzingatia Nafasi
hii ya Mwalimu;
Dhima ya Mwalimu wa
Kiislamu ni kufanya
haya yafuatayo:
90. 7 Machi 2024
a)Kuwapa wanafunzi elimu ya
mwongozo (Elimu ya Dini ya
Kiislamu) na Elimu ya Mazingira
(Geograph,Mathematics, Physics,
Kiswahili, English, Arabic, n.k.)
kwa lengo la kusimamisha
Ukhalifa (Uislamu) katika jamii.
91. 7 Machi 2024
b) Kuwalea na kuwasimamia wanafunzi
waweze:
i. Kuwa na yakini juu ya Uislamu.
ii. Kutekeleza nguzo za Uislamu vilivyo na
kuzihusianisha na maisha yao ya kila siku.
iii. Kuutekeleza Uislamu katika kukiendea kila
kipengele cha maisha yao ya kila siku.
iv. Kuwa na ari na hamasa ya kuutawalisha
Uislamu katika jamii.
93. Mwalimu atakayeweza kutoa
Makhalifa wa Allah ni atakaye
jipamba na sifa zifuatazo:
i. Awe na Elimu sahihi juu ya Uislamu.
ii. Awe na imani thabiti juu ya Uislamu.
iii. Autekeleze Uislamu katika kila
kipengele cha maisha yake ya kila
siku.
7 Machi 2024
94. Qur’ani (2: 208) “Enyi mlio amini!
Ingieni katika Uislamu kwa
ukamilifu, wala msifuate nyayo za
She'tani; hakika yeye kwenu ni adui
aliye wazi.”
7 Machi 2024
95. 7 Machi 2024
iv. Kuutawalisha Uislamu uwe juu ya
mifumo yote ya maisha liwe ndio
lengo lake kuu la maisha.(2:214)
96. Mnadhani kuwa mtaingia Peponi,
bila ya kukujieni kama yaliyo wajia
wale walio pita kabla yenu? Iliwapata
shida na madhara na wakatikiswa
hata Mtume na walio amini pamoja
naye wakasema: Lini nusura ya
Mwenyezi Mungu itakuja? Jueni
kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu ipo
karibu.(2:214)
7 Machi 2024
97. 7 Machi 2024
v. Katika kutekeleza majukumu
yake ya Ualimu atarajie malipo
kutoka kwa Allah (s.w) tu.
Chochote atakachokipata iwe ni
kama mtu aliyelipwa mshahara
kulitumika shamba lake.
98. 7 Machi 2024
“Sema: Ikiwa baba zenu, na wenenu, na ndugu
zenu, na wake zenu, na jamaa zenu, na mali mliyo
yachuma, na biashara mnazo ogopa kuharibika,
na majumba mnayo yapenda, ni vipenzi zaidi
kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake
na Kuipigania Dini yake, basi ngojeni mpaka
Mwenyezi Mungu alete amri yake. Na Mwenyezi
Mungu hawaongoi watu wapotovu”. Q(9:24)
99. vi. Awe na Subira.
7 Machi 2024
Maana halisi ya Subira ni kutenda na kuendelea
kupambana na Madhila mbalimbali. Subira ni kipengele
cha tabia njema chenye maana pana. Miongoni mwa
maeneo ya subira anayotakiwa kuwanayo Mwalimu
Muislamu ni.
I. Kuwa na subira kutokana na mambo yatakayo
kupata.
II. Kutokuwa na haraka ya kupata matunda ya haraka.
III. Ni katika subira Mwalimu Muislamu kubakia na
uamuzi wake mwema mpaka hatua ya mwisho.
100. vii. Awe na hekima.
Hekima ni miongoni mwa sifa kuu muhimu
anayotakiwa awe nayo Mwalimu wa
kiislamu. Kamwe mafanikio hayatapatikana
pasina kutumia Hekima.
Hekima ni kipegele cha tabia njema chenye
maana ya kufanya jambo la sawasawa
kwa namna ya sawasawa kwa wakati wa
sawasawa katika mazingira ya sawasawa.
7 Machi 2024
103. i.Hatujiamini;
Mfano: Mtu anaomba ruhusa ya
kwenda kuswali badala ya kutoa
taarifa, Mwislamu msomi
anaogopa kuzungumzia na kukaa
kwenye vikao vianyohusu dini
tofauti na wale wa upande
mwingine.
104. ii. Hatujui sheria, Haki zetu na
namna ya kuzipigania
tumejitenga na Uislamu na
mambo ya Waislamu. Huwa
tunaona aibu kunasibishwa na
Uislamu na Waislamu. Tofauti
na Wasomi wa Madhehebu
mengine.
105. iii.Huiona jamii ya Waislamu kama
jamii duni ambayo haina lolote
katika Ulimwengu huu
uliosheheni maendeleo ya Vitu
(Materialism).
iv.Mchango wetu katika huduma za
jamii ni kidogo au haupo kabisa.
Mfano: Katika Taasisi za Kikristo Walimu
wazoefu wanafundisha madarasa ya chini.
Masters (Chekechea); PHD(Sekondari) n.k
106. v. Tumekuwa Wacha vitu; nitapata
nini?, Sina uwezo, Sifanyi kazi
ya bure. Tukumbuke Muislamu
anapofanya jambo kwa ajili ya
Allah (s.w) hakuna anachopoteza
bali anapata faida.
vi. Baya zaidi wakati mwingine
huungana na maadui wa Uislamu
katika kukebehi, kusimanga na
kupiga vita Waislamu na Uislamu.
110. a)Kutokuwa na Elimu Sahihi ya
Uislamu.
b)Mfumo wa Elimu ya Mazingira
uliopo.
c)Mbinu duni za kufundishia Elimu
ya Mwongozo zinazotumika.
d)Taasisi na Madhehebu.
111. 7 Machi 2024
i. Kufundisha Elimu ya Muongozo (EDK) na Elimu
ya Mazingira kwa lengo la kuwa andaa
Makhalifa wa Allah (SW).
ii. Kuanzisha Mifuko ya Elimu kwa kila ngazi
iii.Kuandaa na kusimamia Semina elekezi za
mbinu za ufundishaji wa Elimu ya Muongozo
na Mazingira kwa Walimu Waislamu wa
Madrasa, Shule za Msingi na Sekondari.
iv.Kusimamia Taaluma na Malezi kwa vijana wa
Kiislamu ktk shule zote za Msingi na
Sekondari.
KAZI ZA
KUFANYA
112. 7 Machi 2024
iv. Kusimamia Mtihani wa EDK wa Taifa kwa
Darasa la Saba.
v. Kuendesha na kusimamia Itiqafu/Kambi za
Wanafunzi kwa Vidato vya 3 – 6.
vi. Kuanzisha na kusimamia Vituo vya masomo
ya ziada (KATA PROGRAM)
vii. Kuanzisha na Kushiriki katika madarasa ya
Elimu ya Dini kwa Watu wazima (Darasa
Duara).
viii.Kufanya kazi hizi kwa kutegemea malipo
kutoka kwa Allah(SW) pekee na sio kutoka
kwa Wanadamu.