SlideShare a Scribd company logo
1 of 64
Download to read offline
¯ :
 Mimi ni
Mwislamu
   Authorship
Muhammed Ashraf Salah
Mimi ni Mwislamu
Mimi ni Mwislamu
Kwa jina la Mungu wa Rehema


hgfedc ba`_

       : ¯    kji

Na mtu anataka dini nyingine zaidi ya
Uislamu wala kukubali kuwa wakati ni
 mmoja wa wenye kukhasiri Akhera
              Al-Imran: 85
Mimi ni Mwislamu
Copyright, distribution and translation are
    reserved for every Muslim

Legal Deposit No.     22274 / 2008

International Serial   977-6157-64-5


   For charitable distribution call:
      0020101459613
     For suggestions e-mail:
   anamuslim@windowslive.com
    WWW.Iam-Muslim.com
Mimi ni Mwislamu

  (1) KUMWAMINI MWENYEZI
      MUNGU
Mimi ni Mwislamu…
 • Ninamwamini     Mwenyezi    Mungu
   Pekee Asiye na mshirika na hakuna
   mola mwingine isipokuwa Yeye,
   Hakuzaa    wala   Hakuzaliwa,   na
   hakuna kamwe kifano chake.
 • Ameumba mbingu na ardhi, Naye
   Ndiye    Anayezimiliki.   Anayajua
   yaliyofichikana na yenye kuonekana.
   Yu Hai na Hafi, Anayasimamia
   mambo yote milele na Halali.
 • Ana Majina Mazuri Kabisa na Sifa za
   Juu. Kati yake ni Majina tisini na tisa,
   mwenye kuyajua na kuyadhibiti
   vyema na akamwomba Mwenyezi
   Mungu Kwayo, ataingia peponi.
 • Kati yake ni Sifa za Upweke, kwani Yeye
   Subhaanahu wa Taalaa ni Mmoja wa
   Dhati, Sifa na Vitendo, Aliyepwekeka, Aliye
   Pekee,   Mkusudiwa,    Mmiliki  wa
   ufalme.
Mimi ni Mwislamu
• Na Sifa za Utukufu, kwani Yeye ni
 Mwenye hekima, Mwenye habari ya
 kila jambo, Mwelekezaji wa manufaa,
 Haki, wa Mwanzo, wa Mwisho, wa
 Dhahiri, wa Siri, Mrithi, Mwenye
 Kubakia, Mkwasi, Mtakasifu, Mwenye
 Kushuhudia, Aliye Karibu, Mbora wa
 Kupangilia,  Mwadilifu,  Nuru  ya
 mbingu na ardhi, Mwenye Utukufu na
 Ukarimu.
• Na Sifa za Uadhama, kwani Yeye ni
 Mshindi Asiyeshindika, Mwenye Sifa
 zote Tukufu, Mwenye Uadhama,
 Mwenye Sifa za Utukuzo, Mwenye
 Kulazimisha, Mwenye Nguvu, Aliye
 Imara, Mteza nguvu, Mweza, Mwenye
 uwezo wa juu, Mwingi wa Kunusuru,
 Aliye Juu, Aliye Juu ya vyote.
• Na Sifa za Uwezo, kwani Yeye ni
 Mwingi wa Ujuzi, Mwenye Kusikia,
 Mwenye kuona, Yu Hai,
Mwenye Kukamata, Mwenye Kukunjua,
Mwenye     Kushusha,     Mwenye
Kupandisha,   Mwenye    Kutukuza,
Mwenye Kudhalilisha, Mwenye Kutoa,
Mwenye Kuzuia, Mwenye Kunufaisha,
Mimi ni Mwislamu
Mwenye Kudhuru, Mwenye Kuhuisha,
Mwenye Kufisha, Mwenye Kutanguliza
na Mwenye Kuchelewesha.
• Na Sifa za Uumbaji, kwani Yeye ni
  Muumbaji, Msanifu wa Maumbile,
  Mtiaji Sura, Hakimpiti au Kumshinda
  kitu, Mbunifu, Mwenye Kuanzisha,
  Mwenye Kurejesha, Mwenye Kufufua,
  Mwenye Kukusanya, Mpaji Mkuu,
  Mfunguzi wa kila jambo, Mwingi wa
  Kuruzuku,   Mwenye   Kutajirisha,
  Mdhibiti wa idadi, Mwenye Kudhibiti
  mambo, Mwenye Kuhifadhi, Mlinzi na
  Muumbaji wa mbingu na ardhi bila
  ruwaza.
• Sifa za Rehma, kwani Yeye ni Mwingi
  wa Rehma, Mwingi wa Kurehemu,
  Mwingi   wa  Huruma,   Mwenye
  Kuneemesha neema nzuri, Mwingi wa
  Penzi, Mtenda Wema, Mwingi wa
  Kughufiria, Mwenye Kusamehe, Mwingi
  wa Kukubali toba, Mwenye Amani,
  Mtoaji amani na imani, Mpole, Mwenye
  Kulipa vyema, Mkarimu, Mwenye
  Kuneemesha,  Mwingi  wa  Kutoa,
  Mwenye Kusaidia, Mwenye Kujibu,
Mimi ni Mwislamu
  Mkunjufu, Mwingi wa subira, Mvumilivu
  kwa Waja Wake, Latifu, Wakili, Mwenye
  Kutoa Misaada, Mwenye Kuombwa
  msaada na Mwenye Kukubali toba.
•  Amemneemesha mwanadamu neema
  nyingi zisizo na hesabu. Na hakuna
  neema yoyote anayoneemeka nayo
  mja ila hutoka kwa Mwenyezi Mungu
  Pekee, kwani Yeye Ndiye Aliyemuumba
  na Akampa uhai, Akamfanya asikie na
  aone, Akamkirimu, kisha Akamruzuku
  na Akamfanyia wema.
•  Kwa ajili hiyo, ni lazima mja
  amwabudu Mwenyezi Mungu Peke
  Yake – nako ni kufuata amri Yake na
  kuacha makatazo Yake – kwa kuwa
  hastahiki    yeyote  kuabudiwa
  isipokuwa Mwenyezi Mungu Peke
  Yake.
•  Vile vile, bila shaka Mwenyezi Mungu
  Anazijua hali zote za mja kati ya
  utiifu
Mimi ni Mwislamu

na uasi. Hivyo basi, ni wajibu moyo wa
mja ujae haiba kwa Mwenyezi Mungu
Mtukufu, utukuzo na mapenzi, na aone
haya kumwasi na aachane na maasi,
kwani Mwenyezi Mungu Humwona
wakati akiyafanya.
• Anafurahi kwa amali zake njema
 zinazomkurubisha kwenye radhi za
 Muumbaji wake Subhaanahuu wa
 Taala. Hivyo huzidi kufanya amali
 hizo hadi kufikia ngazi ya ihsani,
 kwani imani huzidi kwa matendo
 mema na hupungua kwa maasi.
• Asivutike kwenye matamanio, hawaa
 au bid'a, bali avutike kwa Mwenyezi
 Mungu   Pekee   huku  akifuata
 maamrisho ya Mtume Swalla Allaahu
 Alayhi  wa  Aalihii wa  Sallam.
 Asitafute kwa amali yake starehe
 ndogo ya dunia bali atafute kwayo
 malipo toka kwa Mwenyezi Mungu tu.
• Aidha, hakika Mwenyezi Mungu Ana
 huruma mno kwa mwanadamu kuliko
 huruma ya mama kwa mwanaye. Na
 rehma Yake imekienea kila kitu.
Mimi ni Mwislamu
  Hivyo basi, ni wajibu kwa mja
  amwombe na anyenyekee Kwake
  katika haja zake za kidunia na za
  kiakhera, na wala asimwombe yeyote
  mwingine.
•  Kwa vile hakuna faida yoyote ya
  kumwomba asiye Mwenyezi Mungu,
  kwa kuwa hamiliki uwezo ulio kamili
  isipokuwa Mwenyezi Mungu, na
  hakuna   asikiaye  ya  siri  na
  minong'ono ila Mwenyezi Mungu, na
  hakuna   anayemiliki   makadirio
  isipokuwa Mwenyezi Mungu, basi
  kwa maana hiyo, hakuna wa kujibu
  dua isipokuwa Mwenyezi Mungu.
•  Na kwa ajili hiyo, haijuzu kwa
  Mwislamu   kuliomba   kaburi,  au
  kumwomba     aliyezikwa    humo
  vyovyote awavyo, kwa kuwa yeye
  hamsikii. Na kama hamsikii, basi ni
  vipi atamjibu au kumnufaisha? Hakika
  Mwenyezi   Mungu   Pekee   Ndiye
  Mwenye Kunufaisha na Mwenye
  Kudhuru. Na kwa ajili hiyo, ni wajibu
  kwa Mwislamu asijenge msikiti juu ya
  makaburi,  kwani  Mtume   Swalla
Mimi ni Mwislamu
  Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam
  amelikataza hilo.
•  Kadhalika, ni wajibu kwa mja
  alinganishe kati ya udhaifu wake na
  Nguvu za Mwenyezi Mungu Mtukufu,
  na kati ya umasikini wake na Utajiri
  wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kati
  ya ujinga wake na Elimu      ya
  Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kati ya
  unyonge wake na Utukufu wa
  Mwenyezi Mungu Mtukufu.
•  Na ajue kwamba utukufu ni wa
  Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na
  Waumini.
•  Hivyo yampasa awe ni miongoni mwa
  Waumini hawa ambao hawatawakali
  isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu
  Pekee,  wala   hawaombi  msaada
  isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu,
  wala hawaombi kinga na kujilinda
  isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu,
  wala hawaombi msaada wa dharura
  ila kwa Mwenyezi Mungu, wala
  hawamwogopi isipokuwa Mwenyezi
  Mungu, wala hawataraji isipokuwa
  kwa   Mwenyezi   Mungu,  wala
Mimi ni Mwislamu
   hawamwombi isipokuwa Mwenyezi
   Mungu, wala hawachinji isipokuwa
   kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wala
   hawaweki nadhiri isipokuwa kwa ajili
   ya Mwenyezi Mungu, wala hawaapi
   isipokuwa kwa Jina la Mwenyezi
   Mungu, wala hawaweki talasimu na
   hirizi  (amali),  wala   hawasadiki
   wasemayo    makuhani,   watabiri
   (wanajimu) na wachawi, na wala
   hawawaendei.
  • Na wao hawakosi rajua, na huwa na
   tahadhari ya mponyoko wa ndimi zao
   ili  wasije   kutelezea   motoni.
   Hawasemi: "Amependa Mwenyezi
   Mungu na amependa fulani", "lau si
   Mwenyezi    Mungu    na  wewe",
   "nimetawakali kwa Mwenyezi Mungu
   na   kwako".    Bali   waseme:
   "Nimetawakali kwa Mwenyezi Mungu
   Pekee",   "Amependa    Mwenyezi
   Mungu kisha amependa fulani".
   Maneno     haya   humsawazisha
Mwenyezi Mungu na waja Wake,      na ni
katika shirki ndogo.
Mimi ni Mwislamu
•  Na  kama  ilivyo  wajibu  kwetu
  kumwamini Mwenyezi Mungu, ni
  wajibu wetu vile vile tuwakatae
  mataghuti.
•  Na kigogo wa mataghuti ni shetani
  na kila yule aliyeabudiwa badala ya
  Mwenyezi Mungu naye akaridhia hilo.
•  Na kati ya mataghuti hawa ni yule
  aliyetunga sheria zinazoharamisha
  Aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu,
  au  kuhalalisha  Aliyoyaharamisha
  Mwenyezi Mungu.
•  Aidha,  taghuti   ni  kila yule
  aliyelingania hilo, au akawaamuru
  watu hilo, au akahukumu kwa hilo,
  kwa vile ametaadi na akavuka mpaka
  wa kiumbe wa kusikia na kutii.
• Basi   Allaah  Pekee  Ndiye
  Aliyewaumba wanadamu, na Ndiye
  Anayejua yanayowafaa, na kwa
  hivyo, hakuna  yeyote awezaye
  kuwapangia sheria isipokuwa Yeye
  tu.
Mimi ni Mwislamu

  (2) KUWAAMINI MALAIKA

•  Ninaamini kuwepo malaika ambao
  Mwenyezi   Mungu   Amewaumba
  kutokana na nuru, na Akawafanya
  kuwa na mbawa mbili mbili, tatu
  tatu, na nne nne. Nao hawali,
  hawanywi, hawalali wala hawaoi.
  Amewaamuru   kufanya  kazi  na
  kusimamia majukumu mbalimbali,
  nao hutekeleza hayo.
•  Malaika siku zote humtii Mwenyezi
  Mungu bila kuchoka. Hawamwasi na
  humwogopa Mola wao toka juu yao.
  Kuna kati yao aliyesujudu toka siku
  Alipoziumba   Mwenyezi   Mungu
  mbingu na ardhi hadi siku ya Kiyama.
  Na atakaponyanyua kichwa chake
  atasema:        "Subhaanak!
  Hatujakuabudu    ukweli   wa
  kukuabudu".
•  Wao ni waja wa Mwenyezi Mungu na
  si wanawake, na wala si wasaidizi
  Wake, na wao watawaombea shifaa
Mimi ni Mwislamu
 Waumini – kwa idhini ya Mwenyezi
 Mungu – siku ya Kiyama.

Kati ya malaika hawa, wapo:
 • Walinzi ambao huwalinda viumbe
   na madhara.
 • Watukufu    waandishi  ambao
   huandika matendo ya wanadamu,
   mema yao na mabaya yao.
 • Wenye    kumsabihi  Mwenyezi
   Mungu.   Hawa    humsabihi
   Mwenyezi Mungu mchana na usiku
   na hawachoki mpaka siku ya
   Kiyama.
 • Wenye     kuvinjari   ambao
   huhudhuria vikao vya dhikri,
   kisomo cha Qura-aan na vikao vya
   elimu.
 • Wabebaji Arshi ambao idadi yao ni
   wanane. Ni viumbe wakubwa mno
   kati ya viumbe wa Mwenyezi
   Mungu. Ndege huruka toka ncha
   ya sikio la mmoja wao hadi
   shingoni kwa muda wa miaka mia
   tano.
Mimi ni Mwislamu
•  Malaika wa mauti anayezitoa roho
  za viumbe kwa Amri ya Mwenyezi
  Mungu. Huyu ana wasaidizi wake.
•  Israfil atakayelipuliza baragumu,
  kisha viumbe vyote vitakufa kabla
  ya   kutokea  Kiyama.  Kisha
  litapulizwa  jingine, na  hapo
  watasimama viumbe wakiangalia.
•  Mikaili anayesimamia jukumu la
  mvua.
•  Ridhwaan ambaye ni mlinzi wa
  Pepo. Yeye ana wasaidizi wake
  walio   mbioni   kuwahudumia
  Waumini Peponi.
•  Maalik ambaye ni mlinzi wa moto.
  Ana   wasaidizi  wake  ambao
  viongozi wao ni kumi na tisa.
  Wana marungu ya chuma ya
  kuwaadhibu makafiri motoni -
  Mwenyezi Mungu Atuepushe na
  hayo.
•  Mkuu   wa  Malaika  ni Jibril
  aliyewakilishwa kupeleka wahyi
  kwa Manabii na Mitume.
Mimi ni Mwislamu
•  Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa
  Aalihii wa Sallam alimwona katika
  umbile lake. Kutokana na ukubwa
  wake, alizifunika peo za mbingu.
  Ana mbawa mia sita, naye ndiye
  aliyekikamata kijiji cha Lut kwa
  ncha   ya   ubawa    wake,
  akakinyanyua hadi juu mbinguni,
  kisha akakipindua juu chini.
•  Kuna malaika wengineo wengi
  zaidi ya hawa, na hakuna ajuaye
  askari wa Mola wako isipokuwa
  Yeye tu.

      :¯  ´ ³ ²± °
•  Malaika  huwapenda  Waumini
  ambao   Mwenyezi   Mungu
  Huwapenda   na  huwaombea
  maghfira.
•  Malaika mbali na nguvu zao hizi
  hupigana pamoja na Waumini.
Mimi ni Mwislamu
  (3) KUVIAMINI VITABU

•  Ninaviamini Vitabu vya Mwenyezi
  Mungu Alivyoviteremsha kwa Mitume
  Wake, na kwamba katika asili ya
  kuteremshwa Kwake, ni Maneno ya
  Mwenyezi Mungu Aliyowafunulia ili
  waifikishe sheria na dini Yake. Vitabu
  vikubwa zaidi ni:
     Quraan Tukufu iliyoteremshwa
  kwa Mtume wetu      Muhammad
  Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa
  Sallam.
     Injili iliyoteremshwa kwa Iysa
  Alayhi Ssalaam.
     Taurat  iliyoteremshwa   kwa
  Musa Alayhi Ssalaam.
     Zaburi  iliyoteremshwa   kwa
  Daud Alayhi Ssalaam.
     Sahifa zilizoteremshwa   kwa
  Ibrahim Alayhi Ssalaam.
Mimi ni Mwislamu
•  Kati ya hivi, kuna vilivyopotolewa na
  kubadilishwa kabla ya kushuka Qur-
  aan.
•  Na Qur-aan ndiyo iliyo juu ya Vitabu
  hivi, na ndiyo yenye kuongoza sheria
  zote na hukumu zake, na yenye
  kuondosha yale yote yenye kwenda
  kinyume na hukumu zake baada tu
  ya kuteremka kwake.
•  Na   kwamba  Mwenyezi  Mungu
  Hatokubali siku ya Kiyama ila amali
  kupitia  uongofu  wa  Qur-aan.
  Hatokubali amali kwa kufuata Vitabu
  vilivyotangulia baada ya kuteremka
  Qur-aan kwa Mtume Muhammad
  Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa
  Sallam.
•  Na kwamba Qur-aan ni Maneno ya
  Mwenyezi Mungu ya miujiza. Maneno
  haya yana utukufu wake, na wala
  hayaingiliwi na batili kabla yake wala
  baada yake. Mwenye kuyasema,
  amesema   kweli,   na  mwenye
  kuhukumia    kwayo,    amefanya
  uadilifu, na mwenye kuyafanyia kazi
Mimi ni Mwislamu
  basi hakika ameongolewa katika njia
  iliyonyooka, mwenye kushikamana
  nayo amefuzu na kuokoka, na
  mwenye kuyakengeuka atakuwa ni
  katika wenye kuhiliki.
•  Ni kwamba watu wa Qur-aan, hao
  ndio watu wa Mwenyezi Mungu
  waliokurubishwa Kwake, na kwamba
  mbora zaidi wa watu ni yule
  aliyejifundisha   Qur-aan   na
  akawafundisha watu, kwani Qur-aan
  hii  itakuja siku  ya  Kiyama
  ikimwombea shifaa kila aliyeisoma,
  akaihifadhi na akaifanyia kazi, na
  itawaombea watu wake Pepo.
•  Qur-aan   huzitwaharisha  nyoyo
  kutokana na shubha na matamanio
  yanayozichafua, huzikurubisha kwa
  Muumbaji Wake Subhaanahuu wa
  Ta'alaa, na huzihimiza kufanya kazi
  ili kufuzu na kupata neema za
  kudumu milele.
•  Kati ya adabu za kusoma Qur-aan ni:
     Kuwa twahara na wudhuu.
Mimi ni Mwislamu
 Kuelekea Kibla.
 Kukaa kwa adabu na heshima.
 Kutoisoma kwa haraka.
 Kuwa na unyenyekevu.
  Kuonyesha  huzuni  kwa
madhambi na kuvuka mipaka.
 Kulia kutokana na kumwogopa
Mwenyezi Mungu na Utukufu wa
Maneno Yake.
 Kusoma kwa sauti nzuri.
 Kusoma kwa sauti ya chini ili
kutowabughudhi wenye kuswali.
 Kuzingatia maana ya maneno.
 Kuhudhurisha moyo.
 Kutaamuli kwa kina Aayah za
Mwenyezi Mungu.
  Tuwe  na  yakini kuwa
kusimamisha hukumu za Kitabu
hiki kwa watu ni moja kati ya
sababu za kumakinishwa katika
ardhi na kuwashinda maadui.
Mimi ni Mwislamu
Basi harakia ndugu yangu Mwislamu
kwenda kwa Mola wako, na kikamate
Kitabu hiki kwa hima. Kuwa na shime
asikutangulie yeyote kuelekea kwa
Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi
Mungu Hufurahi zaidi kwa kurejea
kwako Kwake kuliko wanavyofurahi
watu kwa kurejea mtu wao aliyekuwa
mbali.
Mimi ni Mwislamu

   (4) KUWAAMINI MITUME
•  Ninawaamini  Mitume   wa   Mwenyezi
  Mungu.  Hakika   Mwenyezi   Mungu
  Aliwateua Mitume kati ya wanadamu,
  Akawafunulia Sheria Yake kwa njia ya
  wahyi, na Akawaamuru kuifikisha kwa
  watu, na kwamba mwenye kuwatii
  ataingia peponi, na mwenye kuwaasi
  ataingia motoni.

•  Kisha Akawatilia nguvu kwa miujiza
  yenye  kuonyesha   ukweli  wao  ili
  iwasaidie mbele ya wakadhibishaji, na
  ili iwe ni hoja kwao.

•  Na kwamba Mtume wa mwanzo ni
  Nuhu,  na  wa   mwisho   wao  ni
  Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa
  Aalihii wa Sallam.
Mimi ni Mwislamu

•  Na   kuwa  Mitume   hawa   ni   watu;
  wanakula,           wanakunywa,
  wanaoa,wanaugua na wanakufa. Wao
  ndio viumbe bora kabisa wa Mwenyezi
  Mungu na wamehifadhiwa na maasi.

•  Mitume wa Mwenyezi Mungu ni wengi.
  Mwenyezi Mungu Amewataja baadhi
  yao katika Qur-aan. Nao ni Muhammad
  Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa
  Sallam,    Ibrahim   Khalili   wa   Ar-
  Rahmaan,    Musa   aliyesemeshwa    na
  Allaah, Iysa Neno la Mwenyezi Mungu
  na Nuhu. Hawa ndio Mitume wenye
  azma ya juu Rehma na Amani ziwe juu
  yao.  Pia  Ismail,   Is-haaq,   Yakub,
  Harun,  Ayyub,     Yunus,   Sulayman,
  Daawud, Yahya, Zakariya, Hud, Saleh,
Mimi ni Mwislamu

  Yusuf, Shuayb, Ilyaas, Lut, Dhulkifl,
  Idris, na wengi wengineo. Kati yao
  kuna Aliowahadithia Mwenyezi Mungu
  katika     Qur-aan   na    wengineo
  Hakuwahadithia.

•  Jambo   la  kwanza   walilolilingania
  Mitume ni tawhid, na jambo kubwa
  zaidi walilolikataza ni shirki, na wote
  wamekuja na Uislamu na wito.

•  wa   tawhid.  Lakini  sheria  zao  na
  mifumo   ya   kumwabudu     Mwenyezi
  Mungu Mtukufu ilitofautiana kutokana
  na kutofautiana zama zao na nchi zao.

•  Na kwamba Mitume walitoa bishara ya
  kuja   kwa  Nabii  Muhammad   Swalla
  Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam na
Mimi ni Mwislamu

  wakawaamrisha          kaumu     zao
  kumwamini Muhammad Swalla Allaahu
  Alayhi   wa     Aalihii   wa    Sallam
  atakapotumwa kwao.

•  Tofauti kati ya Rasuli (Mtume) na
  Nabii   ni   kuwa   Rasuli    ni   yule
  aliyefunuliwa      sheria    mpya    na
  akaamrishwa    kuifikisha    kwa   watu.
  Ama   Nabii,  ni  yule   aliyetumwa    ili
  kuithibitisha na kuipitisha sheria ya
  Rasuli aliyemtangulia.

•  Ninaamini kuwa mbora wa Mitume
  mbele ya Allaah ni Muhammad Swalla
  Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam
  toka   kwa   mwana    wa  Ismaili   bin
  Ibrahim    Alayhima   Ssalaam.     Allaah
  Amemtuma      kwa      watu    wote,
Mimi ni Mwislamu

  Akahitimisha Unabii kwa Unabii wake,
  na Utume kwa Utume wake.

•  Akamtilia   nguvu    kwa    miujiza,
  Akamfanya bora kuliko Mitume wote.
  Pia  Ameufanya    Utume  wake   kuwa
  bora kuliko Utume wote uliotangulia,
  na  sheria  yake   kuwa  bora  kuliko
  sheria zinginezo zilizopita, na Kitabu
  chake  Qur-aan    kuwa  bora  kuliko
  Vitabu  vyote,   na  umati  wake  –
  Waislamu – kuwa bora kuliko uma
  nyinginezo.

•  Na Mola wake Akampa mambo ambayo
  Hakumpa    yeyote   katika   Manabii
  waliomtangulia. Kati ya mambo hayo
  ni:
Mimi ni Mwislamu

(1) Al Wasiylah: Nayo ndiyo daraja ya
  juu   kabisa    Peponi   ambayo
  Mwenyezi    Mungu   Amemwandalia
  Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa
  Aalihii wa Sallam.

(2) Al Kawthar: Nao ni mto Peponi
  wenye kupita chini ya Arshi ya Ar
  Rahman.

(3) Al  Hawdh:   Ni  sehemu   ambayo
  Waislamu     peke   yao   ndio
  watakayokunywa siku ya Kiyama.
  Siku ambayo watu watapatwa na
  kiu kikali, na jasho litawafika hadi
  magotini, viunoni na mabegani –
  kila mmoja kwa mujibu wa amali
  yake – na Waislamu watakunywa
  hapo kwa vikombe atakavyowapa
Mimi ni Mwislamu

  Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa
  Aalihii wa Sallam kwa mikono yake
  mitukufu.     Baada    ya  hapo
  hawatapatwa na kiu milele.

(4) Shafaa: Ni makamu ya kuhimidiwa
  siku ya Kiyama. Hapo Mtume Swalla
  Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam
  ataomba     shifaa  kwa   Mwenyezi
  Mungu   ili  Waislamu    waliofanya
  maasi   watolewe     motoni,   na
  hatobakia ndani ya moto yeyote
  anayeshuhudia      kwamba   hapana
  Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu
  na Muhammad ni Mtume wa Allaah.
  Aliyefanya maasi hatosalia milele
  motoni,   bali  atatoka   baada  ya
  kutakaswa na maasi yake.
Mimi ni Mwislamu

  Aliyewaamini Manabii wote na wala
  hakumwamini   Muhammad     Swalla
  Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam,
  basi hatatoka motoni.

(5) Na kwamba Allaah Amemnusuru na
  Akawanusuru     askari  wake  na
  wafuasi wake hadi siku ya Kiyama
  kwa kuzagaza hofu ndani ya nyoyo
  za maadui umbali wa mwendo wa
  mwezi. Na hakuna Nabii      yeyote
  aliyepewa   hili   kabla   yake
  Muhammad Swalla Allaahu Alayhi
  wa Aalihii wa Sallam.

(6) Na  ardhi  imefanywa   kwake  na
  Waislamu kuwa msikiti (sehemu ya
  kuswalia)   na   twahara,   na
Mimi ni Mwislamu

    haikufanywa   hivyo  kwa  Manabii
    waliomtangulia.

 (7) Na Allaah Amemtuma kwa watu na
    majini wote, lakini Mitume wengine
    wametumwa maalumu kwa watu
    wao tu.

 (8) Na kuwa yeye ndiye wa mwanzo
    kaburi lake kufunguka, na ndiye
    mwombezi wa kwanza, na ndiye wa
    kwanza kupewa shifaa, na ndiye wa
    kwanza kugonga mlango wa Pepo.
    Atakapougonga, mlinzi

wa  Pepo  Ridhwaan   atamuuliza:  "Nani
wewe?" Atajibu: "Muhammad". Ridhwaan
atamwambia:   "Kwako    nimeamrishwa
nisimfungulie yeyote kabla yako".
Mimi ni Mwislamu

Na  kati  ya  miujiza  ya  Mtume   Swalla
Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam ni:

       Kupasuka mwezi.

       Alilirejesha   jicho  la  Qatada
   lilipopofuliwa siku ya Uhud, macho yake
   yakarudi yakawa mazima kabisa.

       Aliurejesha muundi wa Ibn Al
   Hakam kama ulivyokuwa ulipovunjwa
   siku ya Vita vya Badr.

       Aliutaka mti utamke shahada,
   nao ukatamka shahada mbili mara tatu
   mbele ya kafiri, naye akasilimu.

       Kigogo   cha   mti  alichokuwa
   akihutubia  juu  yake    kililia  wakati
   alipokiacha na hakikunyamaza mpaka
   alipoiweka mikono yake juu yake.
Mimi ni Mwislamu

     Alikifanya chakula kidogo kuwa
kingi baina ya mikono yake miwili, na
wakaweza kula na kushiba zaidi ya
watu 80 chakula cha kujaa viganja
viwili.

     Aliyafanya maji kidogo kuwa
mengi siku ya Hudaybiyah wakati jeshi
lilipobakiwa na bakuli moja tu ya maji.
Hapo Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa
Aalihii wa Sallam aliingiza mikono yake
ndani, maji yakaanza kububujika kati ya
vidole  vyake   kama   chemchemu,
wakanywa   maji  Waislamu   wote  na
wakatawadhia   maji  hayo.  Walikuwa
kiasi cha watu 1400.

     Alipelekwa usiku hadi Msikiti
wa Al Aqsa, na kisha alipandishwa hadi
Mimi ni Mwislamu

mbingu za juu na kukomea Sidrat Al
Muntahaa.

      Alielezea na kuhadithia habari
za umma zilizotangulia na Manabii wao
nailhali  yeye   hana   kisomo;     hajui
kusoma wala kuandika. Pia alielezea
matukio yatakayotokea siku za usoni
kwa  kufunguliwa    Fursi  na    Rome,
kusambaratishwa     ufalme    wa   Kisra
aliyechanachana barua ya Mtume Swalla
Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam
aliyomtumia,     pamoja   na    miujiza
mingineyo mingi.

      Muujiza   mkubwa     zaidi   wa
Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii
wa  Sallam  ni  Qur-aan   Tukufu.    Ni
Mimi ni Mwislamu

muujiza   utakaosalia   hadi  siku    ya
Kiyama.

     Kisha  Allaah  Ameunyanyua
utajo  wake,  Akaliandamisha    jina  la
Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii
wa Sallam na Jina Lake Subhaanahuu
wa Taalaa, na Akaifanya shahada ya
kuwa hapana mola isipokuwa Allaah na
kwamba   Muhammad    ni  Mtume    wa
Mwenyezi Mungu kuwa ndio jambo la
kwanza   analoingia   nalo  mja  katika
Uislamu,na jambo la mwisho analotoka
nalo duniani. Basi yeyote ambaye neno
lake la mwisho litakuwa ni "Laailaaha
illa Allaah", ataingia peponi.

•  Ni  wajibu  wetu  kwa  upande    wa
  Mtume wetu Swalla Allaahu Alayhi
Mimi ni Mwislamu

  wa Aalihii wa Sallam tusilitangulize
  neno la kiumbe yeyote juu ya neno
  lake, au rai ya yeyote hata kama ana
  sauti  kwa  watu.  Na  ikiwa  watu
  watakutangulia kuhamia kwake, basi
  hama wewe kwenda katika sunnah
  yake katika kila jambo lako na wala
  usimfuate mwingine zaidi yake. Ni
  wajibu  wetu   tushikamane   sote
  pembezoni mwa amri yake na tumtii,
  kwani mwenye kumtii Mtume, basi
  huwa amemtii Mwenyezi Mungu.

       :   GFEDCBA
•  Na tusimwiite ila kwa kusema Mtume
  wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu
  Alayhi  wa   Aalihii  wa  Sallam.
  Tusiseme (Muhammad) basi.
Mimi ni Mwislamu

•  Tujipambe   kwa   adabu  zake,  na
  tumwige katika hali zake zote; kulala
  kwake,  kula    kwake,   kutembea
  kwake,  kuswali    kwake,   kufunga
  kwake,  kutoa  kwake     sadaka,  na
  jihadi yake.

•  Na tumpende zaidi kuliko nafsi zetu,
  wana wetu, wazazi wetu na watu
  wote.

•  Na tumpende kila yule anayempenda
  Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla
  Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam
  na  kumfanya    kiigizo  chake,  na
  tumchukie kila yule anayemchukia
  Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla
  Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam
  na wala hawajibiki na sheria yake.
Mimi ni Mwislamu

•  Hivyo basi, ni lazima kwa Mwislamu
  awapende     Waumini,    awanusuru,
  ajifananishe     nao,   ashughulikie
  mambo yao, asaidiane nao katika
  mambo ya kheri, na awafanye kuwa
  marafiki zake wa dhati.

•  Ni   wajibu    kwake   awabughudhi
  makafiri na   ukafiri   wao,  asiwatii,
  asiungane nao dhidi ya Waislamu,
  wala asisaidiane nao katika ubatilifu
  wao,  na  wala  asishiriki    katika
  sikukuu   zao.  Ni   haramu   kwake
  kuwadhulumu,     na   linalotakiwa  ni
  kuwatendea haki.

•  Ni wajibu wetu tuwapende Mama wa
  Waumini;    Wakeze   Mtume   Swalla
  Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam,
Mimi ni Mwislamu

  na  tuwapende    Maswahaba   Wake
  Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa
  Sallam, kwani wao ndio bora wa
  watu baada ya Manabii.

•  Pia ni wajibu wetu tuihuishe Sunnah
  yake Mtume Swalla Allaahu Alayhi
  wa Aalihii wa Sallam, tuidhihirishe
  sheria   yake,   na   tubalighishe
  ulinganio  wake   kwa  watu  wote.
  Kisha  tusubiri   maudhi  na  kero
  zinazotupata    katika  kuyapigania
  hayo, kwani hayo hayaepukiki.

•  Kwa vile Mwenendo wa Mwenyezi
  Mungu uliopita kwa viumbe Vyake
  unahukumia kuwa hakuna Nabii au
  walii yeyote aliyelingania haki hii ila
  alifanyiwa uadui na kuudhiwa.
Mimi ni Mwislamu

•  Zindukana ndugu yangu Mwislamu!
  Maudhi  ya  makafiri   yasikufanye
  ukaiacha dini yako. Kwani Mtume wa
  Mwenyezi   Mungu   Swalla  Allaahu
  Alayhi  wa   Aalihii   wa   Sallam
  aliudhiwa    wakati    Maswahaba
  walipokuwa   wachache,     nao  pia
  waliudhiwa wakafanya subira.

•  Na wala usilegeze azma yako hata
  kama     watakwambia        kuwa
  unayoyazungumza    ni  upuuzi,   una
  misimamo migumu, au umepitwa na
  wakati. Au wakisema: "ashachezewa
  akili huyo". Kwani wewe una kiigizo
  chema  kwa  Mtume    wa  Mwenyezi
  Mungu, yeye ashaambiwa mshairi na
  hata mwendawazimu.
Mimi ni Mwislamu

•  Wala   usisononeke    ukiambiwa
   mpotevu mwenye siasa kali. Hii ndio
   tabia ya makafiri kwa Waumini.

   :

((Na wanapowaona, husema hakika
  hawa bila shaka ni wapotevu)).

•  Ikiwa watu wako makundi mawili, je
   haikutoshi  wewe  kuwepo   katika
   kundi   aliloko   Mtume   wako
   Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa
   Aalihii wa Sallam?!

•  Achana nao hao mpaka ifike siku
   ambayo  dhalimu   ataviuma  vidole
   vyake    aseme:   "Laiti  mimi
   ningeliifuata njia pamoja na Mtume".
Mimi ni Mwislamu

                   
              : ¯

•  Wala usibabaike au kuchanganyikiwa
  kama watakwambia kuwa wewe ni
  gaidi au mwovu, kwani hayo ndio
  madai  ya  madhalimu    dhidi  ya
  Waumini duniani na akhera. Ni kuwa
  pale  Malaika  watakapowaongoza
  kwenda   Jahannamu  wakisunukia,
  wataangalia humo kisha waseme:

   :   JIH GFEDCBA
       ((Na watasema: Mbona
      hatuwaoni watu tuliokuwa
      tukiwazingatia kuwa ni katika
       waovu?))
Mimi ni Mwislamu

•  Na hapa, Waumini (ambao makafiri
  wamewaita     kuwa     ni  waovu)
  watawaita toka kwenye magorofa ya
  juu kabisa ya Firdaws wakiwaambia:

        : ¯     LKJIHGF
     ٤٤ : ‫اف‬   ‫(( ا‬   ‫ر‬  ‫و‬  ‫و‬  ‫)) أن‬

      ((Hakika sisi tumeyakuta
    Aliyotuahidi Mola wetu kuwa ni
               kweli))
Mimi ni Mwislamu
(5) KUAMINI SIKU YA MWISHO

•  Ninaiamini siku ya mwisho, nayo ni
  iku ambayo dunia (nyumba ya amali)
  itamalizika, na akhera (nyumba ya
  malipo) itasimama, wema wakalipwa
  Pepo, na waovu wakalipwa moto.

•  Katika  siku  ya  Kiyama,  mizani
  itawekwa,  na  kila  mja  atapewa
  kitabu chake. Atakayepokea kitabu
  chake kwa mkono wake wa kuume,
  basi Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa
  Aalihii wa Sallam atakuwa pamoja
  naye Peponi. Ama yule atakayepokea
  kitabu chake kwa mkono wake wa
  kushoto, basi atakuwa pamoja na
Mimi ni Mwislamu

  Firauni   –laana   ziwe   juu   yake–
  motoni.

•  Sirati   itawekwa,   atakayefanikiwa
  kuivuka   basi  atafikia  Peponi.  Ama
  ambaye kulabu zitamnyakua kutokana
  na    amali   zake    mbovu,   basi
  ataangukia motoni.

•  Siku ya Kiyama ina dalili, ina alama
  ndogo na ina alama kubwa.

•  Miongoni     mwa  alama   ndogo   ni
  kupotea uaminifu, kukithiri mauaji,
  madaraka kukamatwa kwa mabavu
  na mafasiki, na masuala muhimu
  kuzungumziwa na wasiojua kitu.

•  Na miongoni mwa alama kubwa ni
  kuibuka Al Mahdi, kusimama ukhalifa
Mimi ni Mwislamu

  wongofu    utakaokwenda    juu   ya
  misingi ya njia ya Utume kabla ya
  kutokea Kiyama, na kudhihiri masihi
  mwongo.

•  Pia kuteremka Iysa Alayhi Ssalaam ili
  awaongoze    Waislamu,    apigane  na
  makafiri, avunje vunje misalaba, aue
  nguruwe,    na  azikatae  dini   zote
  nyingine ila Uislamu tu.

•  Basi haitobakia nyumba yoyote ya
  mjini   au  ya   mashambani     ila
  Mwenyezi Mungu Ataiingiza dini hii,
  kwa heshima ya mwenye nguvu, au
  kwa udhalili wa mnyonge.

•  Vile vile kutoka Yaajuju na Maajuju.
  Pia      atatoka       mnyama
Mimi ni Mwislamu

  anayewasemesha    watu,  na  jua
  litachomoza toka magharibi, Qur-aan
  itaondoshwa na mambo mengineyo.

•  Basi yeyote atakayefanya amali ya
  uzito wa atomu ikiwa ni ya kheri au
  ni ya shari, ataiona siku ya Kiyama
  ndani ya kitabu chake.

•  Basi harakieni kwenye mambo ya
  kheri kabla haujamalizka muda wa
  kusajiliwa kwa kufa mja katika muda
  ambao haujui yeyote ila Mwenyezi
  Mungu Pekee.

•  Wakamwosha      jamaa     zake,
  wakamvisha   sanda,  wakamswalia,
  wakamzika. Kisha akajiwa na Malaika
  wawili;  Munkari    na  Nakiyr,
Mimi ni Mwislamu

  wakamkalisha kitako na kumwuuliza:
  "Nani Mola wako? Nini dini yako?
  Nani Nabii wako?"

•  Ikiwa atajibu kuwa: "Allaah ni Mola
  wangu, na Uislamu ndiyo dini yangu,
  na Muhammad Swalla Allaahu Alayhi
  wa Aalihii wa Sallam ndiye Nabii
  wangu na Mtume wangu" – na Allaah
  Akamwezesha     hilo   –    basi
  itafunguliwa  katika   kaburi   lake
  harufu  ya  rayhaan   hadi  peponi,
  akaona  mashukio  yake   huko,  na
  makasri yake na ufalme wake. Hapo
  atashangilia kwa furaha kubwa, na
  kaburi lake litapanuliwa upeo wa
  macho.
Mimi ni Mwislamu

•  Na ikiwa ni katika makafiri, basi
  hatoweza    kujibu  chochote,    kwani
  majibu wakati huo si kwa akili au
  werevu wa mtu.

•  Bali Mwenyezi Mungu Huwathibitisha
  na   kuwaimarisha   watu    wa  imani
  wakati      huo      kwa     yale
  waliyoyatanguliza     kati   ya  amali
  njema zilizosimamia juu ya tawhid,
  utekelezaji   wa   faradhi,   kushiriki
  jihadi,  kutenda    mema,   kuamrisha
  mema,     kukataza    mabaya,   kutoa
  sadaka, kusoma Qur-aan, kufunga
  siku   za  joto  kali,  na  kusimama
  kuswali muda mrefu usiku wa baridi
  kali.
Mimi ni Mwislamu

•  Ama akiwa ni katika makafiri, basi
  kaburi lake humbana hadi mbavu
  zake zikaingiana katika mwili wake,
  na kaburi lake huwa ni shimo katika
  mashimo ya motoni kwa sababu ya
  amali zake mbaya.

•  Basi jitahidi ndugu yangu Mwislamu,
  kwani leo ni amali na hakuna hisabu,
  lakini kesho ni hisabu na hakuna
  amali.

•  Na  siku  hiyo,  Waislamu  watiifu
  wataingia Peponi peke yao, kwa vile
  Mwenyezi  Mungu  Hatoikubali  dini
  yoyote siku ya Kiyama isipokuwa
  Uislamu.
Mimi ni Mwislamu

•  Ndani ya Pepo kuna neema ambazo
  hakuna sikio lililowahi kuzisikia, wala
  jicho lililowahi kuziona, wala hata
  kuwaziwa    katika   akili   ya
  mwanadamu. Neema zake zitasalia
  milele  wala   hazitomalizika,  na
  waliomo humo hawatakufa milele.
  Neema kubwa zaidi ya zote humo, ni
  kuuangalia Uso wa Mwenyezi Mungu
  Mola wa walimwengu wote.

•  Na  waasi,   waovu  na  makafiri
  wataingia motoni. Ndani ya moto,
  kuna adhabu zisizoweza kuvumilika
  Alizoziandaa Mwenyezi Mungu kwa
  ajili ya makafiri. Milima mirefu thabiti
  haiwezi kuzivumilia adhabu hizi, na
Mimi ni Mwislamu

  hao   wataadhibiwa    humo   bila
  kupumzishwa.

•  Na  humo,  wafuasi  wa  mataghuti
  wataomba      adhabu   iongezwe
  maradufu    kwa   wakubwa   wao
  waliowapoteza. Na hapo Mwenyezi
  Mungu Ataamuru adhabu iongezwe
  maradufu kwa wote.

•  Basi thibiti ndugu yangu Mwislamu
  juu ya haki hii, wala usidanganyike
  kabisa kuona kuwa wavunjaji sheria
  ni wengi zaidi, kwani ikiwa wewe
  utawatii   na  ukawafuata   wengi
  waliomo ardhini, basi watakupoteza
  njia ya Mwenyezi Mungu. Nawe pita
  pamoja na wenye kupita kuelekea
  kwa Mwenyezi Mungu.
Mimi ni Mwislamu

•  Kwani  kundi    katika    umma   wa
  Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa
  Aalihii wa Sallam litaendelea kuwa
  juu ya haki likiwa na nguvu, hawezi
  kuwadhuru yeyote aliyekwenda nao
  kinyume au aliyewasaliti mpaka siku
  ya Kiyama.

•  Basi ni mbinu zipi za kuzijua ngazi
  hizo za kupanda juu, na kuokoka na
  ngazi hizo za kuporomokea chini? Na
  ni  mbinu   zipi   za     kuwafikia
  waliotangulia wenye kukurubishwa,
  na  kujiweka  mbali    na  wapingaji
  wenye kuangamia? Bila shaka ni toba
  ya  kweli   ya   kusahihisha     na
  kurekebisha   yaliyopita,    na   amali
  njema  za   kuweka     sawa    umri
Mimi ni Mwislamu

  uliosalia, na kuweka nia ya kweli ya
  kunyooka na kutokengeuka.

•  Basi  kuwa  pamoja  na   watu  kwa
  kiwiliwili chako, ukiuza, ukinunua,
  ukioa na ukiiamirisha ardhi kwa yale
  Aliyokuhalalishia Mwenyezi Mungu.

• Wala moyo wako usifungamane na
  kitu chochote cha kidunia, bali nenda
  na   moyo   wako  pale   ambapo
  unatakikana uwe, huko chini ya Arshi
  ya Ar Rahmaan, na sujudu kwa moyo
  wako  sijdah  ambayo   utaendelea
  kuisujudu hadi siku ya Kiyama.
Mimi ni Mwislamu

(6) KUAMINI QADHAA NA QADARI


 •  Nako ni kuamini kwamba Mwenyezi
   Mungu   Anayajua    yote   yaliyomo
   ulimwenguni, yote yanayofanyika na
   yatakayotokea hadi siku ya Kiyama.
   Hata   chembe   ndogo  mno,  Yeye
   Hakosi  kuijua.  Na  kwamba   Yeye
   Anavijua vitendo vya waja, riziki zao,
   muda wao wa kuishi, na nani kati yao
   atakuwa wa peponi, na nani kati yao
   atakuwa    wa     motoni   kabla
   Hajawaumba.

 •  Na   kwamba    Mwenyezi    Mungu
   Ameyaandika makadirio haya katika
   Lawh   Al  Mahfuudh   kabla   hata
   Hajaziumba mbingu na ardhi kwa
   miaka elfu hamsini, na kwamba Lawh
Mimi ni Mwislamu

  Al Mahfuudh hii hakuna malaika wa
  karibu  au   hata  Nabii  aliyetumwa
  awezaye kuichungulia.

•  Hata   kijusi  kinapokuwa    ndani   ya
  tumbo   la   uzazi  la  mama     yake,
  Mwenyezi     Mungu    Huwaamrisha
  Malaika waandike kama ni cha kike
  au kiume, waandike na riziki yake,
  amali yake, muda wake wa kuishi na
  hatima yake (ima peponi au motoni).
  Pia  waandike   mazuri    na  mabaya
  atakayokabiliana nayo.

•  Kisha   unapoingia    usiku    wa  cheo
  (Laylatul     Qadr),     huteremka
  makadirio ya     mwaka mzima      toka
  Lawh al Mahfuudh kati ya ajali za
  watu, riziki zao, nani kati yao atahiji
  mwaka huo na mengineyo. Katika
Mimi ni Mwislamu

  usiku huo, hukadiriwa mambo ya
  mwaka mzima.

•  Kisha huteremka makadirio ya kila
  siku kwa nyakati zake na watu wake,
  hapo Mwenyezi Mungu Huwanyanyua
  watu na wengine Huwashusha.

•  Na  tuamini  kuwa   Mapendeleo  ya
  Mwenyezi    Mungu   ndiyo  yawayo,
  Alilolitaka huwa na Asilolitaka haliwi.
  Mwenyezi    Mungu    Hana   wa
  kumshinda, na Yeye Ndiye Mwenye
  kuzipindua   nyoyo.   Humwongoa
  Amtakaye kwa fadhila Zake na rehma
  Zake, na Humpoteza Amtakaye kwa
  Uadilifu  Wake  na  Hekima   Yake,
  kwani Yeye Ndiye Ajuaye zaidi nani
  anastahiki   uongofu   na   nani
  anastahiki upotevu.
Mimi ni Mwislamu

•  Na Mwenyezi Mungu Haulizwi yale
  Ayafanyayo lakini watu huulizwa.

•  Na tuamini kuwa Mwenyezi Mungu
  Amekiumba   kila  kitu,  na  hakuna
  chembe yoyote ndogo ulimwenguni
  isipokuwa     Mwenyezi       Mungu
  Ameiumba   na  Akaumba    kutikisika
  kwake na kutulia kwake.

•  `Na kwamba Yeye Amewaumba waja
  na vitendo vyao, na kwamba Yeye
  Amewaumbia     waja    uwezo    na
  mapendeleo   yao  ili  wajichagulie
  wenyewe vitendo vyao.

•  Na   kwamba    Mwenyezi     Mungu
  Mtukufu Amewaamuru viumbe Wake
  wamtii, na Akawaahidi kuwapa Pepo
  Yake   wakifanya      hivyo,   na
  Amewakataza    kumwasi    Yeye,   na
Mimi ni Mwislamu

  Akawapa onyo la kuwaingiza ndani
  ya moto Wake wakifanya hivyo, na
  wala Hakuwakalifisha kazi isipokuwa
  ile ambayo wanaweza kuifanya. Na
  hapo   wakagawanyika    makundi
  mawili: Waumini na makafiri; kwa
  hiari yao wenyewe, kwa mapendeleo
  yao wenyewe na kwa uwezo wao
  wenyewe, na yote hayo Mwenyezi
  Mungu Amewaumbia.

•  Na  kwamba  thawabu  na  adhabu
  hutokana na kuifuata sheria, si kwa
  kutangulia Elimu ya Mwenyezi Mungu
  kwao. Basi yeyote atakayefanya amali
  yoyote ya kheri ya uzito wa atomu,
  atalipwa kwayo. Na yeyote atakayefanya
  amali yoyote ya shari ya uzito wa
  atomu, basi ataadhibiwa kwayo.
Mimi ni Mwislamu

•  Na  kwamba    kinachozingatiwa   ni
  mwisho wa matendo, na kwamba kila
  mja ni mwenye kuendeshwa katika
  lile aliloumbiwa kati ya kufurahika
  Peponi au kupata shakawa motoni.

•  Na kwa ajili hiyo, ni wajibu kwa mja
  aogope mwisho mbaya, na aendelee
  daima kumwomba Mwenyezi Mungu
  na  amhitajie,  Amhidi  katika  njia
  iliyonyooka, na adumu kumwomba
  Amsaidie katika kumtii, na ajilinde
  Kwake na maasia, kwa vile mja hana
  hila wala nguvu zozote za kuyafanya
  hayo ila kwa Uwezo wa Mwenyezi
  Mungu.

•  Na  kwamba    Waumini   Huridhia
  Qadhaa  ya  Mwenyezi   Mungu  na
  Qadari Yake; ya kheri yake na ya
Mimi ni Mwislamu

   shari yake, katika misukosuko na
   katika furaha, na wana yakini kuwa
   hawezi   yeyote     kuwanufaisha
   isipokuwa kwa Qadari ya Mwenyezi
   Mungu,   na   wala   hawadhuru
   isipokuwa  liwe  lisha  andikwa  na
   Mwenyezi Mungu.

 •  Na mja hatopata utamu wa imani
   mpaka  pale  atakapojua  kwamba
   lililompata lisingekuwa la kumkosa,
   na  lililomkosa   lisingekuwa   la
   kumpata.

    Na mwisho naomba nikisema:
   "Ninamhimidi Mwenyezi Mungu, na
ninamwomba Aniingize Peponi mimi na
Waislamu wengine, na Anilinde na moto
 mimi na Waislamu wengine". Aamiyn.
Mimi ni Mwislamu
Mimi ni Mwislamu
  ed c b a ` _
     k j ih g f
[٨٥:‫ان‬  ‫]ل‬
               Ù        
anamuslim@windowslive.com       Ø    ×    ª Ø
        WWW.Iam-Muslim.com           ٢٠١٠ J ١٤٣١
         ‫و‬        ‫ق‬    ‫ا‬
        ٢٠٠٩L٢٢٢٧٤ W

     ٠١٢٠١٥٢٩٠٨ :ª              W
Mimi ni Mwislamu

          ª
        a


٠١٢٥٨٣٤٥٧٤     ٠١٠٦٧١٤٧٦٨

More Related Content

More from iam-muslim

Iam muslim persian
Iam muslim persianIam muslim persian
Iam muslim persianiam-muslim
 
Hokm almabtoor-shatem-alrasool ara
Hokm almabtoor-shatem-alrasool araHokm almabtoor-shatem-alrasool ara
Hokm almabtoor-shatem-alrasool araiam-muslim
 
Iam muslim eng
Iam muslim engIam muslim eng
Iam muslim engiam-muslim
 
Iam muslim greek
Iam muslim greekIam muslim greek
Iam muslim greekiam-muslim
 
Iam muslim french
Iam muslim frenchIam muslim french
Iam muslim frenchiam-muslim
 
Iam muslim ger
Iam muslim gerIam muslim ger
Iam muslim geriam-muslim
 
Iam muslim ara
Iam muslim araIam muslim ara
Iam muslim araiam-muslim
 
Iam muslim hausa
Iam muslim hausaIam muslim hausa
Iam muslim hausaiam-muslim
 
Iam muslim chin
Iam muslim chinIam muslim chin
Iam muslim chiniam-muslim
 
Abwab almagfera ara
Abwab almagfera araAbwab almagfera ara
Abwab almagfera araiam-muslim
 
Iam muslim ital
Iam muslim italIam muslim ital
Iam muslim italiam-muslim
 
Iam muslim fulani
Iam muslim fulaniIam muslim fulani
Iam muslim fulaniiam-muslim
 
Iam muslim amharic
Iam muslim amharicIam muslim amharic
Iam muslim amhariciam-muslim
 
Iam muslim malay
Iam muslim malayIam muslim malay
Iam muslim malayiam-muslim
 
العبادات القلبية
العبادات القلبية العبادات القلبية
العبادات القلبية iam-muslim
 

More from iam-muslim (15)

Iam muslim persian
Iam muslim persianIam muslim persian
Iam muslim persian
 
Hokm almabtoor-shatem-alrasool ara
Hokm almabtoor-shatem-alrasool araHokm almabtoor-shatem-alrasool ara
Hokm almabtoor-shatem-alrasool ara
 
Iam muslim eng
Iam muslim engIam muslim eng
Iam muslim eng
 
Iam muslim greek
Iam muslim greekIam muslim greek
Iam muslim greek
 
Iam muslim french
Iam muslim frenchIam muslim french
Iam muslim french
 
Iam muslim ger
Iam muslim gerIam muslim ger
Iam muslim ger
 
Iam muslim ara
Iam muslim araIam muslim ara
Iam muslim ara
 
Iam muslim hausa
Iam muslim hausaIam muslim hausa
Iam muslim hausa
 
Iam muslim chin
Iam muslim chinIam muslim chin
Iam muslim chin
 
Abwab almagfera ara
Abwab almagfera araAbwab almagfera ara
Abwab almagfera ara
 
Iam muslim ital
Iam muslim italIam muslim ital
Iam muslim ital
 
Iam muslim fulani
Iam muslim fulaniIam muslim fulani
Iam muslim fulani
 
Iam muslim amharic
Iam muslim amharicIam muslim amharic
Iam muslim amharic
 
Iam muslim malay
Iam muslim malayIam muslim malay
Iam muslim malay
 
العبادات القلبية
العبادات القلبية العبادات القلبية
العبادات القلبية
 

Iam muslim sawhilil

 • 1. ¯ : Mimi ni Mwislamu Authorship Muhammed Ashraf Salah
 • 3. Mimi ni Mwislamu Kwa jina la Mungu wa Rehema hgfedc ba`_ : ¯ kji Na mtu anataka dini nyingine zaidi ya Uislamu wala kukubali kuwa wakati ni mmoja wa wenye kukhasiri Akhera Al-Imran: 85
 • 4. Mimi ni Mwislamu Copyright, distribution and translation are reserved for every Muslim Legal Deposit No. 22274 / 2008 International Serial 977-6157-64-5 For charitable distribution call: 0020101459613 For suggestions e-mail: anamuslim@windowslive.com WWW.Iam-Muslim.com
 • 5. Mimi ni Mwislamu (1) KUMWAMINI MWENYEZI MUNGU Mimi ni Mwislamu… • Ninamwamini Mwenyezi Mungu Pekee Asiye na mshirika na hakuna mola mwingine isipokuwa Yeye, Hakuzaa wala Hakuzaliwa, na hakuna kamwe kifano chake. • Ameumba mbingu na ardhi, Naye Ndiye Anayezimiliki. Anayajua yaliyofichikana na yenye kuonekana. Yu Hai na Hafi, Anayasimamia mambo yote milele na Halali. • Ana Majina Mazuri Kabisa na Sifa za Juu. Kati yake ni Majina tisini na tisa, mwenye kuyajua na kuyadhibiti vyema na akamwomba Mwenyezi Mungu Kwayo, ataingia peponi. • Kati yake ni Sifa za Upweke, kwani Yeye Subhaanahu wa Taalaa ni Mmoja wa Dhati, Sifa na Vitendo, Aliyepwekeka, Aliye Pekee, Mkusudiwa, Mmiliki wa ufalme.
 • 6. Mimi ni Mwislamu • Na Sifa za Utukufu, kwani Yeye ni Mwenye hekima, Mwenye habari ya kila jambo, Mwelekezaji wa manufaa, Haki, wa Mwanzo, wa Mwisho, wa Dhahiri, wa Siri, Mrithi, Mwenye Kubakia, Mkwasi, Mtakasifu, Mwenye Kushuhudia, Aliye Karibu, Mbora wa Kupangilia, Mwadilifu, Nuru ya mbingu na ardhi, Mwenye Utukufu na Ukarimu. • Na Sifa za Uadhama, kwani Yeye ni Mshindi Asiyeshindika, Mwenye Sifa zote Tukufu, Mwenye Uadhama, Mwenye Sifa za Utukuzo, Mwenye Kulazimisha, Mwenye Nguvu, Aliye Imara, Mteza nguvu, Mweza, Mwenye uwezo wa juu, Mwingi wa Kunusuru, Aliye Juu, Aliye Juu ya vyote. • Na Sifa za Uwezo, kwani Yeye ni Mwingi wa Ujuzi, Mwenye Kusikia, Mwenye kuona, Yu Hai, Mwenye Kukamata, Mwenye Kukunjua, Mwenye Kushusha, Mwenye Kupandisha, Mwenye Kutukuza, Mwenye Kudhalilisha, Mwenye Kutoa, Mwenye Kuzuia, Mwenye Kunufaisha,
 • 7. Mimi ni Mwislamu Mwenye Kudhuru, Mwenye Kuhuisha, Mwenye Kufisha, Mwenye Kutanguliza na Mwenye Kuchelewesha. • Na Sifa za Uumbaji, kwani Yeye ni Muumbaji, Msanifu wa Maumbile, Mtiaji Sura, Hakimpiti au Kumshinda kitu, Mbunifu, Mwenye Kuanzisha, Mwenye Kurejesha, Mwenye Kufufua, Mwenye Kukusanya, Mpaji Mkuu, Mfunguzi wa kila jambo, Mwingi wa Kuruzuku, Mwenye Kutajirisha, Mdhibiti wa idadi, Mwenye Kudhibiti mambo, Mwenye Kuhifadhi, Mlinzi na Muumbaji wa mbingu na ardhi bila ruwaza. • Sifa za Rehma, kwani Yeye ni Mwingi wa Rehma, Mwingi wa Kurehemu, Mwingi wa Huruma, Mwenye Kuneemesha neema nzuri, Mwingi wa Penzi, Mtenda Wema, Mwingi wa Kughufiria, Mwenye Kusamehe, Mwingi wa Kukubali toba, Mwenye Amani, Mtoaji amani na imani, Mpole, Mwenye Kulipa vyema, Mkarimu, Mwenye Kuneemesha, Mwingi wa Kutoa, Mwenye Kusaidia, Mwenye Kujibu,
 • 8. Mimi ni Mwislamu Mkunjufu, Mwingi wa subira, Mvumilivu kwa Waja Wake, Latifu, Wakili, Mwenye Kutoa Misaada, Mwenye Kuombwa msaada na Mwenye Kukubali toba. • Amemneemesha mwanadamu neema nyingi zisizo na hesabu. Na hakuna neema yoyote anayoneemeka nayo mja ila hutoka kwa Mwenyezi Mungu Pekee, kwani Yeye Ndiye Aliyemuumba na Akampa uhai, Akamfanya asikie na aone, Akamkirimu, kisha Akamruzuku na Akamfanyia wema. • Kwa ajili hiyo, ni lazima mja amwabudu Mwenyezi Mungu Peke Yake – nako ni kufuata amri Yake na kuacha makatazo Yake – kwa kuwa hastahiki yeyote kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu Peke Yake. • Vile vile, bila shaka Mwenyezi Mungu Anazijua hali zote za mja kati ya utiifu
 • 9. Mimi ni Mwislamu na uasi. Hivyo basi, ni wajibu moyo wa mja ujae haiba kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, utukuzo na mapenzi, na aone haya kumwasi na aachane na maasi, kwani Mwenyezi Mungu Humwona wakati akiyafanya. • Anafurahi kwa amali zake njema zinazomkurubisha kwenye radhi za Muumbaji wake Subhaanahuu wa Taala. Hivyo huzidi kufanya amali hizo hadi kufikia ngazi ya ihsani, kwani imani huzidi kwa matendo mema na hupungua kwa maasi. • Asivutike kwenye matamanio, hawaa au bid'a, bali avutike kwa Mwenyezi Mungu Pekee huku akifuata maamrisho ya Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam. Asitafute kwa amali yake starehe ndogo ya dunia bali atafute kwayo malipo toka kwa Mwenyezi Mungu tu. • Aidha, hakika Mwenyezi Mungu Ana huruma mno kwa mwanadamu kuliko huruma ya mama kwa mwanaye. Na rehma Yake imekienea kila kitu.
 • 10. Mimi ni Mwislamu Hivyo basi, ni wajibu kwa mja amwombe na anyenyekee Kwake katika haja zake za kidunia na za kiakhera, na wala asimwombe yeyote mwingine. • Kwa vile hakuna faida yoyote ya kumwomba asiye Mwenyezi Mungu, kwa kuwa hamiliki uwezo ulio kamili isipokuwa Mwenyezi Mungu, na hakuna asikiaye ya siri na minong'ono ila Mwenyezi Mungu, na hakuna anayemiliki makadirio isipokuwa Mwenyezi Mungu, basi kwa maana hiyo, hakuna wa kujibu dua isipokuwa Mwenyezi Mungu. • Na kwa ajili hiyo, haijuzu kwa Mwislamu kuliomba kaburi, au kumwomba aliyezikwa humo vyovyote awavyo, kwa kuwa yeye hamsikii. Na kama hamsikii, basi ni vipi atamjibu au kumnufaisha? Hakika Mwenyezi Mungu Pekee Ndiye Mwenye Kunufaisha na Mwenye Kudhuru. Na kwa ajili hiyo, ni wajibu kwa Mwislamu asijenge msikiti juu ya makaburi, kwani Mtume Swalla
 • 11. Mimi ni Mwislamu Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam amelikataza hilo. • Kadhalika, ni wajibu kwa mja alinganishe kati ya udhaifu wake na Nguvu za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kati ya umasikini wake na Utajiri wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kati ya ujinga wake na Elimu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kati ya unyonge wake na Utukufu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. • Na ajue kwamba utukufu ni wa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na Waumini. • Hivyo yampasa awe ni miongoni mwa Waumini hawa ambao hawatawakali isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu Pekee, wala hawaombi msaada isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, wala hawaombi kinga na kujilinda isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, wala hawaombi msaada wa dharura ila kwa Mwenyezi Mungu, wala hawamwogopi isipokuwa Mwenyezi Mungu, wala hawataraji isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, wala
 • 12. Mimi ni Mwislamu hawamwombi isipokuwa Mwenyezi Mungu, wala hawachinji isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wala hawaweki nadhiri isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wala hawaapi isipokuwa kwa Jina la Mwenyezi Mungu, wala hawaweki talasimu na hirizi (amali), wala hawasadiki wasemayo makuhani, watabiri (wanajimu) na wachawi, na wala hawawaendei. • Na wao hawakosi rajua, na huwa na tahadhari ya mponyoko wa ndimi zao ili wasije kutelezea motoni. Hawasemi: "Amependa Mwenyezi Mungu na amependa fulani", "lau si Mwenyezi Mungu na wewe", "nimetawakali kwa Mwenyezi Mungu na kwako". Bali waseme: "Nimetawakali kwa Mwenyezi Mungu Pekee", "Amependa Mwenyezi Mungu kisha amependa fulani". Maneno haya humsawazisha Mwenyezi Mungu na waja Wake, na ni katika shirki ndogo.
 • 13. Mimi ni Mwislamu • Na kama ilivyo wajibu kwetu kumwamini Mwenyezi Mungu, ni wajibu wetu vile vile tuwakatae mataghuti. • Na kigogo wa mataghuti ni shetani na kila yule aliyeabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu naye akaridhia hilo. • Na kati ya mataghuti hawa ni yule aliyetunga sheria zinazoharamisha Aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu, au kuhalalisha Aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu. • Aidha, taghuti ni kila yule aliyelingania hilo, au akawaamuru watu hilo, au akahukumu kwa hilo, kwa vile ametaadi na akavuka mpaka wa kiumbe wa kusikia na kutii. • Basi Allaah Pekee Ndiye Aliyewaumba wanadamu, na Ndiye Anayejua yanayowafaa, na kwa hivyo, hakuna yeyote awezaye kuwapangia sheria isipokuwa Yeye tu.
 • 14. Mimi ni Mwislamu (2) KUWAAMINI MALAIKA • Ninaamini kuwepo malaika ambao Mwenyezi Mungu Amewaumba kutokana na nuru, na Akawafanya kuwa na mbawa mbili mbili, tatu tatu, na nne nne. Nao hawali, hawanywi, hawalali wala hawaoi. Amewaamuru kufanya kazi na kusimamia majukumu mbalimbali, nao hutekeleza hayo. • Malaika siku zote humtii Mwenyezi Mungu bila kuchoka. Hawamwasi na humwogopa Mola wao toka juu yao. Kuna kati yao aliyesujudu toka siku Alipoziumba Mwenyezi Mungu mbingu na ardhi hadi siku ya Kiyama. Na atakaponyanyua kichwa chake atasema: "Subhaanak! Hatujakuabudu ukweli wa kukuabudu". • Wao ni waja wa Mwenyezi Mungu na si wanawake, na wala si wasaidizi Wake, na wao watawaombea shifaa
 • 15. Mimi ni Mwislamu Waumini – kwa idhini ya Mwenyezi Mungu – siku ya Kiyama. Kati ya malaika hawa, wapo: • Walinzi ambao huwalinda viumbe na madhara. • Watukufu waandishi ambao huandika matendo ya wanadamu, mema yao na mabaya yao. • Wenye kumsabihi Mwenyezi Mungu. Hawa humsabihi Mwenyezi Mungu mchana na usiku na hawachoki mpaka siku ya Kiyama. • Wenye kuvinjari ambao huhudhuria vikao vya dhikri, kisomo cha Qura-aan na vikao vya elimu. • Wabebaji Arshi ambao idadi yao ni wanane. Ni viumbe wakubwa mno kati ya viumbe wa Mwenyezi Mungu. Ndege huruka toka ncha ya sikio la mmoja wao hadi shingoni kwa muda wa miaka mia tano.
 • 16. Mimi ni Mwislamu • Malaika wa mauti anayezitoa roho za viumbe kwa Amri ya Mwenyezi Mungu. Huyu ana wasaidizi wake. • Israfil atakayelipuliza baragumu, kisha viumbe vyote vitakufa kabla ya kutokea Kiyama. Kisha litapulizwa jingine, na hapo watasimama viumbe wakiangalia. • Mikaili anayesimamia jukumu la mvua. • Ridhwaan ambaye ni mlinzi wa Pepo. Yeye ana wasaidizi wake walio mbioni kuwahudumia Waumini Peponi. • Maalik ambaye ni mlinzi wa moto. Ana wasaidizi wake ambao viongozi wao ni kumi na tisa. Wana marungu ya chuma ya kuwaadhibu makafiri motoni - Mwenyezi Mungu Atuepushe na hayo. • Mkuu wa Malaika ni Jibril aliyewakilishwa kupeleka wahyi kwa Manabii na Mitume.
 • 17. Mimi ni Mwislamu • Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam alimwona katika umbile lake. Kutokana na ukubwa wake, alizifunika peo za mbingu. Ana mbawa mia sita, naye ndiye aliyekikamata kijiji cha Lut kwa ncha ya ubawa wake, akakinyanyua hadi juu mbinguni, kisha akakipindua juu chini. • Kuna malaika wengineo wengi zaidi ya hawa, na hakuna ajuaye askari wa Mola wako isipokuwa Yeye tu. :¯ ´ ³ ²± ° • Malaika huwapenda Waumini ambao Mwenyezi Mungu Huwapenda na huwaombea maghfira. • Malaika mbali na nguvu zao hizi hupigana pamoja na Waumini.
 • 18. Mimi ni Mwislamu (3) KUVIAMINI VITABU • Ninaviamini Vitabu vya Mwenyezi Mungu Alivyoviteremsha kwa Mitume Wake, na kwamba katika asili ya kuteremshwa Kwake, ni Maneno ya Mwenyezi Mungu Aliyowafunulia ili waifikishe sheria na dini Yake. Vitabu vikubwa zaidi ni: Quraan Tukufu iliyoteremshwa kwa Mtume wetu Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam. Injili iliyoteremshwa kwa Iysa Alayhi Ssalaam. Taurat iliyoteremshwa kwa Musa Alayhi Ssalaam. Zaburi iliyoteremshwa kwa Daud Alayhi Ssalaam. Sahifa zilizoteremshwa kwa Ibrahim Alayhi Ssalaam.
 • 19. Mimi ni Mwislamu • Kati ya hivi, kuna vilivyopotolewa na kubadilishwa kabla ya kushuka Qur- aan. • Na Qur-aan ndiyo iliyo juu ya Vitabu hivi, na ndiyo yenye kuongoza sheria zote na hukumu zake, na yenye kuondosha yale yote yenye kwenda kinyume na hukumu zake baada tu ya kuteremka kwake. • Na kwamba Mwenyezi Mungu Hatokubali siku ya Kiyama ila amali kupitia uongofu wa Qur-aan. Hatokubali amali kwa kufuata Vitabu vilivyotangulia baada ya kuteremka Qur-aan kwa Mtume Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam. • Na kwamba Qur-aan ni Maneno ya Mwenyezi Mungu ya miujiza. Maneno haya yana utukufu wake, na wala hayaingiliwi na batili kabla yake wala baada yake. Mwenye kuyasema, amesema kweli, na mwenye kuhukumia kwayo, amefanya uadilifu, na mwenye kuyafanyia kazi
 • 20. Mimi ni Mwislamu basi hakika ameongolewa katika njia iliyonyooka, mwenye kushikamana nayo amefuzu na kuokoka, na mwenye kuyakengeuka atakuwa ni katika wenye kuhiliki. • Ni kwamba watu wa Qur-aan, hao ndio watu wa Mwenyezi Mungu waliokurubishwa Kwake, na kwamba mbora zaidi wa watu ni yule aliyejifundisha Qur-aan na akawafundisha watu, kwani Qur-aan hii itakuja siku ya Kiyama ikimwombea shifaa kila aliyeisoma, akaihifadhi na akaifanyia kazi, na itawaombea watu wake Pepo. • Qur-aan huzitwaharisha nyoyo kutokana na shubha na matamanio yanayozichafua, huzikurubisha kwa Muumbaji Wake Subhaanahuu wa Ta'alaa, na huzihimiza kufanya kazi ili kufuzu na kupata neema za kudumu milele. • Kati ya adabu za kusoma Qur-aan ni: Kuwa twahara na wudhuu.
 • 21. Mimi ni Mwislamu Kuelekea Kibla. Kukaa kwa adabu na heshima. Kutoisoma kwa haraka. Kuwa na unyenyekevu. Kuonyesha huzuni kwa madhambi na kuvuka mipaka. Kulia kutokana na kumwogopa Mwenyezi Mungu na Utukufu wa Maneno Yake. Kusoma kwa sauti nzuri. Kusoma kwa sauti ya chini ili kutowabughudhi wenye kuswali. Kuzingatia maana ya maneno. Kuhudhurisha moyo. Kutaamuli kwa kina Aayah za Mwenyezi Mungu. Tuwe na yakini kuwa kusimamisha hukumu za Kitabu hiki kwa watu ni moja kati ya sababu za kumakinishwa katika ardhi na kuwashinda maadui.
 • 22. Mimi ni Mwislamu Basi harakia ndugu yangu Mwislamu kwenda kwa Mola wako, na kikamate Kitabu hiki kwa hima. Kuwa na shime asikutangulie yeyote kuelekea kwa Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu Hufurahi zaidi kwa kurejea kwako Kwake kuliko wanavyofurahi watu kwa kurejea mtu wao aliyekuwa mbali.
 • 23. Mimi ni Mwislamu (4) KUWAAMINI MITUME • Ninawaamini Mitume wa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu Aliwateua Mitume kati ya wanadamu, Akawafunulia Sheria Yake kwa njia ya wahyi, na Akawaamuru kuifikisha kwa watu, na kwamba mwenye kuwatii ataingia peponi, na mwenye kuwaasi ataingia motoni. • Kisha Akawatilia nguvu kwa miujiza yenye kuonyesha ukweli wao ili iwasaidie mbele ya wakadhibishaji, na ili iwe ni hoja kwao. • Na kwamba Mtume wa mwanzo ni Nuhu, na wa mwisho wao ni Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam.
 • 24. Mimi ni Mwislamu • Na kuwa Mitume hawa ni watu; wanakula, wanakunywa, wanaoa,wanaugua na wanakufa. Wao ndio viumbe bora kabisa wa Mwenyezi Mungu na wamehifadhiwa na maasi. • Mitume wa Mwenyezi Mungu ni wengi. Mwenyezi Mungu Amewataja baadhi yao katika Qur-aan. Nao ni Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam, Ibrahim Khalili wa Ar- Rahmaan, Musa aliyesemeshwa na Allaah, Iysa Neno la Mwenyezi Mungu na Nuhu. Hawa ndio Mitume wenye azma ya juu Rehma na Amani ziwe juu yao. Pia Ismail, Is-haaq, Yakub, Harun, Ayyub, Yunus, Sulayman, Daawud, Yahya, Zakariya, Hud, Saleh,
 • 25. Mimi ni Mwislamu Yusuf, Shuayb, Ilyaas, Lut, Dhulkifl, Idris, na wengi wengineo. Kati yao kuna Aliowahadithia Mwenyezi Mungu katika Qur-aan na wengineo Hakuwahadithia. • Jambo la kwanza walilolilingania Mitume ni tawhid, na jambo kubwa zaidi walilolikataza ni shirki, na wote wamekuja na Uislamu na wito. • wa tawhid. Lakini sheria zao na mifumo ya kumwabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu ilitofautiana kutokana na kutofautiana zama zao na nchi zao. • Na kwamba Mitume walitoa bishara ya kuja kwa Nabii Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam na
 • 26. Mimi ni Mwislamu wakawaamrisha kaumu zao kumwamini Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam atakapotumwa kwao. • Tofauti kati ya Rasuli (Mtume) na Nabii ni kuwa Rasuli ni yule aliyefunuliwa sheria mpya na akaamrishwa kuifikisha kwa watu. Ama Nabii, ni yule aliyetumwa ili kuithibitisha na kuipitisha sheria ya Rasuli aliyemtangulia. • Ninaamini kuwa mbora wa Mitume mbele ya Allaah ni Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam toka kwa mwana wa Ismaili bin Ibrahim Alayhima Ssalaam. Allaah Amemtuma kwa watu wote,
 • 27. Mimi ni Mwislamu Akahitimisha Unabii kwa Unabii wake, na Utume kwa Utume wake. • Akamtilia nguvu kwa miujiza, Akamfanya bora kuliko Mitume wote. Pia Ameufanya Utume wake kuwa bora kuliko Utume wote uliotangulia, na sheria yake kuwa bora kuliko sheria zinginezo zilizopita, na Kitabu chake Qur-aan kuwa bora kuliko Vitabu vyote, na umati wake – Waislamu – kuwa bora kuliko uma nyinginezo. • Na Mola wake Akampa mambo ambayo Hakumpa yeyote katika Manabii waliomtangulia. Kati ya mambo hayo ni:
 • 28. Mimi ni Mwislamu (1) Al Wasiylah: Nayo ndiyo daraja ya juu kabisa Peponi ambayo Mwenyezi Mungu Amemwandalia Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam. (2) Al Kawthar: Nao ni mto Peponi wenye kupita chini ya Arshi ya Ar Rahman. (3) Al Hawdh: Ni sehemu ambayo Waislamu peke yao ndio watakayokunywa siku ya Kiyama. Siku ambayo watu watapatwa na kiu kikali, na jasho litawafika hadi magotini, viunoni na mabegani – kila mmoja kwa mujibu wa amali yake – na Waislamu watakunywa hapo kwa vikombe atakavyowapa
 • 29. Mimi ni Mwislamu Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam kwa mikono yake mitukufu. Baada ya hapo hawatapatwa na kiu milele. (4) Shafaa: Ni makamu ya kuhimidiwa siku ya Kiyama. Hapo Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam ataomba shifaa kwa Mwenyezi Mungu ili Waislamu waliofanya maasi watolewe motoni, na hatobakia ndani ya moto yeyote anayeshuhudia kwamba hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Allaah. Aliyefanya maasi hatosalia milele motoni, bali atatoka baada ya kutakaswa na maasi yake.
 • 30. Mimi ni Mwislamu Aliyewaamini Manabii wote na wala hakumwamini Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam, basi hatatoka motoni. (5) Na kwamba Allaah Amemnusuru na Akawanusuru askari wake na wafuasi wake hadi siku ya Kiyama kwa kuzagaza hofu ndani ya nyoyo za maadui umbali wa mwendo wa mwezi. Na hakuna Nabii yeyote aliyepewa hili kabla yake Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam. (6) Na ardhi imefanywa kwake na Waislamu kuwa msikiti (sehemu ya kuswalia) na twahara, na
 • 31. Mimi ni Mwislamu haikufanywa hivyo kwa Manabii waliomtangulia. (7) Na Allaah Amemtuma kwa watu na majini wote, lakini Mitume wengine wametumwa maalumu kwa watu wao tu. (8) Na kuwa yeye ndiye wa mwanzo kaburi lake kufunguka, na ndiye mwombezi wa kwanza, na ndiye wa kwanza kupewa shifaa, na ndiye wa kwanza kugonga mlango wa Pepo. Atakapougonga, mlinzi wa Pepo Ridhwaan atamuuliza: "Nani wewe?" Atajibu: "Muhammad". Ridhwaan atamwambia: "Kwako nimeamrishwa nisimfungulie yeyote kabla yako".
 • 32. Mimi ni Mwislamu Na kati ya miujiza ya Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam ni: Kupasuka mwezi. Alilirejesha jicho la Qatada lilipopofuliwa siku ya Uhud, macho yake yakarudi yakawa mazima kabisa. Aliurejesha muundi wa Ibn Al Hakam kama ulivyokuwa ulipovunjwa siku ya Vita vya Badr. Aliutaka mti utamke shahada, nao ukatamka shahada mbili mara tatu mbele ya kafiri, naye akasilimu. Kigogo cha mti alichokuwa akihutubia juu yake kililia wakati alipokiacha na hakikunyamaza mpaka alipoiweka mikono yake juu yake.
 • 33. Mimi ni Mwislamu Alikifanya chakula kidogo kuwa kingi baina ya mikono yake miwili, na wakaweza kula na kushiba zaidi ya watu 80 chakula cha kujaa viganja viwili. Aliyafanya maji kidogo kuwa mengi siku ya Hudaybiyah wakati jeshi lilipobakiwa na bakuli moja tu ya maji. Hapo Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam aliingiza mikono yake ndani, maji yakaanza kububujika kati ya vidole vyake kama chemchemu, wakanywa maji Waislamu wote na wakatawadhia maji hayo. Walikuwa kiasi cha watu 1400. Alipelekwa usiku hadi Msikiti wa Al Aqsa, na kisha alipandishwa hadi
 • 34. Mimi ni Mwislamu mbingu za juu na kukomea Sidrat Al Muntahaa. Alielezea na kuhadithia habari za umma zilizotangulia na Manabii wao nailhali yeye hana kisomo; hajui kusoma wala kuandika. Pia alielezea matukio yatakayotokea siku za usoni kwa kufunguliwa Fursi na Rome, kusambaratishwa ufalme wa Kisra aliyechanachana barua ya Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam aliyomtumia, pamoja na miujiza mingineyo mingi. Muujiza mkubwa zaidi wa Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam ni Qur-aan Tukufu. Ni
 • 35. Mimi ni Mwislamu muujiza utakaosalia hadi siku ya Kiyama. Kisha Allaah Ameunyanyua utajo wake, Akaliandamisha jina la Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam na Jina Lake Subhaanahuu wa Taalaa, na Akaifanya shahada ya kuwa hapana mola isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kuwa ndio jambo la kwanza analoingia nalo mja katika Uislamu,na jambo la mwisho analotoka nalo duniani. Basi yeyote ambaye neno lake la mwisho litakuwa ni "Laailaaha illa Allaah", ataingia peponi. • Ni wajibu wetu kwa upande wa Mtume wetu Swalla Allaahu Alayhi
 • 36. Mimi ni Mwislamu wa Aalihii wa Sallam tusilitangulize neno la kiumbe yeyote juu ya neno lake, au rai ya yeyote hata kama ana sauti kwa watu. Na ikiwa watu watakutangulia kuhamia kwake, basi hama wewe kwenda katika sunnah yake katika kila jambo lako na wala usimfuate mwingine zaidi yake. Ni wajibu wetu tushikamane sote pembezoni mwa amri yake na tumtii, kwani mwenye kumtii Mtume, basi huwa amemtii Mwenyezi Mungu. : GFEDCBA • Na tusimwiite ila kwa kusema Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam. Tusiseme (Muhammad) basi.
 • 37. Mimi ni Mwislamu • Tujipambe kwa adabu zake, na tumwige katika hali zake zote; kulala kwake, kula kwake, kutembea kwake, kuswali kwake, kufunga kwake, kutoa kwake sadaka, na jihadi yake. • Na tumpende zaidi kuliko nafsi zetu, wana wetu, wazazi wetu na watu wote. • Na tumpende kila yule anayempenda Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam na kumfanya kiigizo chake, na tumchukie kila yule anayemchukia Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam na wala hawajibiki na sheria yake.
 • 38. Mimi ni Mwislamu • Hivyo basi, ni lazima kwa Mwislamu awapende Waumini, awanusuru, ajifananishe nao, ashughulikie mambo yao, asaidiane nao katika mambo ya kheri, na awafanye kuwa marafiki zake wa dhati. • Ni wajibu kwake awabughudhi makafiri na ukafiri wao, asiwatii, asiungane nao dhidi ya Waislamu, wala asisaidiane nao katika ubatilifu wao, na wala asishiriki katika sikukuu zao. Ni haramu kwake kuwadhulumu, na linalotakiwa ni kuwatendea haki. • Ni wajibu wetu tuwapende Mama wa Waumini; Wakeze Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam,
 • 39. Mimi ni Mwislamu na tuwapende Maswahaba Wake Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam, kwani wao ndio bora wa watu baada ya Manabii. • Pia ni wajibu wetu tuihuishe Sunnah yake Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam, tuidhihirishe sheria yake, na tubalighishe ulinganio wake kwa watu wote. Kisha tusubiri maudhi na kero zinazotupata katika kuyapigania hayo, kwani hayo hayaepukiki. • Kwa vile Mwenendo wa Mwenyezi Mungu uliopita kwa viumbe Vyake unahukumia kuwa hakuna Nabii au walii yeyote aliyelingania haki hii ila alifanyiwa uadui na kuudhiwa.
 • 40. Mimi ni Mwislamu • Zindukana ndugu yangu Mwislamu! Maudhi ya makafiri yasikufanye ukaiacha dini yako. Kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam aliudhiwa wakati Maswahaba walipokuwa wachache, nao pia waliudhiwa wakafanya subira. • Na wala usilegeze azma yako hata kama watakwambia kuwa unayoyazungumza ni upuuzi, una misimamo migumu, au umepitwa na wakati. Au wakisema: "ashachezewa akili huyo". Kwani wewe una kiigizo chema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, yeye ashaambiwa mshairi na hata mwendawazimu.
 • 41. Mimi ni Mwislamu • Wala usisononeke ukiambiwa mpotevu mwenye siasa kali. Hii ndio tabia ya makafiri kwa Waumini. : ((Na wanapowaona, husema hakika hawa bila shaka ni wapotevu)). • Ikiwa watu wako makundi mawili, je haikutoshi wewe kuwepo katika kundi aliloko Mtume wako Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam?! • Achana nao hao mpaka ifike siku ambayo dhalimu ataviuma vidole vyake aseme: "Laiti mimi ningeliifuata njia pamoja na Mtume".
 • 42. Mimi ni Mwislamu : ¯ • Wala usibabaike au kuchanganyikiwa kama watakwambia kuwa wewe ni gaidi au mwovu, kwani hayo ndio madai ya madhalimu dhidi ya Waumini duniani na akhera. Ni kuwa pale Malaika watakapowaongoza kwenda Jahannamu wakisunukia, wataangalia humo kisha waseme: : JIH GFEDCBA ((Na watasema: Mbona hatuwaoni watu tuliokuwa tukiwazingatia kuwa ni katika waovu?))
 • 43. Mimi ni Mwislamu • Na hapa, Waumini (ambao makafiri wamewaita kuwa ni waovu) watawaita toka kwenye magorofa ya juu kabisa ya Firdaws wakiwaambia: : ¯ LKJIHGF ٤٤ : ‫اف‬ ‫(( ا‬ ‫ر‬ ‫و‬ ‫و‬ ‫)) أن‬ ((Hakika sisi tumeyakuta Aliyotuahidi Mola wetu kuwa ni kweli))
 • 44. Mimi ni Mwislamu (5) KUAMINI SIKU YA MWISHO • Ninaiamini siku ya mwisho, nayo ni iku ambayo dunia (nyumba ya amali) itamalizika, na akhera (nyumba ya malipo) itasimama, wema wakalipwa Pepo, na waovu wakalipwa moto. • Katika siku ya Kiyama, mizani itawekwa, na kila mja atapewa kitabu chake. Atakayepokea kitabu chake kwa mkono wake wa kuume, basi Mtume Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam atakuwa pamoja naye Peponi. Ama yule atakayepokea kitabu chake kwa mkono wake wa kushoto, basi atakuwa pamoja na
 • 45. Mimi ni Mwislamu Firauni –laana ziwe juu yake– motoni. • Sirati itawekwa, atakayefanikiwa kuivuka basi atafikia Peponi. Ama ambaye kulabu zitamnyakua kutokana na amali zake mbovu, basi ataangukia motoni. • Siku ya Kiyama ina dalili, ina alama ndogo na ina alama kubwa. • Miongoni mwa alama ndogo ni kupotea uaminifu, kukithiri mauaji, madaraka kukamatwa kwa mabavu na mafasiki, na masuala muhimu kuzungumziwa na wasiojua kitu. • Na miongoni mwa alama kubwa ni kuibuka Al Mahdi, kusimama ukhalifa
 • 46. Mimi ni Mwislamu wongofu utakaokwenda juu ya misingi ya njia ya Utume kabla ya kutokea Kiyama, na kudhihiri masihi mwongo. • Pia kuteremka Iysa Alayhi Ssalaam ili awaongoze Waislamu, apigane na makafiri, avunje vunje misalaba, aue nguruwe, na azikatae dini zote nyingine ila Uislamu tu. • Basi haitobakia nyumba yoyote ya mjini au ya mashambani ila Mwenyezi Mungu Ataiingiza dini hii, kwa heshima ya mwenye nguvu, au kwa udhalili wa mnyonge. • Vile vile kutoka Yaajuju na Maajuju. Pia atatoka mnyama
 • 47. Mimi ni Mwislamu anayewasemesha watu, na jua litachomoza toka magharibi, Qur-aan itaondoshwa na mambo mengineyo. • Basi yeyote atakayefanya amali ya uzito wa atomu ikiwa ni ya kheri au ni ya shari, ataiona siku ya Kiyama ndani ya kitabu chake. • Basi harakieni kwenye mambo ya kheri kabla haujamalizka muda wa kusajiliwa kwa kufa mja katika muda ambao haujui yeyote ila Mwenyezi Mungu Pekee. • Wakamwosha jamaa zake, wakamvisha sanda, wakamswalia, wakamzika. Kisha akajiwa na Malaika wawili; Munkari na Nakiyr,
 • 48. Mimi ni Mwislamu wakamkalisha kitako na kumwuuliza: "Nani Mola wako? Nini dini yako? Nani Nabii wako?" • Ikiwa atajibu kuwa: "Allaah ni Mola wangu, na Uislamu ndiyo dini yangu, na Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam ndiye Nabii wangu na Mtume wangu" – na Allaah Akamwezesha hilo – basi itafunguliwa katika kaburi lake harufu ya rayhaan hadi peponi, akaona mashukio yake huko, na makasri yake na ufalme wake. Hapo atashangilia kwa furaha kubwa, na kaburi lake litapanuliwa upeo wa macho.
 • 49. Mimi ni Mwislamu • Na ikiwa ni katika makafiri, basi hatoweza kujibu chochote, kwani majibu wakati huo si kwa akili au werevu wa mtu. • Bali Mwenyezi Mungu Huwathibitisha na kuwaimarisha watu wa imani wakati huo kwa yale waliyoyatanguliza kati ya amali njema zilizosimamia juu ya tawhid, utekelezaji wa faradhi, kushiriki jihadi, kutenda mema, kuamrisha mema, kukataza mabaya, kutoa sadaka, kusoma Qur-aan, kufunga siku za joto kali, na kusimama kuswali muda mrefu usiku wa baridi kali.
 • 50. Mimi ni Mwislamu • Ama akiwa ni katika makafiri, basi kaburi lake humbana hadi mbavu zake zikaingiana katika mwili wake, na kaburi lake huwa ni shimo katika mashimo ya motoni kwa sababu ya amali zake mbaya. • Basi jitahidi ndugu yangu Mwislamu, kwani leo ni amali na hakuna hisabu, lakini kesho ni hisabu na hakuna amali. • Na siku hiyo, Waislamu watiifu wataingia Peponi peke yao, kwa vile Mwenyezi Mungu Hatoikubali dini yoyote siku ya Kiyama isipokuwa Uislamu.
 • 51. Mimi ni Mwislamu • Ndani ya Pepo kuna neema ambazo hakuna sikio lililowahi kuzisikia, wala jicho lililowahi kuziona, wala hata kuwaziwa katika akili ya mwanadamu. Neema zake zitasalia milele wala hazitomalizika, na waliomo humo hawatakufa milele. Neema kubwa zaidi ya zote humo, ni kuuangalia Uso wa Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu wote. • Na waasi, waovu na makafiri wataingia motoni. Ndani ya moto, kuna adhabu zisizoweza kuvumilika Alizoziandaa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya makafiri. Milima mirefu thabiti haiwezi kuzivumilia adhabu hizi, na
 • 52. Mimi ni Mwislamu hao wataadhibiwa humo bila kupumzishwa. • Na humo, wafuasi wa mataghuti wataomba adhabu iongezwe maradufu kwa wakubwa wao waliowapoteza. Na hapo Mwenyezi Mungu Ataamuru adhabu iongezwe maradufu kwa wote. • Basi thibiti ndugu yangu Mwislamu juu ya haki hii, wala usidanganyike kabisa kuona kuwa wavunjaji sheria ni wengi zaidi, kwani ikiwa wewe utawatii na ukawafuata wengi waliomo ardhini, basi watakupoteza njia ya Mwenyezi Mungu. Nawe pita pamoja na wenye kupita kuelekea kwa Mwenyezi Mungu.
 • 53. Mimi ni Mwislamu • Kwani kundi katika umma wa Muhammad Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihii wa Sallam litaendelea kuwa juu ya haki likiwa na nguvu, hawezi kuwadhuru yeyote aliyekwenda nao kinyume au aliyewasaliti mpaka siku ya Kiyama. • Basi ni mbinu zipi za kuzijua ngazi hizo za kupanda juu, na kuokoka na ngazi hizo za kuporomokea chini? Na ni mbinu zipi za kuwafikia waliotangulia wenye kukurubishwa, na kujiweka mbali na wapingaji wenye kuangamia? Bila shaka ni toba ya kweli ya kusahihisha na kurekebisha yaliyopita, na amali njema za kuweka sawa umri
 • 54. Mimi ni Mwislamu uliosalia, na kuweka nia ya kweli ya kunyooka na kutokengeuka. • Basi kuwa pamoja na watu kwa kiwiliwili chako, ukiuza, ukinunua, ukioa na ukiiamirisha ardhi kwa yale Aliyokuhalalishia Mwenyezi Mungu. • Wala moyo wako usifungamane na kitu chochote cha kidunia, bali nenda na moyo wako pale ambapo unatakikana uwe, huko chini ya Arshi ya Ar Rahmaan, na sujudu kwa moyo wako sijdah ambayo utaendelea kuisujudu hadi siku ya Kiyama.
 • 55. Mimi ni Mwislamu (6) KUAMINI QADHAA NA QADARI • Nako ni kuamini kwamba Mwenyezi Mungu Anayajua yote yaliyomo ulimwenguni, yote yanayofanyika na yatakayotokea hadi siku ya Kiyama. Hata chembe ndogo mno, Yeye Hakosi kuijua. Na kwamba Yeye Anavijua vitendo vya waja, riziki zao, muda wao wa kuishi, na nani kati yao atakuwa wa peponi, na nani kati yao atakuwa wa motoni kabla Hajawaumba. • Na kwamba Mwenyezi Mungu Ameyaandika makadirio haya katika Lawh Al Mahfuudh kabla hata Hajaziumba mbingu na ardhi kwa miaka elfu hamsini, na kwamba Lawh
 • 56. Mimi ni Mwislamu Al Mahfuudh hii hakuna malaika wa karibu au hata Nabii aliyetumwa awezaye kuichungulia. • Hata kijusi kinapokuwa ndani ya tumbo la uzazi la mama yake, Mwenyezi Mungu Huwaamrisha Malaika waandike kama ni cha kike au kiume, waandike na riziki yake, amali yake, muda wake wa kuishi na hatima yake (ima peponi au motoni). Pia waandike mazuri na mabaya atakayokabiliana nayo. • Kisha unapoingia usiku wa cheo (Laylatul Qadr), huteremka makadirio ya mwaka mzima toka Lawh al Mahfuudh kati ya ajali za watu, riziki zao, nani kati yao atahiji mwaka huo na mengineyo. Katika
 • 57. Mimi ni Mwislamu usiku huo, hukadiriwa mambo ya mwaka mzima. • Kisha huteremka makadirio ya kila siku kwa nyakati zake na watu wake, hapo Mwenyezi Mungu Huwanyanyua watu na wengine Huwashusha. • Na tuamini kuwa Mapendeleo ya Mwenyezi Mungu ndiyo yawayo, Alilolitaka huwa na Asilolitaka haliwi. Mwenyezi Mungu Hana wa kumshinda, na Yeye Ndiye Mwenye kuzipindua nyoyo. Humwongoa Amtakaye kwa fadhila Zake na rehma Zake, na Humpoteza Amtakaye kwa Uadilifu Wake na Hekima Yake, kwani Yeye Ndiye Ajuaye zaidi nani anastahiki uongofu na nani anastahiki upotevu.
 • 58. Mimi ni Mwislamu • Na Mwenyezi Mungu Haulizwi yale Ayafanyayo lakini watu huulizwa. • Na tuamini kuwa Mwenyezi Mungu Amekiumba kila kitu, na hakuna chembe yoyote ndogo ulimwenguni isipokuwa Mwenyezi Mungu Ameiumba na Akaumba kutikisika kwake na kutulia kwake. • `Na kwamba Yeye Amewaumba waja na vitendo vyao, na kwamba Yeye Amewaumbia waja uwezo na mapendeleo yao ili wajichagulie wenyewe vitendo vyao. • Na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu Amewaamuru viumbe Wake wamtii, na Akawaahidi kuwapa Pepo Yake wakifanya hivyo, na Amewakataza kumwasi Yeye, na
 • 59. Mimi ni Mwislamu Akawapa onyo la kuwaingiza ndani ya moto Wake wakifanya hivyo, na wala Hakuwakalifisha kazi isipokuwa ile ambayo wanaweza kuifanya. Na hapo wakagawanyika makundi mawili: Waumini na makafiri; kwa hiari yao wenyewe, kwa mapendeleo yao wenyewe na kwa uwezo wao wenyewe, na yote hayo Mwenyezi Mungu Amewaumbia. • Na kwamba thawabu na adhabu hutokana na kuifuata sheria, si kwa kutangulia Elimu ya Mwenyezi Mungu kwao. Basi yeyote atakayefanya amali yoyote ya kheri ya uzito wa atomu, atalipwa kwayo. Na yeyote atakayefanya amali yoyote ya shari ya uzito wa atomu, basi ataadhibiwa kwayo.
 • 60. Mimi ni Mwislamu • Na kwamba kinachozingatiwa ni mwisho wa matendo, na kwamba kila mja ni mwenye kuendeshwa katika lile aliloumbiwa kati ya kufurahika Peponi au kupata shakawa motoni. • Na kwa ajili hiyo, ni wajibu kwa mja aogope mwisho mbaya, na aendelee daima kumwomba Mwenyezi Mungu na amhitajie, Amhidi katika njia iliyonyooka, na adumu kumwomba Amsaidie katika kumtii, na ajilinde Kwake na maasia, kwa vile mja hana hila wala nguvu zozote za kuyafanya hayo ila kwa Uwezo wa Mwenyezi Mungu. • Na kwamba Waumini Huridhia Qadhaa ya Mwenyezi Mungu na Qadari Yake; ya kheri yake na ya
 • 61. Mimi ni Mwislamu shari yake, katika misukosuko na katika furaha, na wana yakini kuwa hawezi yeyote kuwanufaisha isipokuwa kwa Qadari ya Mwenyezi Mungu, na wala hawadhuru isipokuwa liwe lisha andikwa na Mwenyezi Mungu. • Na mja hatopata utamu wa imani mpaka pale atakapojua kwamba lililompata lisingekuwa la kumkosa, na lililomkosa lisingekuwa la kumpata. Na mwisho naomba nikisema: "Ninamhimidi Mwenyezi Mungu, na ninamwomba Aniingize Peponi mimi na Waislamu wengine, na Anilinde na moto mimi na Waislamu wengine". Aamiyn.
 • 63. Mimi ni Mwislamu ed c b a ` _ k j ih g f [٨٥:‫ان‬ ‫]ل‬ Ù anamuslim@windowslive.com Ø × ª Ø WWW.Iam-Muslim.com ٢٠١٠ J ١٤٣١ ‫و‬ ‫ق‬ ‫ا‬ ٢٠٠٩L٢٢٢٧٤ W ٠١٢٠١٥٢٩٠٨ :ª W
 • 64. Mimi ni Mwislamu ª a ٠١٢٥٨٣٤٥٧٤ ٠١٠٦٧١٤٧٦٨