1. MWANZO WANGU
MTUNZI NA MWANDISHI:Nehemiah Ngumba
nehemiahngumba@gmail.com/+255758089184
Moja ya dhana ambayo hapo mwanzoni ilijengeka kutokana na msingi wa baba wa taifa
mwalimiu Julius K. Nyerere nidhahiri kila mwanachi katika ule usemi wa "ELIMU NDIO
MKOMBOZI".
Mara nyingi tumekuwa tukiona nchi nyingi zikijikwamua katika dimbwi la utumwa hivyo
kuutafta ukombozi ili kuishi maisha ambayo yatakuwa sambamba na ukombozi wao.
Ni wakati wetu kama Taifa changa japo si neno halisi kwa nchi yetu kutokana na kujipatia uhuru
wetu mnamo 1961,december 9 kwa umri huu tulipaswa kuwa Taifa lililokomaa katika kila sekta.
Elimu yetu ambayo tuliachiwa kama ukombozi ili kujikwamua katika changamoto mbalimbali
ikiwemo mardhi, umasikin pamoja na ujinga bado imekuwa ikikumbwa na matitizo kadha wa
kadha na kutufanya tusifikie mnalengo yetu.
Taifa letu bado tutaliita changa ikiwa na maana bado tuko hatua za mwanzo za kuhahikisha
tunajipatia ukombozi ambao ndio urithi wa vizazi vyetu.
Elimu yetu bado imeshindwa kutoa kile tunakiita ukombozi ili wanufaika na elimu hiyo kuleta
mapinduzi yatokanayo na ukombozi huo. Tunaamini kwamba vijana waliopata elimu ndio nguzo
muhimu katika jamii kwani ndio watakao tumika kama draraja la kuleta mapinduzi na hitimae
kujitoa katika dimbwi la giza la utumwa.
Mwalimu Nyerere alihimiza elimu itolewayo iendanae na mahitaji ya jamii huska ili kikidhi
hitaji la jamii huska kuliko kutoa elimu kandamizi ambayo haiendani na hitaji la jamii huska.
2. Umasikin wa nchi yetu ilikuwa moja ya janga katika kuhahikisha kila mzawa wa nchi hii
anajipatia nguzo hii ya elimu ili kuleta ukombozi katika familia, jamii yake pamoja na nchi
kiujumla.
Mwalimu Nyerere kwa kuliona hili aliamua kutoa elimu bure kwa wale wote waliopata vigezo
vya kuendelea na masomo, chagamoto kubwa ilikuwa idadi ya vijana wanaopata nafasi ya
kusoma haikuwa sawa na hitaji la jamii huska hivyo jamii kubaki katika giza.
Mahitjai ya elimiu yalipoongezeka nidhahiri serikali ilishndwa kuhimili mzigo ndipo ada ikaanza
kutozwa kuanzia shule ya msingi mpaka elimu ya juu. Ikumbukwe jamii yetu ilikuwa katika
dimbwi la umasikin hivyo ndoto ya kupeleka watoto shule ilizidi kudidimia.
Elimu yetu bado haikuweza kukidhi matakwa ya jamii kutokana na kile wanauchumu wanakiita
"uwekezaji katika elimu kuwa mdogo ambalo ni zao la umasikini". Kitendo cha nchi yetu kukosa
hela ya kuwekaza katika elimu ili kupata zao kubwa amabalo n sawa na hitaji la jamii yetu
nidhari kuwa eilmu yetu haikuweza kuwafikia watoto wetu{watoto masikin}.
Elimu ilikuwa ipo katika mfumo wa vitendo ili kumuandaa kijana kila anapomaliza ngazi flani
ya elimu kujua kipi afanye ili kumuingizia kipato..
Mabadiliko katika utawala nayo hayakuiacha sekta ya elimu katika kile tunaita utunzaji wa
ELIMU NDIO MKOMBOZI badala yake wamekuja na kile wanachokiona ni sahihi kwa macho
yao huku wakiacha agano la Babba wa TAaifa.
Hatima ya maskini kuokoka katika janga la umaskini ni kupata ukombozi huru ambao
utamuwezesha kuvuka madaraja yote katika maisha. Ikumbukwe kila mtu amezaliwa na
kipaji/vipaji ambavyo vimefichwa na maradhi,ujinga na umaskini vitu hivi vimechangia katika
kudidimiza ndoto za wenye maisha magumu kujinasua katika giza hili la umaskini.
3. Pamoja na chi nyingi za Afrika kudai umaskini wao umesababishwa na ukoloni nidhahiri kuna
ukweli uliofichika kwani mbio za sakafuni huishia ukingoni ni miaka mingi bado bara la Afrika
wapo katika giza hili. Hujuma zilizofanywa na wakoloni kuhakikisha tunakuwa maskini kwa
sasa hazina nafasi kutokana na kile tunaiita “UKOMBOZI WA JAMII” baada ya kujipatia uhuru
wetu. Matatizo yamezidi kuwa lukuki huku idadi ya watu ikizidi kuongeza na elimu yetu ya
kujikomboa imetiwa doa na wenye mamlaka ya kufanya hivyo.
Jukumu la nchi zetu baada ya kujipatia uhuru ilikuwa nikuweka misingi imara ili kuhakikisha
vijana wanajipatia ujuzi wa namna ya kuendesha maisha yao kutokana na sehemu wanazotoka.
Mitaala inayotumika haiksadiki maisha halisi ya wanaafrika kwani utajikuta wakisimulia maisha
ya hao waliowatala katika elimu zao jambo ambalo nchi maskini halina tija kwao. Mwanzo
wangu ni falsafa moja ambayo imenifanya kuwaza na kujua lkwanini niko hapa na ni klwanini
bado jamii iko hivi. Majibu yangu ya juu ya mwanzo nikwanini wimbo wa nchi maskini
umekuwa ni ule ule miaka nenda rudi. Mimi kama mhanga wa janga hili la giza kwa kuzaliwa
katika janga haina maana niendelee kuwa katika dimbwi la giza. Matumaini yangu yalikuwa
kuvuka madaraja yanayopatikana katika nyaja zote japo hali haikuwa kama nilivyodhania hapo
awali.
Elimu kama nilivyoipa kipaumbele ndio chombo ambacho bado kimekuwa kikietesa jamii yetu
na kupelekea wenye ndoto na maono kupotea kwa kile kinachoitwa UKATA. Mbali na neon
ukata hata wanapata bahati ya kuingia katika mfumo wa elimu yetu nidhahiri wanamengi
yakukosoa japo hawana mda wa kutoa ujumbe kwa jamii yao.
Tazama madhara hasi ya elimu yetu ilivopelekwa katika dimbwi la umaskini kwa kufanya kiini
macho juu ya utoaji elimu ambayo ni sambamba na maisha ya wazawa na dadal yake kuelezea
4. maisha ya wageni ambao kwenye matumizi ya mali asili zetu kwao ni faida huku wenyeji
tukikosa hata ujuzi ni wa[pi pakuanzia kuhakikisha tunapata faida.
Wasemavyo ellimu ni gharama na ukiona ni ghari sana jaribu ujinga lakini baba wa Taifa
Mwalimu Nyerere aliongea kuhusu moja ya maadui wa maendeleo kuwa ni ujinga hakika
tumechukua sehemu ya adui na kumkumbatia kuwa rafiki yet undo matokeo bado tunahangaika
ya nini kifanyike kuokoa vizazi vyetu.
Kwanza kabisa tunaamini kuwa kama unamtaji unaweza kutengeneza mipango mikubwa juu ya
biashara yako lakini tisa kumi utafanikiwa endapo utakuwa na timu ya wataalamu ambao wako
tayari kushiriki kuhakiksha mipango yako inaenda sawia. Kwa nchi yetu nidhahiri hatujawekeza
kabisa kwania njema ya kupata matokeo chanya juu ya elimu hata jopo la wataalamu
wanaohuska wameshindwa kujumlisha mazingira ya wazawa ili kutoa elimu inayoendana na
mahtaji ya jamii na sayansi pamoja na teknolojia ili kupata maendeleo ya haraka.
ITAENDELEA……………………………………………………………………………..
ELIMU YANGU NCHI YANGU
Nehemiah Ngumba