SlideShare a Scribd company logo
1 of 11
Download to read offline
IKULU SI MAHALA PA KUKIMBILIA! NI MAHALA
PATAKATIFU; IKULU NI MZIGO; MSITEMEE MATE KABURI
LANGU- Mwal J.K NYERERE (AHERA)
Rai ya Mtanzania
Na: Prof Handley Mpoki Mafwenga
Ph.D (finance -COU), MSc (finance -Strathclyde), MBA (Mg.Eco -ESAMI/MsM),
LLM (taxation- UDSM), LLB (Tudarco), PGD tax mgt (IFM), AD tax mgt (IFM)]
Usiku nalala ghafla usingizi mzito unanipata; Mara namuona Muasisi wa Taifa
hili baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ananipa barua
niwaletee watanzania na kuniagiza wasilitemee mate kaburi langu kwa kivuli
cha Katiba na Madaraka ya Urais. Anaeleza jinsi ambavyo alinusurika kupata
kifo kwa kile alichoita Adha ya Uhaini ya Mwaka 1964 na 1982 kama
ifuatavyo.
Mnamo tarehe 20 Januari, 1964, nilikoswa kupinduliwa na Jeshi la Tanganyika
Rifles ambalo liliasi na Maasi hayo yalizimwa tarehe 25 Januari, 1964. Maasi
yalihusisha Vikosi vya Dar-es-salaam na Tabora Brigedi ya Kwanza na ya Pili.
Kipindi hiki ndicho kipindi cha Majeshi ya Ukombozi ya Msumbiji pia
yalipambana katika nchi yao.
Ilipofika Saa 7.50 alfajiri, ya tarehe 21 Januari, 1964, Mkuu wa Kikosi cha
Kwanza cha TR Brigedia Patrick Sholto Douglas, aliamshwa nyumbani kwake
na Sauti ya Baruji na Ving’ora, karibu na Kambi ya Jeshi la Colito ambayo sasa
inaitwa Lugalo Barracks. Alipotoka nje, aliona askari wake 12 wameshikiliwa
na wenzao wenye silaha na hatimaye kutiwa Mahabusu. Ndipo alipofahamu
kwamba, baadhi ya Askari wa Kikosi hicho walikuwa wameasi. Aliweza
kutoroka yeye na familia yake hadi katikati ya Jiji, akaiacha familia kwa Balozi
wa Australia nchini, kisha akakimbilia kwa Afisa mwenzake eneo ya Oysterbay
Dar-Es-Salaam.
Akiwa huko, akampigia simu Mheshimiwa Oscar Satiel Kambona, akimuomba
kupeleka ndege tatu Kikosi cha pili cha huko Tabora, kuleta askari waliokuwa
bado waaminifu kwa Serikali. Wakati huo, tayari Waasi walikuwa wamefunga
barabara iendayo Uwanja wa ndege huko Ukonga; hii ikawalazimu Marubani
warudi mbio inasemekana Brigedia Patrick Sholto Douglas akakimbilia kwenye
Ubalozi wa Uingereza, akajificha kwa siku tano hadi tarehe 25 Januari, 1964.
Brigedia Patrick Sholto Douglas alimpigia simu Mkuu wa Polisi, ambaye
alikwenda moja kwa moja nyumbani kwa Makamu wa Rais wakati huo Mzee
Rashid Mfaume Kawawa, na kumwamsha, kisha hao wawili wakaja kunipa
habari.
Nilihamaki na kukasirika sana; nikataka kwenda mimi mwenyewe kukutana na
Waasi hao ili wanieleze sababu za kitendo hicho cha aibu; lakini Honey wangu
Mama Maria kwa machozi na kwa kupiga magoti, alinisihi nisitoke kwenda
kukutana na watu wenye silaha. Nilimkaidi mpenzi wangu lakini Juhudi za
ziada zilifanywa baadaye nilikubali. Radhid Kawawa na Mama Maria Nyerere,
wakatorokea mahali nisikokujua. Wakati huo, tayari Waasi walikuwa kwenye
lango kuu la Ikulu wakinitafuta.
Kufikia saa 9.00 alfajiri siku hiyo hiyo, Waasi walikuwa wamekamata Kambi
ya Colito (Lugalo), kisha wakajigawa Vikundi vitatu na kuingia mjini. Kikundi
kimoja kilibakia kulinda Kambi hiyo, Kikundi cha Pili, kikiongozwa na Sajini
Francis Higo Ilogi, ndicho kilichokuja Ikulu kunitafuta, wakati Kikundi cha tatu
kililinda barabara kuu zote mjini.
Kikundi cha Sajini Ilogi kilipofika Ikulu, kiliruhusiwa na Mmoja wa Maafisa
Usalama wa Taifa, wamuone kwanza Waziri Mheshimiwa Oscar Kambona; nao
wakakubali kufanya hivyo. Wakaenda hadi kwa Kambona na kumleta Ikulu, na
kumweleza kwamba walikuwa wamewakamata na kuwaweka Mahabusu baadhi
ya Wanajeshi ambao wanasemekana walikuwa 16; na kwamba, kama
Mheshimiwa Oscar Kambona alikuwa tayari kusikiliza Malalamiko yao,
afuatane nao hadi Colito (Lugalo). Kamabona alikubali, aliondoka akiwa
amepanda gari la Mkuu wa Polisi na aliweza kukubali kuandamana na askari
wenye silaha, na wenye hasira kali kwenda Colito Barracks.
Walipofika Colito Barracks, walimtaka Oscar Kambona aaamue papo hapo,
pamoja na mambo mengine kuondolewa mara moja kwa Maafisa wa Kiingereza
Jeshini, na nafasi zao zishikwe na Wazalendo. Walitaka pia mishahara
iongezwe, kutoa Shilingi za Tanzania 105/= hadi kufikia Shilingi za Tanzania
260/= kwa mwezi. Hata hivyo, Mheshimiwa Oscar Kambona aliomba wateue
wawakilishi wachache ili wafuatane naye hadi Ikulu kwa Mashauriano nami
(Nyerere). Ndipo Kiongozi wa Waasi hao Sajini Francis Higo Ilogi, alipokataa
na kusema “Tunataka kila kitu leo hii” Yowe zikasikika “Apigwe risasi,
apigwe Kambona huyo”. Kwa kuogopa kuuawa, Kambona akauliza, “Mnataka
nani awaongoze?” Lilitajwa jina la Alex Nyirenda; lakini likakataliwa kwamba
alikuwa na majivuno. Akatajwa Luteni Elisha Kavana, akapitishwa kwa kauli
moja na kuvishwa kofia ya Brigedia Douglas.
Walipofika huko, askari hao walijipanga barabara iingiayo Ikulu, ingawa Sajini
Ilogi aliwakataza wasiingie ndani; Baada ya mashauriano kwa muda na
wasaidizi wa Rais pamoja na Mama mzazi wa Mwalimu Nyerere, Kambona
alitoka nje na kuwatangazia Waasi hao kuwa Rais ameyakubali madai yao;
Lakini askari hao wakapiga kelele “Muongo huyo Rais hayumo ndani; mpige
risasi, muongo huyo” Hata hivyo, waliondoka wameridhika, wakarejea
Kambini siku hiyo. Hima, Kambona aliwaondoa Maafisa wa Uingereza na
kuwasafirisha kwao kupitia Nairobi Kenya.
Akiwatangazia Wananchi kupitia Kituo cha Redio wakati huo “Tanganyika
Broadcasting Corporation (TBC), Mzee Oscar Kambona alisema;
“Huyu ni Waziri wenu wa Mambo ya Nje na Ulinzi; Serikali
ingalipo……kumekuwa na kutoelewana baina ya askari Waafrika na Maafisa
wa Uingereza katika Jeshi. Baada ya kuingilia kati Shauri hili, sasa askari
wamerudi kambini”
Kuna uwezekano mkubwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ulinzi
Mheshimiwa Oscar Kamabona ndiye aliyewashawishi Wanajeshi walioasi
Januari, 21, 1964 kurejea Kambini, kwa ahadi ya kushughulikia malalamiko
yao; siku ya pili baada ya kurejea Kambini, askari Waasi walionekana kufurahi
baada ya Maafisa wa Uingereza kuanza kuondoka, kama walivyoahidiwa na
Oscar Kambona. Ingawa, Sajini Francis Higo Ilogi hakuwa na furaha kama
wengine.
Nakumbuka, wakati wa Uasi Mwarabu mmoja alifanikiwa kuwaua Askari
wawili mtaani ambao walizikwa Dar-Es-Salaam. Wakati wa maziko ya askari
hao, ilipokelewa taarifa kwamba, Kikosi cha pili cha Jeshi kilichokuwa Tabora
nacho kilikuwa kimeasi, baada ya kupata habari kwamba wenzao wa Colito
{Lugalo} walikuwa wameasi.
Wakati Kikosi cha Tabora kikiendelea na Maasi, ilipokelewa hapo Tabora simu
ya maandishi (Telegraph) kutoka kwa Mhehimiwa Oscar Kambona kuwa
Kapteni Mirisho Sam Hagai Sarakikya, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Kikosi cha
Tabora. Wakati huo Sarakikya na Maafisa wengine walikuwa wamekamatwa na
kuwekwa Mahabusu na askari walioasi hapo Tabora.
Ndugu yangu Sarakikya akatolewa Mahabusu na akaomba simu hiyo isomwe
kwa sauti; kisha akatoa amri wasimame “Mguu Sawa”, wafunge beneti na kutoa
risasi. Nao wakamtii. Usiku huo, Sarakikya alifanya Mipango ya kuwasafirisha
maafisa wa Uingereza kutoka Tabora kwenda Dar-Es-Salaam na hatimaye
Makwao.
Tukio la Januari, 21 1964 na lile la Tabora pamoja ilienda sambamba na hali ya
Hatari huko Kenya, Uganda na Zanzibar, ambapo Serikali ya Uingereza ilibidi
ichukue tahadhari ya ziada kwa kupeleka askari wanaokisiwa kuwa 2,000 ndani
ya Ukanda wa Afrika ya Mashariki. Kwa hiyo, Manowari iliyoitwa Rhy, ikwa
imetia nanga hima Pwani ya Dar-es-salaam, na nyingine iitwayo Centaur,
iliyobeba ndege iliwasili na askari wapatao kama 600.
Nilifanya mazungumzo na Waasi; lakini ilipofika Ijumaa ya tarehe 25
Mazungumzo hayo hayakufikiwa vyema kwani Viongozi wa Vyama vya
Wafanyakazi, kupitia Chama Kikuu (Shirikisho) cha Wafanyakazi
(TFL),walikuwa wakikutana kwa siri na askari walioasi kwenye Kambi ya
Colito (Bienne P43); na Vyma hivyo vilikuwa vimeandaa Mgomo nchi nzima
kuungana na askari hao. Ilipofika saa 11.30 jioni siku hiyo, nilimuita Ikulu
Naibu Balozi wa Uingereza Bwana F. Stephen Mills; kumuomba Msaada wa
Kijeshi wa nchi yake na Mills bila kuchelewa, akapeleka taarifa London na
maombi kukubaliwa bila masharti yoyote.
Wakati huohuo, Mheshimiwa Oscar Satiel Kambona, akaenda mbio kwenye
Ubalozi wa Uingereza kumtafuta Brigedia Douglas ambaye alikuwa amejificha
humo kwa wiki nzima, kumuomba msaada wa kuratibu Mipango. Usiku wa
siku hiyo, Douglas na Ofisa mwingine, walinyatia hadi kwenye Manowari
Centaur iliyokuwa imefichwa.
Jumamosi ya Januari tarehe 26, 1964 saa 12.20 asubuhi, helikopta sita kutoka
Manowari Centaur zilichukua askari wanaokisiwa kuwa 60 akiwamo Brigedia
Douglas hadi eneo la Karibu na Kambi ya Colito. Dakika kumi baadaye saa
12.30 Manowari hiyo, na meli nyingine ya Vita Cambrian iliyokuwa ikisubiri
zilianza Mashambulizi kwa kupiga Mizinga kuwatisha Waasi. Wakati huo
mpango wa kuwalevya kwa ushindi wao bandia ulifanywa kwa kuchukuwa
pombe kwenye kiwanda cha Bia cha Ilala na Waasi hao wakanywa ipasavyo na
ndiyo msingi wa Colito kuitwa Lugalo ikiwa na maana ya pahali pa kulewea
pombe au tafrija ya pombe kwa lugha ya Kihehe au Kinyakyusa na baadhi ya
makabila yenye asili ya Kibantu. Kutoka umbari upatao kama mita 20 hivi, na
kwa ujasiri mkubwa, Douglas akatangaza kwa kipaza sauti, kwamba alikuwa
ameshika madaraka yake tena; akatoa amri askari wote watoke nje Kambini
“Mikono juu” na kukaa chini barabarani.
Baada ya dakika kumi bila kuona kitu, Brigedia Douglas akaanza kuhesabu
“Moja ; Mbili; …………Kumi”, askari wa Uingereza wakafyatua roketi hadi
Kambini. Waasi wakaanza kujisalimisha. Dakika kumi zingine zilizofuata
askari 150 walijisalimisha na wengine 150 baada ya saa moja. Kufikia saa 1.30
asubuhi, wote walikuwa wamesalimu amri; Maasi yakawa yamezimwa katika
zoezi ambalo askari walioasi, baadhi waliuawa na wengine walijeruhiwa.
Nakubaliana, na maoni ya Balozi Abbas Kleist Sykes akinukuliwa kuwa, “Maasi
ya Jeshi la Tanganyika Rifles (TR) Mwaka 1964 yalitokana na sehemu kubwa
kwa kuchelewa kuwaondoa Makamanda wa Kizungu na kuwapandisha vyeo
Waafrika”. Kama ilivyofanyika kwa Jeshi la Polisi na Watumishi wengine
Serikalini. Na ndivyo ilivyokuwa kwa Maasi ya Kenya na Uganda.
Kutokana na Maasi hayo, nilikifuta Kikosi chote cha Kwanza (Colito Barracks)
na kuwafukuza kazi askari 100 wa Kikosi cha Pili cha Tabora. Nilifukuza pia
asilimia 10 ya askari wa Polisi na Usalama 5,000 waliokuwapo, kwa kushindwa
kutekeleza Wajibu wao wa Kudhibiti Maasi. Watu zaidi ya 400 walikamatwa na
kuhojiwa, wakiwamo viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi; na wengine 500
walitiwa nguvuni chini ya Sheria ya “The Preventive and Detention Act” lakini
wengi waliachiwa.
Nalo lililokuwa Shirikisho la Wafanyakazi nchini (TFL), lilifutwa, badala yake
kikaundwa Chama cha National Union of Tanganyika Workers (NUTA) kama
Jumuiya ya Chama tawaa –TANU. Nilimteua Mirisho Sam Hagai Sarakikya
kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi na kumpandisha cheo kuwa Brigedia.
Mwanzoni mwa Aprili, 1964, Majeshi ya Uingereza yaliondoka na nafasi yake
kuchukuliwa na Kikosi cha Tatu cha Jeshi la Nigeria, chini ya Luteni Kanali
James Pam. Sajini Francis Higo Ilogi alipatikana na Hatia ya Uasi wa Jeshi na
kufungwa miaka 15, ambapo washirika wake 13 wakafungwa kifungo cha kati
ya miaka mitano hadi kumi.
Jeshi la Tanganyika Rifles (TR) liliundwa baada ya Tanganyika kupata Uhuru
tarehe 9 Desemba, 1961 likibadilishwa kutoka Jeshi la Kings African Rifles
(KAR) lililokuwa chini ya Waingereza. Pamoja na kubadilika Jina Tanganyika
Rifles ilikuwa na Muundo sawa na KAR. Jeshi hilo liliongozwa na Jenerali
Morisho Sarakikya kuanzia tarehe 8 Januari, 1964 hadi tarehe 12 Februari, 1974
lilipoongozwa na Jenerali Abdalah Twalipo hadi tarehe 8 Novemba, 1980.
Kipindi Jeshi linaasi, Sheria ya Kuwekwa Kizuizini ilikuwa tayari
imekwishaundwa yaani Tangayika Preventive and Detention Act, Cap 490 ya
Mwaka, 1962 kwa sasa ni Cap 361 [R.E 2002]. Hata hivyo, sikuipenda sana
Sheria hiyo ingawa niliweka saini. Kwa sababu niliamini niSheria
inayomuweka mtu hatiani bila Mashitaka hali anapaswa kuwa na Haki ya
kusikilizwa.
Ukweli ni kuwa nilipata kusema maneno yafuatayo “Take the question of
detention without trial. This is a desperately serious matter. It means that you
are imprisoning a man when he has not broken any written law, or when you
cannot be sure of proving beyong reasonable doubt that he has done. You are
restricting his liberty, and making him suffer materially and spiritually, for
what you belive he has done. Few things are more dangerous to the freedom of
a society than that. For freedom is indivisible, and with such an opportunity
open to the Government of the day, the freedom of every citizen is reduced; to
suspend Rule of Law under any circumtances is to leave open the possibility of
the grossest injustices being perpetrated. Yes knowing these things. I have still
supported the introduction of a law which gives the Government power to
detain people without trial. I have myself signed Detention Orders. I have done
these things as an inevitable part of my responsibilities as President of the
Republic…………………”
Pamoja na Sheria hiyo kuwepo, Mheshimiwa Kasanga Tumbo aliyekuwa
Kiongozi wa Chama cha People’s Democratic Party ndani ya Bunge ambaye pia
aliwahi kuwekwa Kizuizini kuanzia Januari, 1964 hadi Julai, 1966 aliipinga
vikali Sheria hiyo, iliyotangaza pamoja na mambo mengine “Hali ya Hatari kwa
Watu wa Tanganyika” Hata hivyo, niliamini kuwa Sheria hiyo iliwalenga
wahaini.
Ilipofika Mwezi Aprili, 1965 raia 14 wa Tanzania mbali ya Wajumbe wa awali
wa Baraza huko Zanzibar na Wanajeshi wapatao 20 wa Jeshi la Tanganyika
Rifles waliwekwa Kizuizini. Hata hivyo, ilipofika tarehe 25 Julai, 1966
ilitangazwa kuwa Watanzania waliokamatwa kwa ajili ya Uhaini walikuwa
wameachiwa huru; Hayo yalisemwa na Mheshimiwa Job Lusinde wakati huo
akiwa Waziri wangu wa Mambo ya Ndani ambaye alisisitiza kuwa kwa mujibu
wa Sera ya Jumla iliyofikiwa waliotuhumiwa wote wako huru na kuwa kamwe
haiashirii kuhatarisha Amani nchini.
Mnamo Mwezi Agosti, 1967, Ndugu Abdalah Khasim Hanga aliyekuwa
Makamu wa Rais wa Zanzibar, na Mlinzi wake Ndugu Eli Anangisye Mbunge
wa Tanzania Bara, ndugu zake Oscar Kambona na Maafisa watatu wa Wizara
ya Mambo ya Nchi za Nje waliohisiwa kuwa mahasimu wa karibu wa Kambona
waliwekwa ndani kwa kuhusishwa na kufanya njama za Mapinduzi; Hii
ilijumuisha pia kuwaweka ndani baadhi ya viongozi, marafiki na ndugu.
Baadaye, ikatangazwa kuwa viongozi wa tuhuma za Mapinduzi hayo
watafungwa kwa kosa la Uhaini.
Mbali ya Uhaini huo, pia Nusra nipoteze nafasi ya Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, mnamo Mwaka 1982. Jaribio hilo la Mapinduzi
lilifanywa na baadhi ya Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi wa Tanzania wakisaidiana
na Bwana mmoja aliyeitwa Thomas Pius Mtakubwa Rugangira huyu alijulikana
pia kwa majina ya “Father Tom” au “Unle Tom”.
Kipindi hicho idara yangu ya Usalama ilitumia sana usafiri wa Teksi na hata
bendi maarufu ya DDC Mlimani park msingi wake mkubwa ni chama cha
Tanzania Transport, Tax and Services (TTTS) kilikuwa na watu wenye weledi
huo. Hivyo, Watuhumiwa hao walifichuliwa njama zao na dereva teksi mmoja
waliyekuwa wakimtumia mara kwa mara ambapo njama zao zilikuwa kuniua na
kuniondoa Madarakani na Kuipindua Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania. Hivyo walikabiliwa pia na Shitaka mbadala la kuficha kosa la Uhaini
kwa kushindwa kutoa taarifa kwa Mamlaka iliyohusika huku wakielewa juu ya
Mpango wa Kuipindua Serikali.
Sikupenda sana iwepo kesi dhidi yao kwani nikiwa Mkatoliki niliyekuwa
kwenye Jumuiya Parokia ya Msasani na hata Kanisa la Mtakatifu Petro la
Oysterbay nilijifunza kusamehe mara saba sabini. Lakini Dola iliamua Kesi ya
Uhaini iungurume hapa nchini Tanzania chini ya Mheshimiwa Jaji Nassor
Mnzavas. Washitakiwa kwenye kesi hiyo walikuwa 19; miongoni mwao
alikuwepo Thomas Rugangira au “Uncle TOM”au “Father Uncle Chek Bob”,
wenzake walikuwa ni Khatibu Ghandhi au “Hatty MacGhee”, Kapteni
Mohammed Tamimu, Kapteni Ditrick Mbogoro, Kapteni Christopher Kadege,
Luteni Badru Rwechungura Kajaja na Kapteni Vitalis Mapunda. Wengine
walikuwa ni Banyikwa na Mkewe, Christopher Ngaiza, Zacharia Has Pope,
Kapteni Rodrick Rosham Robert na wengine ambao jumla yao walikuwa 19.
Kundi hilo lilikuwa na vijana watundu waliojiita Makomandoo sikumbuki
walijifunza wapi? Ambao ni Rugangira na Hatty MacGhee ambao wakati Kesi
inaendelea walipanga njama na kufanikiwa kutoroka katika Gereza la Keko,
Mjini Dar-Es-Salaam.
Vijana wale walitorokea nchini Kenya na baada ya kufika Kenya, Rugangira
akatorokea nchini Uingereza. Wakati huo viwanja vyetu vya ndege havikuwa na
ulinzi sana na hata mipakani hapakuwa na ulinzi mkali kubaini utorokaji wao.
Kwa bahati nzuri, Yule kijana Hatty MacGhee tukafanikiwa kumkamata na
kumrudisha hapa Tanzania; kukawa na Makubaliano na Kenya ya
kubadilishana wahalifu na ndipo tukabadilishana na mtu mmoja aliyekuwa
akitakiwa Kenya aliyetajwa kwa jina la Private Hezekiah Ochuka ambaye
ilidaiwa kuwa alifanya madudu huko Kenya.
Kijana Hatty MacGhee aliporejeshwa nchini aliunganishwa na wenzake na kesi
ikapamba moto. Nakumbuka, Katika Jaribio hilo, Komandoo Tamimu aliuawa
wakati wa purukushani za kumkamata pale Kinondoni Mkwajuni Dar-Es-
Salaam wakati wakimkimbiza Komandoo Tamimu alidandia gari moja Pick Up
iliyokuwa imebeba masanduku ya bia na kuanza kuwarushia wanaUsalama
waliokuwa wakimkimbiza, hivyo akapigwa risasi na kufa.
Ingawa nakumbuka, Mahakamani wakati wa kutoa ushahidi juu ya Komandoo
huyo mwanaUsalama mmoja aliyekuwa akiitwa MrX alisema walijaribu
kumkamata lakini akawatoroka kwa kuruka ukuta wa nyumba aliyokuwa
akiishi.
Kesi hiyo ya Uhaini ilikuwa imesimamiwa na Wakili machachari wa Utetezi
aliyejulikana kwa jina la Murtaza Lakha mwenye asili ya Asia. Mawakili
wengine wa Utetezi alikuwepo Mucadam, Jadeja na Tarimo. Upande wa
Serikali ulikuwa unaongozwa na Wakili William Sekule, pia alikuwepo Johnson
Mwanyika.
Watuhumiwa wengine sita wa Uhaini waliachiwa huru siku mbili baadaye
kutoka kwenye Gereza la Ukonga Dar-Es-Salaam. Wakati wakiachiwa huru,
Maganga alikuwa amehamishwa kwenye Magereza mengi ndani ya Dar-Es-
Salaam na Gereza lake la mwisho lilikuwa Butimba Mwanza. Pamoja na tabu
walizozipata Gerezani Eugen Maganga anadaiwa kusema;
“Hatujutii kujaribu kuangusha Serikali bali tunajutia tu kwa kushindwa kwa
Mipango ya kupindua.”
Kabla hawajafikia kuwa na wazo la kuangusha Serikali, Maganga aliyekuwa na
miaka 26 na Kadego walifika Jeshini na Tank Battalion. Maganga alikuwa
Luteni wakati Kadego alikuwa Kapteni.
Maganga alikuwa ndiyo anarudi kutoka Mjini London Uingereza ambapo
alikuwa akipata mafunzo ya kujinoa Kijeshi ya kupigana vita ya Uganda
Mwaka 1978. Akiwa mmoja wapo ya askari wa mstari wa mbele, Maganga
anaamini Tanzania ilishinda vita dhidi ya Uganda kwa vile Uganda ilikuwa na
Jeshi dhaifu.
Moja ya sababu walizozibainisha ni pamoja na 1) kutokuwa na furaha jinsi
Watanzania walivyokuwa Maskini na kulazimishwa kwenye Vijiji vya Ujamaa ;
2) Vita dhidi ya Uganda na Tanzania havikuwa na umuhimu na hivyo kuishia
kutumia fedha vibaya-vita havikuwa vya nchi hizi mbili bali vita vya Mwalimu
Julius Nyerere na Idd Amin na pia 3) Hali iliyokuwepo Jeshini ilikuwa siyo
nzuri ukilinganisha na hali iliyokuwepo wakati wa Meja Jenerali Mrisho
Sarakikya, Kiongozi wa Kwanza wa Jeshi la Ulinzi toka Mwaka 1964 hadi
1974 4) Waliopanga njama za kuangusha Serikali walihisi kuwa mimi
(Nyerere) sina imani na watu wa Kaskazini kwa sababu wamesoma nje ya nchi
na hivyo nawahofia kuwa wanaweza kuangusha Serikali 5) Watu waliokuwa
hawajasoma sana ndiyo waliopewa Madaraka na kuwa mambo hayakwenda
sawa; na 6) Wanajeshi hawakupewa vyeo na kuwa mimi nilipenda kujenga
Jeshi lenye watu ambao hawawezi kunipa Changamoto zozote.
Wahaini hao walidhani wangefanya mabadiliko bali inaonekana watu ambao
walijipanga nao hawakuwa tayari kujitoa Mhanga. Hata hivyo, hawakukata
tamaa, wakiwa baadhi yao wanapanga njama hizo wakakutana na Marehemu
Thoma Pius Rugangira ambaye alikuwa Mfanyabiashara wa Tanzania huko
nchini Kenya, na alikuwa akiishi pia Uganda na kwa vile baba yake Mzazi
alikuwa Uganda alikuwa akidhaniwa kuwa ni Afisa Usalama wa Serikali ya
Uganda.
Wahaini hao hawakuwashirikisha kabisa viongozi wa juu wa Jeshi waliweza
kujipanga wenyewe wakiwa vijana wadogo. Thomas Pius Rugangira ndiye
alikuwa mfadhiri wao na kamwe hawakupata fedha zozote nyingi toka nje ya
nchi. Wahaini hao walidhani wangeweza kuleta mfumo wa Demokrasia ya
Vyama Vingi ambako watu huwa huru kutoa mawazo yao na kuchagua Rais wa
nchi wanayemtaka. Waliahidiwa kuwa Thomas Pius Rugangira ndiye ambaye
angechukua nafasi ya Uwaziri Mkuu badala ya kuwa na mimi (Nyerere) kwa
masharti kuwa asingepaswa kugombea nafasi ya Urais kwa muda wa Miaka
iliyokuwa inafuata.
Siku tatu kabla ya Uhaini kufanyika Thoms Pius Rugangira aliwauliza ni nafasi
gani wangehitaji kama wakiunda Serikali mpya; lakini walijibu kuwa
wasingehitaji chochote.
Wakati Mipango yote imekuwa tayari, walisubiri nirudi toka nje ya nchi kwani
nilisafiri; Nilirudi Mnamo Mwezi Januari, 1982 baada ya kukaa nje kwa muda
wa miezi miwili na kwenda nyumbani kwetu Butiama. Lengo lao la kunisubiri
ilikuwa kuniuwa na mipango hiyo ilipendekezwa na Thomas Pius Rugangira.
Bila matarajio, nilikaa muda kidogo pale Butiama na sikurudi Dar-Es-Salaam
katika kipindi cha siku mbili ambazo Mapinduzi yalipangwa ambapo
yalipangwa rasmi siku ya Jumatatu tarehe 9 Januari, 1982. Siku ya Ijumaa
Mnamo tarehe 6 Januari, 1982 wakapanga kukutana kwa mara ya mwisho kabla
ya kutekeleza Uhaini wao; hata hivyo, baadhi ya wenzao hawakuonekana.
Mohammed Tamimu ni mmoja ya Wahaini ambao hawakuonekana siku hiyo.
Wajumbe wengine walihofu sana kitendo cha Mohammed Tamimu
kutoonekana. Wakaamua kumtuma mmoja wao Kinondoni Mkwajuni ambako
alikuwa anakaa, lakini wakashangaa kuona Polisi wamezingira nyumba yake na
wamemuuwa. Hapo wakagundua kuwa suala lao siyo siri tena. Mohammed
Tamimu alikuwa na kawaida ya kutunza rekodi za mikutano yao na majina ya
wahusika.
Ikawa Polisi na Wanausalama wameanza kuwasaka; Kadego na Maganga
wakaamua kutorokea Kenya kupitia Tanga na Mombasa ambapo walikaa
Nairobi miezi kumi kama Wakimbizi wa kisiasa. Hawakujilaumu sana kuvuja
kwa Suala lao kwani waliamini pengine Hatty MacGhee ametoa siri kwa vile
alikuwa raia na alikuwa hajui kutunza siri. Walihisi pia kuwa Mohammed
Tamimu alijua kuwa Hatty MacGhee hakuwa Askari Mstaafu wa Jeshi la
Marekani kama alivyojitapa na wakagundua baadaye kuwa jina lake halisi
alikuwa Khatibu Hassan Ghandhi na alikuwa rubani Mtanzania.
Kuna wakati siku chache baadaye, Maganga na Kadego wakiwa wanazurura
mitaa ya Nairobi ghafla wakawaona Wahaini wenzao Uncle Thom na Hatty
MacGhee waliokuwa wamewaacha Dar-Es-Salaam. Hawa watuhumiwa wawili
walikuwa wametoroka katika Gereza la Keko lililopo mjini Dar-Es-Salaam.
Ingawa walifurahia maisha pale Nairobi, Rugangira aliamua kusafiri kwenda
London Uingereza kujaribu kutafuta njia ya kuwahamishia Malawi. Alihofu
kuwa Serikali ya Kenya ingeshirikiana na Serikali ya Tanzania kuwakamata.
Watuhumiwa wa Uhaini wote nane, walifanikiwa kutorokea Nairobi. Kabla ya
Pius Rugangira hajarudi kutoka London kundi lao likakamatwa Nairobi na
wakabadilishana na Koplo Ochuka na Sajini Pancras Oteyo ambao nao
walikuwa na Mpango kama huo wa kuagusha Serikali ya Rais Daniel Arap Moi
wa Kenya Mwaka huo huo wa 1982 na wakakimbilia Tanzania. Walifungwa
pingu mikononi na kufungwa vitambaa usoni na kupelekwa kwenye Gereza la
Isaka lenye ulinzi Mkali lililopo Mjini Dodoma ambako walikaa kuanzia Mwezi
Novenber, 1983 hadi Oktoba, 1084.
Watu waliokuwa wanawalinda hawakuwa wakali sana, kitu kilichowafanya
waweze kuandika barua Ubalozi wa Marekani wakitaka Dunia ielewe kuwa
walifungwa kwa sababu hakuna mtu alikuwa anajua chochote wakati huo. Hii
ilifanya Kamishana wa Wakimbizi wa Umoja wa Mataifa kutembelea Tanzania
na kulazimisha kupeleka Kesi Mahakamani.
Kesi ilianza kuunguruma rasmi Januari, 1985 na Mnamo tarehe 28 Desemba,
1985 Mheshimiwa Jaji Nassoro Mnzavas alitoa Hukumu ambapo washitakiwa
wengine aliwafunga kifungo cha maisha na wengine walifungwa miaka kadhaa
lakini Banyikwa na Ngaiza waliachiwa huru.
Kwenye Gereza la Butimba, ndipo alipokuwepo Eugene Maganga ambapo
Mnamo tarehe 22 Oktoba, 1995, Rais Ali Hassan Mwinyi alitoa Msamaha na
wenzaka kadhaa.
[HAKIKA IKULU SI PA KUKIMBILIA “MUNGU IBARIKI AFRIKA
IBARIKI TANZANIA”]

More Related Content

What's hot

Biografi Utsman bin Affan (bagian 01)
Biografi Utsman bin Affan (bagian 01)Biografi Utsman bin Affan (bagian 01)
Biografi Utsman bin Affan (bagian 01)Berbagi Semangat
 
Larian merentas desa kertas kerja
Larian merentas desa kertas kerjaLarian merentas desa kertas kerja
Larian merentas desa kertas kerjaEast Smile
 
Kepimpinan Salahuddin Al-Ayubi
Kepimpinan Salahuddin Al-AyubiKepimpinan Salahuddin Al-Ayubi
Kepimpinan Salahuddin Al-AyubiRashdan Mamat
 
7 disaster in malaysian history
7 disaster in malaysian history7 disaster in malaysian history
7 disaster in malaysian historyNur Atikah Amira
 
Peraturan peraturan kawalan hasil tembakau
Peraturan peraturan kawalan hasil tembakauPeraturan peraturan kawalan hasil tembakau
Peraturan peraturan kawalan hasil tembakauHukaida Hamzah
 
Taklimat krusus kod etika
Taklimat krusus kod etikaTaklimat krusus kod etika
Taklimat krusus kod etikaaimm reka
 
Kepimpinan Salahuddin al-Ayyubi
Kepimpinan Salahuddin al-AyyubiKepimpinan Salahuddin al-Ayyubi
Kepimpinan Salahuddin al-Ayyubisyahadatulzikr
 
Peperangan di zaman rasulullah SAW
Peperangan di zaman rasulullah SAWPeperangan di zaman rasulullah SAW
Peperangan di zaman rasulullah SAWNur Fauzi
 
Bab 5-kegemilangan-melaka-ting-1
Bab 5-kegemilangan-melaka-ting-1Bab 5-kegemilangan-melaka-ting-1
Bab 5-kegemilangan-melaka-ting-1slihara
 

What's hot (10)

Biografi Utsman bin Affan (bagian 01)
Biografi Utsman bin Affan (bagian 01)Biografi Utsman bin Affan (bagian 01)
Biografi Utsman bin Affan (bagian 01)
 
Larian merentas desa kertas kerja
Larian merentas desa kertas kerjaLarian merentas desa kertas kerja
Larian merentas desa kertas kerja
 
Kepimpinan Salahuddin Al-Ayubi
Kepimpinan Salahuddin Al-AyubiKepimpinan Salahuddin Al-Ayubi
Kepimpinan Salahuddin Al-Ayubi
 
7 disaster in malaysian history
7 disaster in malaysian history7 disaster in malaysian history
7 disaster in malaysian history
 
Peraturan peraturan kawalan hasil tembakau
Peraturan peraturan kawalan hasil tembakauPeraturan peraturan kawalan hasil tembakau
Peraturan peraturan kawalan hasil tembakau
 
Arahan mkn 20
Arahan mkn 20Arahan mkn 20
Arahan mkn 20
 
Taklimat krusus kod etika
Taklimat krusus kod etikaTaklimat krusus kod etika
Taklimat krusus kod etika
 
Kepimpinan Salahuddin al-Ayyubi
Kepimpinan Salahuddin al-AyyubiKepimpinan Salahuddin al-Ayyubi
Kepimpinan Salahuddin al-Ayyubi
 
Peperangan di zaman rasulullah SAW
Peperangan di zaman rasulullah SAWPeperangan di zaman rasulullah SAW
Peperangan di zaman rasulullah SAW
 
Bab 5-kegemilangan-melaka-ting-1
Bab 5-kegemilangan-melaka-ting-1Bab 5-kegemilangan-melaka-ting-1
Bab 5-kegemilangan-melaka-ting-1
 

Viewers also liked

TUDARCO-PROCUREMENT ISSUES IN OIL AND GAS CONTRACTS
TUDARCO-PROCUREMENT ISSUES IN OIL AND GAS CONTRACTSTUDARCO-PROCUREMENT ISSUES IN OIL AND GAS CONTRACTS
TUDARCO-PROCUREMENT ISSUES IN OIL AND GAS CONTRACTSProf Handley Mpoki Mafwenga
 
Infomedia-InnovationInMotion
Infomedia-InnovationInMotionInfomedia-InnovationInMotion
Infomedia-InnovationInMotionNeil Gunning
 
WARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETE
WARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETEWARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETE
WARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETEProf Handley Mpoki Mafwenga
 
Presentation of Learning
Presentation of LearningPresentation of Learning
Presentation of LearningNatalie Harley
 
MEC Intranet Farewell response
MEC Intranet Farewell responseMEC Intranet Farewell response
MEC Intranet Farewell responseRa Vel
 
Seguridad Industrial call center
Seguridad Industrial call centerSeguridad Industrial call center
Seguridad Industrial call centerAndreGisLara
 

Viewers also liked (12)

Asking Why
Asking WhyAsking Why
Asking Why
 
Mvp #2 data
Mvp #2 dataMvp #2 data
Mvp #2 data
 
TUDARCO-PROCUREMENT ISSUES IN OIL AND GAS CONTRACTS
TUDARCO-PROCUREMENT ISSUES IN OIL AND GAS CONTRACTSTUDARCO-PROCUREMENT ISSUES IN OIL AND GAS CONTRACTS
TUDARCO-PROCUREMENT ISSUES IN OIL AND GAS CONTRACTS
 
Infomedia-InnovationInMotion
Infomedia-InnovationInMotionInfomedia-InnovationInMotion
Infomedia-InnovationInMotion
 
WARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETE
WARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETEWARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETE
WARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETE
 
171202
171202171202
171202
 
Presentation of Learning
Presentation of LearningPresentation of Learning
Presentation of Learning
 
MEC Intranet Farewell response
MEC Intranet Farewell responseMEC Intranet Farewell response
MEC Intranet Farewell response
 
Aplicatii ale matematicii
Aplicatii ale matematiciiAplicatii ale matematicii
Aplicatii ale matematicii
 
MINERAL TAX CLINIC REVISED EDITION 3
MINERAL TAX CLINIC REVISED EDITION 3MINERAL TAX CLINIC REVISED EDITION 3
MINERAL TAX CLINIC REVISED EDITION 3
 
Seguridad Industrial call center
Seguridad Industrial call centerSeguridad Industrial call center
Seguridad Industrial call center
 
Xbox presentation
Xbox presentationXbox presentation
Xbox presentation
 

More from Prof Handley Mpoki Mafwenga

Do mining company able to demonstrate reserves .....
Do mining company able to demonstrate reserves .....Do mining company able to demonstrate reserves .....
Do mining company able to demonstrate reserves .....Prof Handley Mpoki Mafwenga
 
Tax justice and advocacy clinicA Focus on the Revenue Index for Effective Fis...
Tax justice and advocacy clinicA Focus on the Revenue Index for Effective Fis...Tax justice and advocacy clinicA Focus on the Revenue Index for Effective Fis...
Tax justice and advocacy clinicA Focus on the Revenue Index for Effective Fis...Prof Handley Mpoki Mafwenga
 
MASTERS THESIS (ESAMI-MAASTRICHT SCHOOL OF MANAGEMENT -MsM)
MASTERS THESIS (ESAMI-MAASTRICHT SCHOOL OF MANAGEMENT -MsM)MASTERS THESIS (ESAMI-MAASTRICHT SCHOOL OF MANAGEMENT -MsM)
MASTERS THESIS (ESAMI-MAASTRICHT SCHOOL OF MANAGEMENT -MsM)Prof Handley Mpoki Mafwenga
 
The African Interview Questions Between Joyce Mmassy and Prof Handley Mpoki M...
The African Interview Questions Between Joyce Mmassy and Prof Handley Mpoki M...The African Interview Questions Between Joyce Mmassy and Prof Handley Mpoki M...
The African Interview Questions Between Joyce Mmassy and Prof Handley Mpoki M...Prof Handley Mpoki Mafwenga
 
MHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUA
MHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUAMHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUA
MHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUAProf Handley Mpoki Mafwenga
 
TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA
TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZATEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA
TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZAProf Handley Mpoki Mafwenga
 
WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA KWA HAYATI MWAL ...
WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA   KWA HAYATI MWAL ...WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA   KWA HAYATI MWAL ...
WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA KWA HAYATI MWAL ...Prof Handley Mpoki Mafwenga
 
WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZ...
WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZ...WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZ...
WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZ...Prof Handley Mpoki Mafwenga
 
SDGs Tanzania poverty headcount declining as economic growth expands
SDGs Tanzania poverty headcount declining as economic growth expandsSDGs Tanzania poverty headcount declining as economic growth expands
SDGs Tanzania poverty headcount declining as economic growth expandsProf Handley Mpoki Mafwenga
 
LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inawez...
LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inawez...LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inawez...
LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inawez...Prof Handley Mpoki Mafwenga
 
THE OVERSIGHT ROLE OF TANZANIA MINERAL AUDIT AGENCY (TMAA)
THE OVERSIGHT ROLE OF TANZANIA MINERAL AUDIT AGENCY (TMAA)THE OVERSIGHT ROLE OF TANZANIA MINERAL AUDIT AGENCY (TMAA)
THE OVERSIGHT ROLE OF TANZANIA MINERAL AUDIT AGENCY (TMAA)Prof Handley Mpoki Mafwenga
 

More from Prof Handley Mpoki Mafwenga (20)

Do mining company able to demonstrate reserves .....
Do mining company able to demonstrate reserves .....Do mining company able to demonstrate reserves .....
Do mining company able to demonstrate reserves .....
 
East african journal of research
East african journal of researchEast african journal of research
East african journal of research
 
Tax justice and advocacy clinicA Focus on the Revenue Index for Effective Fis...
Tax justice and advocacy clinicA Focus on the Revenue Index for Effective Fis...Tax justice and advocacy clinicA Focus on the Revenue Index for Effective Fis...
Tax justice and advocacy clinicA Focus on the Revenue Index for Effective Fis...
 
MASTERS THESIS (ESAMI-MAASTRICHT SCHOOL OF MANAGEMENT -MsM)
MASTERS THESIS (ESAMI-MAASTRICHT SCHOOL OF MANAGEMENT -MsM)MASTERS THESIS (ESAMI-MAASTRICHT SCHOOL OF MANAGEMENT -MsM)
MASTERS THESIS (ESAMI-MAASTRICHT SCHOOL OF MANAGEMENT -MsM)
 
TAX JUSTICE AND ADVOCACY CLINIC 2
TAX JUSTICE AND ADVOCACY CLINIC  2TAX JUSTICE AND ADVOCACY CLINIC  2
TAX JUSTICE AND ADVOCACY CLINIC 2
 
The African Interview Questions Between Joyce Mmassy and Prof Handley Mpoki M...
The African Interview Questions Between Joyce Mmassy and Prof Handley Mpoki M...The African Interview Questions Between Joyce Mmassy and Prof Handley Mpoki M...
The African Interview Questions Between Joyce Mmassy and Prof Handley Mpoki M...
 
BARUA YA SIRI KWA DR MOHAMED SHEIN TOKA AHELA
BARUA YA SIRI KWA DR MOHAMED SHEIN TOKA AHELABARUA YA SIRI KWA DR MOHAMED SHEIN TOKA AHELA
BARUA YA SIRI KWA DR MOHAMED SHEIN TOKA AHELA
 
MHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUA
MHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUAMHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUA
MHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUA
 
TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA
TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZATEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA
TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA
 
WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA KWA HAYATI MWAL ...
WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA   KWA HAYATI MWAL ...WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA   KWA HAYATI MWAL ...
WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA KWA HAYATI MWAL ...
 
WARAKA WA UPUMBAVU NA ULOFA KATIKA DEMOKRASIA
WARAKA WA UPUMBAVU NA ULOFA KATIKA DEMOKRASIAWARAKA WA UPUMBAVU NA ULOFA KATIKA DEMOKRASIA
WARAKA WA UPUMBAVU NA ULOFA KATIKA DEMOKRASIA
 
WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZ...
WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZ...WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZ...
WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZ...
 
SDGs Tanzania poverty headcount declining as economic growth expands
SDGs Tanzania poverty headcount declining as economic growth expandsSDGs Tanzania poverty headcount declining as economic growth expands
SDGs Tanzania poverty headcount declining as economic growth expands
 
LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inawez...
LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inawez...LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inawez...
LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inawez...
 
UFA WA UTEKELEZAJI WA LOCAL CONTENT
UFA WA UTEKELEZAJI WA LOCAL CONTENTUFA WA UTEKELEZAJI WA LOCAL CONTENT
UFA WA UTEKELEZAJI WA LOCAL CONTENT
 
Analysis of the Budget(2)
Analysis of the Budget(2)Analysis of the Budget(2)
Analysis of the Budget(2)
 
EAST AFRICAN JOURNAL OF RESEARCH
EAST AFRICAN JOURNAL OF RESEARCHEAST AFRICAN JOURNAL OF RESEARCH
EAST AFRICAN JOURNAL OF RESEARCH
 
TEKU publication2
TEKU publication2TEKU publication2
TEKU publication2
 
THE OVERSIGHT ROLE OF TANZANIA MINERAL AUDIT AGENCY (TMAA)
THE OVERSIGHT ROLE OF TANZANIA MINERAL AUDIT AGENCY (TMAA)THE OVERSIGHT ROLE OF TANZANIA MINERAL AUDIT AGENCY (TMAA)
THE OVERSIGHT ROLE OF TANZANIA MINERAL AUDIT AGENCY (TMAA)
 
TAX JUSTICE AND ADVOCACY CLINIC 2
TAX JUSTICE AND ADVOCACY CLINIC  2TAX JUSTICE AND ADVOCACY CLINIC  2
TAX JUSTICE AND ADVOCACY CLINIC 2
 

IKULU SI MAHALA PA KUKIMBILIA HATA KIDOGO

  • 1. IKULU SI MAHALA PA KUKIMBILIA! NI MAHALA PATAKATIFU; IKULU NI MZIGO; MSITEMEE MATE KABURI LANGU- Mwal J.K NYERERE (AHERA) Rai ya Mtanzania Na: Prof Handley Mpoki Mafwenga Ph.D (finance -COU), MSc (finance -Strathclyde), MBA (Mg.Eco -ESAMI/MsM), LLM (taxation- UDSM), LLB (Tudarco), PGD tax mgt (IFM), AD tax mgt (IFM)] Usiku nalala ghafla usingizi mzito unanipata; Mara namuona Muasisi wa Taifa hili baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ananipa barua niwaletee watanzania na kuniagiza wasilitemee mate kaburi langu kwa kivuli cha Katiba na Madaraka ya Urais. Anaeleza jinsi ambavyo alinusurika kupata kifo kwa kile alichoita Adha ya Uhaini ya Mwaka 1964 na 1982 kama ifuatavyo. Mnamo tarehe 20 Januari, 1964, nilikoswa kupinduliwa na Jeshi la Tanganyika Rifles ambalo liliasi na Maasi hayo yalizimwa tarehe 25 Januari, 1964. Maasi yalihusisha Vikosi vya Dar-es-salaam na Tabora Brigedi ya Kwanza na ya Pili. Kipindi hiki ndicho kipindi cha Majeshi ya Ukombozi ya Msumbiji pia yalipambana katika nchi yao. Ilipofika Saa 7.50 alfajiri, ya tarehe 21 Januari, 1964, Mkuu wa Kikosi cha Kwanza cha TR Brigedia Patrick Sholto Douglas, aliamshwa nyumbani kwake na Sauti ya Baruji na Ving’ora, karibu na Kambi ya Jeshi la Colito ambayo sasa inaitwa Lugalo Barracks. Alipotoka nje, aliona askari wake 12 wameshikiliwa na wenzao wenye silaha na hatimaye kutiwa Mahabusu. Ndipo alipofahamu kwamba, baadhi ya Askari wa Kikosi hicho walikuwa wameasi. Aliweza kutoroka yeye na familia yake hadi katikati ya Jiji, akaiacha familia kwa Balozi wa Australia nchini, kisha akakimbilia kwa Afisa mwenzake eneo ya Oysterbay Dar-Es-Salaam.
  • 2. Akiwa huko, akampigia simu Mheshimiwa Oscar Satiel Kambona, akimuomba kupeleka ndege tatu Kikosi cha pili cha huko Tabora, kuleta askari waliokuwa bado waaminifu kwa Serikali. Wakati huo, tayari Waasi walikuwa wamefunga barabara iendayo Uwanja wa ndege huko Ukonga; hii ikawalazimu Marubani warudi mbio inasemekana Brigedia Patrick Sholto Douglas akakimbilia kwenye Ubalozi wa Uingereza, akajificha kwa siku tano hadi tarehe 25 Januari, 1964. Brigedia Patrick Sholto Douglas alimpigia simu Mkuu wa Polisi, ambaye alikwenda moja kwa moja nyumbani kwa Makamu wa Rais wakati huo Mzee Rashid Mfaume Kawawa, na kumwamsha, kisha hao wawili wakaja kunipa habari. Nilihamaki na kukasirika sana; nikataka kwenda mimi mwenyewe kukutana na Waasi hao ili wanieleze sababu za kitendo hicho cha aibu; lakini Honey wangu Mama Maria kwa machozi na kwa kupiga magoti, alinisihi nisitoke kwenda kukutana na watu wenye silaha. Nilimkaidi mpenzi wangu lakini Juhudi za ziada zilifanywa baadaye nilikubali. Radhid Kawawa na Mama Maria Nyerere, wakatorokea mahali nisikokujua. Wakati huo, tayari Waasi walikuwa kwenye lango kuu la Ikulu wakinitafuta. Kufikia saa 9.00 alfajiri siku hiyo hiyo, Waasi walikuwa wamekamata Kambi ya Colito (Lugalo), kisha wakajigawa Vikundi vitatu na kuingia mjini. Kikundi kimoja kilibakia kulinda Kambi hiyo, Kikundi cha Pili, kikiongozwa na Sajini Francis Higo Ilogi, ndicho kilichokuja Ikulu kunitafuta, wakati Kikundi cha tatu kililinda barabara kuu zote mjini. Kikundi cha Sajini Ilogi kilipofika Ikulu, kiliruhusiwa na Mmoja wa Maafisa Usalama wa Taifa, wamuone kwanza Waziri Mheshimiwa Oscar Kambona; nao wakakubali kufanya hivyo. Wakaenda hadi kwa Kambona na kumleta Ikulu, na kumweleza kwamba walikuwa wamewakamata na kuwaweka Mahabusu baadhi ya Wanajeshi ambao wanasemekana walikuwa 16; na kwamba, kama Mheshimiwa Oscar Kambona alikuwa tayari kusikiliza Malalamiko yao, afuatane nao hadi Colito (Lugalo). Kamabona alikubali, aliondoka akiwa amepanda gari la Mkuu wa Polisi na aliweza kukubali kuandamana na askari wenye silaha, na wenye hasira kali kwenda Colito Barracks. Walipofika Colito Barracks, walimtaka Oscar Kambona aaamue papo hapo, pamoja na mambo mengine kuondolewa mara moja kwa Maafisa wa Kiingereza Jeshini, na nafasi zao zishikwe na Wazalendo. Walitaka pia mishahara iongezwe, kutoa Shilingi za Tanzania 105/= hadi kufikia Shilingi za Tanzania
  • 3. 260/= kwa mwezi. Hata hivyo, Mheshimiwa Oscar Kambona aliomba wateue wawakilishi wachache ili wafuatane naye hadi Ikulu kwa Mashauriano nami (Nyerere). Ndipo Kiongozi wa Waasi hao Sajini Francis Higo Ilogi, alipokataa na kusema “Tunataka kila kitu leo hii” Yowe zikasikika “Apigwe risasi, apigwe Kambona huyo”. Kwa kuogopa kuuawa, Kambona akauliza, “Mnataka nani awaongoze?” Lilitajwa jina la Alex Nyirenda; lakini likakataliwa kwamba alikuwa na majivuno. Akatajwa Luteni Elisha Kavana, akapitishwa kwa kauli moja na kuvishwa kofia ya Brigedia Douglas. Walipofika huko, askari hao walijipanga barabara iingiayo Ikulu, ingawa Sajini Ilogi aliwakataza wasiingie ndani; Baada ya mashauriano kwa muda na wasaidizi wa Rais pamoja na Mama mzazi wa Mwalimu Nyerere, Kambona alitoka nje na kuwatangazia Waasi hao kuwa Rais ameyakubali madai yao; Lakini askari hao wakapiga kelele “Muongo huyo Rais hayumo ndani; mpige risasi, muongo huyo” Hata hivyo, waliondoka wameridhika, wakarejea Kambini siku hiyo. Hima, Kambona aliwaondoa Maafisa wa Uingereza na kuwasafirisha kwao kupitia Nairobi Kenya. Akiwatangazia Wananchi kupitia Kituo cha Redio wakati huo “Tanganyika Broadcasting Corporation (TBC), Mzee Oscar Kambona alisema; “Huyu ni Waziri wenu wa Mambo ya Nje na Ulinzi; Serikali ingalipo……kumekuwa na kutoelewana baina ya askari Waafrika na Maafisa wa Uingereza katika Jeshi. Baada ya kuingilia kati Shauri hili, sasa askari wamerudi kambini” Kuna uwezekano mkubwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ulinzi Mheshimiwa Oscar Kamabona ndiye aliyewashawishi Wanajeshi walioasi Januari, 21, 1964 kurejea Kambini, kwa ahadi ya kushughulikia malalamiko yao; siku ya pili baada ya kurejea Kambini, askari Waasi walionekana kufurahi baada ya Maafisa wa Uingereza kuanza kuondoka, kama walivyoahidiwa na Oscar Kambona. Ingawa, Sajini Francis Higo Ilogi hakuwa na furaha kama wengine. Nakumbuka, wakati wa Uasi Mwarabu mmoja alifanikiwa kuwaua Askari wawili mtaani ambao walizikwa Dar-Es-Salaam. Wakati wa maziko ya askari hao, ilipokelewa taarifa kwamba, Kikosi cha pili cha Jeshi kilichokuwa Tabora nacho kilikuwa kimeasi, baada ya kupata habari kwamba wenzao wa Colito {Lugalo} walikuwa wameasi.
  • 4. Wakati Kikosi cha Tabora kikiendelea na Maasi, ilipokelewa hapo Tabora simu ya maandishi (Telegraph) kutoka kwa Mhehimiwa Oscar Kambona kuwa Kapteni Mirisho Sam Hagai Sarakikya, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Kikosi cha Tabora. Wakati huo Sarakikya na Maafisa wengine walikuwa wamekamatwa na kuwekwa Mahabusu na askari walioasi hapo Tabora. Ndugu yangu Sarakikya akatolewa Mahabusu na akaomba simu hiyo isomwe kwa sauti; kisha akatoa amri wasimame “Mguu Sawa”, wafunge beneti na kutoa risasi. Nao wakamtii. Usiku huo, Sarakikya alifanya Mipango ya kuwasafirisha maafisa wa Uingereza kutoka Tabora kwenda Dar-Es-Salaam na hatimaye Makwao. Tukio la Januari, 21 1964 na lile la Tabora pamoja ilienda sambamba na hali ya Hatari huko Kenya, Uganda na Zanzibar, ambapo Serikali ya Uingereza ilibidi ichukue tahadhari ya ziada kwa kupeleka askari wanaokisiwa kuwa 2,000 ndani ya Ukanda wa Afrika ya Mashariki. Kwa hiyo, Manowari iliyoitwa Rhy, ikwa imetia nanga hima Pwani ya Dar-es-salaam, na nyingine iitwayo Centaur, iliyobeba ndege iliwasili na askari wapatao kama 600. Nilifanya mazungumzo na Waasi; lakini ilipofika Ijumaa ya tarehe 25 Mazungumzo hayo hayakufikiwa vyema kwani Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi, kupitia Chama Kikuu (Shirikisho) cha Wafanyakazi (TFL),walikuwa wakikutana kwa siri na askari walioasi kwenye Kambi ya Colito (Bienne P43); na Vyma hivyo vilikuwa vimeandaa Mgomo nchi nzima kuungana na askari hao. Ilipofika saa 11.30 jioni siku hiyo, nilimuita Ikulu Naibu Balozi wa Uingereza Bwana F. Stephen Mills; kumuomba Msaada wa Kijeshi wa nchi yake na Mills bila kuchelewa, akapeleka taarifa London na maombi kukubaliwa bila masharti yoyote. Wakati huohuo, Mheshimiwa Oscar Satiel Kambona, akaenda mbio kwenye Ubalozi wa Uingereza kumtafuta Brigedia Douglas ambaye alikuwa amejificha humo kwa wiki nzima, kumuomba msaada wa kuratibu Mipango. Usiku wa siku hiyo, Douglas na Ofisa mwingine, walinyatia hadi kwenye Manowari Centaur iliyokuwa imefichwa. Jumamosi ya Januari tarehe 26, 1964 saa 12.20 asubuhi, helikopta sita kutoka Manowari Centaur zilichukua askari wanaokisiwa kuwa 60 akiwamo Brigedia Douglas hadi eneo la Karibu na Kambi ya Colito. Dakika kumi baadaye saa 12.30 Manowari hiyo, na meli nyingine ya Vita Cambrian iliyokuwa ikisubiri zilianza Mashambulizi kwa kupiga Mizinga kuwatisha Waasi. Wakati huo
  • 5. mpango wa kuwalevya kwa ushindi wao bandia ulifanywa kwa kuchukuwa pombe kwenye kiwanda cha Bia cha Ilala na Waasi hao wakanywa ipasavyo na ndiyo msingi wa Colito kuitwa Lugalo ikiwa na maana ya pahali pa kulewea pombe au tafrija ya pombe kwa lugha ya Kihehe au Kinyakyusa na baadhi ya makabila yenye asili ya Kibantu. Kutoka umbari upatao kama mita 20 hivi, na kwa ujasiri mkubwa, Douglas akatangaza kwa kipaza sauti, kwamba alikuwa ameshika madaraka yake tena; akatoa amri askari wote watoke nje Kambini “Mikono juu” na kukaa chini barabarani. Baada ya dakika kumi bila kuona kitu, Brigedia Douglas akaanza kuhesabu “Moja ; Mbili; …………Kumi”, askari wa Uingereza wakafyatua roketi hadi Kambini. Waasi wakaanza kujisalimisha. Dakika kumi zingine zilizofuata askari 150 walijisalimisha na wengine 150 baada ya saa moja. Kufikia saa 1.30 asubuhi, wote walikuwa wamesalimu amri; Maasi yakawa yamezimwa katika zoezi ambalo askari walioasi, baadhi waliuawa na wengine walijeruhiwa. Nakubaliana, na maoni ya Balozi Abbas Kleist Sykes akinukuliwa kuwa, “Maasi ya Jeshi la Tanganyika Rifles (TR) Mwaka 1964 yalitokana na sehemu kubwa kwa kuchelewa kuwaondoa Makamanda wa Kizungu na kuwapandisha vyeo Waafrika”. Kama ilivyofanyika kwa Jeshi la Polisi na Watumishi wengine Serikalini. Na ndivyo ilivyokuwa kwa Maasi ya Kenya na Uganda. Kutokana na Maasi hayo, nilikifuta Kikosi chote cha Kwanza (Colito Barracks) na kuwafukuza kazi askari 100 wa Kikosi cha Pili cha Tabora. Nilifukuza pia asilimia 10 ya askari wa Polisi na Usalama 5,000 waliokuwapo, kwa kushindwa kutekeleza Wajibu wao wa Kudhibiti Maasi. Watu zaidi ya 400 walikamatwa na kuhojiwa, wakiwamo viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi; na wengine 500 walitiwa nguvuni chini ya Sheria ya “The Preventive and Detention Act” lakini wengi waliachiwa. Nalo lililokuwa Shirikisho la Wafanyakazi nchini (TFL), lilifutwa, badala yake kikaundwa Chama cha National Union of Tanganyika Workers (NUTA) kama Jumuiya ya Chama tawaa –TANU. Nilimteua Mirisho Sam Hagai Sarakikya kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi na kumpandisha cheo kuwa Brigedia. Mwanzoni mwa Aprili, 1964, Majeshi ya Uingereza yaliondoka na nafasi yake kuchukuliwa na Kikosi cha Tatu cha Jeshi la Nigeria, chini ya Luteni Kanali James Pam. Sajini Francis Higo Ilogi alipatikana na Hatia ya Uasi wa Jeshi na kufungwa miaka 15, ambapo washirika wake 13 wakafungwa kifungo cha kati ya miaka mitano hadi kumi.
  • 6. Jeshi la Tanganyika Rifles (TR) liliundwa baada ya Tanganyika kupata Uhuru tarehe 9 Desemba, 1961 likibadilishwa kutoka Jeshi la Kings African Rifles (KAR) lililokuwa chini ya Waingereza. Pamoja na kubadilika Jina Tanganyika Rifles ilikuwa na Muundo sawa na KAR. Jeshi hilo liliongozwa na Jenerali Morisho Sarakikya kuanzia tarehe 8 Januari, 1964 hadi tarehe 12 Februari, 1974 lilipoongozwa na Jenerali Abdalah Twalipo hadi tarehe 8 Novemba, 1980. Kipindi Jeshi linaasi, Sheria ya Kuwekwa Kizuizini ilikuwa tayari imekwishaundwa yaani Tangayika Preventive and Detention Act, Cap 490 ya Mwaka, 1962 kwa sasa ni Cap 361 [R.E 2002]. Hata hivyo, sikuipenda sana Sheria hiyo ingawa niliweka saini. Kwa sababu niliamini niSheria inayomuweka mtu hatiani bila Mashitaka hali anapaswa kuwa na Haki ya kusikilizwa. Ukweli ni kuwa nilipata kusema maneno yafuatayo “Take the question of detention without trial. This is a desperately serious matter. It means that you are imprisoning a man when he has not broken any written law, or when you cannot be sure of proving beyong reasonable doubt that he has done. You are restricting his liberty, and making him suffer materially and spiritually, for what you belive he has done. Few things are more dangerous to the freedom of a society than that. For freedom is indivisible, and with such an opportunity open to the Government of the day, the freedom of every citizen is reduced; to suspend Rule of Law under any circumtances is to leave open the possibility of the grossest injustices being perpetrated. Yes knowing these things. I have still supported the introduction of a law which gives the Government power to detain people without trial. I have myself signed Detention Orders. I have done these things as an inevitable part of my responsibilities as President of the Republic…………………” Pamoja na Sheria hiyo kuwepo, Mheshimiwa Kasanga Tumbo aliyekuwa Kiongozi wa Chama cha People’s Democratic Party ndani ya Bunge ambaye pia aliwahi kuwekwa Kizuizini kuanzia Januari, 1964 hadi Julai, 1966 aliipinga vikali Sheria hiyo, iliyotangaza pamoja na mambo mengine “Hali ya Hatari kwa Watu wa Tanganyika” Hata hivyo, niliamini kuwa Sheria hiyo iliwalenga wahaini. Ilipofika Mwezi Aprili, 1965 raia 14 wa Tanzania mbali ya Wajumbe wa awali wa Baraza huko Zanzibar na Wanajeshi wapatao 20 wa Jeshi la Tanganyika Rifles waliwekwa Kizuizini. Hata hivyo, ilipofika tarehe 25 Julai, 1966
  • 7. ilitangazwa kuwa Watanzania waliokamatwa kwa ajili ya Uhaini walikuwa wameachiwa huru; Hayo yalisemwa na Mheshimiwa Job Lusinde wakati huo akiwa Waziri wangu wa Mambo ya Ndani ambaye alisisitiza kuwa kwa mujibu wa Sera ya Jumla iliyofikiwa waliotuhumiwa wote wako huru na kuwa kamwe haiashirii kuhatarisha Amani nchini. Mnamo Mwezi Agosti, 1967, Ndugu Abdalah Khasim Hanga aliyekuwa Makamu wa Rais wa Zanzibar, na Mlinzi wake Ndugu Eli Anangisye Mbunge wa Tanzania Bara, ndugu zake Oscar Kambona na Maafisa watatu wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje waliohisiwa kuwa mahasimu wa karibu wa Kambona waliwekwa ndani kwa kuhusishwa na kufanya njama za Mapinduzi; Hii ilijumuisha pia kuwaweka ndani baadhi ya viongozi, marafiki na ndugu. Baadaye, ikatangazwa kuwa viongozi wa tuhuma za Mapinduzi hayo watafungwa kwa kosa la Uhaini. Mbali ya Uhaini huo, pia Nusra nipoteze nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mnamo Mwaka 1982. Jaribio hilo la Mapinduzi lilifanywa na baadhi ya Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi wa Tanzania wakisaidiana na Bwana mmoja aliyeitwa Thomas Pius Mtakubwa Rugangira huyu alijulikana pia kwa majina ya “Father Tom” au “Unle Tom”. Kipindi hicho idara yangu ya Usalama ilitumia sana usafiri wa Teksi na hata bendi maarufu ya DDC Mlimani park msingi wake mkubwa ni chama cha Tanzania Transport, Tax and Services (TTTS) kilikuwa na watu wenye weledi huo. Hivyo, Watuhumiwa hao walifichuliwa njama zao na dereva teksi mmoja waliyekuwa wakimtumia mara kwa mara ambapo njama zao zilikuwa kuniua na kuniondoa Madarakani na Kuipindua Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo walikabiliwa pia na Shitaka mbadala la kuficha kosa la Uhaini kwa kushindwa kutoa taarifa kwa Mamlaka iliyohusika huku wakielewa juu ya Mpango wa Kuipindua Serikali. Sikupenda sana iwepo kesi dhidi yao kwani nikiwa Mkatoliki niliyekuwa kwenye Jumuiya Parokia ya Msasani na hata Kanisa la Mtakatifu Petro la Oysterbay nilijifunza kusamehe mara saba sabini. Lakini Dola iliamua Kesi ya Uhaini iungurume hapa nchini Tanzania chini ya Mheshimiwa Jaji Nassor Mnzavas. Washitakiwa kwenye kesi hiyo walikuwa 19; miongoni mwao alikuwepo Thomas Rugangira au “Uncle TOM”au “Father Uncle Chek Bob”, wenzake walikuwa ni Khatibu Ghandhi au “Hatty MacGhee”, Kapteni Mohammed Tamimu, Kapteni Ditrick Mbogoro, Kapteni Christopher Kadege,
  • 8. Luteni Badru Rwechungura Kajaja na Kapteni Vitalis Mapunda. Wengine walikuwa ni Banyikwa na Mkewe, Christopher Ngaiza, Zacharia Has Pope, Kapteni Rodrick Rosham Robert na wengine ambao jumla yao walikuwa 19. Kundi hilo lilikuwa na vijana watundu waliojiita Makomandoo sikumbuki walijifunza wapi? Ambao ni Rugangira na Hatty MacGhee ambao wakati Kesi inaendelea walipanga njama na kufanikiwa kutoroka katika Gereza la Keko, Mjini Dar-Es-Salaam. Vijana wale walitorokea nchini Kenya na baada ya kufika Kenya, Rugangira akatorokea nchini Uingereza. Wakati huo viwanja vyetu vya ndege havikuwa na ulinzi sana na hata mipakani hapakuwa na ulinzi mkali kubaini utorokaji wao. Kwa bahati nzuri, Yule kijana Hatty MacGhee tukafanikiwa kumkamata na kumrudisha hapa Tanzania; kukawa na Makubaliano na Kenya ya kubadilishana wahalifu na ndipo tukabadilishana na mtu mmoja aliyekuwa akitakiwa Kenya aliyetajwa kwa jina la Private Hezekiah Ochuka ambaye ilidaiwa kuwa alifanya madudu huko Kenya. Kijana Hatty MacGhee aliporejeshwa nchini aliunganishwa na wenzake na kesi ikapamba moto. Nakumbuka, Katika Jaribio hilo, Komandoo Tamimu aliuawa wakati wa purukushani za kumkamata pale Kinondoni Mkwajuni Dar-Es- Salaam wakati wakimkimbiza Komandoo Tamimu alidandia gari moja Pick Up iliyokuwa imebeba masanduku ya bia na kuanza kuwarushia wanaUsalama waliokuwa wakimkimbiza, hivyo akapigwa risasi na kufa. Ingawa nakumbuka, Mahakamani wakati wa kutoa ushahidi juu ya Komandoo huyo mwanaUsalama mmoja aliyekuwa akiitwa MrX alisema walijaribu kumkamata lakini akawatoroka kwa kuruka ukuta wa nyumba aliyokuwa akiishi. Kesi hiyo ya Uhaini ilikuwa imesimamiwa na Wakili machachari wa Utetezi aliyejulikana kwa jina la Murtaza Lakha mwenye asili ya Asia. Mawakili wengine wa Utetezi alikuwepo Mucadam, Jadeja na Tarimo. Upande wa Serikali ulikuwa unaongozwa na Wakili William Sekule, pia alikuwepo Johnson Mwanyika. Watuhumiwa wengine sita wa Uhaini waliachiwa huru siku mbili baadaye kutoka kwenye Gereza la Ukonga Dar-Es-Salaam. Wakati wakiachiwa huru, Maganga alikuwa amehamishwa kwenye Magereza mengi ndani ya Dar-Es-
  • 9. Salaam na Gereza lake la mwisho lilikuwa Butimba Mwanza. Pamoja na tabu walizozipata Gerezani Eugen Maganga anadaiwa kusema; “Hatujutii kujaribu kuangusha Serikali bali tunajutia tu kwa kushindwa kwa Mipango ya kupindua.” Kabla hawajafikia kuwa na wazo la kuangusha Serikali, Maganga aliyekuwa na miaka 26 na Kadego walifika Jeshini na Tank Battalion. Maganga alikuwa Luteni wakati Kadego alikuwa Kapteni. Maganga alikuwa ndiyo anarudi kutoka Mjini London Uingereza ambapo alikuwa akipata mafunzo ya kujinoa Kijeshi ya kupigana vita ya Uganda Mwaka 1978. Akiwa mmoja wapo ya askari wa mstari wa mbele, Maganga anaamini Tanzania ilishinda vita dhidi ya Uganda kwa vile Uganda ilikuwa na Jeshi dhaifu. Moja ya sababu walizozibainisha ni pamoja na 1) kutokuwa na furaha jinsi Watanzania walivyokuwa Maskini na kulazimishwa kwenye Vijiji vya Ujamaa ; 2) Vita dhidi ya Uganda na Tanzania havikuwa na umuhimu na hivyo kuishia kutumia fedha vibaya-vita havikuwa vya nchi hizi mbili bali vita vya Mwalimu Julius Nyerere na Idd Amin na pia 3) Hali iliyokuwepo Jeshini ilikuwa siyo nzuri ukilinganisha na hali iliyokuwepo wakati wa Meja Jenerali Mrisho Sarakikya, Kiongozi wa Kwanza wa Jeshi la Ulinzi toka Mwaka 1964 hadi 1974 4) Waliopanga njama za kuangusha Serikali walihisi kuwa mimi (Nyerere) sina imani na watu wa Kaskazini kwa sababu wamesoma nje ya nchi na hivyo nawahofia kuwa wanaweza kuangusha Serikali 5) Watu waliokuwa hawajasoma sana ndiyo waliopewa Madaraka na kuwa mambo hayakwenda sawa; na 6) Wanajeshi hawakupewa vyeo na kuwa mimi nilipenda kujenga Jeshi lenye watu ambao hawawezi kunipa Changamoto zozote. Wahaini hao walidhani wangefanya mabadiliko bali inaonekana watu ambao walijipanga nao hawakuwa tayari kujitoa Mhanga. Hata hivyo, hawakukata tamaa, wakiwa baadhi yao wanapanga njama hizo wakakutana na Marehemu Thoma Pius Rugangira ambaye alikuwa Mfanyabiashara wa Tanzania huko nchini Kenya, na alikuwa akiishi pia Uganda na kwa vile baba yake Mzazi alikuwa Uganda alikuwa akidhaniwa kuwa ni Afisa Usalama wa Serikali ya Uganda. Wahaini hao hawakuwashirikisha kabisa viongozi wa juu wa Jeshi waliweza kujipanga wenyewe wakiwa vijana wadogo. Thomas Pius Rugangira ndiye
  • 10. alikuwa mfadhiri wao na kamwe hawakupata fedha zozote nyingi toka nje ya nchi. Wahaini hao walidhani wangeweza kuleta mfumo wa Demokrasia ya Vyama Vingi ambako watu huwa huru kutoa mawazo yao na kuchagua Rais wa nchi wanayemtaka. Waliahidiwa kuwa Thomas Pius Rugangira ndiye ambaye angechukua nafasi ya Uwaziri Mkuu badala ya kuwa na mimi (Nyerere) kwa masharti kuwa asingepaswa kugombea nafasi ya Urais kwa muda wa Miaka iliyokuwa inafuata. Siku tatu kabla ya Uhaini kufanyika Thoms Pius Rugangira aliwauliza ni nafasi gani wangehitaji kama wakiunda Serikali mpya; lakini walijibu kuwa wasingehitaji chochote. Wakati Mipango yote imekuwa tayari, walisubiri nirudi toka nje ya nchi kwani nilisafiri; Nilirudi Mnamo Mwezi Januari, 1982 baada ya kukaa nje kwa muda wa miezi miwili na kwenda nyumbani kwetu Butiama. Lengo lao la kunisubiri ilikuwa kuniuwa na mipango hiyo ilipendekezwa na Thomas Pius Rugangira. Bila matarajio, nilikaa muda kidogo pale Butiama na sikurudi Dar-Es-Salaam katika kipindi cha siku mbili ambazo Mapinduzi yalipangwa ambapo yalipangwa rasmi siku ya Jumatatu tarehe 9 Januari, 1982. Siku ya Ijumaa Mnamo tarehe 6 Januari, 1982 wakapanga kukutana kwa mara ya mwisho kabla ya kutekeleza Uhaini wao; hata hivyo, baadhi ya wenzao hawakuonekana. Mohammed Tamimu ni mmoja ya Wahaini ambao hawakuonekana siku hiyo. Wajumbe wengine walihofu sana kitendo cha Mohammed Tamimu kutoonekana. Wakaamua kumtuma mmoja wao Kinondoni Mkwajuni ambako alikuwa anakaa, lakini wakashangaa kuona Polisi wamezingira nyumba yake na wamemuuwa. Hapo wakagundua kuwa suala lao siyo siri tena. Mohammed Tamimu alikuwa na kawaida ya kutunza rekodi za mikutano yao na majina ya wahusika. Ikawa Polisi na Wanausalama wameanza kuwasaka; Kadego na Maganga wakaamua kutorokea Kenya kupitia Tanga na Mombasa ambapo walikaa Nairobi miezi kumi kama Wakimbizi wa kisiasa. Hawakujilaumu sana kuvuja kwa Suala lao kwani waliamini pengine Hatty MacGhee ametoa siri kwa vile alikuwa raia na alikuwa hajui kutunza siri. Walihisi pia kuwa Mohammed Tamimu alijua kuwa Hatty MacGhee hakuwa Askari Mstaafu wa Jeshi la Marekani kama alivyojitapa na wakagundua baadaye kuwa jina lake halisi alikuwa Khatibu Hassan Ghandhi na alikuwa rubani Mtanzania.
  • 11. Kuna wakati siku chache baadaye, Maganga na Kadego wakiwa wanazurura mitaa ya Nairobi ghafla wakawaona Wahaini wenzao Uncle Thom na Hatty MacGhee waliokuwa wamewaacha Dar-Es-Salaam. Hawa watuhumiwa wawili walikuwa wametoroka katika Gereza la Keko lililopo mjini Dar-Es-Salaam. Ingawa walifurahia maisha pale Nairobi, Rugangira aliamua kusafiri kwenda London Uingereza kujaribu kutafuta njia ya kuwahamishia Malawi. Alihofu kuwa Serikali ya Kenya ingeshirikiana na Serikali ya Tanzania kuwakamata. Watuhumiwa wa Uhaini wote nane, walifanikiwa kutorokea Nairobi. Kabla ya Pius Rugangira hajarudi kutoka London kundi lao likakamatwa Nairobi na wakabadilishana na Koplo Ochuka na Sajini Pancras Oteyo ambao nao walikuwa na Mpango kama huo wa kuagusha Serikali ya Rais Daniel Arap Moi wa Kenya Mwaka huo huo wa 1982 na wakakimbilia Tanzania. Walifungwa pingu mikononi na kufungwa vitambaa usoni na kupelekwa kwenye Gereza la Isaka lenye ulinzi Mkali lililopo Mjini Dodoma ambako walikaa kuanzia Mwezi Novenber, 1983 hadi Oktoba, 1084. Watu waliokuwa wanawalinda hawakuwa wakali sana, kitu kilichowafanya waweze kuandika barua Ubalozi wa Marekani wakitaka Dunia ielewe kuwa walifungwa kwa sababu hakuna mtu alikuwa anajua chochote wakati huo. Hii ilifanya Kamishana wa Wakimbizi wa Umoja wa Mataifa kutembelea Tanzania na kulazimisha kupeleka Kesi Mahakamani. Kesi ilianza kuunguruma rasmi Januari, 1985 na Mnamo tarehe 28 Desemba, 1985 Mheshimiwa Jaji Nassoro Mnzavas alitoa Hukumu ambapo washitakiwa wengine aliwafunga kifungo cha maisha na wengine walifungwa miaka kadhaa lakini Banyikwa na Ngaiza waliachiwa huru. Kwenye Gereza la Butimba, ndipo alipokuwepo Eugene Maganga ambapo Mnamo tarehe 22 Oktoba, 1995, Rais Ali Hassan Mwinyi alitoa Msamaha na wenzaka kadhaa. [HAKIKA IKULU SI PA KUKIMBILIA “MUNGU IBARIKI AFRIKA IBARIKI TANZANIA”]