SlideShare a Scribd company logo
1 of 5
Download to read offline
WARAKA WA UPUMBAVU NA ULOFA KATIKA DEMOKRASIA
Rai ya Mtanzania
Na Prof Handley Mpoki Mafwenga
Ph.D (finance -COU), MSc (finance -Strathclyde), MBA (Mg.Eco -ESAMI/MsM),
LLM (taxation- UDSM), LLB (Tudarco), PGD tax mgt (IFM), AD tax mgt (IFM)]
Nikiwa katikati ya mji ghafla namuona Edward Lowasa anapanda Daladala siamini macho
yangu Napata kizunguzungu ghafla naanguka mithiri ya mgonjwa wa kifafa napoteza
fahamu. Mara namuona Mwalimu Nyerere ameshika kisu kinadondosha damu, mkono wa
kulia kashika Katiba ya Tanzania imejaa damu, kisu chake kina maandishi madogomadogo
ya aina mbili “Wapumbavu,…….. Malofa”. Ananipa Katiba anaamrisha niipekue mara
nakutana na picha ya Fredrick Sumaye imezungukwa na maneno "Wapumbavu…Malofa”
picha imeambatana na Waraka ananipa niwape Watanzania na viongozi wetu Ben Mkapa,
Edward Lowasa na Fredrick Sumaye yenye ujumbe ufuatao;
Wanangu Watanzania yumkini hamjui maana hata ya majina ya viongozi wenu; kabla ya
kuwalaumu kwa matamshi yao yafaa mjue maana ya majina yao. Majina huumba tabia,
ukimwita mwanao “Chuki”atakuwa na “Chuki”; “Chausiku atakuwa mtu wa kutoka
usiku’”Shida”atakuwa mwenye shida daima n.k
Mini Baba yenu wa Taifa nilichagua Rais kwa maana ya jina liendalo na matakwa ya
mazingira ya wakati huo; leo mna jina la Edward maana yake hutokana na asili ya Kiingereza
likitoholewa kutokana na jamii ya Wajerumani wa asili ya Angeln na Saxony ambao
walihamia Uingereza baada ya kuanguka kwa Dola la Roma Miaka 410 Baada ya Kristo hao
huitwa Anglo-saxion. Ni jina lijulikanalo kwa asili kama Ēadweard, likiundwa na maneno
mawili “Ead” likiwa na maana ya Mali, Utajiri, Bahati, Matumaini na neno “Weard” likiwa
na maana ya Mlinzi au Mdhibiti. Kwa mujibu wa jina lake siyo ajabu kumsikia anachukia
sana Umaskini na anapenda sana Watanzania wote wawe matajiri kama Mengi na Bhahresa.
ila Kauli hiyo si ya kweli kwani hata nchi zilizoendelea zina Maskini na Tajiri. Lakini kwa
vile anatamani muombeeni kauli zake ziumbe ndoto zake ziwe kweli.
Jina Edward linavumisha sifa ya mtu mwenye nguvu na anayenuwia jambo. Huwa anapenda
kuwa kiongozi pale bahati inapomwangukia ingawa wakati mwingine angependa kuwa
kimya awapo kiongozi na kuwa Mfano wa wengine pale anapoamini hafikiwi na watu. Ni
mtu mwenye nidhamu kwa kiwango kikubwa ambapo hawezi kukubali kuwa mtu wa
kawaida na kufanya mambo ya bandia. Nguvu zake ni dhana ya kujiamini na kupania
mambo, huwa na mvuto wa asili ya Mamlaka na kipaji cha kupangiliza mambo na kuwa na
Uandilifu, Uwezo, Uimara na dhana kuu ya Haki. Kwa upande mwingine mapungufu yake ni
mtu wa kujiona kwa kulingia Ujuzi wake na kuwa mtu mwenye msimamo kitu
kinachomfanya awe mzito kubadilika kutokana na mazingira, hasira alizonazo na kushindwa
kuwa mvumilivu. Huwa ni mtu mwenye tabia ya usumbufu na kufuatilia mambo ya watu.
Lakini kumbuka ni pale tu anapoamini yeye ni sahihi muda wote. Ni mtu wa kupania mambo
ambaye ana kila nafasi ya kuishi kwa umoja na raha. Anapokuwa katika umri mdogo huwa
makini, muwajibikaji, na mwenye kuathiriwa zaidi na mazingira ya familia yake. Jina la
Edward hutoa sifa ya kupenda kuwa Mfano kwa jamii na mtu anayeogopa sana kueleweka
vibaya ndani ya jamii
Mnaye kijana wangu Benjamin Mkapa, Mwanahabari aliyebobea masuala ya Diplomasia
enzi zangu alinisaidia sana. Jina Benjamin maana yake “Kijana wa Mkono wa Kuume” ni
jina lililotumika pia na mtoto wa Mwisho kati ya Watoto 12 wa Yakobo. Jina hili lina maana
pia ya “Kijana wa Kusini” na pengine huwa na maana ya “Kijana wa Uzao wa Uzeeni” ni
Jina lenye asili ya Kiebrania na maana yake ni “Kijana wa Mkono wa Kiume” au “Bahati”.
Ni jina linalotamkwa Ben-Ja-Men. Kama nilivyobainisha, ni mtoto wa Yakobo na Raheli na
mjukuu wa Isaka. Rahel alikufa alipokuwa akimzaa na kumwita jina la “Benon” yaani
“Mtoto wa Uchungu Wangu” Baadaye jina hili likabadilishwa na Yakobo kuwa Benjamin.
Watu wenye Jina la Benjamin ni watu wenye hisia kubwa ya kuwa na Msimamo, wanapenda
familia zao na Jamii kwa ujumla na wanahitaji sana kufanya kazi na watu wengine na zaidi
hupenda kushukuriwa. Watu wa Jina hili wanapenda sana Mabadiliko, kufanya Maajabu na
kuwa Mwanaharakati. Ni wepesi kubadilika kutokana na Mazingira, Wana Mtazamo mpana
na Busara, wanauwezo wa kuweka mazingira mazuri ya kutumia uhuru uliopo. Wanapenda
kupambana na Sheria na Kanuni zinazowazuia kufanya kazi. Ni wepesi pia kubadilishwa
wanachokiamini kwani ni wasikivu, kutopumzika na kuwa wana Mapinduzi halisi.
Kuna kijana huko kwenu tumemsikia akiwa ana enzi dhana yangu ya “Kazi ni Kipimo cha
Utu” nasikia mnamwita Jembe; hii inanikumbusha enzi zangu za Chama kimoja ambapo
wagombea Ubunge niliwagawia uhuru wa kuchagua Jembe au Nyumba. Nilipata Wabunge
wengi wenye alama ya Jembe kuliko Nyumba. Na Jembe ilikuwa ishara ya uwakilishi wa
Wakulima wakati nyumba ilikuwa kwa Wafanyakazi. Sijaelewa tafsiri yenu lakini pengine
inaendana na jina lake. Jina la John maana yake ni “Rehema ya Mungu” lina asili ya
Kiebrania maana yake “Yehova ni Mwenye Rehema, ameonyesha Upendeleo”. Katika Biblia
jina hili lilitumiwa na Yohana Mbatizaji aliyembatiza Yesu Kristo katika Mto Jordan.
Watu wenye jina hili wanapenda sana kuwa na Msimamo, wanapenda familia zao na jamii
kwa ujumla na wanapenda kufanya kazi na watu wengine na kushukuriwa. Watu wenye jina
hili wanahurka ya kuwa wakimya, wenye kushirikiana na wenzao, wenye kujali wenzao,
wenye upendo kama wanavyojipenda wenyewe, wepesi kuishi nao, hawayumbi kwenye
maamuzi na wakati mwingine hupenda kuonea watu soni. Ni watu wenye Uaminifu wa hali
ya juu, wanaheshimu hali ya kujiamini ya watu wengine, na wana diplomasia ya hali ya juu,
wapatanishi na wanapenda kushirikiana na watu. Mara kwa mara ni wabunifu, wanapenda
maelezo ya kina yenye ukweli na sheria na wakati wote wanaona mabadiliko yanapaswa
kuangaliwa kwa umakini. Wanapenda sana kuwa na dhana ya kujiona siyo salama hivyo siyo
watu wa kupumzika.
Lakini pia anatumia jina la Joseph ambalo ni jina la kilatini aina ya Kigiriki kilichoanzia kwa
Waebrania maana yake “Ätaongeza” Jina hili pia mbali ya Mume wa Mariah mama wa yesu
lilitumika na Mtoto wa kumi na moja wa Yakobo kipenzi wake ambaye kaka yake Rubeni
alimuuza Misri na kumwambia baba yake kuwa ameuwawa kwa kumuokoa kuuwawa na
ndugu zake na ndiye alikuwa mshauri wa mfalme wa faraoh aliyewokoa Uzao wa Yakobo
wakati wa Njaa.
Jina la Fredrick ni jina la asili ya Uingereza lenye asili zaidi ya Ujerumani likiwa na maana
“Mtawala wa Amani” likijumuisha maneno frid yaani Ämani”na ric yaani “Mtawala”. Jina
hili lilikuwa maarufu sana kwenye ukanda wa lugha ya Ujerumani likitumiwa zaidi na Dola
la Kiroho la Roma, Ujerumani, Austria, Scandinavia, na Prussia. Watu wenye jina hili
huchukuliwa kuwa ni watu wenye mtazamo chanya (extrovert), wenye akili nyingi, na wenye
ubunifu wa hali ya juu. Watu hawa huwa wajasiriamali wenye kupenda mafanikio na hutumia
akili zao katika kujenga dhana ya ukweli. Watu hawa huwa na mvuto wawapo katika kundi la
watu na wenye kujipenda sana. Huchukuliwa kuwa ni Watawala kwenye familia zao,
marafiki, na hupendwa kwa upekee sana.
Nimesikia kuwa mnalalamika Ben amewatukana, nadhani hamjujui Ben kama ninavyomjua
mimi; Ben mmesahau kuwa ni mzee wa Uwazi na Ukweli na ndiyo maana enzi zake zilikuwa
ni za Uwazi na Ukweli; lakini pia tatizo lenu Watanzania wangu mmezoweshwa kwa muda
wa miaka kumi mkiwa na Rais Jakaya ambaye ni mcheshi, mpole na anatabasamu hata na
adui zake na hata kuwapungia mikono; hamjui kwanini anafanya hivyo ngoja niwaeleze
mambo yalivyo;
Kipindi cha utawala wangu nilikuwa kwa muda mrefu lakini ikabidi niwe nabadilisha
uongozi kutokana na mazingira ya wakati; kuna muda nilihitaji Waziri Mkuu mpole kama
Rashid Kawawa, na pale nilipohitaji Waziri Mkuu wa kupambana na kasi ya Uchumi wa
Kimataifa nilimhitaji Cleopa David Msuya; wakati wa kuwa na Nguvu Kazi na Kuweka
Ukali kwenu nilimtumia Edward Sokoine. Kipindi cha Utawala wa Mzee Mwinyi ilibidi
tukubali kuwa na Utawala wa Upole sana kwavile tulikuwa na hali duni kiuchumi suala la
Uwaziri Mkuu haikuwa tatizo sana ilikuwa lazima uwe na mtu kama Joseph Warioba
mwenye Busara, na alipomaliza ikabidi tuwe na mtu Mwenye Busara katika watu watano
kuliko wote Duniani ndugu Samuel Malecela. Lakini mwishoni mwa Miaka ya tisini tulihitaji
Busara itumike kidogo na hivyo kulazimika kumtumia Augustine Mrema nadhani
mnakumbuka alivyowaendesha Wananchi wangu hadi alipozidisha zaidi Matakwa yetu
ikabidi tumlazimishe ajiuzuru katika Serikali ya awamu ya pili.
Kipindi cha Ben kilikuwa cha Uwazi na Ukweli, ilibidi tumtumie Fredrick Sumaye ambaye
ukweli anayemjua sana ni Ben kwani alikaa naye miaka kumi. Wengi walifikia kusema
Fredrick asingefaa kuwa Waziri Mkuu ndani ya Serikali lakini akazidi kumtumia miaka yote
kumi; najiuliza kama Fredrick pamoja na wenzie aliokaa nao leo ameitwa Mpumbavu na
Lofa na bosi wake wa ndani ya Ikulu nyie Watanzania wangu mnashtuka nini? Kipindi cha
Ben kilikuwa cha kusimamia Maadili walikuwa hawacheki na kutabasamu; Mkumbuke Omar
Mahita, Robbert Mboma, Upson Mwangónda, na Kamanda Banzi, hii ilikuwa safu ya
Unidhamishi. Kijana wangu Ben bado ni wa Uwazi na Ukweli na Mnidhamishi kamwe
hajatukana bali ametoa sifa za watu. Katika siasa kuna hekima na Maarifa, ili uweze kujua
Hekima, Wazimu Na Upumbavu mtambue ni sawa na kujilisha upepo; kwani wingi wa
hekima mna wingi wa huzuni sielewi mnalalamika nini? Mnafaa kujitathmini ili hekima yenu
isiwe na huzuni. Na Mfahamu ya kuwa mgombea Urais anayeongezeya Maarifa huongeza
masikitiko.
Mnashtuka kwasababu mmejaa Ukikwete; Kipindi cha Jakaya ni cha Diplomasia, Upole,
Kufurahi na kuwaunganisha kama ndugu; Jakaya hufurahi na maadui na hata kuwapungia
mkono wa heri; kwani anajua “Heri Wenye Moyo Safi Maana Hao Wataitwa Wana Wa
Mungu”. Watu wanaomtukana Jakaya kwenye Mitandao watamkumbuka kwa kutoa machozi
yasiyofutika kamwe na ni laana. Safu yake imejaa wenye upole na ndiyo maana Edward
mambo yalimshinda miaka miwili tu ya Utawala wake; ikabidi akae Mizengo ambaye muda
wote mlimuonea, mkumbuke Alhaj Mwema, Gen Davis, na sasa Ezekiel; hivyo sioni ajabu
mkishtuka kauli za Unidhamishi kutoka kwa Ben. Na hata Jakaya alipomtumia Harrison
Mwakyembe na John Magufuli, wawili hawa walionekana kama ni timu tofauti kabisa maana
haikuwa muda wao muafaka.
Mioyo yenu iwaongoze kwa hekima jinsi ya kushikana na Upumbavu ambao Ben
amewaambia, ili myaone mema ya kuwafaa Watanzania. Kwani naamini kuwa Edward ni
bidhaa inayopendwa lakini haiuziki ndani ya medani ya soko la siasa wakati John Magufuli
ni bidhaa inayouzika lakini haijapendwa sana ndani ya medani ya soko la siasa. Ben
anapofoka anavaa Ubaba katika Taifa lenu msikilizeni, muulizeni Baba una maana gani
badala ya kulalamika.
Mimi Mwalimu nikageuka kuwaletea Mabadiliko ya Uongozi wa kupokezana kwa heshima
tofauti na Mataifa mengine ili kupambanua Hekima, Wazimu, na Upumbavu. Hata Ben
ameweza kutambua Upumbavu baada ya kuona watu wamegeuka. Nikaona kuwa kweli
Hekima hupita Upumbavu kwa kadri Makada wa CCM wanavyowazidi Makada wa vyama
vingine. Nafahamu kuwa macho yake mwenye hekima yamo ndani ya Ilani zenu za vyama,
lakini Mpumbavu huenda bila Sera wala Dira, naomba mtathmini hayo. Kwani
mmechanganya nyama ya Samaki na nyama ya Mbuzi yaani CCM-Edward na CUF-Duni
iangalieni Ilani ya CHADEMA na siyo kutangaza UKAWA mnauwa CHADEMA
aliyoianzisha ndugu yangu Edwin Mtei na niliisifu sana Katiba yake Mwaka 1992.
Huku kuzimu nikatambua kuwa ni tukio la tarehe 25 Oktoba, 2015 litakalowapata wote
sawasawa kushinda au kushindwa. Hata mimi Mwalimu nilipata kuwaambia kuwa mnaacha
yaliyo mema tuliyoyafanya mnachukua ya Kipumbavu; yumkini kusema yalikuwepo ya
kijinga pia; sioni kama Ben amekosea kutoa hisia zake na kuwajulisha anavyowafahamu
baadhi ya watu. Nikaichukua kazi yangu yote toka nilipopigania Uhuru na ni vyema iachwe
kwa mwenye hekima na siyo Mpumbavu, na atawale yangu yote niliyoshughulika kwa faida
ya Watanzania. Mnalipoteza kaburi la TANU na ASP kwa kupoteza neno la Mapinduzi ndani
ya chama changu CCM kwa dhana ya kujifanya mnataka Mabadiliko? Kabla ya kufanya
Mabadiliko ni vyema mtathmini ni Mabadiliko yapi mnayoyataka. Nimefahamu huku kuzimu
Edward na Regina ni Watanzania wa Kwanza Kuhiji Israel na kwenda Nigeria kwa TB
Joshua baada ya kujiuzuru Mwaka 2008; kijana huyu nasikia ameokoka na sasa ananyoosha
mkono wa kutoa Mbaraka mithiri ya Mpakwa Mafuta; CHADEMA mmesahau hata vidole
viwili vya Amani na Upendo.
Mpumbavu huikunja mikono yake naye hula chakula chake mwenyewe na si kwa ajili ya
Watanzania.Edward anajua hilo ndiyo maana hakunji mikono; John Magufuli ndiyo haswa
ananikuna kwani tafsiri ya mikono siyo mikono ya mwili kiroho, mikono ni kauli zenye
mshiko zitokazo kwenye ulimi wenye Upako. Kama Edward ana Upako wa nywele nyeupe
basi John Magufuli ana Upako kwenye Ulimi wake; naomba Muwatathmini. Ndoto za
kwenda Ikulu huja kwa shughuli nyingi na sauti ya Mpumbavu kwa njia ya wingi wa
maneno. Kazi yote ya Mwanasiasa ni kwa Ilani ya Chama chake; kwa maana mwenye
hekima hupata faida gani kuliko Mpumbavu?. Heri kusikia laumu ya mwenye hekima kama
Ben ndani ya vyama vyenu kuliko mtu kusikia wimbo wa Wapumbavu. Lakini pia CCM
msiwe na jeuri kwa vile mna hekima kwani jeuri hupumbaza mwenye hekima. Heri mwisho
wa Kampeni zenu kuliko mwanzo wake, msilaumu neno mwanzo wa Kampeni, huenda
likawa na maana sana mwisho wake na historia ikageuka kuwahukumu wakati Ben
akipumzika. UKAWA msifanye haraka kukasirika rohoni mwenu; maana hasira hukaa
kifuani mwa Wapumbavu na ndipo Ben atakapoonekana alikuwa sahihi. Siku ya kufanikiwa
furahini na siku ya mabaya fikirini.
Maneno ya wenye hekima kama Ben yanenwayo taratibu husikiwa zaidi ya mlio wake
atawalaye katikati ya Wapumbavu. Hekima ya kusema ni bora zaidi kuliko silaha za vita.
Upumbavu haba ni mzito kuliko hekima na heshima. Moyo wake mwenye hekima upo
upande wa kuume na ndiyo maana niliwapa maana ya Benjamin kuwa ni Mtoto wa mkono wa
Kuume, bali moyo wake Mpumbavu upo mkono wa kushoto. Mpumbavu aendapo njiani
hupungukiwa fahamu zake angalieni UKAWA msije mkapungukiwa ufahamu kabla ya
kufika Ikulu, kwani pia mmenichanganya ni CHADEMA inaenda Ikulu, Edward au
UKAWA?Angalieni Wanangu UKAWA isije ikawa UKIWA.
Edward anafahamu sana kuwa maneno ya kinywa cha mwenye hekima kama Ben yana
neema; na ndiyo maana aliwaomba kuwa kama mnadhani Ben ametukana msameheni kwani
anajua pia kuwa midomo ya Mpumbavu itammeza nafsi yake mwenye Upumbavu; Edward
asingependa nafsi zenu zimezwe kwani mwanzo wa maneno yenu ni upuuzi na mwisho wa
usemi wenu ni wazimu wenye hatari.
Nisingependa kuingilia Uhuru wenu wa kuchagua viongozi lakini chagueni atakaye enzi Sera
zangu hususan atakayejali Kazi kwani Kazi ni kipimo cha Utu wa Mtanzania. Na Maendeleo
yoyote huletwa na Kazi. Ikumbuke Imani niliyowaachia “Nitasema Kweli Daima Fitna
Kwangu Mwiko”.
Mara nikazinduka na nikajikuta niko Muhimbili Hospitali ambayo zamani iliitwa St Magreth
nimelazwa nasikia John Magufuli yuko Nkasi, Edward Uwanja wa Fisi Toobaah.
MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRIKA

More Related Content

More from Prof Handley Mpoki Mafwenga

Tax justice and advocacy clinicA Focus on the Revenue Index for Effective Fis...
Tax justice and advocacy clinicA Focus on the Revenue Index for Effective Fis...Tax justice and advocacy clinicA Focus on the Revenue Index for Effective Fis...
Tax justice and advocacy clinicA Focus on the Revenue Index for Effective Fis...Prof Handley Mpoki Mafwenga
 
MASTERS THESIS (ESAMI-MAASTRICHT SCHOOL OF MANAGEMENT -MsM)
MASTERS THESIS (ESAMI-MAASTRICHT SCHOOL OF MANAGEMENT -MsM)MASTERS THESIS (ESAMI-MAASTRICHT SCHOOL OF MANAGEMENT -MsM)
MASTERS THESIS (ESAMI-MAASTRICHT SCHOOL OF MANAGEMENT -MsM)Prof Handley Mpoki Mafwenga
 
The African Interview Questions Between Joyce Mmassy and Prof Handley Mpoki M...
The African Interview Questions Between Joyce Mmassy and Prof Handley Mpoki M...The African Interview Questions Between Joyce Mmassy and Prof Handley Mpoki M...
The African Interview Questions Between Joyce Mmassy and Prof Handley Mpoki M...Prof Handley Mpoki Mafwenga
 
WARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETE
WARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETEWARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETE
WARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETEProf Handley Mpoki Mafwenga
 
MHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUA
MHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUAMHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUA
MHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUAProf Handley Mpoki Mafwenga
 
TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA
TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZATEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA
TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZAProf Handley Mpoki Mafwenga
 
WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA KWA HAYATI MWAL ...
WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA   KWA HAYATI MWAL ...WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA   KWA HAYATI MWAL ...
WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA KWA HAYATI MWAL ...Prof Handley Mpoki Mafwenga
 
WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZ...
WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZ...WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZ...
WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZ...Prof Handley Mpoki Mafwenga
 
SDGs Tanzania poverty headcount declining as economic growth expands
SDGs Tanzania poverty headcount declining as economic growth expandsSDGs Tanzania poverty headcount declining as economic growth expands
SDGs Tanzania poverty headcount declining as economic growth expandsProf Handley Mpoki Mafwenga
 
LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inawez...
LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inawez...LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inawez...
LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inawez...Prof Handley Mpoki Mafwenga
 
THE OVERSIGHT ROLE OF TANZANIA MINERAL AUDIT AGENCY (TMAA)
THE OVERSIGHT ROLE OF TANZANIA MINERAL AUDIT AGENCY (TMAA)THE OVERSIGHT ROLE OF TANZANIA MINERAL AUDIT AGENCY (TMAA)
THE OVERSIGHT ROLE OF TANZANIA MINERAL AUDIT AGENCY (TMAA)Prof Handley Mpoki Mafwenga
 
The Fiscal Analysis on Capital Gains Taxing Rights
The Fiscal Analysis on Capital Gains Taxing RightsThe Fiscal Analysis on Capital Gains Taxing Rights
The Fiscal Analysis on Capital Gains Taxing RightsProf Handley Mpoki Mafwenga
 

More from Prof Handley Mpoki Mafwenga (20)

Tax justice and advocacy clinicA Focus on the Revenue Index for Effective Fis...
Tax justice and advocacy clinicA Focus on the Revenue Index for Effective Fis...Tax justice and advocacy clinicA Focus on the Revenue Index for Effective Fis...
Tax justice and advocacy clinicA Focus on the Revenue Index for Effective Fis...
 
MASTERS THESIS (ESAMI-MAASTRICHT SCHOOL OF MANAGEMENT -MsM)
MASTERS THESIS (ESAMI-MAASTRICHT SCHOOL OF MANAGEMENT -MsM)MASTERS THESIS (ESAMI-MAASTRICHT SCHOOL OF MANAGEMENT -MsM)
MASTERS THESIS (ESAMI-MAASTRICHT SCHOOL OF MANAGEMENT -MsM)
 
TAX JUSTICE AND ADVOCACY CLINIC 2
TAX JUSTICE AND ADVOCACY CLINIC  2TAX JUSTICE AND ADVOCACY CLINIC  2
TAX JUSTICE AND ADVOCACY CLINIC 2
 
The African Interview Questions Between Joyce Mmassy and Prof Handley Mpoki M...
The African Interview Questions Between Joyce Mmassy and Prof Handley Mpoki M...The African Interview Questions Between Joyce Mmassy and Prof Handley Mpoki M...
The African Interview Questions Between Joyce Mmassy and Prof Handley Mpoki M...
 
BARUA YA SIRI KWA DR MOHAMED SHEIN TOKA AHELA
BARUA YA SIRI KWA DR MOHAMED SHEIN TOKA AHELABARUA YA SIRI KWA DR MOHAMED SHEIN TOKA AHELA
BARUA YA SIRI KWA DR MOHAMED SHEIN TOKA AHELA
 
WARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETE
WARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETEWARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETE
WARAKA WA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA KIKWETE
 
MHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUA
MHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUAMHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUA
MHESHIMIWA PINDA HAKUPINDA BALI WANASHERIA WAMECHEUA
 
IKULU SI MAHALA PA KUKIMBILIA HATA KIDOGO
IKULU SI MAHALA PA KUKIMBILIA HATA KIDOGOIKULU SI MAHALA PA KUKIMBILIA HATA KIDOGO
IKULU SI MAHALA PA KUKIMBILIA HATA KIDOGO
 
TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA
TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZATEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA
TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA
 
WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA KWA HAYATI MWAL ...
WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA   KWA HAYATI MWAL ...WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA   KWA HAYATI MWAL ...
WARAKA WA UPENDO KWA JOHN MAGUFURI NA EDWARD LOWASA KUTOKA KWA HAYATI MWAL ...
 
WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZ...
WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZ...WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZ...
WARAKA WA IKULU TAKATIFU KWA JOHN MAGUFULI, NA EDWARD LOWASA NA HATMA YA TANZ...
 
SDGs Tanzania poverty headcount declining as economic growth expands
SDGs Tanzania poverty headcount declining as economic growth expandsSDGs Tanzania poverty headcount declining as economic growth expands
SDGs Tanzania poverty headcount declining as economic growth expands
 
LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inawez...
LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inawez...LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inawez...
LAANA YA RASILIMALI KATIKA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA- Je Tanzania Inawez...
 
UFA WA UTEKELEZAJI WA LOCAL CONTENT
UFA WA UTEKELEZAJI WA LOCAL CONTENTUFA WA UTEKELEZAJI WA LOCAL CONTENT
UFA WA UTEKELEZAJI WA LOCAL CONTENT
 
EAST AFRICAN JOURNAL OF RESEARCH
EAST AFRICAN JOURNAL OF RESEARCHEAST AFRICAN JOURNAL OF RESEARCH
EAST AFRICAN JOURNAL OF RESEARCH
 
TEKU publication2
TEKU publication2TEKU publication2
TEKU publication2
 
THE OVERSIGHT ROLE OF TANZANIA MINERAL AUDIT AGENCY (TMAA)
THE OVERSIGHT ROLE OF TANZANIA MINERAL AUDIT AGENCY (TMAA)THE OVERSIGHT ROLE OF TANZANIA MINERAL AUDIT AGENCY (TMAA)
THE OVERSIGHT ROLE OF TANZANIA MINERAL AUDIT AGENCY (TMAA)
 
TAX JUSTICE AND ADVOCACY CLINIC 2
TAX JUSTICE AND ADVOCACY CLINIC  2TAX JUSTICE AND ADVOCACY CLINIC  2
TAX JUSTICE AND ADVOCACY CLINIC 2
 
The Fiscal Analysis on Capital Gains Taxing Rights
The Fiscal Analysis on Capital Gains Taxing RightsThe Fiscal Analysis on Capital Gains Taxing Rights
The Fiscal Analysis on Capital Gains Taxing Rights
 
The Commonwealth Natural Resources Forum
The Commonwealth Natural Resources ForumThe Commonwealth Natural Resources Forum
The Commonwealth Natural Resources Forum
 

WARAKA WA UPUMBAVU NA ULOFA KATIKA DEMOKRASIA

  • 1. WARAKA WA UPUMBAVU NA ULOFA KATIKA DEMOKRASIA Rai ya Mtanzania Na Prof Handley Mpoki Mafwenga Ph.D (finance -COU), MSc (finance -Strathclyde), MBA (Mg.Eco -ESAMI/MsM), LLM (taxation- UDSM), LLB (Tudarco), PGD tax mgt (IFM), AD tax mgt (IFM)] Nikiwa katikati ya mji ghafla namuona Edward Lowasa anapanda Daladala siamini macho yangu Napata kizunguzungu ghafla naanguka mithiri ya mgonjwa wa kifafa napoteza fahamu. Mara namuona Mwalimu Nyerere ameshika kisu kinadondosha damu, mkono wa kulia kashika Katiba ya Tanzania imejaa damu, kisu chake kina maandishi madogomadogo ya aina mbili “Wapumbavu,…….. Malofa”. Ananipa Katiba anaamrisha niipekue mara nakutana na picha ya Fredrick Sumaye imezungukwa na maneno "Wapumbavu…Malofa” picha imeambatana na Waraka ananipa niwape Watanzania na viongozi wetu Ben Mkapa, Edward Lowasa na Fredrick Sumaye yenye ujumbe ufuatao; Wanangu Watanzania yumkini hamjui maana hata ya majina ya viongozi wenu; kabla ya kuwalaumu kwa matamshi yao yafaa mjue maana ya majina yao. Majina huumba tabia, ukimwita mwanao “Chuki”atakuwa na “Chuki”; “Chausiku atakuwa mtu wa kutoka usiku’”Shida”atakuwa mwenye shida daima n.k Mini Baba yenu wa Taifa nilichagua Rais kwa maana ya jina liendalo na matakwa ya mazingira ya wakati huo; leo mna jina la Edward maana yake hutokana na asili ya Kiingereza likitoholewa kutokana na jamii ya Wajerumani wa asili ya Angeln na Saxony ambao walihamia Uingereza baada ya kuanguka kwa Dola la Roma Miaka 410 Baada ya Kristo hao huitwa Anglo-saxion. Ni jina lijulikanalo kwa asili kama Ēadweard, likiundwa na maneno mawili “Ead” likiwa na maana ya Mali, Utajiri, Bahati, Matumaini na neno “Weard” likiwa na maana ya Mlinzi au Mdhibiti. Kwa mujibu wa jina lake siyo ajabu kumsikia anachukia sana Umaskini na anapenda sana Watanzania wote wawe matajiri kama Mengi na Bhahresa. ila Kauli hiyo si ya kweli kwani hata nchi zilizoendelea zina Maskini na Tajiri. Lakini kwa vile anatamani muombeeni kauli zake ziumbe ndoto zake ziwe kweli. Jina Edward linavumisha sifa ya mtu mwenye nguvu na anayenuwia jambo. Huwa anapenda kuwa kiongozi pale bahati inapomwangukia ingawa wakati mwingine angependa kuwa kimya awapo kiongozi na kuwa Mfano wa wengine pale anapoamini hafikiwi na watu. Ni mtu mwenye nidhamu kwa kiwango kikubwa ambapo hawezi kukubali kuwa mtu wa kawaida na kufanya mambo ya bandia. Nguvu zake ni dhana ya kujiamini na kupania mambo, huwa na mvuto wa asili ya Mamlaka na kipaji cha kupangiliza mambo na kuwa na Uandilifu, Uwezo, Uimara na dhana kuu ya Haki. Kwa upande mwingine mapungufu yake ni mtu wa kujiona kwa kulingia Ujuzi wake na kuwa mtu mwenye msimamo kitu kinachomfanya awe mzito kubadilika kutokana na mazingira, hasira alizonazo na kushindwa
  • 2. kuwa mvumilivu. Huwa ni mtu mwenye tabia ya usumbufu na kufuatilia mambo ya watu. Lakini kumbuka ni pale tu anapoamini yeye ni sahihi muda wote. Ni mtu wa kupania mambo ambaye ana kila nafasi ya kuishi kwa umoja na raha. Anapokuwa katika umri mdogo huwa makini, muwajibikaji, na mwenye kuathiriwa zaidi na mazingira ya familia yake. Jina la Edward hutoa sifa ya kupenda kuwa Mfano kwa jamii na mtu anayeogopa sana kueleweka vibaya ndani ya jamii Mnaye kijana wangu Benjamin Mkapa, Mwanahabari aliyebobea masuala ya Diplomasia enzi zangu alinisaidia sana. Jina Benjamin maana yake “Kijana wa Mkono wa Kuume” ni jina lililotumika pia na mtoto wa Mwisho kati ya Watoto 12 wa Yakobo. Jina hili lina maana pia ya “Kijana wa Kusini” na pengine huwa na maana ya “Kijana wa Uzao wa Uzeeni” ni Jina lenye asili ya Kiebrania na maana yake ni “Kijana wa Mkono wa Kiume” au “Bahati”. Ni jina linalotamkwa Ben-Ja-Men. Kama nilivyobainisha, ni mtoto wa Yakobo na Raheli na mjukuu wa Isaka. Rahel alikufa alipokuwa akimzaa na kumwita jina la “Benon” yaani “Mtoto wa Uchungu Wangu” Baadaye jina hili likabadilishwa na Yakobo kuwa Benjamin. Watu wenye Jina la Benjamin ni watu wenye hisia kubwa ya kuwa na Msimamo, wanapenda familia zao na Jamii kwa ujumla na wanahitaji sana kufanya kazi na watu wengine na zaidi hupenda kushukuriwa. Watu wa Jina hili wanapenda sana Mabadiliko, kufanya Maajabu na kuwa Mwanaharakati. Ni wepesi kubadilika kutokana na Mazingira, Wana Mtazamo mpana na Busara, wanauwezo wa kuweka mazingira mazuri ya kutumia uhuru uliopo. Wanapenda kupambana na Sheria na Kanuni zinazowazuia kufanya kazi. Ni wepesi pia kubadilishwa wanachokiamini kwani ni wasikivu, kutopumzika na kuwa wana Mapinduzi halisi. Kuna kijana huko kwenu tumemsikia akiwa ana enzi dhana yangu ya “Kazi ni Kipimo cha Utu” nasikia mnamwita Jembe; hii inanikumbusha enzi zangu za Chama kimoja ambapo wagombea Ubunge niliwagawia uhuru wa kuchagua Jembe au Nyumba. Nilipata Wabunge wengi wenye alama ya Jembe kuliko Nyumba. Na Jembe ilikuwa ishara ya uwakilishi wa Wakulima wakati nyumba ilikuwa kwa Wafanyakazi. Sijaelewa tafsiri yenu lakini pengine inaendana na jina lake. Jina la John maana yake ni “Rehema ya Mungu” lina asili ya Kiebrania maana yake “Yehova ni Mwenye Rehema, ameonyesha Upendeleo”. Katika Biblia jina hili lilitumiwa na Yohana Mbatizaji aliyembatiza Yesu Kristo katika Mto Jordan. Watu wenye jina hili wanapenda sana kuwa na Msimamo, wanapenda familia zao na jamii kwa ujumla na wanapenda kufanya kazi na watu wengine na kushukuriwa. Watu wenye jina hili wanahurka ya kuwa wakimya, wenye kushirikiana na wenzao, wenye kujali wenzao, wenye upendo kama wanavyojipenda wenyewe, wepesi kuishi nao, hawayumbi kwenye maamuzi na wakati mwingine hupenda kuonea watu soni. Ni watu wenye Uaminifu wa hali ya juu, wanaheshimu hali ya kujiamini ya watu wengine, na wana diplomasia ya hali ya juu, wapatanishi na wanapenda kushirikiana na watu. Mara kwa mara ni wabunifu, wanapenda maelezo ya kina yenye ukweli na sheria na wakati wote wanaona mabadiliko yanapaswa kuangaliwa kwa umakini. Wanapenda sana kuwa na dhana ya kujiona siyo salama hivyo siyo watu wa kupumzika. Lakini pia anatumia jina la Joseph ambalo ni jina la kilatini aina ya Kigiriki kilichoanzia kwa Waebrania maana yake “Ätaongeza” Jina hili pia mbali ya Mume wa Mariah mama wa yesu lilitumika na Mtoto wa kumi na moja wa Yakobo kipenzi wake ambaye kaka yake Rubeni alimuuza Misri na kumwambia baba yake kuwa ameuwawa kwa kumuokoa kuuwawa na ndugu zake na ndiye alikuwa mshauri wa mfalme wa faraoh aliyewokoa Uzao wa Yakobo wakati wa Njaa.
  • 3. Jina la Fredrick ni jina la asili ya Uingereza lenye asili zaidi ya Ujerumani likiwa na maana “Mtawala wa Amani” likijumuisha maneno frid yaani Ämani”na ric yaani “Mtawala”. Jina hili lilikuwa maarufu sana kwenye ukanda wa lugha ya Ujerumani likitumiwa zaidi na Dola la Kiroho la Roma, Ujerumani, Austria, Scandinavia, na Prussia. Watu wenye jina hili huchukuliwa kuwa ni watu wenye mtazamo chanya (extrovert), wenye akili nyingi, na wenye ubunifu wa hali ya juu. Watu hawa huwa wajasiriamali wenye kupenda mafanikio na hutumia akili zao katika kujenga dhana ya ukweli. Watu hawa huwa na mvuto wawapo katika kundi la watu na wenye kujipenda sana. Huchukuliwa kuwa ni Watawala kwenye familia zao, marafiki, na hupendwa kwa upekee sana. Nimesikia kuwa mnalalamika Ben amewatukana, nadhani hamjujui Ben kama ninavyomjua mimi; Ben mmesahau kuwa ni mzee wa Uwazi na Ukweli na ndiyo maana enzi zake zilikuwa ni za Uwazi na Ukweli; lakini pia tatizo lenu Watanzania wangu mmezoweshwa kwa muda wa miaka kumi mkiwa na Rais Jakaya ambaye ni mcheshi, mpole na anatabasamu hata na adui zake na hata kuwapungia mikono; hamjui kwanini anafanya hivyo ngoja niwaeleze mambo yalivyo; Kipindi cha utawala wangu nilikuwa kwa muda mrefu lakini ikabidi niwe nabadilisha uongozi kutokana na mazingira ya wakati; kuna muda nilihitaji Waziri Mkuu mpole kama Rashid Kawawa, na pale nilipohitaji Waziri Mkuu wa kupambana na kasi ya Uchumi wa Kimataifa nilimhitaji Cleopa David Msuya; wakati wa kuwa na Nguvu Kazi na Kuweka Ukali kwenu nilimtumia Edward Sokoine. Kipindi cha Utawala wa Mzee Mwinyi ilibidi tukubali kuwa na Utawala wa Upole sana kwavile tulikuwa na hali duni kiuchumi suala la Uwaziri Mkuu haikuwa tatizo sana ilikuwa lazima uwe na mtu kama Joseph Warioba mwenye Busara, na alipomaliza ikabidi tuwe na mtu Mwenye Busara katika watu watano kuliko wote Duniani ndugu Samuel Malecela. Lakini mwishoni mwa Miaka ya tisini tulihitaji Busara itumike kidogo na hivyo kulazimika kumtumia Augustine Mrema nadhani mnakumbuka alivyowaendesha Wananchi wangu hadi alipozidisha zaidi Matakwa yetu ikabidi tumlazimishe ajiuzuru katika Serikali ya awamu ya pili. Kipindi cha Ben kilikuwa cha Uwazi na Ukweli, ilibidi tumtumie Fredrick Sumaye ambaye ukweli anayemjua sana ni Ben kwani alikaa naye miaka kumi. Wengi walifikia kusema Fredrick asingefaa kuwa Waziri Mkuu ndani ya Serikali lakini akazidi kumtumia miaka yote kumi; najiuliza kama Fredrick pamoja na wenzie aliokaa nao leo ameitwa Mpumbavu na Lofa na bosi wake wa ndani ya Ikulu nyie Watanzania wangu mnashtuka nini? Kipindi cha Ben kilikuwa cha kusimamia Maadili walikuwa hawacheki na kutabasamu; Mkumbuke Omar Mahita, Robbert Mboma, Upson Mwangónda, na Kamanda Banzi, hii ilikuwa safu ya Unidhamishi. Kijana wangu Ben bado ni wa Uwazi na Ukweli na Mnidhamishi kamwe hajatukana bali ametoa sifa za watu. Katika siasa kuna hekima na Maarifa, ili uweze kujua Hekima, Wazimu Na Upumbavu mtambue ni sawa na kujilisha upepo; kwani wingi wa hekima mna wingi wa huzuni sielewi mnalalamika nini? Mnafaa kujitathmini ili hekima yenu isiwe na huzuni. Na Mfahamu ya kuwa mgombea Urais anayeongezeya Maarifa huongeza masikitiko. Mnashtuka kwasababu mmejaa Ukikwete; Kipindi cha Jakaya ni cha Diplomasia, Upole, Kufurahi na kuwaunganisha kama ndugu; Jakaya hufurahi na maadui na hata kuwapungia mkono wa heri; kwani anajua “Heri Wenye Moyo Safi Maana Hao Wataitwa Wana Wa Mungu”. Watu wanaomtukana Jakaya kwenye Mitandao watamkumbuka kwa kutoa machozi yasiyofutika kamwe na ni laana. Safu yake imejaa wenye upole na ndiyo maana Edward mambo yalimshinda miaka miwili tu ya Utawala wake; ikabidi akae Mizengo ambaye muda wote mlimuonea, mkumbuke Alhaj Mwema, Gen Davis, na sasa Ezekiel; hivyo sioni ajabu mkishtuka kauli za Unidhamishi kutoka kwa Ben. Na hata Jakaya alipomtumia Harrison
  • 4. Mwakyembe na John Magufuli, wawili hawa walionekana kama ni timu tofauti kabisa maana haikuwa muda wao muafaka. Mioyo yenu iwaongoze kwa hekima jinsi ya kushikana na Upumbavu ambao Ben amewaambia, ili myaone mema ya kuwafaa Watanzania. Kwani naamini kuwa Edward ni bidhaa inayopendwa lakini haiuziki ndani ya medani ya soko la siasa wakati John Magufuli ni bidhaa inayouzika lakini haijapendwa sana ndani ya medani ya soko la siasa. Ben anapofoka anavaa Ubaba katika Taifa lenu msikilizeni, muulizeni Baba una maana gani badala ya kulalamika. Mimi Mwalimu nikageuka kuwaletea Mabadiliko ya Uongozi wa kupokezana kwa heshima tofauti na Mataifa mengine ili kupambanua Hekima, Wazimu, na Upumbavu. Hata Ben ameweza kutambua Upumbavu baada ya kuona watu wamegeuka. Nikaona kuwa kweli Hekima hupita Upumbavu kwa kadri Makada wa CCM wanavyowazidi Makada wa vyama vingine. Nafahamu kuwa macho yake mwenye hekima yamo ndani ya Ilani zenu za vyama, lakini Mpumbavu huenda bila Sera wala Dira, naomba mtathmini hayo. Kwani mmechanganya nyama ya Samaki na nyama ya Mbuzi yaani CCM-Edward na CUF-Duni iangalieni Ilani ya CHADEMA na siyo kutangaza UKAWA mnauwa CHADEMA aliyoianzisha ndugu yangu Edwin Mtei na niliisifu sana Katiba yake Mwaka 1992. Huku kuzimu nikatambua kuwa ni tukio la tarehe 25 Oktoba, 2015 litakalowapata wote sawasawa kushinda au kushindwa. Hata mimi Mwalimu nilipata kuwaambia kuwa mnaacha yaliyo mema tuliyoyafanya mnachukua ya Kipumbavu; yumkini kusema yalikuwepo ya kijinga pia; sioni kama Ben amekosea kutoa hisia zake na kuwajulisha anavyowafahamu baadhi ya watu. Nikaichukua kazi yangu yote toka nilipopigania Uhuru na ni vyema iachwe kwa mwenye hekima na siyo Mpumbavu, na atawale yangu yote niliyoshughulika kwa faida ya Watanzania. Mnalipoteza kaburi la TANU na ASP kwa kupoteza neno la Mapinduzi ndani ya chama changu CCM kwa dhana ya kujifanya mnataka Mabadiliko? Kabla ya kufanya Mabadiliko ni vyema mtathmini ni Mabadiliko yapi mnayoyataka. Nimefahamu huku kuzimu Edward na Regina ni Watanzania wa Kwanza Kuhiji Israel na kwenda Nigeria kwa TB Joshua baada ya kujiuzuru Mwaka 2008; kijana huyu nasikia ameokoka na sasa ananyoosha mkono wa kutoa Mbaraka mithiri ya Mpakwa Mafuta; CHADEMA mmesahau hata vidole viwili vya Amani na Upendo. Mpumbavu huikunja mikono yake naye hula chakula chake mwenyewe na si kwa ajili ya Watanzania.Edward anajua hilo ndiyo maana hakunji mikono; John Magufuli ndiyo haswa ananikuna kwani tafsiri ya mikono siyo mikono ya mwili kiroho, mikono ni kauli zenye mshiko zitokazo kwenye ulimi wenye Upako. Kama Edward ana Upako wa nywele nyeupe basi John Magufuli ana Upako kwenye Ulimi wake; naomba Muwatathmini. Ndoto za kwenda Ikulu huja kwa shughuli nyingi na sauti ya Mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno. Kazi yote ya Mwanasiasa ni kwa Ilani ya Chama chake; kwa maana mwenye hekima hupata faida gani kuliko Mpumbavu?. Heri kusikia laumu ya mwenye hekima kama Ben ndani ya vyama vyenu kuliko mtu kusikia wimbo wa Wapumbavu. Lakini pia CCM msiwe na jeuri kwa vile mna hekima kwani jeuri hupumbaza mwenye hekima. Heri mwisho wa Kampeni zenu kuliko mwanzo wake, msilaumu neno mwanzo wa Kampeni, huenda likawa na maana sana mwisho wake na historia ikageuka kuwahukumu wakati Ben akipumzika. UKAWA msifanye haraka kukasirika rohoni mwenu; maana hasira hukaa kifuani mwa Wapumbavu na ndipo Ben atakapoonekana alikuwa sahihi. Siku ya kufanikiwa furahini na siku ya mabaya fikirini. Maneno ya wenye hekima kama Ben yanenwayo taratibu husikiwa zaidi ya mlio wake atawalaye katikati ya Wapumbavu. Hekima ya kusema ni bora zaidi kuliko silaha za vita. Upumbavu haba ni mzito kuliko hekima na heshima. Moyo wake mwenye hekima upo
  • 5. upande wa kuume na ndiyo maana niliwapa maana ya Benjamin kuwa ni Mtoto wa mkono wa Kuume, bali moyo wake Mpumbavu upo mkono wa kushoto. Mpumbavu aendapo njiani hupungukiwa fahamu zake angalieni UKAWA msije mkapungukiwa ufahamu kabla ya kufika Ikulu, kwani pia mmenichanganya ni CHADEMA inaenda Ikulu, Edward au UKAWA?Angalieni Wanangu UKAWA isije ikawa UKIWA. Edward anafahamu sana kuwa maneno ya kinywa cha mwenye hekima kama Ben yana neema; na ndiyo maana aliwaomba kuwa kama mnadhani Ben ametukana msameheni kwani anajua pia kuwa midomo ya Mpumbavu itammeza nafsi yake mwenye Upumbavu; Edward asingependa nafsi zenu zimezwe kwani mwanzo wa maneno yenu ni upuuzi na mwisho wa usemi wenu ni wazimu wenye hatari. Nisingependa kuingilia Uhuru wenu wa kuchagua viongozi lakini chagueni atakaye enzi Sera zangu hususan atakayejali Kazi kwani Kazi ni kipimo cha Utu wa Mtanzania. Na Maendeleo yoyote huletwa na Kazi. Ikumbuke Imani niliyowaachia “Nitasema Kweli Daima Fitna Kwangu Mwiko”. Mara nikazinduka na nikajikuta niko Muhimbili Hospitali ambayo zamani iliitwa St Magreth nimelazwa nasikia John Magufuli yuko Nkasi, Edward Uwanja wa Fisi Toobaah. MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRIKA