1. VVU/UKIMWI HAVIAMBUKIZWI KWA NJIA YA:
Busu kavu
Kuchangia vyombo/choo na mtu mwenye VVU
Kula pamoja na mtu mwenye VVU
Kukaa na mtu mwenye VVU
Kulala pamoja na mtu mwenye VVU
Kuishi na mtu mwenye VVU
Kula chakula kilichoandaliwa na mtu mwenye VVU
Kuishi/kufanya kazi pamoja na mtu mwenye VVU
MAMBO MUHIMU YAKUKUMBUKA:
Inachukua muda mrefu kwa mfumo wa kinga kuharibiwa na VVU na mtu
kufikia hatua ya UKIMWI
Watu wenye maambukizi ya VVU mara nyingine hawaonyeshi dalili yoyote
Mtu aliyeambukizwa anaweza kuambukiza wengine mara apatapo
maambukizi, ingawa anaweza kuonekana mwenye afya njema
Siyo rahisi kumtambua kama mtu ameambukizwa VVU kwa
kumuangalia tu
Njia pekee ya kumtambua kama mtu ameambukizwa VVU ni kupima afya
TUNAWEZA KUZUIA MAAMBUKIZI YA VVU KWA:
Kupima afya zetu Kujua kama tuna maambukizi ama la
Kuacha kabisa kufanya ngono (muhimu kwa vijana na wasiooa)
Kuwa mwaminifu kwa mpenzi mmoja mwaminifu aliyepima na asiye na
maambukizi ya VVU
Kufanya mapenzi salama kwa kutumia kondomu kwa usahihi
Kuzingatia mambo muhimu ya kujikinga na maambukizi hasa wakati wa
kumhudumia wagonjwa
Kuzingatia unyonyeshaji salama
Kupunguza unyanyapaa na ubaguzi
Ukweli Kuhusu
VVU/UKIMWI
Tanzania Agriculture Productivity Program
(TAPP)
Increasedincomes through enhanced productivity
TAPP is a 5-year programto increase smallholder farmer
incomes through enhanced productivity and improved domestic
and export marketing of agriculturalproducts.
P.O. Box 15035 | Arusha, Tanzania |Tel: 255 (0) 27 2545325
tapp@fintrac.com | w w w .tanzania-agric.org
Kipeperushi kimeandaliwa kwa
msaada wa watu wa Marekani
kupitia shirika la misaada la
Marekani (USAID). Fintrac Inc.
atawajibika na matokeo y a kazi hii.
Taarif a hii ni maoni y a mtay arishaji
na si lazima y awakilishe maoni y a
USAID au Serikali y a Marekani.
2. USAID www.tanzania-agric.org USAID-TAPPUSAID-TAPP tapp@fintrac.com
VU ni jina la Virusi Vya UKIMWI ambavyo taratibu hushambulia mfumo
wa kinga ya mwili na kuufanya mwili kuwa katika hatari kubwa ya
kupata magonjwa na maambukizo
UKIMWI ni Upungufu wa Kinga Mwilini. Unaotokana na maambukizi ya VVU.
Unatokea pale ambapo mfumo wa kinga ya mwili unakuwa dhaifu sana na
kushindwa kukabiliana na magonjwa.
VIRUSI HUKAA WAPI KATIKA MWILI?
VVU hupatikana kwenye damu na majimaji ya sehemu za siri za mtu mwenye
maambukizi ya VVU, pia katika maziwa ya mama mwenye maambukizi ya
VVU.
ATHARI ZA UKIMWI NI ZIPI?
Kupungua umri wa kuishi
Kupoteza wanaowezesha familia kupata mahitaji ya kila siku
Kupunguza nguvukazi
Kupungua kwa kipato na maendeleo ya kiuchumi
VVU/UKIMWI HUAMBUKIZWAJE?
VVU/UKIMWI huambukizwaje?
Kufanya ngono isiyo salama na mtu aliye na VVU
Ngono isiyo salama ni kujamiiana kati ya watu wasiojua afya zao bila
kutumia kinga. Sehemu kubwa (zaidi ya asilimia 80) ya maambukizi ya
VVU yanatokana na ngono zisizo salama.
Maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto
Inawezekana mama mjamzito mwenye maambukizi ya VVU
kumwambukiza mwanaye kwa njia ya:
Wakati wa Ujauzito – iwapo mama atapata uambukizo katika mfuko wa
uzazi
Wakati wa Kujifungua – Uzazi wenye matatizo huweza kumuambukiza
mtoto.
Kunyonyesha-mama mwenye virusi anaponyonyesha huweza
kumwambukiza mwanae iwapo hatapata/hatafuata maelekezo ya
wataalamu wa afya.
Kuongezwa damu yenye maambukizi ya VVU
Iwapo mgonjwa ataongezwa damu au viungo vya mwili ambavyo vina
maambukizi ya VVU anaweza kupata maambukizi ya VVU.
Kushirikiana vifaa vyenye ncha kali
Iwapo kutakuwa na kiasi cha damu toka kwa mwenye maambukizi ya
VVU katika kifaa cha kuchomea au kukatia, mtu mwingine anaweza
kuambukizwa VVU iwapo atatumia kifaa hiki.
Kutumia vifaa vya matibabu vyenye uambukizo wa VVU
Hii huwapata zaidi watumishi wa sekta ya afya, hawa wanapojichoma
na sindano au kujikata kwa mikasi iliyotumiwa kumhudumia mgonjwa
mwenye maambukizi ya VVU.
V