3. Utangulizi
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
3
Maradhi ya zinaa ni magonjwa ya
maambukizi zaidi ya 25 ambayo kimsingi
husambazwa kutoka mtu mmoja hadi
mwingine kwa kujamiiana.
Maradhi ya zinaa ni namna ya kutaja
magonjwa yanayosambazwa kwa njia ya
vitendo vya kijinsia.
4. 3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
4
Magonjwa ya zinaa ni miongoni mwa
maambukizi yanayofahamika sana na
yaliyoleta madhara makubwa hasa katika
nchi zinazoendelea ambazo nyingi ziko
barani Afrika.
Maradhi hayo yanaweza yakaambukizwa
kwa njia nyingine pia.
6. Klamidia
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
6
Klamidia ni ugonjwa wa
kuambukiza ambao husababishwa
na bakteria wanaoitwa
kisayansi kama Chlamydia trachomatis.
Ugonjwa huo huwa hauonyeshi dalili za
wazi kwa karibia asilimia 75
ya wanawake na asilimia 50 ya wanaume,
hivyo maambukizi mengi hushindwa
kufahamika mapema.
7. Klamidia...
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
7
Watu ambao hawajafahamu kuwa
wameambukizwa klamidia wanaweza
wasitafute tiba na hivyo wakaendelea
kufanya ngono, bila ya kujua kuwa
wanaeneza ugonjwa.
8. Wakati dalili zinapoanza
kujitokeza
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
8
Wanawake wanaweza kutokwa damu nje
ya kipindi chao, maumivu wakati wa
kukojoa, kutokwa usaha katika uke, au
maumivu chini ya kitovu.
Wanaume husikia maumivu wakati wa
kukojoa au kutokwa usaha katika uume.
10. Kisonono
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
10
Kisonono au Kisalisali ni maradhi ya zinaa
ambayo husababishwa na bakteria
wanaofahamika kisayansi kama Neisseria
gonorrhoeae.
Bakteria hao hushambulia utandotelezi
unaozunguka sehemu za siri.
11. Kisonono...
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
11
Kisonono huonekana kwa urahisi kwa
wanaume ambao hutoa usaha kutoka
katika mfereji wa mkojo (urethra).
Huanza kidogo, lakini huongezeka na
huwa mwingi na kusababisha kusikia haja
ya kukojoa mara kwa mara huku kukiwa
na maumivu.
12. Kisonono...
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
12
Kisonono isiyotibiwa inaweza kusababisha
magonjwa ya uvimbe kwenye via vya
uzazi (Pelvic Infiammatory disease) kwa
wanawake.
Watoto wanaozaliwa na mama wenye
kisonono huwa na hatari ya kuambukizwa
wakati wa kuzaliwa.
Maambukizo haya yanaweza kusababisha
magonjwa ya meno kwa watoto
wachanga.
13. Kisonono...
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
13
Kisonono kikisambaa na kufikia tezi
kibofu, mfereji wa mkojo huziba kwa kiasi
fulani.
Kwa wanawake maambukizi hutokea
katika urethra, uke au mlango wa
uzazi (cervix).
15. Kaswende
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
15
Kaswende ni gonjwa tishio
linalosababishwa
na bakteria wanaofahamika
kama Treponema pallidum.
Katika hatua za mwanzo, vipele katika
sehemu za uzazi huanza kujitokeza muda
mfupi baada ya maambukizi ambavyo
baadaye hupotea vyenyewe.
16. Kaswende...
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
16
Kama ugonjwa hautatibiwa, maambukizi
huendelea kwa miaka, yakishambulia
mifupa, ubongo na moyo na kusababisha
madhara mengine yanayotokana na
matatizo katika mfumo wa fahamu kama
vile:
homa ya uti wa mgongo
magonjwa ya moyo na
kiharusi.
17. Kaswende...
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
17
Kaswende wakati wa ujauzito unaweza
kuwa hatari kubwa kwa kiumbe tumboni,
kama vile kusababisha kutoumbika vizuri
(deformity) na kifo.
19. Malengelenge sehemu za siri
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
19
Ugonjwa wa malengelenge katika sehemu
za siri husababishwa na maambukizi
ya herpes simplex virus(HSV).
20. Dutu za Sehemu za Siri
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
20
Dutu huota katika uume na katika eneo la
kuzunguka uke na mkunduni.
Husababishwa na kundi
la virusi lifahamikalo kama human
papillomavirus (HPV) ambao husambazwa
wakati wa kujamiiana.
Dutu za sehemu za siri zinaweza kutibiwa
na kuondolewa kwa upasuaji mdogo.
21. Trikomonasi
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
21
Trikomonasi husababishwa na
maambukizi ya protozoa anayefahamika
kisayansi kama Trichomonas vaginalis.
Ugonjwa huu husababisha muwasho na
karaha katika uke kwa wanawake na
katika mfereji wa mkojo kwa wanaume.
22. Dalili za kawaida za ugonjwa wa
zinaa
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
22
Kuhisi maumivu au kuungua wakati wa
kukojoa.
Kuwashwa, kutokwa na uchafu au harufu
isiyokuwa ya kawaida ukeni, kwenye uume
au njia ya haja kubwa.
Kwa wanawake hupata maumivu makali
chini ya tumbo (kinena).
Kuwa na uvimbe, vidonda au vipele mara
nyingi kuzunguka sehemu za siri au eneo
la njia ya haja kubwa.
23. Kuzuia na kudhibiti
maambukizi
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
23
Hatua rahisi zinaweza kutumika kuzuia
maambukizi ya magonjwa ya zinaa.
Hatua ambayo ni madhubuti kuliko zote ni
kuepuka ngono kabisa.
Bila ya kukutana kimwili hakuna
uwezekano wa kupata maambukizi
ya zinaa.
24. Kuzuia na kudhibiti
maambukizi
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
24
Kuwa na mwenzi mmoja tu katika ndoa na
kwa wale wanaojiingiza katika mahusiano
pia husaidia kupunguza hatari ya
maambukizi.
Kondomu inakinga dhidi ya maambukizi
hayo lakini si kinga kamili kwa asilimia mia
moja.
25. Kuzuia na kudhibiti
maambukizi
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
25
Kondomu huwa haifuniki sehemu yote ya
siri ambayo hukutana wakati wa kufanya
ngono, na uwezekano wa kupata
maambukizi ya zinaa bado upo,
hasa malengelenge na dutu.
Matibabu yote lazima yafuatwe hata kama
matumizi ya awali ya dawa yalipelekea
dalili zote kutoweka
27. UKIMWI...
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
27
Upungufu wa Kinga Mwilini (kwa kifupi
UKIMWI; ni ugonjwa unaotokana na virusi
ambavyo hushambulia kinga mwili kwa
kuondoa nguvu zake za kupambana na
maradhi.
UKIMWI ni ugonjwa wa zinaa hatari na
usiotibika ambao hushambulia mfumo wa
kinga ya mwili na kumwacha mgonjwa akiwa
hana hata uwezo wa kujikinga dhidi ya
28. UKIMWI...
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
28
Maambukizi ya VVU haimaanishi kuwa
mtu ana UKIMWI.
Baadhi ya watu wanaweza kuwa na
maambukizi ya VVU na wasionyeshe hali
ya kuumwa ile inayotambulika kama
UKIMWI kwa miaka kumi au zaidi.
29. UKIMWI...
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
29
Ugonjwa huu pia unasababisha madhara
ya kiuchumi ambayo ni makubwa, hasa
kwa nchi maskini.
UKIMWI hadi hivi sasa
haina chanjo wala tiba.
30. Uambukizaji
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
30
VVU husambaa hasa kupitia njia tatu kuu:
Ngono (ikiwa ni pamoja na ulawiti na
hata ngono ya mdomoni),
Kuingiliana na viowevu vya mwili
vilivyoambukizwa (hasa kuongezewa
damu au kudungwa sindano) na
Kutoka kwa mama hadi mtoto wakati wa
ujauzito, kuzaa au kunyonyesha.
31. Uhusiano Kati ya VVU na
Magonjwa Mengine Ya Zinaa
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
31
Uambukizo wa ugonjwa wowote wa zinaa
unamfanya mtu awe kwenye hatari zaidi ya
kupata VVU.
Maambukizo ya ugonjwa unaotokana na
ngono huweza kusababisha kuchanika kwa
ngozi, vidonda, au michubuko kwenye
sehemu za mwili ambazo ziko kwenye hatari
ya kupata uambukizo wa VVU kama Uke, na
kufanya iwe rahisi zaidi kwa virusi kuingia
kwenye mishipa ya damu.
32. 3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
32
Tabia hatarishi ambayo inaweza
kusababishia kuambukizwa ugonjwa
mmoja pia huongeza uwezekano wa
kuambukizwa magonjwa mengine.
Mwenzi mwenye ugonjwa mmoja wa
zinaa huweza kuwa na magonjwa
mengine.
33. Jinsi ya kujikinga au kuzuia
maambukizi ya virusi vya
UKIMWI
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
33
Hakikisha unatumia zana pindi
unapofanya ngono.
Nenda kapime na upate tiba ya magonjwa
mengine ya zinaa.
Pima na kujijua mapema, kunasaidia
kulinda afya yako na kuzuia
kuwaambukiza wengine
34. Jinsi ya kujikinga…
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
34
Hakikisha damu unayowekewa imepimwa
na haina virusi vya ukimwi
Kutahiriwa kwa wanamume kunasaidia
kupunguza maambukizi.
35. Jinsi ya kujikinga…
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
35
Matumizi ya mapema na yaliyo bora ya
dawa za kufubama makali ya virusi vya
ukimwi (ARV) husaidia kukufanya uishi na
afya bora pia kupunguza maambukizi kwa
wengine.
Kuishi maisha yanayompendeza mungu
kwa kuacha kuzini kabla na nje ya ndoa
37. 1. Kliniki za afya za umma
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
37
Kliniki za magonjwa yanayoambukizwa
kwa njia ya ngono zilizo chini ya udhamini
wa serikali hutoa huduma bure kwa vijana
na hutoa pia huduma bila kujali uwezo wa
mtu wa kulipa.
38. 3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
38
Wataalamu wa kliniki za magonjwa ya
zinaa ni wenye ujuzi wa hali ya juu katika
kufanya vipimo, kufanya uchunguzi, na
kutibu magonjwa ya aina hii, na mazingira
ya matibabu huwa ni ya usiri zaidi kuliko
ya ofisi ya wahudumu wa kawaida.
39. 2. Kliniki za uzazi wa
mpango
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
39
Wataalam wengi wa uzazi wa mpango pia
hutoa ushauri nasaha kuhusu magonjwa
ya ngono na upimaji au rufaa.
Kama hawatoi huduma hizi watakuelekeza
wapi utakapozipata.
Wengi wao huduma zao huwa ni za
gharama nafuu na huduma hutolewa
kutokana na kipato cha mtu.
40. 3. Wataalam wa afya ya jamii
(madaktari).
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
40
Nenda kwa wahudumu wako wa afya wa
siku zote kama utajisikia huru kuongea
nao na kama wanatoa majibu mazuri
yanayoeleweka ya maswali yako.
Siyo wataalam wote wana vifaa vya
kufanyia vipimo vya ugonjwa wa zinaa kila
mara, na pia wanaweza kuwa
hawafahamu kwa undani zaidi kuhusu
haya magonjwa.
41. HITIMISHO
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
41
Magonjwa ya ngono ni magonjwa
yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiana
na mtu mwenye uambukizo.
UKIMWI ni hatua ya mwisho ya
kushambuliwa kwa kinga mwili ambapo mtu
huonesha dalili za ugonjwa.
42. HITIMISHO…
3/8/2019MAGONJWA YA NGONO NA UKIMWI
42
VVU ni vimelea vidogo visivyoonekana
kwa macho ambavyo hushambulia kinga
mwili.
Mtu mwenye magonjwa ya ngono yupo
kwenye hatari kubwa ya kupata
maambukizi ya VVU/UKIMWI.