Broszura porusza tematykę zdrowia i higieny kobiet i jest skierowana do młodych dziewcząt w wieku 14-18 lat. Broszura została przygotowana w ramach projektu: "Poprawa w dostępie do opieki zdrowotnej w mieście i dystrykcie Mwanga".
2. MTAYARISHAJI WA MAANDISHI: Monika Nowicka
MSANIFU WA JALADA NA DIZAINI: Patrycja Zandberg
Picha kwenye jalada: Monika Nowicka, mjamzito kituo cha afrya Bugisi, Patrycja Zandberg,
mwanamke kutoka Sega, Simba Friends Foundation - mwanafunzi wa Shule ya Msingi Sega.
”Cultures of the World” Foundation
Poland, 2014
Uchapishaji huu unaonesha maoni ya mtunzi na hauwezi kuainishwa na msimamo rasmi wa
Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Poland.
The „Kuwa msichana, mwanamke, mke...” is available under the Creative Commons Attribution
3.0 Poland. Some rights reserved to „Cultures of the World” Foundation. This piece was created
as part of the Polish development cooperation implemented through the Ministry of Foreign
Affairs in 2014. Use of the piece is permitted only if the abovementioned information is kept,
including information about the license, the rights holders and the Polish development coope-ration
programme.
3. 3
"Utajiri wa kweli ni uzima, na wala
sio vipande vya dhahabu au shaba."
Mahatma Ghandhi
4. 1. Afya ni nini?1
Kwa mujibu wa ufafanuzi uliotolewa na kutangazwa na Shirika la Afya Du-niani
1 Makala: „Neno ‚Afya’ linamaanisha nini?”, imepakuliwa kutoka: http://kona-ya-afya.blogspot.
com/
4
WHO, katika mkutano wake wa tarehe 19-22 Juni 1946 na kusainiwa
na wawakilishi wa nchi 61 duniani, afya ni hali ya mtu kuwa vizuri kimwili,
kiakili na kijamii na sio tu kutokuwa na ugonjwa au udhaifu.Ufafanuzi huo
ulianza kutumika Aprili mwaka 1948 na hadi hii leo maana hiyo ya afya ha-ijabadilika.
Ufafanuzi huo unamaanisha kwamba, tunaposema mtu ana afya
sio tu tunakusudia kuwa mwili wake hauna maradhi, upungufu au udhaifu
bali pia mtu huyo anatakiwa asiwe na matatizo ya kimwili, kiakili na hata
kijamii. Kwa mujibu wa tafsri hiyo pana ya neno ‚afya’ tunaona kuwa watu
wengi wanaamini kuwa afya imegawanyika katika makundi mawili muhimu
ambayo ni afya ya kimwili na afya ya kiakili.
Afya ya mwili kwa binadamu ina maana kuwa na mwili wenye afya usiokuwa
na maradhi; afya ambayo kwa kawaida hutokana na kuupa mwili mazoezi ya
mara kwa mara, lishe bora na mapumziko ya kutosha. Katika nchi au maeneo
ambayo watu wanapata lishe bora, huduma nzuri za afya na kuishi katika
hali ya kimaisha inayoambatana na viwango vinavyotakiwa, kwa kawaida
vimo na uzito wao huongezeka. Ukweli ni kuwa, ukiwauliza watu wengi afya
ni nini, watasema kwamba inahusiana na mwili kuwa salama bila ya kuathi-rika
na ugonjwa. Lakini tukienda ndani zaidi, kitiba, afya ya mwili inaama-nisha
ustawi wa mwili hali ambayo mtu anaipata kwa kutekeleza vipengele
vyote vinavyohusiana na afya katika maisha yake. Uzima wa mwili unaakisi
kufanya kazi vizuri kwa moyo na mfumo wa kupumua, uwezo wa misuli,
viungo pamoja na mwili kuweza kukubali mabadiliko tofauti na muundo wa
mwili kwa ujumla. Masuala mengine ni pamoja na lishe bora, uzito wa mwili,
kutokuwepo uraibu wa madawa ya kulevya, pombe, mahusiano salama ya
kimwili, usafi kwa ujumla na pia kulala na kuamka kwa wakati unaotakiwa.
Afya ya akili au uzima wa kiakili ni utambuzi wa mtu na uzima wake kisa-ikolojia.
Mtu ambaye ana afya nzuri ya kiakili hana matatizo ya kiakili au
kichaa. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO‚ „afya ya akili ni pale
mtu anapoweza kufahamu uwezo wake na kustahamili mfadhaiko (stress)
unaotokana na dhiki au matatizo ya kawaida ya kimaisha.
6. 2. Hedhi2
Mabadiliko ya mwili
Kila msichana katika maisha yake anabadilika ili awe mwanamke. Mabadi-liko
6
haya yanachukua muda wa miaka. Mabadiliko haya yanakoma wakati
damu inaanza kutoka kila mwezi. Tangu wakati huo mwanamke huyu ana-weza
kupata mimba na kuzaa mtoto. Damu ya kila mwezi mwanzoni sio kwa
kawaida. Baada ya miaka mitatu au minne damu ya kila mwezi inapashwa
kuwa sawa kila mwezi.
2 Chapisho: Maneno machache kuhusu hedhi, Cultures of the World Foundation, 2014.
7. Mzunguko wa mwanamke
Kila mwanamke ana mzunguko wake wa mwezi, kwa kawaida ni siku 28-30
lakini kuna mwezi mfupi wa siku 21 na mwezi mrefu wa siku hadi 35, na hiyo
ni sawa. Kama damu inaonekana tofauti tofauti huyu mwanamke inambidi
kumwona mganga.
Mzunguko wako wa mwezi unaanza siku ya kwanza damu inapoonekana.
Na unaweza kudumu siku 3 hadi 8. Wakati huu ni muhimu utunze usafi wa
mwili. Chochote unachotumia siku za hedhi hakikisha kwamba ni safi.
Damu inapoanza kutoka unaweza kusikia maumivu tumboni - ni jambo
la kawaida. Kama uchungu unazidi unaweza kumeza vidonge vya kutuliza
maumivu.
Katika kila mwezi mwanamke anaweza kupata mimba akishirikiana na mwa-naume
kuanzia siku 1-2 baada ya siku za damu. Unaonekana mwenye ru-tuba
mpaka siku chache. Siku hizi ni muda ya kutoa kijiyai. Mambo haya
yanatofautiana na kila mwanamke.
Upige hesabu
Kila mwanamke ana mwezi wake na ni lazima ajichunguze mwenyewe. Kati-ka
kila mfano unaweza kupata makosa au tofauti kwa sababu mwili hauon-gozwi
7
na komputa au mashine bali kwa umbile lake.
Mfano: Ikiwa mwezi wako ni siku 31, damu imeonekana tarehe 7 mwezi wa
tatu (Machi) na inakomea tarehe 13. Una uwezekano mkubwa wa kubeba
mimba baada ya siku 2 maana yake kuanzia tarehe 15 na inadumu kwa
muda wa siku 10 hadi tarehe 24. Baada ya tarehe 24 inakuja wakati bila
uwezo wa kupata mimba. Wakati huu unadumu mpaka siku ya kwanza ya
damu: mfano tarehe 6 mwezi wa nne. Wakati damu inatoka haipendezi
kushirikiana na mwanaume kwa sababu uke wako upo wazi.
Namna ya kuweka alama - Kila siku ya damu weka alama X katika kalenda
ya chini. Itakuonyesha mwezi wako na itakusaidia
kufahamu mwili wako. Mambo haya yanaweza kuonekana ni magumu lakini
ukianza kujaza katika kalenda utatambua na utajifunza kuhusu mzunguko
wa mwezi wako.
10. 4. Msingi wa ndoa ni upendo4
Binadamu wanaoishi katika hali ya kutooa huitwa waseja. Waseja ni watu
wasio na ndoa wala kufanya tendo la ndoa. Kazi yao ni kuonesha upendo
kamili kwa njia zote isipokuwa kufanya tendo la ndoa. Tena wanajizuia na
hali zinazoweza kuwafikisha katika tendo la ndoa, kwa sababu wanaona kazi
yao kuu ni kujifunza na kuonyesha upendo kamili kwa njia zote nyingine.
Kufanya tendo la ndoa kabla ya kufunga ndoa, je?
Kuna njia nyingi za kumwonesha upendo mwenzake. Kufanya tendo la ndoa
ni njia moja tu kati ya hizo, na hii ni haki kwa wenye ndoa tu. Kama mume
na mke wakiweza kuoneshana upendo kwa njia ya tendo la ndoa tu, maana
yake kwa njia moja tu, maisha yao yataanza kuchosha. Upendo wao hauja-kamilika.
10
Hii inasababisha kutoridhika na tendo la ndoa, hakutawaridhisha
tena, upendo huu utakuwa wa kijuu juu. Wanadamu wamepata uwezo zaidi
kuelezana upendo. Wanadamu wamepata akili, roho, moyo n.k. Wanaweza
kudhihirisha upendo wao kwa njia ya akili , roho, moyo, n.k.
Mume na mkewe wanaokuja wanatakiwa kujifunza kuonyeshana upendo
kwa njia hizi kabla
ya kufunga ndoa.
Kuna hatari ya ku-katiza
upendo wao
katika tendo la
ndoa. Kufanya hili
kabla ya kufunga
ndoa itakuwa vi-gumu
baadaye ku-jifunza
njia nyin-gine
za kuonesha
upendo. Kwa hiyo
wajifunze njia zote
za upendo toka
mwanzo.
4 Uimarishaji wa familia – Sr Ursula Birgitta Schnell O.S.B. Benedictine Publication Ndanda
– Permiho – Tanzania, 2008
11. Swali jingine:
Je, tendo la ndoa ni baya kama unalazimika kungoja? Hapana.
Tendo la ndoa ni zuri, kwa hiyo unastahili kungoja hadi utakapopata mahali
pazuri sana pa kufanyia na penye maana sana, yaani ndoa.
Kuna tamaa nyingi kwa binadamu. Kwa mfano tamaa ya kula, ya kunywa,
ya kuvuta sigareti, ya kunywa pombe n.k Tamaa ya kufanya tendo la ndoa
(nyege) ni moja kati ya hizo. Wanyama wanafuata tamaa zao, lakini wa-nadamu
wamepata akili na njia ya kutawala tamaa zao. Mtu anayeweza
kujitawala maana yake anayeweza kutawala tamaa zake zote, ni kweli mtu
mzima. Msaada wa kutawala tamaa ni kujikatalia kwa mfano: mtu fulani
anhisi njaa, lakini hali sasa, atakula baadaye au anahisi kiu, lakini hanywi
sasa, atakunywa maji baadaye. Au anahisi nyege (au ashiki), lakini hafanyi
sasa atafanya baadaye anapofunga ndoa. Akifanya mazoezi haya ya kuji-katalia
au kujinyima katika jambo moja tu kila siku kwa wiki chache ataona
anaweza kujitawala katika jambo hili. Tena ataona wakati huo huo anaweza
pia kujitawala katika mambo mengi asiyofanyia mazoezi. Kwa hiyo kama mtu
fulani akipata shida ya kujitawala katika jambo la kufanya tendo la ndoa
anaweza kufunga chakula, halafu ataweza pia kujitawala katika jambo la
nyege (ashiki).
11
13. HADITHI
Peter na Maria hawakufunga ndoa. Peter hataki kufunga ndoa, lakini ana-jaribu
kumwomba Maria kufanya tendo la ndoa. Maria anakataa, anasema
“hapana”. Peter anajibu: „kila mmoja anafanya hii kabla ya ndoa, wewe
unaweza kufanya hii pia”. Maria anafikiri na anajibu: ”Hata, kwa kweli,
siyo kila mmoja anafanya hii”, na anakataa tena. Maria amejibu vizuri kwa
sababu kwa kukataa tendo la ndoa kabla ya ndoa anatoa nafasi kwa Peter
na kwa yeye mwenyewe kujifunza kwa bidii, kuonesha upendo kwa njia
nyingine nyingi kuliko kuonana. Ametoa nafasi ya kukua katika upendo wa
kweli na kuwa mtu mzima anayeweza kujitawala. Tena kwa njia hii ametoa
nafasi ya kupata maisha yenye furaha. Tumeona katika mambo haya kukataa
ni kuzuri, inaleta faida kubwa.
13
17. Kuna baadhi ya alama za mwili zinazokutahadharisha kwamba Ovulation iko
njiani, hivyo kuweza kukusaidia kupanga vyema muda wa kujamiiana kwa
ajili ya kupata mimba. Kama hutaki kupata mimba sasa unaweza kuangalia
alama hizi na utajua muda ya kuacha kujamiiana na mume wako.
Alama nyinginezo zinakufahamisha kwamba Ovulation imewadia au imesha-pita.
Ingawa alama hizo ziko nyingi na nitazungumzia baadhi ya hizo, lakini
usifikiri kwamba unatakiwa utumie zote, kwani kufanya hivyo kunaweza
kukuchanganya. Iwapo hutoona alama zozote za Ovulation au iwapo siku
zako za mwezi hazina mpangilio maalum, ni bora umuone daktari ambaye
atakusaidia zaidi.
Mabadiliko ya joto lako la Mwili
Tunaweza kusema kuwa joto lako la mwili au (Body Basal Temperature) ndio
alama maarufu inayotumiwa na wanawake wengi ili kufahamisha kwamba
Ovulation imewadia pale wanapotaka kubeba mimba. Hii ni kwa sababu joto
lako la mwili huongezeka kwa kiasi kidogo na huendelea kuongezeka baada
ya Ovulation. Ongezeko hilo la joto husababishwa na homoni ya progeste-rone,
ambayo huongezeka sana punde baada ya Ovulation. Kwa kujipima
joto lako la mwili na kuandika chati ya mabadiliko hayo unaweza kufahamu
ongezeko hilo la joto lako la mwili. Unahitaji kipimamoto kwa ajili ya kufa-nikisha
suala hilo. Vipo vipimajoto maalum kwa ajili hiyo lakini unaweza
kutumia kipimajoto cha kawaida pia. Hakikisha unapima joto la mwili wako
asubuhi baada ya kuamka na uhakikishe huna homa, hukukosa usingizi,
hukunywa pombe, si mgonjwa wala huna wasiwasi na fikra nyingi. Ni bora
ufanye hivyo kwa mizunguko kadhaa ya siku zako ili uweze kuijua vyema
chati ya mabadiliko ya joto la mwili kwa mujibu wa mzunguko wako wa
mwezi. Ingawa njia hii haiainishi moja kwa moja kuwa Ovulation imewadia,
lakini joto la mwili huongezeka kidogo kabla ya kipindi hicho na huongezeka
kwa kwa nyuzi 0.4 hadi 0.6 baada tu ya kumalizika Ovulation. Kuongezeka
joto kwa kiasi kikubwa baada ya Ovulation huendelea hadi siku utakayopa-ta
siku zako ambapo hupungua na mzunguko wako wa mwezi huanza tena.
Iwapo utakuwa umepata mimba, joto lako la mwili litaendelea hivyo hivyo
kuwa juu. Kwa kuwa mabadiliko ya joto hutokea wakati wa Ovulation iwapo
unajaribu kubeba mimba, kufuatilia mabadiliko hayo kwa muda usiopungua
miezi miwili ni jambo la dharura ili uweze kujua wakati wa Ovulation amba-po
una uwezekano mkubwa wa kubeba mimba.
17
18. Mabadiliko ya majimaji ya ukeni
Wakati Ovulation inakaribia majimaji ya ukeni hubadilika pia kwa kiasi na
hali. Ikiwa hakuna Ovulation majimaji ya ukeni huwa yanayonata au kama
kremu au hukosekana kabisa. Wakati Ovulation inakaribia majimaji ya ukeni
huongezeka na huwa katika hali ya majimaji na wakati mwingine huwa rangi
nyeupe kama ya yai bichi. Iwapo utapima kwa vidole vyako huvutika kwa
inchi au zaidi kati ya vidole vyako.
Ni bora nikumbushe hapa kwamba, kuna wakati unaweza kuwa na majimaji
ya ukeni yanayofanana na ya wakati wa Ovulation hali ya kuwa hauko
katika Ovulation. Hali hiyo ni ya kawaida kwa watu wenye PCOS. Kutumia
dawa za Clomid au Antihistamin huweza kufanya majimaji ya ukeni yakauke
na hivyo kuwa vigumu kutumia njia hii ili kujua ni zipi siku zenye uwezekano
mkubwa wa mimba. Njia hii huhesabiwa kuwa yenye itibari zaidi.
Mabadiliko ya Ukeni:
Kama ambavyo majimaji ya ukeni yanavyobadilika wakati wa Ovulation,
uke nao (cervix) hubadilika wakati wa kukaribia Ovulation. Wakati huo uke
husogea mbele, huwa laini na hufunguka zaidi.
Maumivu kidogo katika Matiti:
Baadhi ya wanawake wakati wanapokaribia Ovulation au baada ya hapo
matiti yao huwa na maumivu kidogo. Suala hili huhusiana na mabadiliko ya
homoni katika mwili ambazo hujitayarisha kwa ajili ya mimba. Hata hivyo
njia hii sio yenye kutegemewa sana kwani maumivu ya matiti huweza ku-sababishwa
18
na masuala mengine. Pia maumivu ya matiti hutokea kabla ya
hedhi au baada ya kutumia baadhi ya dawa za kusaidia uzazi.
- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
19. Alama nyinginezo
Baadhi ya wanawake huhisi maumivu kidogo ya tumbo ambayo baadhi
huyaita Middle Pain. Maumivu hayo kwa kawaida hutokea upande ule yai
linapotoka yaani upande wa Ovulation. Maumivu hayo hutokana na mwendo
wa yai wakati linapopenya kwenye mirija. Maumivu hayo si ya kuendelea
na wala si makubwa na huisha haraka. Hali hiyo huweza kutokea mara
kadhaa katika siku za Ovulation. Kuna baadhi ya alama kama vile baadhi
ya wanawake huhisi kichefuchefu, gesi, kukojoa mara kwa mara na maumi-vu
wakati wa kujamiiana, hali ambayo haitokei kwa watu wengi. Pia kuna
baadhi ya vifaa vinavyopatikana katika maduka ya dawa katika baadhi ya
nchi ambavyo huweza kukusaidia kujua wakati wako wa Ovuation umewadia,
vifaa hivyo hujulikana kama 'Ovulation Kit"
La muhimu ni kufahamu kuwa wanawake hutofautiana katika kupata ala-ma
hizi, kwani kuna baadhi wanaweza wakapata baadhi ya alama hizi na
wengineo wakapata nyinginezo. Kuuelewa vyema mwili wako ni jambo zuri
linaloweza kukusaidia kuzijua siku zako za Ovulation na hivyo kuweza kujua
siku zako za kubeba mimba.
Uangalifu!
19
20. 7. Usafi7
Kujitunza wakati wa hedhi
Kutokwa na damu kila mwezi ni ishara kwamba umekuwa mwanamke na
unaweza kupata mimba. Hakuna msichana anayejua kabisa muda wa ku-toa
20
damu mara ya kwanza. Kwa kawaida kabla ya kupata hedhi msichana
anaona matiti yake yanakuwa na mwili wake unabadilika. Miezi michache
kabla ya hedhi msichana anapata taarifa kwa kutokwa na majimaji kutoka
uke wake.
Mambo ya usafi
Tangu unapopata hedhi mara ya kwanza ni muhimu mno
kujua mambo ya usafi wako. Wenye pesa za kutosha
wananunua pedi au tampon (kisodo) dukani.
Wanawake wengi wanafanya pedi za nguo au pamba ili
kuzuia damu kutokana na kuchafua nguo. Vitu hivi vina-kaa,
vinavaliwa, katika nafasi kwa ukanda, siri, au chupi.
Ni lazima kubadilisha pedi mara chache kwa siku. Kama unataka kutumia
pedi tena uisafishe na sabuni vizuri ili isibaki na uchafu uchafu.
7 Chapisho: Maneno machache kuhusu usafi, Cultures of the World Foundation, 2014.
26. Bibliografia:
1. Makala: „Neno ‚Afya’ linamaanisha nini?”, imepakuliwa kutoka:
26
http://kona-ya-afya.blogspot.com/
2. Chapisho: Maneno machache kuhusu hedhi, Cultures of the World
Foundation, 2014.
3. „Where woman have no doctor”, A.A. Burns, R.Lovich, J.Maxwell,
K.Shapiro; Hesperian Foundation 2010, USA
4. Uimarishaji wa familia – Sr Ursula Birgitta Schnell O.S.B. Bene
dictine Publication Ndanda – Permiho – Tanzania, 2008
5. Kitabu cha afya kwa watu wazima na walimu – Sr Ursula Birgitta,
Schnell O.S.B. Benedictine Publication Ndanda-Permiho –
Tanzania 1998
28. Uboreshaji wa huduma za afya mjini na wilaya ya Mwanga.
Mradi huu - ulikamilishwa kwa hisani kubwa ya Wizara ya
Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Poland, mnamo mwaka 2014.
THE GRAIL SISTERS TANZANIA