SlideShare a Scribd company logo
1 of 40
Download to read offline
Mimba
MTAYARISHAJI WA MAANDISHI: Monika Nowicka
MSANIFU WA JALADA NA DIZAINI: Patrycja Zandberg
„Cultures of the World” Foundation
Poland, 2014
The Mimba is available under the Creative Commons Attribution 3.0 Poland. Some rights
reserved to „Cultures of the World” Foundation. This piece was created as part of the Polish
development cooperation implemented through the Ministry of Foreign Affairs in 2014. Use of
the piece is permitted only if the abovementioned information is kept, including information
about the license, the rights holders and the Polish development cooperation programme.
Uchapishaji huu unaonesha maoni ya mtunzi na hauwezi kuainishwa na msimamo rasmi wa
Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Poland.
3
1. Kuumba binadamu mpya1
Mimba huchukua muda wa miezi 9. Kila mwezi mama na mtoto wanabadilika
kimwili.
-------------------------------------------
-------------------------------------------
-------------------------------------------
----------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------

-----------------------------------------------------------------------

------------------------------------------
Mwezi wa kwanza
Mtoto bado ni mdogo lakini moyo, ini na tumbo lake
limeanza kuunda fomu. Viungo vidogo vitavyokuwa miguu
na mikono.
1
Kwa msingi wa: http://www.storknet.com/ip/reproductive_years/pregnancy/normal_course_pregnancy.
html, inapatikana: 16-18.06.2014
4
Mwezi wa pili
Viungo muhimu vinatengenezwa. Moyo wa mtoto
unavuta damu. Kichwa cha mtoto kinaanza kutokea
na macho yanaanza kuonekana. Miguu na mikono
pia inaanza kuonekana.
-----------------------------------------------

------------------------------------------------

Mwezi wa tatu
Mafigo yanaanza kutengeneza mkojo ambao mtoto
anauelekeza kwenye maji yake. Maji ya mtoto
yanasafirishwa kwa njia ya kitovu kupitia mama.
5
Mwezi wa nne
Viungo vyote vimeungwa tayari. Mtoto anahitaji
tu kukua. Fizi za meno zinaanza kutengenezwa.
Vinywele vidogodogo vinaanza kumea mwili nzima.
Kucha zinaanza kumea. Mtoto anaweza kunyonya
na kumeza.
Mtoto anaanza kupiga mateke na ngumi lakini bila
mama kuhisi.
------------------------------------------------
------------------------------------------------
------------------------------------------------
------------------------------------------------
------------------------------------------------
------------------------------------------------
------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
----------------------------------------------

Mwezi wa tano
Mtoto bado anakuwa na mama anaanza kusikia
mapigo ya mateke ya mtoto. Mtoto anaanza
kunyonya vidole na anapata nywele kichwani.
Mtoto anaweza kusikia sauti kidogo.
6
Mwezi wa sita
Mtoto anaanza kufungua macho. Mapafu yame-
kuwa tayari kupumua kidogo. Mifupa inakua.
---------------------------------------------
---------------------------------------------
---------------------------------------------
--------------------------------------------
---------------------------------------------
---------------------------------------------
--------------------------------------------
---------------------------------------------
---------------------------------------------
---------------------------------------------
---------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
------------------------------------------
------------------------------------------
------------------------------------------
------------------------------------------
------------------------------------------
Mwezi wa saba
Ubongo umeongezeka. Mtoto ameanza kuwa
mkubwa. Kuna nafasi ndogo zaidi kwenye
mzunguko wa mtoto. Mtoto anasikia vizuri
sauti za karibu.
Mwishoni mwa mwezi wa saba mtoto ana-
weza kuishi peke yake baada ya kuzaliwa
lakini atahitaji msaada kwa ajili ya kupatiwa
joto kama vile inkubeta.
7
Mwezi wa nane
Mapafu yapo tayari kabisa. Michezo ya
mtoto inaonekana tumboni mwa mama. Mtoto
mara kwa mara anapata kwikwi.
Mtoto wa mwezi wa nane akizaliwa anaweza
kuishi peke yake bila shida.

Mwezi wa tisa
Mwishoni mwa mwezi wa tisa mtoto ana-
onekana kama anapunguza michezo kwa
sababu maji yake yamepungua.
Nafasi ya kawaida kichwa cha mtoto kipo
chini, matako yapo juu. Kichwa kinaingia
katika nyonga ya mama na mtoto yupo
tayari kuzaliwa.
8
2.	 Kuhesabu miezi ya mimba:2
Ukienda kumwona mkunga zahanatini yeye anaweza kutumia mzunguko
kwa kupima umri wa mimba. Lakini wakunga wengi wanahesabu mimba kwa
kupima fandasi ya uterasi (tumbo):
Jinsi ya kupima urefu wa fandasi
(ya tumbo) kwa mbinu ya kutumia
vidole: mwanamke amelala chali.
Kila mstari unawakilisha upana
wa vidole viwili. Ikiwa sehemu ya
juu ya uterasi iko chini ya kitovu,
pima ni vidole vingapi vitakuwa
chini ya kitovu. Ikiwa sehemu ya
juu ya uterasi iko juu ya kitovu,
pima ni vidole vingapi vitakuwa
juu ya kitovu.
2
Kwa msingi wa: Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Ujauzito, Sehemu 1”,
ukurasa 104-105, imepakuliwa kutoka: www.open.edu, inapatikana: 22-24.06.2014.
9

----------------------------------------------------------------------

10
3.	 Dalili zinazoweza kuashiria ujauzito3
Kukosa kipindi cha hedhi (amenorea)
Kukosa kipindi cha hedhi mara nyingi huwa ndiyo dalili ya kwanza ambayo
wanawake hutambua wanapokuwa wajawazito. Ikiwa mwanamke amekosa
kipindi cha hedhi (amenorea) au alikoma kupata hedhi kwa miezi kadhaa,
hii ni ishara nzuri ya ushikaji mimba kwa wanawake ambao huwa na mzun-
guko wa hedhi wa kawaida.
Mabadiliko kwa matiti
Wanawake wajawazito wanaweza kuhisi
matiti kuwa laini, yaliyojaa,
yanayonywea, utanukaji na areola (tishu
nyeusi ya mviringo inayozunguka
chuchu) kuwa nyeusi.
Kichefuchefu na kutapika
Dalili hii inayotokea sana kwa wajawazito wengi. Huwa kali zaidi asu-
buhi na ndiyo sababu iliyopelekea hisia hii kuitwa maradhi ya asubuhi.
Lakini inaweza kutokea wakati wowote na inaweza kuchochewa na harufu
za upishi na za viungo vya upishi. Wanawake wengine wajawazito huhisi
kichefuchefu siku nzima. Visababishi vingine vya dalili hii vinaweza kuwa
maradhi au vimelea.Kutapika sana mara kwa mara ni dalili ya hatari kwa
sababu mwanamke huyo anaweza kupoteza uzani kwa haraka.
Kukojoa mara kwa mara
Wanawake wajawazito mara nyingi wanahitaji kukojoa mara kwa mara, hasa
katika miezi mitatu ya kwanza na mwezi mmoja au miwili ya mwisho wa
ujauzito. Visababishi vingine vya dalili hii vinaweza kuwa mfadhaiko, maam-
bukizi ya kibofu au kisukari (ugonjwa wa sukari kwenye damu).
3
Kwa msingi wa: Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Ujauzito, Sehemu 1”,
ukurasa 78-79, imepakuliwa kutoka: www.open.edu, inapatikana: 22-24.06.2014.
11
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
Uchovu
Mwanzoni mwa ujauzito wanawake wanaweza kujihisi wachovu na wenye
usingizi wakati wa mchana na kutaka kupumzika mara kwa mara kuliko
kawaida wanapofanya kazi zao. Visababishi vingine vinaweza kuwa anemia,
lishe duni, matatizo ya kihisia, au kazi nyingi za sulubu.
12
4.	 Utunzaji wa Kiafya4
Pombe na dawa za kulevya
Mama anayekunywa pombe na kutumia dawa za kulevya (kutumia tumba-
ku) huzidisha hatari ya kumzaa mtoto aliye na akili punguani, mlemavu, na
hata aliye na tabia yenye kasoro. Inajulikana kuwa watoto waliozaliwa na
wazazi ambao wamezoea kutumia dawa za kulevya huwa na matatizo kama
ya watu ambao walitumia dawa za kulevya zamani.
Ingawa wengine hudai eti kunywa pombe kidogo
hakuwezi kudhuru, mara nyingi wataalamu hupen-
dekeza akina mama wajawazito wasiinywe hata
kidogo. Wanapaswa pia kuepuka moshi wa sigara.
Chochote mama anachoweka
mwilini mwake humfikia mtoto
wake.
Dawa
Hakuna dawa zinazopaswa kutumiwa ila tu zile zi-
lizopendekezwa na daktari anayejua kuhusu mimba
hiyo na ambaye amechunguza athari zake. Vitamini
fulani pia zinaweza kudhuru. Kwa mfano, kiasi ki-
kubwa sana cha vitamini ya A chaweza kumlemaza
mtoto aliye tumboni.
Kuongeza uzito
Mwanamke mjamzito anapaswa kuepuka kupita kia-
si katika ulaji. Mtoto anayezaliwa akiwa na uzito
wa chini sana anakabiliwa na hatari ya kufa mara
40 zaidi kuliko yule aliyezaliwa akiwa na uzito wa
kawaida. Kwa upande mwingine, kula chakula cha
watu wawili hunenepesha tu. Ongezeko linalofaa la
uzito-ambalo huanza kuonekana katika mwezi wa
nne wa mimba na kuendelea-huonyesha kwamba
mama anakula chakula cha kutosheleza mahitaji yake yanayoongezeka.
4
Kwa msingi wa: Mashahidi wa Yehova, „Kufanya Mimba Yako Iwe Safama Zaidi”, imepakuliwa
kutoka: http://m.wol.jw.org/sw/wol/d/r13/lp-sw/102003005, inapatikana: 24.06.2014.
13
Usafi na mambo mengine
Kuoga kwenye karai na kutumia maji ya bomba kunaweza kufanywa kama
kawaida, lakini haifai kuingiza maji kwa nguvu kupitia sehemu ya siri.
Mwanamke mjamzito anapaswa kuepuka kumkaribia yeyote mwenye ugonj-
wa wa virusi, kama surua ya rubella. Zaidi ya hayo, ili kuzuia ugonjwa
unaoambukiza ubongo na uti wa mgongo hasa katika mtoto mchanga, ni
lazima awe mwangalifu asile nyama ambayo haijaiva vizuri wala kugusa
kinyesi cha paka. Ni muhimu kudumisha usafi wa kawaida kama kunawa
mikono na kuosha vyakula kabla havijapikwa. Mara nyingi kufanya ngono
hakuleti tatizo lolote, ila tu katika majuma ya mwisho-mwisho ya mimba au
kukiwa na mtiririko wa damu, maumivu tumboni, au ikiwa mimba ya awali
ilitoka.

14
Je, unafikiri hii husababiswha na nini?
Mtoto anapokuwa mkubwa, anabana
mapafu ya mama hivyo nafasi ya ku-
pumua hupunguka. Upumuaji unaweza
kuwa rahisi wakati mtoto anapoteremka
chini katika tumbo muda mfupi kabla ya
leba kuanza. Kama upungufu wa pumzi
unamfanya mjamzito kukosa utulivu, hii
ni dalili hatari, hasa kama ana dalili
nyingine za ugonjwa.
5.	 Dalili za hatari5
Anemia (upungufu wa damu)
Wakati mtu ana anemia, kawaida inamaanisha kwamba hajaweza kula
vyakula vilivyo na madini ya ayani ya kutosha. Madini ya ayani husaidia
seli za damu nyekundu kubeba oksijeni kutoka kwenye hewa tunayovuta
hadi sehemu zote za mwili.
		 Ishara na dalili za hatari
•	
Weupe - weupe ndani ya kope, kucha na fizi
•	
Kizunguzungu au kuzirai
•	
Udhaifu au kuchoka
•	
Mapgo kwenye mishipa ya damu yenye
mwendo wa kasi mkubwa (zaidi ya mapigo
100 kwa dakika)
•	
Ugumu wa kupumua (upungufu wa pumzi).
Kupumua kwa shida
Baadhi ya upungufu wa pumzi, hasa wakati
wa kipindi cha mwisho chaujauzito, ni wa kawaida. Wanawake wengi hupata
upungufu wa kiasi cha pumzi wakati wako na mimba ya miezi wa 8 au 9.
Upungufu wa pumzi pia
unaweza kusababishwa na:
Anemia
Matatizo ya moyo
Kifua kikuu
Pumu
Maambukizi ya mapafu
Damu kuganda katika mapafu
Aleji.
5
Kwa msingi wa: Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Ujauzito, Sehemu 1”,
ukurasa 95-99, imepakuliwa kutoka: www.open.edu, inapatikana: 22-24.06.2014.
15
Ugonjwa wa kisukari
Wakati mama ana ugonjwa wa kisukari, mwili wake hauwezi kutumia sukari
yote iliyo kwenye damu, hivyo sukari inakuwa juu sana na baadhi yake
inaweza kuonekana kwenye mkojo wake. Kama mama ana baadhi ya dalili
za hatari zifuatazo, anaweza kuwa na ugonjwa wa kisukari. Kina mama wa-
naougua ugonjwa wa kisukari kwa kawaida hawana ishara hizi zote. Lakini
iwapo mama akiwa na dalili zaidi, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kuwa
na ugonjwa wa kisukari.
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
16

•	 Alikuwa na ugonjwa wa kisukari katika ujauzito wa awali.
•	 Mmoja wa watoto waliozaliwa alikuwa mkubwa sana (zaidi ya kilo 4);
hii ni kwa sababu sukari nyingi katika damu ya mama humfanya mtoto-
kuongeza uzito kupita kiasi.
•	 Mmoja wa watoto wake alikuwa mgonjwa sana au alikufa wakati wa
kuzaliwa bila kujua sababu.
•	 Yeye ni mnene.
•	 Yeye hupatwa na kiu kila wakati.
•	 Yeye huwashwa mara kwa mara na ana harufu mbaya inayotoka kwenye
uke wake.
•	 Majeraha yake hupona polepole.
•	 Yeye hukojoa mara kwa mara zaidi kuliko wajawazito wengine
•	 Uterasi yake ni kubwa kuliko ya kawaida kutokana na ile miezi
aliyokuwa mjamzito.
17
6.	 Mkao wa mtoto6
Inaweza kuwa vigumu kujua mkao wa mtoto kabla ya miezi sita au saba ya
ujauzito, na si muhimu hadi majuma 36 (miezi minane) kwa sababu ni
kawaida mtoto kuzunguka hadi mwezi wa mwisho. Mara tu ujauzito
unapotimiza miezi sita au saba, itakuwa rahisi kuhisi mtoto na kujua mkao
wake kwenye uterasi.
Hisi fumbatio la mama kwa mikono yako kwa kila upande, ukisukuma
pole pole kwa kila mkono kwa zamu. Unapaswa uweze kuhisi mtoto akiwa
amelala wima - yaani kichwa chini. (b) Iwapo
mtoto amelala kingamo, unaweza kuhisi kichwa
na matako yake kwenye pande za mama.
Mwanamke akianza uchungu na mtoto bado
amelala kingamo haiwezekani kumzaa kama
kawaida. Ni lazima kwenda hospitalini kwa
haraka kabla mtoto hajapata shida.
Mtoto huyu lazima azaliwe
kwa upasuaji
6
Kwa msingi wa: Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Ujauzito, Sehemu 1”,
ukurasa 113-121, imepakuliwa kutoka: www.open.edu, inapatikana: 22-24.06.2014.
Wima: kichwa au matako chini Kingamo: kichwa na matako kwenye pande
b.
a.
18
Kufikia mwezi wa mwisho kabla ya kuzaliwa, watoto wengi huwa wamelala
kichwa kikielekea kwenye seviksi ya uterasi . Hali ya kichwa chini huitwa
mlalo wa kutanguliza kichwa, na iwapo sehemu ya fuu la kichwa iitwayo
veteksi itatangulia kwenye njia ya uzazi, huu ndio mlalo bora zaidi kwa
uzazi wa mtoto. Madaktari na wakunga huiita sehemu ya mtoto inayotangu-
lia kwenye seviksi ya uterasi kitangulizi.
Mkunga anafinya kwa uthabiti kwa vidole vyake juu ya mfupa wa kinena
ajue ikiwa anaweza kuhisi kichwa cha mtoto.
matako upande wa chini
-------------------------------------------
-------------------------------------------
-------------------------------------------
------------------------------------------
------------------------------------------
-------------------------------------------
------------------------------------------
-------------------------------------------
-------------------------------------------
---------------------------------------------
---------------------------------------------
kichwa upande wa chini
19
7.	 Kusikia mapigo ya moyo yakienda kasi7
Kufikia miezi miwili ya mwisho ya ujauzito, mkunga anaweza kusikia mapigo
ya moyo wa fetasi mara nyingi akiwa katika chumba kisicho na kelele kwa
kuweka sikio lake kwenye fumbatio la mama. Ni rahisi kusikia mapigo ya
moyo kwa stethoskopu au fetoskopu.
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
----------------------------------------------------------------------
7
Kwa msingi wa: Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Ujauzito, Sehemu 1”,
ukurasa 118-119, imepakuliwa kutoka: www.open.edu, inapatikana: 22-24.06.2014.
20
8.	 Maumivu na matatizo mengine8
Maumivu ya mgongo
Wanawake wengi wajawazito hukumbwa na maumivu ya mgongo. Uzani wa
mtoto, uterasi na kiowevu cha amnioni hubadili mkao wake na kuweka mka-
zo kwenye mifupa na misuli ya mwanamke huyo. Kusimama mahali pamoja
kwa muda mrefu, kuinama au kazi nyingi za sulubu, zinaweza kusababisha
maumivu ya mgongo. Aina nyingi za maumivu ya mgongo ni kawaida katika
ujauzito lakini pia zinaweza kusababishwa na maambukizi ya figo.
Mhimize mume, watoto, jamaa wengine au marafiki wa mwanamke huyu
kuusinga mgongo wake. Kitambaa chenye joto au chupa yenye maji moto
kwenye mgongo wake pia vinaweza kumtuliza. Pia jamaa zake wanaweza
kusaidia kwa kufanya baadhi ya kazi nzito kama vile kubeba watoto wado-
go, kufua, kulima, na kusaga nafaka. Chupi inayokaza, au mshipi unaovaliwa
kwenye nyonga, pamoja na kupumzika kitandani mara kwa mara kunaweza
kupunguza maumivu ya mgongo.
Kukakamaa kwa miguu
Miguu au nyayo za wanawake wengi wajawazito inaweza kukakamaa –
Haya ni maumivu makali ya ghafla na kukaza kwa misuli. Kukakamaa huku
hasa hutokea usiku au wanawake wanapojinyoosha na kuvuta vidole vyao
vya mguu. Ili kukomesha mikakamao, kunja wayo (kuelekea juu) na kisha
usugue mguu huo kwa upole ili kuusaidia utulie (usisugue kwa nguvu).
kunja vidole vya mguu kuelekea juu kisha sugua mguu huo
8
Kwa msingi wa: Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Ujauzito, Sehemu 1”,
ukurasa 127-131, imepakuliwa kutoka: www.open.edu, inapatikana: 22-24.06.2014.
21
Maumivu ya ghafla katika sehemu ya chini ya upande wa fumbatio.
Uterasi, katika nafasi yake, hushikiliwa kwa ligamenti kwa kila upande.
Ligamenti ni kiungo mithili ya kamba zinazoshikanisha uterasi kwenye
fumbatio la mama. Kusonga kwa ghafla kunaweza kusababisha maumivu
makali kwenye ligamenti hizi wakati mwingine. Hii si hatari. Maumivu haya
hukoma baada ya dakika chache. Kusugua kwa upole au kuweka kitambaa
chenye joto kwenye fumbatio kunaweza kusaidia.
Maumivu ya kichwa na kipandauso
Maumivu ya kichwa hutokea sana katika
ujauzito bali si hatari. Maumivu haya
ya kichwa yanaweza kuisha mwanamke
akipumzika na kutulia zaidi, akinywa
juisi au maji zaidi, au akisinga paji la
uso kwa upole. Ni SAWA kwa mwanamke
mjamzito kunywa tembe mbili za parace-
tamol na glasi ya maji mara moja baada
ya muda fulani. Hata hivyo, maumivu ya
kichwa mwishoni mwa ujauzito yanaweza
kuwa ishara ya hatari ya malaria au ya
priklampsia, hasa ikiwa pia kuna shinikizo la juu la damu, au kuvimba kwa
uso au mikono. Kama maumivu hayatulia baada ya vidonge vya paracetamol
mjamzito aende kumwona mganga au mkunga.
22
Edema
Kuvimba nyayo na vifundo vya miguu hutokea sana katika ujauzito, hasa
alasiri au katika hali ya anga yenye joto. Kuvimba huku hutokana na ede-
ma, ambayo ni ubakizaji wa viowevu kwenye tishu za mwili. Chini ya nguvu
za uzito, kiowevu kilichobakizwa huteremka mwilini na kujikusanya kwe-
nye nyayo. Mwanamke huyo aketi akiwa ameinua nyayo zake mara nyingi
iwezekanavyo ili kuwezesha viowevu hivi kufyonzeka na kurudi katika mfumo
wa mzunguko wa damu. Kuvimba kwa miguu si hatari, lakini uvimbe mkali
kwa mwanamke anapoamka asubuhi, au kuvimba kwa mikono na uso wakati
wowote, kunaweza kuwa ishara za priklampsia ambayo ni hali mbaya zaidi
(hata ya kuhatarisha maisha).
Mwanamke anaweza kupata nafuu kutokana na uvimbe kwenye miguu aki-
weka miguu yake juu kwa dakika chache angalau mara mbili au tatu kwa
siku, akiepuka kula vyakula vyenye chumvi nyingi, na akinywa maji au juisi
za matunda kwa wingi.
23
Kuhisi joto au kutokwa na jasho jingi
Kuhisi joto ni jambo linalotokea sana katika ujauzito, na maadamu hakuna
ishara nyingine za hatari (kama vile ishara za
maambukizi), mwanamke huyo asiwe na wasiwasi.
Anaweza kuvaa nguo zinazoweza kupitisha baridi,
kuoga mara kwa mara, kutumia pepeo la karatasi
au jani kubwa, na kunywa maji mengi na viowevu
vingine.
Ugumu wa kuamka na kulala
Ni vyema mwanamke mjamzito kutolala chali,
kwa sababu huenda ikawa vigumu kuamka tena,
na kwa kuwa mwanamke akiwa ameulalia mgongo
wake, uzito wa uterasi huifinya mishipa mikubwa
ya damu ambayo hurudisha damu kwenye moyo. Hii inaweza kupunguza
usambazaji wa oksijeni kwenye ubongo wake kwa muda na kumfanya ahisi
kizunguzungu. Ikiwa mwanamke anataka kuulalia mgongo wake, anafaa
kuweka kitu chini ya mgongo na chini ya magoti yake ili asilale chali
kikamilifu.
(a) Kuamka bila kugeuka upande mmoja kwanza kunaweza kurarua misuli
ya fumbatio.
(b) Kugeuka upande na kujisukuma juu kwa mikono ni salama sana na
atahisi utulivu.
LA!
Aoooh!
ujisukume juu
kwa mikono
geuka upande
simama
24
Chanjo dhidi ya tetanasi
Tetanasi ni maambukizi hatari sana yanayohatarisha maisha na huharibu
mfumo wa neva na husababishwa na bakteria katika mazingira, kwa mfano
udongoni. Chanjo ya tetanasi ndiyo kinga bora zaidi dhidi ya tetanasi kwa
mwanamke na mtoto wake. Kwa hivyo, ni muhimu sana kwake kuchanjwa
kulingana na ratiba iliyo kwenye kadi yake na kuleta kadi yake kila ana-
pokuja kwa uchunguzi wa ujauzito.
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
Sindano hizi zitaku-
kinga wewe na mtoto
dhidi ya tetenasi kwa
muda
Vizuri
25
9.	 Virusi vya Ukimwi VVU9
VVU (Virusi Vya Ukimwi) huharibu kingamwili na kusababisha kifo mtu
asipotibiwa ipasavyo na dawa za kupunguza makali ya VVU. Virusi hube-
bwa kwa damu ya mtu aliyeambukizwa na pia hupatikana katika njia ya
uzazi ya wanaume na wanawake walioambukizwa. Vinaweza kuambukizwa
kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa kufanya ngono bila kinga (ngono
bila kondomu) au uhamishaji wa damu iliyooambukizwa. Mama anaweza
pia kumwambukiza mtoto virusi wakati wa ujauzito, leba na kuzaa, na pia
unyonyeshaji.
Kwa hiyo ni lazima kwa kila mwanamke kupima VVU kabla na wa-
kati wa mimba na kabla ya kuzaa. Kuna taratibu maalum za kufuata ili
mtoto asiamukizwe na mama wakati wa kuzaliwa.
Dawa za kupunguza makali na kukinga maambukizi ya virusi vya VVU
kutoka kwa mama hadi kwa mtoto zinahusisha kumpatia mama dawa za
kurefusha maisha kuanzia wiki 28 za ujauzito, pia kwa mama wakati wa
leba na kuzaa, na kwa mtoto wake mara tu baada ya kuzaliwa. Dawa hizi
hupunguza hatari ya maambukizi ya VVU kwa mtoto. Ni tofauti na tiba
ya kupunguza makali ya virusi anayopewa mama ili kutibu maambukizi ya
VVU, kulingana na uhakiki wa vigezo vyake.
9
Kwa msingi wa: Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Ujauzito, Sehemu 2”,
ukurasa 44, imepakuliwa kutoka: www.open.edu, inapatikana: 27.06.2014.
26
10.	 Leba (kuzaa)10
Hakuna anayeweza kujua wakati leba itaanza. Hata hivyo, baadhi ya dalili
huashiria kwamba itaanza punde. Mara nyingi, watoto hushuka chini ya
fumbatio takriban wiki mbili kabla ya kuzaliwa, hali inayojulikana kama
kusahaulika. Kwa kawaida, mwanamke atahisi kuwa mtoto “haelei” kwenye
fumbatio, na hasukumi juu tum-
bo la mama. Ikiwa mwanamke
aliwahi kuzaa, huyu mtoto
huenda asishuke hadi wakati
wa kuanza kwa leba.
Dalili nyingine zinaweza kuan-
za siku moja au mbili tu kabla
ya kuanza kwa leba. Kinyesi
cha mama kinaweza kubadili-
ka ama kiasi kidogo cha damu
(damu iliyochanganyika na
utelezi) kinaweza kutoka
kwenye uke. Wakati mwingine,
mfuko wa maji hupasuka kabla
ya leba kuanza.
Kutambua leba halisi si jambo
rahisi kwa mama, hasa kama
mimba hii ni ya kwanza. Anaweza kukuita au kuja kwenye kituo cha afya
mara nyingi akifikiria kuwa maumivu madogo ni mwanzo wa leba halisi.
Leba imeainishwa katika awamu hizi nne.
•	 Awamu ya kwanza ya leba ni wakati seviksi hufunguka.
•	 Awamu ya pili ni wakati wa kusukuma, ambayo huisha mtoto
anapozaliwa.
•	 Awamu ya tatu ni kuzaliwa kwa kondo.
•	 Awamu ya nne ni masaa manne ya kwanza baada ya kuzaa.
10
Kwa msingi wa: Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Leba na Kuzaa”,
ukurasa 7-11 na 62, imepakuliwa kutoka: www.open.edu, inapatikana: 27.06.2014.
27
Awamu ya kwanza ya leba
Wakati wa awamu ya kwanza ya leba, seviksi hufunguka pole pole kiasi cha
kuwezesha mtoto kutoka kwenye uterasi. Kwa muda mrefu wakati wa uja-
uzito, hakuna chochote kinachoweza kuingilia au kutokea kwenye sevi-
ksi kwa sababu uwazi huo mdogo huwa umezibwa na utetelezi. Wakati wa
ujauzito, seviksi huwa ndefu na imara, kama kidole gumba cha mguu. Utera-
si ikikazana, seviksi hupanuka huku sehemu ya chini ya uterasi ikifupika.
Awamu fiche ni kipindi kati ya mwanzo
wa mikazo inayofuata utaratibu hadi
seviksi inapopanuka kwa kiasi
cha sentimita 4. Katika awamu
hii, mikazo inaweza kuwa chun-
gu au isiyo chungu, na seviksi
hupanuka pole pole. Awamu
fiche huisha wakati seviksi
inapoanza kupanuka kwa haraka
zaidi. Ongezeko hili la kasi
huashiria mwanzo wa awamu
wazi. Awamu wazi huanza wakati
seviksi imepanuka zaidi ya sentimita 4. Mikazo hii hutokea kwa utaratibu
maalum, mara nyingi na huwa chungu. Seviksi hupanuka haraka zaidi.
Seviksi huendelea kupanuka hadi kufika kipenyo cha sentimita 10, yaani
kupanuka kabisa. Seviksi iliyopanuka kabisa ni pana vya kutosha kupitishia
mtoto.
not effaced
no dilation
fully effaced
1 cm dilated
5 cm dilation fully dilated
at 10 cm
Ukubwa wa serviksi huwa kiasi hiki
wakati wa ujauzito
28
Awamu ya pili ya leba
Awamu ya pili ya leba huanza wakati seviksi imepanuka kabisa (sentimita
10) na kuisha mtoto anapozaliwa. Baada ya seviksi kupanuka kabisa, mama
kawaida hupata hisia za kutaka kusukuma. Mama akisukuma kulingana
na mikazo ya uterusi, mtoto huteremkia kwenye seviksi na kushukia ukeni.
Mwendo huu wa mtoto hujulikana kama kushuka kwa fetasi. Kiwango cha
kushuka kwa fetasi ni kiashirio muhimu cha jinsi leba inavyoendelea. Haba-
ri hii itaelezwa kwa kina hapo baadaye. Muda wa awamu ya pili ni wastani
wa saa 1 masaa 2.
Awamu ya tatu ya leba
Katika awamu ya tatu ya leba, plasenta na membreni hutoka baada ya
mtoto kuzaliwa. Kwa kawaida, awamu ya tatu huchukua hadi dakika 30.
Awamu ya nne ya leba
Saa 4 za kwanza punde baada ya plasenta kutoka huwa muhimu. Baadhi
ya wataalam wamekipa kipindi
hiki jina awamu ya nne ya
leba. Mwanamke anaweza
kuvuja damu kwa wingi baada
ya plasenta kutoka. Hii huto-
kea iwapo mikazo ya uterasi
inasababisha kutofungika kwa
mishipa ya damu iliyofunguka
kufuatia kubanduka kwa pla-
senta pembezoni mwa uterasi.
Kwa hivyo, inafaa uwe makini
ili kutambua na kudhibiti damu
inayovuja baada ya kuzaa.
Damu hii inaweza kuwa dhahiri au iliyofichika.
Ikiwa mama anavuja damu kwa wingi, anahitaji usaidizi wa dharura.
29
Hali ya kwanza na miendo saba kuu ya mtoto anaposhuka kwenye njia
ya uzazi. Picha hizi ndogo zinaonyesha hali ya kichwa cha mtoto, kana
kwamba unatazama kwenda juu ya njia ya uzazi.
30
Hii ndio hufanyika ndani ya mama: Hii ndio unaona nje:
1. Kwanza mtoto hupinda kichwa chake
chini, kidevu hadi kifua. Hali hii hufanya
kichwa kutoshea kwenye pelvisi kwa
urahisi.
2. Kichwa cha mtoto hufinywa na huba-
dilisha umbo lake kikitoka kwa pelvisi
ya mama. Mtoto hugeuza uso wake
kuelekea mgongo wa mama.
3. Mtoto huanza kuinua kidevu chake
kikikaribia ufunguaji wa uke. Hii huitwa
mkondo.
4. Mtoto huinua kidevu chake zaidi
wakati kichwa kinachomoka.
5. Mtoto huendelea kuinua kidevu
chake wakati kichwa kinatoka nje. Yaani
kichwa kinatolewa kwa utaratibu.
6. Mtoto huendelea kuinua kidevu chake
hadi kichwa kitolewe. Mara ya kwanza
uso wa mtoto bado unaangalia mgon-
go wa mama, ilhali mabega yake yako
katika hali fulani.
7. Hivi punde kichwa cha mtoto hugeuka
kuangalia miguu ya mama. Uso wa mtoto
sasa unapangwa na mabega yake.
31
Mkao wa mwendo wakati wa awamu ya kwanza na ya pili ya leba11
Kuna vipengele kadhaa vinavyoathiri uamuzi kuhusu mkao wa mama katika
awamu ya kwanza ya leba. Kati ya mikao yote, ulio muhimu zaidi ni hiari
ya mama - jinsi angependa kuzaa. Hata hivyo, baadhi ya wanawake huhi-
taji kuhimizwa kujaribu mikao tofauti. Msaidie mwanamke kujisogeza wakati
wa leba. Anaweza kuchuchumaa, kuketi, kupiga magoti au mikao mingineyo.
Mikao hii yote ni mizuri. Seviksi hufunguka kwa usawa zaidi mama anapo-
badili hali ya mkao.
11
Kwa msingi wa: Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Leba na Kuzaa”,
ukurasa 32 na 64, imepakuliwa kutoka: www.open.edu, inapatikana: 27.06.2014.
32
Kuketi nusu
Hali hii inaweza kuwa nzuri
zaidi na hurahishisha kazi
kwa mkunga kuelekeza utoaji
wa kichwa cha mtoto
Hali hii ni ya kupumzisha na
kusaidia kuzuia machozi kuingia
kwenye uke na msamba
Hali hii ni nzuri wakati mwa-
namke anahisi leba yake iko
nyuma ya mgongo. Pia inaweza
kusaidia wakati mabega ya
mtoto yamekwama
Hali hizi mbili zinaweza
kusaidia kuleta mtoto chini
wakati uzalishaji unaenda
polepole
Kukalia kifaa
Kulala upande
Kuchuchumaa
33
Mguso12
Leba inaweza kuwa ngumu zaidi iwapo mwanamke ana hofu au wasiwasi.
Ili kumsaidia kupunguza hofu, mthibitishie mwanamke huyu kuwa maumivu
aliyo nayo ni ya kawaida. Ingawa mguso unaweza kumsaidia mwanamke
aliye katika leba, fahamu aina ya mguso anayopendelea. Mifano ya miguso
inayopendelewa mara nyingi na wanawake ni kama:
•	 Kusukuma kwa uthabiti na utulivu kwenye sehemu ya chini ya mgongo-
wakati wa mikazo.
•	 Mpapase baina ya mikazo, hasa miguu na mgongo.
•	 Kijitambaa kilicho na joto au baridi kwenye sehemu ya chini ya mgongo
au tumbo. Iwapo mama anatokwa na jasho, kuweka kijitambaa chenye
ubaridi kwenye paji la uso humfanya kuhisi vyema.
Kupumua wakati wa leba13
Namna ya kupumua kwa mwanamke inaweza kuathiri sana jinsi leba ilivyo.
Katika awamu ya kwanza ya leba, mbinu mbali mbali za kupumua zina-
weza kurahisisha leba zaidi. Mjamzito achague mbinu inayomfaidi zaidi ili
kupunguza maumivu.
•	 Kupumua taratibu. Avute pumzi taratibu kwa
muda mrefu. Ili kutoa pumzi, atumie pua na mdomo kisha atoe pumzi
polepole. Kuvuta pumzi kupitia pua husaidia kupunguza kasi ya kupumua.
•	 Apumue kwa sauti ya ’juu’. Mwanamke huvuta pumzi nzito taratibu,
kisha hutoa pumzi fupi za haraka ili kutoa sauti laini ya „hiii, hiii”.
•	 Kuhema. Mwanamke huvuta pumzi nyepesi za haraka.
Kupuliza kwa nguvu. Mwanamke hupumua kwa nguvu na kasi.
12
Kwa msingi wa: Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Leba na Kuzaa”,
ukurasa 33, imepakuliwa kutoka: www.open.edu, inapatikana: 27.06.2014.
13
Kwa msingi wa: Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Leba na Kuzaa”,
ukurasa 33-34, imepakuliwa kutoka: www.open.edu, inapatikana: 28.06.2014.
34
Kutumia vinywaji
Mwanamke aliye katika leba hutumia nguvu nyingi na maji ya mwili kwa
haraka. Katika awamu ya kwanza ya leba, mwanamke anapaswa kunywa
angalau kikombe kimoja cha kinywaji kilicho na kiwango cha juu cha kalori
kila saa, kama vile chai, vinywaji visivyolevya, supu au maji ya matunda.
Mwanamke huyu asipokunywa vinywaji vya kutosha, anaweza kuishiwa na
maji (kukosa maji ya kutosha mwilini). Jambo hili linaweza kufanya leba
kuwa ndefu na ngumu zaidi na kumfanya kuhisi uchovu. Ukosefu wa maji
mwilini pia unaweza kumfanya mwanamke huyu kujihisi mchovu.
Kitanzi cha
kwanza cha fundo
mraba
Kitanzi cha pili
cha fundo mraba
Funga fundo mraba
Kukata kambakitovu14
14
Kwa msingi wa: Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Leba na Kuzaa”,
ukurasa 67-68, imepakuliwa kutoka: www.open.edu, inapatikana: 28.06.2014.
35
Kumnyonyesha mtoto baada ya kuzaa15
Anza kunyonyesha punde
tu mtoto atakapozaliwa
ili kupunguza kuvuja
damu baada ya kuzaa.
-----------------------
-----------------------
-----------------------
----------------------
-----------------------
-----------------------
----------------------
-----------------------
-----------------------
-----------------------
----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------
15
Kwa msingi wa: Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Leba na Kuzaa”,
ukurasa 145, imepakuliwa kutoka: www.open.edu, inapatikana: 28.06.2014.
36
usahihi
kimakosa
11.	 Baada ya kuzaa16
Watu wanaoishi pamoja na mama aliyjifungua wanapaswa kumsaidia katika
kazi za nyumbani. Mama anatakiwa kumpumzika baada ya leba na lengo
lake liwe mtoto tu kwa sasa. Akijisikia vizuri anaweza kuendelea na kazi
zake za nyumbani pamoja na kumtunza mtoto mchanga.
Kunyonyesha mtoto
Njia ya kushika matiti ni muhimu kwa sababu itakusaidia kumnyonyesha
mtoto au la.
16
Kwa msingi wa: Burns A.A., Lovich R., Maxwell J., Shapiro K., (2010), Where woman have no
doctor, (Berkeley: Hesperian Foundation)
37
38
Chemchemi:
·	 Ukunga, Sr. U.B. Schnell, Benedictine Publication, Tanzania 1993
·	 Uimarishaji wa familia, Sr. U.B. Schnell, Benedictine Publications,
	 Tanzania 2008
·	 Kitabu sha afya kwa watu wazima na waalimu, Sr. U.B. Schnell,
	 Benedictine Publication, Tanzania 1998
·	 Ukunga-mazoezi, M.Troszyński, PZWL, Poland 2009
Bibliografia:
· 	 Burns A.A., Lovich R., Maxwell J., Shapiro K., (2010), Where woman 	
	 have no doctor, (Berkeley: Hesperian Foundation).
· 	 Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Ujauzito,
	 Sehemu 1”, imepakuliwa kutoka: www.open.edu
· 	 Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Ujauzito,
	 Sehemu 2”, imepakuliwa kutoka: www.open.edu.
· 	 Health and Education Learning, (2011), „Utunzaji katika Leba na 	
	 Kuzaa”, imepakuliwa kutoka: www.open.edu.
· 	 Mashahidi wa Jehova, „Kufanya Mimba Yako Iwe Safama Zaidi”, 	
	 kutoka: http://m.wol.jw.org/sw/wol/d/r13/lp-sw/102003005,
· 	 Chapisho kutoka mtandao wa intaneti: http://www.storknet.com/ip/	
	reproductive_years/pregnancy/normal_course_pregnancy.html
Filamu:
· 	 10 Steps to a Clean Delivery https://www.youtube.com/watch?v=	
	gjXZvIehZfw&feature=share
· 	 Management of Primary Postpartum Haemorrhage (PPH) part1 	
	https://www.youtube.com/watch?v=xU7da4SO5Gs&list=UUJpt9KN	
	7frvqdszcQzECI7w
· 	 Management of Primary Postpartum Haemorrhage (PPH) part2
	https://www.youtube.com/watch?v=Vn14vQAIkKk&list=UUJpt9KN	
	7frvqdszcQzECI7w
· 	 HIV Prevention Tutorial
	https://www.youtube.com/watch?v=AZOEpUjIlgI
· 	 Je, mtoto wako ni mgonjwa? Muda mrefu filamu - Kuharisha, Ny	
	 umonia, Malaria
	https://www.youtube.com/watch?v=VWEBr_Ad1uo
· 	 Ujauzito Salama: Ushauri kwa Wanawake
	https://www.youtube.com/watch?v=OHrqHNwHtZ4
KUWA MAMA NI KAZI
Mradi huu - ulikamilishwa kwa hisani kubwa ya Wizara ya
Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Poland, mnamo mwaka 2014.
Uboreshaji wa huduma za afya mjini na wilaya ya Mwanga.
THE GRAIL SISTERS TANZANIA

More Related Content

More from Fundacja "Kultury Świata" (7)

Birmańskie opowieści
Birmańskie opowieściBirmańskie opowieści
Birmańskie opowieści
 
Plansze do kalendarza
Plansze do kalendarzaPlansze do kalendarza
Plansze do kalendarza
 
Kalendarz 2016
Kalendarz 2016Kalendarz 2016
Kalendarz 2016
 
Karty pracy
Karty pracy Karty pracy
Karty pracy
 
Broszura dla nauczycieli
Broszura dla nauczycieliBroszura dla nauczycieli
Broszura dla nauczycieli
 
Aspekty zdrowia reprodukcyjnego kobiet w różnych kontekstach kulturowych
Aspekty zdrowia reprodukcyjnego kobiet w różnych kontekstach kulturowychAspekty zdrowia reprodukcyjnego kobiet w różnych kontekstach kulturowych
Aspekty zdrowia reprodukcyjnego kobiet w różnych kontekstach kulturowych
 
Jak możemy pomagać chorym w Tanzanii
Jak możemy pomagać chorym w Tanzanii Jak możemy pomagać chorym w Tanzanii
Jak możemy pomagać chorym w Tanzanii
 
Broszura na seminaria dla kobiet cieżarnych (Tanzania)

  • 2. MTAYARISHAJI WA MAANDISHI: Monika Nowicka MSANIFU WA JALADA NA DIZAINI: Patrycja Zandberg „Cultures of the World” Foundation Poland, 2014 The Mimba is available under the Creative Commons Attribution 3.0 Poland. Some rights reserved to „Cultures of the World” Foundation. This piece was created as part of the Polish development cooperation implemented through the Ministry of Foreign Affairs in 2014. Use of the piece is permitted only if the abovementioned information is kept, including information about the license, the rights holders and the Polish development cooperation programme. Uchapishaji huu unaonesha maoni ya mtunzi na hauwezi kuainishwa na msimamo rasmi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Poland.
  • 3. 3 1. Kuumba binadamu mpya1 Mimba huchukua muda wa miezi 9. Kila mwezi mama na mtoto wanabadilika kimwili. ------------------------------------------- ------------------------------------------- ------------------------------------------- ---------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------- ---------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------- ---------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ------------------------------------------ Mwezi wa kwanza Mtoto bado ni mdogo lakini moyo, ini na tumbo lake limeanza kuunda fomu. Viungo vidogo vitavyokuwa miguu na mikono. 1 Kwa msingi wa: http://www.storknet.com/ip/reproductive_years/pregnancy/normal_course_pregnancy. html, inapatikana: 16-18.06.2014
  • 4. 4 Mwezi wa pili Viungo muhimu vinatengenezwa. Moyo wa mtoto unavuta damu. Kichwa cha mtoto kinaanza kutokea na macho yanaanza kuonekana. Miguu na mikono pia inaanza kuonekana. ----------------------------------------------- ----------------------------------------------- ----------------------------------------------- ----------------------------------------------- ----------------------------------------------- ----------------------------------------------- ----------------------------------------------- ----------------------------------------------- ----------------------------------------------- ----------------------------------------------- ------------------------------------------------ ------------------------------------------------ ------------------------------------------------ ------------------------------------------------ ------------------------------------------------ ----------------------------------------------- ------------------------------------------------ ------------------------------------------------ ----------------------------------------------- Mwezi wa tatu Mafigo yanaanza kutengeneza mkojo ambao mtoto anauelekeza kwenye maji yake. Maji ya mtoto yanasafirishwa kwa njia ya kitovu kupitia mama.
  • 5. 5 Mwezi wa nne Viungo vyote vimeungwa tayari. Mtoto anahitaji tu kukua. Fizi za meno zinaanza kutengenezwa. Vinywele vidogodogo vinaanza kumea mwili nzima. Kucha zinaanza kumea. Mtoto anaweza kunyonya na kumeza. Mtoto anaanza kupiga mateke na ngumi lakini bila mama kuhisi. ------------------------------------------------ ------------------------------------------------ ------------------------------------------------ ------------------------------------------------ ------------------------------------------------ ------------------------------------------------ ------------------------------------------------ ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ---------------------------------------------- ---------------------------------------------- ---------------------------------------------- ---------------------------------------------- ---------------------------------------------- ---------------------------------------------- ---------------------------------------------- Mwezi wa tano Mtoto bado anakuwa na mama anaanza kusikia mapigo ya mateke ya mtoto. Mtoto anaanza kunyonya vidole na anapata nywele kichwani. Mtoto anaweza kusikia sauti kidogo.
  • 6. 6 Mwezi wa sita Mtoto anaanza kufungua macho. Mapafu yame- kuwa tayari kupumua kidogo. Mifupa inakua. --------------------------------------------- --------------------------------------------- --------------------------------------------- -------------------------------------------- --------------------------------------------- --------------------------------------------- -------------------------------------------- --------------------------------------------- --------------------------------------------- --------------------------------------------- --------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ------------------------------------------ ------------------------------------------ ------------------------------------------ ------------------------------------------ ------------------------------------------ Mwezi wa saba Ubongo umeongezeka. Mtoto ameanza kuwa mkubwa. Kuna nafasi ndogo zaidi kwenye mzunguko wa mtoto. Mtoto anasikia vizuri sauti za karibu. Mwishoni mwa mwezi wa saba mtoto ana- weza kuishi peke yake baada ya kuzaliwa lakini atahitaji msaada kwa ajili ya kupatiwa joto kama vile inkubeta.
  • 7. 7 Mwezi wa nane Mapafu yapo tayari kabisa. Michezo ya mtoto inaonekana tumboni mwa mama. Mtoto mara kwa mara anapata kwikwi. Mtoto wa mwezi wa nane akizaliwa anaweza kuishi peke yake bila shida. ------------------------------------------ ------------------------------------------ ------------------------------------------ ------------------------------------------ ------------------------------------------ ------------------------------------------ ------------------------------------------ ------------------------------------------ ------------------------------------------ ------------------------------------------ ------------------------------------------ ------------------------------------------ ------------------------------------------ ------------------------------------------ ------------------------------------------ Mwezi wa tisa Mwishoni mwa mwezi wa tisa mtoto ana- onekana kama anapunguza michezo kwa sababu maji yake yamepungua. Nafasi ya kawaida kichwa cha mtoto kipo chini, matako yapo juu. Kichwa kinaingia katika nyonga ya mama na mtoto yupo tayari kuzaliwa.
  • 8. 8 2. Kuhesabu miezi ya mimba:2 Ukienda kumwona mkunga zahanatini yeye anaweza kutumia mzunguko kwa kupima umri wa mimba. Lakini wakunga wengi wanahesabu mimba kwa kupima fandasi ya uterasi (tumbo): Jinsi ya kupima urefu wa fandasi (ya tumbo) kwa mbinu ya kutumia vidole: mwanamke amelala chali. Kila mstari unawakilisha upana wa vidole viwili. Ikiwa sehemu ya juu ya uterasi iko chini ya kitovu, pima ni vidole vingapi vitakuwa chini ya kitovu. Ikiwa sehemu ya juu ya uterasi iko juu ya kitovu, pima ni vidole vingapi vitakuwa juu ya kitovu. 2 Kwa msingi wa: Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Ujauzito, Sehemu 1”, ukurasa 104-105, imepakuliwa kutoka: www.open.edu, inapatikana: 22-24.06.2014.
  • 9. 9 ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ---------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- -----------------------------------------------------------------------
  • 10. 10 3. Dalili zinazoweza kuashiria ujauzito3 Kukosa kipindi cha hedhi (amenorea) Kukosa kipindi cha hedhi mara nyingi huwa ndiyo dalili ya kwanza ambayo wanawake hutambua wanapokuwa wajawazito. Ikiwa mwanamke amekosa kipindi cha hedhi (amenorea) au alikoma kupata hedhi kwa miezi kadhaa, hii ni ishara nzuri ya ushikaji mimba kwa wanawake ambao huwa na mzun- guko wa hedhi wa kawaida. Mabadiliko kwa matiti Wanawake wajawazito wanaweza kuhisi matiti kuwa laini, yaliyojaa, yanayonywea, utanukaji na areola (tishu nyeusi ya mviringo inayozunguka chuchu) kuwa nyeusi. Kichefuchefu na kutapika Dalili hii inayotokea sana kwa wajawazito wengi. Huwa kali zaidi asu- buhi na ndiyo sababu iliyopelekea hisia hii kuitwa maradhi ya asubuhi. Lakini inaweza kutokea wakati wowote na inaweza kuchochewa na harufu za upishi na za viungo vya upishi. Wanawake wengine wajawazito huhisi kichefuchefu siku nzima. Visababishi vingine vya dalili hii vinaweza kuwa maradhi au vimelea.Kutapika sana mara kwa mara ni dalili ya hatari kwa sababu mwanamke huyo anaweza kupoteza uzani kwa haraka. Kukojoa mara kwa mara Wanawake wajawazito mara nyingi wanahitaji kukojoa mara kwa mara, hasa katika miezi mitatu ya kwanza na mwezi mmoja au miwili ya mwisho wa ujauzito. Visababishi vingine vya dalili hii vinaweza kuwa mfadhaiko, maam- bukizi ya kibofu au kisukari (ugonjwa wa sukari kwenye damu). 3 Kwa msingi wa: Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Ujauzito, Sehemu 1”, ukurasa 78-79, imepakuliwa kutoka: www.open.edu, inapatikana: 22-24.06.2014.
  • 11. 11 ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ---------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- Uchovu Mwanzoni mwa ujauzito wanawake wanaweza kujihisi wachovu na wenye usingizi wakati wa mchana na kutaka kupumzika mara kwa mara kuliko kawaida wanapofanya kazi zao. Visababishi vingine vinaweza kuwa anemia, lishe duni, matatizo ya kihisia, au kazi nyingi za sulubu.
  • 12. 12 4. Utunzaji wa Kiafya4 Pombe na dawa za kulevya Mama anayekunywa pombe na kutumia dawa za kulevya (kutumia tumba- ku) huzidisha hatari ya kumzaa mtoto aliye na akili punguani, mlemavu, na hata aliye na tabia yenye kasoro. Inajulikana kuwa watoto waliozaliwa na wazazi ambao wamezoea kutumia dawa za kulevya huwa na matatizo kama ya watu ambao walitumia dawa za kulevya zamani. Ingawa wengine hudai eti kunywa pombe kidogo hakuwezi kudhuru, mara nyingi wataalamu hupen- dekeza akina mama wajawazito wasiinywe hata kidogo. Wanapaswa pia kuepuka moshi wa sigara. Chochote mama anachoweka mwilini mwake humfikia mtoto wake. Dawa Hakuna dawa zinazopaswa kutumiwa ila tu zile zi- lizopendekezwa na daktari anayejua kuhusu mimba hiyo na ambaye amechunguza athari zake. Vitamini fulani pia zinaweza kudhuru. Kwa mfano, kiasi ki- kubwa sana cha vitamini ya A chaweza kumlemaza mtoto aliye tumboni. Kuongeza uzito Mwanamke mjamzito anapaswa kuepuka kupita kia- si katika ulaji. Mtoto anayezaliwa akiwa na uzito wa chini sana anakabiliwa na hatari ya kufa mara 40 zaidi kuliko yule aliyezaliwa akiwa na uzito wa kawaida. Kwa upande mwingine, kula chakula cha watu wawili hunenepesha tu. Ongezeko linalofaa la uzito-ambalo huanza kuonekana katika mwezi wa nne wa mimba na kuendelea-huonyesha kwamba mama anakula chakula cha kutosheleza mahitaji yake yanayoongezeka. 4 Kwa msingi wa: Mashahidi wa Yehova, „Kufanya Mimba Yako Iwe Safama Zaidi”, imepakuliwa kutoka: http://m.wol.jw.org/sw/wol/d/r13/lp-sw/102003005, inapatikana: 24.06.2014.
  • 13. 13 Usafi na mambo mengine Kuoga kwenye karai na kutumia maji ya bomba kunaweza kufanywa kama kawaida, lakini haifai kuingiza maji kwa nguvu kupitia sehemu ya siri. Mwanamke mjamzito anapaswa kuepuka kumkaribia yeyote mwenye ugonj- wa wa virusi, kama surua ya rubella. Zaidi ya hayo, ili kuzuia ugonjwa unaoambukiza ubongo na uti wa mgongo hasa katika mtoto mchanga, ni lazima awe mwangalifu asile nyama ambayo haijaiva vizuri wala kugusa kinyesi cha paka. Ni muhimu kudumisha usafi wa kawaida kama kunawa mikono na kuosha vyakula kabla havijapikwa. Mara nyingi kufanya ngono hakuleti tatizo lolote, ila tu katika majuma ya mwisho-mwisho ya mimba au kukiwa na mtiririko wa damu, maumivu tumboni, au ikiwa mimba ya awali ilitoka. ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ---------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- -----------------------------------------------------------------------
  • 14. 14 Je, unafikiri hii husababiswha na nini? Mtoto anapokuwa mkubwa, anabana mapafu ya mama hivyo nafasi ya ku- pumua hupunguka. Upumuaji unaweza kuwa rahisi wakati mtoto anapoteremka chini katika tumbo muda mfupi kabla ya leba kuanza. Kama upungufu wa pumzi unamfanya mjamzito kukosa utulivu, hii ni dalili hatari, hasa kama ana dalili nyingine za ugonjwa. 5. Dalili za hatari5 Anemia (upungufu wa damu) Wakati mtu ana anemia, kawaida inamaanisha kwamba hajaweza kula vyakula vilivyo na madini ya ayani ya kutosha. Madini ya ayani husaidia seli za damu nyekundu kubeba oksijeni kutoka kwenye hewa tunayovuta hadi sehemu zote za mwili. Ishara na dalili za hatari • Weupe - weupe ndani ya kope, kucha na fizi • Kizunguzungu au kuzirai • Udhaifu au kuchoka • Mapgo kwenye mishipa ya damu yenye mwendo wa kasi mkubwa (zaidi ya mapigo 100 kwa dakika) • Ugumu wa kupumua (upungufu wa pumzi). Kupumua kwa shida Baadhi ya upungufu wa pumzi, hasa wakati wa kipindi cha mwisho chaujauzito, ni wa kawaida. Wanawake wengi hupata upungufu wa kiasi cha pumzi wakati wako na mimba ya miezi wa 8 au 9. Upungufu wa pumzi pia unaweza kusababishwa na: Anemia Matatizo ya moyo Kifua kikuu Pumu Maambukizi ya mapafu Damu kuganda katika mapafu Aleji. 5 Kwa msingi wa: Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Ujauzito, Sehemu 1”, ukurasa 95-99, imepakuliwa kutoka: www.open.edu, inapatikana: 22-24.06.2014.
  • 15. 15 Ugonjwa wa kisukari Wakati mama ana ugonjwa wa kisukari, mwili wake hauwezi kutumia sukari yote iliyo kwenye damu, hivyo sukari inakuwa juu sana na baadhi yake inaweza kuonekana kwenye mkojo wake. Kama mama ana baadhi ya dalili za hatari zifuatazo, anaweza kuwa na ugonjwa wa kisukari. Kina mama wa- naougua ugonjwa wa kisukari kwa kawaida hawana ishara hizi zote. Lakini iwapo mama akiwa na dalili zaidi, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na ugonjwa wa kisukari. ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ---------------------------------------------------------------------- -----------------------------------------------------------------------
  • 16. 16 ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ---------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- • Alikuwa na ugonjwa wa kisukari katika ujauzito wa awali. • Mmoja wa watoto waliozaliwa alikuwa mkubwa sana (zaidi ya kilo 4); hii ni kwa sababu sukari nyingi katika damu ya mama humfanya mtoto- kuongeza uzito kupita kiasi. • Mmoja wa watoto wake alikuwa mgonjwa sana au alikufa wakati wa kuzaliwa bila kujua sababu. • Yeye ni mnene. • Yeye hupatwa na kiu kila wakati. • Yeye huwashwa mara kwa mara na ana harufu mbaya inayotoka kwenye uke wake. • Majeraha yake hupona polepole. • Yeye hukojoa mara kwa mara zaidi kuliko wajawazito wengine • Uterasi yake ni kubwa kuliko ya kawaida kutokana na ile miezi aliyokuwa mjamzito.
  • 17. 17 6. Mkao wa mtoto6 Inaweza kuwa vigumu kujua mkao wa mtoto kabla ya miezi sita au saba ya ujauzito, na si muhimu hadi majuma 36 (miezi minane) kwa sababu ni kawaida mtoto kuzunguka hadi mwezi wa mwisho. Mara tu ujauzito unapotimiza miezi sita au saba, itakuwa rahisi kuhisi mtoto na kujua mkao wake kwenye uterasi. Hisi fumbatio la mama kwa mikono yako kwa kila upande, ukisukuma pole pole kwa kila mkono kwa zamu. Unapaswa uweze kuhisi mtoto akiwa amelala wima - yaani kichwa chini. (b) Iwapo mtoto amelala kingamo, unaweza kuhisi kichwa na matako yake kwenye pande za mama. Mwanamke akianza uchungu na mtoto bado amelala kingamo haiwezekani kumzaa kama kawaida. Ni lazima kwenda hospitalini kwa haraka kabla mtoto hajapata shida. Mtoto huyu lazima azaliwe kwa upasuaji 6 Kwa msingi wa: Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Ujauzito, Sehemu 1”, ukurasa 113-121, imepakuliwa kutoka: www.open.edu, inapatikana: 22-24.06.2014. Wima: kichwa au matako chini Kingamo: kichwa na matako kwenye pande b. a.
  • 18. 18 Kufikia mwezi wa mwisho kabla ya kuzaliwa, watoto wengi huwa wamelala kichwa kikielekea kwenye seviksi ya uterasi . Hali ya kichwa chini huitwa mlalo wa kutanguliza kichwa, na iwapo sehemu ya fuu la kichwa iitwayo veteksi itatangulia kwenye njia ya uzazi, huu ndio mlalo bora zaidi kwa uzazi wa mtoto. Madaktari na wakunga huiita sehemu ya mtoto inayotangu- lia kwenye seviksi ya uterasi kitangulizi. Mkunga anafinya kwa uthabiti kwa vidole vyake juu ya mfupa wa kinena ajue ikiwa anaweza kuhisi kichwa cha mtoto. matako upande wa chini ------------------------------------------- ------------------------------------------- ------------------------------------------- ------------------------------------------ ------------------------------------------ ------------------------------------------- ------------------------------------------ ------------------------------------------- ------------------------------------------- --------------------------------------------- --------------------------------------------- kichwa upande wa chini
  • 19. 19 7. Kusikia mapigo ya moyo yakienda kasi7 Kufikia miezi miwili ya mwisho ya ujauzito, mkunga anaweza kusikia mapigo ya moyo wa fetasi mara nyingi akiwa katika chumba kisicho na kelele kwa kuweka sikio lake kwenye fumbatio la mama. Ni rahisi kusikia mapigo ya moyo kwa stethoskopu au fetoskopu. ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ---------------------------------------------------------------------- 7 Kwa msingi wa: Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Ujauzito, Sehemu 1”, ukurasa 118-119, imepakuliwa kutoka: www.open.edu, inapatikana: 22-24.06.2014.
  • 20. 20 8. Maumivu na matatizo mengine8 Maumivu ya mgongo Wanawake wengi wajawazito hukumbwa na maumivu ya mgongo. Uzani wa mtoto, uterasi na kiowevu cha amnioni hubadili mkao wake na kuweka mka- zo kwenye mifupa na misuli ya mwanamke huyo. Kusimama mahali pamoja kwa muda mrefu, kuinama au kazi nyingi za sulubu, zinaweza kusababisha maumivu ya mgongo. Aina nyingi za maumivu ya mgongo ni kawaida katika ujauzito lakini pia zinaweza kusababishwa na maambukizi ya figo. Mhimize mume, watoto, jamaa wengine au marafiki wa mwanamke huyu kuusinga mgongo wake. Kitambaa chenye joto au chupa yenye maji moto kwenye mgongo wake pia vinaweza kumtuliza. Pia jamaa zake wanaweza kusaidia kwa kufanya baadhi ya kazi nzito kama vile kubeba watoto wado- go, kufua, kulima, na kusaga nafaka. Chupi inayokaza, au mshipi unaovaliwa kwenye nyonga, pamoja na kupumzika kitandani mara kwa mara kunaweza kupunguza maumivu ya mgongo. Kukakamaa kwa miguu Miguu au nyayo za wanawake wengi wajawazito inaweza kukakamaa – Haya ni maumivu makali ya ghafla na kukaza kwa misuli. Kukakamaa huku hasa hutokea usiku au wanawake wanapojinyoosha na kuvuta vidole vyao vya mguu. Ili kukomesha mikakamao, kunja wayo (kuelekea juu) na kisha usugue mguu huo kwa upole ili kuusaidia utulie (usisugue kwa nguvu). kunja vidole vya mguu kuelekea juu kisha sugua mguu huo 8 Kwa msingi wa: Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Ujauzito, Sehemu 1”, ukurasa 127-131, imepakuliwa kutoka: www.open.edu, inapatikana: 22-24.06.2014.
  • 21. 21 Maumivu ya ghafla katika sehemu ya chini ya upande wa fumbatio. Uterasi, katika nafasi yake, hushikiliwa kwa ligamenti kwa kila upande. Ligamenti ni kiungo mithili ya kamba zinazoshikanisha uterasi kwenye fumbatio la mama. Kusonga kwa ghafla kunaweza kusababisha maumivu makali kwenye ligamenti hizi wakati mwingine. Hii si hatari. Maumivu haya hukoma baada ya dakika chache. Kusugua kwa upole au kuweka kitambaa chenye joto kwenye fumbatio kunaweza kusaidia. Maumivu ya kichwa na kipandauso Maumivu ya kichwa hutokea sana katika ujauzito bali si hatari. Maumivu haya ya kichwa yanaweza kuisha mwanamke akipumzika na kutulia zaidi, akinywa juisi au maji zaidi, au akisinga paji la uso kwa upole. Ni SAWA kwa mwanamke mjamzito kunywa tembe mbili za parace- tamol na glasi ya maji mara moja baada ya muda fulani. Hata hivyo, maumivu ya kichwa mwishoni mwa ujauzito yanaweza kuwa ishara ya hatari ya malaria au ya priklampsia, hasa ikiwa pia kuna shinikizo la juu la damu, au kuvimba kwa uso au mikono. Kama maumivu hayatulia baada ya vidonge vya paracetamol mjamzito aende kumwona mganga au mkunga.
  • 22. 22 Edema Kuvimba nyayo na vifundo vya miguu hutokea sana katika ujauzito, hasa alasiri au katika hali ya anga yenye joto. Kuvimba huku hutokana na ede- ma, ambayo ni ubakizaji wa viowevu kwenye tishu za mwili. Chini ya nguvu za uzito, kiowevu kilichobakizwa huteremka mwilini na kujikusanya kwe- nye nyayo. Mwanamke huyo aketi akiwa ameinua nyayo zake mara nyingi iwezekanavyo ili kuwezesha viowevu hivi kufyonzeka na kurudi katika mfumo wa mzunguko wa damu. Kuvimba kwa miguu si hatari, lakini uvimbe mkali kwa mwanamke anapoamka asubuhi, au kuvimba kwa mikono na uso wakati wowote, kunaweza kuwa ishara za priklampsia ambayo ni hali mbaya zaidi (hata ya kuhatarisha maisha). Mwanamke anaweza kupata nafuu kutokana na uvimbe kwenye miguu aki- weka miguu yake juu kwa dakika chache angalau mara mbili au tatu kwa siku, akiepuka kula vyakula vyenye chumvi nyingi, na akinywa maji au juisi za matunda kwa wingi.
  • 23. 23 Kuhisi joto au kutokwa na jasho jingi Kuhisi joto ni jambo linalotokea sana katika ujauzito, na maadamu hakuna ishara nyingine za hatari (kama vile ishara za maambukizi), mwanamke huyo asiwe na wasiwasi. Anaweza kuvaa nguo zinazoweza kupitisha baridi, kuoga mara kwa mara, kutumia pepeo la karatasi au jani kubwa, na kunywa maji mengi na viowevu vingine. Ugumu wa kuamka na kulala Ni vyema mwanamke mjamzito kutolala chali, kwa sababu huenda ikawa vigumu kuamka tena, na kwa kuwa mwanamke akiwa ameulalia mgongo wake, uzito wa uterasi huifinya mishipa mikubwa ya damu ambayo hurudisha damu kwenye moyo. Hii inaweza kupunguza usambazaji wa oksijeni kwenye ubongo wake kwa muda na kumfanya ahisi kizunguzungu. Ikiwa mwanamke anataka kuulalia mgongo wake, anafaa kuweka kitu chini ya mgongo na chini ya magoti yake ili asilale chali kikamilifu. (a) Kuamka bila kugeuka upande mmoja kwanza kunaweza kurarua misuli ya fumbatio. (b) Kugeuka upande na kujisukuma juu kwa mikono ni salama sana na atahisi utulivu. LA! Aoooh! ujisukume juu kwa mikono geuka upande simama
  • 24. 24 Chanjo dhidi ya tetanasi Tetanasi ni maambukizi hatari sana yanayohatarisha maisha na huharibu mfumo wa neva na husababishwa na bakteria katika mazingira, kwa mfano udongoni. Chanjo ya tetanasi ndiyo kinga bora zaidi dhidi ya tetanasi kwa mwanamke na mtoto wake. Kwa hivyo, ni muhimu sana kwake kuchanjwa kulingana na ratiba iliyo kwenye kadi yake na kuleta kadi yake kila ana- pokuja kwa uchunguzi wa ujauzito. ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ---------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- Sindano hizi zitaku- kinga wewe na mtoto dhidi ya tetenasi kwa muda Vizuri
  • 25. 25 9. Virusi vya Ukimwi VVU9 VVU (Virusi Vya Ukimwi) huharibu kingamwili na kusababisha kifo mtu asipotibiwa ipasavyo na dawa za kupunguza makali ya VVU. Virusi hube- bwa kwa damu ya mtu aliyeambukizwa na pia hupatikana katika njia ya uzazi ya wanaume na wanawake walioambukizwa. Vinaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa kufanya ngono bila kinga (ngono bila kondomu) au uhamishaji wa damu iliyooambukizwa. Mama anaweza pia kumwambukiza mtoto virusi wakati wa ujauzito, leba na kuzaa, na pia unyonyeshaji. Kwa hiyo ni lazima kwa kila mwanamke kupima VVU kabla na wa- kati wa mimba na kabla ya kuzaa. Kuna taratibu maalum za kufuata ili mtoto asiamukizwe na mama wakati wa kuzaliwa. Dawa za kupunguza makali na kukinga maambukizi ya virusi vya VVU kutoka kwa mama hadi kwa mtoto zinahusisha kumpatia mama dawa za kurefusha maisha kuanzia wiki 28 za ujauzito, pia kwa mama wakati wa leba na kuzaa, na kwa mtoto wake mara tu baada ya kuzaliwa. Dawa hizi hupunguza hatari ya maambukizi ya VVU kwa mtoto. Ni tofauti na tiba ya kupunguza makali ya virusi anayopewa mama ili kutibu maambukizi ya VVU, kulingana na uhakiki wa vigezo vyake. 9 Kwa msingi wa: Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Ujauzito, Sehemu 2”, ukurasa 44, imepakuliwa kutoka: www.open.edu, inapatikana: 27.06.2014.
  • 26. 26 10. Leba (kuzaa)10 Hakuna anayeweza kujua wakati leba itaanza. Hata hivyo, baadhi ya dalili huashiria kwamba itaanza punde. Mara nyingi, watoto hushuka chini ya fumbatio takriban wiki mbili kabla ya kuzaliwa, hali inayojulikana kama kusahaulika. Kwa kawaida, mwanamke atahisi kuwa mtoto “haelei” kwenye fumbatio, na hasukumi juu tum- bo la mama. Ikiwa mwanamke aliwahi kuzaa, huyu mtoto huenda asishuke hadi wakati wa kuanza kwa leba. Dalili nyingine zinaweza kuan- za siku moja au mbili tu kabla ya kuanza kwa leba. Kinyesi cha mama kinaweza kubadili- ka ama kiasi kidogo cha damu (damu iliyochanganyika na utelezi) kinaweza kutoka kwenye uke. Wakati mwingine, mfuko wa maji hupasuka kabla ya leba kuanza. Kutambua leba halisi si jambo rahisi kwa mama, hasa kama mimba hii ni ya kwanza. Anaweza kukuita au kuja kwenye kituo cha afya mara nyingi akifikiria kuwa maumivu madogo ni mwanzo wa leba halisi. Leba imeainishwa katika awamu hizi nne. • Awamu ya kwanza ya leba ni wakati seviksi hufunguka. • Awamu ya pili ni wakati wa kusukuma, ambayo huisha mtoto anapozaliwa. • Awamu ya tatu ni kuzaliwa kwa kondo. • Awamu ya nne ni masaa manne ya kwanza baada ya kuzaa. 10 Kwa msingi wa: Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Leba na Kuzaa”, ukurasa 7-11 na 62, imepakuliwa kutoka: www.open.edu, inapatikana: 27.06.2014.
  • 27. 27 Awamu ya kwanza ya leba Wakati wa awamu ya kwanza ya leba, seviksi hufunguka pole pole kiasi cha kuwezesha mtoto kutoka kwenye uterasi. Kwa muda mrefu wakati wa uja- uzito, hakuna chochote kinachoweza kuingilia au kutokea kwenye sevi- ksi kwa sababu uwazi huo mdogo huwa umezibwa na utetelezi. Wakati wa ujauzito, seviksi huwa ndefu na imara, kama kidole gumba cha mguu. Utera- si ikikazana, seviksi hupanuka huku sehemu ya chini ya uterasi ikifupika. Awamu fiche ni kipindi kati ya mwanzo wa mikazo inayofuata utaratibu hadi seviksi inapopanuka kwa kiasi cha sentimita 4. Katika awamu hii, mikazo inaweza kuwa chun- gu au isiyo chungu, na seviksi hupanuka pole pole. Awamu fiche huisha wakati seviksi inapoanza kupanuka kwa haraka zaidi. Ongezeko hili la kasi huashiria mwanzo wa awamu wazi. Awamu wazi huanza wakati seviksi imepanuka zaidi ya sentimita 4. Mikazo hii hutokea kwa utaratibu maalum, mara nyingi na huwa chungu. Seviksi hupanuka haraka zaidi. Seviksi huendelea kupanuka hadi kufika kipenyo cha sentimita 10, yaani kupanuka kabisa. Seviksi iliyopanuka kabisa ni pana vya kutosha kupitishia mtoto. not effaced no dilation fully effaced 1 cm dilated 5 cm dilation fully dilated at 10 cm Ukubwa wa serviksi huwa kiasi hiki wakati wa ujauzito
  • 28. 28 Awamu ya pili ya leba Awamu ya pili ya leba huanza wakati seviksi imepanuka kabisa (sentimita 10) na kuisha mtoto anapozaliwa. Baada ya seviksi kupanuka kabisa, mama kawaida hupata hisia za kutaka kusukuma. Mama akisukuma kulingana na mikazo ya uterusi, mtoto huteremkia kwenye seviksi na kushukia ukeni. Mwendo huu wa mtoto hujulikana kama kushuka kwa fetasi. Kiwango cha kushuka kwa fetasi ni kiashirio muhimu cha jinsi leba inavyoendelea. Haba- ri hii itaelezwa kwa kina hapo baadaye. Muda wa awamu ya pili ni wastani wa saa 1 masaa 2. Awamu ya tatu ya leba Katika awamu ya tatu ya leba, plasenta na membreni hutoka baada ya mtoto kuzaliwa. Kwa kawaida, awamu ya tatu huchukua hadi dakika 30. Awamu ya nne ya leba Saa 4 za kwanza punde baada ya plasenta kutoka huwa muhimu. Baadhi ya wataalam wamekipa kipindi hiki jina awamu ya nne ya leba. Mwanamke anaweza kuvuja damu kwa wingi baada ya plasenta kutoka. Hii huto- kea iwapo mikazo ya uterasi inasababisha kutofungika kwa mishipa ya damu iliyofunguka kufuatia kubanduka kwa pla- senta pembezoni mwa uterasi. Kwa hivyo, inafaa uwe makini ili kutambua na kudhibiti damu inayovuja baada ya kuzaa. Damu hii inaweza kuwa dhahiri au iliyofichika. Ikiwa mama anavuja damu kwa wingi, anahitaji usaidizi wa dharura.
  • 29. 29 Hali ya kwanza na miendo saba kuu ya mtoto anaposhuka kwenye njia ya uzazi. Picha hizi ndogo zinaonyesha hali ya kichwa cha mtoto, kana kwamba unatazama kwenda juu ya njia ya uzazi.
  • 30. 30 Hii ndio hufanyika ndani ya mama: Hii ndio unaona nje: 1. Kwanza mtoto hupinda kichwa chake chini, kidevu hadi kifua. Hali hii hufanya kichwa kutoshea kwenye pelvisi kwa urahisi. 2. Kichwa cha mtoto hufinywa na huba- dilisha umbo lake kikitoka kwa pelvisi ya mama. Mtoto hugeuza uso wake kuelekea mgongo wa mama. 3. Mtoto huanza kuinua kidevu chake kikikaribia ufunguaji wa uke. Hii huitwa mkondo. 4. Mtoto huinua kidevu chake zaidi wakati kichwa kinachomoka. 5. Mtoto huendelea kuinua kidevu chake wakati kichwa kinatoka nje. Yaani kichwa kinatolewa kwa utaratibu. 6. Mtoto huendelea kuinua kidevu chake hadi kichwa kitolewe. Mara ya kwanza uso wa mtoto bado unaangalia mgon- go wa mama, ilhali mabega yake yako katika hali fulani. 7. Hivi punde kichwa cha mtoto hugeuka kuangalia miguu ya mama. Uso wa mtoto sasa unapangwa na mabega yake.
  • 31. 31 Mkao wa mwendo wakati wa awamu ya kwanza na ya pili ya leba11 Kuna vipengele kadhaa vinavyoathiri uamuzi kuhusu mkao wa mama katika awamu ya kwanza ya leba. Kati ya mikao yote, ulio muhimu zaidi ni hiari ya mama - jinsi angependa kuzaa. Hata hivyo, baadhi ya wanawake huhi- taji kuhimizwa kujaribu mikao tofauti. Msaidie mwanamke kujisogeza wakati wa leba. Anaweza kuchuchumaa, kuketi, kupiga magoti au mikao mingineyo. Mikao hii yote ni mizuri. Seviksi hufunguka kwa usawa zaidi mama anapo- badili hali ya mkao. 11 Kwa msingi wa: Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Leba na Kuzaa”, ukurasa 32 na 64, imepakuliwa kutoka: www.open.edu, inapatikana: 27.06.2014.
  • 32. 32 Kuketi nusu Hali hii inaweza kuwa nzuri zaidi na hurahishisha kazi kwa mkunga kuelekeza utoaji wa kichwa cha mtoto Hali hii ni ya kupumzisha na kusaidia kuzuia machozi kuingia kwenye uke na msamba Hali hii ni nzuri wakati mwa- namke anahisi leba yake iko nyuma ya mgongo. Pia inaweza kusaidia wakati mabega ya mtoto yamekwama Hali hizi mbili zinaweza kusaidia kuleta mtoto chini wakati uzalishaji unaenda polepole Kukalia kifaa Kulala upande Kuchuchumaa
  • 33. 33 Mguso12 Leba inaweza kuwa ngumu zaidi iwapo mwanamke ana hofu au wasiwasi. Ili kumsaidia kupunguza hofu, mthibitishie mwanamke huyu kuwa maumivu aliyo nayo ni ya kawaida. Ingawa mguso unaweza kumsaidia mwanamke aliye katika leba, fahamu aina ya mguso anayopendelea. Mifano ya miguso inayopendelewa mara nyingi na wanawake ni kama: • Kusukuma kwa uthabiti na utulivu kwenye sehemu ya chini ya mgongo- wakati wa mikazo. • Mpapase baina ya mikazo, hasa miguu na mgongo. • Kijitambaa kilicho na joto au baridi kwenye sehemu ya chini ya mgongo au tumbo. Iwapo mama anatokwa na jasho, kuweka kijitambaa chenye ubaridi kwenye paji la uso humfanya kuhisi vyema. Kupumua wakati wa leba13 Namna ya kupumua kwa mwanamke inaweza kuathiri sana jinsi leba ilivyo. Katika awamu ya kwanza ya leba, mbinu mbali mbali za kupumua zina- weza kurahisisha leba zaidi. Mjamzito achague mbinu inayomfaidi zaidi ili kupunguza maumivu. • Kupumua taratibu. Avute pumzi taratibu kwa muda mrefu. Ili kutoa pumzi, atumie pua na mdomo kisha atoe pumzi polepole. Kuvuta pumzi kupitia pua husaidia kupunguza kasi ya kupumua. • Apumue kwa sauti ya ’juu’. Mwanamke huvuta pumzi nzito taratibu, kisha hutoa pumzi fupi za haraka ili kutoa sauti laini ya „hiii, hiii”. • Kuhema. Mwanamke huvuta pumzi nyepesi za haraka. Kupuliza kwa nguvu. Mwanamke hupumua kwa nguvu na kasi. 12 Kwa msingi wa: Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Leba na Kuzaa”, ukurasa 33, imepakuliwa kutoka: www.open.edu, inapatikana: 27.06.2014. 13 Kwa msingi wa: Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Leba na Kuzaa”, ukurasa 33-34, imepakuliwa kutoka: www.open.edu, inapatikana: 28.06.2014.
  • 34. 34 Kutumia vinywaji Mwanamke aliye katika leba hutumia nguvu nyingi na maji ya mwili kwa haraka. Katika awamu ya kwanza ya leba, mwanamke anapaswa kunywa angalau kikombe kimoja cha kinywaji kilicho na kiwango cha juu cha kalori kila saa, kama vile chai, vinywaji visivyolevya, supu au maji ya matunda. Mwanamke huyu asipokunywa vinywaji vya kutosha, anaweza kuishiwa na maji (kukosa maji ya kutosha mwilini). Jambo hili linaweza kufanya leba kuwa ndefu na ngumu zaidi na kumfanya kuhisi uchovu. Ukosefu wa maji mwilini pia unaweza kumfanya mwanamke huyu kujihisi mchovu. Kitanzi cha kwanza cha fundo mraba Kitanzi cha pili cha fundo mraba Funga fundo mraba Kukata kambakitovu14 14 Kwa msingi wa: Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Leba na Kuzaa”, ukurasa 67-68, imepakuliwa kutoka: www.open.edu, inapatikana: 28.06.2014.
  • 35. 35 Kumnyonyesha mtoto baada ya kuzaa15 Anza kunyonyesha punde tu mtoto atakapozaliwa ili kupunguza kuvuja damu baada ya kuzaa. ----------------------- ----------------------- ----------------------- ---------------------- ----------------------- ----------------------- ---------------------- ----------------------- ----------------------- ----------------------- ---------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- ----------------------------------------------------------------------- 15 Kwa msingi wa: Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Leba na Kuzaa”, ukurasa 145, imepakuliwa kutoka: www.open.edu, inapatikana: 28.06.2014.
  • 36. 36 usahihi kimakosa 11. Baada ya kuzaa16 Watu wanaoishi pamoja na mama aliyjifungua wanapaswa kumsaidia katika kazi za nyumbani. Mama anatakiwa kumpumzika baada ya leba na lengo lake liwe mtoto tu kwa sasa. Akijisikia vizuri anaweza kuendelea na kazi zake za nyumbani pamoja na kumtunza mtoto mchanga. Kunyonyesha mtoto Njia ya kushika matiti ni muhimu kwa sababu itakusaidia kumnyonyesha mtoto au la. 16 Kwa msingi wa: Burns A.A., Lovich R., Maxwell J., Shapiro K., (2010), Where woman have no doctor, (Berkeley: Hesperian Foundation)
  • 37. 37
  • 38. 38 Chemchemi: · Ukunga, Sr. U.B. Schnell, Benedictine Publication, Tanzania 1993 · Uimarishaji wa familia, Sr. U.B. Schnell, Benedictine Publications, Tanzania 2008 · Kitabu sha afya kwa watu wazima na waalimu, Sr. U.B. Schnell, Benedictine Publication, Tanzania 1998 · Ukunga-mazoezi, M.Troszyński, PZWL, Poland 2009 Bibliografia: · Burns A.A., Lovich R., Maxwell J., Shapiro K., (2010), Where woman have no doctor, (Berkeley: Hesperian Foundation). · Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Ujauzito, Sehemu 1”, imepakuliwa kutoka: www.open.edu · Health and Education Learning, (2011), “Utunzaji katika Ujauzito, Sehemu 2”, imepakuliwa kutoka: www.open.edu. · Health and Education Learning, (2011), „Utunzaji katika Leba na Kuzaa”, imepakuliwa kutoka: www.open.edu. · Mashahidi wa Jehova, „Kufanya Mimba Yako Iwe Safama Zaidi”, kutoka: http://m.wol.jw.org/sw/wol/d/r13/lp-sw/102003005, · Chapisho kutoka mtandao wa intaneti: http://www.storknet.com/ip/ reproductive_years/pregnancy/normal_course_pregnancy.html Filamu: · 10 Steps to a Clean Delivery https://www.youtube.com/watch?v= gjXZvIehZfw&feature=share · Management of Primary Postpartum Haemorrhage (PPH) part1 https://www.youtube.com/watch?v=xU7da4SO5Gs&list=UUJpt9KN 7frvqdszcQzECI7w · Management of Primary Postpartum Haemorrhage (PPH) part2 https://www.youtube.com/watch?v=Vn14vQAIkKk&list=UUJpt9KN 7frvqdszcQzECI7w · HIV Prevention Tutorial https://www.youtube.com/watch?v=AZOEpUjIlgI · Je, mtoto wako ni mgonjwa? Muda mrefu filamu - Kuharisha, Ny umonia, Malaria https://www.youtube.com/watch?v=VWEBr_Ad1uo · Ujauzito Salama: Ushauri kwa Wanawake https://www.youtube.com/watch?v=OHrqHNwHtZ4
  • 39. KUWA MAMA NI KAZI
  • 40. Mradi huu - ulikamilishwa kwa hisani kubwa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Poland, mnamo mwaka 2014. Uboreshaji wa huduma za afya mjini na wilaya ya Mwanga. THE GRAIL SISTERS TANZANIA