1. HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA
RISALA ILIYOSOMWA NA ENG TANU DEULE, MHANDISI WA MAJI WA WILAYA YA
BUNDA KWENYE SIKU YA KILELE CHA WIKI YA MAJI KATIKA KIJIJI CHA TAIRO
TAREHE 22-MACHI-2011
Mh. Mgeni Rasmi
Wah. Viongozi mliofika hapa wa chama na serikali
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Maji Bunda Mr Jumanne Turbet
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji Bunda
Wafanyakazi wenzangu wa Idara ya Maji ya Halmashauri ya wilaya ya Bunda
Wafanyakazi wenzetu wa Halmashauri mliofika hapa kutuunga mkono
Uongozi mzima wa Shule ya Msingi Tairo
Ndugu zetu waandishi wa habari
Wananchi Mabibi na mabwana
Tumsifu Yesu Kristu
Asalam aleykum
Awali ya yote naomba kumshukuru mwenyezi Mungu, kwa kutujalia pumzi, afya na
nguvu ya kusherehekea kilele cha wiki ya maji hapa Wilayani kwetu. Siku ya leo ni
mhimu kwasababu ni siku ya maji duniani kote yaani “World Water day”.
Ninayofuraha kubwa kupata fursa ya kuadhimisha wiki ya maji katika kijiji hiki kwani
ni nafasi nzuri ya kuzidi kufahamiana na wanajamii ambao ndio wadau mhimu wa
usalama na uendelevu wa miundombinu yetu ya maji ya Mjini Bunda.
2. Mh. Mgeni Rasmi
Tarehe 22 Machi kila mwaka ni siku ya Maji Duniani. Maji ni uhai, na upatikanaji wa
maji ni chachu ya maendeleo kwa kila mwanajamii.Hii ndiyo sababu kuu taifa letu
kuadhimisha wiki ya maji kwa nia ya kutathimini hali ya upatikanaji wa huduma ya
maji na usafi wa mazingira na kujiwekea mikakati ya kuboresha upatikanaji wa maji
safi na salama.
Wananchi wa Wilaya ya Bunda leo wanaungaana na taifa zima kuadhimisha kilele cha
wiki ya maji. Wiki iliyozinduliwa tarehe16/3/2011 Jijini Mwanza na Waziri wa Maji,
Prof Mark Mwandosya (MB). Tangu mwaka 1988, maadhimisho haya ya wiki ya maji ni
ya 23 na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Maji kwaajili ya Miji: kukabiliana na
changamoto mbalimbali Mijini”
Kauli mbiu ya mwaka huu inagusa maji mijini na changamoto zake. Miji inayotajwa
katika kauli mbiu hii ni pamoja na mji wa Bunda. Na hapa utaona maadhimisho ya
wiki ya maji mwaka huu yamezinduliwa kwenye viunga vya mjini na yanahitimishwa
kwenye viunga vya mjini pia.
Mh. Mgeni Rasmi,
Kuhusu malengo ya MKUKUTA na MILENIA kuhusu utoaji wa huduma ya Maji
Sera ya Maji ya Taifa ya mwaka 2002 iliweka madhumuni ya kuongeza na kuimarisha
hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama toka asilimia 54(2005) hadi
asilimia 65 kwa wakazi waishio vijijini, na kutoka asilimia 74 (2005) hadi asilimia 90
kwa wakazi waishio mijini ifikapo mwaka 2010. Lengo kuu ilikuwa ni kupunguza
umasikini na kuwa na maisha bora kwa watu wote. Malengo haya yameshindwa
kufikiwa kwa wilaya ya Bunda kwa sababu mbalimbali na hivyo kuwa nyuma ya
2
3. utekelezaji wa malengo ya MKUKUTA, Malengo ya Milenia (MDGs) na Dira ya Taifa
ya Maendeleo (Development Vision 2025)
Mh. Mgeni Rasmi
Hali ya huduma ya maji kiwilaya
Asilimia 47.7 ya wakazi wa vijijini wanapata maji safi na salama. Vyanzo vikuu vya
huduma ya maji vijinini ni Visima virefu na vifupi, ziwa Victoria, matanki ya kuvuna
maji ya mvua, visima vya asili na malambo. Kiwango cha utoaji huduma ya maji
wilayani Bunda ni cha chini ukilinganisha na wastani wa kitaifa wa utoaji wa huduma
ya maji ambao ni asilimia 58 (2010). Hali hii ni changamoto kwetu kama wilaya na jamii
zetu kuhakikisha tunaongeza upatikanaji wa huduma ya maji wilayani Bunda.
Mh. Mgeni Rasmi
Kuhusu chombo chenye mamlaka ya kutoa huduma ya maji Bunda mjini
Jukumu la utoaji wa huduma ya maji Mjini Bunda lipo chini ya Mamlaka ya Maji
Bunda yaani Bunda Water Supply Authority. Hii ni Mamlaka kamili iliyoanzishwa
tarehe 21/6/2002 baada ya kutangazwa kwenye gazeti la serikali. Bodi yake ya kwanza
iliteuliwa tarehe 1Juni 2003 na hivi sasa kuna Bodi ya tatu iliyoteuliwa rasmi tarehe 10
januari mwaka huu wa 2011.
Mh. Mgeni Rasmi
Kuhusu mafanikio ya Mamlaka ya Maji kwa miaka5 iliyopita (2006-2010)
• Kiwango cha maji yanayozalishwa kwa siku yameongezeka kutoka lita 720,000
mwaka 2006 hadi liata 1,260,000 mwaka 2010
• Wateja wameongezeka kutoka 650 mwaka 2006 hadi wateja1,227 mwaka 2010
• Wastani wa watu wenye maji ya bomba wameongezeka kutoka asilimia 22 mwaka
2006 hadi asilimia 27.4 mwaka 2010
3
4. • Mapato kwa mwaka yamekuwa kutoka 20,246,311(2006) hadi 74,184,663 (2010)
• Mamlaka imepunguza maji yanayopotea Unaccountable for Water) toka 75% (2006)
hadi 42(2010)
• Mamlaka imepata pikipiki 3 na Laptop 1
• Kituo cha ushahi kimejengewa Uzio
• Tangi la Mgaja limekarabatiwa na Maji sasa yanasukumwa hadi hospitali ya
Manyamanyama
• Mtandao wa mabomba umeongezwa kutoka 49km 73km hivi sasa
• Nyumba ya pampu imekarabatiwa na kujengwa chumba cha wahudumu Mgaja
Mh. Mgeni Rasmi
Kuhusu mradi Mpya wa Maji Bunda Mjini
Takwimu iliyoonyeshwa hapo juu kwamba katika watu 100 ni watu 27 tu ndo
wanapata maji ya bomba inadhihirisha ukubwa wa tatizo lililopo na kwamba
changamoto hii ni kubwa sana kwetu. Hivyo basi, Halmashauri kwa kushirikiana na
Wizara ya Maji na kwa Msukumo wa pekee wa mheshimiwa Mbunge wa jimbo la
Bunda, Mh. Stephen M. Wasira (MB) na Waziri wa nchi ofisi ya raisi –Mawasiliano na
Uratibu, tumeanza kutekeleza mradi mpya wa maji hapa Bunda mjini utakaokuwa na
chanzo chake kwenye kijiji cha Nyabehu kilichopo umbali wa kilomita 26 kutoka mjini.
Mradi huu ni mkubwa na una gharimu fedha nyingi. Mradi umekuwa unatekelezwa
kadiri fedha zilivyokuwa zinapatikana kama ifuatavyo;
Awamu ya I: Zimenunuliwa pampu mpya 9 za kusukuma maji na tayari zipo hapa
Wilayani Bunda zimetunzwa kwenye Bohari yetu
Awamu ya II: Umefanyika ujenzi wa
i. Tengi la maji Migungani lenye ujazo wa lita 225,000
ii. Tengi la kwenye Mlima Kaswaka lenye ujazo wa lita 675,000
4
5. iii. Nyumba ya kufunga pampu (Pump House)
iv. Nyumba ya wahudumu wa pamp (pump attendant house) na choo yake
v. Barabara ya kwenda kwenye tengi la maji kwenye Mlima Kaswaka
Awamu ya II: Awamu hii bado haijatekelezwa lakini itahusisha kazi zifuatazo
• Ujenzi wa chujio (treatment plant)
• Kununua na kulaza mabomba ya bomba kuu kilometa 26
• Kusimika pampu
• Kuingiza umeme wenye msongo mkubwa, na
• Kusuka mtandao mpya wa usambazaji maji hapa mjini
Mh. Mgeni Rasmi
Awamu hii ya tatu ndiyo awamu inayohitaji fedha nyingi zaidi kuliko awamu
zilizopita. Makisio ya awali yanaonesha kuwa zitahitajika zaidi ya shilingi billion kumi
(10Billions) kukamilisha mradi huu kiasi ambacho ni kikubwa ukilinganisha na
takribani billion moja ambayo imekwishatumika kwa awamu ya I na awamu ya II.
Habari njema ni kwamba, mradi huu sasa utatengewa bajeti kubwa kwenye mwaka wa
fedha wa 2011/2012 ili ukamilike. Hii pia ilipewa uzito na kauli ya Mh Waziri wa Maji
tarehe 16/3/2011 kwenye uzinduzi wa wiki ya maji pale alipo thibitishia umma kwa
kusema, nanukuu “sasa tumedhamiria kuukamilisha mradi wa Bunda na
tutaukamilisha” mwisho wa kunukuu.
Hata hivyo mheshimiwa mgeni rasmi kazi za awali za maandalizi ya awamu hii ya tatu
zimeshaanza kufanyika kwani mhandisi mshauri ameshapatikana na anafanya kazi ya
kuandaa zabuni za ujenzi wa chujio, zabuni za ununuzi na utandazaji wa mabomba ya
maji, na anaandaa zabuni za uwekaji umeme wa msongo mkubwa na usimikaji wa
mitambo. Mradi huu kwa ujumla unasimamiwa na Mamlaka ya Maji taka na Maji Safi
5
6. Musoma kwaniaba ya Wizara ya Maji na kwa upande wa Halmashauri wapo Mamlaka
ya Maji ya Bunda.
Mh. Mgeni Rasmi
changamoto zinazoikabili Mamlaka ya Maji Bunda Mjini;
i. Miundimbinu ya maji inahujumiwa kwa bomba kutobolewa na wafugaji wa
vijiji vya njiani kwenye bomba kuu ambavyo ni Guta, Tairo na Migungani
ii. Uchakavu wa miundombinu ya maji hasa mabomba na mitambo
iii. Mamlaka inapoteza maji kiasi cha asilimia 46% kwa mwaka 2010
iv. Kukatika nishati ya umeme mara kwa mara kumesababisha kuunguza pampu
zetu za maji na vifaa vyake
v. Watumiaji maji kutolipa Ankara zao za maji kwa wakati
vi. Maji yanayosukumwa kutokidhi mahitaji ya jamii
vii. Ukosefu wa fedha za kulipia Billi ya Umeme kwani ruzuku mara inakuja
kidogo au miezi mingine ruzuku haiji kabisa na TANESCO hutishia kukata
umeme mara kwa mara.
viii. Mwaka 2006 tulikwisha fanya mategenezo ya mabomba mara 253 na hivi sasa
tumefikia mara 1,085 kwa mwaka 2010 hali ambayo inaonesha kuwa uhujumu
wa miundombinu yetu unazidi kuongezeka badala ya kupunguza.
Mikakati inayotumika kukabiliana na changamoto hizi ni kama ifuatavyo;
• Ukamilishaji wa mradi mpya wa maji wenye chanzo chake Nyabehu
• Kuendelea ukarabati wa miundombinu ya maji kwa kutumia fedha kidogo
tunazokusanya kwa wateja kila mwezi
6
7. • Ofisi ya Mkuu wa wilaya kusaidia namna ya kudhibiti hujuma na kwa Kutumia
vyombo vya dola kama vile Mahakama, Polisi na serikali za Vijiji kusaidia kudhibiti
hujuma dhidi ya miundombinu yetu
• Kuendelea kuiomba serikali kutoa fedha za ruzuku kwa wakati kama ilivyo kwenye
bajeti ili shughuli zisikwame
Tunapenda kutoa rai kwa watumiaji maji kulipia Ankara zao za maji kwa wakati na
kuwaasa waepukane na utumiaji wa maji salama kwa Bustani, kuoshea magari n.k Pia
wasikubali kuchepusha maji yasipite kwenye mita kwani kwa kufanya hivyo ni kosa la
jinai na wanaweza kushitakiwa kwa mjibu wa sheria. Wananchi waisaidie Mamlaka
yao kufichua waovu wanaoihujumu Mamlaka isisonge mbele
Aidha tunawaomba Wananchi waendelee kushirikiana na Mamlaka kwa kuwafichua
wahalifu wanaotoboa mabomba ili watiwe nguvuni mara moja kwa maana serikali
inaweka nguvu nyingi katika kujenga miundo mbinu hii na sisi hatuna budi kuitunza
kwa faida yetu na vizazi vijavyo.Tusipobadili tabia na mazoea yetu kwa hili, sheria sasa
itaanza kuchukua mkondo wake.
Mh. Mgeni Rasmi
Wazo mbadala juu ya maji safi kwa Mji wa Bunda
Kwakuwa mji wa Bunda unazungukwa na miamba ya mawe kwa eneo kubwa
(Impermeable Rocks) ambayo inaweza kutumika kuhifadhi maji hivyo tunafikiria
uwezekano wa kuvuna maji ya mvua kwa kuweka uzio wa mifereji ya siment juu
milimani ili kukusanya maji ya mvua ya mwaka mzima na kutumiwa na watu kwa
kunywa n.k kwa njia ya mtiririko bila kutumia nishati ya umeme. Ninayo imani kuwa
baadhi ya eneo la mji wa Bunda litaweza kuhudumiwa kwa njia hii.
7
8. Mh mgeni Rasmi
Kabla ya kumaliza napenda kuzungumzia jambo la UKIMWI. Tukumbuke ukimwi
haubagui mtu mwenye maji wala yule asiye na maji,tajiri wala masikini, mnene wala,
mwembamba, mrefu au mfupi, sura nzuri au mbaya. Ndugu zangu mimi na wewe
“Tubadilike tabia, ukimwi unaua napengine njia ya kujikinga na ukimwi ni kuamini
kuwa kila mtu anao na tujiepushe na ukimwi, hauna dawa. Ukiwa mbishi dhambi
zako mwenyewe.
Mh. Mgeni Rasmi
Mwisho naomba kwa ridhaa yako nitumie fursa hii kukushukuru wewe binafsi kwa
kukubali mwaliko wetu. Pili niwashukuru kwa namna ya pekee wenzetu wa Mamlaka
ya Maji Bunda kwa kufanikisha shughuli hii ya kilele cha wiki ya Maji hapa wilayani
kwetu Bunda. Niwashukuru watumishi wa idara ya maji kwa ushirikiano wao
kufanikisha shughui hii na pia niwashukuru kwa namna pekee waandishi wa habari
wa televisheni, Magazeti na redio waliofika hapa.
Maji ni Uhai na Usafi wa Mazingira ni Utu
Siku ya Maji Duniani Hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
Aksanteni kwa kunisikiliza
8