Risala ya Uzinduzi wa Wiki ya Maji Wilayani Bundailiyosomwa na Eng. Tanu Deule, Mhandisi wa maji wa wilaya    ya Bunda ...
Maadhimisho haya ya wiki ya maji ni ya 23 tangu yaanze kufanyika kitaifa mwaka 1988na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Maji kwa...
Takwimu iliyoonyeshwa hapo juu kwamba katika watu 100 ni watu 27 tu ndowanapata maji ya bomba inadhihirisha ukubwa wa tati...
•  Kuingiza umeme wenye msongo mkubwa, na       •  Kusuka mtandao mpya wa usambazaji maji hapa mjiniMh. Mgeni Rasm...
kuwa imara muda wote. Tengi limejengwa na mkadarasi wa daraja la juu kabisa naamelijengwa kwa kiwango bora kabisa na limej...
•   Ofisi ya Mkuu wa wilaya kusaidia namna ya kudhibiti hujuma na kwa      Kutumia vyombo vya dola kama vile Mahak...
Upcoming SlideShare
Loading in …5
×

Risala uzinduzi wiki ya maji bunda by Eng Deule Tanu

751 views

Published on

The speech that was ready by Eng Deule, Tanu on the inauguration of Water Week In Bunda DC

Published in: Education, News & Politics
0 Comments
0 Likes
Statistics
Notes
 • Be the first to comment

 • Be the first to like this

No Downloads
Views
Total views
751
On SlideShare
0
From Embeds
0
Number of Embeds
3
Actions
Shares
0
Downloads
0
Comments
0
Likes
0
Embeds 0
No embeds

No notes for slide

Risala uzinduzi wiki ya maji bunda by Eng Deule Tanu

 1. 1. Risala ya Uzinduzi wa Wiki ya Maji Wilayani Bundailiyosomwa na Eng. Tanu Deule, Mhandisi wa maji wa wilaya ya Bunda kwenye Tengi la Maji la Mlima Kaswaka Bunda Mjini Tarehe 17 - Machi - 2011Mh. Mgeni Rasmi (Mkuu wa Wilaya ya Bunda)Wah. Viongozi mliofika hapa (Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Bunda)Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji BundaWafanyakazi wenzangu wa Idara ya Maji kwa ujumla wenuWafanyakazi wa Halmashauri yetu mliofika hapa kuungana nasiNdugu zetu waandishi wa habariNdugu WananchiMabibi na mabwanaTumsifu Yesu KristoAsalaam AleykumBwana asifiweKabla ya yote napenda kumshukuru mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwakutujalia uzima na leo tupo hapaMh. Mgeni RasmiLeo Halmashauri yetu inaungana na taifa zima kuadhimisha wiki ya maji ambayoimezinduliwa rasmi na Waziri wa Maji Mh. Prof Mark Mwandosya (MB) kwenyeviwanja vya Nyamagana jijini Mwanza jana tarehe 16/3/2011. Wiki hii ya majiitahitimishwa tarehe 22/3/2011 ambayo ni siku ya Maji kidunia yaani World Water Day.
 2. 2. Maadhimisho haya ya wiki ya maji ni ya 23 tangu yaanze kufanyika kitaifa mwaka 1988na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Maji kwaajili ya Miji: kukabiliana na changamotombalimbali Mijini”Mh. Mgeni RasmiMiji inayotajwa kwenye kauli mbiu ya mwaka huu ni pamoja na mji wa Bunda. Na hiindiyo maana Halmashauri yetu ya Wilaya Ikaonelea kuwa ni vema uzinduzi huu wawiki ya maji kiwilaya ufanyike ndani ya viunga hivi vya Mjini na hasa kwenye mradimpya wa maji Bunda Mjini.Mh. Mgeni RasmiKuhusu chombo chenye mamlaka ya kutoa huduma ya maji Bunda mjiniJukumu la utoaji huduma ya maji hapa Mjini, limekasimiwa kwa Mamlaka ya majiBunda mjini yaani Bunda Water Supply Authority. Hii ni Mamlaka kamiliiliyoanzishwa tarehe 21/6/2002 baada ya kutangazwa kwenye gazeti la serikali. Bodiyake ya kwanza ilianza kutenda kazi tarehe 1Juni 2003 na hivi sasa kuna Bodi ya 3iliyoteuliwa rasmi tarehe 10 januari mwaka huu wa 2011.Mh. Mgeni RasmiKuhusu huduma ya maji hapa mjini.• Kiwango cha maji yanayozalishwa kwa siku yameongezeka kutoka lita 720,000 mwaka 2006 hadi liata 1,260,000 mwaka 2010• Wateja wameongezeka kutoka 650 mwaka 2006 hadi wateja1,227 mwaka 2010• Wastani wa watu wenye maji ya bomba wameongezeka kutoka asilimia 15.4 mwaka 2006 hadi asilimia 27.4 mwaka 2010Mh. Mgeni RasmiKuhusu mradi Mpya wa Maji Bunda Mjini 2
 3. 3. Takwimu iliyoonyeshwa hapo juu kwamba katika watu 100 ni watu 27 tu ndowanapata maji ya bomba inadhihirisha ukubwa wa tatizo lililopo na kwambachangamoto hii ni kubwa sana kwetu. Hivyo basi, Halmashauri kwa kushirikiana naWizara ya Maji na kwa Msukumo wa pekee wa mheshimiwa Mbunge wa jimbo laBunda, Mh. Stephen M. Wasira (MB) na Waziri wa nchi ofisi ya raisi –Mawasiliano naUratibu, tumeanza kutekeleza mradi mpya wa maji hapa Bunda mjini utakaokuwa nachanzo chake kwenye kijiji cha Nyabehu kilichopo umbali wa kilomita 26 kutoka hapamjini.Mradi huu ni mkubwa sana ukiangalia gharama zake hadi hapo utakapo kamilika, nautaona kuwa umekuwa ukitengewa fedha kidogo hadi kupelekea utekelezwe kwaawamu kadiri fedha zilivyokuwa zinapatikana, kwani kusubiri fedha hadi zitimie zotendiyo mradi uanze kujengwa haukuonekana kuwa ni uamuzi mzuri.Kwa fedha zilizokuwa zinapatikana, mradi huu umetekelezwa kama ifuatavyo;Awamu ya I: Zimenunuliwa pampu mpya 9 za kusukuma maji na tayari zipo hapa Wilayani Bunda zimetunzwa kwenye Bohari yetuAwamu ya II: Umefanyika ujenzi wa i. Tengi la maji Migungani lenye ujazo wa lita 225,000 ii. Tengi la kwenye Mlima Kaswaka lenye ujazo wa lita 675,000 iii. Nyumba ya kufunga pampu (Pump House) iv. Nyumba ya wahudumu wa pamp (pump attendant house) na choo yake v. Barabara ya kwenda kwenye tengi la maji kwenye Mlima KaswakaAwamu ya II: Awamu hii bado haijatekelezwa lakini itahusisha kazi zifuatazo • Ujenzi wa chujio (treatment plant) • Kununua na kulaza mabomba ya bomba kuu kilometa 26 • Kusimika pampu 3
 4. 4. • Kuingiza umeme wenye msongo mkubwa, na • Kusuka mtandao mpya wa usambazaji maji hapa mjiniMh. Mgeni RasmiAwamu hii ya tatu ndiyo awamu inayohitaji fedha nyingi zaidi kuliko awamuzilizopita. Makisio ya awali yanaonesha kuwa zitahitajika zaidi ya shilingi billion kumi(10Billions) kukamilisha mradi huu kiasi ambacho ni kikubwa ukilinganisha natakribani billion moja ambayo imekwishatumika kwa awamu ya I na awamu ya II.Habari njema ni kwamba, mradi huu sasa utatengewa bajeti kubwa kwenye mwaka wafedha wa 2011/2012 ili ukamilike. Hii pia imepewa uzito na kauli ya Mh Waziri wa MajiJana tarehe 16/3/2011 kwenye uzinduzi wa wiki ya maji pale alipo thibitishia ummakwa kusema, nanukuuu “ sasa tumedhamiria kuukamilisha mradi wa Bunda natutaukamilisha” mwisho wa kunukuu.Hata hivyo mheshimiwa mgeni rasmi kazi za awali za maandalizi ya awamu hii ya tatuzimeshaanza kufanyika kwani mhandisi mshauri ameshapatikana na anafanya kazi yakuandaa zabuni za ujenzi wa chujio, zabuni za ununuzi na utandazaji wa mabomba yamaji, na anaandaa zabuni za uwekaji umeme wa msongo mkubwa na usimikaji wamitambo.Mradi huu kwa ujumla unasimamiwa na Mamlaka ya Maji taka na Maji Safi Musomakwaniaba ya Wizara ya Maji na kwa upande wa Halmashauri wapo Mamlaka ya Majiya Bunda.Mh. Mgeni RasmiShughuli za awamu ya II ya mradi ambazo pamoja na kazi zingine ilihusisha ujenzi watengi hili hapa tulipo kwenye Mlima Kaswaka, umechukua mwaka mmoja kutokatarehe 18/1/2009 hadi tarehe 31/12/2009 kwa gharamu ya Tsh. 226,567,000. Tengilimejengwa kwa zege kali na nondo imara na limejengwa juu ya mwamba wa mawe ili 4
 5. 5. kuwa imara muda wote. Tengi limejengwa na mkadarasi wa daraja la juu kabisa naamelijengwa kwa kiwango bora kabisa na limejazwa maji na halivuji maji.Naomba kurudia eneo hilo kwamba tengi letu ni imara wala halivuji maji na hivi sasalina maji yamo ndani ya tengi yamejaa na hayavuji hata kidogo.Mh. Mgeni RasmiPamoja na jitahada hizo zote hapo juu lakini Mamlaka ya Maji inachangamotombalilmbali ambazo inakabiliana nazo, changamoto hizi ni; i. Miundimbinu ya maji inahujumiwa kwa bomba kutobolewa na wafugaji wa vijiji vya Guta, Tairo na Migungani ii. Uchakavu wa miundombinu ya maji hasa mabomba na mitambo iii. Kukatika nishati ya umeme mara kwa mara kumesababisha kuunguza pampu zetu za maji na vifaa vyake iv. Watumiaji maji kutolipa Ankara zao za maji kwa wakati v. Maji yanayosukumwa kutokidhi mahitaji ya jamii vi. Ukosefu wa fedha za kulipia Billi ya Umeme kwani ruzuku mara inakuja kidogo au miezi mingine ruzuku haiji kabisa na TANESCO hutishia kwa kutoa masaa 48 kuwa wasipolipwa bili yao watakata umeme kwenye mitambo yetu ya maji bila kujali kuwa Hospitali yetu ya wilaya (DDH) nayo itakosa maji ikiwa ni pamoja na wao wenyewe TANESCO watakosa majiHata hivyo Mamlaka ya maji Bunda ina mikakati kadhaa ili kukabiliana na changamotohizi. Mikakati yenyewe ni pamoja na; • Ukamilshaji wa mradi mpya wa maji wenye chanzo chake Nyabehu • Kuendelea ukarabati wa miundombinu ya maji kwa kutumia fedha kidogo tunazokusanya kwa wateja kila mwezi 5
 6. 6. • Ofisi ya Mkuu wa wilaya kusaidia namna ya kudhibiti hujuma na kwa Kutumia vyombo vya dola kama vile Mahakama, Polisi na serikali za Vijiji kusaidia kudhibiti hujuma dhidi ya miundombinu yetu • Kuendelea kuiomba serikali kutoa fedha za ruzuku kwa wakati kama ilivyo kwenye bajeti ili shughuli zisikwameMh. Mgeni RasmiHitimishoTunapenda kutoa rai kwa watumiaji maji kulipia Ankara zao za maji kwa wakati nakuwaasa waepukane na utumiaji wa maji salama kwa Bustani, kuoshea magari n.k Piawasikubali kuchepusha maji yasipite kwenye mita kwani kwa kufanya hivyo ni kosa lajinai na wanaweza kushitakiwa kwa mjibu wa sheria. Wananchi waisaidie Mamlakayao kufichua waovu wanaoihujumu Mamlaka isisonge mbele.Mh. Mgeni RasmiNapenda pia kutumia nafasi hii kukushukuru wewe binafsi kwa kukubali mwalikowetu na kuwa nasi hapa leo. Pili niwashukuru kwa namna ya pekee wenzetu waMamlaka ya Maji Bunda kwa kufanikisha shughuli hii ya uzindizi wa wiki ya Majihapa wilayani kwetu Bunda. Niwashukuru watumishi wa idara ya maji kwa ujumla nakwa umoja na ushirikiano wao kufanikisha shughui hii na nawaomba waendelee hivyohivyo hadi tumalize Wiki ya Maji. Niwashukuru watumishi na wananchi waliofikahapa na kwa namna ya pekee niwashukuru waandishi wa habari wa TV, Radio namagazeti.Maji ni Uhai na Usafi wa Mazingira ni UtuWiki ya Maji OyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeAksanteni kwa kunisikiliza 6

×