SlideShare a Scribd company logo
MAONO YA BWANA KUHUSU KANISA LA TANZANIA
UJUMBE WA BWANA NA UFUNUO KUHUSU KANISA LA BWANA MNAMO TAREHE
ISHIRINI NA MBILI MWEZI WA SITA MWAKA ELFU MBILI NA TISA (AMOSI 9:11-12)
Bwana Munug mtakatifu wa Israel katika maono yake kuhusu nchi ya Tanzania nikiwa Mji wa Eldoret
sehemu ya Langa’s kwa mwangalio wa ramani alinena nami haraka sana kuhusu nchi ya Tanzania na
kanisa lake alilolipenda.
1. MAONO YA KWANZA YA BWANA
1) Bwana akanionyesha mti wa tunda ambao ni kijani kibichi(kiasi) lakini usio na matunda
yake na wenye afya nzuri ukiwa umetanda juu ya choo kikongwe.
UFUNUO ULIOMO KATIKA MAONO HAYA YA BWANA.
Mti huo wa kijani kibichi ambao hauna matunda una ishara ya kuwa kanisa la Bwana katika nchi ya
Tanzania limekuwa linaonekana kuwa na uzuri usio na matunda au tunda la Toba ilihali limekuwa
likifanya toba mbele za Bwana Mungu mtakatifu katika machhozi, magotini na mavumbini. Hii
inadhihirisha kuwa hili kanisa limekuwa na Toba ya unafiki isiyobadili moyo, na kutakaswa kwa damu ya
Yesu na Roho Mtakatifu. Kanisa halijamgeukia Mungu kikamilifu katika moyo, limemdhihaki Mungu
katika Toba huku kwa hekima yake ya kiulimwengu (Theologia au masomo ya kidini) likijaribu kumjua
Mungu kwa vinywa vyake huku moyo wake ukiwa mbali naye (Isaya 29:13) Mungu aliona kanisa ambalo
limejaribu kumfurahisha kwa aina Fulani ya uungu huku likikana nguvu za utauwa (Roho mtakatifu)
(2 Timotheo 3:5)
Mti huo kutanda juu ya chumba cha choo. Choo ni uchafu unaotoka kwenye tupu ya mbele au ya
nyuma(mavi au mkojo) pia ina maana ya mahali pa kwenda haja.
Hali hii ina sehemu mbili za ufunuo.
1) Kanisa hili lafaa kutubu katika Kristo Yesu wa Nazareti (Matendo ya Mitume 2:21, Warumi
10:13)
2) Kanisa hili limekuwa likitubu lakini pasipo kuzaa tunda lipasalo Toba maana yake ule mti usio na
tunda, limekuwa kwa muda mrefu likitubu na kuungama dhambi lakini pasipo kuzaa tunda la
Toba. Kuna hali pia ya kuchoka kutubu na pia mazoea ya Toba lakini matunda yake hayaonekani
hata kwa kitambo hicho.
Hivyo ina maana ya kuwa kanisa hilli la Tanzania lafaa kutubu au kumrudia Mungu na kuacha kila
uovu kwa jjina la Yesu Kristo wa Nazareti. Ishara hii ni kwamba lazima sasa kanisa hili la nchi ya
Tanzania litubu kikamilifu bila kujadiliana na shetani kwa vyovyote vile na kisha kuzaa tunda
lipasalo Toba. Ujumbe uliojificha hapa ni kuwa lazima kanisa lijitenge na dhambi kwa kumrudia
Mungu mtakatifu wa Israeli kwa kuanza kutembea kwa utakatifu na haki ya Mungu (tunda lipasalo
Toba) kile chumba cha choo kinamaanisha kuwa hili kanisa la Tanzania linafaa sasa kuingia katika
msimu wa Toba kwa ajili ya kanisa kujitoa au kujikwamua kutoka kwa dhambi za kila aina kupitia
kwa Damu ya Yesu Kristo wa Nazareti na jina hilo pekee liwe mwangaza wa ulimwengu na
chimvi ya Dunia (Mathayo Mtakatifu 5:13-16)
Mathayo 3:7-10 “Hata alipoonoa wengi miongoni mwa mafarisayo na masadukayo wakiujia ubatizo
wake, aliwaambia, Enyi wazao wa nyoka, ninani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasiraa itakayokuja? Basi
zaeni matunda yapasayo toba, wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba tunaye baba ndiye Ibrahimu; kwa
maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimi watoto. Na shoka
limekwisha wekwa penye mashina ya mti: kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni!
2. MAONO YA PILI YA BWANA
(2) kisha Bwana akanionyesha mti wa mwiba au mti wa mwiba wa aina ya Mgunga, mmea huu
hupatikana katika sehemu zifuatazo; kavu, Jangwa na nyika. Mti huu hutumika katika
kuchoma mkaa wa kupikia, una ngozi nzito sana na yenye upana
UFUNUO ULIO KATIKA MAONO HAYA YA BWANA.
Mti huo wa mwiba ulikuwa na ishara ya kwamba kanisa la Bwana katika nchi ya Tanzania lafaa kwenda
na kumtolea Bwana ibada kule nyikani au jangwani. Hii ni ibada ya lazima kwa Mungu maana ni mbinu
pekee atumiayo kuwatoa watoto wake katika ufungwa au Misri ya roho na mwili ili wamtolee dhabihu.
Kutoka 5:1, 3;18 “Hata baadaye Musa na Haruni wakaenda wakamwambia Farao wakasema Mungu wa
Israeli asema hivi, wape watu wangu ruhusa waende ili kunifanyia sikukuu jangwani” Mungu aliliona
kanisa lake likiwa katika ufungwa wa wa Misri wa rohoni
1) Rohoni- kupagawa na pepo, magonjwa ya roho, kuteswa na mapepo, kukosa uhuru wa kuabudu
(mipangilio nyeti ya kidini ambayo haijamruhusu roho mtakatifu kutenda kazi katika kanisa)
kutotakaswa katika roho na nafsi (1 Wathesalonike 5:23)
2) Mwilini- Magonjwa, maumivu ya kila aina, kukosa uhuru (Sheria na mafundisho yasiyo ya
kibiblia) na mtendo ya mwilini ambayo ni dhahiri (waraka wa Paulo Mtume kwa Wagalatia
5:19)
Hivi ina maana kwamba moyo wa Mungu unalia kwa sababu wa watoto wake ambalo ndilo kanisa kwa
ajili ya ufungwa huku akitamani kuwa kanisa hili limtengenezee sikukuu jangwani. Kumbuka ya kwamba
sherehe hii ni ya kutoa ibada kwa Mungu katika heshima na utukufu. Ibada ni tendo la kumwabudu
(kumpa heshima na Utukufu) Mungu. Hii ibada anayoinena ni ile ifanyikayo kulingana na maandiko yake
matakatifu kulingana na agano lake kwao. Kabla yao kuondoka Misri kwenda jangwani kumfanyia Bwana
sikukuu Mungu aliwaamuru kufanya maandalizi yafuatayo (Kutoka 12:1-50)
1) Kumtwaa mwanakondoo ambaye angechinjwa na damu yake kupakwa au kutiwa katika miimo
miwili na katika kizingiti cha juu . hiyo ni ishara ya Bwana wetu Yesu kristo kusulubiwa
msalabani na damu yake kutumika kuwa dhabihu tosha utumwani Misri (12:8)
2) Watakula nyama yake usiku ule ule ambayo imeokwa motoni. Hii ni dhabihu inayoteketezwa kwa
moto (Roho mtakatifu na majaribu ya wateule) kuna uharaka wa kanisa hili kumtolea Mungu
dhabihu zilizoteketezwa kwa moto wa roho mtakatifu na kupita katika majaribu ya kuandaa
vyombo vya dhahabu kwa Mungu (12:8)
3) Pia wangekula na mkate usio tiwa chachu. Huu ni mkate ulo safi bila uzinzi, uasherati, uabudu
sanamu, vinyago, wizi, uongo, ufisadi, upendo wa fedha wa fdha, uabudu shetani, udini, na ibada
za uchafu wa uchawi wa kiroho (ujanja, kuogofya, sifa nyingi kupita kimo, utawala au mamlaka,
kuendesha mambo na kukosoa) inamaana kuwa lazima wangemtolea Bwana dhabihu isiyo na
dhambi na inajisi bali takatifu na safi na yenye haki ya Mungu. Kumbuka chachu huifanya mikate
kuwa na kuvimba na kuwa na ladha ya ukali (unajisi, umwili, uchafu na kutokuwa takatifu) hivyo
walifaa kumtolea Mungu dhabihu takatifu. Kanisa hili lafaa kutoa dhabihu takatifu isiyo na uchafu
wa aina yoyote. Kanisa la nchi ya Tanzania limemtolea Mungu dhabihu za upendo wa fedha,
udini, uabudu, shetani, mapepo, na majini, utumizi wa hirizi, kiburi na majivuno, kupenda uzinzi
na uasherati, uganga na ushirikina ambavyo Bwana asema lazima kanisa hili litubu na kumrudia.
4) Walifanya kula mboga zenye uchungu ambayo ilikuwa na maana kuwa wangeondoka katika
ufungwa na kuponywa na Mungu wao na kuwarejesha, kuwabariki na kuwainiua. Mara nyingi
katika Israeli mboga hutumika katika kutengeneza dawa itumiwayo kuponya magonjwa ya kila
aina. Kwa hivyo Mungu alikuwa akiliponya kanisa lake kutokana na uchungu lililopitia katika
Misri ya kiroho na kimwili na kisha kuwekwa huru (12:8)
MAONO YA TATU YA BWANA
Hatimaye Bwana akanionyesha mashine ambayo hutumika kusaga mtama, ngano, mahindi au
nafakailiyovunwa ili kupata unga mwororo wa kupikia vyakula kama vile vyapati, maandazi, keki na
vinginevyo. Nje ya kile chumba cha mashine hiyo kulikuwa na chekecheo ya chuma ikiwa na vyombo
vingi vya plastiki au mpira vya kila aina katika umbo la rangi.
UFUNUO ILIOMO KATIKA MAONO HAYA.
Mashine haya kwa kawaida hutumika kuutengeneza unga kwa kusaga mtama au nafaka ya kila aina ili
kupikia vyakula vizuri kama vile vyapati, maandazi, keki na vinginevyo. Huo unga huwa ni mwororo na
wenye usafi kiwango cha juu sana. Hili ndilo neno la Bwana kwa kanisa hili la Tanzania. Kanisa hili lafaa
sasa kuendelea katika nyumba ya mfinyanzi ili kupokea neno la Bwana (Yeremia 18:1-6)
“neno hili ndilo lililomjia Yeremia kutoka kwa Bwana kusema ondoka, ukashuke mpaka nyumba ya
mfinyanzi na huko nitakusikizisha maneno yangu. Basi nikashuka mpaka nyumba ya mfinyanzi na tazama
alikuwa akifanya kazi yake kwa magurudumu na chombo kile alichokuwa aifinyanga kilipoharibika
mkononi mwake Yule mfinyanzi alikifanya tena kuwa chombo kingine kama alivyoona vema Yule
mfinyanzi kukifanya. Ndipo neno la Bwana likanijia kusema Ee nyumba ya Israeli je siwezi mimi
kuwatendea nyinyi vile vile kama mfinyanzi huyo alivyo tenda? Asema Bwana, angalieni kama udongo
ulivyo katika mkono wa mfinyanzi, ndivyo mlivyo ninyi katika mkono wangu, Ee nyumba ya Israeli”
baada ya kanisa hili kwenda katika chumba cha mfinyanzi litafinyangwa, kuyeyushwa, kutakaswa na
kuoshwa pamoja na kutengenezwa kama jinsi Mungu apendavyo. Kumbuka kuwa kanisa hili laweza tu
kupokea neno la Bwana katika nyumba ya Mfinyanzi kupitia kwa.
1) Damu ya Yesu yenye dhamana (Waebrania 9:11-14)
2) Roho Mtakatifu (Yohana Mtakatifu 16:8-15)
3) Moto wa Roho Mtakatifu (Mathayo Mtakatifu 3:11)
Baada ya hili kanisa la Tanzania kupitia katika mashine (nyumba ya mfinyanzi) kanisa la Tanzania
litaanza kutenda mapenzi ya Mungu, kuishi katika utakatifu na haki kwa kutii sauti ya Mungu na kutenda
neno lake. Kanisa hili pia litakua na hofu ya Bwana moyoni. Picha ya hili kanisa itakua ifuatavyo:-
1) Litakuwa huru na chumvi ya ulimwengu (Mathayo Mtakatifu 5:13-16)
2) Litajaa miujiza ya Mungu (Danieli 12:9-10)
3) Litajaa ibada kamilifu yenye manukato kwa Bwana Mungu wa Mbinguni (Warumi 12:1-2)
4) Litastahimili majaribu, kuudhiwa na mambo yote yale magumu yanayohusu imani katika Kristo
dhahiri katika kanisa hili la Mungu mtakatifu wa Israeli(Waraka wa Paulo Mtume kwa
Wagalatia 5:23)
Lile chekecheo la chuma ndilo lilepimo atakalotumia Mungu kutenga kanisa takatifu kutokana na dhambi,
uchafu na kila uovu wa kila aina. Bwana ataliinua kanisa takatifu na kuliondoa uchafu na kila uovu ili
liandaliwe kwa ajili ya ufalme wake wa Mbinguni Mathayo 3:12 “ambaye pepeto lake mkononi mwake,
naye atausafisha sana uwanda wake na kuikusanya ngao yake ghalani bali makapi atayateketeza kwa moto
usiozimika” chekecho hilo ni damu ya Yesu, Roho mtakatifu na moto ambacho ndicho kipimo cha pekee
cha kujipatia kanisa takatifu lenye kuisikiliza sauti ya Mungu wa Mbinguni. Hali hii inahusika na:-
a. Kutenga kanisa na dhambi.
b. Kutenga wenye haki na wasio haki wajifanyao kuwa safi.
c. Kurejesha utakatifu na kuondoa dhambi na uovu.
Kanisa la nchi ya Tanzania linafaa kujiandaa na kuingia katika pasaka ya kuondoka Misri (Kutoka 12:1-
15) Baaada ya hayo kanisa hili lafaa kuondoka Misri na kwenda jangwani ili kumtolea Bwana dhabihu
kulingana na sheria ya Bwana kwa pasaka ili alipokee kanani katika Baraka zake.
(Yeremia 8:4-9) Huu ndio msimu wa kanisa la nchi ya Tanzania kwenda katika jangwa au nyika ya
uyahudi kwa ajili ya Toba kwa Mungu katika hali ya unyenyekevu. Mathayo 3:1-3 “ siku zile Yohana
mbatizaji akihubiri katika nyika ya uyahudi na kusema tubuni kwa maana ufalme wa Mbinguni
umekaribia kwa sababu huyoo alienenwa na Nabii Isaya akisema, sauti ya mtu aliaye nyikani itengenezeni
njia ya Bwana yanyoosheni mapito yake” Manthari ya jangwani ni kama ifuayavyo; hamna mimea ya
kutosha, hamna maji na njia za kupita, kiangazi au jua ni kali, mchana ni mwingi na vumbi, hakuna
mimea kwa wingi, wadudu na wanyama wengi waharibifu kama nge, nzige, nyoka wa jangwani, mawe
mengi, miti ya miiba, ukosefu wa nyumba za kuishi, mapango ya mashimo yaliyo kaukiwa na maji kwa
sababu ya jua kali. Haya mandhali ya jangwa au nyika yana maana kuu sana katika maisha ya hili kanisa
la Bwana humu nchini Tanzania. Kuanzia kanisa hili lafaa kwenda katika unyenyekevu: kujinyima na
kujitenga na ulimwengu kwa ajili ya kufanya Toba ya kipekee nay a kweli ili kumrudia Mungu. Hii ni
katika hali ya kujitenga na maisha yake ya kawaida kama vile kula, kunywa, maisha ya raha na ukawaida
wa ibada(Injili ya hema la nje la mwili, idaba ya uzinzi, upendo wa fedha, mazingira ya uchafu war oho na
mwili) hali hii inahusishwa na:-
1) Kufunga na kuomba
2) Kujitenga na maisha ya makundi ya kawaida
3) Kujiondoa katika raha za kidunia
4) Kuwa na hofu ya Mungu (kumheshimu Mungu)
5) Kuhubiri injili ya uwezo wa Roho isiyijadiliana na dhambi.
Ukweli ni kwamba kanisa hili lafaa kuingia katika msimu wa Toba na kujitakasa ili kupata msamaha na
ondoleo la dhambi. Katika hali hii ya kanisa hili kutubu na kumrudia Mungu lafaa pia kufanya ubatizo wa
waraka tu pindi mtu anapookoka katika maji mengi. Hiyo ibada ya kanisa la jangwani ina hali ya kukemea
dhambi pasipo kujadiliana hadi watoto wa Mungu kutubu, kubatizwa na kujazwa Roho Mtakatifu
(Mathayo 3:4-17) Kumbuka kuwa kanisa hili la Bwana lafaa kwenda jangwani na kuandaa njia ya Bwana
Mungu mtakatifu wa Israeli. Njia hiyo ni Toba ya kweli maana Mungu wa Mbinguni ni Mtakatifu
(Waraka wa kwanza wa Petro 1:13-16) Baada ya mambo ambayo kanisa hili lafaa kujitenga nayo ni
kama ifuatavyo:-
(1) Upendo wa fedha (1Timotheo 6:10) (2)Michezo ya kuigiza madhabahuni (3)Michezo ya densi
za kiasherati na uzinzi madhabahuni (4)Dhabihu za kimwili (5) Mavazi ya kiasherati na
kiuzinzi (6) Mizaha katika madhabahu ya Bwana (7) Ufisadi katika madhabahu ya Bwana (8)
Upendeleo katika madhabahu ya Bwana (9) Unafiki na tabia za masadukayo na mafarisayo
madhabahuni mwa Bwana (10) injili ya kigeni, mafundisho ya uongo na Philosophia,
Theologia katika madhabahu ya Mungu isiyo na manufaa kwa maisha ya rohoni (11) ibada ya
sanamu, shetani na vinyago madhabahuni (12) kupigania mamlaka, vyeo na madaraka
kanisani. Basai kanisa hili lafaa kwenda katika ibada, haki na utakatifu ili Mungualisamehe na
kuliponya kwa yale maovu yote ambayo limemtenda Mungu na kisha kuliinua hilo kanisa
katika roho na kweli kwa utukufu wa jina lake. Mwisho ni kwamba sasa wakati wa kiunabii wa
kulirejesha kanisa la Tanzania katika utakatifu basi ndio huu asema Bwana wa
mabwana(Yeremia 8:4-9) Amani ya Bwana na iwe nanyi.
Hii inamaana kuwa ni kitakatifu pekee ambacho kitabakia katika madhabahu ya Bwana kwa kazi yeyote
ile nzuri. (Waraka wa pili wa Mtume Paulo kwa Timotheo 2:19-21) “ lakini msingi wa Munguulio
imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake na tena kila alitajaye Jina la Bwana na
auache uovu. Basi katika nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu bali na vya mti, na
vya udongo, vingine vina heshima , vingine havina. Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga nao
atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana kimetengenezwa kwa kila kazi
iliyo njema” ukweli ni kwamba kanisa hili lazima lijitenge na dhambi na uovu wa kila aina ili litumike na
Bwana kwa kazi nzuri yenye kumletea Mungu sifa na utukufu. Toba ya kilindi cha moyo yafaa kufanywa
na kanisa hili ili kusamehewa na kusafika kwa dhambi na udhalimu wa aina yeyote. Hivyo hatua ndiyo ya
pekee ya kuzaa kanisa takatifu litakalo urithi Ufalme wa Mbinguni. Ajabu ni kwamba hili kanisa
laonekana kuwa katika mwili na matendo yake yakiwa dhahiri(Wagalatia 5:19). Hii inaashiriwa na
vyombo vya aina hii vikiwekwa kwenye moto huteketea na kuwa jivu. Kanisa hli la Tanzania
linapopitishwa katika m,ajaribu au mates kwa ajili ya Yesu tabia dhahiri ni ile ya kanisa kuugua na
kuteketea, yaani:-
1) Kuiacha imani (Yeremia 10:20, 3:11na 22)
2) Kurudi nyuma (Yeremia 3:21)
3) Kujadiliana na shetani na kumuacha Mungu na kugeukia miungu (Isaya 28:15)
Wnegi wa watoto wa Mungu katika kanisa hili hawawezi kustahimili majaribu yanapo wakumba katika
safari. Hii hali yaashiria mambo yafuatayo:-
1) Kuiacha imani (Yeremia 10:20,3:11na 22)
2) Kurudi nyuma (Yeremia 3:21)
3) Kujadiliana na shetani na kumuacha Mungu na kugeukia miungu(Isaya 28:15)
Wengi wa watoto wa Mungu katika kanisa hili hawezi kustahimili majaribu yanapowakumba katika
safari.Hii hali yaashiria mambo yafuatayo.
1) Kutoshika imani ya kweli katika kristo Yesu Mnazareth
2) Kutokomaaa katika imani
3) Kutozingatia neno la Mungu kikamilifu
4) Kutotii sauti ya Mungu na kutotenda mapenzi ya Mungu
5) Ukosefu wa utakaso mkamilifu wa Mungu (wakara wa kwanza wa Paulo mtume kwa
wathesalonike 5:25).
6) Kutompenda Mungu kwa moyo wote
7) Kutovaa vazi la ufalme wa Mbinguni (vazi la mwana kondoo wa Mungu).
8) Michezo au dansi za kimwili kanisani.
Kanisa hili lazima litubu na kujitakasa kikamilifu asema Bwana wa Mabwana.
4. MAONO YA NNE YA BWANA.
Bwana Mungu mtakatifu wa Israel kisha akanionyesha birika la chuma katika sehemu ya kisima
chenu.
UFUNUO ULIO KATIKA MAONO HAYA.
Kanisa la nchi ya Tanzania limemuacha Mungu na kuigeukia miungu nyingine kama vile ya fedha
na dhahabu,ya madhehebu na dini,uchawi na uganga ,ushirikina na muingu ya ibda ya mashetani
kama vile legio maria, mizimu pamoja na hirizi,Baali, yezebeli, lucifa, malkia wa mbingu,
Asheroh.
 Kanisa hili pia lina ibada ya sanamuna vinyago 1wafalme 18:1-46,ufunuo 16:2-28,isaya
28:11-15,yerema 1:17-20.
 Kanisa hili la Tanzania limeuacha msaada wake wa pekee na kugeukia misaada mingine
kama vile Misri na Ushelisheli, Kugeukia wachawi kutaka upako wa uongo wa kutenda
miujiza,waganga na wapiga ramli kwa utendaji wa miujiza kunao tumia nguvu za giza
kutenda miujiza ya uongo ya uponyaji na ukombozi ,waimbaji na wahubiri kwenda kutafuta
upako Baharini,na kishetani ili kutenda miujiza na huduma ya Mungu kanisani.
 Kanisa pia lina ibada ya mambo asili ya ulimwengu huu na kumsahau Mungu wa Israel.
Kila kisima kina maana ya kanisa la humu nchni Tanzania.Hivi ni kwamba kanisa la Mungu katika nchi
ya Tanzania linaabudu miungu mingine kama ya kikabila ,madhehebu na dini(Yeremia 7:17-20) Je!
huoni wanavyotenda katika miji ya Yuda na katika njia kuu za Yerusalemu? Watoto huokota kuni na
baba zao huwasha moto na wanawake hukanda unga ili kimfanyizia mikate malkia wa mbinguni na
kuwamiminia miungu mingine sadaka za vinywaji wapate kunikasirisha mimi.Je! watu hawa
wananikasirisha mimi? Asema Bwana hawajikasirisha nafsi zao na kuzitia haya nyuso zao wenyewe? kwa
hiyo Bwana Mungu asema hivi:Tazama hasira yangu na ghadhabu yangu zitamwaga juu ya mahali hapa.:
juu ya wanadamu, na juu ya wanyama, na juu ya juu ya mashamba, na juu ya mazao ya nchi nayo
itateketea’’
Yeremia 19: 1 – 6
Ukisema lisikieni neno la Bwana , enyi wafalme, wa yuda na wenyeji wa yerusalemu: Bwana wa majeshi,
Mungu wa Israeli asema hivi, Angalieni, italeta mabaya juu ya mahali hapa, ambayo mtu yoyote Yule
akisikia habari yake masikio yake yatawaka. kwa sababu wameniacha mimi nao wamepafanya mahali
hapa kuwa mahali pageni nao hapa wamewafukizia uvumba miungu mingine wasiowajua, wala wao, baba
zao, wala wafalme wa yuda : nao wamepajaza mahali hapa damu ya wasio na hatia nao wamemjengea
Baali: tendo nisiloliamuru mimi wala kulinena wala halikuingia moyoni mwangu basi angalieni siku
zinakuja asema Bwana katika siku hizo mahali hapa hapataitwa tena Tfethi, wala bonde la mwana wa
hinomu bali bonde la machinjo?
5. MAONO YA TANO YA BWANA
Kisha Bwana akanena nami kuhusu uchafu ulio katika madhehebu yenu na ukosefu wa maji safi ya
kunywa hata kufulia ( yeremia 7: 9 – 10)
“je mtaiba na kuua na kuzini na kuapa kwa uongo na kuvukizia baali uvumba na kuifuata miungu
mingine ambayo hamkuijua. Kisha mtakuja na kusimama mbele zangu katika nyumba hii iitwayo kwa jina
langu ,mkisema tumepona ili mpate kufanya machukizo haya yote?”
UFUNUO WA MAONO HAYA.
Ninyi watu wake Mungu mmelinajisi hekalula Bwana Mungu wenu kwa dhambi kama vile ngono,
ushirikina,uchawi(wa mwili na roho).Haya mambo mmeyatenda hata madhabahuni mwa Bwana Mungu
wetu,kwa sababu ya uchafu na unajisi huo katika madhabahu ya Bwana.Hamna tena maji safi (Roho
mtakatifu na neno la Mungu)ndani ya nyumba ya Mungu kwani kisima chake kilizibwa na usafi kuondoka
kwa uovu wenu asema Bwana wa majeshi.Mto wa roho mtakatifu wenye maji safi haupo tena
madhabahuni mwa Bwana kwa sababu ulizibwa kwa matendo yenu maovu. Hivyo Mungu mkuu na
mtakaifu wa Israel aona chumba ambacho kimetiwa unajisi na maji yake kuwa chafu yenye kufisha
kondoo wake na kuharibu afya yake.Lazima kanisa la nchi hii ya Tanzania lafaa kurejelea utakatifu kwa
toba ya kilindi cha moyo itakayomsababisha Roho mtakatifu kulitembelea kanisa,kuwa na ushirika nalo
ili kuliuisha, kuliponya na kulikomboa, kutoka katika ufungwa wa misri ya mwilini na rohoni, asema
Bwana Mungu wa majeshi (Yeremia 6:7).
‘Kama vile kisima kitoavyo maji yake, ndivyo utoavyo uovu wake jeuri na kuharibu kwa sikiwa ndani
yake,ugonjwa na jeraha za mbele zangu daima,uadhibishwe, Ee Yerusalemu,nafsi yangu isije ikafarakana
nawe,nisije nikakusanya ukiwa ,nchi isiyokaliwa na watu.
6. MAONO YA SITA YA BWANA KUHUSU KANISA LA TANZANIA.
Hatimaye Bwana akanionyesha mti mkubwa wa tunda ambalo haukuwa na matunda wala au lolote
lililoota juu yake kulikuwa na joka mwenye rangi ya kijani kibichi sawia na ule mti lakini ikiwa na vipaji
vyeusi sehemu sehemu mwilini mwake.Akaniruhusu kulichukua jiwe na kulitupia jiko kisha joka kwa
upesi sana lilitoweka.Mti huo ulikuwa umetandaa juu ya ukuta mkongwe uliokuwa umezingira nyumba
iliyokuwa imejengwa kwa mfano wa kanisa ,ulikuwa ukiwa sana
UFUNUO ULIO KATIKA MAONO HAYA
1. Mti usio na tunda una maana kuwa kuna hali ya toba ambayo si ya kuzaa matunda au tunda
lipasalo toba katika kanisa hili lake la Tanzania (Mathayo 3:7-10).
“Hata alipoona wengi miongoni mwa mafarisayo na masadukayo wakijua ubatizo wake aliwaambia enyi
wazao wa nyoka ni nani aliyewaloga ninyi kuikimbia hasira itakayo kuja? Basi zaeni matunda yapasayo
toba, wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba tunaye baba ndiye Ibrahimu kwa maana nawaambia ya
kwamba aweza katika mawe hayo kumwinulia Ibrahimu watoto.Na shoka limekwisha kuwekwa kwenye
mashina ya mti, basi kila mti usozaa matunda hukatwa na kutupwa motoni”
Hivyo kanisa hili lafaa kubadili mawazo yake kuhusu kumurudia Bwana na kuanza kumrudia Mungu
kikamilifu na kurejea utakatifu pamoja na kujazwa Roho mtakatifu.
2. Nyoka ni alama tosha kuwa kanisani hili lina uabudu wa shetani, miungu mingine ambayo
imelinajisi kanisa hili la Tanzania. Kuna ibada pia inayotolewa kwa miungu ya upendo wa
miungu (mara nyingi huwaongoza watu kufanya uzinzi na uasherati, ukahaba na tabia mbovu
za kingono) (Isaya 28:14-15)
“Basi sikieni neno la Bwana enyi watu wenye dharau mnaowatawala watu hawa ndani ya Yerusalemu
kwa sababu mmesema tumefanya agano na mauti, tumepatana na kuzimu, pigo lifurikalo litakapo pita
halitatufikia sisi kwa maana tumefanya maneno ya uongo kuwa kimbilio letu, tumejificha chini ya maneno
yasiyo kweli”
3. Yule joka kufanana na ule mmea ni dhahiri kwamba kuna hali ya kukubaliana na uabudu wa
shetani (yeremia 7: 30-31) “Maana wana wa yuda wametenda yaliyo maovu machoni pangu
asema Bwana, wameweka machukizo yao ndani ya nyumba hiyo iitwayo kwa jina langu, hata
kuitia unajisi.Nao wamepajenga mahali palipoinuka pa Tofethi palipo katika bonde la mwana
wa hinomu ili kuwateketeza wana wao na binti zao motoni. Jambo ambalo mimi sikuliagiza
wala halikuingia moyoni mwangu”.
4. Kuna haja kubwa ya kumuondoa shetani katika madhabahu ya Bwana ili yasafike na kuwa safi.
Hii ni kupitia tu kwa toba katika kristo yesu Mnazareti (Yeremia 4: 1- 4)
“Kama ukitaka kurudi, Ee Israel, asema Bwana utanirudia mimi na kama ukitaka kuyaondoa machukizo
yako yasiwe mbele ya macho yangu. Ndipo hutaondolewa nawe utaapa hivi, kama Bwana aishivyo, katika
kweli na katika hukumu, na katika haki ndipo mataifa watajibariki katika yeye,nao watajitukuza katika
yeye.Maana Bwana awaambia hivi watu wa Yuda na Yerusalemu,ulimeni udongo katika konde zenu wala
msipande mbegu kati ya miiba.Jitahirini kwa Bwana,mkaziondoe ngozi za mioyo yenu enyi watu wa
Yuda na wenyeji wa Yesusalemu,ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto ikawaka hata mtu asiweze
kuizima kwa sababu ya uovu wa matendo yenu. Ndiyo sababu Bwana alinuruhusu kuchukua jiwe na
kulitupa lile joka na kisha likatoweka.
5. Ule ukuta uliokuwa mkongwe na kutandwa na matunda ni maana ya kuwa ukuta wa Roho wa
Bwana wetu Yesu Kristo ambao aliujenga kwa kazi ya msalaba umeachwa ukiwa (Yeremia
10:20-21) ukuhani hautimizi sheria ya ukuhani.(Malaki 2:1-11,Yer 12:10-11) na hali watoto
wa Mungu wanakaa katika starehe katika nyumba nzuri .Mwili wa Bwana wetu Yesu Kristo
umeachwa ukiwa na kuonekana kuwa mkongwe sana.Hakuna ulinzi na mwavuli wa Bwana
kwa kanisa.Mungu aliona kanisa ambalo limeachwa ukiwa na kuwa na hali ifuatayo:.
1. Ukosefu wa ibada na ukombozi wa kweli.
2. Kwa kuabudu sanamu na shetani
3. Uchawi,uganga,ushirikina na hirizi katika madhabahu ya Bwana.
Mungu basi anataka kanisa lake lianze kuoshwa kujengwa upya.Kurejeshwa kwa sehemu yake ya urembo
wake war oho.(Hagai 1:1-11,Hagai 2:5-9).
(Yeremia 6:7) Maana Bwana wa majeshi asema hivi jikatieni miti mfanyize boma juu ya Yerusalemu.Mji
ni mji unaojiliwa ,dhuluma tupu ndani yake.’
7. MAONO YA SABA YA BWANA KUHUSU KANISA LAKE LA TANZANIA
TAREHE 31 MWEZI WA TISA ,MWAKA 2009
Bwana katika mtembeleo wake alinichukua katika roho na kunionyesha sayari ikipita kutoka upande
mmoja wa mawingu juu katika mbingu hadi upande mwingine ,mawingu yalikuwa ya samawati na
shwari.Kulikuwa na mwezi mkubwa ambao ulikuwa shwari bila kusonga hata nukta.Sayari hiyo ilikuwa
kuu na yenye muundo wa trapeze.Hiyo sayari ilipita juu mbinguni kutoka sehemu ya kushoto hadi sehemu
tofaui hadi sehemu kinyume na ile ya kwanza.Hali hii ilikuwa ni dhimisho ya nyakati za mwisho kabla ya
siku ya Bwana.(Yoel 2:30-31)
Nami nitaonyesha mambo ya ajabu katika mbingu na katika dunia damu,na moto na minara ya moshi.jua
litageuzwa kuwa giza na mwezi kuwa damu,kabla haijaja siku hiyo ya Bwana iliyo kuu na itishayo.
UJUMBE ULIOMO KATIKA MAONO HAYA KWA KANISA LA YESU KRISTO.
Hii ni dhahiri kwamba nyakati za kiunabii kwa kanisa la Kristo zimebadilika.Maanake ni kwamba
tunaelekea katika upeo mkuu wa unyakuzi wa kanisa takatifu la Kristo Hii ni dhahiri kwamba nyakati za
kiunabii kwa kanisa la Kristo zimebadilika.Maanake ni kwamba tunaelekea katika upeo mkuu wa
unyakuzi wa kanisa takatifu la Kristo Yesu.
1. Kanisa lafaa kutubu kikamilifu na kujazwa kwa Roho mtakatifu kiwango cha mafuta ya
nyakati za mwisho (Matendo ya Mitume 2:38,Ezekiel 47:1-5)
2. Kanisa lafaa kutubu na kisha kuandaa njia ya Bwana yaani ufalme wa Mbingu (Mathayo
mtakatifu 3:1-3(2)
3. Kanisa lafaa kuvalia vazi la harusi ya mwanakondoo wa Mungu kitani nyeupe ing’arayo
(Ufunuo 6:9-11,Ufunuo 7:9,Ufunuo 19:1-8 Ufunuo 19:9).
4. Kanisa lafaa kujiandaa kusimama mbele ya kiti cha enzi cha hukumu (Ufunuo 20:11-15.)
5. Kanisa lafaa kumsikiliza Mungu kwa upesi na kujiandaa kurithi ufalme wa mbinguni.(Ufunuo
2:29,Ufunuo 3:22).
8. MAONO YA NANE KUHUSU KANISA LA TANZANIA ,TAREHE 31 MWEZI WA TISA SAA
KUMI NA MOJA.
Bwana kisha akanena nami kwa sauti kuhusu kuja kwake Yesu kulinyakua kanisa katika unyakuzi .Kwa
sauti akasema, kama mwivi ajavyo ndivyo itakavyokuwa kwa Mwana wa Adamu (Mathayo 24:42-51)
MTUMWA WA YESU VICTOR MSERE AKIDIVA
0719 434702
0762 179401.
MUNGU APEWE SIFA NA UTUKUFU.

More Related Content

What's hot

Academic excellence
Academic excellenceAcademic excellence
Academic excellence
Magori Kihore
 
Prayer manual 2013 by Elimringi Moshi 0714112062
Prayer manual 2013 by Elimringi Moshi 0714112062Prayer manual 2013 by Elimringi Moshi 0714112062
Prayer manual 2013 by Elimringi Moshi 0714112062
Elimringi Moshi
 
Kusudi la mungu kwa kanisa huduma na karama
Kusudi la mungu kwa kanisa   huduma na karamaKusudi la mungu kwa kanisa   huduma na karama
Kusudi la mungu kwa kanisa huduma na karama001111111111
 
Sadaka na-maana-ya-utoaji
Sadaka na-maana-ya-utoajiSadaka na-maana-ya-utoaji
Sadaka na-maana-ya-utoaji001111111111
 
Corpus christi 1 - in the bible (swahili)
Corpus christi   1 - in the bible (swahili)Corpus christi   1 - in the bible (swahili)
Corpus christi 1 - in the bible (swahili)
Martin M Flynn
 
Kanuni za kiroho za ushindi
Kanuni za kiroho za ushindiKanuni za kiroho za ushindi
Kanuni za kiroho za ushindi001111111111
 
Ujana na mafanikio
Ujana na mafanikioUjana na mafanikio
Ujana na mafanikio001111111111
 
Trinity (swahili)
Trinity (swahili)Trinity (swahili)
Trinity (swahili)
Martin M Flynn
 
Nguvu ya neno la mungu
Nguvu ya neno la munguNguvu ya neno la mungu
Nguvu ya neno la mungu001111111111
 
Uchumi wa kibiblia
Uchumi wa kibibliaUchumi wa kibiblia
Uchumi wa kibiblia001111111111
 

What's hot (12)

Nguvu ya maombi
Nguvu ya maombiNguvu ya maombi
Nguvu ya maombi
 
Academic excellence
Academic excellenceAcademic excellence
Academic excellence
 
Prayer manual 2013 by Elimringi Moshi 0714112062
Prayer manual 2013 by Elimringi Moshi 0714112062Prayer manual 2013 by Elimringi Moshi 0714112062
Prayer manual 2013 by Elimringi Moshi 0714112062
 
Kusudi la mungu kwa kanisa huduma na karama
Kusudi la mungu kwa kanisa   huduma na karamaKusudi la mungu kwa kanisa   huduma na karama
Kusudi la mungu kwa kanisa huduma na karama
 
Sadaka na-maana-ya-utoaji
Sadaka na-maana-ya-utoajiSadaka na-maana-ya-utoaji
Sadaka na-maana-ya-utoaji
 
Nguvu ya sadaka
Nguvu ya sadakaNguvu ya sadaka
Nguvu ya sadaka
 
Corpus christi 1 - in the bible (swahili)
Corpus christi   1 - in the bible (swahili)Corpus christi   1 - in the bible (swahili)
Corpus christi 1 - in the bible (swahili)
 
Kanuni za kiroho za ushindi
Kanuni za kiroho za ushindiKanuni za kiroho za ushindi
Kanuni za kiroho za ushindi
 
Ujana na mafanikio
Ujana na mafanikioUjana na mafanikio
Ujana na mafanikio
 
Trinity (swahili)
Trinity (swahili)Trinity (swahili)
Trinity (swahili)
 
Nguvu ya neno la mungu
Nguvu ya neno la munguNguvu ya neno la mungu
Nguvu ya neno la mungu
 
Uchumi wa kibiblia
Uchumi wa kibibliaUchumi wa kibiblia
Uchumi wa kibiblia
 

Viewers also liked

adverb
adverbadverb
adverb
Reena Riyas
 
Meu Bairro Centro - Abril
Meu Bairro Centro - AbrilMeu Bairro Centro - Abril
Meu Bairro Centro - Abril
ACIDADE ON
 
Paulistao
PaulistaoPaulistao
Paulistao
ACIDADE ON
 
Sindrome de asperguer sarita beas
Sindrome de asperguer sarita beasSindrome de asperguer sarita beas
Sindrome de asperguer sarita beas
Sari2105
 
Portfolio_June Lee (10212015)
Portfolio_June Lee (10212015)Portfolio_June Lee (10212015)
Portfolio_June Lee (10212015)
June (Hye Jun) Lee
 
Undervisningsdifferentiering - Gå-hjem-møde
Undervisningsdifferentiering - Gå-hjem-mødeUndervisningsdifferentiering - Gå-hjem-møde
Undervisningsdifferentiering - Gå-hjem-møde
Ole Ditlev Nielsen
 
Powerpoint assignment by Florida Sikwese
Powerpoint assignment by Florida SikwesePowerpoint assignment by Florida Sikwese
Powerpoint assignment by Florida Sikwese
florida sikwese
 
Aksha Group | 1,2 & 3BHK residential flats top builders in Pune.
 Aksha Group | 1,2 & 3BHK residential flats top builders in Pune. Aksha Group | 1,2 & 3BHK residential flats top builders in Pune.
Aksha Group | 1,2 & 3BHK residential flats top builders in Pune.
aksha11
 
ParanaVision Presentation (English)
ParanaVision Presentation (English)ParanaVision Presentation (English)
ParanaVision Presentation (English)
Alphan Manas
 
Ejmp
EjmpEjmp
Adote Pet
Adote PetAdote Pet
Adote Pet
ACIDADE ON
 
Rodeio de Sertãozinho
Rodeio de SertãozinhoRodeio de Sertãozinho
Rodeio de Sertãozinho
ACIDADE ON
 
Final Portfolio
Final PortfolioFinal Portfolio
Final Portfolio
caseylynn5196
 
Folsom dore
Folsom doreFolsom dore
The Softer Side of Scheduling
The Softer Side of SchedulingThe Softer Side of Scheduling
The Softer Side of Scheduling
Sreedhar Yedavalli
 

Viewers also liked (15)

adverb
adverbadverb
adverb
 
Meu Bairro Centro - Abril
Meu Bairro Centro - AbrilMeu Bairro Centro - Abril
Meu Bairro Centro - Abril
 
Paulistao
PaulistaoPaulistao
Paulistao
 
Sindrome de asperguer sarita beas
Sindrome de asperguer sarita beasSindrome de asperguer sarita beas
Sindrome de asperguer sarita beas
 
Portfolio_June Lee (10212015)
Portfolio_June Lee (10212015)Portfolio_June Lee (10212015)
Portfolio_June Lee (10212015)
 
Undervisningsdifferentiering - Gå-hjem-møde
Undervisningsdifferentiering - Gå-hjem-mødeUndervisningsdifferentiering - Gå-hjem-møde
Undervisningsdifferentiering - Gå-hjem-møde
 
Powerpoint assignment by Florida Sikwese
Powerpoint assignment by Florida SikwesePowerpoint assignment by Florida Sikwese
Powerpoint assignment by Florida Sikwese
 
Aksha Group | 1,2 & 3BHK residential flats top builders in Pune.
 Aksha Group | 1,2 & 3BHK residential flats top builders in Pune. Aksha Group | 1,2 & 3BHK residential flats top builders in Pune.
Aksha Group | 1,2 & 3BHK residential flats top builders in Pune.
 
ParanaVision Presentation (English)
ParanaVision Presentation (English)ParanaVision Presentation (English)
ParanaVision Presentation (English)
 
Ejmp
EjmpEjmp
Ejmp
 
Adote Pet
Adote PetAdote Pet
Adote Pet
 
Rodeio de Sertãozinho
Rodeio de SertãozinhoRodeio de Sertãozinho
Rodeio de Sertãozinho
 
Final Portfolio
Final PortfolioFinal Portfolio
Final Portfolio
 
Folsom dore
Folsom doreFolsom dore
Folsom dore
 
The Softer Side of Scheduling
The Softer Side of SchedulingThe Softer Side of Scheduling
The Softer Side of Scheduling
 

More from worldrepentanceandrestoration.org

Website profile (2)
Website profile (2)Website profile (2)
Website profile (2)
Website profile (2)Website profile (2)
The mighty vision of God almighty on 18 th october concerning the church a...
The mighty  vision  of God almighty on 18 th october  concerning the church a...The mighty  vision  of God almighty on 18 th october  concerning the church a...
The mighty vision of God almighty on 18 th october concerning the church a...
worldrepentanceandrestoration.org
 
End time prophecies
End time propheciesEnd time prophecies
THE LORDS MESSAGE ON REPENTANCE AND RESTORATION OF TANZANIA
THE LORDS MESSAGE ON REPENTANCE AND RESTORATION OF TANZANIATHE LORDS MESSAGE ON REPENTANCE AND RESTORATION OF TANZANIA
THE LORDS MESSAGE ON REPENTANCE AND RESTORATION OF TANZANIA
worldrepentanceandrestoration.org
 
Website profile (2)
Website profile (2)Website profile (2)
The mighty vision of god almighty on 18 th october concerning the church a...
The mighty  vision  of god almighty on 18 th october  concerning the church a...The mighty  vision  of god almighty on 18 th october  concerning the church a...
The mighty vision of god almighty on 18 th october concerning the church a...
worldrepentanceandrestoration.org
 
The lords message on repentance and restoration of tanzania
The lords message on repentance and restoration of tanzaniaThe lords message on repentance and restoration of tanzania
The lords message on repentance and restoration of tanzania
worldrepentanceandrestoration.org
 

More from worldrepentanceandrestoration.org (9)

Website profile (2)
Website profile (2)Website profile (2)
Website profile (2)
 
Website profile (2)
Website profile (2)Website profile (2)
Website profile (2)
 
The mighty vision of God almighty on 18 th october concerning the church a...
The mighty  vision  of God almighty on 18 th october  concerning the church a...The mighty  vision  of God almighty on 18 th october  concerning the church a...
The mighty vision of God almighty on 18 th october concerning the church a...
 
End time prophecies
End time propheciesEnd time prophecies
End time prophecies
 
THE LORDS MESSAGE ON REPENTANCE AND RESTORATION OF TANZANIA
THE LORDS MESSAGE ON REPENTANCE AND RESTORATION OF TANZANIATHE LORDS MESSAGE ON REPENTANCE AND RESTORATION OF TANZANIA
THE LORDS MESSAGE ON REPENTANCE AND RESTORATION OF TANZANIA
 
Website profile (2)
Website profile (2)Website profile (2)
Website profile (2)
 
The mighty vision of god almighty on 18 th october concerning the church a...
The mighty  vision  of god almighty on 18 th october  concerning the church a...The mighty  vision  of god almighty on 18 th october  concerning the church a...
The mighty vision of god almighty on 18 th october concerning the church a...
 
Maisha ya ujana
Maisha ya ujanaMaisha ya ujana
Maisha ya ujana
 
The lords message on repentance and restoration of tanzania
The lords message on repentance and restoration of tanzaniaThe lords message on repentance and restoration of tanzania
The lords message on repentance and restoration of tanzania
 

Maono ya bwana kuhusu kanisa la tanzania

  • 1. MAONO YA BWANA KUHUSU KANISA LA TANZANIA UJUMBE WA BWANA NA UFUNUO KUHUSU KANISA LA BWANA MNAMO TAREHE ISHIRINI NA MBILI MWEZI WA SITA MWAKA ELFU MBILI NA TISA (AMOSI 9:11-12) Bwana Munug mtakatifu wa Israel katika maono yake kuhusu nchi ya Tanzania nikiwa Mji wa Eldoret sehemu ya Langa’s kwa mwangalio wa ramani alinena nami haraka sana kuhusu nchi ya Tanzania na kanisa lake alilolipenda. 1. MAONO YA KWANZA YA BWANA 1) Bwana akanionyesha mti wa tunda ambao ni kijani kibichi(kiasi) lakini usio na matunda yake na wenye afya nzuri ukiwa umetanda juu ya choo kikongwe. UFUNUO ULIOMO KATIKA MAONO HAYA YA BWANA. Mti huo wa kijani kibichi ambao hauna matunda una ishara ya kuwa kanisa la Bwana katika nchi ya Tanzania limekuwa linaonekana kuwa na uzuri usio na matunda au tunda la Toba ilihali limekuwa likifanya toba mbele za Bwana Mungu mtakatifu katika machhozi, magotini na mavumbini. Hii inadhihirisha kuwa hili kanisa limekuwa na Toba ya unafiki isiyobadili moyo, na kutakaswa kwa damu ya Yesu na Roho Mtakatifu. Kanisa halijamgeukia Mungu kikamilifu katika moyo, limemdhihaki Mungu katika Toba huku kwa hekima yake ya kiulimwengu (Theologia au masomo ya kidini) likijaribu kumjua Mungu kwa vinywa vyake huku moyo wake ukiwa mbali naye (Isaya 29:13) Mungu aliona kanisa ambalo limejaribu kumfurahisha kwa aina Fulani ya uungu huku likikana nguvu za utauwa (Roho mtakatifu) (2 Timotheo 3:5) Mti huo kutanda juu ya chumba cha choo. Choo ni uchafu unaotoka kwenye tupu ya mbele au ya nyuma(mavi au mkojo) pia ina maana ya mahali pa kwenda haja. Hali hii ina sehemu mbili za ufunuo. 1) Kanisa hili lafaa kutubu katika Kristo Yesu wa Nazareti (Matendo ya Mitume 2:21, Warumi 10:13) 2) Kanisa hili limekuwa likitubu lakini pasipo kuzaa tunda lipasalo Toba maana yake ule mti usio na tunda, limekuwa kwa muda mrefu likitubu na kuungama dhambi lakini pasipo kuzaa tunda la Toba. Kuna hali pia ya kuchoka kutubu na pia mazoea ya Toba lakini matunda yake hayaonekani hata kwa kitambo hicho. Hivyo ina maana ya kuwa kanisa hilli la Tanzania lafaa kutubu au kumrudia Mungu na kuacha kila uovu kwa jjina la Yesu Kristo wa Nazareti. Ishara hii ni kwamba lazima sasa kanisa hili la nchi ya Tanzania litubu kikamilifu bila kujadiliana na shetani kwa vyovyote vile na kisha kuzaa tunda lipasalo Toba. Ujumbe uliojificha hapa ni kuwa lazima kanisa lijitenge na dhambi kwa kumrudia Mungu mtakatifu wa Israeli kwa kuanza kutembea kwa utakatifu na haki ya Mungu (tunda lipasalo Toba) kile chumba cha choo kinamaanisha kuwa hili kanisa la Tanzania linafaa sasa kuingia katika msimu wa Toba kwa ajili ya kanisa kujitoa au kujikwamua kutoka kwa dhambi za kila aina kupitia kwa Damu ya Yesu Kristo wa Nazareti na jina hilo pekee liwe mwangaza wa ulimwengu na chimvi ya Dunia (Mathayo Mtakatifu 5:13-16) Mathayo 3:7-10 “Hata alipoonoa wengi miongoni mwa mafarisayo na masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi wazao wa nyoka, ninani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasiraa itakayokuja? Basi zaeni matunda yapasayo toba, wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba tunaye baba ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimi watoto. Na shoka limekwisha wekwa penye mashina ya mti: kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni!
  • 2. 2. MAONO YA PILI YA BWANA (2) kisha Bwana akanionyesha mti wa mwiba au mti wa mwiba wa aina ya Mgunga, mmea huu hupatikana katika sehemu zifuatazo; kavu, Jangwa na nyika. Mti huu hutumika katika kuchoma mkaa wa kupikia, una ngozi nzito sana na yenye upana UFUNUO ULIO KATIKA MAONO HAYA YA BWANA. Mti huo wa mwiba ulikuwa na ishara ya kwamba kanisa la Bwana katika nchi ya Tanzania lafaa kwenda na kumtolea Bwana ibada kule nyikani au jangwani. Hii ni ibada ya lazima kwa Mungu maana ni mbinu pekee atumiayo kuwatoa watoto wake katika ufungwa au Misri ya roho na mwili ili wamtolee dhabihu. Kutoka 5:1, 3;18 “Hata baadaye Musa na Haruni wakaenda wakamwambia Farao wakasema Mungu wa Israeli asema hivi, wape watu wangu ruhusa waende ili kunifanyia sikukuu jangwani” Mungu aliliona kanisa lake likiwa katika ufungwa wa wa Misri wa rohoni 1) Rohoni- kupagawa na pepo, magonjwa ya roho, kuteswa na mapepo, kukosa uhuru wa kuabudu (mipangilio nyeti ya kidini ambayo haijamruhusu roho mtakatifu kutenda kazi katika kanisa) kutotakaswa katika roho na nafsi (1 Wathesalonike 5:23) 2) Mwilini- Magonjwa, maumivu ya kila aina, kukosa uhuru (Sheria na mafundisho yasiyo ya kibiblia) na mtendo ya mwilini ambayo ni dhahiri (waraka wa Paulo Mtume kwa Wagalatia 5:19) Hivi ina maana kwamba moyo wa Mungu unalia kwa sababu wa watoto wake ambalo ndilo kanisa kwa ajili ya ufungwa huku akitamani kuwa kanisa hili limtengenezee sikukuu jangwani. Kumbuka ya kwamba sherehe hii ni ya kutoa ibada kwa Mungu katika heshima na utukufu. Ibada ni tendo la kumwabudu (kumpa heshima na Utukufu) Mungu. Hii ibada anayoinena ni ile ifanyikayo kulingana na maandiko yake matakatifu kulingana na agano lake kwao. Kabla yao kuondoka Misri kwenda jangwani kumfanyia Bwana sikukuu Mungu aliwaamuru kufanya maandalizi yafuatayo (Kutoka 12:1-50) 1) Kumtwaa mwanakondoo ambaye angechinjwa na damu yake kupakwa au kutiwa katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu . hiyo ni ishara ya Bwana wetu Yesu kristo kusulubiwa msalabani na damu yake kutumika kuwa dhabihu tosha utumwani Misri (12:8) 2) Watakula nyama yake usiku ule ule ambayo imeokwa motoni. Hii ni dhabihu inayoteketezwa kwa moto (Roho mtakatifu na majaribu ya wateule) kuna uharaka wa kanisa hili kumtolea Mungu dhabihu zilizoteketezwa kwa moto wa roho mtakatifu na kupita katika majaribu ya kuandaa vyombo vya dhahabu kwa Mungu (12:8) 3) Pia wangekula na mkate usio tiwa chachu. Huu ni mkate ulo safi bila uzinzi, uasherati, uabudu sanamu, vinyago, wizi, uongo, ufisadi, upendo wa fedha wa fdha, uabudu shetani, udini, na ibada za uchafu wa uchawi wa kiroho (ujanja, kuogofya, sifa nyingi kupita kimo, utawala au mamlaka, kuendesha mambo na kukosoa) inamaana kuwa lazima wangemtolea Bwana dhabihu isiyo na dhambi na inajisi bali takatifu na safi na yenye haki ya Mungu. Kumbuka chachu huifanya mikate kuwa na kuvimba na kuwa na ladha ya ukali (unajisi, umwili, uchafu na kutokuwa takatifu) hivyo walifaa kumtolea Mungu dhabihu takatifu. Kanisa hili lafaa kutoa dhabihu takatifu isiyo na uchafu wa aina yoyote. Kanisa la nchi ya Tanzania limemtolea Mungu dhabihu za upendo wa fedha, udini, uabudu, shetani, mapepo, na majini, utumizi wa hirizi, kiburi na majivuno, kupenda uzinzi na uasherati, uganga na ushirikina ambavyo Bwana asema lazima kanisa hili litubu na kumrudia. 4) Walifanya kula mboga zenye uchungu ambayo ilikuwa na maana kuwa wangeondoka katika ufungwa na kuponywa na Mungu wao na kuwarejesha, kuwabariki na kuwainiua. Mara nyingi katika Israeli mboga hutumika katika kutengeneza dawa itumiwayo kuponya magonjwa ya kila aina. Kwa hivyo Mungu alikuwa akiliponya kanisa lake kutokana na uchungu lililopitia katika Misri ya kiroho na kimwili na kisha kuwekwa huru (12:8)
  • 3. MAONO YA TATU YA BWANA Hatimaye Bwana akanionyesha mashine ambayo hutumika kusaga mtama, ngano, mahindi au nafakailiyovunwa ili kupata unga mwororo wa kupikia vyakula kama vile vyapati, maandazi, keki na vinginevyo. Nje ya kile chumba cha mashine hiyo kulikuwa na chekecheo ya chuma ikiwa na vyombo vingi vya plastiki au mpira vya kila aina katika umbo la rangi. UFUNUO ILIOMO KATIKA MAONO HAYA. Mashine haya kwa kawaida hutumika kuutengeneza unga kwa kusaga mtama au nafaka ya kila aina ili kupikia vyakula vizuri kama vile vyapati, maandazi, keki na vinginevyo. Huo unga huwa ni mwororo na wenye usafi kiwango cha juu sana. Hili ndilo neno la Bwana kwa kanisa hili la Tanzania. Kanisa hili lafaa sasa kuendelea katika nyumba ya mfinyanzi ili kupokea neno la Bwana (Yeremia 18:1-6) “neno hili ndilo lililomjia Yeremia kutoka kwa Bwana kusema ondoka, ukashuke mpaka nyumba ya mfinyanzi na huko nitakusikizisha maneno yangu. Basi nikashuka mpaka nyumba ya mfinyanzi na tazama alikuwa akifanya kazi yake kwa magurudumu na chombo kile alichokuwa aifinyanga kilipoharibika mkononi mwake Yule mfinyanzi alikifanya tena kuwa chombo kingine kama alivyoona vema Yule mfinyanzi kukifanya. Ndipo neno la Bwana likanijia kusema Ee nyumba ya Israeli je siwezi mimi kuwatendea nyinyi vile vile kama mfinyanzi huyo alivyo tenda? Asema Bwana, angalieni kama udongo ulivyo katika mkono wa mfinyanzi, ndivyo mlivyo ninyi katika mkono wangu, Ee nyumba ya Israeli” baada ya kanisa hili kwenda katika chumba cha mfinyanzi litafinyangwa, kuyeyushwa, kutakaswa na kuoshwa pamoja na kutengenezwa kama jinsi Mungu apendavyo. Kumbuka kuwa kanisa hili laweza tu kupokea neno la Bwana katika nyumba ya Mfinyanzi kupitia kwa. 1) Damu ya Yesu yenye dhamana (Waebrania 9:11-14) 2) Roho Mtakatifu (Yohana Mtakatifu 16:8-15) 3) Moto wa Roho Mtakatifu (Mathayo Mtakatifu 3:11) Baada ya hili kanisa la Tanzania kupitia katika mashine (nyumba ya mfinyanzi) kanisa la Tanzania litaanza kutenda mapenzi ya Mungu, kuishi katika utakatifu na haki kwa kutii sauti ya Mungu na kutenda neno lake. Kanisa hili pia litakua na hofu ya Bwana moyoni. Picha ya hili kanisa itakua ifuatavyo:- 1) Litakuwa huru na chumvi ya ulimwengu (Mathayo Mtakatifu 5:13-16) 2) Litajaa miujiza ya Mungu (Danieli 12:9-10) 3) Litajaa ibada kamilifu yenye manukato kwa Bwana Mungu wa Mbinguni (Warumi 12:1-2) 4) Litastahimili majaribu, kuudhiwa na mambo yote yale magumu yanayohusu imani katika Kristo dhahiri katika kanisa hili la Mungu mtakatifu wa Israeli(Waraka wa Paulo Mtume kwa Wagalatia 5:23) Lile chekecheo la chuma ndilo lilepimo atakalotumia Mungu kutenga kanisa takatifu kutokana na dhambi, uchafu na kila uovu wa kila aina. Bwana ataliinua kanisa takatifu na kuliondoa uchafu na kila uovu ili liandaliwe kwa ajili ya ufalme wake wa Mbinguni Mathayo 3:12 “ambaye pepeto lake mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake na kuikusanya ngao yake ghalani bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika” chekecho hilo ni damu ya Yesu, Roho mtakatifu na moto ambacho ndicho kipimo cha pekee cha kujipatia kanisa takatifu lenye kuisikiliza sauti ya Mungu wa Mbinguni. Hali hii inahusika na:- a. Kutenga kanisa na dhambi. b. Kutenga wenye haki na wasio haki wajifanyao kuwa safi. c. Kurejesha utakatifu na kuondoa dhambi na uovu. Kanisa la nchi ya Tanzania linafaa kujiandaa na kuingia katika pasaka ya kuondoka Misri (Kutoka 12:1- 15) Baaada ya hayo kanisa hili lafaa kuondoka Misri na kwenda jangwani ili kumtolea Bwana dhabihu kulingana na sheria ya Bwana kwa pasaka ili alipokee kanani katika Baraka zake.
  • 4. (Yeremia 8:4-9) Huu ndio msimu wa kanisa la nchi ya Tanzania kwenda katika jangwa au nyika ya uyahudi kwa ajili ya Toba kwa Mungu katika hali ya unyenyekevu. Mathayo 3:1-3 “ siku zile Yohana mbatizaji akihubiri katika nyika ya uyahudi na kusema tubuni kwa maana ufalme wa Mbinguni umekaribia kwa sababu huyoo alienenwa na Nabii Isaya akisema, sauti ya mtu aliaye nyikani itengenezeni njia ya Bwana yanyoosheni mapito yake” Manthari ya jangwani ni kama ifuayavyo; hamna mimea ya kutosha, hamna maji na njia za kupita, kiangazi au jua ni kali, mchana ni mwingi na vumbi, hakuna mimea kwa wingi, wadudu na wanyama wengi waharibifu kama nge, nzige, nyoka wa jangwani, mawe mengi, miti ya miiba, ukosefu wa nyumba za kuishi, mapango ya mashimo yaliyo kaukiwa na maji kwa sababu ya jua kali. Haya mandhali ya jangwa au nyika yana maana kuu sana katika maisha ya hili kanisa la Bwana humu nchini Tanzania. Kuanzia kanisa hili lafaa kwenda katika unyenyekevu: kujinyima na kujitenga na ulimwengu kwa ajili ya kufanya Toba ya kipekee nay a kweli ili kumrudia Mungu. Hii ni katika hali ya kujitenga na maisha yake ya kawaida kama vile kula, kunywa, maisha ya raha na ukawaida wa ibada(Injili ya hema la nje la mwili, idaba ya uzinzi, upendo wa fedha, mazingira ya uchafu war oho na mwili) hali hii inahusishwa na:- 1) Kufunga na kuomba 2) Kujitenga na maisha ya makundi ya kawaida 3) Kujiondoa katika raha za kidunia 4) Kuwa na hofu ya Mungu (kumheshimu Mungu) 5) Kuhubiri injili ya uwezo wa Roho isiyijadiliana na dhambi. Ukweli ni kwamba kanisa hili lafaa kuingia katika msimu wa Toba na kujitakasa ili kupata msamaha na ondoleo la dhambi. Katika hali hii ya kanisa hili kutubu na kumrudia Mungu lafaa pia kufanya ubatizo wa waraka tu pindi mtu anapookoka katika maji mengi. Hiyo ibada ya kanisa la jangwani ina hali ya kukemea dhambi pasipo kujadiliana hadi watoto wa Mungu kutubu, kubatizwa na kujazwa Roho Mtakatifu (Mathayo 3:4-17) Kumbuka kuwa kanisa hili la Bwana lafaa kwenda jangwani na kuandaa njia ya Bwana Mungu mtakatifu wa Israeli. Njia hiyo ni Toba ya kweli maana Mungu wa Mbinguni ni Mtakatifu (Waraka wa kwanza wa Petro 1:13-16) Baada ya mambo ambayo kanisa hili lafaa kujitenga nayo ni kama ifuatavyo:- (1) Upendo wa fedha (1Timotheo 6:10) (2)Michezo ya kuigiza madhabahuni (3)Michezo ya densi za kiasherati na uzinzi madhabahuni (4)Dhabihu za kimwili (5) Mavazi ya kiasherati na kiuzinzi (6) Mizaha katika madhabahu ya Bwana (7) Ufisadi katika madhabahu ya Bwana (8) Upendeleo katika madhabahu ya Bwana (9) Unafiki na tabia za masadukayo na mafarisayo madhabahuni mwa Bwana (10) injili ya kigeni, mafundisho ya uongo na Philosophia, Theologia katika madhabahu ya Mungu isiyo na manufaa kwa maisha ya rohoni (11) ibada ya sanamu, shetani na vinyago madhabahuni (12) kupigania mamlaka, vyeo na madaraka kanisani. Basai kanisa hili lafaa kwenda katika ibada, haki na utakatifu ili Mungualisamehe na kuliponya kwa yale maovu yote ambayo limemtenda Mungu na kisha kuliinua hilo kanisa katika roho na kweli kwa utukufu wa jina lake. Mwisho ni kwamba sasa wakati wa kiunabii wa kulirejesha kanisa la Tanzania katika utakatifu basi ndio huu asema Bwana wa mabwana(Yeremia 8:4-9) Amani ya Bwana na iwe nanyi. Hii inamaana kuwa ni kitakatifu pekee ambacho kitabakia katika madhabahu ya Bwana kwa kazi yeyote ile nzuri. (Waraka wa pili wa Mtume Paulo kwa Timotheo 2:19-21) “ lakini msingi wa Munguulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake na tena kila alitajaye Jina la Bwana na auache uovu. Basi katika nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu bali na vya mti, na vya udongo, vingine vina heshima , vingine havina. Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga nao atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema” ukweli ni kwamba kanisa hili lazima lijitenge na dhambi na uovu wa kila aina ili litumike na Bwana kwa kazi nzuri yenye kumletea Mungu sifa na utukufu. Toba ya kilindi cha moyo yafaa kufanywa
  • 5. na kanisa hili ili kusamehewa na kusafika kwa dhambi na udhalimu wa aina yeyote. Hivyo hatua ndiyo ya pekee ya kuzaa kanisa takatifu litakalo urithi Ufalme wa Mbinguni. Ajabu ni kwamba hili kanisa laonekana kuwa katika mwili na matendo yake yakiwa dhahiri(Wagalatia 5:19). Hii inaashiriwa na vyombo vya aina hii vikiwekwa kwenye moto huteketea na kuwa jivu. Kanisa hli la Tanzania linapopitishwa katika m,ajaribu au mates kwa ajili ya Yesu tabia dhahiri ni ile ya kanisa kuugua na kuteketea, yaani:- 1) Kuiacha imani (Yeremia 10:20, 3:11na 22) 2) Kurudi nyuma (Yeremia 3:21) 3) Kujadiliana na shetani na kumuacha Mungu na kugeukia miungu (Isaya 28:15) Wnegi wa watoto wa Mungu katika kanisa hili hawawezi kustahimili majaribu yanapo wakumba katika safari. Hii hali yaashiria mambo yafuatayo:- 1) Kuiacha imani (Yeremia 10:20,3:11na 22) 2) Kurudi nyuma (Yeremia 3:21) 3) Kujadiliana na shetani na kumuacha Mungu na kugeukia miungu(Isaya 28:15) Wengi wa watoto wa Mungu katika kanisa hili hawezi kustahimili majaribu yanapowakumba katika safari.Hii hali yaashiria mambo yafuatayo. 1) Kutoshika imani ya kweli katika kristo Yesu Mnazareth 2) Kutokomaaa katika imani 3) Kutozingatia neno la Mungu kikamilifu 4) Kutotii sauti ya Mungu na kutotenda mapenzi ya Mungu 5) Ukosefu wa utakaso mkamilifu wa Mungu (wakara wa kwanza wa Paulo mtume kwa wathesalonike 5:25). 6) Kutompenda Mungu kwa moyo wote 7) Kutovaa vazi la ufalme wa Mbinguni (vazi la mwana kondoo wa Mungu). 8) Michezo au dansi za kimwili kanisani. Kanisa hili lazima litubu na kujitakasa kikamilifu asema Bwana wa Mabwana. 4. MAONO YA NNE YA BWANA. Bwana Mungu mtakatifu wa Israel kisha akanionyesha birika la chuma katika sehemu ya kisima chenu. UFUNUO ULIO KATIKA MAONO HAYA. Kanisa la nchi ya Tanzania limemuacha Mungu na kuigeukia miungu nyingine kama vile ya fedha na dhahabu,ya madhehebu na dini,uchawi na uganga ,ushirikina na muingu ya ibda ya mashetani kama vile legio maria, mizimu pamoja na hirizi,Baali, yezebeli, lucifa, malkia wa mbingu, Asheroh.  Kanisa hili pia lina ibada ya sanamuna vinyago 1wafalme 18:1-46,ufunuo 16:2-28,isaya 28:11-15,yerema 1:17-20.  Kanisa hili la Tanzania limeuacha msaada wake wa pekee na kugeukia misaada mingine kama vile Misri na Ushelisheli, Kugeukia wachawi kutaka upako wa uongo wa kutenda miujiza,waganga na wapiga ramli kwa utendaji wa miujiza kunao tumia nguvu za giza kutenda miujiza ya uongo ya uponyaji na ukombozi ,waimbaji na wahubiri kwenda kutafuta upako Baharini,na kishetani ili kutenda miujiza na huduma ya Mungu kanisani.  Kanisa pia lina ibada ya mambo asili ya ulimwengu huu na kumsahau Mungu wa Israel.
  • 6. Kila kisima kina maana ya kanisa la humu nchni Tanzania.Hivi ni kwamba kanisa la Mungu katika nchi ya Tanzania linaabudu miungu mingine kama ya kikabila ,madhehebu na dini(Yeremia 7:17-20) Je! huoni wanavyotenda katika miji ya Yuda na katika njia kuu za Yerusalemu? Watoto huokota kuni na baba zao huwasha moto na wanawake hukanda unga ili kimfanyizia mikate malkia wa mbinguni na kuwamiminia miungu mingine sadaka za vinywaji wapate kunikasirisha mimi.Je! watu hawa wananikasirisha mimi? Asema Bwana hawajikasirisha nafsi zao na kuzitia haya nyuso zao wenyewe? kwa hiyo Bwana Mungu asema hivi:Tazama hasira yangu na ghadhabu yangu zitamwaga juu ya mahali hapa.: juu ya wanadamu, na juu ya wanyama, na juu ya juu ya mashamba, na juu ya mazao ya nchi nayo itateketea’’ Yeremia 19: 1 – 6 Ukisema lisikieni neno la Bwana , enyi wafalme, wa yuda na wenyeji wa yerusalemu: Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli asema hivi, Angalieni, italeta mabaya juu ya mahali hapa, ambayo mtu yoyote Yule akisikia habari yake masikio yake yatawaka. kwa sababu wameniacha mimi nao wamepafanya mahali hapa kuwa mahali pageni nao hapa wamewafukizia uvumba miungu mingine wasiowajua, wala wao, baba zao, wala wafalme wa yuda : nao wamepajaza mahali hapa damu ya wasio na hatia nao wamemjengea Baali: tendo nisiloliamuru mimi wala kulinena wala halikuingia moyoni mwangu basi angalieni siku zinakuja asema Bwana katika siku hizo mahali hapa hapataitwa tena Tfethi, wala bonde la mwana wa hinomu bali bonde la machinjo? 5. MAONO YA TANO YA BWANA Kisha Bwana akanena nami kuhusu uchafu ulio katika madhehebu yenu na ukosefu wa maji safi ya kunywa hata kufulia ( yeremia 7: 9 – 10) “je mtaiba na kuua na kuzini na kuapa kwa uongo na kuvukizia baali uvumba na kuifuata miungu mingine ambayo hamkuijua. Kisha mtakuja na kusimama mbele zangu katika nyumba hii iitwayo kwa jina langu ,mkisema tumepona ili mpate kufanya machukizo haya yote?” UFUNUO WA MAONO HAYA. Ninyi watu wake Mungu mmelinajisi hekalula Bwana Mungu wenu kwa dhambi kama vile ngono, ushirikina,uchawi(wa mwili na roho).Haya mambo mmeyatenda hata madhabahuni mwa Bwana Mungu wetu,kwa sababu ya uchafu na unajisi huo katika madhabahu ya Bwana.Hamna tena maji safi (Roho mtakatifu na neno la Mungu)ndani ya nyumba ya Mungu kwani kisima chake kilizibwa na usafi kuondoka kwa uovu wenu asema Bwana wa majeshi.Mto wa roho mtakatifu wenye maji safi haupo tena madhabahuni mwa Bwana kwa sababu ulizibwa kwa matendo yenu maovu. Hivyo Mungu mkuu na mtakaifu wa Israel aona chumba ambacho kimetiwa unajisi na maji yake kuwa chafu yenye kufisha kondoo wake na kuharibu afya yake.Lazima kanisa la nchi hii ya Tanzania lafaa kurejelea utakatifu kwa toba ya kilindi cha moyo itakayomsababisha Roho mtakatifu kulitembelea kanisa,kuwa na ushirika nalo ili kuliuisha, kuliponya na kulikomboa, kutoka katika ufungwa wa misri ya mwilini na rohoni, asema Bwana Mungu wa majeshi (Yeremia 6:7). ‘Kama vile kisima kitoavyo maji yake, ndivyo utoavyo uovu wake jeuri na kuharibu kwa sikiwa ndani yake,ugonjwa na jeraha za mbele zangu daima,uadhibishwe, Ee Yerusalemu,nafsi yangu isije ikafarakana nawe,nisije nikakusanya ukiwa ,nchi isiyokaliwa na watu. 6. MAONO YA SITA YA BWANA KUHUSU KANISA LA TANZANIA. Hatimaye Bwana akanionyesha mti mkubwa wa tunda ambalo haukuwa na matunda wala au lolote lililoota juu yake kulikuwa na joka mwenye rangi ya kijani kibichi sawia na ule mti lakini ikiwa na vipaji vyeusi sehemu sehemu mwilini mwake.Akaniruhusu kulichukua jiwe na kulitupia jiko kisha joka kwa upesi sana lilitoweka.Mti huo ulikuwa umetandaa juu ya ukuta mkongwe uliokuwa umezingira nyumba iliyokuwa imejengwa kwa mfano wa kanisa ,ulikuwa ukiwa sana
  • 7. UFUNUO ULIO KATIKA MAONO HAYA 1. Mti usio na tunda una maana kuwa kuna hali ya toba ambayo si ya kuzaa matunda au tunda lipasalo toba katika kanisa hili lake la Tanzania (Mathayo 3:7-10). “Hata alipoona wengi miongoni mwa mafarisayo na masadukayo wakijua ubatizo wake aliwaambia enyi wazao wa nyoka ni nani aliyewaloga ninyi kuikimbia hasira itakayo kuja? Basi zaeni matunda yapasayo toba, wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba tunaye baba ndiye Ibrahimu kwa maana nawaambia ya kwamba aweza katika mawe hayo kumwinulia Ibrahimu watoto.Na shoka limekwisha kuwekwa kwenye mashina ya mti, basi kila mti usozaa matunda hukatwa na kutupwa motoni” Hivyo kanisa hili lafaa kubadili mawazo yake kuhusu kumurudia Bwana na kuanza kumrudia Mungu kikamilifu na kurejea utakatifu pamoja na kujazwa Roho mtakatifu. 2. Nyoka ni alama tosha kuwa kanisani hili lina uabudu wa shetani, miungu mingine ambayo imelinajisi kanisa hili la Tanzania. Kuna ibada pia inayotolewa kwa miungu ya upendo wa miungu (mara nyingi huwaongoza watu kufanya uzinzi na uasherati, ukahaba na tabia mbovu za kingono) (Isaya 28:14-15) “Basi sikieni neno la Bwana enyi watu wenye dharau mnaowatawala watu hawa ndani ya Yerusalemu kwa sababu mmesema tumefanya agano na mauti, tumepatana na kuzimu, pigo lifurikalo litakapo pita halitatufikia sisi kwa maana tumefanya maneno ya uongo kuwa kimbilio letu, tumejificha chini ya maneno yasiyo kweli” 3. Yule joka kufanana na ule mmea ni dhahiri kwamba kuna hali ya kukubaliana na uabudu wa shetani (yeremia 7: 30-31) “Maana wana wa yuda wametenda yaliyo maovu machoni pangu asema Bwana, wameweka machukizo yao ndani ya nyumba hiyo iitwayo kwa jina langu, hata kuitia unajisi.Nao wamepajenga mahali palipoinuka pa Tofethi palipo katika bonde la mwana wa hinomu ili kuwateketeza wana wao na binti zao motoni. Jambo ambalo mimi sikuliagiza wala halikuingia moyoni mwangu”. 4. Kuna haja kubwa ya kumuondoa shetani katika madhabahu ya Bwana ili yasafike na kuwa safi. Hii ni kupitia tu kwa toba katika kristo yesu Mnazareti (Yeremia 4: 1- 4) “Kama ukitaka kurudi, Ee Israel, asema Bwana utanirudia mimi na kama ukitaka kuyaondoa machukizo yako yasiwe mbele ya macho yangu. Ndipo hutaondolewa nawe utaapa hivi, kama Bwana aishivyo, katika kweli na katika hukumu, na katika haki ndipo mataifa watajibariki katika yeye,nao watajitukuza katika yeye.Maana Bwana awaambia hivi watu wa Yuda na Yerusalemu,ulimeni udongo katika konde zenu wala msipande mbegu kati ya miiba.Jitahirini kwa Bwana,mkaziondoe ngozi za mioyo yenu enyi watu wa Yuda na wenyeji wa Yesusalemu,ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto ikawaka hata mtu asiweze kuizima kwa sababu ya uovu wa matendo yenu. Ndiyo sababu Bwana alinuruhusu kuchukua jiwe na kulitupa lile joka na kisha likatoweka. 5. Ule ukuta uliokuwa mkongwe na kutandwa na matunda ni maana ya kuwa ukuta wa Roho wa Bwana wetu Yesu Kristo ambao aliujenga kwa kazi ya msalaba umeachwa ukiwa (Yeremia 10:20-21) ukuhani hautimizi sheria ya ukuhani.(Malaki 2:1-11,Yer 12:10-11) na hali watoto wa Mungu wanakaa katika starehe katika nyumba nzuri .Mwili wa Bwana wetu Yesu Kristo umeachwa ukiwa na kuonekana kuwa mkongwe sana.Hakuna ulinzi na mwavuli wa Bwana kwa kanisa.Mungu aliona kanisa ambalo limeachwa ukiwa na kuwa na hali ifuatayo:. 1. Ukosefu wa ibada na ukombozi wa kweli. 2. Kwa kuabudu sanamu na shetani 3. Uchawi,uganga,ushirikina na hirizi katika madhabahu ya Bwana.
  • 8. Mungu basi anataka kanisa lake lianze kuoshwa kujengwa upya.Kurejeshwa kwa sehemu yake ya urembo wake war oho.(Hagai 1:1-11,Hagai 2:5-9). (Yeremia 6:7) Maana Bwana wa majeshi asema hivi jikatieni miti mfanyize boma juu ya Yerusalemu.Mji ni mji unaojiliwa ,dhuluma tupu ndani yake.’ 7. MAONO YA SABA YA BWANA KUHUSU KANISA LAKE LA TANZANIA TAREHE 31 MWEZI WA TISA ,MWAKA 2009 Bwana katika mtembeleo wake alinichukua katika roho na kunionyesha sayari ikipita kutoka upande mmoja wa mawingu juu katika mbingu hadi upande mwingine ,mawingu yalikuwa ya samawati na shwari.Kulikuwa na mwezi mkubwa ambao ulikuwa shwari bila kusonga hata nukta.Sayari hiyo ilikuwa kuu na yenye muundo wa trapeze.Hiyo sayari ilipita juu mbinguni kutoka sehemu ya kushoto hadi sehemu tofaui hadi sehemu kinyume na ile ya kwanza.Hali hii ilikuwa ni dhimisho ya nyakati za mwisho kabla ya siku ya Bwana.(Yoel 2:30-31) Nami nitaonyesha mambo ya ajabu katika mbingu na katika dunia damu,na moto na minara ya moshi.jua litageuzwa kuwa giza na mwezi kuwa damu,kabla haijaja siku hiyo ya Bwana iliyo kuu na itishayo. UJUMBE ULIOMO KATIKA MAONO HAYA KWA KANISA LA YESU KRISTO. Hii ni dhahiri kwamba nyakati za kiunabii kwa kanisa la Kristo zimebadilika.Maanake ni kwamba tunaelekea katika upeo mkuu wa unyakuzi wa kanisa takatifu la Kristo Hii ni dhahiri kwamba nyakati za kiunabii kwa kanisa la Kristo zimebadilika.Maanake ni kwamba tunaelekea katika upeo mkuu wa unyakuzi wa kanisa takatifu la Kristo Yesu. 1. Kanisa lafaa kutubu kikamilifu na kujazwa kwa Roho mtakatifu kiwango cha mafuta ya nyakati za mwisho (Matendo ya Mitume 2:38,Ezekiel 47:1-5) 2. Kanisa lafaa kutubu na kisha kuandaa njia ya Bwana yaani ufalme wa Mbingu (Mathayo mtakatifu 3:1-3(2) 3. Kanisa lafaa kuvalia vazi la harusi ya mwanakondoo wa Mungu kitani nyeupe ing’arayo (Ufunuo 6:9-11,Ufunuo 7:9,Ufunuo 19:1-8 Ufunuo 19:9). 4. Kanisa lafaa kujiandaa kusimama mbele ya kiti cha enzi cha hukumu (Ufunuo 20:11-15.) 5. Kanisa lafaa kumsikiliza Mungu kwa upesi na kujiandaa kurithi ufalme wa mbinguni.(Ufunuo 2:29,Ufunuo 3:22). 8. MAONO YA NANE KUHUSU KANISA LA TANZANIA ,TAREHE 31 MWEZI WA TISA SAA KUMI NA MOJA. Bwana kisha akanena nami kwa sauti kuhusu kuja kwake Yesu kulinyakua kanisa katika unyakuzi .Kwa sauti akasema, kama mwivi ajavyo ndivyo itakavyokuwa kwa Mwana wa Adamu (Mathayo 24:42-51) MTUMWA WA YESU VICTOR MSERE AKIDIVA 0719 434702 0762 179401. MUNGU APEWE SIFA NA UTUKUFU.