SlideShare a Scribd company logo
SEMINA KWA
JAMII JUU YA
NAFASI YA
SANAA KATIKA
ELIMU NA
UCHUMI NCHINI
TANZANIA
| MAYUNI JOSEPH
Utangulizi
Sanaa katika maisha ya binadamu
inachukua Nafasi kubwa sana. Kabla ya kujua
Nafasi ya sanaa katika elimu na uchumi, hebu
tujadili maana ya sanaa, licha ya wataalamu
wengi kujadili maana ya sanaa kama vile Plato,
Kirsty Wark, Joseph Beuys, Emmanuel Kant na
Allexander Baumgarten. Hapa tutaangalia
maana ya sanaa moja kwa moja kwa kujumuisha
mawazo ya wataalamu waliofafanua maana ya
sanaa. Kwa ujumla sanaa ni uwezo alionao kila
binadamu wa kuunda kitu kwa upekee kwa
madhumuni ya kukidhi mahitaji ya jamii kwa
kuanagalia nyanja za kisiasa, kijamii na
kiuchumi kwa faida ya kizazi cha sasa na kizazi
cha badae. Kwa namna hiyo sanaa ni ujuzi
ambao binadamu anautumia kuunda vitu
mbalimbali kwa ajili ya manufaa ya jamii.kwa
mfano msanii anapochora picha, anapoimba
wimbo na anapochonga kinyago lengo kuu sio
kufurahisjha nafsi yake, bali lengo ni
kuhakikisha jamii inanufaika kwa kugusa
nyanza zote za jamii yaani kiuchumi, kisiasa na
kijamii. Kwa hiyo hapa kila binadamu ni msanii,
Kwani kila binadamu anazaliwa na kipaji kama
anavyosema Plato alipokuwa kufafanua falsafa
ya elimu juu ya asili ya mwanafunzi. Lakini pia
wazo hili linaungwa mkono na mwanafalsafa wa
kijerumani ajukanaae kama Joseph Beuys.
Joseph Bueys anafafanua kuwa
“Every human being is an artist…by artist I
don’t just mean people who produce and
scripture or play the piano, or composers or
writers. For me a nurses is also an artist, or, of
course, a doctor or a teacher. a student too, a
young person responsible for his own
development. The essence of man is captured in
the description ‘artist’ Extracted from state of
art, Sandy Nairne, Chatto and Windus, 1987
Kwa namna hiyo tunatambua mchango wa
sanaa kwa kuona vitu ambavyo vinaundwa
kutokana na sanaa hiyo ambayo binadamu
anaitumia katika maisha yake ya kila siku.
Lakini pia ni wazi kuwa jamii inatambua kuwa
katika maisha ya binadamu sanaa ina nafasi
kubwa sana. kimsingi tumeona kuwa sanaa
ilikuwepo hata baada ya binadamu kuwepo, na
binadamu ameikuta sanaa kama alivyokuta vitu
vingine hapa duniani kama vitabu vya
dini(ukristo na uislamu) vinavyosema.
Lakini je? sana ya Tanzania imegawanyika
katika sehemu kuu ngapi. Mgawanyiko wa sanaa
kwa mujibu wa Baraa la Sanaa Tanzania
(BASATA) katika kitabu kijulikanacho kama
Falsafa ya sanaa ya Tanzania linagawa sanaa
katika makundi mawili ambayo ni sanaa za hisi
na sanaa za zana. Kwa kuanza na sanaa za hisi,
ni aina ya sanaa ambazo o bindamu anatambua
kwa kutumia milango ya fahamu inayojulikana
kama, ulimi kwa kuonja, macho kwa kuona,
ngozi kwa kugusa na pua kwa kunusa.
Kwanamna hii fungu hili la sanaa binadamu
anapaswa kutambua ujumbe ambao msanii
anataka kuutoa kwa jamii yake kwa kutumia
milango hiyo ya fahamu. Kimsingi sanaa hisi
mara nyingi huitaji akili nyingi itumike na
binadamu ili kujua msanii ana malengo gani kwa
Jamii husika. Kwa mfano wa sanaa za hisi ni
matumizi ya michoro amayo haina maelezo na
hata kama yanamaelezo huwa si laisi kutambua
msanii analengo gani kwa Jamii yake. Kwa
mfano katika kazi nyingi za kifasihi kwa upande
wa fasihi andishi, ambapo tunapata ushairi,
riwaya na tamthilia. Mara nyingi tunashuhudia
ganda la kitabu likiwa na picha ambazo zipo
zinazofanana na jina la kitabu na zingine
hazifanani na jina la kitabu kwa mfano, katika
kitabu cha , Morani, Kivuli Kinaishi, Watoto wa
mama N’tilie, ukiangalia maganda ya vitabu hivi
vya kifasihi utagundua kuwa umetumika usanii
wa kutosha katika kuunda picha na mpangilio
wa rangi, ambapo inampasa msomaji awe
makini ili kutambua uhusiano uliopo kati ya
ganda la kitabu na jina la kitabu, na vilivyomo
ndani ya kitabu . Kwa ujumla sanaa hizi
zinajulikana sanaa za hisi kwani zinahitaji
kutambuliwa kwa milango ya fahamu ya
binadamu kwa kuhususha fikra yakinifu. Kwa
upande wa sanaa za zana, hizi ni sanaa ambazo
zinaweza kutumika katika kutoa mafunzo ya
wazi na mara nyingi vifaa na zana zilizotumika
uonekana na kuguswa, kwani fungu hilim la
sanaa mara nyingi vinavyoundwa na jamii
hutumika moja kw moja na jamii husika kama
zana katika shughuri maalumu. Hapa binadamu
sio lazima utumie milango yote ya fahamu ili
kuweza kutambua ujumbe uliokusudiwa na
msanii kwa jamii yake. Cha msingi hapa ni
kwamba sanaa hizi za zana utumia maumbo
halisi ambayo binadamua anayatumia kila
kukicha, kwa mfano alama za barabarani, zana
za kufundishia darasani, ambapo zana hizi
utumia usanii wa hali ya juu katika uundaji
wake. Kwa ujumla sanaa za zana ni laisi
kutambuliwa na zinakuwepo kwa lengo
maalumu kwa Jamii bila kificho.Kwa namana
hiyo tunaona nI kwa jinsi gani Baraa la Sanaa
Tanzania (BASATA) katika kitabu
kijulikanacho kama Falsafa ya sanaa ya
Tanzania limefanikiwa kugawa makundi haya
ya sanaa kwa kuangalia Jamii ya kitanzania na
mazingira yake. Na baaada ya kuona mafungu
haya ya sanaa sasa tuone Nafasi ya sanaa katika
Jamii ya kitanzania kwa kipindi chote
MAISHA YA BINADAMU NA SANAA
Kwa kipindi kirefu binadamu amekuwa
akitumia sanaa kama nyenzo muhimu katika
shughuri mbalimbali za kiuchumi, kisiasa na
kijamii. Kwa namna hiyo sanaa imekuwa na
umuhimu mkubwa kwa maisha ya binadamu
kwa kipindi chote.Kwa mfano katika siasa
UMBO 1: Nyumba inajengwa kwa udongo ambao
umefinyangwa na kukandikwa kwa usanii wa hali ya
juu
binadamu alitumia sanaa za zana kuunda vitu
mbalimbali ambavyo vilitumiwa na viongozi
mbalimbali kwa mfano, mavazi ya wanajeshi na
mavazi kwa ajili ya watemi na wafalme na vifaa
vya kufanyia kazi kama vile meza na viti
ambavyo vimebuniwa kwa usanii ambao
bindamu aliutumia.Kwa upande wa uchumi
binadamu alitumia zana mbalimbali ambazo pia
zimebuniwa na kutumika kama bidhaa, kwa
mfano nyungo, vigoda,kawa na viatu , ambavyo
viliuzwa na vilitumika kama bidhaa zenye
thamani. Lakini pia sanaa in nafasi katika
masuala ya kijamii, ambapo sanaa inatumika
kutengenezea vitu ambavyo vinatumika na
makabila mbalimbali kama kitambulisho na vitu
muhimu kwa kabila hilo, kwa mfano usanii
unaotumika kutengenezea vinyago kwa kabila
ya Wamakonde, ni kitambulisho tosha kwa
Wamakonde. Na hata kwa upande wa michoro
inayochorwa na kabila la Wamakonde ambayo
inajulikana kama (chale) inatumia usanii wa
kutosha wakati wa kuchora. Kwa namna hiyo
sanaa ina nafasi kubwa sana katika Jamii ya
Tanzania tokea wanzo hadi sasa kwenye karne
ya 21.Hivyo ni jukumu la kila mtanzania kujua
nafasi ya sanaa katika nyanja za elimu, uchumi
na kijamii.Sasa tuangalie kwa ufupi nafasi ya
sanaa katika elimu na uchumi katika jamii ya
kitanzania.
NAFASI YA SANAA
KATIKA ELIMU NCHINI
TANZANIA
Kwa kuwa tumeshafahamu maana ya sanaa,
hivyo haina haja ya kurudia kufafanua dhana hii.
Na hivyo tutaangalia maana ya msingi ya neno
Elimu, dhana ya Elimu imefafanuliwa na
wanafalsafa wengi sana wa elimu na hapa
nitataja wachache tu kwa mfano Julius
Kambarage Nyerere, Plato, Aristotle, Socrates,
john Agrey na Maria Montessori. Lakini ki
msingi elimu ni utaratibu uliowekwa na Jamii
ambapo mafunzo, ujuzi, hekima na urithi
unahamishwa kutoka kwa kizazi kimoja hadi
kingine kwa lengo la kuhakikisha mahitaji na
malengo ya Jamii yanatimizwa bila kukiuka
imani na maadili ya jamii husika.Ufafanuzi huu
unafanana sana na ule wa maana ya sanaa,
kwani malengo ya sanaa ni kukidhi mahitaji ya
jamii, tukichunguza kwa umakini malengo ni
hayo hayo yanayolengwa na dhana ya elimu.
Kwa namna hiyo kutokana na uhusiano huo wa
elimu na sanaa, Jamii inapaswa kutumia elimu
na sanaa kama nguzo au nyenzo muhimu ya
kukidhi mahitaji ya Jamii kwa kipindi chote.
Jamii itatumia vitu mbalimbali vilivyoundwa na
binadamu kwa usanii na akili ya hali ya juu
kama sehemu ya kutolea mafunzo. Na mara
nyingi utengenezwaji wa zana hizo zinahitaji
usanii na elimu wa hali ya juu ili kuvutia na
kuleta ujumbe kwa Jamii husika.Kwa kuwa
Jamii inahitaji watu ambao watatumia akili zao
na ujuzi wao katiuka kubuni na kuunda zana za
kutolewa elimu kwa mfano, Mwalimu darasani
anapotumia zana ambayo imetumia usanii wa
hali ya juu kufundishia , kwa mfano mwalimu
anapohitaji kufundisha wanafunzi kuhusu mlima
Kilimanjaro ni wazi kwamba picha itayochorwa
pale ni mlima kilimanjro.Lakini mlima huo
hautachorwa kwa mzaha, bali utatumia usanii
mwingi na akili nyingi. Hivyo kwa kuwa lengo
la elimu ni kutoa mafunzo kwa wanafunzi, ni
wazi kuwa uchoraji wa mlima kilimanjaro
hautakuwa wa mzaha, bali utahitaji umakini kwa
msanii atayechora au kuchonga kitu kitakacho
fanana na mlima kilimanjaro. Mpaka hapa sanaa
imetambulika wazi katika suala zima la elimu.na
kwa namna hivyo ufundishaji ambao unatumia
zana zilizoundwa kwa usanii zitakuwa na faida
zifuatazo kwa wanafunzi.
•Ufundishaji unaotumia zana za kisanii
hukuza udadisi kwa wanafunzi, Kwani picha
hiyo itamfanaya mwanafunzi kujenga picha juu
ya kitu halisi katika ubongo wake.kwan kitabia
picha huwa na vitu vingi, vitu hivyo vitamfanya
mwanafunzi kuwa mdadisi kwa kujifunza vitu
vingi zaidi ya mlima, kwa mfano kwenye mlima
kuna miti, hivyo wanafunzi wanaweza kutoa
maelezo mengi juu ya mlima Kilimanjaro
kuhusiana na miti iliyokuwepo. Hivyo kufanya
wanafunzi kuwa na ujuzi wa kudadisi kutokana
na picha wanayoiona ambayo imetumia usanii
wa hali ya juu.na mwisho itasababisha kuwa na
taifa ambalo watu wake ni wadadisi kwa
maendeleo ya taifa.
•Ufundishaji unaotumia zana za kisanii
hukuza vipaji vya wanafunzi, kwa kuwa
wanasaikolojia na wanafalsafa wanaamini kuwa
kuwa kila binadamu ni msanii, bila shaka hata
darasani kuna wasnii pia. Niweke wazi kwamba,
wanafunzi wanapokuwa shuleni huwa
wanafanya mambo mengi yenye kuhusiana na
viapaji, wapo wanaofanya mambo makubwa na
kushangaza walimu wao na wapo wanaofanya
ya kawaida, ila hoja ipo palepale nvyote ni
vipaji.kama sula hapa ni vipaji vya wanafunzi, ni
vema tukampa nafasi Mwalimu ambaye
anatumia zana zilizochorwa kwa usanii wa hali
ya juu. Kwani mwanafunzi atakapoona picha
mbele ya ubao, ataweza kujaribu kuchora picha
hiyo. Hivyo usanii utachukua nafasi kwa
mwanafunzi huyo kutokana na zana iliyotumiwa
na Mwalimu wakati wa kutoa Elimu.
• Ufundishaji unaotumia zana za kisanii
hukuza ushirikiano baina ya Mwalimu na
wanafunzi, lazima tufahamu kuwa, katika
mchakato wa ufundishaji darasani jambo la
msingi ni ushirikiano baina ya mwalimu na
mwanafunzi. Hivyo matumizi ya zana za kisanii
katika mchakato wa ufundishaji utajenga
ushirikiano kati ya Mwalimu na mwanafunzi
ambapo kila mwanafunzi atakuwa tayari na
makini kuona picha ambayo imechorwa kwa
ubunifu kutokana na usanii wa mwalimu.
Kitendo hicho kinamfanya mwalimu kuwa
karibu na wanafunzi Kwani, kuna baadhi ya
picha zitamfanya mwanafunzi kuuliza maswali
kwa Mwalimu. Wakati mwingine, mwanafunzi
atataka, kujua zaidi juu ya usanii uliotumika
hapo. Hivyo itamlazimu kuwa karibu na
Mwalimu na kufanya majadiliano ya kina na
yenye kueleweka na mwanafunzi husika. Na
ikumbukwe kuwa lengo la Mwalimu kutumia
zana za kufundishia ni kutoa mafunzo yenye
kueleweka , ambapo Mwalimu atahitaji
kufahamu na kujua kila mwanafunzi kama
ameelewa somo au lah! Kitu ambacho kinakuza
ushikiano na mahusiano baina ya Mwalimu na
mwanafunzi.
Kimsingi sana katika elimu ina nafasi
kubwa sana kwani asilimia kadhaa ya zana na
vitu vinatumika shuleni hasa wakati wa
kufundishia vimeundwa kwa usanii mkubwa
sana.lakini pia sanaa kwenye elimu inatumika
pia kwenye nyimbo, mashairi na maigizo,
ambayo hubeba ujumbe ambapo Jamii inapaswa
kujifunza, kwa wakati huu, msanii anakuwa
walimu na jamii inakuwa mwanafunzi. Kwa
hiyo ni matarajio ya Jamii kuona usanii wa
msanii atatumika kuundia zana ambayo itatoa
Elimu kwa Jamii hiyo kwa mfano, nyimbo
zitakazoimbwa, maigizo yatakayoigizwa na
vinyago vitakavyochongwa ni wazi kwamba
vinapaswa kutoa ujumbe kwa Jamii hisuka. Kwa
ujumla Jamii ya kitanzania inatambua nafasi ya
sanaa kwenye elimu, Kwani katika Jamii ya
kitanzania msanii anaheshimika na kupewa
nafasi kubwa katika jamii.Hivyo sanaa ina nafasi
katika elimu hapa nchini Tanzania.
Mbali na shuleni sanaa inatumika kutolea
Elimu katika Jamii hapa nchini Tanzania, kupitia
kampeni mbalimbali. Elimu inatolewa na sanaa
kwa Jamii huwa inalengo la, kutoa maelekezo au
kuonya. Kwa namna hiyo katika jamii mbali na
sanaa ya mziki na maigizo ambayo ndo
yanafahamika sanaa na Jamii zetu hapa nchini
Tanzania, zipo sanaa ambazo zinatumika sana
kutolea Elimu kwa Jamii kuzidi sanaa ya kuimba
au sanaa ya maigizo.kwa mfano sanaa ya
uchoraji ni moja ya sanaa ambayo inashika
safasi kubwa katika kuahakikisha Jamii ya
Tanzania inapata Elimu inayotakiwa. Labda
tuchukue mfano huu wa alama za barabarani,
alama za barabarani ni moja ya mfano wa sanaa
za zana, hivyo kazi kubwa za alama barabarani
ni kutoa maelekezo kwa watumiaji wa barabara.
Lakini ukiangalia kwa makini sanaa iliyotumika
kuchora alama zile utagundua kuwa kuna usanii
umechukua Nafasi yake. Licha ya kwamba
lengo la alama hizi sio kutambulisha usanii, ila
hapa tunaangalia Nafasi ya sanaa katika
utengenezwaji wa alama hizi. Uchoraji na
upangaji wa rangi unahitaji usanii wa hali ya
juu. Kwa mfano alama inayoonesha hapa ni
kivuko cha ng’ombe ni lazima achorwe
ng’ombe, kwa namna hiyo tunaona sanaa ya
uchoraji inachukua Nafasi yake. Labda tuchukue
mfano mwingine, alama inayoonesha kuwa hapa
ni kutuo cha basi, ni lazima picha inayofanana
na basi itachorwa, ambapo sanaa ya uchoraji
inatumika.
Mbali na alama za barabarani kuna Elimu
zinatolewa kupitia uchoraji wa katuni. Mfano
mzuri katika gaezeti laMwananchi kuna katuni
anazochora Masoud Kipanya utagundua kuwa
sanaa inayotumika kuchora katuni hizo ni ya hali
ya juu, na zaidi katuni hizo licha ya kuburudisha
huwa zinatoa ujumbe kwa Jamii juu ya mambo
mbalimbali kama vile siasa, ukizingatia mwaka
huu wa 2015 ni mwaka wa uchaguzi mkuu hapa
nchini Tanzania. Mbali na katuni zinazopatikana
katika gazeti la Mwananchi, pia kuna katuni
zinazochorwa na kuonyeshwa kwenye runinga
kwa mfano, kituo cha televisheni cha ITV katika
kipindi cha Habari kirushwapo hewani kuanzaia
saa mbili, kabla ya utabiri wa hali hewe huwa
kunaonyeshwa katuni kwa jina la “Kibonzo cha
leo” lengo ni kutoa ujumbe kwa Jamii na wakati
huohuo kuburudika kutokana na uasanii
uliotumika kuchorea katuni hizo.kwa upande
mwingine katika majarida ya FEMA huwa kuna
kipengele cha Mpendwa Aunt au Mpenndwa
uncle, huwa kuna maswali na majibu, lakini
maswali hayo yanayoulizwa huwa
yanaambatana na michoro ya katuni ambayo
uchorwa kwa ubunifu wa hali ya juu kwa lengo
la kusisitiza na kuleta picha halisi kutokana na
swali lilivyoulizwa.Hii ni mifano michache , wa
sanaa za zana ambazo zimechorwa kwa usanii
ila ipo mingi ambayo inatumika katika kutolea
Elimu kwa Jamii. Kwa namna hiyo utagundua
kuwa sanaa ina Nafasi kubwa sana katika Elimu
hapa nchini Tanzania.
NAFASI YA SANAA
KATIKA UCHUMI NCHINI
TANZANIA
Maisha ya binadamu kwa asilimia kubwa
yanatawaliwa na uchumi. Wakati tukizungumzia
uchumu , kila mwanadamu atakuwa na wazo juu
ya shughuri yoyote ambayo inahusisha
mzunguko wa fedha. Kwa namana hivyo kwa
kipindi kirefu binadamu amekuwa akifanya
shughuri nyingi za kiuchumi kama vile biashara,
uvuvi, kilimo na utarii. Japokuwa katika
shughuri za uchumi kuna vitu vingi, bado
binadamu hakuacha kutumia sanaa yake katika
shughuri za kiuchumi kwa kuunda vitu amabvyo
vilitumiaka kama bidhaa ambazo ziliuzwa na
kununuliwa kwa mfumo wa bidhaa kwa bidhaa
na kwa mfumo wa bidhaa kwa fedha. kwa
naman hiyo kila jamiii ilitumia wasanii ipasavyo
katika shughuri za kiuchumi. Na mpaka hivi
sasa kuna Jamii zinatumia sanaa katika uchumi
kwa kubuni na kuzalisha bidhaa mbalimbali
,kwa mfano kabila la Wamakonde wanaosifika
katika uchongaji wa vinyago, ambapo vinyago
hivyo vinauzwa na kununuliwa ndani na nje ya
Tanzania. Kutokana na biashara ya vinyago
hivyo jamii inaamini kuwa uchumi wao
unakuzwa au unaendelezwa kutokana na
biashara ya vinyago ambayo mchongaji
anatumia usanii wa hali ya juu kwa uhakikisha
kinyago kinakuwa na muonekano mzuri. Kwani
muonekano mzuri na wenye kuvutia ni kielelezo
cha bei ya kinyago hiko. Mbali na kukuza
utamaduni wamakonde wanaamini kuwa
biashara ya vinyago ni kubwa na inawanufaisha
wengi. Mbali na baishra ya vinyago hapa nchini
Tanzania sanaa inachukua nafasi hata kwenye
kilimo.usanii kwenye kilimo unahusika wakati
wa utengenezaji wa zana mbalimbali za kulimia.
Hapa inatupasa tuelewwe kuwa, usanii
unaotumika kutengenezea jembe, panga na visu
ni wa hali ya juu na sio kila mtu anaweza
kufanya hivyo. Sasa hali ya mtu kushindwa
kutengeneza zana za kilimo ndo unatoa nafasi
kwa msanii kutumia muda mwingi katika
kutengeneza zana za kilimo. Hapa tunapaswa
tuelewe kuwa usanii unaotumika kuundia jembe
ni wa hali ya juu, Kwani jembe linakuwa na
muonekano mzuri, japo tuelewe kuwa sio kila
kizuri ni zao la usanii,ila hapa tuanaangalia ni
kwa jinsi gani zana hizo zinaundwa na
kutumika katika shughuri za kiuchumi kama
kilimo.kwa upande mwingine shughuri kama ya
utalii, japo inatupasa tuelewe maana ya utalii,
kimsingi utalii ni hali ya watu au mtu kusafiri
ndani au nje ya nchi yake kwa lengo la kuona au
kusikia vitu mbavyo aidha vipo au havipo
mahali ambapo watu au mtu huyo anaish ili
kujifunza, kufurahi na kufanya utafiti. Kwa
namna hiyo kama kuna mtu kwa mfano anatoka
Mwanza
kuja Mtwara kuona kinyago cha kimakonde
huyu pia ni mtalii. Lakini pia kama kuna mtu
anatoka Ureno au Italia anakuja Tanzania
kuangalia kigoda cha mnyamwezi huyu pia ni
mtalii. Hivyo hapa tunaangalia nafasi ya sanaa
katika shughuri za utalii. Wizara ya maliasili na
utalii, inatambua kuwa utamdauni unachangia
kwa kiasi kikubwa katika kukuza utalii wa ndani
na wa nje. Kikubwa zaidi Jamii ambazo
zinatumia utamaduni wao kama sehemu ya utalii
ni kama wamasai wanaopatikana mkoani Arusha
na wamakonde ambao wanpatikiana kusini mwa
Tanzania. Hivyo utamaduni wa watu hawa
unatambulika kupitia nyimbo zao, mavazi yao
na michoro yao katika mwili. Ukichunguza kwa
umakini utagundua kuwa michoro, mavazi na
nyimbo hizo zinaundwa kwa usanii ,mkubwa
sana. Kuna usanii unatumika katika kuchora, na
kuna usanii unatumika katika kushona mavazi ili
yatambulishe Jamii husika. Hivyo basi kama
kuna usanii unatumika katika kuunda zana hizo ,
ambazo zinatambulisha utamaduni wa Jamii
fulani, na wizara ya maliasili na utalii inatambua
mchango wa utamaduni katika kukuza utalii,
basi wazi kuwa sanaa ina nafasi kubwa katika
kukuza utalii hapa nchini Tanzania. Labda
tutumie mfano mwingine wa makumbusho
ambapo ni moja ya sehemu muhimu za kitalii,
asilimia kubwa ya vitu ambavyo vinapatikana
makumbusho vingi vimeundwa kwa kutumia
usanii wa hali ya juu. Pamoja na zana hizo
zinatumiaka kuelezea historia ya Jamii fulani,
lakini ukiangalia kwa umakini utagundua zana
hizo zimetumia usanii wa hali ya juu. Kwa
mfano, vinyago vilivyopo katika makumbusho
ya Bagamoyo ni mfano mzuri wa zana zenye
kutambulisha utamaduni wa watu fulani. zana za
kivita na kilimo zilizopo makumbusho ya
Tembe la Dr. Livingstone pale Kwihala mkoani
Tabora zinawakilisha sanaa, kwani ufundi
mkubwa umetumika katika kuundia zana hizo.
Lakini pia zana za uvuvi zinazopatikana pale
makumbusho ya taifa mkoani Dar es salaam
utagundua kuwa zana hizo za asili zimeundwa
kwa usanii wa hali ya juu. Kwa namna hiyo
usanii huo ambao unawakilisha utamaduni wa
Jamii fulani umekuwa ni kivutio kwa watalii wa
ndani na wa nje hapa nchini Tanzania. Hivyo
tunatambua Nafasi ya sanaa katika uchumi
kupitia shughuri kama, kilimo, biashara na utalii.
Hitimisho
Kwa kuwa tumeshajua nafasi ya sanaa katika
elimu na uchumi hapa nchini Tanzania na kuona
faida zake kwenye Jamii, hivyo Jamii inapaswa
kutambua na kuthamini wanasanii. Kwani
wasanii hawa wana nafasi kubwa katika kujenga
na kuendeleza Jamii hapa nchini Tanzania. Kwa
kuwa hata serikali inatambua mchango wa
sanaa katika sekta mbalimbali kama sekta ya
maliasili na utalii, utamaduni na elimu, basi ni
wazi kwamba serikali inatakiwa kutoa elimu
kwa jamii, juu ya nafasi ya sanaa katika
shughuri za maendeleo. Elimu hiyo inapaswa
kutolewa katika mihadhara mbalimbali,
mashuleni na hata vyuoni. Elimu hiyo itasaidia
sana jamii kuelewa nafasi ya sanaa na faida zake
katika maendeleo ya taifa letu. Pamoja ya
kwamba wasanii wanatoka katika Jamii, ni wazi
kuwa Jamii inafahamu tu kuwa msanii ni nani,
lakini wengi hawatambui mchango wa usanii wa
msanii kwa Jamii hiyo. Mbali na utolewaji wa
elimu kwa jamii, serikali inapaswa kutambua
safasi ya sanaa katika uchumi na kufanya sanaa
kuwa na tija kwa msanii kwa kuona bidhaaa
zilizoundwa na msanii huyo zinapata soko la
uhakika. Hivyo serikali inapswa kuunda sera
ambayo italinda haki za wasanii na kuhakikisha
sanaa inanufaisha msanii mwenyewe, Jamii na
serikali. Lakini mbali na kuwa na sera
itakayolinda na kuendeleza sanaa na kuwa na
faida kwa msanii, jamii na serikali, serikali
inapaswa kuwa na orodha ya wasanii ili kujua
idadi ya wasanii ili iwe lahisi kutoa misaada kwa
wasanii hao, kwa mfano utoaji wa mikopo na
elimu. Kwa kufanya hivyo serikali itafanikiwa,
kwani misaada kwa wasanii inafika kama
ilivyopangwa na haitakuwa vigumu kwa
serilkali kukusanya mapato yatokanayo na
mauzo ya sanaa. Mbali na serikali jamii pia
inapaswa kuheshimu kazi za msanii na kutoa
mchango pale inapohitajika. Na kwa upande wa
msanii, yeye mwenyewe anapaswa kujitambua
na kuheshimu Nafasi aliyopewa na Jamii yake,
na vilevile wasanii wanapaswa kusoma kwa
bidii ili kuweza kutambua ulimwengu na
mabadiliko yake ya kila siku. Kwa kuzingatia
haya, sanaa hapa nchini itakuwa ni moja ya vitu
ambavyo vinachangia sana katika maendeleo ya
nchi kama ilivyo kwa nchi kama Marekani,
Uchina na Japani. Mungu ibariki Tanzania,
Mungu ibariki Afrika.
BIBLIOGRAFIA
Baraza La Sanaa Tanzania (1982) Falsafa ya sanaa Tanzania.
Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi (1999) sera ya utamaduni
Wark, K (2003) Art History. Hodder Arnold, 338 Euston Road, London, UK.
UNESCO (202) Tell Me About: World Heritage. Published by United National Educational, Science and
Cultural Organization, 7, place de Fontenoy 75352, Paris 07 SP, France.

More Related Content

Featured

AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdfAI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
marketingartwork
 
Skeleton Culture Code
Skeleton Culture CodeSkeleton Culture Code
Skeleton Culture Code
Skeleton Technologies
 
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
Neil Kimberley
 
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
contently
 
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
Albert Qian
 
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie InsightsSocial Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Kurio // The Social Media Age(ncy)
 
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Search Engine Journal
 
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
SpeakerHub
 
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
Clark Boyd
 
Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next
Tessa Mero
 
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search IntentGoogle's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Lily Ray
 
How to have difficult conversations
How to have difficult conversations How to have difficult conversations
How to have difficult conversations
Rajiv Jayarajah, MAppComm, ACC
 
Introduction to Data Science
Introduction to Data ScienceIntroduction to Data Science
Introduction to Data Science
Christy Abraham Joy
 
Time Management & Productivity - Best Practices
Time Management & Productivity -  Best PracticesTime Management & Productivity -  Best Practices
Time Management & Productivity - Best Practices
Vit Horky
 
The six step guide to practical project management
The six step guide to practical project managementThe six step guide to practical project management
The six step guide to practical project management
MindGenius
 
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
RachelPearson36
 
Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...
Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...
Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...
Applitools
 
12 Ways to Increase Your Influence at Work
12 Ways to Increase Your Influence at Work12 Ways to Increase Your Influence at Work
12 Ways to Increase Your Influence at Work
GetSmarter
 
ChatGPT webinar slides
ChatGPT webinar slidesChatGPT webinar slides
ChatGPT webinar slides
Alireza Esmikhani
 
More than Just Lines on a Map: Best Practices for U.S Bike Routes
More than Just Lines on a Map: Best Practices for U.S Bike RoutesMore than Just Lines on a Map: Best Practices for U.S Bike Routes
More than Just Lines on a Map: Best Practices for U.S Bike Routes
Project for Public Spaces & National Center for Biking and Walking
 

Featured (20)

AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdfAI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
 
Skeleton Culture Code
Skeleton Culture CodeSkeleton Culture Code
Skeleton Culture Code
 
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
 
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
 
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
 
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie InsightsSocial Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
 
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
 
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
 
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
 
Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next
 
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search IntentGoogle's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
 
How to have difficult conversations
How to have difficult conversations How to have difficult conversations
How to have difficult conversations
 
Introduction to Data Science
Introduction to Data ScienceIntroduction to Data Science
Introduction to Data Science
 
Time Management & Productivity - Best Practices
Time Management & Productivity -  Best PracticesTime Management & Productivity -  Best Practices
Time Management & Productivity - Best Practices
 
The six step guide to practical project management
The six step guide to practical project managementThe six step guide to practical project management
The six step guide to practical project management
 
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
 
Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...
Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...
Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...
 
12 Ways to Increase Your Influence at Work
12 Ways to Increase Your Influence at Work12 Ways to Increase Your Influence at Work
12 Ways to Increase Your Influence at Work
 
ChatGPT webinar slides
ChatGPT webinar slidesChatGPT webinar slides
ChatGPT webinar slides
 
More than Just Lines on a Map: Best Practices for U.S Bike Routes
More than Just Lines on a Map: Best Practices for U.S Bike RoutesMore than Just Lines on a Map: Best Practices for U.S Bike Routes
More than Just Lines on a Map: Best Practices for U.S Bike Routes
 

MAKALA

  • 1. SEMINA KWA JAMII JUU YA NAFASI YA SANAA KATIKA ELIMU NA UCHUMI NCHINI TANZANIA | MAYUNI JOSEPH
  • 2. Utangulizi Sanaa katika maisha ya binadamu inachukua Nafasi kubwa sana. Kabla ya kujua Nafasi ya sanaa katika elimu na uchumi, hebu tujadili maana ya sanaa, licha ya wataalamu wengi kujadili maana ya sanaa kama vile Plato, Kirsty Wark, Joseph Beuys, Emmanuel Kant na Allexander Baumgarten. Hapa tutaangalia maana ya sanaa moja kwa moja kwa kujumuisha mawazo ya wataalamu waliofafanua maana ya sanaa. Kwa ujumla sanaa ni uwezo alionao kila binadamu wa kuunda kitu kwa upekee kwa madhumuni ya kukidhi mahitaji ya jamii kwa kuanagalia nyanja za kisiasa, kijamii na kiuchumi kwa faida ya kizazi cha sasa na kizazi cha badae. Kwa namna hiyo sanaa ni ujuzi ambao binadamu anautumia kuunda vitu mbalimbali kwa ajili ya manufaa ya jamii.kwa mfano msanii anapochora picha, anapoimba wimbo na anapochonga kinyago lengo kuu sio kufurahisjha nafsi yake, bali lengo ni kuhakikisha jamii inanufaika kwa kugusa nyanza zote za jamii yaani kiuchumi, kisiasa na kijamii. Kwa hiyo hapa kila binadamu ni msanii, Kwani kila binadamu anazaliwa na kipaji kama anavyosema Plato alipokuwa kufafanua falsafa ya elimu juu ya asili ya mwanafunzi. Lakini pia wazo hili linaungwa mkono na mwanafalsafa wa kijerumani ajukanaae kama Joseph Beuys. Joseph Bueys anafafanua kuwa “Every human being is an artist…by artist I don’t just mean people who produce and scripture or play the piano, or composers or writers. For me a nurses is also an artist, or, of course, a doctor or a teacher. a student too, a young person responsible for his own development. The essence of man is captured in the description ‘artist’ Extracted from state of art, Sandy Nairne, Chatto and Windus, 1987 Kwa namna hiyo tunatambua mchango wa sanaa kwa kuona vitu ambavyo vinaundwa kutokana na sanaa hiyo ambayo binadamu anaitumia katika maisha yake ya kila siku. Lakini pia ni wazi kuwa jamii inatambua kuwa katika maisha ya binadamu sanaa ina nafasi kubwa sana. kimsingi tumeona kuwa sanaa ilikuwepo hata baada ya binadamu kuwepo, na binadamu ameikuta sanaa kama alivyokuta vitu vingine hapa duniani kama vitabu vya dini(ukristo na uislamu) vinavyosema. Lakini je? sana ya Tanzania imegawanyika katika sehemu kuu ngapi. Mgawanyiko wa sanaa kwa mujibu wa Baraa la Sanaa Tanzania (BASATA) katika kitabu kijulikanacho kama Falsafa ya sanaa ya Tanzania linagawa sanaa katika makundi mawili ambayo ni sanaa za hisi na sanaa za zana. Kwa kuanza na sanaa za hisi, ni aina ya sanaa ambazo o bindamu anatambua kwa kutumia milango ya fahamu inayojulikana kama, ulimi kwa kuonja, macho kwa kuona, ngozi kwa kugusa na pua kwa kunusa. Kwanamna hii fungu hili la sanaa binadamu anapaswa kutambua ujumbe ambao msanii anataka kuutoa kwa jamii yake kwa kutumia milango hiyo ya fahamu. Kimsingi sanaa hisi mara nyingi huitaji akili nyingi itumike na binadamu ili kujua msanii ana malengo gani kwa Jamii husika. Kwa mfano wa sanaa za hisi ni matumizi ya michoro amayo haina maelezo na hata kama yanamaelezo huwa si laisi kutambua msanii analengo gani kwa Jamii yake. Kwa mfano katika kazi nyingi za kifasihi kwa upande wa fasihi andishi, ambapo tunapata ushairi, riwaya na tamthilia. Mara nyingi tunashuhudia ganda la kitabu likiwa na picha ambazo zipo zinazofanana na jina la kitabu na zingine hazifanani na jina la kitabu kwa mfano, katika kitabu cha , Morani, Kivuli Kinaishi, Watoto wa mama N’tilie, ukiangalia maganda ya vitabu hivi vya kifasihi utagundua kuwa umetumika usanii wa kutosha katika kuunda picha na mpangilio wa rangi, ambapo inampasa msomaji awe makini ili kutambua uhusiano uliopo kati ya ganda la kitabu na jina la kitabu, na vilivyomo ndani ya kitabu . Kwa ujumla sanaa hizi
  • 3. zinajulikana sanaa za hisi kwani zinahitaji kutambuliwa kwa milango ya fahamu ya binadamu kwa kuhususha fikra yakinifu. Kwa upande wa sanaa za zana, hizi ni sanaa ambazo zinaweza kutumika katika kutoa mafunzo ya wazi na mara nyingi vifaa na zana zilizotumika uonekana na kuguswa, kwani fungu hilim la sanaa mara nyingi vinavyoundwa na jamii hutumika moja kw moja na jamii husika kama zana katika shughuri maalumu. Hapa binadamu sio lazima utumie milango yote ya fahamu ili kuweza kutambua ujumbe uliokusudiwa na msanii kwa jamii yake. Cha msingi hapa ni kwamba sanaa hizi za zana utumia maumbo halisi ambayo binadamua anayatumia kila kukicha, kwa mfano alama za barabarani, zana za kufundishia darasani, ambapo zana hizi utumia usanii wa hali ya juu katika uundaji wake. Kwa ujumla sanaa za zana ni laisi kutambuliwa na zinakuwepo kwa lengo maalumu kwa Jamii bila kificho.Kwa namana hiyo tunaona nI kwa jinsi gani Baraa la Sanaa Tanzania (BASATA) katika kitabu kijulikanacho kama Falsafa ya sanaa ya Tanzania limefanikiwa kugawa makundi haya ya sanaa kwa kuangalia Jamii ya kitanzania na mazingira yake. Na baaada ya kuona mafungu haya ya sanaa sasa tuone Nafasi ya sanaa katika Jamii ya kitanzania kwa kipindi chote MAISHA YA BINADAMU NA SANAA Kwa kipindi kirefu binadamu amekuwa akitumia sanaa kama nyenzo muhimu katika shughuri mbalimbali za kiuchumi, kisiasa na kijamii. Kwa namna hiyo sanaa imekuwa na umuhimu mkubwa kwa maisha ya binadamu kwa kipindi chote.Kwa mfano katika siasa UMBO 1: Nyumba inajengwa kwa udongo ambao umefinyangwa na kukandikwa kwa usanii wa hali ya juu binadamu alitumia sanaa za zana kuunda vitu mbalimbali ambavyo vilitumiwa na viongozi mbalimbali kwa mfano, mavazi ya wanajeshi na mavazi kwa ajili ya watemi na wafalme na vifaa vya kufanyia kazi kama vile meza na viti ambavyo vimebuniwa kwa usanii ambao bindamu aliutumia.Kwa upande wa uchumi binadamu alitumia zana mbalimbali ambazo pia zimebuniwa na kutumika kama bidhaa, kwa mfano nyungo, vigoda,kawa na viatu , ambavyo viliuzwa na vilitumika kama bidhaa zenye thamani. Lakini pia sanaa in nafasi katika masuala ya kijamii, ambapo sanaa inatumika kutengenezea vitu ambavyo vinatumika na makabila mbalimbali kama kitambulisho na vitu muhimu kwa kabila hilo, kwa mfano usanii unaotumika kutengenezea vinyago kwa kabila
  • 4. ya Wamakonde, ni kitambulisho tosha kwa Wamakonde. Na hata kwa upande wa michoro inayochorwa na kabila la Wamakonde ambayo inajulikana kama (chale) inatumia usanii wa kutosha wakati wa kuchora. Kwa namna hiyo sanaa ina nafasi kubwa sana katika Jamii ya Tanzania tokea wanzo hadi sasa kwenye karne ya 21.Hivyo ni jukumu la kila mtanzania kujua nafasi ya sanaa katika nyanja za elimu, uchumi na kijamii.Sasa tuangalie kwa ufupi nafasi ya sanaa katika elimu na uchumi katika jamii ya kitanzania. NAFASI YA SANAA KATIKA ELIMU NCHINI TANZANIA Kwa kuwa tumeshafahamu maana ya sanaa, hivyo haina haja ya kurudia kufafanua dhana hii. Na hivyo tutaangalia maana ya msingi ya neno Elimu, dhana ya Elimu imefafanuliwa na wanafalsafa wengi sana wa elimu na hapa nitataja wachache tu kwa mfano Julius Kambarage Nyerere, Plato, Aristotle, Socrates, john Agrey na Maria Montessori. Lakini ki msingi elimu ni utaratibu uliowekwa na Jamii ambapo mafunzo, ujuzi, hekima na urithi unahamishwa kutoka kwa kizazi kimoja hadi kingine kwa lengo la kuhakikisha mahitaji na malengo ya Jamii yanatimizwa bila kukiuka imani na maadili ya jamii husika.Ufafanuzi huu unafanana sana na ule wa maana ya sanaa, kwani malengo ya sanaa ni kukidhi mahitaji ya jamii, tukichunguza kwa umakini malengo ni hayo hayo yanayolengwa na dhana ya elimu. Kwa namna hiyo kutokana na uhusiano huo wa elimu na sanaa, Jamii inapaswa kutumia elimu na sanaa kama nguzo au nyenzo muhimu ya kukidhi mahitaji ya Jamii kwa kipindi chote. Jamii itatumia vitu mbalimbali vilivyoundwa na binadamu kwa usanii na akili ya hali ya juu kama sehemu ya kutolea mafunzo. Na mara nyingi utengenezwaji wa zana hizo zinahitaji usanii na elimu wa hali ya juu ili kuvutia na kuleta ujumbe kwa Jamii husika.Kwa kuwa Jamii inahitaji watu ambao watatumia akili zao na ujuzi wao katiuka kubuni na kuunda zana za kutolewa elimu kwa mfano, Mwalimu darasani anapotumia zana ambayo imetumia usanii wa hali ya juu kufundishia , kwa mfano mwalimu anapohitaji kufundisha wanafunzi kuhusu mlima Kilimanjaro ni wazi kwamba picha itayochorwa pale ni mlima kilimanjro.Lakini mlima huo hautachorwa kwa mzaha, bali utatumia usanii mwingi na akili nyingi. Hivyo kwa kuwa lengo la elimu ni kutoa mafunzo kwa wanafunzi, ni wazi kuwa uchoraji wa mlima kilimanjaro hautakuwa wa mzaha, bali utahitaji umakini kwa msanii atayechora au kuchonga kitu kitakacho fanana na mlima kilimanjaro. Mpaka hapa sanaa imetambulika wazi katika suala zima la elimu.na kwa namna hivyo ufundishaji ambao unatumia
  • 5. zana zilizoundwa kwa usanii zitakuwa na faida zifuatazo kwa wanafunzi. •Ufundishaji unaotumia zana za kisanii hukuza udadisi kwa wanafunzi, Kwani picha hiyo itamfanaya mwanafunzi kujenga picha juu ya kitu halisi katika ubongo wake.kwan kitabia picha huwa na vitu vingi, vitu hivyo vitamfanya mwanafunzi kuwa mdadisi kwa kujifunza vitu vingi zaidi ya mlima, kwa mfano kwenye mlima kuna miti, hivyo wanafunzi wanaweza kutoa maelezo mengi juu ya mlima Kilimanjaro kuhusiana na miti iliyokuwepo. Hivyo kufanya wanafunzi kuwa na ujuzi wa kudadisi kutokana na picha wanayoiona ambayo imetumia usanii wa hali ya juu.na mwisho itasababisha kuwa na taifa ambalo watu wake ni wadadisi kwa maendeleo ya taifa. •Ufundishaji unaotumia zana za kisanii hukuza vipaji vya wanafunzi, kwa kuwa wanasaikolojia na wanafalsafa wanaamini kuwa kuwa kila binadamu ni msanii, bila shaka hata darasani kuna wasnii pia. Niweke wazi kwamba, wanafunzi wanapokuwa shuleni huwa wanafanya mambo mengi yenye kuhusiana na viapaji, wapo wanaofanya mambo makubwa na kushangaza walimu wao na wapo wanaofanya ya kawaida, ila hoja ipo palepale nvyote ni vipaji.kama sula hapa ni vipaji vya wanafunzi, ni vema tukampa nafasi Mwalimu ambaye anatumia zana zilizochorwa kwa usanii wa hali ya juu. Kwani mwanafunzi atakapoona picha mbele ya ubao, ataweza kujaribu kuchora picha hiyo. Hivyo usanii utachukua nafasi kwa mwanafunzi huyo kutokana na zana iliyotumiwa na Mwalimu wakati wa kutoa Elimu. • Ufundishaji unaotumia zana za kisanii hukuza ushirikiano baina ya Mwalimu na wanafunzi, lazima tufahamu kuwa, katika mchakato wa ufundishaji darasani jambo la msingi ni ushirikiano baina ya mwalimu na mwanafunzi. Hivyo matumizi ya zana za kisanii katika mchakato wa ufundishaji utajenga ushirikiano kati ya Mwalimu na mwanafunzi ambapo kila mwanafunzi atakuwa tayari na makini kuona picha ambayo imechorwa kwa ubunifu kutokana na usanii wa mwalimu. Kitendo hicho kinamfanya mwalimu kuwa karibu na wanafunzi Kwani, kuna baadhi ya picha zitamfanya mwanafunzi kuuliza maswali kwa Mwalimu. Wakati mwingine, mwanafunzi atataka, kujua zaidi juu ya usanii uliotumika hapo. Hivyo itamlazimu kuwa karibu na Mwalimu na kufanya majadiliano ya kina na yenye kueleweka na mwanafunzi husika. Na ikumbukwe kuwa lengo la Mwalimu kutumia zana za kufundishia ni kutoa mafunzo yenye kueleweka , ambapo Mwalimu atahitaji kufahamu na kujua kila mwanafunzi kama ameelewa somo au lah! Kitu ambacho kinakuza ushikiano na mahusiano baina ya Mwalimu na mwanafunzi. Kimsingi sana katika elimu ina nafasi kubwa sana kwani asilimia kadhaa ya zana na vitu vinatumika shuleni hasa wakati wa kufundishia vimeundwa kwa usanii mkubwa sana.lakini pia sanaa kwenye elimu inatumika pia kwenye nyimbo, mashairi na maigizo, ambayo hubeba ujumbe ambapo Jamii inapaswa
  • 6. kujifunza, kwa wakati huu, msanii anakuwa walimu na jamii inakuwa mwanafunzi. Kwa hiyo ni matarajio ya Jamii kuona usanii wa msanii atatumika kuundia zana ambayo itatoa Elimu kwa Jamii hiyo kwa mfano, nyimbo zitakazoimbwa, maigizo yatakayoigizwa na vinyago vitakavyochongwa ni wazi kwamba vinapaswa kutoa ujumbe kwa Jamii hisuka. Kwa ujumla Jamii ya kitanzania inatambua nafasi ya sanaa kwenye elimu, Kwani katika Jamii ya kitanzania msanii anaheshimika na kupewa nafasi kubwa katika jamii.Hivyo sanaa ina nafasi katika elimu hapa nchini Tanzania. Mbali na shuleni sanaa inatumika kutolea Elimu katika Jamii hapa nchini Tanzania, kupitia kampeni mbalimbali. Elimu inatolewa na sanaa kwa Jamii huwa inalengo la, kutoa maelekezo au kuonya. Kwa namna hiyo katika jamii mbali na sanaa ya mziki na maigizo ambayo ndo yanafahamika sanaa na Jamii zetu hapa nchini Tanzania, zipo sanaa ambazo zinatumika sana kutolea Elimu kwa Jamii kuzidi sanaa ya kuimba au sanaa ya maigizo.kwa mfano sanaa ya uchoraji ni moja ya sanaa ambayo inashika safasi kubwa katika kuahakikisha Jamii ya Tanzania inapata Elimu inayotakiwa. Labda tuchukue mfano huu wa alama za barabarani, alama za barabarani ni moja ya mfano wa sanaa za zana, hivyo kazi kubwa za alama barabarani ni kutoa maelekezo kwa watumiaji wa barabara. Lakini ukiangalia kwa makini sanaa iliyotumika kuchora alama zile utagundua kuwa kuna usanii umechukua Nafasi yake. Licha ya kwamba lengo la alama hizi sio kutambulisha usanii, ila hapa tunaangalia Nafasi ya sanaa katika utengenezwaji wa alama hizi. Uchoraji na upangaji wa rangi unahitaji usanii wa hali ya juu. Kwa mfano alama inayoonesha hapa ni kivuko cha ng’ombe ni lazima achorwe ng’ombe, kwa namna hiyo tunaona sanaa ya uchoraji inachukua Nafasi yake. Labda tuchukue mfano mwingine, alama inayoonesha kuwa hapa ni kutuo cha basi, ni lazima picha inayofanana na basi itachorwa, ambapo sanaa ya uchoraji inatumika. Mbali na alama za barabarani kuna Elimu zinatolewa kupitia uchoraji wa katuni. Mfano mzuri katika gaezeti laMwananchi kuna katuni anazochora Masoud Kipanya utagundua kuwa sanaa inayotumika kuchora katuni hizo ni ya hali ya juu, na zaidi katuni hizo licha ya kuburudisha huwa zinatoa ujumbe kwa Jamii juu ya mambo mbalimbali kama vile siasa, ukizingatia mwaka huu wa 2015 ni mwaka wa uchaguzi mkuu hapa nchini Tanzania. Mbali na katuni zinazopatikana katika gazeti la Mwananchi, pia kuna katuni zinazochorwa na kuonyeshwa kwenye runinga kwa mfano, kituo cha televisheni cha ITV katika kipindi cha Habari kirushwapo hewani kuanzaia saa mbili, kabla ya utabiri wa hali hewe huwa kunaonyeshwa katuni kwa jina la “Kibonzo cha leo” lengo ni kutoa ujumbe kwa Jamii na wakati huohuo kuburudika kutokana na uasanii uliotumika kuchorea katuni hizo.kwa upande mwingine katika majarida ya FEMA huwa kuna kipengele cha Mpendwa Aunt au Mpenndwa uncle, huwa kuna maswali na majibu, lakini maswali hayo yanayoulizwa huwa yanaambatana na michoro ya katuni ambayo uchorwa kwa ubunifu wa hali ya juu kwa lengo la kusisitiza na kuleta picha halisi kutokana na swali lilivyoulizwa.Hii ni mifano michache , wa sanaa za zana ambazo zimechorwa kwa usanii ila ipo mingi ambayo inatumika katika kutolea Elimu kwa Jamii. Kwa namna hiyo utagundua kuwa sanaa ina Nafasi kubwa sana katika Elimu hapa nchini Tanzania.
  • 7. NAFASI YA SANAA KATIKA UCHUMI NCHINI TANZANIA Maisha ya binadamu kwa asilimia kubwa yanatawaliwa na uchumi. Wakati tukizungumzia uchumu , kila mwanadamu atakuwa na wazo juu ya shughuri yoyote ambayo inahusisha mzunguko wa fedha. Kwa namana hivyo kwa kipindi kirefu binadamu amekuwa akifanya shughuri nyingi za kiuchumi kama vile biashara, uvuvi, kilimo na utarii. Japokuwa katika shughuri za uchumi kuna vitu vingi, bado binadamu hakuacha kutumia sanaa yake katika shughuri za kiuchumi kwa kuunda vitu amabvyo vilitumiaka kama bidhaa ambazo ziliuzwa na kununuliwa kwa mfumo wa bidhaa kwa bidhaa na kwa mfumo wa bidhaa kwa fedha. kwa naman hiyo kila jamiii ilitumia wasanii ipasavyo katika shughuri za kiuchumi. Na mpaka hivi sasa kuna Jamii zinatumia sanaa katika uchumi kwa kubuni na kuzalisha bidhaa mbalimbali ,kwa mfano kabila la Wamakonde wanaosifika katika uchongaji wa vinyago, ambapo vinyago hivyo vinauzwa na kununuliwa ndani na nje ya Tanzania. Kutokana na biashara ya vinyago hivyo jamii inaamini kuwa uchumi wao unakuzwa au unaendelezwa kutokana na biashara ya vinyago ambayo mchongaji anatumia usanii wa hali ya juu kwa uhakikisha kinyago kinakuwa na muonekano mzuri. Kwani muonekano mzuri na wenye kuvutia ni kielelezo cha bei ya kinyago hiko. Mbali na kukuza utamaduni wamakonde wanaamini kuwa biashara ya vinyago ni kubwa na inawanufaisha wengi. Mbali na baishra ya vinyago hapa nchini Tanzania sanaa inachukua nafasi hata kwenye kilimo.usanii kwenye kilimo unahusika wakati wa utengenezaji wa zana mbalimbali za kulimia. Hapa inatupasa tuelewwe kuwa, usanii unaotumika kutengenezea jembe, panga na visu ni wa hali ya juu na sio kila mtu anaweza kufanya hivyo. Sasa hali ya mtu kushindwa kutengeneza zana za kilimo ndo unatoa nafasi kwa msanii kutumia muda mwingi katika kutengeneza zana za kilimo. Hapa tunapaswa tuelewe kuwa usanii unaotumika kuundia jembe ni wa hali ya juu, Kwani jembe linakuwa na muonekano mzuri, japo tuelewe kuwa sio kila kizuri ni zao la usanii,ila hapa tuanaangalia ni kwa jinsi gani zana hizo zinaundwa na kutumika katika shughuri za kiuchumi kama kilimo.kwa upande mwingine shughuri kama ya utalii, japo inatupasa tuelewe maana ya utalii, kimsingi utalii ni hali ya watu au mtu kusafiri ndani au nje ya nchi yake kwa lengo la kuona au kusikia vitu mbavyo aidha vipo au havipo mahali ambapo watu au mtu huyo anaish ili kujifunza, kufurahi na kufanya utafiti. Kwa namna hiyo kama kuna mtu kwa mfano anatoka Mwanza
  • 8. kuja Mtwara kuona kinyago cha kimakonde huyu pia ni mtalii. Lakini pia kama kuna mtu anatoka Ureno au Italia anakuja Tanzania kuangalia kigoda cha mnyamwezi huyu pia ni mtalii. Hivyo hapa tunaangalia nafasi ya sanaa katika shughuri za utalii. Wizara ya maliasili na utalii, inatambua kuwa utamdauni unachangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza utalii wa ndani na wa nje. Kikubwa zaidi Jamii ambazo zinatumia utamaduni wao kama sehemu ya utalii ni kama wamasai wanaopatikana mkoani Arusha na wamakonde ambao wanpatikiana kusini mwa Tanzania. Hivyo utamaduni wa watu hawa unatambulika kupitia nyimbo zao, mavazi yao na michoro yao katika mwili. Ukichunguza kwa umakini utagundua kuwa michoro, mavazi na nyimbo hizo zinaundwa kwa usanii ,mkubwa sana. Kuna usanii unatumika katika kuchora, na kuna usanii unatumika katika kushona mavazi ili yatambulishe Jamii husika. Hivyo basi kama kuna usanii unatumika katika kuunda zana hizo , ambazo zinatambulisha utamaduni wa Jamii fulani, na wizara ya maliasili na utalii inatambua mchango wa utamaduni katika kukuza utalii, basi wazi kuwa sanaa ina nafasi kubwa katika kukuza utalii hapa nchini Tanzania. Labda tutumie mfano mwingine wa makumbusho ambapo ni moja ya sehemu muhimu za kitalii, asilimia kubwa ya vitu ambavyo vinapatikana makumbusho vingi vimeundwa kwa kutumia usanii wa hali ya juu. Pamoja na zana hizo zinatumiaka kuelezea historia ya Jamii fulani, lakini ukiangalia kwa umakini utagundua zana hizo zimetumia usanii wa hali ya juu. Kwa mfano, vinyago vilivyopo katika makumbusho ya Bagamoyo ni mfano mzuri wa zana zenye kutambulisha utamaduni wa watu fulani. zana za kivita na kilimo zilizopo makumbusho ya Tembe la Dr. Livingstone pale Kwihala mkoani Tabora zinawakilisha sanaa, kwani ufundi mkubwa umetumika katika kuundia zana hizo. Lakini pia zana za uvuvi zinazopatikana pale makumbusho ya taifa mkoani Dar es salaam utagundua kuwa zana hizo za asili zimeundwa kwa usanii wa hali ya juu. Kwa namna hiyo usanii huo ambao unawakilisha utamaduni wa Jamii fulani umekuwa ni kivutio kwa watalii wa ndani na wa nje hapa nchini Tanzania. Hivyo tunatambua Nafasi ya sanaa katika uchumi kupitia shughuri kama, kilimo, biashara na utalii.
  • 9. Hitimisho Kwa kuwa tumeshajua nafasi ya sanaa katika elimu na uchumi hapa nchini Tanzania na kuona faida zake kwenye Jamii, hivyo Jamii inapaswa kutambua na kuthamini wanasanii. Kwani wasanii hawa wana nafasi kubwa katika kujenga na kuendeleza Jamii hapa nchini Tanzania. Kwa kuwa hata serikali inatambua mchango wa sanaa katika sekta mbalimbali kama sekta ya maliasili na utalii, utamaduni na elimu, basi ni wazi kwamba serikali inatakiwa kutoa elimu kwa jamii, juu ya nafasi ya sanaa katika shughuri za maendeleo. Elimu hiyo inapaswa kutolewa katika mihadhara mbalimbali, mashuleni na hata vyuoni. Elimu hiyo itasaidia sana jamii kuelewa nafasi ya sanaa na faida zake katika maendeleo ya taifa letu. Pamoja ya kwamba wasanii wanatoka katika Jamii, ni wazi kuwa Jamii inafahamu tu kuwa msanii ni nani, lakini wengi hawatambui mchango wa usanii wa msanii kwa Jamii hiyo. Mbali na utolewaji wa elimu kwa jamii, serikali inapaswa kutambua safasi ya sanaa katika uchumi na kufanya sanaa kuwa na tija kwa msanii kwa kuona bidhaaa zilizoundwa na msanii huyo zinapata soko la uhakika. Hivyo serikali inapswa kuunda sera ambayo italinda haki za wasanii na kuhakikisha sanaa inanufaisha msanii mwenyewe, Jamii na serikali. Lakini mbali na kuwa na sera itakayolinda na kuendeleza sanaa na kuwa na faida kwa msanii, jamii na serikali, serikali inapaswa kuwa na orodha ya wasanii ili kujua idadi ya wasanii ili iwe lahisi kutoa misaada kwa wasanii hao, kwa mfano utoaji wa mikopo na elimu. Kwa kufanya hivyo serikali itafanikiwa, kwani misaada kwa wasanii inafika kama ilivyopangwa na haitakuwa vigumu kwa serilkali kukusanya mapato yatokanayo na mauzo ya sanaa. Mbali na serikali jamii pia inapaswa kuheshimu kazi za msanii na kutoa mchango pale inapohitajika. Na kwa upande wa msanii, yeye mwenyewe anapaswa kujitambua na kuheshimu Nafasi aliyopewa na Jamii yake, na vilevile wasanii wanapaswa kusoma kwa bidii ili kuweza kutambua ulimwengu na mabadiliko yake ya kila siku. Kwa kuzingatia haya, sanaa hapa nchini itakuwa ni moja ya vitu ambavyo vinachangia sana katika maendeleo ya nchi kama ilivyo kwa nchi kama Marekani, Uchina na Japani. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
  • 10. BIBLIOGRAFIA Baraza La Sanaa Tanzania (1982) Falsafa ya sanaa Tanzania. Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi (1999) sera ya utamaduni Wark, K (2003) Art History. Hodder Arnold, 338 Euston Road, London, UK. UNESCO (202) Tell Me About: World Heritage. Published by United National Educational, Science and Cultural Organization, 7, place de Fontenoy 75352, Paris 07 SP, France.