SlideShare a Scribd company logo
1 of 84
THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY
LTD
KARIBUNI
KWENYE MAFUNZO YANAYOHUSU UFUATILIAJI NA
TATHIMINI NA UANDIKAJI WA RIPOTI
MUDA WA MASOMO
TAREHE: J uly 15 – 19, 2013
Wawezeshaji: Adam Makarang
Ibrahim
Ugullumu
Phares Maugo
08/15/15 3
Mambo muhimu
 Kujitambulisha
◦ Jina
◦ Taasisi unayotoka
◦ Nafasi yako katika taasisi tajwa
◦ Nk
 Kukubaliana juu ya kanuni za warsha
 Kuchagua M/kiti, katibu na mtunza muda
 Mafunzo kuanza
Matarajio ya washiriki
1
2
3
4
5
Lengo la mafunzo
1.Kuwawezesha washiriki wa washa kutambua
na kutofautisha kati ya Mradi na shughuli za
mradi.
2.Kuwawezesha washiriki wa washa kuelewa
maana ya ufuatiliaji na tathimini na tofauti
zake.
3.kutumia Bao Mantiki kama nyenzo ya kubuni
na kuendeshaji mradi na njisi inavyotumika
wakati wa ufuatiliaji na tathimini.
4. Kujengea washiriki umuhimu faida ya kufanya
ufuatiliaji na tathimini kwa manufaa ya kufikia
matokeo yaliyoktarajiwa.
5. Kuwawezesha washiriki kuandaa nyesho rahisi
ya mfumo wa ufuatiliaji na tathimini ambayo
inaweza kutumiwa na asasi zao.
6. Kuwajengea washiriki uelewa na ujuzi wa jinsi
ya kupata taarifa na takwimu kwa ajili ya
mfumo wa ufuatiliaji na tathimini ya asasi zao
7.Kuwawezesha kufanya makisiyo ya matokeo.
8. Kuwajengea msingi wa ujuzi kuhusiana na
mfumo wa ufuatiliaji na tathimini katika
kukusanya, kutoa na kusambaza taarifa.
9. Kutambua viashira/Vigezo na namna ya
kuvitumia na kuvifuatilia.
10. Kupima Matokeo na mabadiliko yatokanayo na
utekelezaji wa mradi husika katika Asasi zenu
MADA ZA MAFUNZO YA UFUATILIAJI NA TATHIMINI
1. Maana ya maneno muhimu katika mafunzo
ya ufuatiliaji na tathimini.
2. Bao Mantiki kama nyenzo ya ufuatiliaji na
tathimini.
3. Uandaaji na matumizi ya mpango wa
ufuatiliaji na tathimini
4. Ukusanyaji, utunzaji wa taarifa
5. Uandaaji na usambazaji wa taarifa(Utoaji wa
Ripoti)
UFUATILIAJI NA TATHIMINI
 MAANA YA UFUATILIAJI:
 Ufuatiliaji ni mchakato wa kuhakiki au kuthibitisha kama mpango
wa utekelezaji wa shughuli za mradi unaendelea kama
ulivyopangwa
 Ufuatiliaji hutoa taswira juu ya namna gani mradi unavyo
simamiwa. Hii ni shughuli ambayo hufanyika muda wote wa
mradi, yaani kila siku, kila wiki na kila mwezi. Kiutendaji,
ufuatiliaji unajikita katika kukusanya taarifa zinazoonyesha kama
rasilimali zimekusanywa, shughuli zimefanyika na kama matokeo
ya awali yamepatikana kama ilivyopangwa.
Umuhimu wa Ufuatiliaji
Kwa ujumla, Ufuatiliaji husaidia:
 Kubaini mapungufu kwa wakati muafaka ili kutoa
ufumbuzi kabla mapungufu hayo hayajawa makubwa.
 Kufahamu jinsi rasilimali zinavyotumika.
 Kujua wa kiwango gani shughuli zimetekelezwa.
 Kutoa taarifa mahususi kwa wakati muafaka ili kufanya
maamuzi yanayowezesha kusimamia vizuri rasilimali na
hivyo kuweza kupata matokeo mazuri kwa gharama
nafuu.
Umuhimu wa Ufuatiliaji ( inaendelea)
Ufuatiliaji mzuri huwezesha kuwepo mchanganyiko
mzuri wa rasilimali ili kutekeleza shughuli tarajiwa na
kuhakikisha walengwa wanatumia matokeo ili
kuboresha hali zao
Tathmini
 Maana ya Tathmini
 Ni mchakato wa kukusanya taarifa/takwimu na
kuzichambua ili kupima kama lengo mahususi
limefanikiwa ili kupima mabadiliko (impact)
ambayo mradi umechangia katika maisha ya
walengwa kutokana na mradi. Tathmini pia
huchambua kufaa (relevance) kwa mradi na
muundo wake.
Umuhimu wa Tathmini
Kwa ujumla, Tathmini:
 Huboresha ufanisi (performance):
• Kama tathmini ikifanyika kwa nia njema na kwa msukumo wa
ndani (siyo wa wafadhili tu), taarifa na mapendekezo ya
Tathmini husaidia kuboresha mradi mzima.
• Ujuzi toka mradi uliokamilika unaweza kutumika kuboresha na
kusaidia uundaji wa mradi unaofuata.
 Huongeza uwajibikaji
• Taarifa za mradi zinazotolewa mara kwa mara kwa wadau husaidia
kubaini mapungufu na kuyadhibiti.
• Tathmini hujenga uwazi mwingi juu ya kutokufanikiwa au kufanikiwa
kwa mradi na hivyo kuongeza kuaminiana na kujituma miongoni mwa
wadau.
• Tathmini husaidia kujenga hoja juu ya uhalali wa matumizi ya
rasilimali za mradi.
Umuhimu wa Tathmini
(Unaendelea)
 Hujenga uwezo
• Watendaji hujifunza namna na kuboresha
mbinu na utendaji
• Kupitia ushirikishwaji, wadau hujengewa ari
kubwa ya kushiriki katika mradi na miradi
mingine.
• Kupitia Tathmini, washiriki huongeza upeo wa
uchambuzi na uwezo wa kuhoji mambo.
 Huboresha mawasiliano kwa kiwango kikubwa
• Kama ikitekelezwa kwa ufanisi, Tathmini
huongeza mawasiliano miongoni mwa wadau.
Tathimini ya dharula
Tathimini ya dharula
Tathimini iliyopangwa
Inalenga
 kuthibiti matumizi ya rasirimali
 kuchambua mafanikio na kushindwa kwa baadhi ya
vipengele vya mradi (mfano sera)
 Kubaini kama mradi umefikia malengo yake
 Kubaini kama rasilimali za kutosha zinapatikana.
 Kubaini matumizi mazuri ya rasirimali
 Kubaini kama kuna vikwazo vyovyote vitokanavyo na
mpango wa utekelezaji wa mradi
Uhusiano kati ya ufuatiliaji na
Tathimini
 Vinahusiana na husaidiana na zote ni muhimu
 Zinawajibu na huwajibika kwa kutoa taarifa muhimu
ambayo huainisha kama:
• Kama mradi unafanikisha wahitaji na vipaumbele vya
wadau wa nje na ndani.
• Inaleta mabadiliko yanayotarajiwa
 Ufuatiliaji na tathimini makini huhitaji utafiti mzuri wa
awali na viashiria bora kwa ajili ya utekelezaji na matokeo
sahihi
 Ufuatiliaji na tathimini hauna manufaa kama mradi hauna
malengo yaliyoainishwa na viashiria ili kubaini mafanikio
au mapungufu
Viashiria
 Maana ya Viashiria
• Viashiria ni vigezo au vionyeshi,
vinavyopima kiasi ambacho malengo ya
mradi yamefikiwa. Viashiria huweka
viwango vinavyotumika kupima,
kutathmini, au kuonyesha maendeleo ya
mradi dhidi ya malengo yaliyowekwa. Kwa
mantiki hii, viashiria vinatokana na malengo
husika katika Ubao Mantiki.
Viashiria ( vinaendelea)
Viashiria vinapaswa kuwa na sifa zifuatazo:
 Kiwe Maalum (specific)
 Kinapimika(measurable)
 Kinafikika (achievable)
 Kinaendana(Realistic)
 Muda maalum (Time Specific)
Umuhimu wa Viashiria
Kwa ujumla, viashiria vina umhimu ufuatao:
 Vinasaidia kubaini maendeleo halisi yaliyofikiwa na
mradi. Hivyo viashiria ni vegezo vya kupima
mafanikio.
 Vinaweka msingi wa kufanya Ufuatiliaji na Tathmini
ya mradi. Kwa maneno mengine, Ufuatiliaji na
Tathmini haviwezi kufanyika sawasawa kama mradi
hauna viashiria.
Vipengele vinavyotakiwa kufuatiliwa
Kwa ujumla vipengele vya kufuatiliwa vinategemea na
aina ya mradi na mambo yaliyobainishwa kuwa ya
muhimu na wadau wa mradi.Hata hivyo, vifuatavyo in
baadhi ya vipengele ambavyo ni muhimu katika
Ufuatiliaji
Rasilimali:
 Rasilimali hujumisha pesa, vifaa, watu na ujuzi.
Matumizi ya rasilimali hizi katika utekelezaji wa
shughuli lazima yaangaliwe. Kunatakiwa kuwe na
mifumo mizuri ya kutawala matumizi ya
rasilimali hizi ili kuleta uwajibikaji.
• Ufuatiliaji mzuri huangalia uwiano wa rasilimali
na matokeo ya kazi zilizofanyika.  
• Maendeleo ya kazi (shughuli): Hii ni
muhimu kufuatilia, hasa ili walengwa wajue
kwa kiasi gani shughuli zilizopangwa
zimetekelezwa na matokeo gani yamepatikana.
• Muda: Kuna Uhusiano mkubwa baina ya muda
na matokeo ya kazi pamoja na kiasi cha pesa
iliyotumika.
Kazi ya vikundi
Aina za Viashiria
Viashiria vipo vya aina kuu mbili. Viashiria vya kupimika
(Quantitative). Hivi ni vile ambavyo vinapimika kirahisi.
Mfano, idadi ya wakulima waliofundishwa kutumia mboji.
Aina ya pili ni Viashiria vya ubora (qualitative). Viashiria
vya ubora havipimiki kirahisi. Mfano: utamu au rangi ya
maharage.
Hatua za kutengeneza viashiria
• Soma malengo ya mradi kwa uangalifu
• Bainisha na uainishe vitu vyote vinavyoweza kupimika
kutoka kwenye lengo husika
Hatua za kutengeneza viashiria(zinaendelea)
Pitia vitu vilivyo ainishwa hapo juu na kubaini vile
vinavyoweza kupimwa kwa gharama ndogo na muda
mfupi.
Tengeneza Viashiria kwa kutumia maswali yafuatayo:
 Kwa ajili ya nani?
 Kiasi gani; mara ngapi?
 Kwa uzuri gani (How well?)
 Ifikapo lini?
 Wapi?
Mwisho tengeneza sentensi itakayokuwa kiashiria
chako.
Taarifa za awali ni muhimu sana unapotengeneza
Viashiria!
Day 2
Utumiaji wa Bao Mantiki kama
nyenzo ya Ufuatiliaji na Tathimini
28
UTUMIAJI WA BAO MANTIKI
UFAFANUZI/MAELEZO YA MBAO MANTIKI
 Safu wima 1
Safu hii inawakilisha mbinu yetu inatufahamisha nini
tunatarajia kufanya na matarajio yetu tutakayofikia (huu ni
mkakati tuliodhamiria kutekeleza).
 Safu wima 2
Katika safu hii tunapima maendeleo ya lengo kuu. Hivyo
tunatakiwa kutambua vigezo mbali mbali vitakavyobaini
maendeleo ya kufikia lengo kuu. Vigezo hivi lazima viwe na
sifa zifuatazo; rahis,i vinafikika, vinafikiwa, kinapimika,
vinaamiminika, vinaendana na muda.
Panatakiwa stadi kuzichagua.

 Safu wima 3
Safu hii inatoa maelezo ni wapi patapatikana
taarifa/takwimu. Muhimu ikiwa taarifa za mradi,
kumbukumbu za ufauatiliaji ni vema zikiwapo
na ziwe rahisi kufikiwa.
 Safu wima 4
Safu hii inawakilisha dhanio ambazo hutakiwa
kuzingatiwa. Hujazwa kwa kuzingatia ngazi kutoka
chini wakati huo tukijaribu kubaini sababu
zilizo nje ya uwezo wetu zinazoweza kusababisha
kutotekelezwa kwa mradi.
Namna ya kukamilisha bao mantiki
 Maelezo ya mradi yanakamilishwa kwanza
halafu madhanio nayo yanashughulikiwa,
kisha viashiria na hatimaye namna ya
kuhakiki. Hata hivyo ukamilishaji wa jedwali
unawezekana ukawa tofauti kutokana na hali
halisi ilivyo na wanaohusika kujenga hilo
jedwali.
Kuanisha maelezo ya mradi (lengo kuu, lengo
mahsusi, matokeo na shughuli)
i.Kuchagua lengo kuu
 Mara nyingi matawi ya juu kabisa ya mti wa
malengo yatatoa picha nini liwe lengo kuu.
Kwa mchoro wa hapo chini yapo dhahiri
malengo makuu mawili
 Kuongeza kipato na
 Kuongeza lishe
 Hata hivyo kwa kuwa mkakati
tuliouchagua ni ule wa kilimo ambao
unalenga zaidi katika kuongeza kipato basi
lengo kuu litakuwa ni kuongeza kipato.
ii. Chagua utakaochangia katika lengo kuu
 Kuna njia mbalimbali za kuweza kuongeza kipato
kwa kuangalia mti wa malengo moja ya njia
inayoweza kutumika ni kuboresha masoko kwa
wakulima. Kwa hiyo Lengo mahususi litakuwa :
Masoko ya uhakika kwa wakulima yanapatikana3.
• iii. Orodhesha matokeo
 Watu wengi huwa wanashida ya kutofautisha
matokeo na lengo mahususi na wanapofikia hatua hii
wanapata shida sana kujua nini kinahitajika kwenye
matokeo (outputs)
Matokeo (Outputs) ni huduma au bidhaa
zitolewazo na mradi kwa lengo la kufikia lengo
mahsusi. Mfano
Taarifa za masoko zinapatikana kwa urahisi na
Wakulima wanalima kwa mkataba
Itasaidia sana kuwezesha masoko ya uhakika
kupatikana
 Unapozungumzia lengo mahususi yale matokeo ya awali
(immediate results) ambayo yatatokea kwa mkulima
mwenyewe kwa mfano apatapo taarifa za masoko.
Kwanza atapata elimu ambayo itasaidia kubadilisha
mtazamo wake kuhusu masoko.
iv. Orodhesha shughuli
Kila tokeo lililoainishwa ni muhimu
kuorodhesha shughuli gani zifanywe na
mradi ili kupata tokeo hilo.
 Mfano
o Tokeo :Taarifa za masoko zinapatikana kwa
urahisi
 Shughuli :
o Kutoa mafunzo
o Kuunda kamati ya masoko
o Kuandaa vipeperushi
v. Ainisha rasilimali zinazohitajika
kukamilisha shughuli
 Mfano
1.1 Kutoa mafunzo : Mkufunzi, ukumbi, watu,
kalamu, daftari, usafiri……
1.2Kuunda kamati : Usafiri, mtaalamu,
kalamu, daftari, watu……….
1.3Kuandaa vipeperushi :
Mtaalamu « printer », karatasi, usafiri………..
1.4Tayarisha bajeti ya mradi kwa kuainisha
nyenzo katika fedha.
Kutengeneza madhanio
 Dhanio (Assumption)
Hizi ni ali kuendana na shughuli na malengo ambazo lazima
ziwe zimetokea au kuwepo ili mradi ufanikiwe. Lakini hizi
haziwezi kudhibitiwa na mradi wenyewe:
 Hizi (assumptions) huonyesha kiasi cha vikwazo katika mazingira
(risks) vinavyokabili mradi.
 Ili kupunguza athari za vikwazo (risks) hivi, wakati mwingine
inatubidi kubadilisha baadhi ya shughuli na matokeo.
 Katika kila hatua ya jedwali la mpango wa mradi, angalia na kuona
kama shughuli zitaleta matokeo uliyokusudia au kama kuna kitu cha
ziada nje ya mradi (assumptions) kinahitajika kuwepo ili shughuli
zilete matokeo yaliyokusudiwa.
 Tunaweza kukamilisha jedwali letu kuhusiana na Dhanio
(assumptions) kwa kutumia maneno “kama” na “hivyo” na kuchora
mishale kuonyesha uhusiano.
Namna ya kutengeneza Viashiria
Viashiria vinahusu taarifa tunazohitaji kupima
maendeleo ya mradi kufikia malengo yake. Viashiria
huonyesha kiwango cha utekelezaji kinachotakiwa kufikiwa
ili kuweza kufanikisha malengo tuliyojiwekea kwenye
mradi. Viashiria huweka msingi wa kufanya ufuatiliaji na
tathmini.
Viashiria huonyesha dhahiri ni vithibitisho (evidence)
gani vitakavyokueleza kama lengo kuu, lengo mahususi au
matokeo yamefikiwa kwa jinsi ya
Uwingi (quantity) – kiasi gani?
Ubora (quality) – hali gani?
Muda upi?
Eneo gani la kijiografia?
 Kiashiria kizuri huwa na sifa zifuatazo:
 Kinajitegemea: kiashiria kinapaswa kuonekana mara moja tu katika
jedwali la mpango wa mradi (PPM). Kiashiria kimoja hakipaswi
kutumika zaidi ya level moja katika jedwali hili.
 Kiashiria budi kionyeshe mambo ya kweli yaliyopo (facts) na siyo
vitu vya kufikirika (kuhisi)
 Badiliko linalorekodiwa litokane na shughuli za mradi wako na si
vinginevyo
 Andika viashiria ambavyo ni rahisi kupata taarifa na kwa bei nafuu.
Ikiwa bei ya kupata taarifa za viashiria ni ghali, itapelekea ufuatiliaji
na tathmini kuwa ngumu na ghali pia.
 Data za viashiria ziwe SMART ili hata wale walio nje wenye mashaka
na mradi wako waweze kupima na kuona kwamba mabadiliko
yaliyotokea ni ya kweli.
Aina za Viashiria
Viashiria ambavyo ni sehemu ya lengo (direct
indicators). Kiashiria na lengo vinahusiana moja kwa
moja.
Viashiria na lengo havihusiani moja kwa moja lakini
bado viashiria hivyo havionyeshi ni kazi gani
tumefanikiwa kufikia malengo yetu (indirect
indicators)
 Mfano
Jinsi ya Kuandaa / Kutengeneza Viashiria
 Soma lengo kwa makini upate kuelewa kwa ufasaha
sana
 Ainisha na kuorodhesha mambo (parameter) yote
katika lengo ambayo yanaweza kupimwa.
 Chagua mambo machache yanayoweza kupimika
kiuchuni kwa maana ya muda na fedha
 Tengeneza kiashiria kwa kuzingatia yafuatayo:
• Walengwa-Kwa ajili ya nani?
• Kiasi gani, mara ngapi?
• Ubora wa kiasi gani ?
• Muda -Kufikia muda gani kutaleta mabadiliko ?
• Eneo (Wapi) ?
Utafiti wa awali
UTAFITI WA AWALI
(baseline survey)
 Taarifa za Awali huelezea hali halisi kwa wakati huu.
Ili kupata taarifa za awali, ni budi kufanya Utafiti wa
Awali, ambao hukusanya taarifa zinazosaidia kupima
maendeleo ya utekezaji wa shughuli.
 Lengo kuu la utafiti wa awali ni kupata hali halisi
ilivyo ili hapo baadaye tuweze kupima maendeleo
yaliyofikiwa kutokana na utekelezaji wa mradi.
 Utafiti wa awali unapaswa kufanywa kabla ya kuandaa
mradi. Hii ni kwa sababu taarifa hii husaidia katika
kuandaa Viashiria
Utafiti wa awali (inaendelea)
Namna ya Kufanya utafiti wa awali:
 Hatua tano zifuatazo ni muhimu katika kufanya
utafiti wa awali
• Amua ni taarifa zipi zinahitajika
• Andaa njia za kukusanya taarifa mf. Dodoso
• Hakiki dodoso (pre-test)
• Fanya ziara za kukusanya taarifa
• Fanya uchambuzi wa taarifa
• Andika matokeo ya utafiti
46
Mwisho….
THANK YOU
========================
CELEBRATING PROJECT
ACHIEVEMENTS
KAZI ZA VIKUNDI
Rejea bao mantiki fanya maboresho kama
tulivyoelekezana
Uandaaji wa mpango wa ufuatiliaji
Utayarishaji wa mpango wa Ufuatiliaji
Hatua za utayalishaji mpango wa Ufuatiliaji
 Elewa na kuchambua lengo kuu, malengo mengine na
shughuli ukizingatia viashiria na shabaha (targets), na
njia za kuthibitisha.
 Ainisha nini cha kufanyia Ufuatiliaji.
 Amua namna gani Ufuatiaji utafanyika; Njia za
kuthibitisha au Vyanzo vya taarifa.
 Amua namna gani taarifa zitakua zinakusanywa (Njia
za kuthibitisha (Means of verification) zinaweza
kusaidia).
 Kusanya taarifa
Kutayarisha mpango wa Ufuatiliaji (inaendelea)
 Chambua hali ya taarifa kwa kuhesabu, kupima, au
kulinganisha takwimu mbalimbali.
 Weka katika kumbukumbu taarifa/data
zilizokusanywa na kuchambuliwa.
 Linganisha na shabaha (target) iliyokuwa imewekwa
au kiashiria.
 Andika na kupeleka ripoti kwa wadau husika ili
waweze kuchukua hatua.
Mfano wa mpango wa UfuatiliajiLengo au
shughuli
Kiashiria au
shabaha
(target)
Chanzo cha
taarifa/data
Taarifa/data
ikusanywe
kila baada ya
muda gani?
Gharama Mhusika Nani
atatumia
taarifa?
Atatumia
taarifa kwa
ajili ya nini?
Dhanio
Mpango wa Ufuatiliaji ni budi uweze kujibu
maswali yafuatayo:
 Nini cha kufuatilia?
 Namna gani ya kufuatilia?
 Nani afuatilie?
 Lini Ufuatiliaji ufanyike?
 Rasilimali zipi zinahitajika?
 Nani atatumia taarifa hizo na kwa namna gani?
Mchakato wa Tathimini
2. NINI CHA KUFANYIA
TATHMINI?
Mchakato wa Tathmini
 Tathmini huangalia vipengele muhimu
vifuatavyo:
• Maendeleo ya utekelezaji ukilinganisha na ‘vigezo vya
kusudio’ (targets) vilivyopangwa.
• Fedha zilivyopatkana na vile zilivyotumika.
• Ushiriki wa wadau mbalimbali (collaborators)
• Muda uliotumika katika kutekeleza mradi na ufanisi
katika matumizi ya rasilimali katika kutekeleza mradi.
Mchakato wa Tathmini (inaendelea)
Namna malengo yaliyowekwa wakati wa kuandaa
mradi yalivyo na mafanikio yanayotarajiwa.
Mabadiliko ya maisha ya walengwa na jamii kwa
ujumla (mabadiliko ya kijamii na kiuchumi).
Jamii kupata mtazamo mpya/ujuzi/utendaji mpya.
AINA ZA TATHMINI
Aina za Tathmini
 Tathmini ya nje (External evaluation):
• Aina hii ya Tathmini mara nyingi hufanywa na watu kutoka nje
ya shirika linalotekeleza mradi (External evaluators).
• Tathmini hii hufanyika katikati ya kipindi kizima cha
utekelezaji wa mradi, mwisho wa mradi au baada ya mradi
kukamilika.
• Kwa ruzuku ndogo na zile za kati yamkini Tathmini ya mwisho
wa mradi na baada ya mradi kukamilika hufaa zaidi.
 Tathmini ya ndani ([internal]Self-evaluation):
• Hii hufanywa na watekeleza mradi ndani ya shirika na shirika
ndilo linaamua lifanye katika kipindi gani cha utekelezaji wa
mradi.
Aina zote za Tathmini zinaweza kufanywa kawaida au
uchambuzi wake ukawa wa kina sana.
FIKIRI KWA UNDANI
Day 4
Ukusanyaji na utumiaji wa
taarifa/takwimu
62
Ukusanyaji wa taarifa/takwimu
 Ukusanyaji wa taarifa/takwimu unahusika na
uchaguzi wa njia za kufanya uchunguzi.
 Hakuna njia moja bora ya ukusanyaji taarifa:
• Uchaguzi wa njia ya kukusanya taarifa unategemea
aina ya taarifa inayo hitajika.
• Uchaguzi unategemea pia kitu gani kinawezekana
kulingana na muda na rasilimali nyingine zinazo
hitajika. Njia mbalimbali zinapendekezwa.
• Ukusanyaji wa Taarifa/Takwimu kwa ajili ya
Ufuatiliaji na Tathmini huanzia siku ya kwanza
unapoanza utekelezaji wa mradi.
Ukusanyaji wa taarifa/takwimu (inaendelea)
• Ukusanyaji wa taarifa/takwimu unahitaji kujituma
sana.
• Katika mtazamo wa Ufuatiliaji na Tathmini,
tunakusanya taarifa/takwimu ili kuthibitisha
viashiria tulivyoweka katika ngazi mbalimbali za
ubao mantiki. Kwa hiyo kila siku taarifa/takwimu
budi zihifadhiwe katika madaftari, mafaili au
komputa na kutolewa pindi zinapo hitajika.
JE TAARIFA ZOTE NI MUHIMU
Ukusanyaji wa taarifa/takwimu (inaendelea)
• Wakati wote viashiria hutoa mwelekeo wa njia ipi itumike
katika ukusanyaji wa taarifa. Na hii huonyeshwa
katika ‘Njia ya kuthibitisha’ ( Means of Verification).
• Ni muhimu sana wakati wa kutengeneza viashiria kubaini
njia za kukusanya taarifa/takwimu ambazo ni rahisi kwa
maana ya fedha na muda.
• Epuka kukusanya taarifa nyingi sana au kidogo sana
ambazo hazitaweza kufanyiwa uchambuzi au kutumika.
• Kumbuka:
• 55% ya taarifa katika jamii Ni nzuri kuzifahamu (Nice to
Know)
Ukusanyaji wa taarifa/takwimu (inaendelea)
• 35% ya taarifa katika jamii ni vizuri kuzifahamu
(Useful to know)
• 10% tu ya taarifa katika jamii ni lazima kujifahamu
(Must Know )
 Kwa maana nyingine ni kwamba kuna
taarifa/takwimu nyingi sana katika jamii. Inabidi
kutoa kipaumbele kukusanya zile taarifa tu
ambazo lazima uzifahamu. Muda ukitosha
unaweza kukusanya taarifa nyingine.
Uchambuzi wa taarifa/takwimu na kuzitafsiri
 Uchambuzi wa taarifa/takwimu na kutafsiri
(interpretation) ni kitendo cha kubadili
taarifa/takwimu na kuzigeuza ziwe sentensi zenye
kutoa ujumbe wenye maana. Hii inaweza kufanyika
wakati wote au kwa vipindi maalum.
 Uchambuzi wa taarifa/takwimu unaweza kufanyika
kwa namna tofauti tofauti kutegemeana na kama
taarifa/data ziko katika ubora (qualitative) au katika
vipimo (quantitative).
 Unapozipa taarifa/takwimu maana unakua
unaoanisha viashiria na matokeo na mpango wa kazi.
VIPENGELE VYA UCHAMBUZI WA MABADILIKO YATOKANAYO NA MRADI
VIPENGELE VYA UCHAMBUZI WA MABADILIKO YATOKANAYO NA
MRADI
(Impact assessment)
Vipengele muhimu vya uchambuzi wa mabadiliko
 Lengo la Uchambuzi wa Mabadiliko
 Hatua ya kuzingatia wakati wa uchambuzi
 Mbinu/Njia ya kufanya uchambuzi
 Hadithi rejea za kufanya tathimini
Vipengele vya uchambuzi wa mabadiliko (inaendelea)
Lengo la Uchambuzi wa Mabadiliko
 Huu ni mchakato wa utambuzi wa mabadiliko
ambayo yamekadiliwa ili kuboresha hali ya
walengwa, kijamii, mazingira na uchumi).
Uchambuzi huo huzingatia:
• Hali ilivyokuwa kabla ya mradi kuanzishwa
• Jinsi shughuli za mradi zilivyotekelezwa
• Taratibu za uchambuzi zilivyoainishwa
• Uchambuzi kuwa shirikishi
Hatua ya kuzingatia
 Ufuatiliaji na tathmini ya ndani ya asasi huwa ni kwa ajili
mafunzo endelezu ya watendaji na wadau wa mradi,
(mfano tathimini ya viashiria vya mfumo wa utoaji na
upatikanaji wa taarifa)
 Tathmini inayofanywa na watu wa nje ya mradi ripoti yake
huwa kwa ajili ya madhumuni maalumu
Mifano ya uchambuzi wa mabadiliko ya walengwa
husika:
 Mabadiliko ya hali ya umasikini
 Mabadiliko ya taratibu
 Mabadiliko hali ya Kijamii
 Mabadiliko ya hali ya afya
 Mabadiliko ya Mazingira
Uchambuzi wa kubaadiliko kwa ujumla hufanyika
kwa kujumuisha maswali ya kijamii, kiuchumi na
kimazingira. Uchambuzi huo hulenga kuleta.
 Uwajibikaji
 Kuwepo na ushahidi wa mafanikio ya shughuli na
kuzingatia garama halisi
 Kuboresha hali ya walengwa
 Kutoa mwongozo wa ambavyo sera za serikali na
wafadhili zinavyotakiwa zitekelezwe ili zikubalike na
kufanikisha kuleta maendeleo.
NGAZI ZA UCHAMBUZI
TUNAANZA KUTUA
Ngazi za uchambuzi
 Ngazi ya juu (mfano serikali)
Mara nyingi Serikalini na ngazi ya kiutawala za Asasi
hujishughulisha zaidi na masuala ya sera.
 Ngazi za Kati ( mfano uongozi wa Asasi)
Huchambua Sera, sheria na miongozo na kufanya
marekebisho kuwezesha mafanikio
 Ngazi ya chini (hii ni ngazi ambayo mradi
hutekelezwa, mnahusika nayo)
• Huzingatia vipengele vifuatavyo
• Jinsi mradi / Program ilivyoandaliwa.
Ngazi ya chini (inaendelea)
• Je bao mantiki lilitayarishwa
• Je nyaraka za mradi husika zipo
• Je viashiria na vyanzo vyake vya uhakiki
vimeainishwa
• Je utaratibu wa utekelezaji wa shughuli za mradi
ulivyo umezingatiwa.
• Hali ya matumizi na mapato (rasilimali) ilivyo.
• Jinsi uongozi wa mradi/ programu ulivyo
• Taratibu zilizowekwa za ufuatiliaji utekelezaji wa
mradi ulivyo
Njia/ jinsi ya kufanya uchambuzi wa mabadiliko ya mradi
 Ubora/ Ustahilifu (qualitative)
 Kwa kupima mabadiliko muhimu (quantitative)
 Shirikishi (Participatory)
Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kufanya uchambuzi wa
mabadiliko
 Uwazi wa taratibu ya uchambuzi.
 Ushiriki wa wadau katika uchambuzi wa mabadiliko
 Uhakika wa vyanzo vya taarifa/ Takwimu
 Nia ya kutumia repoti kuboresha; sera, taratibu na
miongozo ya utendaji wa Asasi
 Uzoefu wa asasi husika na garama zinazohusu
uchambuzi wa mabadiliko.
Hadidu za rejea za kufanya tathimini (ToR)
Huonyesha kwa uwazi nini timu ya uchambuzi inatakiwa
ifanye
Huzingatia masuala yafuatayo:
 Hubainisha shughuli za kufanyika
 Matokeo tarajiwa
 Mbinu za uchambuzi wa mabadiliko
 hueleza historia ya mradi husika kwa ufupi
 Huainisha vyanzo vya taarifa za utekelezaji wa
mradi husika
 Huanisha madhumuni ya uchambuzi, walengwa na
matumizi ya ripoti ya uchambuzi
 Inafafanua timu ya watakaofanya uchambuzi na
ushiriki wa wadau wengine
AHSANTENI NA NINAWATAKIA SAFARI
NJEMA
79
UANDIKAJI WA REPOTI
Uandikaji wa Ripoti
• Ripoti huandikwa ili kupelekwa kwa mamlaka
uongozi au ile ipelekwayo kwa walengwa.
• Ripoti huandaliwa tangu mradi unapoanza
kutekelezwa. Chochote kinachotekelezwa na mradi,
lazima ripoti ya maandishi iandaliwe. Hizi ripoti za
utekelezaji baadaye hukusanywa pamoja ili kupata
ripoti za mwezi, robo mwaka au mwaka na hujadiliwa
na walengwa /mamlaka husika.
Uandikaji wa Ripoti (inaendelea)
 Ripoti za utekelezaji wa miradi budi zieleze vipengele
vifuatavyo:
1. Shughuli zilizo pangwa.
2.Shughuli zilizoweza kutekelezwa (kama kuna tofauti,
kwa nini?).
3. Njia iliyotumika katika utekelezaji
4.Changamoto zilizojitokeza
5.Mafunzo gani yamepatikana kutokana na utekelezaji
wa mradi
6.Mna mapendekezo gani.
Usambazaji wa Ripoti
Kukabithi rasimu
Kila mshiriki kukabithi rasimu ya bao Mantiki na
mpango wa ufuatiliaji wa mradi husika wa Asasi yake.

More Related Content

What's hot

Nothing less than God's best Lifeclass wek 8
Nothing less than God's best Lifeclass wek 8Nothing less than God's best Lifeclass wek 8
Nothing less than God's best Lifeclass wek 8Maria Teresa Gimeno
 
Ang dungog sa pagpaubos ug ang kadaotan
Ang dungog sa pagpaubos ug ang kadaotanAng dungog sa pagpaubos ug ang kadaotan
Ang dungog sa pagpaubos ug ang kadaotanrrg_19882012
 
“The Power of God’s Grace”
“The Power of God’s Grace”“The Power of God’s Grace”
“The Power of God’s Grace”Don McClain
 
How to live in each season of life ecclesiastes 3 1 11
How to live in each season of life ecclesiastes 3 1 11How to live in each season of life ecclesiastes 3 1 11
How to live in each season of life ecclesiastes 3 1 11Grace4Families Inc.
 
The Power of the Holy Spirit
The Power of the Holy SpiritThe Power of the Holy Spirit
The Power of the Holy SpiritKaren Gutierrez
 
How to cultivate the excellent spirit
How to cultivate the excellent spiritHow to cultivate the excellent spirit
How to cultivate the excellent spiritOKE OLUSEGUN
 
Uchumi wa kibiblia
Uchumi wa kibibliaUchumi wa kibiblia
Uchumi wa kibiblia001111111111
 
A new beginning lifeclass week 9
A new beginning lifeclass week 9A new beginning lifeclass week 9
A new beginning lifeclass week 9Maria Teresa Gimeno
 
An Introduction to Catholic Leadership
An Introduction to Catholic LeadershipAn Introduction to Catholic Leadership
An Introduction to Catholic LeadershipPaul Kierney
 

What's hot (14)

Nothing less than God's best Lifeclass wek 8
Nothing less than God's best Lifeclass wek 8Nothing less than God's best Lifeclass wek 8
Nothing less than God's best Lifeclass wek 8
 
Ang dungog sa pagpaubos ug ang kadaotan
Ang dungog sa pagpaubos ug ang kadaotanAng dungog sa pagpaubos ug ang kadaotan
Ang dungog sa pagpaubos ug ang kadaotan
 
“The Power of God’s Grace”
“The Power of God’s Grace”“The Power of God’s Grace”
“The Power of God’s Grace”
 
How to live in each season of life ecclesiastes 3 1 11
How to live in each season of life ecclesiastes 3 1 11How to live in each season of life ecclesiastes 3 1 11
How to live in each season of life ecclesiastes 3 1 11
 
Prosperity
ProsperityProsperity
Prosperity
 
The Power of the Holy Spirit
The Power of the Holy SpiritThe Power of the Holy Spirit
The Power of the Holy Spirit
 
How to cultivate the excellent spirit
How to cultivate the excellent spiritHow to cultivate the excellent spirit
How to cultivate the excellent spirit
 
Uchumi wa kibiblia
Uchumi wa kibibliaUchumi wa kibiblia
Uchumi wa kibiblia
 
Scetion 27
Scetion 27Scetion 27
Scetion 27
 
A new beginning lifeclass week 9
A new beginning lifeclass week 9A new beginning lifeclass week 9
A new beginning lifeclass week 9
 
Parable of the talents ツ
Parable of the talents ツParable of the talents ツ
Parable of the talents ツ
 
The Power of Forgiveness
The Power of ForgivenessThe Power of Forgiveness
The Power of Forgiveness
 
Grow a godly lifestyle
Grow a godly lifestyleGrow a godly lifestyle
Grow a godly lifestyle
 
An Introduction to Catholic Leadership
An Introduction to Catholic LeadershipAn Introduction to Catholic Leadership
An Introduction to Catholic Leadership
 

Viewers also liked

Segment 001 of Segment 002 of IELR15_5_187-224
Segment 001 of Segment 002 of IELR15_5_187-224Segment 001 of Segment 002 of IELR15_5_187-224
Segment 001 of Segment 002 of IELR15_5_187-224Michael Davar
 
Kelompok 1 sel
Kelompok 1 selKelompok 1 sel
Kelompok 1 selAde Misbah
 
M|SOURCE WORK ORDER SYSTEM
M|SOURCE WORK ORDER SYSTEMM|SOURCE WORK ORDER SYSTEM
M|SOURCE WORK ORDER SYSTEMScott Urich
 
Principles and ambitions for cultural mobility
Principles and ambitions for cultural mobilityPrinciples and ambitions for cultural mobility
Principles and ambitions for cultural mobilityRhys Williams
 
Balo153 quan-3-le-van-sy-ruth-balo-nu-yellow
Balo153 quan-3-le-van-sy-ruth-balo-nu-yellowBalo153 quan-3-le-van-sy-ruth-balo-nu-yellow
Balo153 quan-3-le-van-sy-ruth-balo-nu-yellowbalo153
 
July 2015 - Market Snapshot - San Benito County
July 2015 - Market Snapshot - San Benito CountyJuly 2015 - Market Snapshot - San Benito County
July 2015 - Market Snapshot - San Benito CountyMLSListings Inc
 
An ACNET Application Program to Measure the Energy Spread in the Booster at i...
An ACNET Application Program to Measure the Energy Spread in the Booster at i...An ACNET Application Program to Measure the Energy Spread in the Booster at i...
An ACNET Application Program to Measure the Energy Spread in the Booster at i...Jovan Nelson
 
Wearables and the science of human behavior change - part 1 (january 2014)
Wearables and the science of human behavior change - part 1 (january 2014)Wearables and the science of human behavior change - part 1 (january 2014)
Wearables and the science of human behavior change - part 1 (january 2014)Endeavour Partners
 
The Bottom Line on Homeowner Associations
The Bottom Line on Homeowner AssociationsThe Bottom Line on Homeowner Associations
The Bottom Line on Homeowner AssociationsMichael Brown
 

Viewers also liked (13)

Segment 001 of Segment 002 of IELR15_5_187-224
Segment 001 of Segment 002 of IELR15_5_187-224Segment 001 of Segment 002 of IELR15_5_187-224
Segment 001 of Segment 002 of IELR15_5_187-224
 
Kelompok 1 sel
Kelompok 1 selKelompok 1 sel
Kelompok 1 sel
 
RING-USAID
RING-USAIDRING-USAID
RING-USAID
 
M|SOURCE WORK ORDER SYSTEM
M|SOURCE WORK ORDER SYSTEMM|SOURCE WORK ORDER SYSTEM
M|SOURCE WORK ORDER SYSTEM
 
corazon tan blanco
corazon tan blancocorazon tan blanco
corazon tan blanco
 
Principles and ambitions for cultural mobility
Principles and ambitions for cultural mobilityPrinciples and ambitions for cultural mobility
Principles and ambitions for cultural mobility
 
Balo153 quan-3-le-van-sy-ruth-balo-nu-yellow
Balo153 quan-3-le-van-sy-ruth-balo-nu-yellowBalo153 quan-3-le-van-sy-ruth-balo-nu-yellow
Balo153 quan-3-le-van-sy-ruth-balo-nu-yellow
 
July 2015 - Market Snapshot - San Benito County
July 2015 - Market Snapshot - San Benito CountyJuly 2015 - Market Snapshot - San Benito County
July 2015 - Market Snapshot - San Benito County
 
2015 Resume
2015 Resume2015 Resume
2015 Resume
 
An ACNET Application Program to Measure the Energy Spread in the Booster at i...
An ACNET Application Program to Measure the Energy Spread in the Booster at i...An ACNET Application Program to Measure the Energy Spread in the Booster at i...
An ACNET Application Program to Measure the Energy Spread in the Booster at i...
 
Wearables and the science of human behavior change - part 1 (january 2014)
Wearables and the science of human behavior change - part 1 (january 2014)Wearables and the science of human behavior change - part 1 (january 2014)
Wearables and the science of human behavior change - part 1 (january 2014)
 
The Bottom Line on Homeowner Associations
The Bottom Line on Homeowner AssociationsThe Bottom Line on Homeowner Associations
The Bottom Line on Homeowner Associations
 
Sudhanshu_CV
Sudhanshu_CVSudhanshu_CV
Sudhanshu_CV
 

Similar to M & E 2013 LEO 18july

Ce partners meeting Nrb Enos_Swahili version
Ce partners meeting Nrb Enos_Swahili versionCe partners meeting Nrb Enos_Swahili version
Ce partners meeting Nrb Enos_Swahili versionEnos Omondi
 
Mpango mkakati presentation
Mpango mkakati presentationMpango mkakati presentation
Mpango mkakati presentationwilliam mwaisumo
 
MKAKATI WA KUJENGA MSINGI WA HUDUMA YA YKM
MKAKATI WA KUJENGA  MSINGI  WA HUDUMA YA YKMMKAKATI WA KUJENGA  MSINGI  WA HUDUMA YA YKM
MKAKATI WA KUJENGA MSINGI WA HUDUMA YA YKMyouthkingdomministries
 
Mpango_wa_biashara_inayoanza.ppt
Mpango_wa_biashara_inayoanza.pptMpango_wa_biashara_inayoanza.ppt
Mpango_wa_biashara_inayoanza.pptWaltonJrSmithTZ
 

Similar to M & E 2013 LEO 18july (6)

Ce partners meeting Nrb Enos_Swahili version
Ce partners meeting Nrb Enos_Swahili versionCe partners meeting Nrb Enos_Swahili version
Ce partners meeting Nrb Enos_Swahili version
 
MPANGO MKAKATI
MPANGO MKAKATIMPANGO MKAKATI
MPANGO MKAKATI
 
Mpango mkakati presentation
Mpango mkakati presentationMpango mkakati presentation
Mpango mkakati presentation
 
MKAKATI WA KUJENGA MSINGI WA HUDUMA YA YKM
MKAKATI WA KUJENGA  MSINGI  WA HUDUMA YA YKMMKAKATI WA KUJENGA  MSINGI  WA HUDUMA YA YKM
MKAKATI WA KUJENGA MSINGI WA HUDUMA YA YKM
 
UTAFITI WA KIELIMU
UTAFITI  WA KIELIMUUTAFITI  WA KIELIMU
UTAFITI WA KIELIMU
 
Mpango_wa_biashara_inayoanza.ppt
Mpango_wa_biashara_inayoanza.pptMpango_wa_biashara_inayoanza.ppt
Mpango_wa_biashara_inayoanza.ppt
 

M & E 2013 LEO 18july

  • 1. THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY LTD KARIBUNI KWENYE MAFUNZO YANAYOHUSU UFUATILIAJI NA TATHIMINI NA UANDIKAJI WA RIPOTI
  • 2. MUDA WA MASOMO TAREHE: J uly 15 – 19, 2013 Wawezeshaji: Adam Makarang Ibrahim Ugullumu Phares Maugo
  • 3. 08/15/15 3 Mambo muhimu  Kujitambulisha ◦ Jina ◦ Taasisi unayotoka ◦ Nafasi yako katika taasisi tajwa ◦ Nk  Kukubaliana juu ya kanuni za warsha  Kuchagua M/kiti, katibu na mtunza muda  Mafunzo kuanza
  • 5. Lengo la mafunzo 1.Kuwawezesha washiriki wa washa kutambua na kutofautisha kati ya Mradi na shughuli za mradi. 2.Kuwawezesha washiriki wa washa kuelewa maana ya ufuatiliaji na tathimini na tofauti zake. 3.kutumia Bao Mantiki kama nyenzo ya kubuni na kuendeshaji mradi na njisi inavyotumika wakati wa ufuatiliaji na tathimini.
  • 6. 4. Kujengea washiriki umuhimu faida ya kufanya ufuatiliaji na tathimini kwa manufaa ya kufikia matokeo yaliyoktarajiwa. 5. Kuwawezesha washiriki kuandaa nyesho rahisi ya mfumo wa ufuatiliaji na tathimini ambayo inaweza kutumiwa na asasi zao. 6. Kuwajengea washiriki uelewa na ujuzi wa jinsi ya kupata taarifa na takwimu kwa ajili ya mfumo wa ufuatiliaji na tathimini ya asasi zao
  • 7. 7.Kuwawezesha kufanya makisiyo ya matokeo. 8. Kuwajengea msingi wa ujuzi kuhusiana na mfumo wa ufuatiliaji na tathimini katika kukusanya, kutoa na kusambaza taarifa. 9. Kutambua viashira/Vigezo na namna ya kuvitumia na kuvifuatilia. 10. Kupima Matokeo na mabadiliko yatokanayo na utekelezaji wa mradi husika katika Asasi zenu
  • 8. MADA ZA MAFUNZO YA UFUATILIAJI NA TATHIMINI 1. Maana ya maneno muhimu katika mafunzo ya ufuatiliaji na tathimini. 2. Bao Mantiki kama nyenzo ya ufuatiliaji na tathimini. 3. Uandaaji na matumizi ya mpango wa ufuatiliaji na tathimini 4. Ukusanyaji, utunzaji wa taarifa 5. Uandaaji na usambazaji wa taarifa(Utoaji wa Ripoti)
  • 9. UFUATILIAJI NA TATHIMINI  MAANA YA UFUATILIAJI:  Ufuatiliaji ni mchakato wa kuhakiki au kuthibitisha kama mpango wa utekelezaji wa shughuli za mradi unaendelea kama ulivyopangwa  Ufuatiliaji hutoa taswira juu ya namna gani mradi unavyo simamiwa. Hii ni shughuli ambayo hufanyika muda wote wa mradi, yaani kila siku, kila wiki na kila mwezi. Kiutendaji, ufuatiliaji unajikita katika kukusanya taarifa zinazoonyesha kama rasilimali zimekusanywa, shughuli zimefanyika na kama matokeo ya awali yamepatikana kama ilivyopangwa.
  • 10. Umuhimu wa Ufuatiliaji Kwa ujumla, Ufuatiliaji husaidia:  Kubaini mapungufu kwa wakati muafaka ili kutoa ufumbuzi kabla mapungufu hayo hayajawa makubwa.  Kufahamu jinsi rasilimali zinavyotumika.  Kujua wa kiwango gani shughuli zimetekelezwa.  Kutoa taarifa mahususi kwa wakati muafaka ili kufanya maamuzi yanayowezesha kusimamia vizuri rasilimali na hivyo kuweza kupata matokeo mazuri kwa gharama nafuu.
  • 11. Umuhimu wa Ufuatiliaji ( inaendelea) Ufuatiliaji mzuri huwezesha kuwepo mchanganyiko mzuri wa rasilimali ili kutekeleza shughuli tarajiwa na kuhakikisha walengwa wanatumia matokeo ili kuboresha hali zao
  • 12. Tathmini  Maana ya Tathmini  Ni mchakato wa kukusanya taarifa/takwimu na kuzichambua ili kupima kama lengo mahususi limefanikiwa ili kupima mabadiliko (impact) ambayo mradi umechangia katika maisha ya walengwa kutokana na mradi. Tathmini pia huchambua kufaa (relevance) kwa mradi na muundo wake.
  • 13. Umuhimu wa Tathmini Kwa ujumla, Tathmini:  Huboresha ufanisi (performance): • Kama tathmini ikifanyika kwa nia njema na kwa msukumo wa ndani (siyo wa wafadhili tu), taarifa na mapendekezo ya Tathmini husaidia kuboresha mradi mzima. • Ujuzi toka mradi uliokamilika unaweza kutumika kuboresha na kusaidia uundaji wa mradi unaofuata.  Huongeza uwajibikaji • Taarifa za mradi zinazotolewa mara kwa mara kwa wadau husaidia kubaini mapungufu na kuyadhibiti. • Tathmini hujenga uwazi mwingi juu ya kutokufanikiwa au kufanikiwa kwa mradi na hivyo kuongeza kuaminiana na kujituma miongoni mwa wadau. • Tathmini husaidia kujenga hoja juu ya uhalali wa matumizi ya rasilimali za mradi.
  • 14. Umuhimu wa Tathmini (Unaendelea)  Hujenga uwezo • Watendaji hujifunza namna na kuboresha mbinu na utendaji • Kupitia ushirikishwaji, wadau hujengewa ari kubwa ya kushiriki katika mradi na miradi mingine. • Kupitia Tathmini, washiriki huongeza upeo wa uchambuzi na uwezo wa kuhoji mambo.  Huboresha mawasiliano kwa kiwango kikubwa • Kama ikitekelezwa kwa ufanisi, Tathmini huongeza mawasiliano miongoni mwa wadau.
  • 16. Tathimini iliyopangwa Inalenga  kuthibiti matumizi ya rasirimali  kuchambua mafanikio na kushindwa kwa baadhi ya vipengele vya mradi (mfano sera)  Kubaini kama mradi umefikia malengo yake  Kubaini kama rasilimali za kutosha zinapatikana.  Kubaini matumizi mazuri ya rasirimali  Kubaini kama kuna vikwazo vyovyote vitokanavyo na mpango wa utekelezaji wa mradi
  • 17. Uhusiano kati ya ufuatiliaji na Tathimini  Vinahusiana na husaidiana na zote ni muhimu  Zinawajibu na huwajibika kwa kutoa taarifa muhimu ambayo huainisha kama: • Kama mradi unafanikisha wahitaji na vipaumbele vya wadau wa nje na ndani. • Inaleta mabadiliko yanayotarajiwa  Ufuatiliaji na tathimini makini huhitaji utafiti mzuri wa awali na viashiria bora kwa ajili ya utekelezaji na matokeo sahihi  Ufuatiliaji na tathimini hauna manufaa kama mradi hauna malengo yaliyoainishwa na viashiria ili kubaini mafanikio au mapungufu
  • 18. Viashiria  Maana ya Viashiria • Viashiria ni vigezo au vionyeshi, vinavyopima kiasi ambacho malengo ya mradi yamefikiwa. Viashiria huweka viwango vinavyotumika kupima, kutathmini, au kuonyesha maendeleo ya mradi dhidi ya malengo yaliyowekwa. Kwa mantiki hii, viashiria vinatokana na malengo husika katika Ubao Mantiki.
  • 19. Viashiria ( vinaendelea) Viashiria vinapaswa kuwa na sifa zifuatazo:  Kiwe Maalum (specific)  Kinapimika(measurable)  Kinafikika (achievable)  Kinaendana(Realistic)  Muda maalum (Time Specific)
  • 20. Umuhimu wa Viashiria Kwa ujumla, viashiria vina umhimu ufuatao:  Vinasaidia kubaini maendeleo halisi yaliyofikiwa na mradi. Hivyo viashiria ni vegezo vya kupima mafanikio.  Vinaweka msingi wa kufanya Ufuatiliaji na Tathmini ya mradi. Kwa maneno mengine, Ufuatiliaji na Tathmini haviwezi kufanyika sawasawa kama mradi hauna viashiria.
  • 21. Vipengele vinavyotakiwa kufuatiliwa Kwa ujumla vipengele vya kufuatiliwa vinategemea na aina ya mradi na mambo yaliyobainishwa kuwa ya muhimu na wadau wa mradi.Hata hivyo, vifuatavyo in baadhi ya vipengele ambavyo ni muhimu katika Ufuatiliaji Rasilimali:  Rasilimali hujumisha pesa, vifaa, watu na ujuzi. Matumizi ya rasilimali hizi katika utekelezaji wa shughuli lazima yaangaliwe. Kunatakiwa kuwe na mifumo mizuri ya kutawala matumizi ya rasilimali hizi ili kuleta uwajibikaji.
  • 22. • Ufuatiliaji mzuri huangalia uwiano wa rasilimali na matokeo ya kazi zilizofanyika.   • Maendeleo ya kazi (shughuli): Hii ni muhimu kufuatilia, hasa ili walengwa wajue kwa kiasi gani shughuli zilizopangwa zimetekelezwa na matokeo gani yamepatikana. • Muda: Kuna Uhusiano mkubwa baina ya muda na matokeo ya kazi pamoja na kiasi cha pesa iliyotumika.
  • 24. Aina za Viashiria Viashiria vipo vya aina kuu mbili. Viashiria vya kupimika (Quantitative). Hivi ni vile ambavyo vinapimika kirahisi. Mfano, idadi ya wakulima waliofundishwa kutumia mboji. Aina ya pili ni Viashiria vya ubora (qualitative). Viashiria vya ubora havipimiki kirahisi. Mfano: utamu au rangi ya maharage. Hatua za kutengeneza viashiria • Soma malengo ya mradi kwa uangalifu • Bainisha na uainishe vitu vyote vinavyoweza kupimika kutoka kwenye lengo husika
  • 25. Hatua za kutengeneza viashiria(zinaendelea) Pitia vitu vilivyo ainishwa hapo juu na kubaini vile vinavyoweza kupimwa kwa gharama ndogo na muda mfupi. Tengeneza Viashiria kwa kutumia maswali yafuatayo:  Kwa ajili ya nani?  Kiasi gani; mara ngapi?  Kwa uzuri gani (How well?)  Ifikapo lini?  Wapi? Mwisho tengeneza sentensi itakayokuwa kiashiria chako. Taarifa za awali ni muhimu sana unapotengeneza Viashiria!
  • 26. Day 2
  • 27. Utumiaji wa Bao Mantiki kama nyenzo ya Ufuatiliaji na Tathimini
  • 29. UFAFANUZI/MAELEZO YA MBAO MANTIKI  Safu wima 1 Safu hii inawakilisha mbinu yetu inatufahamisha nini tunatarajia kufanya na matarajio yetu tutakayofikia (huu ni mkakati tuliodhamiria kutekeleza).  Safu wima 2 Katika safu hii tunapima maendeleo ya lengo kuu. Hivyo tunatakiwa kutambua vigezo mbali mbali vitakavyobaini maendeleo ya kufikia lengo kuu. Vigezo hivi lazima viwe na sifa zifuatazo; rahis,i vinafikika, vinafikiwa, kinapimika, vinaamiminika, vinaendana na muda. Panatakiwa stadi kuzichagua. 
  • 30.  Safu wima 3 Safu hii inatoa maelezo ni wapi patapatikana taarifa/takwimu. Muhimu ikiwa taarifa za mradi, kumbukumbu za ufauatiliaji ni vema zikiwapo na ziwe rahisi kufikiwa.  Safu wima 4 Safu hii inawakilisha dhanio ambazo hutakiwa kuzingatiwa. Hujazwa kwa kuzingatia ngazi kutoka chini wakati huo tukijaribu kubaini sababu zilizo nje ya uwezo wetu zinazoweza kusababisha kutotekelezwa kwa mradi.
  • 31. Namna ya kukamilisha bao mantiki  Maelezo ya mradi yanakamilishwa kwanza halafu madhanio nayo yanashughulikiwa, kisha viashiria na hatimaye namna ya kuhakiki. Hata hivyo ukamilishaji wa jedwali unawezekana ukawa tofauti kutokana na hali halisi ilivyo na wanaohusika kujenga hilo jedwali.
  • 32. Kuanisha maelezo ya mradi (lengo kuu, lengo mahsusi, matokeo na shughuli) i.Kuchagua lengo kuu  Mara nyingi matawi ya juu kabisa ya mti wa malengo yatatoa picha nini liwe lengo kuu. Kwa mchoro wa hapo chini yapo dhahiri malengo makuu mawili  Kuongeza kipato na  Kuongeza lishe  Hata hivyo kwa kuwa mkakati tuliouchagua ni ule wa kilimo ambao unalenga zaidi katika kuongeza kipato basi lengo kuu litakuwa ni kuongeza kipato.
  • 33. ii. Chagua utakaochangia katika lengo kuu  Kuna njia mbalimbali za kuweza kuongeza kipato kwa kuangalia mti wa malengo moja ya njia inayoweza kutumika ni kuboresha masoko kwa wakulima. Kwa hiyo Lengo mahususi litakuwa : Masoko ya uhakika kwa wakulima yanapatikana3. • iii. Orodhesha matokeo  Watu wengi huwa wanashida ya kutofautisha matokeo na lengo mahususi na wanapofikia hatua hii wanapata shida sana kujua nini kinahitajika kwenye matokeo (outputs)
  • 34. Matokeo (Outputs) ni huduma au bidhaa zitolewazo na mradi kwa lengo la kufikia lengo mahsusi. Mfano Taarifa za masoko zinapatikana kwa urahisi na Wakulima wanalima kwa mkataba Itasaidia sana kuwezesha masoko ya uhakika kupatikana  Unapozungumzia lengo mahususi yale matokeo ya awali (immediate results) ambayo yatatokea kwa mkulima mwenyewe kwa mfano apatapo taarifa za masoko. Kwanza atapata elimu ambayo itasaidia kubadilisha mtazamo wake kuhusu masoko.
  • 35. iv. Orodhesha shughuli Kila tokeo lililoainishwa ni muhimu kuorodhesha shughuli gani zifanywe na mradi ili kupata tokeo hilo.  Mfano o Tokeo :Taarifa za masoko zinapatikana kwa urahisi  Shughuli : o Kutoa mafunzo o Kuunda kamati ya masoko o Kuandaa vipeperushi
  • 36. v. Ainisha rasilimali zinazohitajika kukamilisha shughuli  Mfano 1.1 Kutoa mafunzo : Mkufunzi, ukumbi, watu, kalamu, daftari, usafiri…… 1.2Kuunda kamati : Usafiri, mtaalamu, kalamu, daftari, watu………. 1.3Kuandaa vipeperushi : Mtaalamu « printer », karatasi, usafiri……….. 1.4Tayarisha bajeti ya mradi kwa kuainisha nyenzo katika fedha.
  • 37. Kutengeneza madhanio  Dhanio (Assumption) Hizi ni ali kuendana na shughuli na malengo ambazo lazima ziwe zimetokea au kuwepo ili mradi ufanikiwe. Lakini hizi haziwezi kudhibitiwa na mradi wenyewe:  Hizi (assumptions) huonyesha kiasi cha vikwazo katika mazingira (risks) vinavyokabili mradi.  Ili kupunguza athari za vikwazo (risks) hivi, wakati mwingine inatubidi kubadilisha baadhi ya shughuli na matokeo.  Katika kila hatua ya jedwali la mpango wa mradi, angalia na kuona kama shughuli zitaleta matokeo uliyokusudia au kama kuna kitu cha ziada nje ya mradi (assumptions) kinahitajika kuwepo ili shughuli zilete matokeo yaliyokusudiwa.  Tunaweza kukamilisha jedwali letu kuhusiana na Dhanio (assumptions) kwa kutumia maneno “kama” na “hivyo” na kuchora mishale kuonyesha uhusiano.
  • 38. Namna ya kutengeneza Viashiria Viashiria vinahusu taarifa tunazohitaji kupima maendeleo ya mradi kufikia malengo yake. Viashiria huonyesha kiwango cha utekelezaji kinachotakiwa kufikiwa ili kuweza kufanikisha malengo tuliyojiwekea kwenye mradi. Viashiria huweka msingi wa kufanya ufuatiliaji na tathmini. Viashiria huonyesha dhahiri ni vithibitisho (evidence) gani vitakavyokueleza kama lengo kuu, lengo mahususi au matokeo yamefikiwa kwa jinsi ya Uwingi (quantity) – kiasi gani? Ubora (quality) – hali gani? Muda upi? Eneo gani la kijiografia?
  • 39.  Kiashiria kizuri huwa na sifa zifuatazo:  Kinajitegemea: kiashiria kinapaswa kuonekana mara moja tu katika jedwali la mpango wa mradi (PPM). Kiashiria kimoja hakipaswi kutumika zaidi ya level moja katika jedwali hili.  Kiashiria budi kionyeshe mambo ya kweli yaliyopo (facts) na siyo vitu vya kufikirika (kuhisi)  Badiliko linalorekodiwa litokane na shughuli za mradi wako na si vinginevyo  Andika viashiria ambavyo ni rahisi kupata taarifa na kwa bei nafuu. Ikiwa bei ya kupata taarifa za viashiria ni ghali, itapelekea ufuatiliaji na tathmini kuwa ngumu na ghali pia.  Data za viashiria ziwe SMART ili hata wale walio nje wenye mashaka na mradi wako waweze kupima na kuona kwamba mabadiliko yaliyotokea ni ya kweli.
  • 40. Aina za Viashiria Viashiria ambavyo ni sehemu ya lengo (direct indicators). Kiashiria na lengo vinahusiana moja kwa moja. Viashiria na lengo havihusiani moja kwa moja lakini bado viashiria hivyo havionyeshi ni kazi gani tumefanikiwa kufikia malengo yetu (indirect indicators)  Mfano
  • 41. Jinsi ya Kuandaa / Kutengeneza Viashiria  Soma lengo kwa makini upate kuelewa kwa ufasaha sana  Ainisha na kuorodhesha mambo (parameter) yote katika lengo ambayo yanaweza kupimwa.  Chagua mambo machache yanayoweza kupimika kiuchuni kwa maana ya muda na fedha  Tengeneza kiashiria kwa kuzingatia yafuatayo: • Walengwa-Kwa ajili ya nani? • Kiasi gani, mara ngapi? • Ubora wa kiasi gani ? • Muda -Kufikia muda gani kutaleta mabadiliko ? • Eneo (Wapi) ?
  • 44. (baseline survey)  Taarifa za Awali huelezea hali halisi kwa wakati huu. Ili kupata taarifa za awali, ni budi kufanya Utafiti wa Awali, ambao hukusanya taarifa zinazosaidia kupima maendeleo ya utekezaji wa shughuli.  Lengo kuu la utafiti wa awali ni kupata hali halisi ilivyo ili hapo baadaye tuweze kupima maendeleo yaliyofikiwa kutokana na utekelezaji wa mradi.  Utafiti wa awali unapaswa kufanywa kabla ya kuandaa mradi. Hii ni kwa sababu taarifa hii husaidia katika kuandaa Viashiria
  • 45. Utafiti wa awali (inaendelea) Namna ya Kufanya utafiti wa awali:  Hatua tano zifuatazo ni muhimu katika kufanya utafiti wa awali • Amua ni taarifa zipi zinahitajika • Andaa njia za kukusanya taarifa mf. Dodoso • Hakiki dodoso (pre-test) • Fanya ziara za kukusanya taarifa • Fanya uchambuzi wa taarifa • Andika matokeo ya utafiti
  • 47. KAZI ZA VIKUNDI Rejea bao mantiki fanya maboresho kama tulivyoelekezana
  • 48. Uandaaji wa mpango wa ufuatiliaji
  • 49. Utayarishaji wa mpango wa Ufuatiliaji Hatua za utayalishaji mpango wa Ufuatiliaji  Elewa na kuchambua lengo kuu, malengo mengine na shughuli ukizingatia viashiria na shabaha (targets), na njia za kuthibitisha.  Ainisha nini cha kufanyia Ufuatiliaji.  Amua namna gani Ufuatiaji utafanyika; Njia za kuthibitisha au Vyanzo vya taarifa.  Amua namna gani taarifa zitakua zinakusanywa (Njia za kuthibitisha (Means of verification) zinaweza kusaidia).  Kusanya taarifa
  • 50. Kutayarisha mpango wa Ufuatiliaji (inaendelea)  Chambua hali ya taarifa kwa kuhesabu, kupima, au kulinganisha takwimu mbalimbali.  Weka katika kumbukumbu taarifa/data zilizokusanywa na kuchambuliwa.  Linganisha na shabaha (target) iliyokuwa imewekwa au kiashiria.  Andika na kupeleka ripoti kwa wadau husika ili waweze kuchukua hatua.
  • 51. Mfano wa mpango wa UfuatiliajiLengo au shughuli Kiashiria au shabaha (target) Chanzo cha taarifa/data Taarifa/data ikusanywe kila baada ya muda gani? Gharama Mhusika Nani atatumia taarifa? Atatumia taarifa kwa ajili ya nini? Dhanio
  • 52. Mpango wa Ufuatiliaji ni budi uweze kujibu maswali yafuatayo:  Nini cha kufuatilia?  Namna gani ya kufuatilia?  Nani afuatilie?  Lini Ufuatiliaji ufanyike?  Rasilimali zipi zinahitajika?  Nani atatumia taarifa hizo na kwa namna gani?
  • 54. 2. NINI CHA KUFANYIA TATHMINI?
  • 55. Mchakato wa Tathmini  Tathmini huangalia vipengele muhimu vifuatavyo: • Maendeleo ya utekelezaji ukilinganisha na ‘vigezo vya kusudio’ (targets) vilivyopangwa. • Fedha zilivyopatkana na vile zilivyotumika. • Ushiriki wa wadau mbalimbali (collaborators) • Muda uliotumika katika kutekeleza mradi na ufanisi katika matumizi ya rasilimali katika kutekeleza mradi.
  • 56. Mchakato wa Tathmini (inaendelea) Namna malengo yaliyowekwa wakati wa kuandaa mradi yalivyo na mafanikio yanayotarajiwa. Mabadiliko ya maisha ya walengwa na jamii kwa ujumla (mabadiliko ya kijamii na kiuchumi). Jamii kupata mtazamo mpya/ujuzi/utendaji mpya.
  • 58. Aina za Tathmini  Tathmini ya nje (External evaluation): • Aina hii ya Tathmini mara nyingi hufanywa na watu kutoka nje ya shirika linalotekeleza mradi (External evaluators). • Tathmini hii hufanyika katikati ya kipindi kizima cha utekelezaji wa mradi, mwisho wa mradi au baada ya mradi kukamilika. • Kwa ruzuku ndogo na zile za kati yamkini Tathmini ya mwisho wa mradi na baada ya mradi kukamilika hufaa zaidi.  Tathmini ya ndani ([internal]Self-evaluation): • Hii hufanywa na watekeleza mradi ndani ya shirika na shirika ndilo linaamua lifanye katika kipindi gani cha utekelezaji wa mradi. Aina zote za Tathmini zinaweza kufanywa kawaida au uchambuzi wake ukawa wa kina sana.
  • 60. Day 4
  • 61. Ukusanyaji na utumiaji wa taarifa/takwimu
  • 62. 62
  • 63. Ukusanyaji wa taarifa/takwimu  Ukusanyaji wa taarifa/takwimu unahusika na uchaguzi wa njia za kufanya uchunguzi.  Hakuna njia moja bora ya ukusanyaji taarifa: • Uchaguzi wa njia ya kukusanya taarifa unategemea aina ya taarifa inayo hitajika. • Uchaguzi unategemea pia kitu gani kinawezekana kulingana na muda na rasilimali nyingine zinazo hitajika. Njia mbalimbali zinapendekezwa. • Ukusanyaji wa Taarifa/Takwimu kwa ajili ya Ufuatiliaji na Tathmini huanzia siku ya kwanza unapoanza utekelezaji wa mradi.
  • 64. Ukusanyaji wa taarifa/takwimu (inaendelea) • Ukusanyaji wa taarifa/takwimu unahitaji kujituma sana. • Katika mtazamo wa Ufuatiliaji na Tathmini, tunakusanya taarifa/takwimu ili kuthibitisha viashiria tulivyoweka katika ngazi mbalimbali za ubao mantiki. Kwa hiyo kila siku taarifa/takwimu budi zihifadhiwe katika madaftari, mafaili au komputa na kutolewa pindi zinapo hitajika.
  • 65. JE TAARIFA ZOTE NI MUHIMU
  • 66. Ukusanyaji wa taarifa/takwimu (inaendelea) • Wakati wote viashiria hutoa mwelekeo wa njia ipi itumike katika ukusanyaji wa taarifa. Na hii huonyeshwa katika ‘Njia ya kuthibitisha’ ( Means of Verification). • Ni muhimu sana wakati wa kutengeneza viashiria kubaini njia za kukusanya taarifa/takwimu ambazo ni rahisi kwa maana ya fedha na muda. • Epuka kukusanya taarifa nyingi sana au kidogo sana ambazo hazitaweza kufanyiwa uchambuzi au kutumika. • Kumbuka: • 55% ya taarifa katika jamii Ni nzuri kuzifahamu (Nice to Know)
  • 67. Ukusanyaji wa taarifa/takwimu (inaendelea) • 35% ya taarifa katika jamii ni vizuri kuzifahamu (Useful to know) • 10% tu ya taarifa katika jamii ni lazima kujifahamu (Must Know )  Kwa maana nyingine ni kwamba kuna taarifa/takwimu nyingi sana katika jamii. Inabidi kutoa kipaumbele kukusanya zile taarifa tu ambazo lazima uzifahamu. Muda ukitosha unaweza kukusanya taarifa nyingine.
  • 68. Uchambuzi wa taarifa/takwimu na kuzitafsiri  Uchambuzi wa taarifa/takwimu na kutafsiri (interpretation) ni kitendo cha kubadili taarifa/takwimu na kuzigeuza ziwe sentensi zenye kutoa ujumbe wenye maana. Hii inaweza kufanyika wakati wote au kwa vipindi maalum.  Uchambuzi wa taarifa/takwimu unaweza kufanyika kwa namna tofauti tofauti kutegemeana na kama taarifa/data ziko katika ubora (qualitative) au katika vipimo (quantitative).  Unapozipa taarifa/takwimu maana unakua unaoanisha viashiria na matokeo na mpango wa kazi.
  • 69. VIPENGELE VYA UCHAMBUZI WA MABADILIKO YATOKANAYO NA MRADI
  • 70. VIPENGELE VYA UCHAMBUZI WA MABADILIKO YATOKANAYO NA MRADI (Impact assessment) Vipengele muhimu vya uchambuzi wa mabadiliko  Lengo la Uchambuzi wa Mabadiliko  Hatua ya kuzingatia wakati wa uchambuzi  Mbinu/Njia ya kufanya uchambuzi  Hadithi rejea za kufanya tathimini
  • 71. Vipengele vya uchambuzi wa mabadiliko (inaendelea) Lengo la Uchambuzi wa Mabadiliko  Huu ni mchakato wa utambuzi wa mabadiliko ambayo yamekadiliwa ili kuboresha hali ya walengwa, kijamii, mazingira na uchumi). Uchambuzi huo huzingatia: • Hali ilivyokuwa kabla ya mradi kuanzishwa • Jinsi shughuli za mradi zilivyotekelezwa • Taratibu za uchambuzi zilivyoainishwa • Uchambuzi kuwa shirikishi
  • 72. Hatua ya kuzingatia  Ufuatiliaji na tathmini ya ndani ya asasi huwa ni kwa ajili mafunzo endelezu ya watendaji na wadau wa mradi, (mfano tathimini ya viashiria vya mfumo wa utoaji na upatikanaji wa taarifa)  Tathmini inayofanywa na watu wa nje ya mradi ripoti yake huwa kwa ajili ya madhumuni maalumu Mifano ya uchambuzi wa mabadiliko ya walengwa husika:  Mabadiliko ya hali ya umasikini  Mabadiliko ya taratibu  Mabadiliko hali ya Kijamii  Mabadiliko ya hali ya afya  Mabadiliko ya Mazingira
  • 73. Uchambuzi wa kubaadiliko kwa ujumla hufanyika kwa kujumuisha maswali ya kijamii, kiuchumi na kimazingira. Uchambuzi huo hulenga kuleta.  Uwajibikaji  Kuwepo na ushahidi wa mafanikio ya shughuli na kuzingatia garama halisi  Kuboresha hali ya walengwa  Kutoa mwongozo wa ambavyo sera za serikali na wafadhili zinavyotakiwa zitekelezwe ili zikubalike na kufanikisha kuleta maendeleo.
  • 75. Ngazi za uchambuzi  Ngazi ya juu (mfano serikali) Mara nyingi Serikalini na ngazi ya kiutawala za Asasi hujishughulisha zaidi na masuala ya sera.  Ngazi za Kati ( mfano uongozi wa Asasi) Huchambua Sera, sheria na miongozo na kufanya marekebisho kuwezesha mafanikio  Ngazi ya chini (hii ni ngazi ambayo mradi hutekelezwa, mnahusika nayo) • Huzingatia vipengele vifuatavyo • Jinsi mradi / Program ilivyoandaliwa.
  • 76. Ngazi ya chini (inaendelea) • Je bao mantiki lilitayarishwa • Je nyaraka za mradi husika zipo • Je viashiria na vyanzo vyake vya uhakiki vimeainishwa • Je utaratibu wa utekelezaji wa shughuli za mradi ulivyo umezingatiwa. • Hali ya matumizi na mapato (rasilimali) ilivyo. • Jinsi uongozi wa mradi/ programu ulivyo • Taratibu zilizowekwa za ufuatiliaji utekelezaji wa mradi ulivyo
  • 77. Njia/ jinsi ya kufanya uchambuzi wa mabadiliko ya mradi  Ubora/ Ustahilifu (qualitative)  Kwa kupima mabadiliko muhimu (quantitative)  Shirikishi (Participatory) Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kufanya uchambuzi wa mabadiliko  Uwazi wa taratibu ya uchambuzi.  Ushiriki wa wadau katika uchambuzi wa mabadiliko  Uhakika wa vyanzo vya taarifa/ Takwimu  Nia ya kutumia repoti kuboresha; sera, taratibu na miongozo ya utendaji wa Asasi  Uzoefu wa asasi husika na garama zinazohusu uchambuzi wa mabadiliko.
  • 78. Hadidu za rejea za kufanya tathimini (ToR) Huonyesha kwa uwazi nini timu ya uchambuzi inatakiwa ifanye Huzingatia masuala yafuatayo:  Hubainisha shughuli za kufanyika  Matokeo tarajiwa  Mbinu za uchambuzi wa mabadiliko  hueleza historia ya mradi husika kwa ufupi  Huainisha vyanzo vya taarifa za utekelezaji wa mradi husika  Huanisha madhumuni ya uchambuzi, walengwa na matumizi ya ripoti ya uchambuzi  Inafafanua timu ya watakaofanya uchambuzi na ushiriki wa wadau wengine
  • 79. AHSANTENI NA NINAWATAKIA SAFARI NJEMA 79
  • 81. Uandikaji wa Ripoti • Ripoti huandikwa ili kupelekwa kwa mamlaka uongozi au ile ipelekwayo kwa walengwa. • Ripoti huandaliwa tangu mradi unapoanza kutekelezwa. Chochote kinachotekelezwa na mradi, lazima ripoti ya maandishi iandaliwe. Hizi ripoti za utekelezaji baadaye hukusanywa pamoja ili kupata ripoti za mwezi, robo mwaka au mwaka na hujadiliwa na walengwa /mamlaka husika.
  • 82. Uandikaji wa Ripoti (inaendelea)  Ripoti za utekelezaji wa miradi budi zieleze vipengele vifuatavyo: 1. Shughuli zilizo pangwa. 2.Shughuli zilizoweza kutekelezwa (kama kuna tofauti, kwa nini?). 3. Njia iliyotumika katika utekelezaji 4.Changamoto zilizojitokeza 5.Mafunzo gani yamepatikana kutokana na utekelezaji wa mradi 6.Mna mapendekezo gani.
  • 84. Kukabithi rasimu Kila mshiriki kukabithi rasimu ya bao Mantiki na mpango wa ufuatiliaji wa mradi husika wa Asasi yake.

Editor's Notes

  1. Tizama jadwali ukurasa wa 17
  2. Kwa maelezo zaidi tizama ukurasa wa 2 Moduli ya mafunzo
  3. Tizama ukurasa wa 20 wa Moduli ya mafunzo
  4. Mfano : Tizama ukurasa 22 wa moduli ya mafunzo