Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Mpango_wa_biashara_inayoanza.ppt
1. Mpango wa biashara
inayoanza
Paul Pm Ndomba
Mob: +255 712 288 012; Email: ndopa4@yahoo.com
Skype ID: Maprosoo2; Fb: mcndomba Maprosoo
“Wanaoongoza vyombo vya usafiri, wanaweza kwenda kokote
wanakotaka kufika bila kupotea; ili mradi tu wawe na ramani zenye
vipimo sahihi”
12/27/2022 1
mcndomba
2. Matarajio ya mada hii ujue;
1. Maana ya mpango wa biashara
2. Umuhimu wa kuwa na mpango wa biashara
3. Waandaaji na watumiaji wa mpango wa
biashara
4. Namna ya kuandika mpango wa biashara
5. Jinsi ya kutumia mpango wa biashara
12/27/2022 2
mcndomba
3. Kupanga ni nini?
Kupanga ni kuchagua matendo yanayotumia
muda na rasilimali za kifedha ili kuzitumia kwa
ufanisi/uchache ili kupata matokeo makubwa
ama mazuri
Watu wanajua kupanga, ila wanatofautiana
katika namna ya kupanga na namna ya
kutekeleza vizuri walichopanga
12/27/2022 3
mcndomba
4. 1. Asiyepanga chochote, tayari amechagua
kushindwa
2. Asiyepanga vizuri, anapanga vizuri namna
ya kushindwa
3. Asiyetekeleza anachopanga vizuri,
anatekeleza kushindwa
4. Anayetekeleza vizuri aliyepanga vizuri,
amechagua kufanikiwa vizuri
Idadi kubwa ya watu inatekeleza mipango yao
kwa kauli namba 1 hadi 3 na ndio maana wengi
wanashindwa
Kauli hizi ni za kweli
12/27/2022 4
mcndomba
5. 1. Mpango wa biashara ni nini?
Mpango wa biashara ni andiko linalofafanua
namna biashara mpya itakavyoanzishwa au;
namna biashara iliyopo itakavyopanuliwa ama
kuundwa upya
Unahitaji mpango mzuri wa biashara kabla ya
kuanza shughuli yoyote ya kuanzisha biashara
mpya au kupanua uliyonayo
12/27/2022 5
mcndomba
6. 2. Umuhimu wa mpango wa biashara
i. Unaongeza mafanikio katika biashara yako
ii. Unaonyesha dira ya kutekeleza shughuli na
namna ya kutumia rasilimali zilizopo
iii. Utaweza kujua muda uliojiwekea kupata
malengo ya kumiliki biashara yako
iv. Utawezesha kujua vyanzo vya mapato
v. Ni rahisi kufanya tathmini ya biashara yako
vi. Unawezesha kuchanganua shughuli
zilizopo; nani, wapi, lini, zana, vipi, ngapi, nk
12/27/2022 6
mcndomba
7. Hasara inayopatikana inaashiria
Kutokuwa na mpango mzuri
Kutekeleza vibaya mpango mzuri
Kutekeleza vizuri mpango mbaya
Kuto kutekeleza kilichopangwa vizuri
Kupata faida nzuri ni lengo la kila
mfanyabiashara
Anapopata faida kubwa inaweza kuashiria kuwa
mpango wa biashara ulipangwa na kutekelezwa
vizuri
12/27/2022 7
mcndomba
8. 3. Waandaaji na watumiaji
Mpango kazi huandaliwa kwa ajili ya;
1. Wamiliki wa biashara au mradi
2. Mameneja watakaoendesha mradi huo
3. Wawekezaji walio tayari kukupa mitaji yao
4. Wajumbe wa kikao cha utendaji (bodi)
5. Kitengo cha usajiri wa biashara au mradi
6. Kupata ruzuku au kukopeshwa fedha na
benki au mtu makini
12/27/2022 8
mcndomba
9. Watumiaji wanapenda kujua yafuatayo;
1. Je, kazi maalumu ya biashara inatekelezeka au la?
2. Watendaji/wasimamizi wa mradi wanasifa?
3. Gharama za biashara kabla ya kuuza bidhaa
zenyewe ni zipi?
4. Fedha za kulipia gharama hizo zitatoka wapi?
5. Je, bidhaa yako itapata soko la uhakika?
6. Mauzo yataleta mapato yanayotosha gharama za
shughuli na kuongeza mtaji?
7. Je, mapato yatatosheleza ulipaji wa deni, gawio la
faida kwa waliotoa mtaji na kuacha faida?
Majibu ya maswali hayo ni mafanikio ya biashara yako
12/27/2022 9
mcndomba
10. Nani anapaswa kuandaa?
Mpango wa biashara yako unapaswa kuandaliwa na
wewe mwenyewe
Kama biashara yako inagharimu mamilioni ya shilingi
za kitanzania, unaweza kushirikiana na wataalamu
wa kifedha/ wahasibu/ watu wazoefu katika aina ya
biashara yako
Meneja wa biashara anapaswa kuwepo wakati wa
mchanganuo wa biashara
Kama meneja hakuwepo anapaswa kuelezwa kwa
ufafanuzi wa karibu ili ajue na kuelewa kilichopangwa
12/27/2022 10
mcndomba
11. 4. Namna ya kuandika mpango wa
biashara
Sura muhimu za mpango wa biashara
i. Utangulizi na historia fupi ya biashara
ii. Wasifu na malengo ya biashara
iii. Bidhaa au huduma itakayotolewa
iv. Menejimenti na utawala
v. Masoko na uuzaji
vi. Mahitaji ya kifedha
vii. viambatanisho
12/27/2022 11
mcndomba
12. a) Utangulizi & historia fupi ya biashara
Andika mhutasari mfupi wa biashara unayopendekeza
kuianzisha. Zungumzia kwa ufupi maeneo yafuatayo;
Jina la biashara yako
Hali halisi ya biashara kama yako mtaani/nchini
Hali ya uchumi na kubadilika kwa tabia ya matumizi
ya wateja
Masoko na urahisi wa kuuza
Hitaji la mtaji na makisio ya faida
Umahiri wa meneja au wasimamizi wa biashara yako
kwenye soko kwa urahisi
12/27/2022 12
mcndomba
13. b) Wasifu wa malengo ya biashara
Changanua hali halisi ya biashara au huduma unayotoa
au unayokusudia kutoa, na weka malengo ya biashara
yako. Zingatia;
Utume na njozi ya biashara yako (mission&vision)
Nembo au alama ya bidhaa kama ipo
Lengo mahususi la biashara
Mahali biashara ilipo
Malengo katika muda mfupi na mrefu
Uimara na udhaifu wa biashara yako
Fursa na vitisho vinavyowakabili
Namna unavyoweza kuchangamkia fursa na
kukabiliana na vitisho kwa mafanikio
12/27/2022 13
mcndomba
14. c)Bidhaa au huduma itakayotolewa
Fafanua kwa undani namna bidhaa ilivyo,
unavyokusudia kuizalisha, kuiboresha na kuifanya
ipenye kwenye soko. Zingatia;
Orodha ya bidhaa au aina ya huduma utakazotoa
Malighafi ya kutengenezea
Mchakato wa kuitengeneza hadi ikamilike
Picha au mchoro wake kama upo
Ulinganifu wa bidhaa/huduma za wengine
zinazofanana na yako
Mbinu za kuwashinda washindani
Matokeo/faida watakayopata watumiaji wa
bidhaa/huduma yako
12/27/2022 14
mcndomba
15. d) Menejimenti na utawala
Eleza umahiri wa meneja, elimu na uzoefu wake, mipango ya
kujiendeleza na kuendeleza wafanyakazi wengi
Taja idadi za biashara au mradi wako
Idadi ya wafanyakazi na namna utakavyowalipa
Onyesha chati ya mfumo wa utawala
Eleza utekelezaji wa majukumu ya kila siku
Utaratibu wa kuweka kumbukumbu ya kazi zilizokamilika kwa
siku
Taratibu za vikao na namna ya kuviendesha
Udhibiti wa ndani katika manunuzi, utunzaji wa malighafi,
bidhaa, vifaa na fedha
Taratibu za kisheria. Mf. Kujisajili, utambulisho wa mlipa kodi
(TIN no).,nk
12/27/2022 15
mcndomba
16. e)Masoko na uuzaji
Fafanua kwa ufupi yafuatayo;
Walengwa wa bidhaa au huduma yako. Nani,
wapi, lini, vipi, namna gani, nk
Utakavyoipenyeza kwenye soko
Wapi bidhaa yako itasambazwa
Namna ya kuwajulisha watumiaji. Mf. Redio,
tv, magazeti, nk
Namna ya kupanga bei ya kuuzia
12/27/2022 16
mcndomba
17. f) Mahitaji ya kifedha
Taja fedha zinazotakiwa kuanzisha biashara yako
Eleza vyanzo vya mapato
Eleza kiasi kitakachotosha kuendeshea shughuli zote
(working capital)
Kama ni mkopo au msaada taja kiasi utakacho
changia
Taja idadi na thamani ya vifaa unavyohitaji
Andika taarifa ya utendaji, mauzo na matumizi
Andika taarifa ya ukuaji wa mtaji
12/27/2022 17
mcndomba
18. g) Viambatisho
Viambatisho vinavyotakiwa ni kama;
Picha za bidhaa
Mfano wa fomu kutoka kwa wateja
wanaotaka kununua bidhaa (customers’ order
forms,) nk
12/27/2022 18
mcndomba
19. 5. Jinsi ya kuutumia mpango kazi
Namna ya kuutumia ni kurejea katika kila
kipengele na kuona jinsi kinavyotekelezwa
kama ndivyo kilikuwa kimepangwa
Ni muhimu pia kuandaa mpango mkakati
ambao utaonyesha muda wa kuanza na
kukamilisha kila kipengele
Utataja kila muhusika na majukumu yake
Zana atakazotumia na watu atakaoshirikiana
nao
12/27/2022 19
mcndomba