SlideShare a Scribd company logo
1 of 37
Download to read offline
UTANGULIZI

Mwongozo huu umeandaliwa kwa ajili ya wakufunzi ambao wanataka kuendesha mafunzo
shirikishi ya kilimo hifadhi ya mazingira katika ngazi ya vijiji, pia kimeandaliwa kwa namna
ambayo matumizi bora ya ardhi na rasilimali za misitu yatazingatiwa.
Mafunzo haya yatatolewa kwa wakulima wadogo wadogo walioko kwenye eneo la Mradi hasa
wale waliojiunga kwenye vikundi vya shamba darasa na wadau mbalimbali wanaonufaika kwa
namna moja au nyingine na Mradi wa CCAP. Mafunzo haya yataongeza uelewa wa wakulima
kuhusu kilimo hifadhi na yatawawezesha wananchi kutekeleza kwa vitendo zana nzima ya
kilimo hifadhi kwenye mashamba yao.

Shughuli hii inatekelezwa chini ya Mradi        wa Mabadiliko ya Tabia nchi, kilimo na
kupunguza umasikini ( CCAP) ambao unatekelezwa kwa ushirikiano wa mashirika matano
ambayo ni MJUMITA, MVIWATA, TFCG, Action Aid na TOAM. Mradi huu una lengo la
kupunguza umasikini miongoni mwa wakulima wadogo wadogo wanaolima mashamba yenye
ukubwa wa hekta 2 Tanzania na kuwajengea uwezo wa kukabiliana na kuhimili mabadiliko ya
tabianchi ikiwa ni pamoja na kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa kwa kuboresha njia za kilimo.

MPANGILIO WA MUONGOZO WA MAFUNZO

Muongozo huu umegawanyika katika sehemu kuu nne, nazo ni:-

   1. Utangulizi
   2. Mabadiliko ya tabia nchi
       Baada ya mafunzo, washiriki watakuwa wameweza kuelezea yafuatayo;-
          o Mabadiliko ya tabianchi yanamaanisha nini
          o Mabadiliko ya tabianchi yanatokeaje
          o Ushahidi wa mabadiliko ya tabia nchi
          o Sababu za mabadiliko ya tabia nchia
          o Athari zake
   3. Kilimo rafiki wa mazingira kwa chakula na kipato
       Baada ya mafunzo, washiriki watakuwa na uwezo wa kuelewa:-

             KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
    MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
o Maana ya kilimo rafiki wa mazingira
       o Umuhimu wa kilimo rafiki wa mazingira
       o Kanuni za kilimo rafiki wa mazingira
       o Mbinu/hatua za kufuata katika kilimo rafiki wa mazingira
       o Faida ya kilimo rafiki wa mazingira
       o Changamoto
4. Udongo
   Baada ya mafunzo washiriki watakuwa wamefahamu
       •   Maana ya udongo
       •   Umuhimu wa viumbe wanaoishi ardhini
       •   Udongo wenye rutuba ukoje
       •   Mbinu za kurutubisha udongo
5. Utengenezaji wa mboji
   Baada ya mafunzo washiriki watakuwa wamefahamu
       •   Maana na umuhimu wa mboji
       •   Vifaa visivyofaa kutumiwa wakati wa kutengeneza mboji
       •   Vitu vinavyofaa kutumiwa wakati wa kutengeneza mboji
       •   Namna ya kutengeneza mboji
       •   Wadudu wenye manufaa na mazingira yafaayo kwa utengenezaji wa mboji
       •   Muda wa kukomaa na matumizi ya mboji
6. Hifadhi ya maji
   Baada ya mafunzo washiriki watakuwa wanaelewa:-
       • Umuhimu wa maji
       • Namna ya kuhifadhi maji ardhini
       • Kuvuna maji
7. Kuundwa kwa Vikundi vya shamba darasa
   •   Maana na umuhimu wa kikundi

   •   Kutofautisha kati ya kikundi na mkusanyiko

   • Mambo ya kuzingatia wakati wa kuunda kikundi kilicho imara
         KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
•   Kazi za kikundi

       •   Umuhimu wa kuwa na uongozi wa kikundi na sifa za uongozi

       •   Jinsi ya kuandaa rasimu ya katiba ya kikundi

       •   Kanuni za katiba bora

       •   Zana ya mtandao

       •   Namna ya kuwaunganisha wanakikundi na mitandao ya MJUMITA na MVIWATA




MADA 1: MABADILIKO YA TABIANCHI

1.1 Mabadiliko ya tabia nchi yanamaanisha nini?

Tabia nchi kwa kawaida hufafanuliwa kama wastani wa hali ya hewa, hivyo tabia nchi na
hali ya hewa huingiliana japo ni vitu tofauti. Mabadiliko ya tabia nchi ni mabadiliko ya muda
mrefu ambayo yametokea katika maeneo mbalimbali ya dunia. Mabadiliko haya huweza
kupimwa kwa kuzingatia hali ya hewa kama vile kiwango cha joto na baridi, mvua na ukame.

1.2 Mabadiliko ya Tabia nchi yanatokeaje?

Mabadiliko ya tabia nchi hutokea wakati ambapo hali ya hewa katika eneo fulani hubadilika
katika kipindi cha muda fulani (mfano baada ya miaka 10). Mabadiliko hayo hutokea wakati
miale ya jua inapokuja moja kwa moja duniani.

Mabadiliko ya tabia nchi ni tishio kwa maendeleo kwa sababu huathiri afya zetu, makazi,
miundo mbinu, kilimo na mfumo wa ekolojia. Pamoja na hayo, mabadiliko ya tabia nchi
husababisha kutetereka kwa hali ya maisha katika maeneo mbalimbali ya dunia.

1.3 Ushahidi wa mabadiliko ya tabia nchi.

Ushahidi wa mabadiliko ya tabia nchi ni kuwepo kwa mafuriko na ukame katika maeneo
mbalimbali nchini na dunia nzima. Kwa upande wa Tanzania tumeshuhudia mafuriko hayo
wilayani Kilosa na ukame Mkoani Manyara.

             KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
    MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
1.3.1 Milipuko ya magonjwa

Ugonjwa kama malaria umejitokeza katika maeneo ambayo hapo awali haukuwepo. Katika
mkoa wa Njombe ambao uko nyanda za juu kwenye baridi, ugonjwa wa malaria haukua tatizo
katika wilaya za Njombe na Mafinga. Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, joto limeongezeka
na kusababisha kuwepo na makazi ya mbu wanaosababisha malaria katika maeneo hayo.

1.3.2 Ukame

Kutokana na ukame unaosababishwa na mvua zisizokuwa na mpangilio, imepelekea kupungua
kwa mavuno. Mvua zisizoaminika ni mojawapo ya madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia
nchi. Haya yote yamepelekea watu wengi duniani kukosa chakula na hatimaye wengine kufariki
                       kwa sababu ya njaa.

                       Kuyeyuka kwa barafu katika vilele vya milima (mfano Mlima
                       Kilimanjaro)

Kuyeyuka kwa barafu katika vilele vya milima ni kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha
joto. Kiwango cha joto kinaongezeka kutokana na kuharibika kwa tabaka la ozone lililopo angani
ambalo kazi yake ni kupunguza miale ya jua inayokuja duniani. 80% yatheluji ya mlima
Kilimanjaro , ambao ni mlima mrefu zaidi katika bara la afrika imetoweka kwa kipindi cha tokea
mwaka 1912.

1.3.3 Kuongezeka kwa kina cha bahari

Kuongezeka kwa kina cha bahari ni ushahidi wa kuwepo kwa
mabadiliko ya tabia nchi. Hivi leo kuna pwani au fukwe za bahari
ambazo zimeanza kutoweka kutokana na kuongezeka kwa kina cha
bahari. Haya yote ni matokeo ya mabadiliko ya tabia nchi.

1.4 SABABU ZA MABADILIKO YA TABIA NCHI



             KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
    MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
Mabadiliko ya tabia nchi yamesababishwa na vitu ama vitendo mbalimbali ambavyo
vimechangia kwa sehemu kubwa uharibifu wa mazingira. Vitendo vilivyochangia uharibufu wa
mazingira na kusababisha mabadiliko ya tabia nchi ni pamoja na:-

1.4.1 Kilimo cha Kuhamahama

Mabadiliko ya tabia nchi kwa namna moja au nyingine yanasababishwa na kilimo cha kuhama
hama. Wakulima wadogo wadogo walio wengi Tanzania wanalima kilimo cha kuhama hama
ambapo shughuli hiyo hupelekea kufyekwa kwa misitu mingi katika maeneo ambayo mashamba
mapya hufunguliwa. Katika shughuli hii, miti na uoto wote uliopo juu ya uso wa ardhi
unaosaidia kufyonza hewa ukaa huaribiwa. Hewa hii hukusanyika angani na kuharibu tabaka la
ozone na kusababisha ongezeko la joto duniani na hivyo kutokea mabadiliko ya tabia nchi

1.4.2 Uchomaji moto wa mabaki ya mazao shambani

Shughuli za uchomaji moto mabaki ya mazao shambani huambatana na moshi unaokusanyika
angani na kuchangia kuharibika kwa tabaka la ozoni na kusababisha mabadiliko ya tabia nchi.

1.4.3 Moshi kutoka viwandani na kwenye magari

Leo hii kuna idadi kubwa sana ya viwanda na magari duniani kote ukilinganisha na miaka ya
nyuma. Moshi kutoka viwandani na kwenye magari unachangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la
mabadiliko ya tabia nchi. Moshi huu huharibu tabaka la ozone angani ambalo kazi yake ni
kupunguza ukali wa miale ya jua ifikayo duniani na hivyo husababisha ongezeko la joto duniani.

1.4.4 Uchomaji mkaa usio endelevu

Uchomaji mkaa ni mojawapo ya shughuli zinazofanywa na mwanadamu ambazo zinachangia
kwa kiasi kikubwa katika mabadiliko ya tabia nchi. Uchomaji wa mkaa huambatana na ukataji
wa miti na uchomaji wa magogo. Shughuli hii huharibu tabaka la ozone na hivyo kuongezeka
kwa kiwango cha joto duniani.




             KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
    MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
Mchoro 1: Uandaaji wa tanuru      Mchoro 2: Utengenezaji wa mkaa
          kwa ajili ya mkaa                      husababisha hewa ya ukaa




1.4.5 Ukataji miti hovyo




Mchoro 3: Ukataji wa miti kwa matumizi ya kuni           Mchoro 4: Ukataji wa miti kwa ajili
ya kujengea

Kwa kawaida miti hufyonza hewa ukaa. Kwa maana hiyo, miti ikikatwa hovyo hewa ukaa
haitafyonzwa tena badala yake itaenda kuharibu tabaka la ozone lililoko angani ambalo kazi
yake ni kupunguza ukali wa miale ya jua. Baada ya uharibifu huo kiwango cha joto duniani


             KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
    MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
huongezeka kwa kiasi kikubwa na hivyo kusababisha madhara mengi kama vile ukame na
ukosefu wa mvua.

1.4.6 Uchomaji wa misitu

Uchomaji wa misitu unaosababishwa na shughuli mbalimbali kama vile urinaji wa asali,
uwindaji wa wanyama na uchomaji misitu kwa imani potofu, huchangia kuongezeka kwa hewa
ukaa angani ambayo huadhiri tabaka la ozoni na kusababisha ongezeko la joto duniani. Mfano:
Katika maeneo mengi Tanzania watu wanaamini kwamba wakichoma moto na kusafiri umbali
mrefu aliyechoma moto ataishi muda mrefu.

1.4.7 Uchimbaji wa madini.

Uchimbaji wa madini ni shughuli inayoambata na kubadili maeneo ya misitu kuwa katika
matumizi mengine. Katika shughuli hii, miti na uoto wote uliopo juu ya uso wa ardhi unaosaidia
kufyonza hewa ukaa huaribiwa. Hewa hii hukusanyika angani na kuharibu tabaka la ozone na
kusababisha ongezeko la joto duniani na hivyo kutokea mabadiliko ya tabia nchi.

1.4.8 Ufugaji wa mifugo

Mifugo mingi ikifugwa katika eneo dogo la malisho huharibu uoto wa asili ikiwa ni pamoja na
nyasi, vichaka na miti michanga ambayo ingesaidia kunyonya hewa ukaa




MADA 2: KILIMO RAFIKI WA MAZINGIRA KWA CHAKULA NA KIPATO

2.1 Maana ya Kilimo rafiki na mazingira/kilimo endelevu.

          •   Mfumo huu ni ule unaotumia mbinu mbalimbali zinazoendelea kulinda afya ya
              udongo, maslahi ya kimazingira, wanyama na binadamu.


          •   Kilimo hai na hifadhi ya mazingira kinatuwezesha kuzalisha chakula salama bila
              kuathiri matumizi ya ardhi kwa vizazi vilivyopo na vijavyo .


             KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
    MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
•   Kilimo hiki kinahimiza uzalishaji wa mazao kwa kutumia samadi na mboji na
              udhibiti wa wadudu na magonjwa kwa kutumia njia za asili.


          •   Kilimo hiki hakitumiii madawa na mbolea toka viwandani au hutumika kwa
              kiwango kidogo sana pale inapohitajika na kinapinga matumizi ya viwatilifu
              vyenye sumu na mbegu zenye vinasaba na shughuli zozote            zinazopelekea
              uharibifu wa udongo , maji na maliasili zinginezo.


       Inadaiwa kuwa Kilimo hai na hifadhi ya mazingira ni jibu la matatizo yanayoathiri
       mazingira kutokana na uendelevu kiuchumi, rafiki katika matumizi ya malighafi na
       hifadhi ya mazingira na rasilimali, chenye kukubalika katika jamii, na kumudu ushindani
       wa kibiashara. Mafunzo haya yatajikita zaidi katika kuelezea mfumo wa kilimo hai na
       hifadhi ya mazingira kama njia itakayowawezesha wananchi kukabiliana na mabadiliko
       ya tabianchi.



2.2 Umuhimu wa Kilimo hai na hifadhi ya mazingira

   •   Ni kilimo kinachozingatia njia zote za kilimo bora. Mfano kilimo cha makinga maji,
       mazao funika, mseto, mzunguko na kutifua eneo la kupanda tu.

   •   Ni mfumo unaohusisha matumizi ya udongo na mazao kwa utaratibu ambao hupunguza
       mmomonyoko wa udongo mashambani.

   •   Ni mfumo wa ukulima unaowezesha wakulima kupata matokeo bora kutoka kwenye
       rasilimali yoyote wanayoweza kupata.

   •   Kanuni za kilimo hifadhi zinawalenga wakulima wote (mkono, plau au trekta).

   •   Kilimo hifadhi hakihusiani na aina gani ya mazao yanafaa kwa viwango tofauti vya mvua
       au udongo, mbolea kiasi gani itumike kwa mazao haya n.k.

2.3 Kanuni na misingi ya kilimo rafiki wa mazingira
             KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
    MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
Kilimo rafiki wa mazingira ni kilimo kinachozingatia mchanganyiko wa kanuni na misingi
   mbalimbali ya mbinu za kilimo bora. Mfumo huu huzingatia mzunguko wa virutubisho vya
   mimea kwa kufuata kanuni kuu nne ambazo ni:

   1. Jiandae mapema baada ya kuvuna

   2. Kutifua udongo kwa kiwango kidogo au kutotifua kabisa

   3. Kufunika udongo muda wote kutochoma/masalia ya mazao baada ya mavuno

   4. Kilimo cha mzunguko au mbadilishano wa mazao na ya jamii ya mikunde/mazao

   5. Kilimo mchanganyiko na miti/wanyama

2.3.1   Kutifua udongo kwa kiwango kidogo au kutotifua kabisa

        Kutifua ardhi ni pamoja na kufungua, kugeuza, na kuchanganya udongokwa kutumia
        jembe, plau, na vifaa vinavyokokotwa na maksai au trakta. Tunapolima kwa kutifua
        ardhi mara nyingi tunasababisha ardhi kutoa hewa ukaa ambayo mara nyingi huhifadhiwa
        ardhini, vilevile muundo wa udongo ambao hurahisha maji kuingia kwa urahisi kwenye
        udongo huharibika na hivyo kusababisha mmomonyoko wa udongo.

Kulima kwa uangalifu kwa kutifua udongo kwa kiwango kidogo au kutotifua kabisa kunaongeza
uwezo wa ardhi kuhifadhi maji,kuingiza hewa, kurahisisha kutiririka maji, kupata joto na
kuhifadhi hewa ukaa ndani ya udongo.

Hii hufanyika kwa kupanda moja kwa moja kwenye udongo bila kutifua au kuchimba mashimo
(beseni) ya kupandia bila kulima. Kilimo hiki kisichohitaji kutifua ardhi namavuno yake ni
mazuri kabisa.




Faida za kutifua udongo kwa kiwango kidogo au kutotifua kabisa

   1. Kulainisha na kulegeza udongo ili mizizi ya mimea ipenyeze kwa urahisi


             KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
    MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
2. Kuingiza hewa, naitrojeni na oksijeni kutoka angani

3. Kuchangamsha viumbe hai ardhini vifanye kazi

4. Kuongeza uwezo wa maji wa kupenyeza ardhini

5. Kuongeza uwezo wa maji wa kupenyeza ardhini

6. Kupunguza unyaufu wa ardhi

7. Kudhibiti wadudu ardhini na magugu

8. Kusaidia kuchanganya masalia ya mazao pamoja na mbolea ardhini

9. Kutayarisha shamba kwa kuotesha na kusia mbegu

10. Kurekebisha ugumu unaosababishwa na shughuli mbalimbali juu ya ardhi




Mfano wa mfumo wa kilimo cha kutokutifua au kutifua ardhi kidogo tu ( Kilimo
Hifadhi);Zambia, Chololo kondoa.

Ukanda wa Pwani wakulima hufanya yafuatayo;

   • Wanakata uoto katika usawa wa ardhi

   • Kufuata kontua, umbali wa kuotesha mazao udongo unatifuliwa

   • Samadi inawekwa katika mistari iliyolimwa

   • Mazao yanaoteshwa katika mistari hiyo

   • Magugu katikati ya mistari yanakatwa mara kwa mara na ni matandazo

• Mfumo unaweza kutumia mikunde kama zao la kufunika ardhi, kadhalika jimbo hilo
mahindi yanaoteshwa kwenye shamba lenye masalia ya msimu uliotangulia.

   • Mahindi yanaoteshwa ndani ya matandazo
         KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
• Mwezi 1 hadi 2 baadaye maharage yanaoteshwa

    • Mahindi yakishavunwa masalia hutandazwa shambani na maharage huendelea kukua.

    • Maharage hayo huandaa shamba tayari kwa kuotesha zao jingine la mahindi

    • Kwa kutumia mtindo huu mahindi na maharage huvunwa mara mbili kila mwaka na kutoa
    mavuno mazuri.




2.3.2   Kufunika ardhi muda wote

Ili Kuukinga udongo kutokana na jua kali na mvua kubwa unatakiwa kuufunika udongo kwa
kutumia matandazo, kuacha masalia ya mazao au kupanda mazao ya kufunika shambani. Kwa
njia nyingine tunazuia mmomonyoko wa udongo na kuhifadhi unyevu.

2.3.2.1 Matandazo

Kuweka matandazo ni kazi ya kufunika udongo wa juu kwa kutumia magugu, masalia ya mazao
ya kilimo na misitu, majani, matawi, vijiti, na mabua.Matandazo na wakati wa kutandaza
hutegemea mazingira na mbinu za kilimo. Matandazo huongeza kasi ya kazi za viumbe hai ndani
ya ardhi, huboresha udongo ili maji yaweze kunywea ndani, na hupunguza mmomonyoko.
Matandazo yanapooza tunapata mboji inayoshikiza sehemu za udongo vizuri ili zisichukuliwe na
maji. Matandazo hutoa chakula cha wadudu rafiki waishio udongoni.

2.3.2.2 Faida za Matandazo

•   Kuukinga udongo na mmomonyoko wa upepo na maji.

• Kuboresha uwezo wa maji kupenyeza ndani ya udongo, ili kudumisha unyevu na kuzuia
unyaufu

• Kulisha na kulinda viumbe hai ndani ya ardhi

• Kuzuia magugu

             KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
    MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
• Udongo haupati joto kali

• Matandazo ni chanzo cha virutubisho vya mazao

• Kuongeza mboji ardhini

Zingatia:

•   Kila inapowezekana ni vyema kusambaza matandazo shambani kabla au mara tu msimu wa
    mvua unapoanza. Hicho ni kipindi ambapo ardhi huweza kuathirikasana. Inafaa kuwekea
    matandazo miche ya mboga ikishapata nguvu na kujishikiza vizuri na udongo.

•   Kadhalika matandazo yawekwe kwa kiasi kidogo tu hasa pale ambapo mazao hayajaota.
    Kwenye shamba la mazao ya kudumu, matandazo yawekwe mara baada tu ya kutifua ardhi.
    Matandazo huweza kutandazwa katikati ya mazao, kuzungushia mazao ya miti au kwenye
    shamba lote.

•   Endapo matandazo yanachelewa kuoza, kinyesi cha kuku kinatandazwa juu yake

2.3.2.3 Kuacha masalia ya mazao

Njia nyingine ya kufunika udongo ni kutumia masalia ya mazao, hii hufanyika pindi mkulima
anapomaliza kuvuna mazao ya msimu uliopita.Masalia ya mazao kama mahindi, maharage,
mtama, alizeti yakatwe na kulazwa juu ya udongo ili kuzuia Matone ya mvua na jua kupiga
ardhini moja kwa moja.




2.3.3   Mzunguko wa mazao

•   Upandaji wa mazao yanayochangamana vizuri kwenye shamba moja na kufanya mzunguko
    wa mazao msimu hadi msimu. Kuna sababu nyingi za msingi za kufanya kilimo cha
    kubadilisha mazao na yale aina ya mikunde kama vile soya, maharagwe, kunde, choroko,
    mbaazi na mengineyo.


             KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
    MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
•   Kilimo hiki cha kubadilisha mazao na ya jamii ya kunde hupunguza matumizi ya mbolea za
    viwandani mashambani (na hivyo kuokoa matumizi zaidi ya pesa pia!).

•   Mazao aina ya mikunde hurutubisha udongo kwa kutumia hewa ya naitrojeni kutoka angani
    na kuibadilisha na hivyo kufanya mimea mingine isiyo jamii ya kunde ifaidike vile vile.

•   Mbaazi hutumia mizizi yake mirefu kuingia chini kabisa ya ardhi na kuchimbua virutubisho
    aina ya fosforasi, huvileta virutubisho hivyo juu ya ardhi na kufanya mimea yenye mizizi
    yenye kina kifupi itakayopandwa kwenye mbadilishano msimu unaofuata kunufaika nayo.

•   Mazao aina ya kunde yanayokomaa mapema ni chanzo kizuri cha protini kwa familia kwa
    mwezi Februari, wakati ambao unahitaji zaidi kwa uhakika wa chakula kwenye familia.

•   Inawezekana kuvuna mara mbili kwa mazao yanayokomaa mapema katika msimu mmoja.
    Mazao jamii ya mikunde yanapaswa kupandwa angalau theluthi moja ya ukubwa wa shamba
    unalolima katika utaratibu wa kubadilishana mazao kila mwaka.

•   Mimea ya mbolea za kijani inaoteshwa mara baada ya kuvuna zao kuu.

•   Ni vyema kuotesha kwa kukinga mitelemko mikali kupunguza kasi ya maji ya mvua
    inayotelemka milimani. Kwa yale mazao yasiyofunika ardhi mapema inafaa kuotesha zao
    kama alfalfa au maharage yatakayofunika ardhi mapema.

•   Faida yake ni kwamba kilimo hiki hupunguza madhara ya wadudu na magonjwa.

2.3.4   Kilimo cha kuchanganya mazao na miti

    •   Miti kama vile Mkondachao (Faidherbia albida) yaweza kuchukua hewa ya naitrojeni
        iliyoko angani na kuibadilisha kuwa rutuba ifikapo ardhini na kuifanya mimea mingine
        kunufaika nayo.

    •   Unaweza kupanda miti iongezayo rutuba na          mboji kwenye udongo ili kuongeza
        uzalishaji wa mazao. Miti kama mkondachao yaweza kupandwa nafasi ya mita10 kwa10
        na unaweza kupata miti 40 kwa ekari.

             KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
    MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
•    Miti ya mkondachao inayo sifa moja ya pekee; hupukutisha majani yake kipindi cha
        mvua badala ya kipindi cha kiangazi kama inavyofanya miti mingine. Hivyo basi hali
        hiyo inakuwezesha kupanda mazao mbalimbali chini ya mwamvuli wa miti hiyo pasipo
        kuathiri ufanisi wa mazao hayo kwa vile hapawi na kivuli.

2.4 Hatua za kufuata katika kilimo hifadhi

2.4.1   Acha masalia ya mazao shambani- usiyachome

Palizi la magugu la mara kwa mara ni muhimu sana katika Kilimo Hifadhi. Jinsi unavyoacha
masalia mengi shambani ni vizuri zaidi. Masalia unapoyaacha shambani hurutubisha udongo,
yanadhibiti upotevu wa maji ya mvua na yanaruhusu maji kunywea ndani ya udongo. Unapoacha
masalia   shambani    kila   mwaka,   yanaboresha    udongo.   Mchwa   wanayashambulia   na
kuyachanganya na matamahuluku kwenye udongo. Masalia yanavyokua mengi ndivyo mchwa
wanavyoyashambulia na hatimaye hawawezi kushambulia mazao yako shambani.
2.4.2   Andaa mashimo ya kupandia ya kudumu

Wakati unapochimba mashimo ya kupandia badala ya kuutibua udongo husaidia kupunguza
matumizi ya fedha na muda. Mashimo ya kupandia ya kudumu yanavuna maji ya mvua za awali
na hivyo kurahisisha uotaji wa mbegu na kuboresha uchipuaji mzuri wa mazao yako shambani.
2.4.3   Panda mbegu mapema

   •    Anza matayarisho ya shamba mapema mara tu baada ya kumaliza kuvuna, ili uweze
        kusambaza uzito wa kazi zako kwa miezi mingine kabla ya kuanza kwa msimu mwingine
        wa kupanda.
   •    Jinsi unavyowahi kuandaa shamba lako mapema,ndivyo unavyoweza kuwahi kupanda
        mara tu baada ya mvua za kwanza za kupandia kunyesha.
   •    Upandaji mbegu wa mapema ni muhimu kwa sababu mvua hizo za awali husaidia mmea
        katika uotaji wake/upevukaji wake kutokana na naitrojeni inayoachwa na viumbe hai wa
        udongoni.


2.4.4   Wahi kupalilia mara kwa mara msimu wote

             KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
    MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
•    Palizi la mapema na la mara kwa mara katika mwaka mzima ni jambo muhimu sana
        katika Kilimo Hifadhi.
   •    Uotaji wa magugu shambani utakuwa unapungua baada ya muda fulani kutokana na
        palizi la mara kwa mara.
   •    Palizi ni sharti lifanyike ndani ya wiki kati ya nne na sita baada ya mbegu kuota
        shambani wakati magugu yatakuwa yamefikia kimo cha sentimeta 2.5.
   •     Ni muhimu uendelee kufanya palizi hata wakati mazao yanapokuwa yamekomaa hata
        baada ya mavuno, ili kuyadhibiti kabisa magugu yasizalishe mbegu na kuzipukutisha
        shambani, vinginevyo yatakuongezea kazi ya ziada ya palizi kwa mwaka ufuatao.




2.5 Faida ya kilimo hai na hifadhi ya mazingira

       2.5.1   Huhifadhi udongo na kudumisha rutuba ya ardhi

       2.5.2   Hupunguza uchafuzi wa maji kwenye mito, maziwa na chini ya ardhi.

       2.5.3   Hulinda bioanuai.

       2.5.4   Hudumisha aina mbalimbali za uoto wa asili.

       2.5.5   Hutunza vizuri mifugo.

       2.5.6   Matumizi ya malighafi mbadala, na nishati asilia.

       2.5.7   Hakuna masalia mengi ya viuatilifu kwenye vyakula.

       2.5.8   Hakuna vichochezi na madawa katika mazao ya mifugo.

       2.5.9   Mazao ya thamani bora zaidi; (mwonjo na hifadhi).




2.6 Changamoto za kilimo hifadhi na mazingira


             KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
    MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
1. Woga wa wakulima kuhusu kushukuka kwa mavuno kunakosababishwa na mabadiliko
       ya mavuno

   2. Upatikanaji wa aina za mbegu zinazofaa

   3. Gharama za mbegu

   4. Upatikanaji wa maji

   5. Mahitaji ya nguvu kazi

   6. Matumizi ya ziada kutokana na mazao mengine ya pembeni

   7. Uhakika wa chakula

MADA 3: UDONGO

3.1 Udongo ni nini?

Udongo ni tabaka la juu ya ardhi linalosaidia ukuaji wa mimea. Udongo ni mchanganyiko wa
miamba iliyopasuka, madini, maji, hewa, wadudu na wanyama wadogo na wakubwa walio hai
na waliokufa, masalia ya mimea na mboji.

Kuna aina kuu tatu za udongo katika maeneo yetu ambazo ni kichanga, mfinyazi na tifutifu.
Ustawi wa zao fulani hutegemeana na aina ya udongo ulioko katika eneo hilo. Udongo wa aina
ya tifutifu ndio unaofaa zaidi kwa ajili ya kilimo. Udongo wa kichanga hupoteza maji kirahisi na
hivyo haufai kwa kilimo. Hata hivyo udongo wa mfinyanzi hutuwamisha maji na kusababisha
mizizi kushindwa kupumua na kusababisha mimea isiyotaka maji mengi kama mahindi na
maharage kufa.

   •   Udongo ni hitaji muhimu kuliko mengine katika kilimo na mkulima anayo mamlaka
       makubwa juu yake. Udongo una uhai kwa sababu ni makazi ya mimea, wanyama na
       viumbe vingine vyenye mahusiano nao. Udongo una yabisi, mboji na nafasi wazi.

   •   Udongo wenye ujazo wa kijiko cha chai huweza kuwa na mamilioni ya viumbe. Baadhi
       hutokana na mimea na wanyama. Viumbe vingine huonekana kwa macho kama minyoo,
             KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
    MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
buibui, konokono, jongoo na mchwa. Viumbe muhimu sana ardhini ni bakteria, fangi na
       protozoa.

   •   Wakulima wengi wanadhani kuwa viumbe wanaoishi ndani ya ardhi husababisha
       madhara na kufikiria tu namna ya kuwaua. Ukweli ni kwamba ni wadudu wachache sana
       wanaodhuru mazao. Viumbe wengi ndani ya udongo ni wa manufaa makubwa na
       hurutubisha udongo.

3.1 Umuhimu wa viumbe wanaoishi ardhini:-

       • Kuozesha mabaki na kutengeneza mboji.

       • Kuchanganya masalia ya mazao ndani ya sehemu za ardhi na kuimarisha udongo.

       • Kuchimba vinjia na hivyo kurahisisha mizizi kupenya na kuingiza hewa ardhini.

       • Kusaidia upatikanaji wa virutubisho ardhini.

       • Kuzuia wadudu na magonjwa yanayoathiri mizizi ya mimea.

       • Minyoo ni alama ya udongo wenye rutuba, wana kazi nyeti ardhini mfano kuyeyusha
       masalia ya viumbe hai, kusaidia kuchanganya masalia na sehemu za udongo ili
       kuuimarisha

       • Njia wanazozichimba ndani ya ardhi, zinarahisisha kupenyeza hewa na maji, hivyo
       kupunguza mmomonyoko wa udongo na maji kusimama juu ya ardhi.

        • Minyoo wanahitaji masalia hai, joto la kiasi na unyevu wa kutosha. Husitawi vizuri
        ndani ya udongo wenye matandazo. Kilimo cha mara kwa mara na matumizi ya
        viuatilifu huathiri sana idadi ya minyoo ardhini.

3.2 Udongo wenye rutuba unategemea kuwa na vitu vifuatavyo;

   •   Kina cha udongo: Kuwepo kwa ujazo/kina cha udongo wa kutosha unaotumiwa na
       mizizi ya mimea.


            KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
   MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
• Upatikanaji maji: uwepo wa unyevu wa kutosha kwa kipindi kirefu.

• Urahisi wa maji kupita: Uwezo wa kupitisha maji kwa urahisi.

• Hewa: Hewa ya kutosha inahitajika kuwepo kwa afya ya mizizi na maisha hai ya udongo.

• pH Uchachu: Udongo hauna tindikali au chumvi nyingi.

• Madini: upatikanaji wa virutubisho kutoka mwamba asilia, na muundo wa udongo.

• Mboji: Kuwepo kwa kiasi cha kutosha cha mboji inahusiana vizuri na uwezo wa udongo
kushika virutubisho, maji na maisha ya udongo na muundo wa udongo.

• Viumbe hai kwenye udongo:Kuwepo kwa viumbe hai kwenye udongo husaidia upatikanaji
wa virutubisho, kushikilia maji, muundo na afya ya udongo, na kuyeyushwa kwa mboji ardhini.

Endapo udongo utakosa baadhi ya vitu vilivyotajwa hapo juu hali ya udongo haitafaa kwa
ukuaji wa mimea. Mifano ni kutuama maji, uchachu, udongo mgumu na uhaba wa virutubisho,
unaosababisha upungufu mkubwa wa mavuno.



3.3 Mbinu za Kurutubisha udongo

Wakulima wanaweza kuboresha rutuba ya udongo kwa kuzingatia njia zifuatazo:

   1. Kuukinga udongo kutokana na jua kali na mvua kubwa kwa kuufunika na matandazo,
       mbolea ya kijani au mazao ya kufunika. Kwa njia nyingine tunazuia mmomonyoko wa
       udongo na kuhifadhi unyevu.

   2. Kilimo mseto na mzunguko wa kufaa wa mazao ya msimu unadumisha rutuba ya
       udongo.

   3. Tifua udongo ipasavyo ili kudumisha rutuba na ubora wake kwa kuzuia mmomonyoko
       na udongo kugandamana.




             KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
    MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
4. Kuwa na mpangilio mzuri wa virutubisho kwa kutumia mbolea za asili kulingana na
          mahitaji ya mazao kama samadi na mboji

   5. Kuainisha malisho na hifadhi ya viumbe hai walio ardhini, kwa kuongeza masalia ya
          mimea tunawezesha viumbe hai wenye faida kuishi na kufanya kazi.



MADA 4: KUTENGENEZA MBOJI
4.0 Mboji ni nini?
Mboji ni sehemu ya viumbe (mabaki ya mimea na wanyama (matamahuruku)) ambayo
imeozeshwa kwa muda mrefu ili kusazwa na viumbe vidogo vidogo. Sehemu za vitu kama
majani, matunda na mabaki ya mboga hutengeneza mbolea ya mboji. Mboji iliyoiva hubadilika
rangi na kuwa ya hudhurungi, tifutifu na hunukia vizuri. Mboji ni rahisi kutengeneza, gharama
zake ni za chini sana na inafaa mno kuongezwa kwenye udongo ili kuinua mazao ya shamba.


Mboji iliyotunzwa vyema huwa na rutuba nzuri kwa mimea inapotumiwa shambani. Mboji
huchemka hata kiasi cha kuua magonjwa ya mimea na mbegu za magugu.
Majani makavu ya ndizi ni mazuri kwa kutunza vifaa vya mbolea na kuweka ukavu. Hali hii
huwa huzuia kupotea kwa maji kabla ya kujenga lundo la mboji na wakati mbolea inapokuwa
inaiva.

4.1 Vifaa visivyofaa kuwekwa kwenye mboji
   •      Sehemu za mimea ambazo zimenyunyiziwa dawa ya kuwaua wadudu (viuatilifu) na
          magugu.


   •      Vipande vya nyama kwa sababu vinavutia panya na wadudu wengine.
   •      Vifaa vilivyo na ncha kali kama mwiba ambavyo vyaweza kujeruhi mikono na miguu.
   •      Magugu ambayo yanarudiarudia kila mwaka. Magugu kama hayo huuliwa kwa kuanikwa
          kwenye jua kali ili yakauke baadaye huchomwa ili yasienee na jivu lake laweza
          kuongezwa kwenye lundo la mbolea.
   •      Vitu visivyo kua na uhai kama plastiki na chuma.

             KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
    MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
5.2   Vitu ambavyo vyaweza kutumiwa kutengeneza mboji
          5.2.1   Vifaa vya nyumbani
              •   Maganda ya matunda
              •   Jivu la kuni
              •   Taka taka za kufagia
          5.2.2   Shambani

                  •   Mabaki ya mimea baada ya kuvuna, katakat vitu vigumu, kama ni vigumu
                      nyunyizia maji. Vitu vigumu huoza pole pole. Usitumie vile vilivyowekwa
                      dawa juzijuzi
                  •   Majani makavu/ yaliokauka
                  •   Mimea/majani ya kijani au mabichi, kata kata kama ni makubwa. Mimea
                      jamii ya mikunde hupendekezwa
                  •   Magugu, katakata kama ni makubwa. Usitumie mizizi ya magugu ama
                      mbegu za magugu


          5.2.3   Asili
                      •   Samadi kutoka kwa mifugo na mabaki ya mimea ni nzuri sana katika
                          kutengeneza mbolea hai na ina rutuba nzuri sana
                      •   Mkojo, ni vigumu kukusanya mkojo ila hupatikana kwenye zizi la
                          ng’ombe.    Nyunyuzia kwenye biwi/lundo la mbolea kwa kiwango
                          kidogo. Mkojo hufanya mbolea kuoza haraka
                      •   Udongo, tumia udongo kama sentimita 10 kutoka tabaka la juu ya
                          shamba. Hutumika kufunika Biwi/lundo la mbolea.
                      •   Magugu ya baharini (Mwani) Yafaa yakaushwe na hutumiwa na
                          majani yaliyo kauka yana madini muhimu kwa wingi

4.3 Namna ya kutengeneza mboji ya mimea
Kusanya vitu na vifaa vinavyohitajika katika utengenezaji wa mboji ambayo ni;

             KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
    MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
•     Majani mengi mabichi/kijani na makavu. Majani jamii ya mikunde ni mazuri sana kwani
         hutengeneza kirutubishi cha naitrojeni (N) kwa wingi.


   •     Mabua ya mahindi au vitawi vya miti


   •     Udongo wa kawaida wa juu


   •     Mboji ya zamani


   •     Majivu au vumbi la mkaa


   •     Maji




4.3.1    Hatua za kufuata
        1. Chagua sehemu karibu na eneo ambalo mboji itaenda kutumika na ambapo kuna
             hifadhi ya kutosha kukinga dhidi ya upepo, jua na mvua.


        2. Katakata majani yawe madogo madogo ili yaweze kuoza haraka.


        3. Tengeneza msingi kama mita sita (6) urefu na upana wake mita 2 kwa kutumia majani
             magumu kama matawi/vijiti. Hii itahakikisha maji yanatiririka na hewa ina zunguka
             vizuri. Hakikisha kuna nafasi ya kutosha kufanyia kazi kwenye biwi bila kulikanyaga.


        4.   Weka sentimita 10 ya majani ambayo hayaozi haraka kwa mfano mabua vya mahindi
             au mimea mibichi/kijani.


        5. Weka sentimita 10 ya vifaa ambavyo huoza haraka kwa mfano maganda ya mboga na
             matunda.

             KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
    MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
6.   Weka sentimita 2 ya samadi (mbolea-hai ya wanyama), mabaki ya mbolea ya zamani
            kama yaweza kupatikana.


       7.   Weka udongo wa juu sentimita 10 kutoka kwenye shamba ambalo hulimwa.


       8.    Majivu na mkojo vyaweza kunyunyuziwa juu ili kufanya biwi/lundo kuoza haraka.


       9. Nyunyizia maji kwenye biwi mpaka lilowe.


       10. Rudia mpangilio huu kuanzia namba nne (4) mpaka lundo lifike mita moja (1.m) hadi
            moja na nusu (1.5m) kwenda juu isipokuwa vijiti/matawi ya kwanza.




4.3.2 Zingatia
   •    Biwi/lundo cha mboji kinatakiwa kifunukwe ili kupunguza/kuzuia mvuke ama mvua
        nyingi ambayo hubeba rutuba kutoka kwenye mbolea. Weka gunia, nyasi ama matawi ya
        migomba yaliyokauka.


   •    Kila tabaka/kunjo/safu yafaa kupangwa kuanzia kwenye ukingo ili lundo la mbolea
        lisiporomoke.


   •    Namna nyigine ya kuzuia lundo kuporomoka ni kwa kuweka vipande vya mbao kando ya
        biwi. Wavu wa nyuzi za chuma utafanya biwi kukauka.


   •    Katika sehemu zenye ukavu mwingi. Mianzi iliyo na mashimo husaidia kufanya hewa
        kuingia na kuzunguka kwa urahisi




             KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
    MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
4.4 Wadudu wenye manufaa na mazingira yanayohitajika kwenye Biwi
4.4.1 Wadudu ambao husaidia kufanya biwi kuoza
Viumbe wengi wanaohusika na kazi hii ya kuoza ni wadogo hawaonekani kwa macho matupu.
Ila viumbe hawa huhitaji maji, hewa na vipande/sehemu ya viumbe wengine ambazo kwao ni
chakula. Viumbe hawa hula vipande hivyo na hutoa hewa ya carbon dioxide, maji na joto.


4.4.2 Hatua 3 kubwa za biwi kuoza
Kuna hatua tatu kubwa wakati biwi linapooza;
   1. Hatua ya kupanda joto
   2. Hatua ya kupoa/kuwa baridi
   3. Hatua ya kukomaa.


4.4.2.1 Hatua ya kupanda joto
Wakati ya hatua ya kupanda joto, joto hufikia kiwango cha juu sana katikati mwa biwi. Uzuri
wa joto hili ni kwamba magonjwa yaliyokuwa kwenye viungo vya biwi na mbegu za magugu
huchomwa hadi kufa. Maelezo ya msingi kuhusu mboji/mbolea vunde/mbolea hai
uyoga (fungi) huwa na faida nyingi kwa sababu kazi yake ni kuzisaga nyuzi ngumu ambazo
zimo kwenye viungo vya mimea au majani.


4.4.2.2 Hatua ya kukomaa
Kwenye hatua ya tatu, ‘hatua ya kukomaa’ viumbe wakubwa kama mchwa na nyungunyungu
husaidia kusaga na kuchanganya mbolea. Hali ya anga ikiwa na joto jingi viumbe hawa hufanya
kazi haraka kuliko wakati ambapo hali ya anga ni baridi. Aina ya viungo vilivyotumika
kujenga/kukuza biwi na ukali/uchungu (pH) wa udongo pia huathiri kiwango cha mbolea kuoza.


4.4.3 Mazingira yanayohitajika kwenye biwi
Biwi huhitaji vitu vitatu: hewa, maji na joto.
   •   Hewa



             KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
    MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
Viumbe wadogo kwenye biwi huhitaji hewa ili waweze kuishi. Hewa ya carbon dioxide (CO2)
ambayo imetolewa na wadudu hawa huhitaji kutolewa nje. Ikiwa hewa safi itakosekana, viumbe
wengine wasiohitajika huingia na kutoa harufu mbaya na pia kufanya mbolea isioze haraka.
   •   Maji
Kazi ya viumbe wadogo huwa polepole ikiwa biwi ni kavu. Aidha ikiwa biwi litalowa maji basi
viumbe wadogo watakufa na kufanya biwi kuwa na uchachu badala ya kutengeneza mbolea.
Hivyo basi kukagua kiwango halisi cha maji huhitaji ujuzi fulani.
   •   Joto
Biwi hutoa joto wakati linaoza. Lundo likiwa na joto jingi viumbe wadogo hutoka, kisha huweza
kurudi pindi linapopoa. Muhimu kuhakikisha kuwa joto halizidi sana ili kuweza kuwa na mboji
nzuri yenye virutubisho.




4.5 Matunzo ya Biwi
Ili kupata mbolea nzuri, biwi linapojengwa yafaa lishughulikiwe kwa utaratibu. Biwi hilo
litahitaji maji, kupinduliwa, joto na muda unaofaa wa kukomaa.


4.5.1 Maji
   •   Wakati wa kiangazi biwi/lundo la mboji huhitaji kumwagiliwa maji kila wiki. Maji katika
       lundo la mbolea hupimwa kwa kuweka fungu dogo la nyasi na kulitoa baada ya dakika
       tano. Nyasi isipoonyesha majimaji au unyevu itabidi maji yamwagwe kwenye lundo hilo

   •   Kuna njia kadha za kuzuia mvuke kuinuka kutoka kwenye biwi, hali kadhalika kiwango
       cha maji yanayomwagiliwa:
   •    Funika lundo kwa majani ya ndizi ama nyasi.
   •   Funika lundo kwa udongo.
   •   Lundo lisigeuzwegeuzwe
   •   Biwi likilowa maji itabidi kifunuliwe na kuachwa kikauke kwenye jua kabla ya kujengwa
       tena.

             KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
    MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
4.6 Kupindua/kugeuza
   •   Katika muda wa wiki tatu (3) baada ya kujenga/kukuza biwi/lundo ukubwa wake
       utakuwa umepungua sana.
   •   Kupindua biwi uhakikishe ya kwamba majani yaliyo kando yameoza pia hewa safi
       imerejeshwa.
   •   Kupindua biwi huchanganya majani yaliyotengenezwa na kukijenga upya. Majani
       yalivyo kando huwekwa katikati, ikiwa kuna ukavu, maji mengi na majani/viungo vikavu
       huongezwa.
   •   Kupindua kunatikiwa kufanyike kila baada ya wiki tatu.
   •   Hali ya joto na kiwango cha maji yafaa kupimwa siku chache baada ya kupinduliwa.
   •   Kupinduliwa kwa mara ya tatu kutahitajika ikiwa viungo havitakuwa vimeoza kikamilifu.
   •   Mbolea yaweza kutengenezwa bila kupinduliwa ila viungo vilivyo kando havitaoza.
       Mbegu za magugu na viungo na magonjwa ya mimea hayatakufa.
   •   Viungo vilivyobaki hutengwa na kutumiwa kwenye biwi lingine. Japokuwa kugeuza
       hakuna lazima, kunapendekezwa ili kupata mbolea nzuri.



4.6 Muda wa kukomaa na matumizi ya mboji
4.6.1 Muda wa kukomaa
   •   Lundo la mbolea yafaa liachwe likomae baada ya joto kupoa. Mbolea yaweza kutumiwa
       mara tu viungo vya kwanza vinapokosa ama vinapopoteza utambusho, na rangi yake
       ikageuka kuwa nyeusi na harufu ikawa ya kuvutia.


   •   Hata wakati huu mbolea yahitaji kufunikwa ili isilowe kwa maji ya mvua ama kukauka
       kwa ajili ya jua bali ibakie na unyevunyevu. Mboji ikikawia muda mrefu kabla ya
       kutumiwa, hupoteza rotuba na wanyama wadogo huifanya makazi yao.


4.6.2 Matumizi ya mboji



             KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
    MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
•   Umuhimu mkuu wa mboji ni kuongeza mazao ya shamba kwa kusaidia udongo kushikilia
      maji kwa muda mrefu na kufanya udongo kuwa na afya bora. Pia mbolea hufanya
      udongo kushikamana hivyo hupunguza mmomonyoko wa udongo.

  •   Mbolea hutumiwa mara nyingi kwenye shamba lililoko karibu nyumbani na mbali na
      nyumba. Wakati shamba huandaliwa kwa kupanda mbegu, mbolea huchanganywa
      kwenye udongo wa juu. Mbolea haifai kuwekwa ndani ya udongo kiasi cha kwamba
      mizizi ya mimea haitaifikia.

  •   Njia bora ni kuweka mbolea kidogo kwenye shimo ambamo mmea utapandwa. Kwenye
      sehemu za ukame, mitaro huchimbwa kisha mbolea ikawekwa ambamo maji
      hukusanyika na kutumiwa na mimea.

  •   Hupunguza magonjwa na wadudu waharibifu wa mimea yalioko udongoni hivyo basi
      mimea huwa na nguvu, afya na hustahimili magonjwa na wadudu waharibifu.

  •   Mbolea vunde pia yaweza kutumiwa ili kufunika udongo usipoteze maji mengi. Mbolea
      ambayo haiko tayari hasa kutumika kwa kazi kama hii iwekwe udongoni ili iendelee
      kuoza na kuchanganyika kwenye udongo. Mbolea inapotumika kwa kuzuia maji kwenye
      udongo, yafaa ifunikwe kwa majani madogo (matandazo). Hii itazuia mbolea isipoteze
      rotuba kwa sababu ya joto jingi na miale ya jua.

  •   Mboji pia hutumika kukuza miche na hata kwa kuwalisha samaki.




MADA 5: HIFADHI YA MAJI

  •   Uhaba wa maji kwenye shughuli za kilimo katika nchi za tropiki ni jambo la kawaida.
      Zipo sehemu ambazo ni budi kumwagilia ili mavuno yaweze kupatikana. Hata katika
      maeneo yale yanayopata kiasi kikubwa cha mvua, mazao yanapungukiwa maji kipindi
      cha kiangazi.



            KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
   MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
•   Kilimo hai kinalenga kutumia kwa uendelevu rasilimali za asili zinazopatikana
    mashambani. Kupatikana, kuvuna, na kuhifadhi maji ni mada muhimu kwa wale
    wanaohimiza Kilimo hai na hifadhi ya mazingira.

•   Kwenye mfumo wa kilimo cha kawaida tunatumia huduma za umwagiliaji kukabiliana na
    upungufu wa maji. Kwa Kilimo hai na hifadhi ya mazingira mkulima anaweka
    kipaumbele upatikanaji na upenyezaji maji ndani ya ardhi.

5.1 Uhifadhi wa maji ardhini

•   Kipindi cha kiangazi kuna aina za udongo zinazoweza na zisizoweza kuipatia mimea
    maji.

•   Udongo mfinyanzi unaweza kuhifadhi maji mara tatu zaidi ya kile kiasi
    kinachohifadhiwa na udongo kichanga.

•   Kazi ya kuhifadhi maji ardhini inapunguza gharama za kumwagilia.

5.2 Namna ya kuhifadhi maji ardhini

•   Wakati wa kiangazi mazao yanategemea unyevu kutoka ardhini. Uwezo wa udongo wa
    kunyonya maji hutegemea mpangilio wa sehemu za udongo na kiasi cha mboji kilicho
    ndani yake.

•   Mboji kama spongi ni ghala ya maji. Udongo wenye mboji, unaweza kuhifadhi maji kwa
    muda mrefu zaidi. Tunaweza kuongeza mboji mashambani kwa njia za samadi,mbolea
    vunde, matandazo, na mbolea za majani.

•   Matandazo yanapunguza unyaufu wa maji ardhini. Huuwekea udongo kivuli kutokana na
    jua pamoja na kulinda ardhi isipate mno joto.

•   Kulima kijuu juu au kuparua huzuia kukauka kwa udongo wa chini.

•   Kuondoa magugu kunapunguza maji yanayopotea kupitia majani ya mimea hiyo.


         KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
5.3 Kuvuna maji

•   Wakati wa mvua kubwa, kiasi kidogo sana cha maji kinanywea ardhini. Sehemu kubwa
    ya maji huwa inatiririka kama mkondo na huenda mbali bila kutumiwa na mimea.

•   Ili kuvuna kiasi kikubwa cha maji ya mvua na kuyaingiza ardhini, hatuna budi kuongeza
    uwezo wa udongo wa kunyonya maji. Udongo wa juu unapaswa kuwa na mpangilio
    mzuri na nafasi wazi (pores and cavities) zinazosababishwa na minyoo.

•   Mazao ya kufunika ardhi pamoja na matandazo huboresha mpangilio wa sehemu za
    udongo. Tena hupunguza kasi ya mtiririko wa maji juu ya ardhi na kuyafanya yanywee
    ndani yake.

•   Kwenye mitelemko matuta ya kukinga maji, yanayasaidia yanywee ardhini hasa mitaro
    inayotuamisha maji.

•   Visahani vya kuzungukia miti hufanya kazi hiyo hiyo.

•   Kwenye mashamba ya tambarare tunaweka mazao ndani ya mashimo (planting pits).

•   Mitego hii ya maji inapofunikwa na matandazo inaleta faida kubwa. Ziada ya maji
    kipindi cha mvua huweza kutumika wakati wa kiangazi.

•   Njia nyingi za kuhifadhi maji zinahitaji nguvu kazi na gharama kubwa.
    Tunapohifadhi maji ndani ya bwawa,tunaweza kufuga samaki ingawa maji huzama
    ardhini au kunyauka kuelekea angani kama mvuke.

•   Vile vile tunaweza kutengeneza matangi ya kuhifadhi maji. Ni vyema kupima na kuamua
    endapo tunahitaji kutengeneza chombo cha kuhifadhi maji kwa kulinganisha matumizi,
    mapato, na/au kupunguza eneo la kilimo ili kuweka hiyo huduma ya kuhifadhia maji.




         KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
MADA 6: DHANA YA VIKUNDI

6.0 UUNDAJI WA KIKUNDI

6.1 KIKUNDI NI NINI?

        •   Ni idadi maalumu ya watu waliokubaliana/waliungana wenye lengo na nia ya
            kukusanya nguvu, rasiliamali, na mawazo yao ili kutatua changamoto
            zinazowakabili katika mazingira yao.
        •   Ni watu kadhaa walioungana pamoja kufikia lengo maalumu la pamoja la
            maendeleo ya kiuchumi,kijamii na kisiasa.
        •   Ni idadi ya watu wenye nia,mwelekeo na lengo moja kufanya shughuli fulani ya
            kijamii na kiuchumi.


6.2 UMUHIMU WA KIKUNDI
            KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
   MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
Kikundi huwaunganisha wakulima na:
   •   Masoko
   •   Asasi za kifedha
   •   Watoa huduma za kilimo
   •   Kuwa na uwezo wa kupanga bei za mazao yao
   •   Kuwa na sauti ya pamoja
   •   Kufanya kazi kwa juhudi(kazi kubwa bila maumivu)
   •   Kufanya kazi kwa kushirikiana
   •   Kuwa na vikao vya mara kwa mara


6.3 AINA ZA VIKUNDI
Kuna aina kuu mbili za vikundi
                  •   Vikundi vyenye malengo ya kiuchumi (ujasiliamali)
                  •   Vikundi vyenye malengo ya kijamii(utoaji wa huduma)eg UKIMWI


6.4 TOFAUTI KATI YA KIKUNDI NA MKUSANYIKO


       KIKUNDI                                     MKUSANYIKO
           → Sifa maalumu huwekwa           hakuna sifa maalumu.
           → Idadi maalumu ya watu          hakuna idadi maalum ya watu
           → Kuna uongozi                   hakuna uongozi
           → Mipango endelevu               hakuna mipango
           → Sheria +taratibu               hakuna sheria/taratibu
           → Mda maalum                     hakuna mda maalumu
           → Utunzaji wa kumbukumbu         hakuna taarifa inawekwa
       Ni bora mbaki 10 wenye msimamo kuliko 30 wasiofuta taratibu za kikundi.


6.5 SIFA KUU ZA WANAKIKUNDI
       •   Kufahamiana(historia ya kazi, ukweli, utendaji)
             KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
    MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
•     Kupendana(kutakiana maendeleo)
      •     Kushibana(utayali wa kusaidiana)
      •     Kuaminiana(kutokuwa tayari kuangusha wenzio)
      •     UMOJA
      •     Mkulima ,mwenye mashamba anayoyalima karibia kila msimu(wenye mafanikio na
            wa ngazi ya chini)
      •     Wanao kubalika na wana kijiji wenzake
      •     Angalau wajue kusoma na kuandika
      •     Wanao ruhusu wenzake kujifunza kutoka kwake
      •     Jinsia zote ziwepo(ke na me)
      •     Awe tayari kujifunza na kupokea ushauri
      •     Upatikanaji wao uwe wa uhakika
      •     Kuanzia miaka 18 mpaka 45
      •     Mkazi wa mda mrefu kitongojini na kjijini kwa ujumla
      •     Awe tayari kufanya alichoona na kufundisha wengine
      •     Awe tayari kutumia sehemu ya shamba lake kufundishwa na kufundishia wengine
            siku zijazo
      •     Wawe tayari kufanya shughuli za kikundi bila kutegemea
       posho/malipo ya Fedha.
      •     Wawe na ari ya kujiendeleza kwa kufuata mbinu walizojifunza.
      •     Wawe tayari kufanya kazi kwa pamoja kwenye kikundi
      •     Wanaopendana na kujaliana.


Zingatia:

Watakao chaguliwa wana jukumu la kubadili mfumo wa ulimaji/kilimo hapo kitongojini baada
ya kujifunza KILIMO HIFADHI, HIVYO WASIANGUSHE MRADI NA KIJIJI .



6.6 JINSI YA KUANZISHA VIKUNDI
             KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
    MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
6.6.1 VIKUNDI VINAANZAJE?
Uzoefu unaonyesha vikundi vinaweza kuanzishwa kwa njia tofauti
           i.    Semina,warsha na ziara za mafunzo ya kubadilishana uzoefu na ujuzi maeneo
                 mengine.
          ii.    Mashirika,wanasiasa, kwa kutaka kufanikisha mipango maalumu huanzisha
                 vikundi ili kurahisisha utekelezaji.
          iii.   Vikundi vinaweza kuundwa kutokana na tatizo au hitaji maalumu la wenyeji.
          iv.    Kikundi kinaweza kuzaliwa kutokana na wazo la mtu mmoja.


6.6.2 MAMBO/VIGEZO VYA KUZINGATIA KABLA YA UUNDAJI KIKUNDI IMARA.
   •     Kuwepo na sababu/lengo la kuanzisha kukundi
   •     Kuwepo na matokeo yatakayowanufaisha au kuwavutia
   •     Kuwe na haja mfano elimu, soko au mtaji
   •     Kuwe na kazi
   •     Wanachama wote wawe na nia/lengo moja
   •     Wanakikundi wawe ni watu wa tabia,tatizo,shughuli,mtizamo mmoja
   •     Wanachama lazima wawe wakazi wa eneo husika.
   •     Viongozi wasitoke kwenye familia moja.
   •     Wanachama wote wawe na mtazamo chanya juu ya kikundi
   •     Idadi ya wanakikundi isiwe kubwa wala kidogo sana.Mtu asilazimishwe kuingia kwenye
         kikundi na awe huru kutoka(muungano uwe wa hiari)
   •     Kikundi kiwe na uhuru na kuamua mambo yake (kisijihisi ni cha mradi au mradi au
         mtaalamu,kitalemaa kimawazo)


6.6.3 JINSI YA KUANZISHA KIKUNDI
  i.     Hakikisha msukumo wa kuanzisha kikundi unatoka ndani ya wahusika ,wazo laweza
         toka nje.
 ii.     Kikundi kiwe na watu wachache (20-30)_Hurahisisha kufahamiana na kuaminiana.

                KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
       MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
iii.     Hakikisha utengenezaji wa malengo,katiba,kanuni,jina la kikundi unahusisha walengwa.
 iv.     Pendekeza viongozi wa vikundi watakavyo patikana(m/kiti,msaidizi na katibu)
         mwanachama aelewe sifa za kiongozi bora.
 v.      Tengeneza katiba kulingana na malengo ya kikundi.
 vi.     Kuwe na sheria na kanuni za kikundi na kila mwanakikundi awe anazijua ili akikiuka
         aonywe(kuhudhuria vikao,kutoa mchango,kusaidiana katika matatizo)
vii.     Tengeneza katiba ya kikundi.siku nzuri/huru kwa wote kuhudhuria.

6.7 KAZI ZA KIKUNDI

  I.     KUPANGA NA KUWEKA MALENGO
         Hii ni kazi ya wanakikundi wote
         Inabidi ifanyike mara kwa mara
         Uzoefu wa wanakikundi wa mazingira yao uzingatiwe


 II.     KUTATUA TOFAUTI ZA MAWAZO
           Kila penye watu wengi pana mawazo mengi yanayotofautiana
           Ni vipi kutofautiana bila uhasama
           Ni vipi kufika muafaka
           Ni vipi mawazo tofauti yanaweza leta umoja


III.     KUTAFUTA VITENDEA KAZI
            Ili kufanikisha malengo vinahitajika
            Fedha
            Utaalamu/Ushauri
            Nguvu za mikono
            Pembejeo
            Huduma nyingine(usafiri)


IV.      MATUMIZI BORA YA VIFAA VYA KAZI


                KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
       MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
Vitendea kazi vizuri vikipatikana muhimu vitumike ipasavyo ili kufikia malengo ya kikundi. Iwe
majengo, pembejeo, duka, nguvu za watu n.k.
Lazima ziratibiwe vizuri,kuwe na kumbukumbu nzuri na uwasilishaji wa mahesabu.


 V.     KUTOA HUDUMA KWA WANAKIKUNDI
Mradi na viongozi inabidi kutoa huduma               fulani fulani kwa wanakikundi; Kutafuta
ushauri,masoko,mikopo,pembejeo n.k. Kikundi kisipotoa huduma hizo wengine hawatapata
hamasa ya kujiunga kwenye kikundi.


VI.     KUTETEA HAKI ZA WANAKIKUNDI
Jukumu mojawapo la kikundi ni kujenga uwezo na kujiamini kwa wanakikundi ili waweze
kutetea maslahi yao pale inapobidi. Ili kuleta mafanikio kikundini mara nyingine inabidi
kupingana na sera za watu/makundi mengine




6.8 UONGOZI

6.10.1 Kiongozi ni nani?
Kiongozi ni mtu/mwanakikundi
   -    Anayechaguliwa na wenzake
   -    Ndiye msimamizi wa sheria na taratibu za kikundi na kuhakikisha kwamba rasilimali zao
        ziko salama na lengo la kikundi linafikiwa
   -    Uongozi una jukumu la kutufikisha pale tulipokubaliana tufike.


6.10.2 Sifa za kiongozi
   -    Mwajibikaji – Awe na uwezo wa kuwatumikia watu wengine kadri ya mahitaji yao
   -    Muwazi – Wambie watu ukweli hata kama unauma
   -    Mkweli – usiwaahidi watu uongo


               KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
      MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
i. Mwenyekiti
  -    Kazi zake ( Ndiye msimamizi mkuu wa shughuli zote za kikundi)
  -    Sifa (awe mpigania haki za watu wengine na asiwe mwepesi kudhurumu haki za
           Watu.


  ii. Katibu
  -    Kazi zake (kutunza kumbukumbu)
  -    Sifa (ajue kuandika vizuri na haraka)


  iii. Mweka hazina
      Taratibu zifuatwe msisubiri kumlaani mtu leo na mbinguni


6.10.3 JE WEWE NI KIONGOZI??
       K---- Kubali kushauriwa
       I---- Ielewe hali ya mahali ulipo
       O----Ondoa upendeleo
       N----Nena kauli thabiti na zinazotekelezeka
       G----Gawa Majukumu
       O----Onesha mifano kwa matendo(onesha njia)
       Z---- Zuia mipasuko na Migawanyiko.
       I---- Inua kiwango cha utendaji wa majukumu(inua unaowaongoza)



6.10.4 UCHAGUZI

  -    Viongozi wa kikundi watachaguliwa kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na
       kikundi. Katiba ieleze waziwazi ni uongozi wa kikundi utafanyika.
  -    Wanakikundi wapendekeze ni aina gani ya uchaguzi utafanyika ili kuwapata viongozi
       wao kwa mfano Kura – siri, kupendekezwa, kuteuliwa
       Wanakikundi wachague mfumo wa kuchagua

            KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
   MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
6.10.5 KATIBA (roho ya kikundi)
Kila kikundi kinatakiwa kutengeneza katiba yake itakayowaongoza katika utekelezaji wa
shughuli zao za kila siku. Katiba ni muongozo wa kimsingi ambao haki, majukumu na wajibu wa
wanachama hulindwa na kuhifadhi.


  6.10.5.1     Wajibu/Umuhimu wa Katiba katika kikundi
             1. Inahamasisha usawa miongoni mwa wanakikundi
             2. Huelekeza umuhimu, majukumu na wajibu wa vyombo vyote
             3. Hulinda shughuli za kila siku na shughuli za kikundi pia husema nini kifanyike na
                nini kisifanyike
             4. Hufafanua malengo ya kikundi
             5. Huongeza uwajibikaji wa uwazi
             6. Huhamasisha ushirikiano kwa wanachama wote kwa kuwa huelezea kwa wajibu
                na majukumu ya kila mwanachama na viongozi
             7. Husaidia kupunguza kutoelewana/ugomvi kwa kuweka njia ya kutatua
   6.10.5.2 Njia za kuandaa rasimu ya katiba
             Uundaji wa katiba hufanywa tofauti kwa kila kikundi, baadhi yao husaidiwa na
             mwanasheria kwa gharama za wanakikundi na nyingine hufanywa na wanakikundi
             (kamati) iliyoidhinishwa na mkutano mkuu. Kamati hii huitajika kuundwa na watu
             wenye uelewa wa masuala ya kisheria. Baada ya kamati kumaliza kuandaa rasimu
             ya katiba, wanachama hujadili katika mkutano mkuu na kuifanyia marekebisho.
             Baada ya ushauri wa wadau kujumuisha , toleo la mwisho huandaliwa na
             kudhibitishwa na mkutano mkuu.


   6.10.5.3 Kanuni za katiba bora


             a) Ushirikishwaji
             b) Isiyopendelea
             c) Isiyobadilika
             KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
    MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
d) Rahisi
      e) Imara




         KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA
MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)

More Related Content

More from Climate Change Agriculture and Poverty Alleviation in Tanzania

More from Climate Change Agriculture and Poverty Alleviation in Tanzania (13)

District budget analysis study report final
District budget analysis study report finalDistrict budget analysis study report final
District budget analysis study report final
 
Tor for assessing impact of radio programmes
Tor for assessing impact of radio programmesTor for assessing impact of radio programmes
Tor for assessing impact of radio programmes
 
Final report dadp study mjumita consultancy- stephen nyagonde 2013
Final report dadp study  mjumita consultancy- stephen nyagonde 2013Final report dadp study  mjumita consultancy- stephen nyagonde 2013
Final report dadp study mjumita consultancy- stephen nyagonde 2013
 
Policy Analysis in relation to climate change adaptation, mitigation, agricul...
Policy Analysis in relation to climate change adaptation, mitigation, agricul...Policy Analysis in relation to climate change adaptation, mitigation, agricul...
Policy Analysis in relation to climate change adaptation, mitigation, agricul...
 
DADP ANALYSIS REPORT 2013
DADP ANALYSIS REPORT 2013DADP ANALYSIS REPORT 2013
DADP ANALYSIS REPORT 2013
 
Documentation of lessons and the best practice for csa
Documentation of lessons and the best practice for csaDocumentation of lessons and the best practice for csa
Documentation of lessons and the best practice for csa
 
CSA SOURCEBOOK - FAO
CSA SOURCEBOOK - FAOCSA SOURCEBOOK - FAO
CSA SOURCEBOOK - FAO
 
Demand and Supply Challenges in Sub-Saharan Africa
Demand and Supply Challenges in Sub-Saharan AfricaDemand and Supply Challenges in Sub-Saharan Africa
Demand and Supply Challenges in Sub-Saharan Africa
 
ToR for policy review for CCAP
ToR for policy review for CCAPToR for policy review for CCAP
ToR for policy review for CCAP
 
ToR for DADP recommendations
ToR for DADP recommendationsToR for DADP recommendations
ToR for DADP recommendations
 
Baseline survey report 2013 final
Baseline survey report 2013 finalBaseline survey report 2013 final
Baseline survey report 2013 final
 
CCAP in Tanzania
CCAP in TanzaniaCCAP in Tanzania
CCAP in Tanzania
 
Ccap leaflet brochure
Ccap leaflet brochureCcap leaflet brochure
Ccap leaflet brochure
 

Manual for climate smart agricultural training

  • 1. UTANGULIZI Mwongozo huu umeandaliwa kwa ajili ya wakufunzi ambao wanataka kuendesha mafunzo shirikishi ya kilimo hifadhi ya mazingira katika ngazi ya vijiji, pia kimeandaliwa kwa namna ambayo matumizi bora ya ardhi na rasilimali za misitu yatazingatiwa. Mafunzo haya yatatolewa kwa wakulima wadogo wadogo walioko kwenye eneo la Mradi hasa wale waliojiunga kwenye vikundi vya shamba darasa na wadau mbalimbali wanaonufaika kwa namna moja au nyingine na Mradi wa CCAP. Mafunzo haya yataongeza uelewa wa wakulima kuhusu kilimo hifadhi na yatawawezesha wananchi kutekeleza kwa vitendo zana nzima ya kilimo hifadhi kwenye mashamba yao. Shughuli hii inatekelezwa chini ya Mradi wa Mabadiliko ya Tabia nchi, kilimo na kupunguza umasikini ( CCAP) ambao unatekelezwa kwa ushirikiano wa mashirika matano ambayo ni MJUMITA, MVIWATA, TFCG, Action Aid na TOAM. Mradi huu una lengo la kupunguza umasikini miongoni mwa wakulima wadogo wadogo wanaolima mashamba yenye ukubwa wa hekta 2 Tanzania na kuwajengea uwezo wa kukabiliana na kuhimili mabadiliko ya tabianchi ikiwa ni pamoja na kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa kwa kuboresha njia za kilimo. MPANGILIO WA MUONGOZO WA MAFUNZO Muongozo huu umegawanyika katika sehemu kuu nne, nazo ni:- 1. Utangulizi 2. Mabadiliko ya tabia nchi Baada ya mafunzo, washiriki watakuwa wameweza kuelezea yafuatayo;- o Mabadiliko ya tabianchi yanamaanisha nini o Mabadiliko ya tabianchi yanatokeaje o Ushahidi wa mabadiliko ya tabia nchi o Sababu za mabadiliko ya tabia nchia o Athari zake 3. Kilimo rafiki wa mazingira kwa chakula na kipato Baada ya mafunzo, washiriki watakuwa na uwezo wa kuelewa:- KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 2. o Maana ya kilimo rafiki wa mazingira o Umuhimu wa kilimo rafiki wa mazingira o Kanuni za kilimo rafiki wa mazingira o Mbinu/hatua za kufuata katika kilimo rafiki wa mazingira o Faida ya kilimo rafiki wa mazingira o Changamoto 4. Udongo Baada ya mafunzo washiriki watakuwa wamefahamu • Maana ya udongo • Umuhimu wa viumbe wanaoishi ardhini • Udongo wenye rutuba ukoje • Mbinu za kurutubisha udongo 5. Utengenezaji wa mboji Baada ya mafunzo washiriki watakuwa wamefahamu • Maana na umuhimu wa mboji • Vifaa visivyofaa kutumiwa wakati wa kutengeneza mboji • Vitu vinavyofaa kutumiwa wakati wa kutengeneza mboji • Namna ya kutengeneza mboji • Wadudu wenye manufaa na mazingira yafaayo kwa utengenezaji wa mboji • Muda wa kukomaa na matumizi ya mboji 6. Hifadhi ya maji Baada ya mafunzo washiriki watakuwa wanaelewa:- • Umuhimu wa maji • Namna ya kuhifadhi maji ardhini • Kuvuna maji 7. Kuundwa kwa Vikundi vya shamba darasa • Maana na umuhimu wa kikundi • Kutofautisha kati ya kikundi na mkusanyiko • Mambo ya kuzingatia wakati wa kuunda kikundi kilicho imara KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 3. Kazi za kikundi • Umuhimu wa kuwa na uongozi wa kikundi na sifa za uongozi • Jinsi ya kuandaa rasimu ya katiba ya kikundi • Kanuni za katiba bora • Zana ya mtandao • Namna ya kuwaunganisha wanakikundi na mitandao ya MJUMITA na MVIWATA MADA 1: MABADILIKO YA TABIANCHI 1.1 Mabadiliko ya tabia nchi yanamaanisha nini? Tabia nchi kwa kawaida hufafanuliwa kama wastani wa hali ya hewa, hivyo tabia nchi na hali ya hewa huingiliana japo ni vitu tofauti. Mabadiliko ya tabia nchi ni mabadiliko ya muda mrefu ambayo yametokea katika maeneo mbalimbali ya dunia. Mabadiliko haya huweza kupimwa kwa kuzingatia hali ya hewa kama vile kiwango cha joto na baridi, mvua na ukame. 1.2 Mabadiliko ya Tabia nchi yanatokeaje? Mabadiliko ya tabia nchi hutokea wakati ambapo hali ya hewa katika eneo fulani hubadilika katika kipindi cha muda fulani (mfano baada ya miaka 10). Mabadiliko hayo hutokea wakati miale ya jua inapokuja moja kwa moja duniani. Mabadiliko ya tabia nchi ni tishio kwa maendeleo kwa sababu huathiri afya zetu, makazi, miundo mbinu, kilimo na mfumo wa ekolojia. Pamoja na hayo, mabadiliko ya tabia nchi husababisha kutetereka kwa hali ya maisha katika maeneo mbalimbali ya dunia. 1.3 Ushahidi wa mabadiliko ya tabia nchi. Ushahidi wa mabadiliko ya tabia nchi ni kuwepo kwa mafuriko na ukame katika maeneo mbalimbali nchini na dunia nzima. Kwa upande wa Tanzania tumeshuhudia mafuriko hayo wilayani Kilosa na ukame Mkoani Manyara. KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 4. 1.3.1 Milipuko ya magonjwa Ugonjwa kama malaria umejitokeza katika maeneo ambayo hapo awali haukuwepo. Katika mkoa wa Njombe ambao uko nyanda za juu kwenye baridi, ugonjwa wa malaria haukua tatizo katika wilaya za Njombe na Mafinga. Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, joto limeongezeka na kusababisha kuwepo na makazi ya mbu wanaosababisha malaria katika maeneo hayo. 1.3.2 Ukame Kutokana na ukame unaosababishwa na mvua zisizokuwa na mpangilio, imepelekea kupungua kwa mavuno. Mvua zisizoaminika ni mojawapo ya madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi. Haya yote yamepelekea watu wengi duniani kukosa chakula na hatimaye wengine kufariki kwa sababu ya njaa. Kuyeyuka kwa barafu katika vilele vya milima (mfano Mlima Kilimanjaro) Kuyeyuka kwa barafu katika vilele vya milima ni kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha joto. Kiwango cha joto kinaongezeka kutokana na kuharibika kwa tabaka la ozone lililopo angani ambalo kazi yake ni kupunguza miale ya jua inayokuja duniani. 80% yatheluji ya mlima Kilimanjaro , ambao ni mlima mrefu zaidi katika bara la afrika imetoweka kwa kipindi cha tokea mwaka 1912. 1.3.3 Kuongezeka kwa kina cha bahari Kuongezeka kwa kina cha bahari ni ushahidi wa kuwepo kwa mabadiliko ya tabia nchi. Hivi leo kuna pwani au fukwe za bahari ambazo zimeanza kutoweka kutokana na kuongezeka kwa kina cha bahari. Haya yote ni matokeo ya mabadiliko ya tabia nchi. 1.4 SABABU ZA MABADILIKO YA TABIA NCHI KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 5. Mabadiliko ya tabia nchi yamesababishwa na vitu ama vitendo mbalimbali ambavyo vimechangia kwa sehemu kubwa uharibifu wa mazingira. Vitendo vilivyochangia uharibufu wa mazingira na kusababisha mabadiliko ya tabia nchi ni pamoja na:- 1.4.1 Kilimo cha Kuhamahama Mabadiliko ya tabia nchi kwa namna moja au nyingine yanasababishwa na kilimo cha kuhama hama. Wakulima wadogo wadogo walio wengi Tanzania wanalima kilimo cha kuhama hama ambapo shughuli hiyo hupelekea kufyekwa kwa misitu mingi katika maeneo ambayo mashamba mapya hufunguliwa. Katika shughuli hii, miti na uoto wote uliopo juu ya uso wa ardhi unaosaidia kufyonza hewa ukaa huaribiwa. Hewa hii hukusanyika angani na kuharibu tabaka la ozone na kusababisha ongezeko la joto duniani na hivyo kutokea mabadiliko ya tabia nchi 1.4.2 Uchomaji moto wa mabaki ya mazao shambani Shughuli za uchomaji moto mabaki ya mazao shambani huambatana na moshi unaokusanyika angani na kuchangia kuharibika kwa tabaka la ozoni na kusababisha mabadiliko ya tabia nchi. 1.4.3 Moshi kutoka viwandani na kwenye magari Leo hii kuna idadi kubwa sana ya viwanda na magari duniani kote ukilinganisha na miaka ya nyuma. Moshi kutoka viwandani na kwenye magari unachangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la mabadiliko ya tabia nchi. Moshi huu huharibu tabaka la ozone angani ambalo kazi yake ni kupunguza ukali wa miale ya jua ifikayo duniani na hivyo husababisha ongezeko la joto duniani. 1.4.4 Uchomaji mkaa usio endelevu Uchomaji mkaa ni mojawapo ya shughuli zinazofanywa na mwanadamu ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa katika mabadiliko ya tabia nchi. Uchomaji wa mkaa huambatana na ukataji wa miti na uchomaji wa magogo. Shughuli hii huharibu tabaka la ozone na hivyo kuongezeka kwa kiwango cha joto duniani. KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 6. Mchoro 1: Uandaaji wa tanuru Mchoro 2: Utengenezaji wa mkaa kwa ajili ya mkaa husababisha hewa ya ukaa 1.4.5 Ukataji miti hovyo Mchoro 3: Ukataji wa miti kwa matumizi ya kuni Mchoro 4: Ukataji wa miti kwa ajili ya kujengea Kwa kawaida miti hufyonza hewa ukaa. Kwa maana hiyo, miti ikikatwa hovyo hewa ukaa haitafyonzwa tena badala yake itaenda kuharibu tabaka la ozone lililoko angani ambalo kazi yake ni kupunguza ukali wa miale ya jua. Baada ya uharibifu huo kiwango cha joto duniani KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 7. huongezeka kwa kiasi kikubwa na hivyo kusababisha madhara mengi kama vile ukame na ukosefu wa mvua. 1.4.6 Uchomaji wa misitu Uchomaji wa misitu unaosababishwa na shughuli mbalimbali kama vile urinaji wa asali, uwindaji wa wanyama na uchomaji misitu kwa imani potofu, huchangia kuongezeka kwa hewa ukaa angani ambayo huadhiri tabaka la ozoni na kusababisha ongezeko la joto duniani. Mfano: Katika maeneo mengi Tanzania watu wanaamini kwamba wakichoma moto na kusafiri umbali mrefu aliyechoma moto ataishi muda mrefu. 1.4.7 Uchimbaji wa madini. Uchimbaji wa madini ni shughuli inayoambata na kubadili maeneo ya misitu kuwa katika matumizi mengine. Katika shughuli hii, miti na uoto wote uliopo juu ya uso wa ardhi unaosaidia kufyonza hewa ukaa huaribiwa. Hewa hii hukusanyika angani na kuharibu tabaka la ozone na kusababisha ongezeko la joto duniani na hivyo kutokea mabadiliko ya tabia nchi. 1.4.8 Ufugaji wa mifugo Mifugo mingi ikifugwa katika eneo dogo la malisho huharibu uoto wa asili ikiwa ni pamoja na nyasi, vichaka na miti michanga ambayo ingesaidia kunyonya hewa ukaa MADA 2: KILIMO RAFIKI WA MAZINGIRA KWA CHAKULA NA KIPATO 2.1 Maana ya Kilimo rafiki na mazingira/kilimo endelevu. • Mfumo huu ni ule unaotumia mbinu mbalimbali zinazoendelea kulinda afya ya udongo, maslahi ya kimazingira, wanyama na binadamu. • Kilimo hai na hifadhi ya mazingira kinatuwezesha kuzalisha chakula salama bila kuathiri matumizi ya ardhi kwa vizazi vilivyopo na vijavyo . KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 8. Kilimo hiki kinahimiza uzalishaji wa mazao kwa kutumia samadi na mboji na udhibiti wa wadudu na magonjwa kwa kutumia njia za asili. • Kilimo hiki hakitumiii madawa na mbolea toka viwandani au hutumika kwa kiwango kidogo sana pale inapohitajika na kinapinga matumizi ya viwatilifu vyenye sumu na mbegu zenye vinasaba na shughuli zozote zinazopelekea uharibifu wa udongo , maji na maliasili zinginezo. Inadaiwa kuwa Kilimo hai na hifadhi ya mazingira ni jibu la matatizo yanayoathiri mazingira kutokana na uendelevu kiuchumi, rafiki katika matumizi ya malighafi na hifadhi ya mazingira na rasilimali, chenye kukubalika katika jamii, na kumudu ushindani wa kibiashara. Mafunzo haya yatajikita zaidi katika kuelezea mfumo wa kilimo hai na hifadhi ya mazingira kama njia itakayowawezesha wananchi kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. 2.2 Umuhimu wa Kilimo hai na hifadhi ya mazingira • Ni kilimo kinachozingatia njia zote za kilimo bora. Mfano kilimo cha makinga maji, mazao funika, mseto, mzunguko na kutifua eneo la kupanda tu. • Ni mfumo unaohusisha matumizi ya udongo na mazao kwa utaratibu ambao hupunguza mmomonyoko wa udongo mashambani. • Ni mfumo wa ukulima unaowezesha wakulima kupata matokeo bora kutoka kwenye rasilimali yoyote wanayoweza kupata. • Kanuni za kilimo hifadhi zinawalenga wakulima wote (mkono, plau au trekta). • Kilimo hifadhi hakihusiani na aina gani ya mazao yanafaa kwa viwango tofauti vya mvua au udongo, mbolea kiasi gani itumike kwa mazao haya n.k. 2.3 Kanuni na misingi ya kilimo rafiki wa mazingira KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 9. Kilimo rafiki wa mazingira ni kilimo kinachozingatia mchanganyiko wa kanuni na misingi mbalimbali ya mbinu za kilimo bora. Mfumo huu huzingatia mzunguko wa virutubisho vya mimea kwa kufuata kanuni kuu nne ambazo ni: 1. Jiandae mapema baada ya kuvuna 2. Kutifua udongo kwa kiwango kidogo au kutotifua kabisa 3. Kufunika udongo muda wote kutochoma/masalia ya mazao baada ya mavuno 4. Kilimo cha mzunguko au mbadilishano wa mazao na ya jamii ya mikunde/mazao 5. Kilimo mchanganyiko na miti/wanyama 2.3.1 Kutifua udongo kwa kiwango kidogo au kutotifua kabisa Kutifua ardhi ni pamoja na kufungua, kugeuza, na kuchanganya udongokwa kutumia jembe, plau, na vifaa vinavyokokotwa na maksai au trakta. Tunapolima kwa kutifua ardhi mara nyingi tunasababisha ardhi kutoa hewa ukaa ambayo mara nyingi huhifadhiwa ardhini, vilevile muundo wa udongo ambao hurahisha maji kuingia kwa urahisi kwenye udongo huharibika na hivyo kusababisha mmomonyoko wa udongo. Kulima kwa uangalifu kwa kutifua udongo kwa kiwango kidogo au kutotifua kabisa kunaongeza uwezo wa ardhi kuhifadhi maji,kuingiza hewa, kurahisisha kutiririka maji, kupata joto na kuhifadhi hewa ukaa ndani ya udongo. Hii hufanyika kwa kupanda moja kwa moja kwenye udongo bila kutifua au kuchimba mashimo (beseni) ya kupandia bila kulima. Kilimo hiki kisichohitaji kutifua ardhi namavuno yake ni mazuri kabisa. Faida za kutifua udongo kwa kiwango kidogo au kutotifua kabisa 1. Kulainisha na kulegeza udongo ili mizizi ya mimea ipenyeze kwa urahisi KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 10. 2. Kuingiza hewa, naitrojeni na oksijeni kutoka angani 3. Kuchangamsha viumbe hai ardhini vifanye kazi 4. Kuongeza uwezo wa maji wa kupenyeza ardhini 5. Kuongeza uwezo wa maji wa kupenyeza ardhini 6. Kupunguza unyaufu wa ardhi 7. Kudhibiti wadudu ardhini na magugu 8. Kusaidia kuchanganya masalia ya mazao pamoja na mbolea ardhini 9. Kutayarisha shamba kwa kuotesha na kusia mbegu 10. Kurekebisha ugumu unaosababishwa na shughuli mbalimbali juu ya ardhi Mfano wa mfumo wa kilimo cha kutokutifua au kutifua ardhi kidogo tu ( Kilimo Hifadhi);Zambia, Chololo kondoa. Ukanda wa Pwani wakulima hufanya yafuatayo; • Wanakata uoto katika usawa wa ardhi • Kufuata kontua, umbali wa kuotesha mazao udongo unatifuliwa • Samadi inawekwa katika mistari iliyolimwa • Mazao yanaoteshwa katika mistari hiyo • Magugu katikati ya mistari yanakatwa mara kwa mara na ni matandazo • Mfumo unaweza kutumia mikunde kama zao la kufunika ardhi, kadhalika jimbo hilo mahindi yanaoteshwa kwenye shamba lenye masalia ya msimu uliotangulia. • Mahindi yanaoteshwa ndani ya matandazo KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 11. • Mwezi 1 hadi 2 baadaye maharage yanaoteshwa • Mahindi yakishavunwa masalia hutandazwa shambani na maharage huendelea kukua. • Maharage hayo huandaa shamba tayari kwa kuotesha zao jingine la mahindi • Kwa kutumia mtindo huu mahindi na maharage huvunwa mara mbili kila mwaka na kutoa mavuno mazuri. 2.3.2 Kufunika ardhi muda wote Ili Kuukinga udongo kutokana na jua kali na mvua kubwa unatakiwa kuufunika udongo kwa kutumia matandazo, kuacha masalia ya mazao au kupanda mazao ya kufunika shambani. Kwa njia nyingine tunazuia mmomonyoko wa udongo na kuhifadhi unyevu. 2.3.2.1 Matandazo Kuweka matandazo ni kazi ya kufunika udongo wa juu kwa kutumia magugu, masalia ya mazao ya kilimo na misitu, majani, matawi, vijiti, na mabua.Matandazo na wakati wa kutandaza hutegemea mazingira na mbinu za kilimo. Matandazo huongeza kasi ya kazi za viumbe hai ndani ya ardhi, huboresha udongo ili maji yaweze kunywea ndani, na hupunguza mmomonyoko. Matandazo yanapooza tunapata mboji inayoshikiza sehemu za udongo vizuri ili zisichukuliwe na maji. Matandazo hutoa chakula cha wadudu rafiki waishio udongoni. 2.3.2.2 Faida za Matandazo • Kuukinga udongo na mmomonyoko wa upepo na maji. • Kuboresha uwezo wa maji kupenyeza ndani ya udongo, ili kudumisha unyevu na kuzuia unyaufu • Kulisha na kulinda viumbe hai ndani ya ardhi • Kuzuia magugu KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 12. • Udongo haupati joto kali • Matandazo ni chanzo cha virutubisho vya mazao • Kuongeza mboji ardhini Zingatia: • Kila inapowezekana ni vyema kusambaza matandazo shambani kabla au mara tu msimu wa mvua unapoanza. Hicho ni kipindi ambapo ardhi huweza kuathirikasana. Inafaa kuwekea matandazo miche ya mboga ikishapata nguvu na kujishikiza vizuri na udongo. • Kadhalika matandazo yawekwe kwa kiasi kidogo tu hasa pale ambapo mazao hayajaota. Kwenye shamba la mazao ya kudumu, matandazo yawekwe mara baada tu ya kutifua ardhi. Matandazo huweza kutandazwa katikati ya mazao, kuzungushia mazao ya miti au kwenye shamba lote. • Endapo matandazo yanachelewa kuoza, kinyesi cha kuku kinatandazwa juu yake 2.3.2.3 Kuacha masalia ya mazao Njia nyingine ya kufunika udongo ni kutumia masalia ya mazao, hii hufanyika pindi mkulima anapomaliza kuvuna mazao ya msimu uliopita.Masalia ya mazao kama mahindi, maharage, mtama, alizeti yakatwe na kulazwa juu ya udongo ili kuzuia Matone ya mvua na jua kupiga ardhini moja kwa moja. 2.3.3 Mzunguko wa mazao • Upandaji wa mazao yanayochangamana vizuri kwenye shamba moja na kufanya mzunguko wa mazao msimu hadi msimu. Kuna sababu nyingi za msingi za kufanya kilimo cha kubadilisha mazao na yale aina ya mikunde kama vile soya, maharagwe, kunde, choroko, mbaazi na mengineyo. KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 13. Kilimo hiki cha kubadilisha mazao na ya jamii ya kunde hupunguza matumizi ya mbolea za viwandani mashambani (na hivyo kuokoa matumizi zaidi ya pesa pia!). • Mazao aina ya mikunde hurutubisha udongo kwa kutumia hewa ya naitrojeni kutoka angani na kuibadilisha na hivyo kufanya mimea mingine isiyo jamii ya kunde ifaidike vile vile. • Mbaazi hutumia mizizi yake mirefu kuingia chini kabisa ya ardhi na kuchimbua virutubisho aina ya fosforasi, huvileta virutubisho hivyo juu ya ardhi na kufanya mimea yenye mizizi yenye kina kifupi itakayopandwa kwenye mbadilishano msimu unaofuata kunufaika nayo. • Mazao aina ya kunde yanayokomaa mapema ni chanzo kizuri cha protini kwa familia kwa mwezi Februari, wakati ambao unahitaji zaidi kwa uhakika wa chakula kwenye familia. • Inawezekana kuvuna mara mbili kwa mazao yanayokomaa mapema katika msimu mmoja. Mazao jamii ya mikunde yanapaswa kupandwa angalau theluthi moja ya ukubwa wa shamba unalolima katika utaratibu wa kubadilishana mazao kila mwaka. • Mimea ya mbolea za kijani inaoteshwa mara baada ya kuvuna zao kuu. • Ni vyema kuotesha kwa kukinga mitelemko mikali kupunguza kasi ya maji ya mvua inayotelemka milimani. Kwa yale mazao yasiyofunika ardhi mapema inafaa kuotesha zao kama alfalfa au maharage yatakayofunika ardhi mapema. • Faida yake ni kwamba kilimo hiki hupunguza madhara ya wadudu na magonjwa. 2.3.4 Kilimo cha kuchanganya mazao na miti • Miti kama vile Mkondachao (Faidherbia albida) yaweza kuchukua hewa ya naitrojeni iliyoko angani na kuibadilisha kuwa rutuba ifikapo ardhini na kuifanya mimea mingine kunufaika nayo. • Unaweza kupanda miti iongezayo rutuba na mboji kwenye udongo ili kuongeza uzalishaji wa mazao. Miti kama mkondachao yaweza kupandwa nafasi ya mita10 kwa10 na unaweza kupata miti 40 kwa ekari. KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 14. Miti ya mkondachao inayo sifa moja ya pekee; hupukutisha majani yake kipindi cha mvua badala ya kipindi cha kiangazi kama inavyofanya miti mingine. Hivyo basi hali hiyo inakuwezesha kupanda mazao mbalimbali chini ya mwamvuli wa miti hiyo pasipo kuathiri ufanisi wa mazao hayo kwa vile hapawi na kivuli. 2.4 Hatua za kufuata katika kilimo hifadhi 2.4.1 Acha masalia ya mazao shambani- usiyachome Palizi la magugu la mara kwa mara ni muhimu sana katika Kilimo Hifadhi. Jinsi unavyoacha masalia mengi shambani ni vizuri zaidi. Masalia unapoyaacha shambani hurutubisha udongo, yanadhibiti upotevu wa maji ya mvua na yanaruhusu maji kunywea ndani ya udongo. Unapoacha masalia shambani kila mwaka, yanaboresha udongo. Mchwa wanayashambulia na kuyachanganya na matamahuluku kwenye udongo. Masalia yanavyokua mengi ndivyo mchwa wanavyoyashambulia na hatimaye hawawezi kushambulia mazao yako shambani. 2.4.2 Andaa mashimo ya kupandia ya kudumu Wakati unapochimba mashimo ya kupandia badala ya kuutibua udongo husaidia kupunguza matumizi ya fedha na muda. Mashimo ya kupandia ya kudumu yanavuna maji ya mvua za awali na hivyo kurahisisha uotaji wa mbegu na kuboresha uchipuaji mzuri wa mazao yako shambani. 2.4.3 Panda mbegu mapema • Anza matayarisho ya shamba mapema mara tu baada ya kumaliza kuvuna, ili uweze kusambaza uzito wa kazi zako kwa miezi mingine kabla ya kuanza kwa msimu mwingine wa kupanda. • Jinsi unavyowahi kuandaa shamba lako mapema,ndivyo unavyoweza kuwahi kupanda mara tu baada ya mvua za kwanza za kupandia kunyesha. • Upandaji mbegu wa mapema ni muhimu kwa sababu mvua hizo za awali husaidia mmea katika uotaji wake/upevukaji wake kutokana na naitrojeni inayoachwa na viumbe hai wa udongoni. 2.4.4 Wahi kupalilia mara kwa mara msimu wote KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 15. Palizi la mapema na la mara kwa mara katika mwaka mzima ni jambo muhimu sana katika Kilimo Hifadhi. • Uotaji wa magugu shambani utakuwa unapungua baada ya muda fulani kutokana na palizi la mara kwa mara. • Palizi ni sharti lifanyike ndani ya wiki kati ya nne na sita baada ya mbegu kuota shambani wakati magugu yatakuwa yamefikia kimo cha sentimeta 2.5. • Ni muhimu uendelee kufanya palizi hata wakati mazao yanapokuwa yamekomaa hata baada ya mavuno, ili kuyadhibiti kabisa magugu yasizalishe mbegu na kuzipukutisha shambani, vinginevyo yatakuongezea kazi ya ziada ya palizi kwa mwaka ufuatao. 2.5 Faida ya kilimo hai na hifadhi ya mazingira 2.5.1 Huhifadhi udongo na kudumisha rutuba ya ardhi 2.5.2 Hupunguza uchafuzi wa maji kwenye mito, maziwa na chini ya ardhi. 2.5.3 Hulinda bioanuai. 2.5.4 Hudumisha aina mbalimbali za uoto wa asili. 2.5.5 Hutunza vizuri mifugo. 2.5.6 Matumizi ya malighafi mbadala, na nishati asilia. 2.5.7 Hakuna masalia mengi ya viuatilifu kwenye vyakula. 2.5.8 Hakuna vichochezi na madawa katika mazao ya mifugo. 2.5.9 Mazao ya thamani bora zaidi; (mwonjo na hifadhi). 2.6 Changamoto za kilimo hifadhi na mazingira KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 16. 1. Woga wa wakulima kuhusu kushukuka kwa mavuno kunakosababishwa na mabadiliko ya mavuno 2. Upatikanaji wa aina za mbegu zinazofaa 3. Gharama za mbegu 4. Upatikanaji wa maji 5. Mahitaji ya nguvu kazi 6. Matumizi ya ziada kutokana na mazao mengine ya pembeni 7. Uhakika wa chakula MADA 3: UDONGO 3.1 Udongo ni nini? Udongo ni tabaka la juu ya ardhi linalosaidia ukuaji wa mimea. Udongo ni mchanganyiko wa miamba iliyopasuka, madini, maji, hewa, wadudu na wanyama wadogo na wakubwa walio hai na waliokufa, masalia ya mimea na mboji. Kuna aina kuu tatu za udongo katika maeneo yetu ambazo ni kichanga, mfinyazi na tifutifu. Ustawi wa zao fulani hutegemeana na aina ya udongo ulioko katika eneo hilo. Udongo wa aina ya tifutifu ndio unaofaa zaidi kwa ajili ya kilimo. Udongo wa kichanga hupoteza maji kirahisi na hivyo haufai kwa kilimo. Hata hivyo udongo wa mfinyanzi hutuwamisha maji na kusababisha mizizi kushindwa kupumua na kusababisha mimea isiyotaka maji mengi kama mahindi na maharage kufa. • Udongo ni hitaji muhimu kuliko mengine katika kilimo na mkulima anayo mamlaka makubwa juu yake. Udongo una uhai kwa sababu ni makazi ya mimea, wanyama na viumbe vingine vyenye mahusiano nao. Udongo una yabisi, mboji na nafasi wazi. • Udongo wenye ujazo wa kijiko cha chai huweza kuwa na mamilioni ya viumbe. Baadhi hutokana na mimea na wanyama. Viumbe vingine huonekana kwa macho kama minyoo, KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 17. buibui, konokono, jongoo na mchwa. Viumbe muhimu sana ardhini ni bakteria, fangi na protozoa. • Wakulima wengi wanadhani kuwa viumbe wanaoishi ndani ya ardhi husababisha madhara na kufikiria tu namna ya kuwaua. Ukweli ni kwamba ni wadudu wachache sana wanaodhuru mazao. Viumbe wengi ndani ya udongo ni wa manufaa makubwa na hurutubisha udongo. 3.1 Umuhimu wa viumbe wanaoishi ardhini:- • Kuozesha mabaki na kutengeneza mboji. • Kuchanganya masalia ya mazao ndani ya sehemu za ardhi na kuimarisha udongo. • Kuchimba vinjia na hivyo kurahisisha mizizi kupenya na kuingiza hewa ardhini. • Kusaidia upatikanaji wa virutubisho ardhini. • Kuzuia wadudu na magonjwa yanayoathiri mizizi ya mimea. • Minyoo ni alama ya udongo wenye rutuba, wana kazi nyeti ardhini mfano kuyeyusha masalia ya viumbe hai, kusaidia kuchanganya masalia na sehemu za udongo ili kuuimarisha • Njia wanazozichimba ndani ya ardhi, zinarahisisha kupenyeza hewa na maji, hivyo kupunguza mmomonyoko wa udongo na maji kusimama juu ya ardhi. • Minyoo wanahitaji masalia hai, joto la kiasi na unyevu wa kutosha. Husitawi vizuri ndani ya udongo wenye matandazo. Kilimo cha mara kwa mara na matumizi ya viuatilifu huathiri sana idadi ya minyoo ardhini. 3.2 Udongo wenye rutuba unategemea kuwa na vitu vifuatavyo; • Kina cha udongo: Kuwepo kwa ujazo/kina cha udongo wa kutosha unaotumiwa na mizizi ya mimea. KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 18. • Upatikanaji maji: uwepo wa unyevu wa kutosha kwa kipindi kirefu. • Urahisi wa maji kupita: Uwezo wa kupitisha maji kwa urahisi. • Hewa: Hewa ya kutosha inahitajika kuwepo kwa afya ya mizizi na maisha hai ya udongo. • pH Uchachu: Udongo hauna tindikali au chumvi nyingi. • Madini: upatikanaji wa virutubisho kutoka mwamba asilia, na muundo wa udongo. • Mboji: Kuwepo kwa kiasi cha kutosha cha mboji inahusiana vizuri na uwezo wa udongo kushika virutubisho, maji na maisha ya udongo na muundo wa udongo. • Viumbe hai kwenye udongo:Kuwepo kwa viumbe hai kwenye udongo husaidia upatikanaji wa virutubisho, kushikilia maji, muundo na afya ya udongo, na kuyeyushwa kwa mboji ardhini. Endapo udongo utakosa baadhi ya vitu vilivyotajwa hapo juu hali ya udongo haitafaa kwa ukuaji wa mimea. Mifano ni kutuama maji, uchachu, udongo mgumu na uhaba wa virutubisho, unaosababisha upungufu mkubwa wa mavuno. 3.3 Mbinu za Kurutubisha udongo Wakulima wanaweza kuboresha rutuba ya udongo kwa kuzingatia njia zifuatazo: 1. Kuukinga udongo kutokana na jua kali na mvua kubwa kwa kuufunika na matandazo, mbolea ya kijani au mazao ya kufunika. Kwa njia nyingine tunazuia mmomonyoko wa udongo na kuhifadhi unyevu. 2. Kilimo mseto na mzunguko wa kufaa wa mazao ya msimu unadumisha rutuba ya udongo. 3. Tifua udongo ipasavyo ili kudumisha rutuba na ubora wake kwa kuzuia mmomonyoko na udongo kugandamana. KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 19. 4. Kuwa na mpangilio mzuri wa virutubisho kwa kutumia mbolea za asili kulingana na mahitaji ya mazao kama samadi na mboji 5. Kuainisha malisho na hifadhi ya viumbe hai walio ardhini, kwa kuongeza masalia ya mimea tunawezesha viumbe hai wenye faida kuishi na kufanya kazi. MADA 4: KUTENGENEZA MBOJI 4.0 Mboji ni nini? Mboji ni sehemu ya viumbe (mabaki ya mimea na wanyama (matamahuruku)) ambayo imeozeshwa kwa muda mrefu ili kusazwa na viumbe vidogo vidogo. Sehemu za vitu kama majani, matunda na mabaki ya mboga hutengeneza mbolea ya mboji. Mboji iliyoiva hubadilika rangi na kuwa ya hudhurungi, tifutifu na hunukia vizuri. Mboji ni rahisi kutengeneza, gharama zake ni za chini sana na inafaa mno kuongezwa kwenye udongo ili kuinua mazao ya shamba. Mboji iliyotunzwa vyema huwa na rutuba nzuri kwa mimea inapotumiwa shambani. Mboji huchemka hata kiasi cha kuua magonjwa ya mimea na mbegu za magugu. Majani makavu ya ndizi ni mazuri kwa kutunza vifaa vya mbolea na kuweka ukavu. Hali hii huwa huzuia kupotea kwa maji kabla ya kujenga lundo la mboji na wakati mbolea inapokuwa inaiva. 4.1 Vifaa visivyofaa kuwekwa kwenye mboji • Sehemu za mimea ambazo zimenyunyiziwa dawa ya kuwaua wadudu (viuatilifu) na magugu. • Vipande vya nyama kwa sababu vinavutia panya na wadudu wengine. • Vifaa vilivyo na ncha kali kama mwiba ambavyo vyaweza kujeruhi mikono na miguu. • Magugu ambayo yanarudiarudia kila mwaka. Magugu kama hayo huuliwa kwa kuanikwa kwenye jua kali ili yakauke baadaye huchomwa ili yasienee na jivu lake laweza kuongezwa kwenye lundo la mbolea. • Vitu visivyo kua na uhai kama plastiki na chuma. KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 20. 5.2 Vitu ambavyo vyaweza kutumiwa kutengeneza mboji 5.2.1 Vifaa vya nyumbani • Maganda ya matunda • Jivu la kuni • Taka taka za kufagia 5.2.2 Shambani • Mabaki ya mimea baada ya kuvuna, katakat vitu vigumu, kama ni vigumu nyunyizia maji. Vitu vigumu huoza pole pole. Usitumie vile vilivyowekwa dawa juzijuzi • Majani makavu/ yaliokauka • Mimea/majani ya kijani au mabichi, kata kata kama ni makubwa. Mimea jamii ya mikunde hupendekezwa • Magugu, katakata kama ni makubwa. Usitumie mizizi ya magugu ama mbegu za magugu 5.2.3 Asili • Samadi kutoka kwa mifugo na mabaki ya mimea ni nzuri sana katika kutengeneza mbolea hai na ina rutuba nzuri sana • Mkojo, ni vigumu kukusanya mkojo ila hupatikana kwenye zizi la ng’ombe. Nyunyuzia kwenye biwi/lundo la mbolea kwa kiwango kidogo. Mkojo hufanya mbolea kuoza haraka • Udongo, tumia udongo kama sentimita 10 kutoka tabaka la juu ya shamba. Hutumika kufunika Biwi/lundo la mbolea. • Magugu ya baharini (Mwani) Yafaa yakaushwe na hutumiwa na majani yaliyo kauka yana madini muhimu kwa wingi 4.3 Namna ya kutengeneza mboji ya mimea Kusanya vitu na vifaa vinavyohitajika katika utengenezaji wa mboji ambayo ni; KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 21. Majani mengi mabichi/kijani na makavu. Majani jamii ya mikunde ni mazuri sana kwani hutengeneza kirutubishi cha naitrojeni (N) kwa wingi. • Mabua ya mahindi au vitawi vya miti • Udongo wa kawaida wa juu • Mboji ya zamani • Majivu au vumbi la mkaa • Maji 4.3.1 Hatua za kufuata 1. Chagua sehemu karibu na eneo ambalo mboji itaenda kutumika na ambapo kuna hifadhi ya kutosha kukinga dhidi ya upepo, jua na mvua. 2. Katakata majani yawe madogo madogo ili yaweze kuoza haraka. 3. Tengeneza msingi kama mita sita (6) urefu na upana wake mita 2 kwa kutumia majani magumu kama matawi/vijiti. Hii itahakikisha maji yanatiririka na hewa ina zunguka vizuri. Hakikisha kuna nafasi ya kutosha kufanyia kazi kwenye biwi bila kulikanyaga. 4. Weka sentimita 10 ya majani ambayo hayaozi haraka kwa mfano mabua vya mahindi au mimea mibichi/kijani. 5. Weka sentimita 10 ya vifaa ambavyo huoza haraka kwa mfano maganda ya mboga na matunda. KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 22. 6. Weka sentimita 2 ya samadi (mbolea-hai ya wanyama), mabaki ya mbolea ya zamani kama yaweza kupatikana. 7. Weka udongo wa juu sentimita 10 kutoka kwenye shamba ambalo hulimwa. 8. Majivu na mkojo vyaweza kunyunyuziwa juu ili kufanya biwi/lundo kuoza haraka. 9. Nyunyizia maji kwenye biwi mpaka lilowe. 10. Rudia mpangilio huu kuanzia namba nne (4) mpaka lundo lifike mita moja (1.m) hadi moja na nusu (1.5m) kwenda juu isipokuwa vijiti/matawi ya kwanza. 4.3.2 Zingatia • Biwi/lundo cha mboji kinatakiwa kifunukwe ili kupunguza/kuzuia mvuke ama mvua nyingi ambayo hubeba rutuba kutoka kwenye mbolea. Weka gunia, nyasi ama matawi ya migomba yaliyokauka. • Kila tabaka/kunjo/safu yafaa kupangwa kuanzia kwenye ukingo ili lundo la mbolea lisiporomoke. • Namna nyigine ya kuzuia lundo kuporomoka ni kwa kuweka vipande vya mbao kando ya biwi. Wavu wa nyuzi za chuma utafanya biwi kukauka. • Katika sehemu zenye ukavu mwingi. Mianzi iliyo na mashimo husaidia kufanya hewa kuingia na kuzunguka kwa urahisi KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 23. 4.4 Wadudu wenye manufaa na mazingira yanayohitajika kwenye Biwi 4.4.1 Wadudu ambao husaidia kufanya biwi kuoza Viumbe wengi wanaohusika na kazi hii ya kuoza ni wadogo hawaonekani kwa macho matupu. Ila viumbe hawa huhitaji maji, hewa na vipande/sehemu ya viumbe wengine ambazo kwao ni chakula. Viumbe hawa hula vipande hivyo na hutoa hewa ya carbon dioxide, maji na joto. 4.4.2 Hatua 3 kubwa za biwi kuoza Kuna hatua tatu kubwa wakati biwi linapooza; 1. Hatua ya kupanda joto 2. Hatua ya kupoa/kuwa baridi 3. Hatua ya kukomaa. 4.4.2.1 Hatua ya kupanda joto Wakati ya hatua ya kupanda joto, joto hufikia kiwango cha juu sana katikati mwa biwi. Uzuri wa joto hili ni kwamba magonjwa yaliyokuwa kwenye viungo vya biwi na mbegu za magugu huchomwa hadi kufa. Maelezo ya msingi kuhusu mboji/mbolea vunde/mbolea hai uyoga (fungi) huwa na faida nyingi kwa sababu kazi yake ni kuzisaga nyuzi ngumu ambazo zimo kwenye viungo vya mimea au majani. 4.4.2.2 Hatua ya kukomaa Kwenye hatua ya tatu, ‘hatua ya kukomaa’ viumbe wakubwa kama mchwa na nyungunyungu husaidia kusaga na kuchanganya mbolea. Hali ya anga ikiwa na joto jingi viumbe hawa hufanya kazi haraka kuliko wakati ambapo hali ya anga ni baridi. Aina ya viungo vilivyotumika kujenga/kukuza biwi na ukali/uchungu (pH) wa udongo pia huathiri kiwango cha mbolea kuoza. 4.4.3 Mazingira yanayohitajika kwenye biwi Biwi huhitaji vitu vitatu: hewa, maji na joto. • Hewa KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 24. Viumbe wadogo kwenye biwi huhitaji hewa ili waweze kuishi. Hewa ya carbon dioxide (CO2) ambayo imetolewa na wadudu hawa huhitaji kutolewa nje. Ikiwa hewa safi itakosekana, viumbe wengine wasiohitajika huingia na kutoa harufu mbaya na pia kufanya mbolea isioze haraka. • Maji Kazi ya viumbe wadogo huwa polepole ikiwa biwi ni kavu. Aidha ikiwa biwi litalowa maji basi viumbe wadogo watakufa na kufanya biwi kuwa na uchachu badala ya kutengeneza mbolea. Hivyo basi kukagua kiwango halisi cha maji huhitaji ujuzi fulani. • Joto Biwi hutoa joto wakati linaoza. Lundo likiwa na joto jingi viumbe wadogo hutoka, kisha huweza kurudi pindi linapopoa. Muhimu kuhakikisha kuwa joto halizidi sana ili kuweza kuwa na mboji nzuri yenye virutubisho. 4.5 Matunzo ya Biwi Ili kupata mbolea nzuri, biwi linapojengwa yafaa lishughulikiwe kwa utaratibu. Biwi hilo litahitaji maji, kupinduliwa, joto na muda unaofaa wa kukomaa. 4.5.1 Maji • Wakati wa kiangazi biwi/lundo la mboji huhitaji kumwagiliwa maji kila wiki. Maji katika lundo la mbolea hupimwa kwa kuweka fungu dogo la nyasi na kulitoa baada ya dakika tano. Nyasi isipoonyesha majimaji au unyevu itabidi maji yamwagwe kwenye lundo hilo • Kuna njia kadha za kuzuia mvuke kuinuka kutoka kwenye biwi, hali kadhalika kiwango cha maji yanayomwagiliwa: • Funika lundo kwa majani ya ndizi ama nyasi. • Funika lundo kwa udongo. • Lundo lisigeuzwegeuzwe • Biwi likilowa maji itabidi kifunuliwe na kuachwa kikauke kwenye jua kabla ya kujengwa tena. KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 25. 4.6 Kupindua/kugeuza • Katika muda wa wiki tatu (3) baada ya kujenga/kukuza biwi/lundo ukubwa wake utakuwa umepungua sana. • Kupindua biwi uhakikishe ya kwamba majani yaliyo kando yameoza pia hewa safi imerejeshwa. • Kupindua biwi huchanganya majani yaliyotengenezwa na kukijenga upya. Majani yalivyo kando huwekwa katikati, ikiwa kuna ukavu, maji mengi na majani/viungo vikavu huongezwa. • Kupindua kunatikiwa kufanyike kila baada ya wiki tatu. • Hali ya joto na kiwango cha maji yafaa kupimwa siku chache baada ya kupinduliwa. • Kupinduliwa kwa mara ya tatu kutahitajika ikiwa viungo havitakuwa vimeoza kikamilifu. • Mbolea yaweza kutengenezwa bila kupinduliwa ila viungo vilivyo kando havitaoza. Mbegu za magugu na viungo na magonjwa ya mimea hayatakufa. • Viungo vilivyobaki hutengwa na kutumiwa kwenye biwi lingine. Japokuwa kugeuza hakuna lazima, kunapendekezwa ili kupata mbolea nzuri. 4.6 Muda wa kukomaa na matumizi ya mboji 4.6.1 Muda wa kukomaa • Lundo la mbolea yafaa liachwe likomae baada ya joto kupoa. Mbolea yaweza kutumiwa mara tu viungo vya kwanza vinapokosa ama vinapopoteza utambusho, na rangi yake ikageuka kuwa nyeusi na harufu ikawa ya kuvutia. • Hata wakati huu mbolea yahitaji kufunikwa ili isilowe kwa maji ya mvua ama kukauka kwa ajili ya jua bali ibakie na unyevunyevu. Mboji ikikawia muda mrefu kabla ya kutumiwa, hupoteza rotuba na wanyama wadogo huifanya makazi yao. 4.6.2 Matumizi ya mboji KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 26. Umuhimu mkuu wa mboji ni kuongeza mazao ya shamba kwa kusaidia udongo kushikilia maji kwa muda mrefu na kufanya udongo kuwa na afya bora. Pia mbolea hufanya udongo kushikamana hivyo hupunguza mmomonyoko wa udongo. • Mbolea hutumiwa mara nyingi kwenye shamba lililoko karibu nyumbani na mbali na nyumba. Wakati shamba huandaliwa kwa kupanda mbegu, mbolea huchanganywa kwenye udongo wa juu. Mbolea haifai kuwekwa ndani ya udongo kiasi cha kwamba mizizi ya mimea haitaifikia. • Njia bora ni kuweka mbolea kidogo kwenye shimo ambamo mmea utapandwa. Kwenye sehemu za ukame, mitaro huchimbwa kisha mbolea ikawekwa ambamo maji hukusanyika na kutumiwa na mimea. • Hupunguza magonjwa na wadudu waharibifu wa mimea yalioko udongoni hivyo basi mimea huwa na nguvu, afya na hustahimili magonjwa na wadudu waharibifu. • Mbolea vunde pia yaweza kutumiwa ili kufunika udongo usipoteze maji mengi. Mbolea ambayo haiko tayari hasa kutumika kwa kazi kama hii iwekwe udongoni ili iendelee kuoza na kuchanganyika kwenye udongo. Mbolea inapotumika kwa kuzuia maji kwenye udongo, yafaa ifunikwe kwa majani madogo (matandazo). Hii itazuia mbolea isipoteze rotuba kwa sababu ya joto jingi na miale ya jua. • Mboji pia hutumika kukuza miche na hata kwa kuwalisha samaki. MADA 5: HIFADHI YA MAJI • Uhaba wa maji kwenye shughuli za kilimo katika nchi za tropiki ni jambo la kawaida. Zipo sehemu ambazo ni budi kumwagilia ili mavuno yaweze kupatikana. Hata katika maeneo yale yanayopata kiasi kikubwa cha mvua, mazao yanapungukiwa maji kipindi cha kiangazi. KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 27. Kilimo hai kinalenga kutumia kwa uendelevu rasilimali za asili zinazopatikana mashambani. Kupatikana, kuvuna, na kuhifadhi maji ni mada muhimu kwa wale wanaohimiza Kilimo hai na hifadhi ya mazingira. • Kwenye mfumo wa kilimo cha kawaida tunatumia huduma za umwagiliaji kukabiliana na upungufu wa maji. Kwa Kilimo hai na hifadhi ya mazingira mkulima anaweka kipaumbele upatikanaji na upenyezaji maji ndani ya ardhi. 5.1 Uhifadhi wa maji ardhini • Kipindi cha kiangazi kuna aina za udongo zinazoweza na zisizoweza kuipatia mimea maji. • Udongo mfinyanzi unaweza kuhifadhi maji mara tatu zaidi ya kile kiasi kinachohifadhiwa na udongo kichanga. • Kazi ya kuhifadhi maji ardhini inapunguza gharama za kumwagilia. 5.2 Namna ya kuhifadhi maji ardhini • Wakati wa kiangazi mazao yanategemea unyevu kutoka ardhini. Uwezo wa udongo wa kunyonya maji hutegemea mpangilio wa sehemu za udongo na kiasi cha mboji kilicho ndani yake. • Mboji kama spongi ni ghala ya maji. Udongo wenye mboji, unaweza kuhifadhi maji kwa muda mrefu zaidi. Tunaweza kuongeza mboji mashambani kwa njia za samadi,mbolea vunde, matandazo, na mbolea za majani. • Matandazo yanapunguza unyaufu wa maji ardhini. Huuwekea udongo kivuli kutokana na jua pamoja na kulinda ardhi isipate mno joto. • Kulima kijuu juu au kuparua huzuia kukauka kwa udongo wa chini. • Kuondoa magugu kunapunguza maji yanayopotea kupitia majani ya mimea hiyo. KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 28. 5.3 Kuvuna maji • Wakati wa mvua kubwa, kiasi kidogo sana cha maji kinanywea ardhini. Sehemu kubwa ya maji huwa inatiririka kama mkondo na huenda mbali bila kutumiwa na mimea. • Ili kuvuna kiasi kikubwa cha maji ya mvua na kuyaingiza ardhini, hatuna budi kuongeza uwezo wa udongo wa kunyonya maji. Udongo wa juu unapaswa kuwa na mpangilio mzuri na nafasi wazi (pores and cavities) zinazosababishwa na minyoo. • Mazao ya kufunika ardhi pamoja na matandazo huboresha mpangilio wa sehemu za udongo. Tena hupunguza kasi ya mtiririko wa maji juu ya ardhi na kuyafanya yanywee ndani yake. • Kwenye mitelemko matuta ya kukinga maji, yanayasaidia yanywee ardhini hasa mitaro inayotuamisha maji. • Visahani vya kuzungukia miti hufanya kazi hiyo hiyo. • Kwenye mashamba ya tambarare tunaweka mazao ndani ya mashimo (planting pits). • Mitego hii ya maji inapofunikwa na matandazo inaleta faida kubwa. Ziada ya maji kipindi cha mvua huweza kutumika wakati wa kiangazi. • Njia nyingi za kuhifadhi maji zinahitaji nguvu kazi na gharama kubwa. Tunapohifadhi maji ndani ya bwawa,tunaweza kufuga samaki ingawa maji huzama ardhini au kunyauka kuelekea angani kama mvuke. • Vile vile tunaweza kutengeneza matangi ya kuhifadhi maji. Ni vyema kupima na kuamua endapo tunahitaji kutengeneza chombo cha kuhifadhi maji kwa kulinganisha matumizi, mapato, na/au kupunguza eneo la kilimo ili kuweka hiyo huduma ya kuhifadhia maji. KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 29. MADA 6: DHANA YA VIKUNDI 6.0 UUNDAJI WA KIKUNDI 6.1 KIKUNDI NI NINI? • Ni idadi maalumu ya watu waliokubaliana/waliungana wenye lengo na nia ya kukusanya nguvu, rasiliamali, na mawazo yao ili kutatua changamoto zinazowakabili katika mazingira yao. • Ni watu kadhaa walioungana pamoja kufikia lengo maalumu la pamoja la maendeleo ya kiuchumi,kijamii na kisiasa. • Ni idadi ya watu wenye nia,mwelekeo na lengo moja kufanya shughuli fulani ya kijamii na kiuchumi. 6.2 UMUHIMU WA KIKUNDI KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 30. Kikundi huwaunganisha wakulima na: • Masoko • Asasi za kifedha • Watoa huduma za kilimo • Kuwa na uwezo wa kupanga bei za mazao yao • Kuwa na sauti ya pamoja • Kufanya kazi kwa juhudi(kazi kubwa bila maumivu) • Kufanya kazi kwa kushirikiana • Kuwa na vikao vya mara kwa mara 6.3 AINA ZA VIKUNDI Kuna aina kuu mbili za vikundi • Vikundi vyenye malengo ya kiuchumi (ujasiliamali) • Vikundi vyenye malengo ya kijamii(utoaji wa huduma)eg UKIMWI 6.4 TOFAUTI KATI YA KIKUNDI NA MKUSANYIKO KIKUNDI MKUSANYIKO → Sifa maalumu huwekwa hakuna sifa maalumu. → Idadi maalumu ya watu hakuna idadi maalum ya watu → Kuna uongozi hakuna uongozi → Mipango endelevu hakuna mipango → Sheria +taratibu hakuna sheria/taratibu → Mda maalum hakuna mda maalumu → Utunzaji wa kumbukumbu hakuna taarifa inawekwa Ni bora mbaki 10 wenye msimamo kuliko 30 wasiofuta taratibu za kikundi. 6.5 SIFA KUU ZA WANAKIKUNDI • Kufahamiana(historia ya kazi, ukweli, utendaji) KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 31. Kupendana(kutakiana maendeleo) • Kushibana(utayali wa kusaidiana) • Kuaminiana(kutokuwa tayari kuangusha wenzio) • UMOJA • Mkulima ,mwenye mashamba anayoyalima karibia kila msimu(wenye mafanikio na wa ngazi ya chini) • Wanao kubalika na wana kijiji wenzake • Angalau wajue kusoma na kuandika • Wanao ruhusu wenzake kujifunza kutoka kwake • Jinsia zote ziwepo(ke na me) • Awe tayari kujifunza na kupokea ushauri • Upatikanaji wao uwe wa uhakika • Kuanzia miaka 18 mpaka 45 • Mkazi wa mda mrefu kitongojini na kjijini kwa ujumla • Awe tayari kufanya alichoona na kufundisha wengine • Awe tayari kutumia sehemu ya shamba lake kufundishwa na kufundishia wengine siku zijazo • Wawe tayari kufanya shughuli za kikundi bila kutegemea posho/malipo ya Fedha. • Wawe na ari ya kujiendeleza kwa kufuata mbinu walizojifunza. • Wawe tayari kufanya kazi kwa pamoja kwenye kikundi • Wanaopendana na kujaliana. Zingatia: Watakao chaguliwa wana jukumu la kubadili mfumo wa ulimaji/kilimo hapo kitongojini baada ya kujifunza KILIMO HIFADHI, HIVYO WASIANGUSHE MRADI NA KIJIJI . 6.6 JINSI YA KUANZISHA VIKUNDI KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 32. 6.6.1 VIKUNDI VINAANZAJE? Uzoefu unaonyesha vikundi vinaweza kuanzishwa kwa njia tofauti i. Semina,warsha na ziara za mafunzo ya kubadilishana uzoefu na ujuzi maeneo mengine. ii. Mashirika,wanasiasa, kwa kutaka kufanikisha mipango maalumu huanzisha vikundi ili kurahisisha utekelezaji. iii. Vikundi vinaweza kuundwa kutokana na tatizo au hitaji maalumu la wenyeji. iv. Kikundi kinaweza kuzaliwa kutokana na wazo la mtu mmoja. 6.6.2 MAMBO/VIGEZO VYA KUZINGATIA KABLA YA UUNDAJI KIKUNDI IMARA. • Kuwepo na sababu/lengo la kuanzisha kukundi • Kuwepo na matokeo yatakayowanufaisha au kuwavutia • Kuwe na haja mfano elimu, soko au mtaji • Kuwe na kazi • Wanachama wote wawe na nia/lengo moja • Wanakikundi wawe ni watu wa tabia,tatizo,shughuli,mtizamo mmoja • Wanachama lazima wawe wakazi wa eneo husika. • Viongozi wasitoke kwenye familia moja. • Wanachama wote wawe na mtazamo chanya juu ya kikundi • Idadi ya wanakikundi isiwe kubwa wala kidogo sana.Mtu asilazimishwe kuingia kwenye kikundi na awe huru kutoka(muungano uwe wa hiari) • Kikundi kiwe na uhuru na kuamua mambo yake (kisijihisi ni cha mradi au mradi au mtaalamu,kitalemaa kimawazo) 6.6.3 JINSI YA KUANZISHA KIKUNDI i. Hakikisha msukumo wa kuanzisha kikundi unatoka ndani ya wahusika ,wazo laweza toka nje. ii. Kikundi kiwe na watu wachache (20-30)_Hurahisisha kufahamiana na kuaminiana. KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 33. iii. Hakikisha utengenezaji wa malengo,katiba,kanuni,jina la kikundi unahusisha walengwa. iv. Pendekeza viongozi wa vikundi watakavyo patikana(m/kiti,msaidizi na katibu) mwanachama aelewe sifa za kiongozi bora. v. Tengeneza katiba kulingana na malengo ya kikundi. vi. Kuwe na sheria na kanuni za kikundi na kila mwanakikundi awe anazijua ili akikiuka aonywe(kuhudhuria vikao,kutoa mchango,kusaidiana katika matatizo) vii. Tengeneza katiba ya kikundi.siku nzuri/huru kwa wote kuhudhuria. 6.7 KAZI ZA KIKUNDI I. KUPANGA NA KUWEKA MALENGO Hii ni kazi ya wanakikundi wote Inabidi ifanyike mara kwa mara Uzoefu wa wanakikundi wa mazingira yao uzingatiwe II. KUTATUA TOFAUTI ZA MAWAZO Kila penye watu wengi pana mawazo mengi yanayotofautiana Ni vipi kutofautiana bila uhasama Ni vipi kufika muafaka Ni vipi mawazo tofauti yanaweza leta umoja III. KUTAFUTA VITENDEA KAZI Ili kufanikisha malengo vinahitajika Fedha Utaalamu/Ushauri Nguvu za mikono Pembejeo Huduma nyingine(usafiri) IV. MATUMIZI BORA YA VIFAA VYA KAZI KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 34. Vitendea kazi vizuri vikipatikana muhimu vitumike ipasavyo ili kufikia malengo ya kikundi. Iwe majengo, pembejeo, duka, nguvu za watu n.k. Lazima ziratibiwe vizuri,kuwe na kumbukumbu nzuri na uwasilishaji wa mahesabu. V. KUTOA HUDUMA KWA WANAKIKUNDI Mradi na viongozi inabidi kutoa huduma fulani fulani kwa wanakikundi; Kutafuta ushauri,masoko,mikopo,pembejeo n.k. Kikundi kisipotoa huduma hizo wengine hawatapata hamasa ya kujiunga kwenye kikundi. VI. KUTETEA HAKI ZA WANAKIKUNDI Jukumu mojawapo la kikundi ni kujenga uwezo na kujiamini kwa wanakikundi ili waweze kutetea maslahi yao pale inapobidi. Ili kuleta mafanikio kikundini mara nyingine inabidi kupingana na sera za watu/makundi mengine 6.8 UONGOZI 6.10.1 Kiongozi ni nani? Kiongozi ni mtu/mwanakikundi - Anayechaguliwa na wenzake - Ndiye msimamizi wa sheria na taratibu za kikundi na kuhakikisha kwamba rasilimali zao ziko salama na lengo la kikundi linafikiwa - Uongozi una jukumu la kutufikisha pale tulipokubaliana tufike. 6.10.2 Sifa za kiongozi - Mwajibikaji – Awe na uwezo wa kuwatumikia watu wengine kadri ya mahitaji yao - Muwazi – Wambie watu ukweli hata kama unauma - Mkweli – usiwaahidi watu uongo KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 35. i. Mwenyekiti - Kazi zake ( Ndiye msimamizi mkuu wa shughuli zote za kikundi) - Sifa (awe mpigania haki za watu wengine na asiwe mwepesi kudhurumu haki za Watu. ii. Katibu - Kazi zake (kutunza kumbukumbu) - Sifa (ajue kuandika vizuri na haraka) iii. Mweka hazina Taratibu zifuatwe msisubiri kumlaani mtu leo na mbinguni 6.10.3 JE WEWE NI KIONGOZI?? K---- Kubali kushauriwa I---- Ielewe hali ya mahali ulipo O----Ondoa upendeleo N----Nena kauli thabiti na zinazotekelezeka G----Gawa Majukumu O----Onesha mifano kwa matendo(onesha njia) Z---- Zuia mipasuko na Migawanyiko. I---- Inua kiwango cha utendaji wa majukumu(inua unaowaongoza) 6.10.4 UCHAGUZI - Viongozi wa kikundi watachaguliwa kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na kikundi. Katiba ieleze waziwazi ni uongozi wa kikundi utafanyika. - Wanakikundi wapendekeze ni aina gani ya uchaguzi utafanyika ili kuwapata viongozi wao kwa mfano Kura – siri, kupendekezwa, kuteuliwa Wanakikundi wachague mfumo wa kuchagua KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 36. 6.10.5 KATIBA (roho ya kikundi) Kila kikundi kinatakiwa kutengeneza katiba yake itakayowaongoza katika utekelezaji wa shughuli zao za kila siku. Katiba ni muongozo wa kimsingi ambao haki, majukumu na wajibu wa wanachama hulindwa na kuhifadhi. 6.10.5.1 Wajibu/Umuhimu wa Katiba katika kikundi 1. Inahamasisha usawa miongoni mwa wanakikundi 2. Huelekeza umuhimu, majukumu na wajibu wa vyombo vyote 3. Hulinda shughuli za kila siku na shughuli za kikundi pia husema nini kifanyike na nini kisifanyike 4. Hufafanua malengo ya kikundi 5. Huongeza uwajibikaji wa uwazi 6. Huhamasisha ushirikiano kwa wanachama wote kwa kuwa huelezea kwa wajibu na majukumu ya kila mwanachama na viongozi 7. Husaidia kupunguza kutoelewana/ugomvi kwa kuweka njia ya kutatua 6.10.5.2 Njia za kuandaa rasimu ya katiba Uundaji wa katiba hufanywa tofauti kwa kila kikundi, baadhi yao husaidiwa na mwanasheria kwa gharama za wanakikundi na nyingine hufanywa na wanakikundi (kamati) iliyoidhinishwa na mkutano mkuu. Kamati hii huitajika kuundwa na watu wenye uelewa wa masuala ya kisheria. Baada ya kamati kumaliza kuandaa rasimu ya katiba, wanachama hujadili katika mkutano mkuu na kuifanyia marekebisho. Baada ya ushauri wa wadau kujumuisha , toleo la mwisho huandaliwa na kudhibitishwa na mkutano mkuu. 6.10.5.3 Kanuni za katiba bora a) Ushirikishwaji b) Isiyopendelea c) Isiyobadilika KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)
  • 37. d) Rahisi e) Imara KILIMO HAI NA HIFADHI YA MAZINGIRA MUONGOZO WA MAFUNZO UMEANDALIWA NA JEROME ERNEST NA ELIDA FUNDI ( MJUMITA)