SlideShare a Scribd company logo
1 of 10
Download to read offline
Prepeared by hebron venance
UFUGAJI WA NGURUWE
Nguruwe ni mnyama mwenye faida, ni rafiki kwa mazingira na hahitaji gharama kubwa. Katika nchi nyingi zinazo
endelea ikiwemo Tanzania kiasi kikubwa cha nyama kinatokana na wanyama wenye matumbo Zaidi ya moja kama
ng’ombe, mbuzi, kondoo, nk. Kutokana na kukua na kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya watu kunaumuhimu
mkubwa wa mabadiliko ya vyanzo vya nyama ili kuweza kukidhi mahitaji ya idadi kubwa ya ongezeko hilo la
watu. Moja ya chazo kizuri na kinacho weza kupunguza uhaba wa nyama kwa muda mfupi ni pamoja na nguruwe
ambao wanakuwa kwa muda mfupi, wanatupatia protini nyingi, gharama zake za uzalishaji si kubwa sana kwani
wanatumia aina nyingi za vyakula kulingana na mazingira husika na pia wanaweza kuzaliana kwa vingi kwa muda
mfupi. Mfano nguruwe anaweza kufikisha kilo 90-120 akifugwa vizuri ndani ya miezi sita(6) na hivyo tayari kwa
kuchinjwa kwaajili ya nyama, na kwa mzao mmoja anaweza kuzaa vitoto 9-14 ambapo kwa mwaka anazaa mara
mbili hivyo twaweza kupata vitoto 14-24 kwa mwaka.
Prepeared by hebron venance
Jamii nyingi hapa Tanzania huchukulia nguruwe kama mnyama mchafu na asiyefaa kuwa karibu naye na hata kwa
matumizi kama lishe. Zaidi, nyama yake inapendwa na haina madhara kwa afya na inapendekezwa kuliwa zaidi
kuliko nyama nyekundu. Unaweza kuanzisha mradi wa nguruwe kwa gharama ndogo lakini baada ya kipindi cha
miezi tisa tu ukaanza kujipatia kipato kutokana na ufugaji huo.
Ufugaji
Kwa kawaida nguruwe wanafugwa na watu wa kada zote, wafugaji wadogo wadogo na hata wakubwa. Aina hii ya
ufugaji huweza kumpatia mkulima kipato pamoja na lishe kwa familia, na hauhitaji gharama kubwa.
AINA ZA NGURUWE
Hampshire (USA)
 Wana rangi ya dhahabu – nyeusi na msitari mweupe kuzunguka mabega.
 Mdomo mfupi,masiko makubwa na yametazama nyuma.
 Wana ngozi ngumu na rangi ya kahawia.
 Wanakua haraka, nyama pana na mabega mapana
 Ni wapole
Prepeared by hebron venance
Landrace (Denmark)
 Ni weupe na miili yao ni mikubwa
 Masiko yaliyo anguka na yametazama mbele
 Mdomo mrefu na ulionyooka
 Wanazaa vizuri na vitoto vinakua kwa haraka
 Wanatoa nyama nzuri
 Wanavumilia mazingira magumu na wanahitaji matunzo mazuri.
Prepeared by hebron venance
LARGE WHITE / YORKSHIRE(Yorkshire, England)
 Masikio yaliyo simama, uso mpana na umebonyea ndani na mabega makubwa na mapana
 Wanaathiriwa na jua na wanaweza kuvumilia kwa muda mfupi
 Wanazaa vizuri na watoto wanakua haraka
 Wana miili mirefu na wanatoa protini kwa wingi
SADDLEBACK, England (Essex and Wessex)
 Wana rangi nyeusi na mabaka meupe kuzunguka mabega na miguu ya mbele.
 uso mrefu na ulio nyooka
 Masikio yaliyo anguka
 Saizi ya kati
 Wanauwezo mzuri wa kulea vitoto
 Wazuri kwa kuwafugia nje
Prepeared by hebron venance
NGURUWE WA KIENYEJI
 Ndio wanao patikana kwa kiasi kikubwa nchini
 Wanakua polepole na wanadumaa
 Uzaaji mdogo (5 paka 6 vitoto kwa mzao mmoja)
 Wanavumilia mlo mbovu, magonjwa na wadudu.
 Wakiwa wamekua huwa na miili midogo
 Wanastahimili joto kali na jua
 Midomo yao imenyooka na miguu yenye ncha kali
 Rangi ya ngozi inaweza kuwa nyeusi au nyeusi yenye mabaka
UCHAGUZI WA MBEGU BORA YA NGURUWE
Tabia nzuri za nguruwe wa mbegu.
 Uwezo mkubwa wa kuzaa.
 Anaye sitahimili magojwa na hali ya hewa ya mazingira husika
 Uwezo mzuri wa kukibadilisha chakula na kufanya nyama nzuri inayo pendwa na watu.
 Uwezo mzuri wa kulea watoto.
 Aina ya nguruwe.
 Isiwe na magonjwa ya kurithi.
 Awe na miguu imara na yenye nguvu
 Awe angalau na matiti yasiyo pungua 12 na yawe na mpangilio mzuri.
 Mrefu na awe na misuli imara.
Prepeared by hebron venance
MIFUMO MBALI MBALI YA UFUGAJI WA NGURUWE
KUFUGIA NJE (KUWACHIA HURU)
 Ni ufugaji wa kieneji wenye gharama ndogo na idadi ya nguruwe jike wanaofugwa wanaweza kuwa 1-3.
 Mfumo huu unaendeshwa aidha kwa kuto wapatia chakula cha ziada wanyama wanapo toka kuzunguka
zunguka nje au hupewa chakula kisicho na ubora.
 Ni mfumo wa ufugaji usio na mpangilio maalumu.
 Nguruwe wa kienyeji ndio wanaofugwa kwa kiasi kikubwa na huwa wanachiwa huru kuzunguka.
 Ukuaji na uzalishaji wake ni mdogo ukiambatana na vifo vingi
 Wanyama huwa na wadudu wengi katika miili yao
 Mara nyingi ni kwaajili ya kuipatia familia mahitaji yao. Ni rahisi kwa nguruwe kupata magonjwa na
wadudu.
NUSU NDANI NUSU NJE
 Nguruwe wanafungiwa kwenye mabanda nyuma ya makazi na mara nyingine wanaruhusiwa kutoka nje.
 Wanalisha mabaki ya jikoni, mboga na masalia mengine kama pumba.
 Matunzo ya kawaida
 Mavuno madogo na kiasi kikubwa cha vifo
 Nguruwe wano fugwa ni wale wa kienyeji na chotara
 Mavuno ni makubwa kwa kiasi ukilinganisha na wale wanao fungwa kwa kuachiwa huru.
KUFUGIA NDANI
 ni ufugaji wa kisasa ambapo wanyama wanafungiwa ndani na hawaruhusiwi kutoka nje
 uzalishaji kwaajili ya biashara mkulima huwa na nguruwe kuanzia hamsini na kuendelea
 chakula kinacho tumika ni bora na huwa chakula cha kununuliwa.
 mabanda mazuri na yenye nafasi ya kutosha
 matunzo makubwa yanayopelekea mavuno mazuri
 nguruwe si rahisi kupata magonjwa na wadudu.
 mara nyingi nguruwe wa kigeni na wa kienyeji wanaofanya vizuri
 masoko ni mabucha ya kawaida (kienyeji)
Prepeared by hebron venance
Picha hapo juu inaonyesha ufugaji wa nguruwe kwa kuwachia nje (picha 1) na kufugia ndani kwa ujumla
bila kuwaachia nje (picha 2).
Picha hapo juu inaonyesha mfumo wa ufugaji wa nguruwe kwa kuwachia huru au kuwafungia nje.
UJENZI WA BANDA LA NGURUWE
Sehemu ya kujenga banda la nguruwe.
• Eneo liwe linafikika kwa urahisi.
• Iwe ni sehemu ambayo haituamishi maji.
• Iwe nisehemu ambayo iko mbali kidogo na makazi ya watu.
• Liwe ni eneo ambalo halipigwi na mionzi ya jua moja kwa moja)
• Eneo liwe na maji ya kutosha kwaajili ya usafi wa mabanda
Ujenzi wa banda bora la nguruwe
• Inashauliwa banda la nguruwe liwe na 25 sentimita za urefu; 1.5 mita za mraba kwa nguruwe mmoja mkubwa
ambaye ni jike na banda liwe limeezekwa.
Prepeared by hebron venance
• Eneo la kutosha kwaajili ya maji ya kunywa, chakula na kufanya usafi
• Unapo jenga zingatia mwelekeo wa upepo ili kusaidia mzunguko wa hewa ndani ya banda.
• Banda bora ni lile lililo ezekwa kwa nyasi au mianzi ili kupunguza joto ndani. Endapo banda litaezekwa kwa
bati upande wa juu wa bati unatakiwa upakwe rangi nyeupe na kuta zake lazima ziwe ndefu (2.4-3.0m kwenda
juu na 1.8-2.1m kutoka chini) ili kusaidia mzunguko wa hewa kwenye banda
• Nguruwe wanahitaji kuwa na banda lililojengwa kwa vifaa nafuu. Unaweza kutumia mchanga na simenti
kuweka sakafu, ama ukatumia udongo wa mfinyanzi kwa ajili ya kuweka sakafu. Ukubwa wa banda
unategemeana na idadi ya nguruwe unaotaka kufuga. Mita 3 kwa mita 2.5 zitawaweka guruwe 8-10
wanaonenepeshwa kwa soko au nguruwe jike mmoja na nguruwe ndume mmoja.
ZINGATIA: Usafi ni muhimu katika banda ili kuepuka magonjwa.
Picha hapo juu inaonyesha Mabanda ya nguruwe yanavyo onekana kwa ndani
Picha hapo juu ni banda la nguruwe linavyo onekana kwa nje.
Prepeared by hebron venance
Malisho
Ulishaji wa nguruwe ni rahisi kwa kuwa wanakula aina mbalimbali za vyakula kulingana na mazingira
wanayofugwa. Unaweza kuwalisha kwa kutumia majani laini ya aina mbalimbali, na pia hulishwa kwa kutumia
masalia ya nafaka (pumba). Unaweza kuwalisha kwa kutumia mashudu na pumba. Pia unaweza kuwalisha kwa
kutumia mabaki ya jikoni.
Kuzaliana
Nguruwe hubeba mimba kwa kipindi cha siku 114, ambazo hugawanyika kwa miezi 3, wiki 3 na siku 3. Nguruwe
mmoja ana uwezo wa kuzaa watoto 9 hadi 14 kwa mara moja. Watoto wa nguruwe (piglets) huanza kula chakula
cha kawaida wanapofika umri wa mwezi mmoja na nusu mpaka miezi miwili. Endapo nguruwe watapata matunzo
mazuri, baada ya miezi 6-8 wanakuwa na uzito kati ya kilo 90-120 na wanaweza kuuzwa.
Matunzo
Baada ya nguruwe kuzaa siku ya kwanza asipewe kitu chochote ila apewe maji ya kutosha, baada ya hapo
anatakiwa kupatiwa chakula cha kutosha na cha kutia nguvu ili kupata maziwa ya kutosha kwa ajili ya watoto
wake. Watoto wa nguruwe wachomwe sindano ya madini ya chuma (Iron injection) baada ya siku moja au mbili
toka kuzaliwa. Hii ni muhimu sana vinginevyo wanaweza kufa wote. Kata meno (tooth clipping) baada ya miezi
mitatu. Unaweza kuhasi madume (castration) baada ya miezi miwili.
MAGONJWA YANAYOATHIRI NGURUWE
Kuna aina nyingi za magonjwa yanayoshambulia nguruwe, lakini yapo yale yaliyozoeleka ambapo ni lazima
kukabiliana nayo ili kuwa na ufugaji wenye tija.
Ugonjwa wa miguu na midomo
Ugonjwa huu huathiri nguruwe sehemu za miguu na midomo. Ni ugonjwa ambao hushambulia nguruwe mara kwa
mara hasa wasipokuwa na matunzo mazuri. Ugonjwa wa miguu na midomo, hudhoofisha nguruwe kwa haraka
sana, ikiwa ni pamoja na kupungua uzito.
Chanjo: Chanjo kwa ajili ya ugonjwa wa midomo na miguu (FMD vaccine) hutolewa kila baada ya mwaka mmoja.
Hii inasaidia kuwaweka nguruwe wako katika hali nzuri zaidi bila kushambuliwa na magonjwa hayo.
Tiba: Ugonjwa huu hauna tiba halisi. Inapotokea nguruwe wakawa wameshambuliwa kinachofanyika ni kutibu
magonjwa nyemelezi kwa kutumia antibiotics.
Homa ya Nguruwe (Swine fever)
Virusi vinavyosababisha ugonjwa wa homa ya nguruwe huenea kwa haraka sana miongoni mwa makundi ya
nguruwe, na huua kwa haraka sana, lakini hauna madhara kwa binadamu na hauambukizwi kwa binadamu.
Nguruwe walioambukizwa waanshikwa na vindonda ama mapunye kwenye ngozi. Pia masikio na ngozi huwa
mekundu.
Chanjo: Ugonjwa huu hauna chanjo wala tiba. Kinachofanyika mlipuko unapotokea ili kuwa salama ni
kuwateketeza nguruwe wote walioathirika na kuanza upya. Unaweza kuteketeza kwa kuwachoma moto.
Prepeared by hebron venance
 Muhimu: Baada ya kuwateketeza nguruwe wagonjwa, safisha banda kisha nyunyiza dawa aiana ya Acon au
Ectomin, na uache banda wazi kwa kipindi cha wiki moja kabla ya kuweka nguruwe wengine.
 Ugonjwa wa mapafu (Pneumonia)
Huu ni ugonjwa unaoshambulia sehemu za koo na mapafu ya nguruwe, ambapo husababisha kukohoa na
kupumua kwa shida. Ugonjwa huu husababishwa na bacteria (Secondary bacterial), joto kupita kiasi, vumbi
na gesi inayotokana na madawa makali.
Tiba: Homa ya mapafu kwa nguruwe inatibika kwa kutumia antibiotics. Pamoja na kuwaweka wanyama
sehemu safi, isiyo na baridi kali au joto la kupitiliza kiwango.
 Kimeta (Anthrax)
Huu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria wanaojulikana kama Bacillus anthracis, wadudu hawa
wanabaki kuwa hai kwa muda mrefu na wanaweza kuwa kwenye udongo wakiwa hai kwa kipindi cha miaka
mingi.
Chanjo: Chanja nguruwe wako dhidi ya kimeta kama utakavyoelekezwa na wataalamu wa mifugo walio
karibu nawe.
Tiba: Unaweza kutibu nguruwe wako kwa kutumia dawa aina ya Penisilin au Oxytetracycline.
Muhimu: Homa ya nguruwe ni lazima iwekewe karatini kwa sababu husambaa kwa haraka sana. Nchini
Tanzania mlipuko wa homa ya nguruwe umekuwa ukitokea mara kwa mara maeneo ya mpakani mwa
Tanzania na Malawi na katika mkoa wa Mbeya.

More Related Content

What's hot

Family breakdown
Family breakdownFamily breakdown
Family breakdownsahar18
 
Descent Units and Groups
Descent Units and GroupsDescent Units and Groups
Descent Units and GroupsPaulVMcDowell
 
Functional and dysfunctional families
Functional and dysfunctional familiesFunctional and dysfunctional families
Functional and dysfunctional familiesNilu Thapa
 
Inequality, Economic Growth and Development
Inequality, Economic Growth and DevelopmentInequality, Economic Growth and Development
Inequality, Economic Growth and Developmenttutor2u
 
Family & Marriage
Family & MarriageFamily & Marriage
Family & MarriageJ_Wheat
 
Family, A social institution
Family, A social institution Family, A social institution
Family, A social institution Ayesha Rana
 
Concept of community "What is community" Concept about it
Concept of community "What is community" Concept about itConcept of community "What is community" Concept about it
Concept of community "What is community" Concept about itProfessor5G
 
Social Case work in De-addiction Centre
Social Case work in De-addiction CentreSocial Case work in De-addiction Centre
Social Case work in De-addiction CentreZaeem Jifri
 
Population explosion causes and its consequences
Population explosion causes  and its consequencesPopulation explosion causes  and its consequences
Population explosion causes and its consequencesSrinivas Gajjela
 
POVERTY AND THEORIES USED TO EXPLAIN POVERTY
POVERTY AND THEORIES USED TO EXPLAIN POVERTYPOVERTY AND THEORIES USED TO EXPLAIN POVERTY
POVERTY AND THEORIES USED TO EXPLAIN POVERTYDevine Espante
 

What's hot (20)

Youth social work
Youth social workYouth social work
Youth social work
 
Kinship
KinshipKinship
Kinship
 
Kinship and family
Kinship and familyKinship and family
Kinship and family
 
Poverty
PovertyPoverty
Poverty
 
Family breakdown
Family breakdownFamily breakdown
Family breakdown
 
Descent Units and Groups
Descent Units and GroupsDescent Units and Groups
Descent Units and Groups
 
Measurements of poverty
Measurements of povertyMeasurements of poverty
Measurements of poverty
 
Functional and dysfunctional families
Functional and dysfunctional familiesFunctional and dysfunctional families
Functional and dysfunctional families
 
Sociology
SociologySociology
Sociology
 
Inequality, Economic Growth and Development
Inequality, Economic Growth and DevelopmentInequality, Economic Growth and Development
Inequality, Economic Growth and Development
 
Family & Marriage
Family & MarriageFamily & Marriage
Family & Marriage
 
Family society
Family societyFamily society
Family society
 
Family, A social institution
Family, A social institution Family, A social institution
Family, A social institution
 
Changing structure of family
Changing structure of familyChanging structure of family
Changing structure of family
 
Concept of community "What is community" Concept about it
Concept of community "What is community" Concept about itConcept of community "What is community" Concept about it
Concept of community "What is community" Concept about it
 
Social Case work in De-addiction Centre
Social Case work in De-addiction CentreSocial Case work in De-addiction Centre
Social Case work in De-addiction Centre
 
Population explosion causes and its consequences
Population explosion causes  and its consequencesPopulation explosion causes  and its consequences
Population explosion causes and its consequences
 
POVERTY AND THEORIES USED TO EXPLAIN POVERTY
POVERTY AND THEORIES USED TO EXPLAIN POVERTYPOVERTY AND THEORIES USED TO EXPLAIN POVERTY
POVERTY AND THEORIES USED TO EXPLAIN POVERTY
 
DEFINITIONS
DEFINITIONSDEFINITIONS
DEFINITIONS
 
Culture
CultureCulture
Culture
 

Nguruwe ni mnyama mwenye faida

  • 1. Prepeared by hebron venance UFUGAJI WA NGURUWE Nguruwe ni mnyama mwenye faida, ni rafiki kwa mazingira na hahitaji gharama kubwa. Katika nchi nyingi zinazo endelea ikiwemo Tanzania kiasi kikubwa cha nyama kinatokana na wanyama wenye matumbo Zaidi ya moja kama ng’ombe, mbuzi, kondoo, nk. Kutokana na kukua na kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya watu kunaumuhimu mkubwa wa mabadiliko ya vyanzo vya nyama ili kuweza kukidhi mahitaji ya idadi kubwa ya ongezeko hilo la watu. Moja ya chazo kizuri na kinacho weza kupunguza uhaba wa nyama kwa muda mfupi ni pamoja na nguruwe ambao wanakuwa kwa muda mfupi, wanatupatia protini nyingi, gharama zake za uzalishaji si kubwa sana kwani wanatumia aina nyingi za vyakula kulingana na mazingira husika na pia wanaweza kuzaliana kwa vingi kwa muda mfupi. Mfano nguruwe anaweza kufikisha kilo 90-120 akifugwa vizuri ndani ya miezi sita(6) na hivyo tayari kwa kuchinjwa kwaajili ya nyama, na kwa mzao mmoja anaweza kuzaa vitoto 9-14 ambapo kwa mwaka anazaa mara mbili hivyo twaweza kupata vitoto 14-24 kwa mwaka.
  • 2. Prepeared by hebron venance Jamii nyingi hapa Tanzania huchukulia nguruwe kama mnyama mchafu na asiyefaa kuwa karibu naye na hata kwa matumizi kama lishe. Zaidi, nyama yake inapendwa na haina madhara kwa afya na inapendekezwa kuliwa zaidi kuliko nyama nyekundu. Unaweza kuanzisha mradi wa nguruwe kwa gharama ndogo lakini baada ya kipindi cha miezi tisa tu ukaanza kujipatia kipato kutokana na ufugaji huo. Ufugaji Kwa kawaida nguruwe wanafugwa na watu wa kada zote, wafugaji wadogo wadogo na hata wakubwa. Aina hii ya ufugaji huweza kumpatia mkulima kipato pamoja na lishe kwa familia, na hauhitaji gharama kubwa. AINA ZA NGURUWE Hampshire (USA)  Wana rangi ya dhahabu – nyeusi na msitari mweupe kuzunguka mabega.  Mdomo mfupi,masiko makubwa na yametazama nyuma.  Wana ngozi ngumu na rangi ya kahawia.  Wanakua haraka, nyama pana na mabega mapana  Ni wapole
  • 3. Prepeared by hebron venance Landrace (Denmark)  Ni weupe na miili yao ni mikubwa  Masiko yaliyo anguka na yametazama mbele  Mdomo mrefu na ulionyooka  Wanazaa vizuri na vitoto vinakua kwa haraka  Wanatoa nyama nzuri  Wanavumilia mazingira magumu na wanahitaji matunzo mazuri.
  • 4. Prepeared by hebron venance LARGE WHITE / YORKSHIRE(Yorkshire, England)  Masikio yaliyo simama, uso mpana na umebonyea ndani na mabega makubwa na mapana  Wanaathiriwa na jua na wanaweza kuvumilia kwa muda mfupi  Wanazaa vizuri na watoto wanakua haraka  Wana miili mirefu na wanatoa protini kwa wingi SADDLEBACK, England (Essex and Wessex)  Wana rangi nyeusi na mabaka meupe kuzunguka mabega na miguu ya mbele.  uso mrefu na ulio nyooka  Masikio yaliyo anguka  Saizi ya kati  Wanauwezo mzuri wa kulea vitoto  Wazuri kwa kuwafugia nje
  • 5. Prepeared by hebron venance NGURUWE WA KIENYEJI  Ndio wanao patikana kwa kiasi kikubwa nchini  Wanakua polepole na wanadumaa  Uzaaji mdogo (5 paka 6 vitoto kwa mzao mmoja)  Wanavumilia mlo mbovu, magonjwa na wadudu.  Wakiwa wamekua huwa na miili midogo  Wanastahimili joto kali na jua  Midomo yao imenyooka na miguu yenye ncha kali  Rangi ya ngozi inaweza kuwa nyeusi au nyeusi yenye mabaka UCHAGUZI WA MBEGU BORA YA NGURUWE Tabia nzuri za nguruwe wa mbegu.  Uwezo mkubwa wa kuzaa.  Anaye sitahimili magojwa na hali ya hewa ya mazingira husika  Uwezo mzuri wa kukibadilisha chakula na kufanya nyama nzuri inayo pendwa na watu.  Uwezo mzuri wa kulea watoto.  Aina ya nguruwe.  Isiwe na magonjwa ya kurithi.  Awe na miguu imara na yenye nguvu  Awe angalau na matiti yasiyo pungua 12 na yawe na mpangilio mzuri.  Mrefu na awe na misuli imara.
  • 6. Prepeared by hebron venance MIFUMO MBALI MBALI YA UFUGAJI WA NGURUWE KUFUGIA NJE (KUWACHIA HURU)  Ni ufugaji wa kieneji wenye gharama ndogo na idadi ya nguruwe jike wanaofugwa wanaweza kuwa 1-3.  Mfumo huu unaendeshwa aidha kwa kuto wapatia chakula cha ziada wanyama wanapo toka kuzunguka zunguka nje au hupewa chakula kisicho na ubora.  Ni mfumo wa ufugaji usio na mpangilio maalumu.  Nguruwe wa kienyeji ndio wanaofugwa kwa kiasi kikubwa na huwa wanachiwa huru kuzunguka.  Ukuaji na uzalishaji wake ni mdogo ukiambatana na vifo vingi  Wanyama huwa na wadudu wengi katika miili yao  Mara nyingi ni kwaajili ya kuipatia familia mahitaji yao. Ni rahisi kwa nguruwe kupata magonjwa na wadudu. NUSU NDANI NUSU NJE  Nguruwe wanafungiwa kwenye mabanda nyuma ya makazi na mara nyingine wanaruhusiwa kutoka nje.  Wanalisha mabaki ya jikoni, mboga na masalia mengine kama pumba.  Matunzo ya kawaida  Mavuno madogo na kiasi kikubwa cha vifo  Nguruwe wano fugwa ni wale wa kienyeji na chotara  Mavuno ni makubwa kwa kiasi ukilinganisha na wale wanao fungwa kwa kuachiwa huru. KUFUGIA NDANI  ni ufugaji wa kisasa ambapo wanyama wanafungiwa ndani na hawaruhusiwi kutoka nje  uzalishaji kwaajili ya biashara mkulima huwa na nguruwe kuanzia hamsini na kuendelea  chakula kinacho tumika ni bora na huwa chakula cha kununuliwa.  mabanda mazuri na yenye nafasi ya kutosha  matunzo makubwa yanayopelekea mavuno mazuri  nguruwe si rahisi kupata magonjwa na wadudu.  mara nyingi nguruwe wa kigeni na wa kienyeji wanaofanya vizuri  masoko ni mabucha ya kawaida (kienyeji)
  • 7. Prepeared by hebron venance Picha hapo juu inaonyesha ufugaji wa nguruwe kwa kuwachia nje (picha 1) na kufugia ndani kwa ujumla bila kuwaachia nje (picha 2). Picha hapo juu inaonyesha mfumo wa ufugaji wa nguruwe kwa kuwachia huru au kuwafungia nje. UJENZI WA BANDA LA NGURUWE Sehemu ya kujenga banda la nguruwe. • Eneo liwe linafikika kwa urahisi. • Iwe ni sehemu ambayo haituamishi maji. • Iwe nisehemu ambayo iko mbali kidogo na makazi ya watu. • Liwe ni eneo ambalo halipigwi na mionzi ya jua moja kwa moja) • Eneo liwe na maji ya kutosha kwaajili ya usafi wa mabanda Ujenzi wa banda bora la nguruwe • Inashauliwa banda la nguruwe liwe na 25 sentimita za urefu; 1.5 mita za mraba kwa nguruwe mmoja mkubwa ambaye ni jike na banda liwe limeezekwa.
  • 8. Prepeared by hebron venance • Eneo la kutosha kwaajili ya maji ya kunywa, chakula na kufanya usafi • Unapo jenga zingatia mwelekeo wa upepo ili kusaidia mzunguko wa hewa ndani ya banda. • Banda bora ni lile lililo ezekwa kwa nyasi au mianzi ili kupunguza joto ndani. Endapo banda litaezekwa kwa bati upande wa juu wa bati unatakiwa upakwe rangi nyeupe na kuta zake lazima ziwe ndefu (2.4-3.0m kwenda juu na 1.8-2.1m kutoka chini) ili kusaidia mzunguko wa hewa kwenye banda • Nguruwe wanahitaji kuwa na banda lililojengwa kwa vifaa nafuu. Unaweza kutumia mchanga na simenti kuweka sakafu, ama ukatumia udongo wa mfinyanzi kwa ajili ya kuweka sakafu. Ukubwa wa banda unategemeana na idadi ya nguruwe unaotaka kufuga. Mita 3 kwa mita 2.5 zitawaweka guruwe 8-10 wanaonenepeshwa kwa soko au nguruwe jike mmoja na nguruwe ndume mmoja. ZINGATIA: Usafi ni muhimu katika banda ili kuepuka magonjwa. Picha hapo juu inaonyesha Mabanda ya nguruwe yanavyo onekana kwa ndani Picha hapo juu ni banda la nguruwe linavyo onekana kwa nje.
  • 9. Prepeared by hebron venance Malisho Ulishaji wa nguruwe ni rahisi kwa kuwa wanakula aina mbalimbali za vyakula kulingana na mazingira wanayofugwa. Unaweza kuwalisha kwa kutumia majani laini ya aina mbalimbali, na pia hulishwa kwa kutumia masalia ya nafaka (pumba). Unaweza kuwalisha kwa kutumia mashudu na pumba. Pia unaweza kuwalisha kwa kutumia mabaki ya jikoni. Kuzaliana Nguruwe hubeba mimba kwa kipindi cha siku 114, ambazo hugawanyika kwa miezi 3, wiki 3 na siku 3. Nguruwe mmoja ana uwezo wa kuzaa watoto 9 hadi 14 kwa mara moja. Watoto wa nguruwe (piglets) huanza kula chakula cha kawaida wanapofika umri wa mwezi mmoja na nusu mpaka miezi miwili. Endapo nguruwe watapata matunzo mazuri, baada ya miezi 6-8 wanakuwa na uzito kati ya kilo 90-120 na wanaweza kuuzwa. Matunzo Baada ya nguruwe kuzaa siku ya kwanza asipewe kitu chochote ila apewe maji ya kutosha, baada ya hapo anatakiwa kupatiwa chakula cha kutosha na cha kutia nguvu ili kupata maziwa ya kutosha kwa ajili ya watoto wake. Watoto wa nguruwe wachomwe sindano ya madini ya chuma (Iron injection) baada ya siku moja au mbili toka kuzaliwa. Hii ni muhimu sana vinginevyo wanaweza kufa wote. Kata meno (tooth clipping) baada ya miezi mitatu. Unaweza kuhasi madume (castration) baada ya miezi miwili. MAGONJWA YANAYOATHIRI NGURUWE Kuna aina nyingi za magonjwa yanayoshambulia nguruwe, lakini yapo yale yaliyozoeleka ambapo ni lazima kukabiliana nayo ili kuwa na ufugaji wenye tija. Ugonjwa wa miguu na midomo Ugonjwa huu huathiri nguruwe sehemu za miguu na midomo. Ni ugonjwa ambao hushambulia nguruwe mara kwa mara hasa wasipokuwa na matunzo mazuri. Ugonjwa wa miguu na midomo, hudhoofisha nguruwe kwa haraka sana, ikiwa ni pamoja na kupungua uzito. Chanjo: Chanjo kwa ajili ya ugonjwa wa midomo na miguu (FMD vaccine) hutolewa kila baada ya mwaka mmoja. Hii inasaidia kuwaweka nguruwe wako katika hali nzuri zaidi bila kushambuliwa na magonjwa hayo. Tiba: Ugonjwa huu hauna tiba halisi. Inapotokea nguruwe wakawa wameshambuliwa kinachofanyika ni kutibu magonjwa nyemelezi kwa kutumia antibiotics. Homa ya Nguruwe (Swine fever) Virusi vinavyosababisha ugonjwa wa homa ya nguruwe huenea kwa haraka sana miongoni mwa makundi ya nguruwe, na huua kwa haraka sana, lakini hauna madhara kwa binadamu na hauambukizwi kwa binadamu. Nguruwe walioambukizwa waanshikwa na vindonda ama mapunye kwenye ngozi. Pia masikio na ngozi huwa mekundu. Chanjo: Ugonjwa huu hauna chanjo wala tiba. Kinachofanyika mlipuko unapotokea ili kuwa salama ni kuwateketeza nguruwe wote walioathirika na kuanza upya. Unaweza kuteketeza kwa kuwachoma moto.
  • 10. Prepeared by hebron venance  Muhimu: Baada ya kuwateketeza nguruwe wagonjwa, safisha banda kisha nyunyiza dawa aiana ya Acon au Ectomin, na uache banda wazi kwa kipindi cha wiki moja kabla ya kuweka nguruwe wengine.  Ugonjwa wa mapafu (Pneumonia) Huu ni ugonjwa unaoshambulia sehemu za koo na mapafu ya nguruwe, ambapo husababisha kukohoa na kupumua kwa shida. Ugonjwa huu husababishwa na bacteria (Secondary bacterial), joto kupita kiasi, vumbi na gesi inayotokana na madawa makali. Tiba: Homa ya mapafu kwa nguruwe inatibika kwa kutumia antibiotics. Pamoja na kuwaweka wanyama sehemu safi, isiyo na baridi kali au joto la kupitiliza kiwango.  Kimeta (Anthrax) Huu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria wanaojulikana kama Bacillus anthracis, wadudu hawa wanabaki kuwa hai kwa muda mrefu na wanaweza kuwa kwenye udongo wakiwa hai kwa kipindi cha miaka mingi. Chanjo: Chanja nguruwe wako dhidi ya kimeta kama utakavyoelekezwa na wataalamu wa mifugo walio karibu nawe. Tiba: Unaweza kutibu nguruwe wako kwa kutumia dawa aina ya Penisilin au Oxytetracycline. Muhimu: Homa ya nguruwe ni lazima iwekewe karatini kwa sababu husambaa kwa haraka sana. Nchini Tanzania mlipuko wa homa ya nguruwe umekuwa ukitokea mara kwa mara maeneo ya mpakani mwa Tanzania na Malawi na katika mkoa wa Mbeya.