Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Implementation of NRM based project in Lushoto district Tanzania
1. Kuboresha mazingira na maisha ya
wakulima katika Bonde Maji la Baga,
mafanikio na mapendekezo
Vijiji vya Mbelei, Kwekitui, Kwadoe, Kwalei,
Kwehangala na Dule.
2. Historia ya AHI
• AHI ilianza 1998 hapa Tanzania katika wilaya ya
Lushoto
• Matatizo makuu yaliyopo (ya raslimali)
– Mmomonyoko mkubwa wa ardhi/udongo
– Uzalishaji mdogo wa mazao na mifugo
- upungufu wa rutuba, mbegu zisizo bora, kilimo
kisichozingatia utaalamu, magonjwa ya mazao na
mifugo,ukosefu wa malisho,
– Vyanzo vya maji kukauka
– masoko yasiyo ya kuaminika
– Ukosefu wa mitaji kwa wakulima
Yamesababisha umaskini na uharibifu wa
mazingira
3. Historia ya AHI
• tukaanza na kuongeza uzalishaji ktk
mashamba
kijiji chote
bonde maji
5. Mikakati tuliyotumia kutatua
matatizo yaliyojitokeza
• Kuchunguza na kutambua matatizo
• Kuweka Mipango ya ufumbuzi
• Utekelezaji
6. Mbinu zilizotumika
Kuchunguza na kutambua matatizo
1.1 Uchunguzi yakinifu wa Bondemaji (WS
characterization)
Zoezi hili lilishirikisha wakulima, watafifi na wadau
mbalimbali kwa kutumia madodoso, mikutano
matembezi mkato nk
• sehemu zilizoathirika (hot spots) zilianishwa
• tuliweza kujua kiasi cha usumbufu waupatao kinamama,
watoto, wazee
• tuliweza kujua miti yenye kuathiri mazao
• Matatizo mtambuka yaliainishwa
7. Mbinu zilizotumika
Kuchunguza na kutambua matatizo
1.2. utafiti wa udongo na mimea ya asili:
– Imetupa hali halisi ya rutuba ya udongo na
viwango vya virutubisho katika mimea ya asili
(tughutu, alizeti mwitu, mshai)
8. 1.3. Utafiti wa uhusiano kati ya miti na
maji:
• Utafiti wa kitaalamu na kiasili umetumika
kupata miti iliyo rafiki na yenye athari kwa maji.
• Tumeweza kuthibitisha kuna miti inaathiri
mazao
• Watu waliokuwa wakitofautiana wameweza
kuwa na utamaduni wa kukaa pamoja na
kuondoa tofauti zao.
9. Takwimu zilizopatikana kwa kutumia mbinu
hii zilitumika katika mikutano ya marejesho
• vijiji vilijisikia wamoja, wenye matatizo
yanayofanana na yenye kuhitaji ufumbuzi wa aina
moja
• wakulima walihamasika na kukubali kubadilika
10. 2. Kuweka mipango: (Planning)
2.1 Mipango shirikishi ya kijiji ikilenga mipango
ya bonde maji
– Wakulima walijiundia vikundi vyao vya kazi za pamoja
(mf. kamati ya mazingira,
– Waliunda kamati za vijiji kuhamasisha na kuratibu
shughuli zao
– Kwalei waliunda SACCOs - 2001/2 na mtaji wa
30,000 Tsh
– hii ilileta ushindani
2.2. Mipango shirikishi ya bonde maji
- kuundwa kamati ya mazingira ya bonde maji.
- SACCOs ya Kwalei ilipanuka na kuwa ya Bondemaji
11. 2.3. kuunda mkakati wa
kurejesha na kutunza
vyanzo vya maji
• wakulima walichangia
mawe, mchanga, miti,
nguvu kazi,
• walifufua sheria
ndogondogo zilizo
kuwepo.
• Moyo wa kufanya kazi
pamoja na ushindani kati
ya kijiji na kijiji
uliongezeka
12. 3. Utekelezaji: (Implementation)
3.1 Majaribio ya kuhakiki teknolojia
Vishamba vya Maonyesho
– Tunatoa takwimu za kuhakiki
– Tunafanya mchanganuo wa kiuchumi
– Takwimu hizo zinatumika kutengeneza vipeperushi,
vijarida
– Kuzalishia mbegu/miche bora
3.2. Kuifanya jamii kuwa na umoja kwa
kuwawezesha kielimu,
– kuwasaidia kuanzisha chama cha kuweka na kukopa
(SACCOS) na kuwapatia mafunzo.
13. 3.3. Kilimo-Biashara:
– Mradi uliwaunganisha wakulima na masoko
• Kuwapeleka wakulima kwenye masoko
• Kupata taarifa za masoko na
• kuongeza thamani ya bidhaa za kilimo kwa
kupanga mazao kwa madaraja
• utafutaji wa masoko mapya.
• Mazao bora yanayokidhi matakwa ya soko
nyanya, kabichi, migomba
14. 3.4. Semina na mafunzo:
– Wakulima watafiti 40 (paraprofessionals)
– Tekinolojia za kuongeza tija (integrated)
– Wakulima kuzalisha mbegu za mahindi,
nyanya, maharage, migomba
– Ziara za mafunzo, ndani na nje ya wilaya, nje
ya mkoa na nchi jirani ya Kenya
15. 3.5. Ufuatiliaji na tathmini shirikishi
(PM&E)
– wakulima wamefundishwa kufanya tathmini
na wanaitumia elimu hiyo kuboresha shughuli
zao
3.6. Ushirikishaji wa taasisi zingine katika
utekelezaji wa shughuli za mradi
- Tunahusisha taasisi zingine kwenye
utekelezaji vijijini (eg. TAFORI, Lishe Trust,
TIP, Extension) katika kutoa mafunzo na
kubadilishana uzoefu
16. 3.7. Hifadhi za mazingira;
– vyanzo vya maji vimehifadhiwa kwa
ushirikiano na wakulima.
– Wakulima wameimarisha sheria ndogondogo
– wameanzisha vitalu vya miti ya asili ambayo
ni rafiki wa maji.
– Wakulima kwa wakulima wanapimiana
makingamaji, terasi nk.
17. 3.8. Kufanya utafiti wa matatizo ambayo hayana
uthibitisho wa kisayansi na hayana utatuzi mpaka
sasa:
– Athari za miti kwenye mazao na maji
– Utafiti wa mazao mbalimbali ya kanda za juu
– Utafiti kutoka machapisho mbalimbali ili kupata miti
bora zaidi kwa vyanzo vya maji na mazingira yetu.
– Utafiti wa kuainisha ni jinsi gani uhifadhi wa vyanzo
vya maji umempunguzia mama na mtoto mzigo wa
kutafuta maji, umeboreshaje maisha ya kaya.
– Kutafiti njia bora za kufikia wakulima
18. 4. Mafanikio:
• Vyanzo vya maji
32 vimehifadhiwa
na kujengewa
19. • m 74,000 za
miundo mbinu za
kuhifadhi udongo
20. • SACCOS imekuwa na mtaji wa shilingi
32,000,000, ina wanachama 170 na kiwango
cha mkopo ni 120m.
• 80% ya wakulima wa nyanya wanatumia
Tengeru na Tanya.
– 70% ya wakulima wa mbogamboga
wanatumia mbinu bora za kurutubisha ardhi.
21. • Wakulima-wataalamu wanawafundisha
wakulima wenzao ndani ya Bonde maji
• Baadhi ya wakulima-wataalamu kutoka Baga
wamefundisha wakulima wenzao kama vile
Moshi na Makanya.
• Muda wa kuchota maji umepungua toka masaa
saba mpaka ¼ saa kwa sehemu nyingi.
• maisha ya wakulima yameboreka.
– Wamenunua magari, mashamba, baiskeli, mabati,
ada za shule, lishe imeongezeka nk.
22. • Wakulima wengi
wanafuata matakwa
ya soko (market
demand) katika
kuzalisha mazao.
23. • Sheria ndogo ndogo sasa zimefanya kazi kwa baadhi ya
vijiji (mharibu wa mazingira amefungwa mwaka 1.5)
• Uelewa wa matatizo ya mazingira umekuwa mkubwa.
• Vitalu vya miti isiyo na athari kwa vyanzo vya maji na
mazao imeanzishwa (Mbelei vitalu viwili, Kwadoe 2,
Kwekitui 1).
24. 5. Matatizo:
• Upokeaji mdogo wa teknolojia hususani za kuhifadhi
ardhi
– pendekezo - sheria ziwawajibishe wasiohifadhi
• Sheria ndogondogo kutofanya kazi ipasavyo (adhabu
hazilingani na makosa mfano kifungo cha nje cha miezi
6 lakini mkulima akarudia na kufanya makosa yaleyale)
– Pendekezo – adhabu ziwe kali zaidi
» - sheria fuatiliwe zaidi na wahusika
• Masoko hayana uhakika na bei ndogo za mazao.
- pendekezo – wilaya iweke na kutekeleza mikakati ya
kuendeleza usindikaji na kutafuta masoko
25. • Uwezeshwaji mdogo wa watafiti, wanaughani.
• Wakulima wengi kukosa mwamko wa kujitegemea
• Wakulima wengi kukosa mwamko wa kilimo-biashara
26. • Bado tunaendelea kuongeza uzalishaji ktk
mashamba
kijiji chote
bonde maji
wilaya nzima
Twahitaji nguvu zaidi, wadau zaidi,