Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
TAARIFA YA UFUNGUZI WA MRADI WA TIMIZA MALENGO.doc
1. TAARIFA YA UFUATILIAJI WA MRADI WA TIMIZA MALENGO (MABINTI BALEHE NA
WANAWAKE VIJANA)
Lengo la mradi huu ni kuhakikisha mabinti balehe na wanawake vijana wanawezeshwa kupata pesa kwa ajili ya
michakato tofauti ya biashara
Mkoa wa Morogoro una Halmashauri 9, mradi huu ulifanyika katika mkoa wa Morogoro umehusisha Halmashauri 5 tu ambazo ni
Morogoro Mjini , Ifakara, Mlimba, Ulanga na Malinyi.
HALI HALISI BAADA YA UFUATILIAJI
HALMASHAURI
IDADI
LENGWA
WALIO
NA
ACCOUNT
AKAUNTI
ZILIZOLALALA
WASIO
NA
ACCOUNT
MAOMBI
MAPYA
YA
PESA
WALIO
POKEA
PESA
AWAMU
YA
I
WALIOHAMA
MAKAZI
WALIOFARIKI
WATOTO
WENYE
NIDA
WASIO
NA
NIDA
MAOMBI
YA
VYETI
VYA
KUZALIWA
YALIYOPELEKWA
RITA
MORO MC 1616 1577 94 39 955 517 8 3 700 . HAWA-
KUFANYA ZOEZI
IFAKARA 2071 1326 526 745 - - - - 1100 526 427
MLIMBA 1287 953 287 30 622 HANA IDADI
KAMILI
HANA
TAARIFA
65 157 93
ULANGA 1010 752 130 247 280 472 HANA IDADI
KAMILI
HANA
TAARIFA
187 157 157
MALINYI 927 310 .. 82 228 5 .. 43 107 96
2. MAFANIKIO
Idadi kubwa ya walengwa wamefungua akaunti kwa kutumia barua ya serikali ya
mtaa na maombi maalumu kwa ma meneja wa matawi ya banki ikiwa kama akaunti ya
muda ndani ya miezi 6 isipokuwa itakuwa endelevu pale tu atakapopata namba ya
nida/cheti cha kuzaliwa baadhi wamefungua kwa kutumia namba ya nida na cheti cha
kuzaliwa akaunti hizo ni za kudumu.
CHANGAMOTO
MOROGORO
Walengwa wengi walishindwa kupata namba za Nida kwa sababu hawakuwa na vyeti
vya kuzaliwa.
Ililazimika kuomba Bank kufungua akaunti za muda kwa kutumia barua za serikali za
mtaa kwa kuwa Walengwa wengi hawakuwa na namba za nida/vyeti vya kuazaliwa .
ULANGA
Baadhi ya walengwa waliongiziwa fedha wameshindwa kutoa kutokana na makosa
tofauti tofauti mfano majina kutofautina Bank na Nida n.k.
Baadhi ya walengwa hawana viambatanisho kwa ajili ya kuomba cheti cha kuzaliwa
imepelekea baadhi mpaka sasa hazijapelekwa Rita zinasubiria viambata.
Mratibu katika kufuatilia Akaunti amekuta Akaunti 120 bado hazijaingiziwa fedha na
hawajui sababu ni nini.
MLIMBA
Baadhi ya walengwa hawajui umri wao pia baadhi ya wazazi hawana kitambulisho cha
kura/namba ya Nida.
IFAKARA
Wakati wa usajili Nida/cheti cha kuzaliwa/Barua kwa lengwa kulikuwa na shida ya
umeme baadhi ya kata ilibidi kukodi generator.
Uelewa mdogo wa walengwa umechangia kutofanikisha lengo hili kwa kiasi kikubwa.
MALINYI
3. Walengwa wengi hawa kuwa na vyeti vya kuzaliwa Vilevile awakuwa na nyaraka zinazo hotajika
iliwaweze kupata vyeti vya kuzaliwa na hii imepelekea walengwa 163 mpka sasa bado
wanasubiriwa kuleta viambatanisho na NIDA
Baaddhi ya Walengwa wengi wanapoitwa wanakataa na wa naona ni usumbufu kwasababu
zoezi inachukua muda mrefu bila mafanikio.
CHANGAMOTO ZA JUMLA
Kutokana na mradi kukaa muda mrefu tangu walengwa walipopewa mafunzo
wengi wao wamehama makazi kutoka nje kabisa ya Kata/Halmashauri zao mfano
kuolewa, kutafuta kipato nk.
Kipindi hiki si rafiki kwa kuwa ni kipindi cha kilimo hivyo walengwa waliopata
mafunzo wamehamia mashambani kulima mashamba yao/kufanya vibarua.
Wahusika wa kuwafatilia walengwa (Walimu) katika kila kata ambao wangeweza
kuwatafuta wanafunzi wao (walengwa) kwa kuwa hawakuwezeshwa/
hawakulipwa wanasuasua kuendelea na zoezi na imekuwa vigumu kwa Mratibu
kuwapata wanafunzi ambao hawapo/waliohama/waliosafiri/waliofariki n.k.
ukizingatia Mratibu hana mawasiliano ya mtu mmoja mmoja.
Ukosefu namba za Nida/cheti cha kuzaliwa imepelekea kupunguza kasi ya
ufunguzi wa akaunti za kudumu vile vile walengwa wengi kufunguliwa akaunti za
muda.
Walengwa wengi hawana uelewa/kujua umuhimu wa cheti cha kuzaliwa hivyo
wengi hawana vyeti hivyo.
Shirika limeingiza pesa kwa walengwa bila kutoa taarifa kwa waratibu wa zoezi
hivyo watu wengi (walengwa) baada ya kutoa wamebadili matumizi. Mratibu
alipopata taarifa/alipofatilia alikuta walengwa wengi wameshatumia fedha hizo
kinyume na malengo.
MAPENDEKEZO
4. 1. Mwalimu kwenye kila kata wawezeshwe/walipwe ili kufanya zoezi ifanyike kwa ufanisi, maana wao
ndio wapo karibu na walengwa, wao ni rahisi kuwa pata walengwa bila kusahau waingiza data pia.
2. Walengwa wakiwekewa pesa ni vema waratibu wapewe taarifa ili waweze kuwasiliana na walimu na
kufanya kufwatilia wa pamoja ili walengwa watume pesa katika lengo husika.
3. Mazoezi kama haya yasichukue muda mrefu baada ya mafunzo. Maana apeleke wahusika kukaa
tamaa, vile vile yasifanyike wakati wa masika kwani watu wengi katika maeneo haya wanakuwa
wamehamia mashambani na wanakuwa bize kwenye kilimo.
Naomba kuwasilisha.