1. 27, FEBRUARY 2017
TANZANIA RANGELANDS
STUDENTS’ ASSOCIATION (TRSA)
MADA: MATUMIZI YA
MACHUNGA TANZANIA, JE
NI ENDELEVU?
2. YALIYOMO
1. Utangulizi
2. Hali halisi ya
machunga nchini
3. Faida za machunga
4. Changamoto
zinazokabili maeneo
ya machunga
5. Mapendekezo ya
utatuzi wa
changamoto za
machunga
6. Hitimisho
3. UTANGULIZI
Eneo kubwa la machunga ya mifugo na
wanyama pori hapa nchini lipo katika nyanda
kame.
Eneo hili ni takribani asilimia 40 ya ardhi yote
ya nchi ambayo ni hekta milioni 94.
Wastani wa mvua kwa mwaka ni milimita 250
hadi 500 kwa mwaka.
Japokuwa wakati mwingine mvua hufikia
wastani zaidi ya milimita 500 kwa mwaka,
lakini hali hii hutokea mara chache (miaka 5 kati
ya miaka 30).
4. UTANGULIZI
Eneo la machunga hukumbwa
na mvukizo (evaporation) kwa
kiasi kikubwa.
Mvukizo katika maeneo ya
ukame ni karibia mara nne ya
mvua inayonyesha
Kwa kawaida maeneo hayo
kulingana na hali ilivyo
elezwa hapo juu yanafaa kwa
kuchungia wanyama na sio
kwa kulima mazao.
5. HALI HALISI YA MACHUNGA NCHINI
Maeneo mengi ya
machunga yamevamiwa
na shughuli za kilimo kwa
sababu ya ukosefu wa
utambuzi wa machunga
kisheria.
Miundombinu katika
maeneo ya machunga
kama vile majosho,
malambo na mapalio ya
kupitishia mifugo haikidhi
mahitaji ya mifugo.
6. HALI HALISI…
Maeneo mengi ya nyanda za
malisho yanatumiwa kiholela
kwa kilimo cha kuhamahama
kisichohifadhi udongo na
maji, kuvuna mbao bila
mpangilio na kuchoma mkaa.
Maeneo mengi yamejaa
vichaka na mimea vamizi
kutokana na ukosefu wa
usimamizi fasaha katika
machunga kama vile kudhibiti
vichaka na mimea vamizi.
7.
8. HALI HALISI……
Kwa hali hiyo machunga
mengi yamepoteza ubora, uoto
wa asili unapotea kwa kasi
hivyo basi maeneo mengi
yamejaa vipara ( bare land),
kwa hiyo hali hii inasababisha
mmomonyoko wa udongo na
kupelekea kuwepo kwa
makorongo.
• Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi kwa sasa,
machunga mengi yamepoteza uoto, hivyo malisho
kwa wanyama yanapungua sana.
9. CHANGAMOTO ZINAZOKABILI MAENEO YA
MACHUNGA.
Ongezeko la watu linapelekea
kubadili utumiaji wa ardhi ya
machunga kuwa maeneo ya
kilimo na makazi.
Mabadiliko ya tabianchi
yamesababisha upungufu
mkubwa malisho na maji kwa
wanyama.
Kubadili matumizi ya ardhi
kama vile kilimo, uwekezaji na
maeneo ya hifadhi za wanyama
pori.
10. CHANGAMOTO….
Maeneo mengi ya machunga
bado yanakabiliwa na uwepo wa
magonjwa pamoja na wadudu
waenezao magonjwa kama vile
kupe na ndorobo.
Utekelezaji wa sera zinazowezesha utambuzi na
umiliki wa machunga kisheria ni dhaifu. Mfano
Sheria no 13 ya mwaka 2010 haina meno makali ya
kumpa nguvu Waziri kutangaza maeneo kuwa
hifadhi ya Malisho (Gazzeted Grazing reserves).
11. CHANGAMOTO …
Upungufu wa miundombinu kama
vile majosho na malambo, hivyo
husababisha mtawanyiko usio
sahihi wa wanyama
Upungufu wa wataalamu wa
usimamizi wa machunga hivyo
inasababisha kutokuwa na
usimamizi mzuri katika machunga.
Wataalum wanazalishwa SUA
lakini bado hawajaajiriwa.
12. MAPENDEKEZO
1. Kuboresha miundombinu katika maeneo ya
machunga kama vile majosho, mapalio na
malambo.
2. Kupeleka wataalamu wa nyanda za malisho kwa
ajili ya usimamiaji wa matumizi bora ya ardhi ili
kuyafanya endelevu.
3. Matumizi bora ya ardhi yanayozingatia matumizi
endelevu ya rasilimali ardhi (proper land use
planning).
4. Uondoaji vichaka na mimea vamizi katika
machunga ifanyike ili kuongeza uzalishaji wa
malisho.
13. Mapendekezo….
5. Kuwe na ushirikishwaji wa wadau kutoka sekta
mbalimbali kama vile wataalamu wa mifugo, tiba ya
wanyama na misitu/ hifadhi.
6. Sheria na 13 ya mwaka 2010 iboreshwe ili kumpa
Waziri mwenye dhamana nguvu ya kusajili na
kutangaza Grazing reserves.
7. Kuwe na vikao vya ushirikishwaji wa sekta zote
zinazohusiana na matumizi na uendelezaji wa ardhi.
14. Mapendekezo…
8. Kuwe na tathimini yakinifu katika maeneo ya
machunga ili kuweza kujua rasilimali halisi
zilizopo katika maeneo ya machunga.
9. Kuimarisha huduma za tiba ya mifugo katika
maeneo ya machunga ili kuzuia uenezaji wa
magonjwa ya mifugo pamoja na wadudu
waenezao magonjwa kwa kuongeza
wataalamu .
15. HITIMISHO
Kutokana na hali halisi na changamoto
zilizopo katika machunga ni dhahili
kwamba machunga katika nchi yetu si
endelevu .
Hivyo juhudi za makusudi zinahitajika
ili kunusuru na kuboresha hali ya
nyanda za malisho hapa nchini.