SlideShare a Scribd company logo
1 of 3
DADA YANGU SURA YA ..1..
By Adela Dally Kavishe in UWANJA WA SIMULIZI · Edit Doc
Mapenzi ni kitu ambacho kimechukua nafasi kubwa sana katika maisha ya watu
kote duniani. Mapenzi haya yanaweza kuleta furaha sana endapo mtu atampata
mtu sahihi ambaye atakuwa ni muwazi, mwenye mapenzi ya kweli na kuheshimu
uhusiano huo. Lakini mapenzi yanaweza kuleta karaha au kukosa amani kabisa
kama kutakuwa na migogoro ambayo unakuta inasababishwa na kukosa uaminifu
na kuleta ugomvi kati ya wawili wapendanao. Mapenzi haya yanaweza
yakasababisha ndugu kugombana, marafiki kukosana na hata kuuana.
*****
Eliza na Upendo ni wasichana warembo waliozaliwa katika familia ya kitajiri
mkoani Morogoro. Wasichana hawa waliishi katika maisha ya kifahari kutokana na
Baba yao Mzee Bondi kuwa na uwezo mkubwa sana kifedha. Mzee Bondi
aliwapenda sana mabinti zake na alipenda wasome kwa bidii ili baadaye waje
kuwa na maisha bora. Eliza na Upendo walisoma katika hali nzuri sana hadi
kufikia elimu ya chuo, ambapo Upendo alikuwa akisoma Chuo Kikuuu cha Dar es
salaam na Eliza Chuo cha Uhasibu Arusha. Kutokana na masomo walitengana na
kuonana mara chache kipindi cha likizo.
Baadaye Eliza na Upendo walijikuta wakijiingiza katika uhusiano wa kimapenzi
wote wawili kwa kijana mmoja mtanashati aliyeitwa James bila kujijua. Uhusiano
wa kimapenzi kwa mwanamume mmoja ulileta migogoro katika familia yao.
*********
Baada ya kumaliza Kidato cha Sita Upendo alipangiwa kwenda kuendelea na
masomo ya Chuo Mkoa wa Dar es salaam. Baba yake alifurahi sana na kumuahidi
kuwa angempa zawadi nono kama angefanya vizuri akiwa Chuo. Kabla ya
kujiunga na chuo Upendo alifanyiwa sherehe kubwa ya kumpongeza, ambayo
ilihudhuriwa na watu wengi sana ndugu jamaa na marafiki. Wakati huo mdogo
wake Eliza alikuwa Kidato cha Sita kwani walipishana mwaka mmoja tu na kwa
jinsi walivyokuwa, walionekana kama mapacha. Wakati mwingine ilikuwa ni
vigumu kwa watu ambao walikuwa hawajawaona kujua mkubwa ni yupi na mdogo
ni yupi.
Siku zilipokaribia za kwenda Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Upendo alijiandaa
barabara kwa ajili ya kuanza masomo ya Chuo. Siku moja kabla ya kuondoka
Mama na Baba yake walimwita na kuzungumza naye mazungumzo ili kumwasa na
kumpa ushauri.
“Upendo tumeishi wote kutoka ukiwa mdogo, hujawahi kuishi mbali nasi kuanzia
masomo ya elimu ya shule ya msingi hadi elimu ya Sekondari. Umesomea
Morogoro, sasa unakwenda Dar es salaam kuanza maisha mapya ya kuishi mbali
na sisi. Ninakuomba ukasome kwa bidii ili ujiandalie maisha yako ya baadaye.”
Mzee Bondi alimaliza kutoa nasaha zake, huku Upendo akisikiliza kwa makini
kabisa.
“Umsikilize baba yako kwa makini kwa sababu dunia ya sasa imeharibika
mwanangu. Magonjwa ni mengi na ukifika huko sio ndio ukasahau
kilichokupeleka. Kumbuka kinachokupeleka ni masomo na sio starehe. Nadhani
umenielewa.” Alisisitiza Mama yake.
“Jamani Mama nitasoma kwa bidii mbona unaongea hivyo.” Upendo alihamaki
“Lazima niongee mwanangu vijana wa sasa mnakutana na mambo mengi na
vishawishi vingi usipokuwa makini utapoteza kabisa mwelekeo na malengo yako.”
Mama upendo aliendelea kutoa nasaha.
“Baba na Mama nimewasikia, kamwe sitoenda kutenda yasiyo sahihi, nitasoma na
nitawafurahisha siku zote wazazi wangu.” Upendo alijibu kwa unyenyekevu.
Baada ya maongezi hayo wote walisimama na kuelekea kulala ili Upendo akaanze
kujiandaa na safari. Upendo aliingia chumbani na kuanza kupanga vitu vyake
akisaidiana na mdogo wake Eliza.
“Ndugu yangu si nilikuwa nimekaa na Mama na Baba sebuleni wananipa wosia
namna ya kuishi huko Chuo.” Alisema Upendo.
“Eheh! Ilikuaje? Kwa sababu Mama naye akiamua kuongea ni balaa wamesemaje
hao wazee?” Alidadisi Eliza.
“Mwenzangu, Baba na Mama wameniambia nikienda nisisahau kilichonipeleka
nisiendekeze starehe.” Alisema Upendo.
“Heh! Hao wazee nao inamaana ukakae tu unasoma hata disko usijichanganye?
Aka mwaya sisi bado vijana lazima tujirushe we ngoja mi nimalize Kidato cha Sita
nikienda chuo nitajirusha sana kwani hapa nyumbani hawa wazee wanatubania
sana.” Alizungumza Eliza.
“Usiseme hivyo mdogo wangu mimi naona Baba na Mama wapo sahihi, kwani
nikianza kujiingiza kwenye starehe nitajikuta nafeli mitihani halafu malengo yangu
ya kuwa mwanasheria yasitimie, we mwenzangu unawaza kujirusha tu.” Alijibu
Upendo.
“Kujirusha ni wajibu na kusoma nitasoma tu, haya bwana tufanye haraka tuwahi
kulala hao wazee watakuamsha mapema kesho.” Alimaliza Eliza. Usikose uhondo
zaidi itaendelea katika sura ya 2

More Related Content

Featured

Everything You Need To Know About ChatGPT
Everything You Need To Know About ChatGPTEverything You Need To Know About ChatGPT
Everything You Need To Know About ChatGPTExpeed Software
 
Product Design Trends in 2024 | Teenage Engineerings
Product Design Trends in 2024 | Teenage EngineeringsProduct Design Trends in 2024 | Teenage Engineerings
Product Design Trends in 2024 | Teenage EngineeringsPixeldarts
 
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental Health
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental HealthHow Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental Health
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental HealthThinkNow
 
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdfAI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdfmarketingartwork
 
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024Neil Kimberley
 
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)contently
 
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024Albert Qian
 
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie InsightsSocial Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie InsightsKurio // The Social Media Age(ncy)
 
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024Search Engine Journal
 
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summarySpeakerHub
 
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd Clark Boyd
 
Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next Tessa Mero
 
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search IntentGoogle's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search IntentLily Ray
 
Time Management & Productivity - Best Practices
Time Management & Productivity -  Best PracticesTime Management & Productivity -  Best Practices
Time Management & Productivity - Best PracticesVit Horky
 
The six step guide to practical project management
The six step guide to practical project managementThe six step guide to practical project management
The six step guide to practical project managementMindGenius
 
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...RachelPearson36
 
Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...
Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...
Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...Applitools
 
Featured (20)

Everything You Need To Know About ChatGPT
Everything You Need To Know About ChatGPTEverything You Need To Know About ChatGPT
Everything You Need To Know About ChatGPT
 
Product Design Trends in 2024 | Teenage Engineerings
Product Design Trends in 2024 | Teenage EngineeringsProduct Design Trends in 2024 | Teenage Engineerings
Product Design Trends in 2024 | Teenage Engineerings
 
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental Health
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental HealthHow Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental Health
How Race, Age and Gender Shape Attitudes Towards Mental Health
 
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdfAI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
AI Trends in Creative Operations 2024 by Artwork Flow.pdf
 
Skeleton Culture Code
Skeleton Culture CodeSkeleton Culture Code
Skeleton Culture Code
 
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
PEPSICO Presentation to CAGNY Conference Feb 2024
 
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
Content Methodology: A Best Practices Report (Webinar)
 
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
How to Prepare For a Successful Job Search for 2024
 
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie InsightsSocial Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
Social Media Marketing Trends 2024 // The Global Indie Insights
 
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
Trends In Paid Search: Navigating The Digital Landscape In 2024
 
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
5 Public speaking tips from TED - Visualized summary
 
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
ChatGPT and the Future of Work - Clark Boyd
 
Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next Getting into the tech field. what next
Getting into the tech field. what next
 
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search IntentGoogle's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
Google's Just Not That Into You: Understanding Core Updates & Search Intent
 
How to have difficult conversations
How to have difficult conversations How to have difficult conversations
How to have difficult conversations
 
Introduction to Data Science
Introduction to Data ScienceIntroduction to Data Science
Introduction to Data Science
 
Time Management & Productivity - Best Practices
Time Management & Productivity -  Best PracticesTime Management & Productivity -  Best Practices
Time Management & Productivity - Best Practices
 
The six step guide to practical project management
The six step guide to practical project managementThe six step guide to practical project management
The six step guide to practical project management
 
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
Beginners Guide to TikTok for Search - Rachel Pearson - We are Tilt __ Bright...
 
Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...
Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...
Unlocking the Power of ChatGPT and AI in Testing - A Real-World Look, present...
 
Dada yangu sura y1

  • 1. DADA YANGU SURA YA ..1.. By Adela Dally Kavishe in UWANJA WA SIMULIZI · Edit Doc Mapenzi ni kitu ambacho kimechukua nafasi kubwa sana katika maisha ya watu kote duniani. Mapenzi haya yanaweza kuleta furaha sana endapo mtu atampata mtu sahihi ambaye atakuwa ni muwazi, mwenye mapenzi ya kweli na kuheshimu uhusiano huo. Lakini mapenzi yanaweza kuleta karaha au kukosa amani kabisa kama kutakuwa na migogoro ambayo unakuta inasababishwa na kukosa uaminifu na kuleta ugomvi kati ya wawili wapendanao. Mapenzi haya yanaweza yakasababisha ndugu kugombana, marafiki kukosana na hata kuuana. ***** Eliza na Upendo ni wasichana warembo waliozaliwa katika familia ya kitajiri mkoani Morogoro. Wasichana hawa waliishi katika maisha ya kifahari kutokana na Baba yao Mzee Bondi kuwa na uwezo mkubwa sana kifedha. Mzee Bondi aliwapenda sana mabinti zake na alipenda wasome kwa bidii ili baadaye waje kuwa na maisha bora. Eliza na Upendo walisoma katika hali nzuri sana hadi kufikia elimu ya chuo, ambapo Upendo alikuwa akisoma Chuo Kikuuu cha Dar es salaam na Eliza Chuo cha Uhasibu Arusha. Kutokana na masomo walitengana na kuonana mara chache kipindi cha likizo. Baadaye Eliza na Upendo walijikuta wakijiingiza katika uhusiano wa kimapenzi wote wawili kwa kijana mmoja mtanashati aliyeitwa James bila kujijua. Uhusiano wa kimapenzi kwa mwanamume mmoja ulileta migogoro katika familia yao. ********* Baada ya kumaliza Kidato cha Sita Upendo alipangiwa kwenda kuendelea na masomo ya Chuo Mkoa wa Dar es salaam. Baba yake alifurahi sana na kumuahidi kuwa angempa zawadi nono kama angefanya vizuri akiwa Chuo. Kabla ya kujiunga na chuo Upendo alifanyiwa sherehe kubwa ya kumpongeza, ambayo
  • 2. ilihudhuriwa na watu wengi sana ndugu jamaa na marafiki. Wakati huo mdogo wake Eliza alikuwa Kidato cha Sita kwani walipishana mwaka mmoja tu na kwa jinsi walivyokuwa, walionekana kama mapacha. Wakati mwingine ilikuwa ni vigumu kwa watu ambao walikuwa hawajawaona kujua mkubwa ni yupi na mdogo ni yupi. Siku zilipokaribia za kwenda Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Upendo alijiandaa barabara kwa ajili ya kuanza masomo ya Chuo. Siku moja kabla ya kuondoka Mama na Baba yake walimwita na kuzungumza naye mazungumzo ili kumwasa na kumpa ushauri. “Upendo tumeishi wote kutoka ukiwa mdogo, hujawahi kuishi mbali nasi kuanzia masomo ya elimu ya shule ya msingi hadi elimu ya Sekondari. Umesomea Morogoro, sasa unakwenda Dar es salaam kuanza maisha mapya ya kuishi mbali na sisi. Ninakuomba ukasome kwa bidii ili ujiandalie maisha yako ya baadaye.” Mzee Bondi alimaliza kutoa nasaha zake, huku Upendo akisikiliza kwa makini kabisa. “Umsikilize baba yako kwa makini kwa sababu dunia ya sasa imeharibika mwanangu. Magonjwa ni mengi na ukifika huko sio ndio ukasahau kilichokupeleka. Kumbuka kinachokupeleka ni masomo na sio starehe. Nadhani umenielewa.” Alisisitiza Mama yake. “Jamani Mama nitasoma kwa bidii mbona unaongea hivyo.” Upendo alihamaki “Lazima niongee mwanangu vijana wa sasa mnakutana na mambo mengi na vishawishi vingi usipokuwa makini utapoteza kabisa mwelekeo na malengo yako.” Mama upendo aliendelea kutoa nasaha. “Baba na Mama nimewasikia, kamwe sitoenda kutenda yasiyo sahihi, nitasoma na nitawafurahisha siku zote wazazi wangu.” Upendo alijibu kwa unyenyekevu. Baada ya maongezi hayo wote walisimama na kuelekea kulala ili Upendo akaanze kujiandaa na safari. Upendo aliingia chumbani na kuanza kupanga vitu vyake akisaidiana na mdogo wake Eliza. “Ndugu yangu si nilikuwa nimekaa na Mama na Baba sebuleni wananipa wosia namna ya kuishi huko Chuo.” Alisema Upendo.
  • 3. “Eheh! Ilikuaje? Kwa sababu Mama naye akiamua kuongea ni balaa wamesemaje hao wazee?” Alidadisi Eliza. “Mwenzangu, Baba na Mama wameniambia nikienda nisisahau kilichonipeleka nisiendekeze starehe.” Alisema Upendo. “Heh! Hao wazee nao inamaana ukakae tu unasoma hata disko usijichanganye? Aka mwaya sisi bado vijana lazima tujirushe we ngoja mi nimalize Kidato cha Sita nikienda chuo nitajirusha sana kwani hapa nyumbani hawa wazee wanatubania sana.” Alizungumza Eliza. “Usiseme hivyo mdogo wangu mimi naona Baba na Mama wapo sahihi, kwani nikianza kujiingiza kwenye starehe nitajikuta nafeli mitihani halafu malengo yangu ya kuwa mwanasheria yasitimie, we mwenzangu unawaza kujirusha tu.” Alijibu Upendo. “Kujirusha ni wajibu na kusoma nitasoma tu, haya bwana tufanye haraka tuwahi kulala hao wazee watakuamsha mapema kesho.” Alimaliza Eliza. Usikose uhondo zaidi itaendelea katika sura ya 2