2. MIGOGORO
Ni hali ya kutokua na makubaliano baina ya pande
mbili tofauti.
AMANI
Ni uwepoo wa upendo na kutokuwepo kwa
uhasama,kutokua na machafuko pamoja na usimamizi
wa haki za binadamu.
3. AMANI ENDELEVU
Ni kitendo cha kusimamia ,kuendeleza na kuhamasisha
haki za binadamu kwa faida ya kizazi kilichopo na kizazi
kijachoo yaani kuwepo kwa haki na usawa ndani ya jamii.
MACHAFUKO
Ni hali ya kukosekana kwa makubaliano au maelewano
baina ya pande mbili na kupelekea kutumia nguvu
ambazo zitasababisha madhara kwa upande mojawapo.
VITA
Ni hali ya kutokuwa na maelewano baina ya pande mbili
na ikahusisha matumizi ya majeshi na silaha nzito kwa
ajili ya maslahi ya kiuchumi,kisiasa au kijamii.
4. AINA ZA MIGOGORO
Migogoro ya Nafsi
Hii ni migogoro ambayo mtu anakua nayo yeye mwenyew
ndani ya nafsi yake ambayo ikizidi sana hupelekea mtu kuwa
na msongo wa mawazo.
Migogoro baina ya Mtu na Mtu
Hii ni migogoro ambayo hua baina ya mtu mmoja na
mwingine eidha ndani ya familia,jamii husika au kati ya
wapenzi wawili.
Migogoro ya jamii au nchi
Migogoro ya aina hii hua ni mikubwa na jamii ndo huijua
kwa kiasi kikubwa kuliko aina ya kwanza naya pili. Migogoro
hii inahusisha jamii moja na nyingine, kikundi kimoja na
kingine, nchi na nchi na mara nyingi hua na madhara
makubwa sana kwa jamii zitakazo husika ndani ya mgogoro
huo.
5. CHANZO CHA MGOGORO
Hapa inahitaji uelewa mzuri kuweza kujua chanzo halisi cha mgogoro
sababu kuu huweza kuwa kisiasa,kiuchumi,kijamii,kiteknolojia ambayo hivi
hupelekea sababu zifuatatazo kutokea kwa mgogoro
Kutokua na makubaliano au maridhiano: watu kutokana na sababu
hizo za kisiasa,kiuchumi au kijamii hupelekea watu kutokua na
makubaliano katika jambo husika na kupelekea mgogoro kuzuka.
Kutokuaminiana: Pia sababu hizo huweza kupelekea watu kutokua na
uaminifu ndani ya swala husika na kusababisha mgogoro
Kukosekana kwa haki na usawa: kama sababu hizo za kiuchumi,kisiasa
au kijamii hazitakua katika usawa na haki huenda zikawa chanzo cha
migogoro kwakukosekana kwa haki na usawa
6. Kukata tamaa: Pia iwapo mambo hayoo yatafikia kiwango ambacho kitapelekea
watu kukata tamaa na kuamua kufanya maamuzi mengine hapo sasa ndo
kunapoweza kutokea kwa mgogoro
Kutokua na uwezo au nguvu: Inapotokea upande mmoja ukajihisi hauna
nguvu katika swala husika hautoweza kukubali kirahisi na kuamua kutumia kila
mbinu ili na wenyewe uonekane una nguvu ili hali kua hauna nguvu yoyote ndipo
kinakua chanzo kikubwa cha mgogoro
Kujikweza: Pia kuna makundi ambayo hupenda kujikweza na kujiona yao ndio
bora zaidi yaw engine na kutaka kuwa juu katika kila jambo hata kama wengine
hawakubaliani nalo hivyo kupelekea kuwa na migogoro
7. ILI MGOGORO UTOKEE UNAHITAJI YAFUATAYO
Kutokua na Makubaliano au Maridhiano(sababu)
Upande mmoja kuwa na nguvu zaidi ya mwingine
Kupinga wazo la mwingine
Kueneza chuki katika jambo hilo
Kua na uwezo wa kupambana
8. MUONEKANO WA MIGOGORO
KISAIKOLOJIA; Hapa migogoro hua na muonekano au imepelekewa
kutokea kutokana na mambo ya kisaikolojia mf;(stereotype), ubaguzi,
Vimisemo vinavyozuka kwenye jamii vyenye lengo la kumkandamiza mtu
wa kundi jingine huenda kuwa ni kweli au ni uzushi.
KIBAIOLOJIA; hutokana na saabu za hali ya kimaumbile ya mtu, mf Mtu
kuingilia katika himaya ya mwingine ambayo inamuathiri kaimaumbile
KIJAMII; mfano migogor ya ukabila,baina ya jamii husika
KISIASA; Hii ni migogoro inayo onekana kisiasa zaidi.mfKugombania
madaraka
9. HATUA ZA MGOGORO
Migogoro hupitia hatua zifuatazo katika kutokea kwake:
1. Utofauti(vimisemo),kutofautisha watu
2. Kutengeneza matabaka ; watu kujigawa kimakundii
3. Kichocheo/Sababu ya Kuanza mapambano/ chanzo
4. Machafuko; mauaji,uharibifu na ukosekenaji wa haki na
usawa
5. Kuhalalisha mabaya kua mazuri
6. Suluhisho la mgogoro
12. NJIA ZA UTATUZI WA MIGOGORO
Kua na Maridhiano au makubaliano
Ni njia mojawapo ya kutatua migogoro kwa njia ya kuweka pamoja chini
pande zote mbili katika mgogoro na kuongea nao ili kutafuta tatizo na
kutatua mgogoro kwa njia ya maridhiano au makubaliano baina yao. Hii
ni njia nzuri na rahisi ya kutatua migogoro ambayo inaweza kusaidia
jamii kuondokana na msawala ya machafuko na migogoro
Kutumia Migogoro kama Fursa ya Kimaendeleo
Mbinu hii pia ni nzuri ambayo hutumia chanzo cha migogoro kuzifanya
ziwe chachu za maendeleo katika jamii na kuepusha kutokea kwa
machafuko katika jamii.
Kudhibiti migogoro iliyopo na Kuepuka migogoro mipyaa
Katika njia hii inashauriwa kwa wapenda amani na jamii kwa ujumla
kufundisha juu ya tabia njema na watu waishi vipi ili kulinda amani na
kuepusha kutokea kwa migogoro mengine.
13. AMANI KWA UJUMLA
AMANI
Ni uwepoo wa upendo na kutokuwepo kwa
uhasama,kutokua na machafuko pamoja na usimamizi
wa haki za binadamu.
AMANI ENDELEVU
Ni kitendo cha kusimamia ,kuendeleza na kuhamasisha
haki za binadamu kwa faida ya kizazi kilichopo na
kizazi kijachoo yaani kuwepo kwa haki na usawa
ndani ya jamii.
14. MBINU ZA KUTUNZA AMANI
KULINDA AMANI ILIYOPO
Ni hali ya wana jamii kutumia mbinu mbalimbali katika maeneo yao ili
kulinda amani iliyopo.kwa kutumia mbinu mbalimbali kama
sanaa,michezo, vikundi vya kiulinzi.nk.
KUHAMASISHA AMANI
Ni kitendo cha watu au vikundi au mashirika kuweza kutumia mbninu
mbalimbali kwa ajili ya kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa amani
katika maisha ya binadamu na eneo husika.kwa kutumia midahalo na
kampeni mbalimbali ambao lengo lake ni kuhamasisha amani
KUJENGA AMANI
Ni hali ya jamii kuamua kutengeneza amani ikishirikiana na mashirika
makubwa kama Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na mengine ambayo
yanatumika kwa ajili ya kuhamasisha Amani.
15. HATUA ZA KUHESHIMU IMANI ZETU KATIKA
KUJENGA AMANI
•Kukataa
•Kulinda
•Kuvumila na kukubali
•Kuheshimu
•Kuthamini
16. Prepared by Peace ambassodors
Albert Andrew
Selina Komba
Dedan Kapogo
Christina Mbaga
Mohhamed Mtumwa