SlideShare a Scribd company logo
1 of 3
Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu
Hamdu zote ni zake Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu na sala na salamu zimshukie
Bwana wa Manabii na Mitume wa Mwenyezi Mungu na Aali zake watukufu na masahaba zake
wema.
Kuwadia kwa msimu wa Hija kunapaswa kutambuliwa kuwa ni sikukuu kubwa ya Umma wa
Kiislamu. Fursa kubwa inayoletwa na siku hizi zenye thamani katika miaka yote kwa Waislamu
duniani ni kemia inayofanya muujiza ambayo iwapo itathaminiwa ipasavyo na kutumiwa vizuri
inaweza kutibu magonjwa mengi ya ulimwengu wa Kiislamu.
Hija ni chemchemi ya baraka tele za Mwenyezi Mungu. Ninyi Mahujaji mliopata saada,
mumepata fursa ya kuosha nyoyo zenu katika amali na ibada hii iliyojaa usafi na umaanawi na
kutumia hazina hii ya rehma, izza na qudra kwa ajili ya kujiwekea akiba ya umri wenu wote.
Msimu huu wa ibada ya Hija ni shule ya kujifunza na kujistawisha ambayo ina masomo ya kuwa
wanyenyekevu na kujisalimisha kwa Mola Mlezi, kubeba majukumu waliyopewa Waislamu na
Mwenyezi Mungu, kufanya jitihada, nishati na harakati katika kazi za dini na dunia,
kurehemeana na kusameheana katika kuamiliana na ndugu, masomo ya ushujaa na kujiamini
katika kukabiliana na matukio mazito na kuwa na matumaini na msaada wa Mola Karima katika
kila mahala na katika kila kitu. Kwa ufupi tunasema kuwa, msimu wa ibada ya Hija ni uwanja
wa kujenga shakhsia ya mwanadamu kwa mujibu wa vigezo vya Kiislamu. Kwa msingi huo
mnaweza kujipamba humo kwa vito hivyo vya kiroho na kufaidika na hazina hiyo tukufu na
kuchukua matunda yake kwa ajili ya nafsi zenu na zawadi kwa nchi, mataifa yenu na Umma
mzima wa Kiislamu.
Hii leo Umma wa Kiislamu unahitajia zaidi wanadamu wanaoambatanisha pamoja amali, imani,
usafi wa roho, ikhlasi, muqawama mbele ya maadui wenye vinyongo pamoja na kuijenga nafsi
kiroho na kimaanawi. Hii ndiyo njia pekee ya wokovu wa jamii kubwa ya Waislamu kwa kipindi
kirefu kutoka kwenye matatizo iliyotumbukia ndani yake ama kwa mikono ya adui au kutokana
na udhaifu wa azma, imani na busuri.
Hapana shaka kuwa kipindi cha sasa ni kipindi cha mwamko na kupata utambulisho wa
Waislamu; uhakika huu unaweza kuonekana waziwazi kupitia changamoto zinazozikabili nchi za
Waislamu. Ni katika mazingira haya ndipo azma na irada inayoegamia kwenye imani,
kutawakali kwa Mwenyezi Mungu, kuona mbali na tadbiri vinapoweza kuyapatia ushindi na
fahari mataifa ya Waislamu katika changamoto hizi na kuyafikisha kwenye mustakbali wenye
izza na utukufu. Kambi nyingine ambayo haiwezi kustahamili mwamko na izza ya Waislamu,
imejitosa katika medani kwa nguvu zake zote na inatumia nyenzo zake zote za kiusalama,
kinafsi, kijeshi, kiuchumi na kipropaganda kwa ajili ya kuwatibua na kuwakandamiza Waislamu
na kuwashughulisha wao kwa wao. Hali ya nchi za magharibi mwa Asia kuanzia Pakistan hadi
Syria, Iraq na Palestina, nchi za Ghuba ya Uajemi, na vilevile nchi za kaskazini mwa Afrika
kuanzia Libya, Misri na Tunisia hadi Sudan na baadhi ya nchi nyingine, inaweka wazi mambo
mengi. Vita vya ndani, taasubiri kipofu za kidini na kimadhehebu, machafuko ya kisiasa, kuenea
ugaidi uliojaa ukatili, kujitokeza makundi na mirengo yenye misimamo ya kufurutu mipaka
ambayo yanatumia mbinu za kaumu zilizokuwa zikiishi maisha ya kishenzi katika historia kama
kupasua vifua vya wanadamu na kutafuna nyoyo zao, watu wanaobeba silaha wanaoua watoto na
wanawake, watu wanaochinja vichwa vya wanaume na kuwabaka wanawake na wakati
mwingine kufanya jinai hizo za kukirihisha na kuchafua moyo kwa kutumia jina na bendera ya
dini, yote hayo ni matokeo ya mpango wa kishetani na kibeberu wa mashirika ya kijasusi ya
wageni na tawala vibaraka wao katika Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika ambayo
yanatayarisha mazingira ya ndani kwa ajili ya matukio hayo na kuyaonjesha shubiri mataifa
mbalimbali. Ni wazi kuwa katika hali kama hii hatuwezi kutarajia kuwa nchi za Waislamu
zitajaza mapengo yao ya masuala ya kimaanawi na kiroho na kupata amani, hali bora ya maisha
na maendeleo ya kisayansi na nguvu ya kimataifa ambavyo ndiyo baraka za mwamko na kupata
utambulisho wa Kiislamu. Hali hii ya maafa inaweza kuutia ugumba mwamko wa Kiislamu na
kuharibu utayarifu wa kiroho uliojitokeza katika dunia ya Kiislamu, na kwa mara nyingine
kuyatumbukiza kwa muda mrefu mataifa ya Waislamu katika mkwamo, hali ya kutengwa na
mporomoko na hatimaye kusahaulisha kabisa masuala muhimu ya Waislamu kama kadhia ya
kuikomboa Palestina na mataifa mengine ya Waislamu kutoka kwenye makucha ya Marekani na
Wazayuni.
Tiba mujarabu na ya kimsingi inaweza kufupishwa katika sentensi mbili muhimu ambazo zote ni
katika masomo muhimu ya ibada ya Hija:
Kwanza: Umoja na udugu wa Waislamu chini ya bendera ya tauhidi.
Pili: Kumjua adui na kukabiliana na njama na mbinu zake.
Somo kubwa la ibada ya Hija ni kuimarisha udugu na mshikamano. Hapa, katika ibada ya Hija,
inazuiwa pia kufanya ubishani na malumbano. Vazi la aina moja, amali za aina moja, harakati za
aina moja na mwenendo wa upole hapa katika Hija vina maana ya usawa na udugu wa watu wote
wanaoamini tauhidi. Hili ni jibu la wazi la Uislamu kwa kila fikra, itikadi na wito unaowaondoa
katika Uislamu baadhi ya Waislamu na watu wanaoamini al Kaaba na Tauhidi. Watu wenye
fikra za kuwakufurisha Waislamu ambao wamekuwa wanasesere wa siasa za Wazayuni mahaini
na waungaji mkono wao wa Kimagharibi ambao wanafanya jinai za kutisha na kumwaga damu
za Waislamu wasio na hatia, na wale wanaojidai kushikamana na dini na kuvaa mavazi ya
wanazuoni wa dini wanaochochea moto wa hitilafu kati ya Shia na Suni na wengineo mfano
wao, wanapaswa kuelewa kwamba ibada ya Hija inabatilisha madai yao.
Mimi, kama walivyo maulamaa wengi wa Kiislamu na wale wanaoumizwa na masuala ya Umma
wa Kiislamu, ninatangaza tena kwamba, kila neno au amali inayochochea moto wa hitilafu kati
ya Waislamu, kuvunjiwa heshima matukufu ya mojawapo ya makundi ya Waislamu au
kukufurisha moja kati ya madhehebu za Kiislamu ni kuhudumia kambi ya ukafiri na shirki na
kusaliti Uislamu; na amali hiyo ni haramu.
Kumtambua adui na mbinu anazotumia ndiyo nguzo ya pili. Kwanza kabisa hatupasi kughafilika
na kumsahau adui mwenye kinyongo, na marasimu ya kumpiga mawe mara kadhaa shetani
katika ibada ya Hija ni nembo ya kukumbuka suala hilo daima katika fikra na akili zetu. Pili ni
kwamba hatupasi kufanya makosa katika kumtambua adui yetu asili ambaye hii leo ni kambi ya
ubeberu wa kimataifa na kanali ya watenda jinai ya Kizayuni. Tatu ni kuwa, tunalazimika
kuainisha vyema mbinu za adui huyo mkaidi ambazo ni kuzusha hitilafu kati ya Waislamu,
kueneza ufisadi wa kisiasa na kimaadili, kutoa vitisho na vivutio kwa shakhsia na watu
mashuhuri, kuweka mashinikizo ya kiuchumi dhidi ya mataifa mbalimbali na kuzusha shaka
katika imani na itikadi za Kiislamu na vilevile kuwatambua vibaraka na vikaragosi wao
wanaowafanyia kazi kwa kujua au bila ya kujua.
Madola ya kibeberu yakiongozwa na Marekani yanaficha sura zao halisi kwa kutumia msaada
wa zana za kisasa za vyombo vya habari na kutumia hila na ujanja mbele ya fikra za mataifa
mbalimbali kwa madai ya kutetea haki za binadamu na demokrasia. Madola haya yanadai
kutetea haki za mataifa ilhali mataifa ya Waislamu kila siku yanaona kwa macho na kuhisi kwa
nyoyo moto wa fitina zao. Tunapotazama taifa linalodhulumiwa la Palestina ambalo kwa miongo
kadhaa sasa linaendelea kujeruhiwa kwa jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel na waungaji
mkono wake, au katika nchi za Afghanistan, Pakistan na Iraq ambako ugaidi uliotengenezwa na
siasa za ubeberu na vibaraka wao umeyafanya machungu kama shubiri maisha ya mataifa hayo,
au nchini Syria ambayo inashambuliwa na chuki za mabeberu wa kimataifa na vikaragosi wao
wa kieneo na imetumbukizwa katika vita vya umwagaji damu vya ndani kwa dhambi ya kuunga
mkono harakati ya mapambano dhidi ya Wazayuni, au Bahrain au Myanmar ambako katika kila
mojawapo ya nchi hizo Waislamu wanaosumbuliwa na mashaka mbalimbali wamesahaulika na
maadui zao wanaungwa mkono, au mataifa mengine ambayo yanatishiwa mara kwa mara na
Marekani na waitifaki wake kushambuliwa kijeshi au kuwekewa vikwazo vya kiuchumi au
kukabiliwa na uharibu wa kiusalama, yote hayo yanaweza kuonesha vyema sura halisi ya vinara
hawa wa mfumo wa ubeberu kwa walimwengu wote.
Shakhsia wa kisiasa, kiutamaduni na kidini katika maeneo yote ya ulimwengu wa Kiislamu
wanalazimika kufichua uhakika huu. Huu ni wajibu wetu sote wa kidini na kiakhlaki. Nchi za
kaskazini mwa Afrika ambazo kwa masikitiko makubwa zimekumbwa na hitilafu kubwa za
ndani, zinalazimika kuliko nchi nyingine, kutilia maanani wajibu huu adhimu, yaani kumtambua
adui, mbinu na njama zake. Kuendelea hitilafu kati ya mirengo mbalimbali ya kitaifa na
kughafilika na hatari ya vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi hizo ni hatari kubwa
ambayo hasara zake kwa Umma wa Kiislamu haziwezi kufidika haraka.
Hatuna shaka kwamba mataifa yaliyosimama kidete katika eneo hilo linaloonesha kielelezo cha
Mwamko wa Kiislamu, kwa idhini yake Mwenyezi Mungu, hayataruhusu mshale wa saa urejee
nyuma na kurejesha kipindi cha watawala waovu, vibaraka na madikteta; hata hivyo ni wazi
kuwa kughafilika na nafasi ya madola ya kibeberu katika kuzusha fitina na kuingilia mambo yao
ya ndani vitatatiza kazi zao na kuchelewesha kwa miaka mingi kipindi cha izza, usalama na hali
bora ya kimaisha. Tuna imani kubwa na uwezo wa mataifa na nguvu iliyowekwa na Mwenyezi
Mungu Mwenye hikima katika azma, imani na busuri ya watu na tumeiona na kuijaribu nguvu
hiyo kwa macho yetu katika kipindi cha zaidi ya miongo mitatu katika Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran. Hima yetu ni kuyalingania mataifa ya Waislamu tajiriba hii ya ndugu zao katika nchi hii
yenye fahari na isiyochoka.
Namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu arekebishe hali za Waislamu na kuwaepusha na vitimbi
vya adui. Vilevile namuomba Mwenyezi Mungu atakabali Hija na kuwapa uzima wa mwili na
roho na tunu kubwa ya kimaanawi ninyi nyote Mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu.
Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.
Sayyid Ali Khamenei
5 Dhulhija 1434 Hijria
19 / Mehr/ 1392 Hijria Shamsia
11/ Oktoba/ 2013 Miladia.

More Related Content

Viewers also liked (17)

Rex Obatay_ID-1
Rex Obatay_ID-1Rex Obatay_ID-1
Rex Obatay_ID-1
 
Excel
ExcelExcel
Excel
 
Aula 2 - A Largada - O Salto
Aula 2 - A Largada - O SaltoAula 2 - A Largada - O Salto
Aula 2 - A Largada - O Salto
 
Being respectful
Being respectfulBeing respectful
Being respectful
 
Saúde com consciência
Saúde com consciênciaSaúde com consciência
Saúde com consciência
 
Certificate Anti Corrupção Global 2016
Certificate Anti Corrupção Global 2016Certificate Anti Corrupção Global 2016
Certificate Anti Corrupção Global 2016
 
Lançamentos da Editora Draco
Lançamentos da Editora DracoLançamentos da Editora Draco
Lançamentos da Editora Draco
 
SenecaFTI_Capabilities_Web
SenecaFTI_Capabilities_WebSenecaFTI_Capabilities_Web
SenecaFTI_Capabilities_Web
 
Msemillas
MsemillasMsemillas
Msemillas
 
Presentacionedu2 0
Presentacionedu2 0Presentacionedu2 0
Presentacionedu2 0
 
Tecnicas de ventas
Tecnicas de ventasTecnicas de ventas
Tecnicas de ventas
 
Blog
BlogBlog
Blog
 
As bases do trabalho
As bases do trabalhoAs bases do trabalho
As bases do trabalho
 
Sonido
SonidoSonido
Sonido
 
Direito do Consumidor - Apostila
Direito do Consumidor - ApostilaDireito do Consumidor - Apostila
Direito do Consumidor - Apostila
 
4 velas
4 velas4 velas
4 velas
 
Project Manager5
Project Manager5Project Manager5
Project Manager5
 

More from hajj2013

神聖なコーラン
神聖なコーラン神聖なコーラン
神聖なコーランhajj2013
 
古蘭經 Al qur'an
古蘭經 Al qur'an古蘭經 Al qur'an
古蘭經 Al qur'anhajj2013
 
신성한 크어랜
신성한 크어랜신성한 크어랜
신성한 크어랜hajj2013
 
The holy quran
The holy quranThe holy quran
The holy quranhajj2013
 
The holy quran sveti kur’an
The holy quran sveti kur’anThe holy quran sveti kur’an
The holy quran sveti kur’anhajj2013
 
The holy quran svet quran translation of the meanings in croatian prevođenje ...
The holy quran svet quran translation of the meanings in croatian prevođenje ...The holy quran svet quran translation of the meanings in croatian prevođenje ...
The holy quran svet quran translation of the meanings in croatian prevođenje ...hajj2013
 
Tagalog santo quran
Tagalog santo quranTagalog santo quran
Tagalog santo quranhajj2013
 
Suci quran
Suci quranSuci quran
Suci quranhajj2013
 
Quran greek
Quran greekQuran greek
Quran greekhajj2013
 
Pyhä quran finnish
Pyhä quran  finnishPyhä quran  finnish
Pyhä quran finnishhajj2013
 
Latin sanctus quran
Latin sanctus quranLatin sanctus quran
Latin sanctus quranhajj2013
 
Holy quran slovak
Holy quran  slovakHoly quran  slovak
Holy quran slovakhajj2013
 
Helligst quran norwegian
Helligst quran  norwegianHelligst quran  norwegian
Helligst quran norwegianhajj2013
 
Helig quran översättning om mening
Helig quran översättning om meningHelig quran översättning om mening
Helig quran översättning om meninghajj2013
 
Esperanto holy quran
Esperanto holy quranEsperanto holy quran
Esperanto holy quranhajj2013
 
El quran santo (koran)interpretación española de los significados el ajustar ...
El quran santo (koran)interpretación española de los significados el ajustar ...El quran santo (koran)interpretación española de los significados el ajustar ...
El quran santo (koran)interpretación española de los significados el ajustar ...hajj2013
 
El quran santo(koran)
El quran santo(koran)El quran santo(koran)
El quran santo(koran)hajj2013
 
Quran ukrainian
Quran  ukrainianQuran  ukrainian
Quran ukrainianhajj2013
 
Belgili tanımlık kutsal quran
Belgili tanımlık kutsal quranBelgili tanımlık kutsal quran
Belgili tanımlık kutsal quranhajj2013
 
Dumnezeiesc quran romanian
Dumnezeiesc quran romanianDumnezeiesc quran romanian
Dumnezeiesc quran romanianhajj2013
 

More from hajj2013 (20)

神聖なコーラン
神聖なコーラン神聖なコーラン
神聖なコーラン
 
古蘭經 Al qur'an
古蘭經 Al qur'an古蘭經 Al qur'an
古蘭經 Al qur'an
 
신성한 크어랜
신성한 크어랜신성한 크어랜
신성한 크어랜
 
The holy quran
The holy quranThe holy quran
The holy quran
 
The holy quran sveti kur’an
The holy quran sveti kur’anThe holy quran sveti kur’an
The holy quran sveti kur’an
 
The holy quran svet quran translation of the meanings in croatian prevođenje ...
The holy quran svet quran translation of the meanings in croatian prevođenje ...The holy quran svet quran translation of the meanings in croatian prevođenje ...
The holy quran svet quran translation of the meanings in croatian prevođenje ...
 
Tagalog santo quran
Tagalog santo quranTagalog santo quran
Tagalog santo quran
 
Suci quran
Suci quranSuci quran
Suci quran
 
Quran greek
Quran greekQuran greek
Quran greek
 
Pyhä quran finnish
Pyhä quran  finnishPyhä quran  finnish
Pyhä quran finnish
 
Latin sanctus quran
Latin sanctus quranLatin sanctus quran
Latin sanctus quran
 
Holy quran slovak
Holy quran  slovakHoly quran  slovak
Holy quran slovak
 
Helligst quran norwegian
Helligst quran  norwegianHelligst quran  norwegian
Helligst quran norwegian
 
Helig quran översättning om mening
Helig quran översättning om meningHelig quran översättning om mening
Helig quran översättning om mening
 
Esperanto holy quran
Esperanto holy quranEsperanto holy quran
Esperanto holy quran
 
El quran santo (koran)interpretación española de los significados el ajustar ...
El quran santo (koran)interpretación española de los significados el ajustar ...El quran santo (koran)interpretación española de los significados el ajustar ...
El quran santo (koran)interpretación española de los significados el ajustar ...
 
El quran santo(koran)
El quran santo(koran)El quran santo(koran)
El quran santo(koran)
 
Quran ukrainian
Quran  ukrainianQuran  ukrainian
Quran ukrainian
 
Belgili tanımlık kutsal quran
Belgili tanımlık kutsal quranBelgili tanımlık kutsal quran
Belgili tanımlık kutsal quran
 
Dumnezeiesc quran romanian
Dumnezeiesc quran romanianDumnezeiesc quran romanian
Dumnezeiesc quran romanian
 

• Swahili

  • 1. Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu Hamdu zote ni zake Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu na sala na salamu zimshukie Bwana wa Manabii na Mitume wa Mwenyezi Mungu na Aali zake watukufu na masahaba zake wema. Kuwadia kwa msimu wa Hija kunapaswa kutambuliwa kuwa ni sikukuu kubwa ya Umma wa Kiislamu. Fursa kubwa inayoletwa na siku hizi zenye thamani katika miaka yote kwa Waislamu duniani ni kemia inayofanya muujiza ambayo iwapo itathaminiwa ipasavyo na kutumiwa vizuri inaweza kutibu magonjwa mengi ya ulimwengu wa Kiislamu. Hija ni chemchemi ya baraka tele za Mwenyezi Mungu. Ninyi Mahujaji mliopata saada, mumepata fursa ya kuosha nyoyo zenu katika amali na ibada hii iliyojaa usafi na umaanawi na kutumia hazina hii ya rehma, izza na qudra kwa ajili ya kujiwekea akiba ya umri wenu wote. Msimu huu wa ibada ya Hija ni shule ya kujifunza na kujistawisha ambayo ina masomo ya kuwa wanyenyekevu na kujisalimisha kwa Mola Mlezi, kubeba majukumu waliyopewa Waislamu na Mwenyezi Mungu, kufanya jitihada, nishati na harakati katika kazi za dini na dunia, kurehemeana na kusameheana katika kuamiliana na ndugu, masomo ya ushujaa na kujiamini katika kukabiliana na matukio mazito na kuwa na matumaini na msaada wa Mola Karima katika kila mahala na katika kila kitu. Kwa ufupi tunasema kuwa, msimu wa ibada ya Hija ni uwanja wa kujenga shakhsia ya mwanadamu kwa mujibu wa vigezo vya Kiislamu. Kwa msingi huo mnaweza kujipamba humo kwa vito hivyo vya kiroho na kufaidika na hazina hiyo tukufu na kuchukua matunda yake kwa ajili ya nafsi zenu na zawadi kwa nchi, mataifa yenu na Umma mzima wa Kiislamu. Hii leo Umma wa Kiislamu unahitajia zaidi wanadamu wanaoambatanisha pamoja amali, imani, usafi wa roho, ikhlasi, muqawama mbele ya maadui wenye vinyongo pamoja na kuijenga nafsi kiroho na kimaanawi. Hii ndiyo njia pekee ya wokovu wa jamii kubwa ya Waislamu kwa kipindi kirefu kutoka kwenye matatizo iliyotumbukia ndani yake ama kwa mikono ya adui au kutokana na udhaifu wa azma, imani na busuri. Hapana shaka kuwa kipindi cha sasa ni kipindi cha mwamko na kupata utambulisho wa Waislamu; uhakika huu unaweza kuonekana waziwazi kupitia changamoto zinazozikabili nchi za Waislamu. Ni katika mazingira haya ndipo azma na irada inayoegamia kwenye imani, kutawakali kwa Mwenyezi Mungu, kuona mbali na tadbiri vinapoweza kuyapatia ushindi na fahari mataifa ya Waislamu katika changamoto hizi na kuyafikisha kwenye mustakbali wenye izza na utukufu. Kambi nyingine ambayo haiwezi kustahamili mwamko na izza ya Waislamu, imejitosa katika medani kwa nguvu zake zote na inatumia nyenzo zake zote za kiusalama, kinafsi, kijeshi, kiuchumi na kipropaganda kwa ajili ya kuwatibua na kuwakandamiza Waislamu na kuwashughulisha wao kwa wao. Hali ya nchi za magharibi mwa Asia kuanzia Pakistan hadi Syria, Iraq na Palestina, nchi za Ghuba ya Uajemi, na vilevile nchi za kaskazini mwa Afrika kuanzia Libya, Misri na Tunisia hadi Sudan na baadhi ya nchi nyingine, inaweka wazi mambo mengi. Vita vya ndani, taasubiri kipofu za kidini na kimadhehebu, machafuko ya kisiasa, kuenea ugaidi uliojaa ukatili, kujitokeza makundi na mirengo yenye misimamo ya kufurutu mipaka ambayo yanatumia mbinu za kaumu zilizokuwa zikiishi maisha ya kishenzi katika historia kama kupasua vifua vya wanadamu na kutafuna nyoyo zao, watu wanaobeba silaha wanaoua watoto na wanawake, watu wanaochinja vichwa vya wanaume na kuwabaka wanawake na wakati mwingine kufanya jinai hizo za kukirihisha na kuchafua moyo kwa kutumia jina na bendera ya dini, yote hayo ni matokeo ya mpango wa kishetani na kibeberu wa mashirika ya kijasusi ya wageni na tawala vibaraka wao katika Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika ambayo yanatayarisha mazingira ya ndani kwa ajili ya matukio hayo na kuyaonjesha shubiri mataifa
  • 2. mbalimbali. Ni wazi kuwa katika hali kama hii hatuwezi kutarajia kuwa nchi za Waislamu zitajaza mapengo yao ya masuala ya kimaanawi na kiroho na kupata amani, hali bora ya maisha na maendeleo ya kisayansi na nguvu ya kimataifa ambavyo ndiyo baraka za mwamko na kupata utambulisho wa Kiislamu. Hali hii ya maafa inaweza kuutia ugumba mwamko wa Kiislamu na kuharibu utayarifu wa kiroho uliojitokeza katika dunia ya Kiislamu, na kwa mara nyingine kuyatumbukiza kwa muda mrefu mataifa ya Waislamu katika mkwamo, hali ya kutengwa na mporomoko na hatimaye kusahaulisha kabisa masuala muhimu ya Waislamu kama kadhia ya kuikomboa Palestina na mataifa mengine ya Waislamu kutoka kwenye makucha ya Marekani na Wazayuni. Tiba mujarabu na ya kimsingi inaweza kufupishwa katika sentensi mbili muhimu ambazo zote ni katika masomo muhimu ya ibada ya Hija: Kwanza: Umoja na udugu wa Waislamu chini ya bendera ya tauhidi. Pili: Kumjua adui na kukabiliana na njama na mbinu zake. Somo kubwa la ibada ya Hija ni kuimarisha udugu na mshikamano. Hapa, katika ibada ya Hija, inazuiwa pia kufanya ubishani na malumbano. Vazi la aina moja, amali za aina moja, harakati za aina moja na mwenendo wa upole hapa katika Hija vina maana ya usawa na udugu wa watu wote wanaoamini tauhidi. Hili ni jibu la wazi la Uislamu kwa kila fikra, itikadi na wito unaowaondoa katika Uislamu baadhi ya Waislamu na watu wanaoamini al Kaaba na Tauhidi. Watu wenye fikra za kuwakufurisha Waislamu ambao wamekuwa wanasesere wa siasa za Wazayuni mahaini na waungaji mkono wao wa Kimagharibi ambao wanafanya jinai za kutisha na kumwaga damu za Waislamu wasio na hatia, na wale wanaojidai kushikamana na dini na kuvaa mavazi ya wanazuoni wa dini wanaochochea moto wa hitilafu kati ya Shia na Suni na wengineo mfano wao, wanapaswa kuelewa kwamba ibada ya Hija inabatilisha madai yao. Mimi, kama walivyo maulamaa wengi wa Kiislamu na wale wanaoumizwa na masuala ya Umma wa Kiislamu, ninatangaza tena kwamba, kila neno au amali inayochochea moto wa hitilafu kati ya Waislamu, kuvunjiwa heshima matukufu ya mojawapo ya makundi ya Waislamu au kukufurisha moja kati ya madhehebu za Kiislamu ni kuhudumia kambi ya ukafiri na shirki na kusaliti Uislamu; na amali hiyo ni haramu. Kumtambua adui na mbinu anazotumia ndiyo nguzo ya pili. Kwanza kabisa hatupasi kughafilika na kumsahau adui mwenye kinyongo, na marasimu ya kumpiga mawe mara kadhaa shetani katika ibada ya Hija ni nembo ya kukumbuka suala hilo daima katika fikra na akili zetu. Pili ni kwamba hatupasi kufanya makosa katika kumtambua adui yetu asili ambaye hii leo ni kambi ya ubeberu wa kimataifa na kanali ya watenda jinai ya Kizayuni. Tatu ni kuwa, tunalazimika kuainisha vyema mbinu za adui huyo mkaidi ambazo ni kuzusha hitilafu kati ya Waislamu, kueneza ufisadi wa kisiasa na kimaadili, kutoa vitisho na vivutio kwa shakhsia na watu mashuhuri, kuweka mashinikizo ya kiuchumi dhidi ya mataifa mbalimbali na kuzusha shaka katika imani na itikadi za Kiislamu na vilevile kuwatambua vibaraka na vikaragosi wao wanaowafanyia kazi kwa kujua au bila ya kujua. Madola ya kibeberu yakiongozwa na Marekani yanaficha sura zao halisi kwa kutumia msaada wa zana za kisasa za vyombo vya habari na kutumia hila na ujanja mbele ya fikra za mataifa mbalimbali kwa madai ya kutetea haki za binadamu na demokrasia. Madola haya yanadai kutetea haki za mataifa ilhali mataifa ya Waislamu kila siku yanaona kwa macho na kuhisi kwa nyoyo moto wa fitina zao. Tunapotazama taifa linalodhulumiwa la Palestina ambalo kwa miongo kadhaa sasa linaendelea kujeruhiwa kwa jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel na waungaji mkono wake, au katika nchi za Afghanistan, Pakistan na Iraq ambako ugaidi uliotengenezwa na siasa za ubeberu na vibaraka wao umeyafanya machungu kama shubiri maisha ya mataifa hayo,
  • 3. au nchini Syria ambayo inashambuliwa na chuki za mabeberu wa kimataifa na vikaragosi wao wa kieneo na imetumbukizwa katika vita vya umwagaji damu vya ndani kwa dhambi ya kuunga mkono harakati ya mapambano dhidi ya Wazayuni, au Bahrain au Myanmar ambako katika kila mojawapo ya nchi hizo Waislamu wanaosumbuliwa na mashaka mbalimbali wamesahaulika na maadui zao wanaungwa mkono, au mataifa mengine ambayo yanatishiwa mara kwa mara na Marekani na waitifaki wake kushambuliwa kijeshi au kuwekewa vikwazo vya kiuchumi au kukabiliwa na uharibu wa kiusalama, yote hayo yanaweza kuonesha vyema sura halisi ya vinara hawa wa mfumo wa ubeberu kwa walimwengu wote. Shakhsia wa kisiasa, kiutamaduni na kidini katika maeneo yote ya ulimwengu wa Kiislamu wanalazimika kufichua uhakika huu. Huu ni wajibu wetu sote wa kidini na kiakhlaki. Nchi za kaskazini mwa Afrika ambazo kwa masikitiko makubwa zimekumbwa na hitilafu kubwa za ndani, zinalazimika kuliko nchi nyingine, kutilia maanani wajibu huu adhimu, yaani kumtambua adui, mbinu na njama zake. Kuendelea hitilafu kati ya mirengo mbalimbali ya kitaifa na kughafilika na hatari ya vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi hizo ni hatari kubwa ambayo hasara zake kwa Umma wa Kiislamu haziwezi kufidika haraka. Hatuna shaka kwamba mataifa yaliyosimama kidete katika eneo hilo linaloonesha kielelezo cha Mwamko wa Kiislamu, kwa idhini yake Mwenyezi Mungu, hayataruhusu mshale wa saa urejee nyuma na kurejesha kipindi cha watawala waovu, vibaraka na madikteta; hata hivyo ni wazi kuwa kughafilika na nafasi ya madola ya kibeberu katika kuzusha fitina na kuingilia mambo yao ya ndani vitatatiza kazi zao na kuchelewesha kwa miaka mingi kipindi cha izza, usalama na hali bora ya kimaisha. Tuna imani kubwa na uwezo wa mataifa na nguvu iliyowekwa na Mwenyezi Mungu Mwenye hikima katika azma, imani na busuri ya watu na tumeiona na kuijaribu nguvu hiyo kwa macho yetu katika kipindi cha zaidi ya miongo mitatu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hima yetu ni kuyalingania mataifa ya Waislamu tajiriba hii ya ndugu zao katika nchi hii yenye fahari na isiyochoka. Namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu arekebishe hali za Waislamu na kuwaepusha na vitimbi vya adui. Vilevile namuomba Mwenyezi Mungu atakabali Hija na kuwapa uzima wa mwili na roho na tunu kubwa ya kimaanawi ninyi nyote Mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu. Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh. Sayyid Ali Khamenei 5 Dhulhija 1434 Hijria 19 / Mehr/ 1392 Hijria Shamsia 11/ Oktoba/ 2013 Miladia.