SlideShare a Scribd company logo
1 of 7
Download to read offline
1
Utangulizi
Kabila lolote ulimwenguni, hutokana na mambo manne yakiwemo jadi, kazi, mji na sifa za watu.
Na upande mwingine nayo lugha hutokamana na mazingira maalum ya watu na tamaduni
zao. Ikiwa kabila ni desturi na mila za watu, au ni watu walofungamana na kuwa na tabia na
nyendo ambazo zitawatofautisha wao na watu wengine, basi waswahili wana mila zao na desturi
zao kama makabila mengine ulimwenguni. Kama kwenye maingiliano ya kibinadamu kwa
mfano: ndoa, majina, itikadi za pepo na kadhalika, basi liko kabila ila la waswahili lenye mambo
kama hayo.
Neno itikadi ni istilahi ya kimsingi katika nyugo za kiutamaduni, za fasihi na taaluma zinazohusu
filamu. Maana ya istilahi 'itikadi' kiasilia inatokana na maandishi ya mwanafalsafa wa
Kijerumani, Karl Marx na mwenzake Friedrich Engels (Abdulla, Mansur na wenzake, 2014).
Katika uchanganuzi wao wa kimsingi wa jamii, walifafanua itikadi kama dhana na imani za
tabaka tawala katika kipindi maalumu. Dhana na imani za tabaka tawala ndizo hutamalaki
taratibu za kuunda fikra, mawazo na mielekeo ya wanajamii kwa ujumla. Kwa hivyo, mfumo
wote wa fikra za tabaka tawala ndio unajenga itikadi ya jamii fulani ndiposa tukaona Waswahili
wana itikadi na mila tofauti tofauti.
2
Kama tulivyosema hapo awali kuwa itikadi ni taasisi iliyo hai katika tamaduni za jamii zote za
wanadamu huku zikiwa zimegawanyika aina kuu mbili za itikadi: itikadi za kisiasa, na itikadi za
kiepistemolojia (ni sehemu ya falsafa ambayo inahusu utafiti wa jinsi tunavyojua mambo).
Itikadi ya kisiasa ni upangiliaji unaohusu mawazo ya kimaadili na vipi nchi itaendeshwa. Itikadi
za kiepistemolojia ni upangiliaji unaohusu mawazo ya kifalsafa, ulimwengu, na jinsi gani watu
wanapaswa kufanya maamuzi.Kuna aina nyingi za itikadi. Moja kati ya hizo ni pamoja na
Ukomunisti, Usoshalisti, na ubepari ni itikadi kubwa sana za kiuchumi na kisiasa kwa ujumla.
Kwa sasa tutaangalia itikadi za Waswahili pekee yake.
Waswahili wana itikadi nyingi sana na mifano ni kama : kula gizani ni kula na shetani. Hivyo
basi walijiepusha na kula gizani kwani waliamini sana. Mtu yeyote akila gizani basi akaumwa na
tumbo au akawa mgonjwa kisa na maana alikula na shetani yaani alikula gizani.
Mtu hafai kula ovyo ovyo bila kujali mazingira. Waswahili itikadi yao hueleza kuwa kula kitu
kitamu kinjia njia mtu atasibiwa na shetani yaani ni tabia mbaya na chafu kula wakati
unatembea. Ama mwenye kula miguu ya kuku atakuwa daima katika mwendo tu kwa sababu ni
nyama moto inayojaza hisia kama ngisi ndiposa Waswahili wakaeka itikadi mtu kama huyo
atakuwa na tabia ya kurangaranga.
Ni lazima ja ya ibada kwa kila jambo kumtanguliza Maulana. Waswahili waliamini
kutomtanguliza Jalali katika maakuli basi ni kosa adhimu. Wao huamini mtu akila bila ya kupiga
Bismillahi basi baraka itaondoka na mtu hataweza kushiba.Na isitoshe hata mgeni akija ghafla
wakati wa chakula na hakuna aliyepija Bismillahi basi chakula hakitatosha na italeta izara baada
yake.
3
Sote tunaamini ubadhirifu kwa jambo lolote lile halifai. Waswahili walikuwa na itikadi ya
kuukomesha ubadhirifu na israfu kwa kuwa na itikadi ya ukikanyaga chakula makusudi utasibika
na maradhi ya matende (elephantiasis). Ni ada kukataza watoto haswa kula sufuriani kwa sababu
hudhihakiwa kuwa harusi yakoitanyesha. Maneno haya yamesadikishwa na Waswahili na
wakaamini kwamba mwenye kuzowea kula ndani ya chungu basi atapata mvua kubwa siku ya
harusi yake.
Lingine ni kunywa maji msalani mtu huwa mwongo. Iwapo mtu ana mazoea ya kudangaya basi
Waswahili huamini mtu huyo amekunywa maji msalani kwa sababu wakaazi msalani ni ma jini.
Wao majini ndiyo husababisha mtu kudangaya akinywa maji msalani. Eti wamekunywesha maji
hayo ndiposa ukawa na tabia ya kudanganya. Aidha, Kwa mwanadamu kuwa na afya bora ni lazima
achunge usafi. Hii ni kwa sababu maradhi mengi husababishwa na kutotilia maanani usafi wa vyakula na
vinywaji ndiposa Waswahili wakakataza kunywa maji ndani ya kata pasi na kuikung’uta. Hii ni kwa
sababu huenda maji yale yakawa na wadudu na kusababisha maradhi yasiyo na tiba.
Bundi ni ndege mweusi anayeonkana sana sana wakati wa usiku.Waswahili wanaamini bundi
akilia juu ya nyumba anatangaza kifo cha mtu katika nyumba hio. Pindi mtu anapomwona bundi
basi ni bora kujiepusha na pahali hapo ili asije akafa yeye. Aidha watu wazima katika jamii ya
waswahili ni watu wanaopenda mavazi ya kikoi ambamo ndani ya kikoi ni aghalabu kwa mtu kuvaa
suruali ya ndani ndiposa wakatoa ilani kali kwa wenye tabia ya macho makali kwa kuashiria kuwa
kumchungulia mtu mzima aliyekaa uchi kunaleta upofu.Hapa si ule upofu wa macho bali ni kukosa
nuru ya macho kama kuto ona vizuri.
4
Kushona nguo mwilini kunaleta ufukara; tabiahii aidha inajongeza kifo, maana inakuwa kama
mtu anajishonea sanda yake mwenyewe.Na ni kupitia kwa itikadi kama hizi Waswahili
waliepuka sana hata kushona nguo kwa cherehani kwa sababu waliamini hio ndio sababu
mwafaka ya kujitafutia jongomeo.
Ulishuhudia wapi binadamu akitembea kwa kiatu kimoja kama sio kurukwa na akili? Waswahili
katika itikadi zao waliamini kutembea hali ya kuwa mtu amevaa kiatu kimoja tu kunavimbisha
ziwa la mama wake. Je ni nani leo atakaetaka kumwadhibu Mama mlezi wake? Ni jambo adhimu
ambalo ni itikadi ya Waswahili.
Karne hii ya sasa twanywa maji kwa kutumia mageleni huku tukisahau mitungi na vyungu. Basi
kuanzia leo fahamu kuwa mtu akinywa maji usiku pasi na kuufunika mtungi wa maji, usiku roho
yake itaingia ndani ya mtungi na iwapo atatokea mtu akaufunika huo mtungi wakati uo huo, basi
atakufa papo hapo.Hii ni itikadi kali iliyo na msingi wa mtu kuwa mwangilifu wakati wowote
anapotumia kifaa chake.
Wageni ni Baraka kama tujuavyo. Iwapo leo utafikwa na sisimizi wengi nyumbani kwako basi
fahamu kuwa utabahatika na wageni kwako. Waswahili wana itikadi kuwa iwapo mtu ataona
chunguchungu ama sisimizi ukutani basi atafikiwa na wageni wa ghafla.Hii ni ishara kwa
mwanadamu apate kujitayarisha kuwalaki wageni hao.
Ni watu wengi ulimwenguni hukoga kabla ya kulala. Je, ushawahi kujiuliza kwa nini? Kwa
sababu Waswahili wanaamini Kwenda kulala pasi na kuosha miguu, basi hiyo miguu italazwa
katika moto wa Jahannam. Mtu akilala pasipo kuosha miguu, nyayo zake zitarambwa na
shetani.Na hii ni ishara mtu huyo ni mchafu na shetani anapenda uchafu.
5
Pia mtu akifagia usiku ati anafukuza baraka katika nyumba yao. Je kitu cha sukari kikimwagika
hatutasafisha ili tusifukuze baraka? Lakini cha kustaajabisha sana ni kuwa itikadi za Waswahili
hutokea kweli kwa kila anayeamini kwa sababu ni taasisi ilyokokotezwa katika jamii yao.
Kuchanganya mikasa katika jamii ni jambo lianloepukwa sana na Waswahili katika itikadi zao
wakakataza watu kukusanya taka za chumba kimoja na kupeleke chumba kingine hii ni kwa
sababu huko ni miongoni mwa sababu zitakazo changia kuongeza na kuleta matatizo wakati
mmoja. Vilevile, Kuuza chumvi usiku ni nuksi kwa mwenye duka.Hii ni itikadi iliyo nzito
kufahamika katika fahamu zetu za kileo.
Aidha, watoto wamehusishwa sana katika itikadi za Waswahili. Nilipokuwa mdogo nilikanywa
kuchezea moto wa koroboi na wala sikufahamu maana yake na la kustaajabisha usiku wake
nilijipata nimeamka huku nikiwa nimelowa mikojo. Waswahili waliamini katika itikadi zao
kuwa mtoto mwenye kuchezea kivuli chake cha taa atakojoa kitandani na hili mimi nakubaliana
nalo mia kwa mia. Isitoshe, mtoto mchanga akiachwa peke yake, atageuzwa na shetani.
Inaaminika na jamii ya Waswahili kuwa Shetani yupo kila sehemu haswa sehemu ambazo hazina
watu ndiposa tunakanywa tusiwaache watoto wachanga pekee yao. Si ajabu ukaona watoto
wengi wa karne hii na majivuno mengi kwa sababu Waswahili wanaamini itikadi zao kuwa
kumbusu mtoto usingizini kunasabibisha mtoto huyo kuwa na majivuno ukubwani mwake. Hizo
ni baadhi za itikadi zinazohusishwa na watoto.
Aidha, kuna sehemu ya nyumba ijulikanayo kama Kizingiti. Sehemu hii ina athari kubwa katika
itikadi za waswahili kwani wao huamini kwamba Mwenye kufanya mazowea ya kukaa
kizingitini atakawia kuoa. Hii ina maana kuwa mtu huyo anawaza zaidi ya yanayotarajiwa na
atapoteza muda tele hao kizingitini bila kunufaika. Isitoshe ya kuoa, mja mzito pia atakapokukaa
6
kizingitini basi kutasababisha mwanae kuzaliwa kuchelewa kuliko ule muda uliyotarajiwa na
Wauguzi.Mbali na hayo, Kula wima kizingitini, mtu atapigwa dafrau na shetani. Hii ni kwa
sababu kizingiti sio mahali sahihi kupata chakula.
Hitimisho
Waswahili wana itikadi na mila nyingi sana tofauti. Katika kitabu cha Mbaabu anamalizia sura
ya mwisho wa kitabu chake na maneno haya: `Itikadi ... zina mafunzo mengi yanayostahili
kuhifadhiwa na kuzingatiwa ' (uk.49).
7
MAREJELEO
 Abeid K.A. 1965. Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri. Dar
es Salaam: East African Literature Bureau.
 Akida H. 1977. Utamaduni,matumizi na misingi ya lugha ya Kiswahili.
MULIKA 11, kur. 9-18.
 Chiraghdin S. 1974. Kiswahili na Wenyewe. Kiswahili 44:1, kur. 48-53.
 Chum H. Utamaduni wa Watu wa Wilaya ya Kusini-Unguja. (Mswada
unaotayarishwa kutolewa kitabu, Mhariri Dkt. T.S.Y. Sengo).
 Mbaabu I. (Mhar.) 1985. Utamaduni wa Waswahili. Nairobi: Kenya
Publishing & Book Marketing Co. Ltd.
 Mwinyihaji, Esha Faki (2001). “The Contribution of Islam Towards
women Emancipation: A case Study of the Swahili Muslims in
Mombasa District”, Unpublished M.Phil Thesis, Moi University,2001.
 Ndzovu, Hassan Juma (2001). “The impact of Islam on witchcraft and
sorcery among the Adigo community”, Unpublished M.Phil Thesis,
Moi University, pp. 98-99
 Sengo T.S.Y. 1985. The Indian Ocean Complex and the Kiswahili folklore:
The case of Zanzibarian Tale-Performance. Unpublished Ph.D thesis.
Khartoum University

More Related Content

Viewers also liked

Portfolio vchitelya fizichnoyi_kulturi_
Portfolio vchitelya fizichnoyi_kulturi_Portfolio vchitelya fizichnoyi_kulturi_
Portfolio vchitelya fizichnoyi_kulturi_vlad2909
 
CER Protocol Development Next Steps
CER Protocol Development Next StepsCER Protocol Development Next Steps
CER Protocol Development Next StepsMarion Sills
 
02640414.2011.624537
02640414.2011.62453702640414.2011.624537
02640414.2011.624537Jacki Duthie
 
Audience research
Audience researchAudience research
Audience researchRachMedia
 
Implementing Point-of-Care PROMs
Implementing Point-of-Care PROMsImplementing Point-of-Care PROMs
Implementing Point-of-Care PROMsMarion Sills
 
Blam games art outsourcing
Blam games art outsourcingBlam games art outsourcing
Blam games art outsourcingBlam! Games
 
Образование в Финляндии
Образование в ФинляндииОбразование в Финляндии
Образование в ФинляндииYulyane4ka
 
INNOVATIVE LESSON TEMPLATE
INNOVATIVE LESSON TEMPLATEINNOVATIVE LESSON TEMPLATE
INNOVATIVE LESSON TEMPLATERejith Raghavan
 
Наша жизнь
Наша жизньНаша жизнь
Наша жизньulianaVor
 
Wholesale chakra bracelets | universal exports
Wholesale chakra bracelets | universal exportsWholesale chakra bracelets | universal exports
Wholesale chakra bracelets | universal exportsAlakik.net
 

Viewers also liked (15)

Portfolio vchitelya fizichnoyi_kulturi_
Portfolio vchitelya fizichnoyi_kulturi_Portfolio vchitelya fizichnoyi_kulturi_
Portfolio vchitelya fizichnoyi_kulturi_
 
Ijaret 06 10_014
Ijaret 06 10_014Ijaret 06 10_014
Ijaret 06 10_014
 
CER Protocol Development Next Steps
CER Protocol Development Next StepsCER Protocol Development Next Steps
CER Protocol Development Next Steps
 
02640414.2011.624537
02640414.2011.62453702640414.2011.624537
02640414.2011.624537
 
Audience research
Audience researchAudience research
Audience research
 
Implementing Point-of-Care PROMs
Implementing Point-of-Care PROMsImplementing Point-of-Care PROMs
Implementing Point-of-Care PROMs
 
Ijmet 06 09_012
Ijmet 06 09_012Ijmet 06 09_012
Ijmet 06 09_012
 
Blam games art outsourcing
Blam games art outsourcingBlam games art outsourcing
Blam games art outsourcing
 
Образование в Финляндии
Образование в ФинляндииОбразование в Финляндии
Образование в Финляндии
 
INNOVATIVE LESSON TEMPLATE
INNOVATIVE LESSON TEMPLATEINNOVATIVE LESSON TEMPLATE
INNOVATIVE LESSON TEMPLATE
 
Наша жизнь
Наша жизньНаша жизнь
Наша жизнь
 
Ijciet 06 10_001
Ijciet 06 10_001Ijciet 06 10_001
Ijciet 06 10_001
 
Ethnicity
EthnicityEthnicity
Ethnicity
 
At resume
At resumeAt resume
At resume
 
Wholesale chakra bracelets | universal exports
Wholesale chakra bracelets | universal exportsWholesale chakra bracelets | universal exports
Wholesale chakra bracelets | universal exports
 

ITIKADI assigno

  • 1. 1 Utangulizi Kabila lolote ulimwenguni, hutokana na mambo manne yakiwemo jadi, kazi, mji na sifa za watu. Na upande mwingine nayo lugha hutokamana na mazingira maalum ya watu na tamaduni zao. Ikiwa kabila ni desturi na mila za watu, au ni watu walofungamana na kuwa na tabia na nyendo ambazo zitawatofautisha wao na watu wengine, basi waswahili wana mila zao na desturi zao kama makabila mengine ulimwenguni. Kama kwenye maingiliano ya kibinadamu kwa mfano: ndoa, majina, itikadi za pepo na kadhalika, basi liko kabila ila la waswahili lenye mambo kama hayo. Neno itikadi ni istilahi ya kimsingi katika nyugo za kiutamaduni, za fasihi na taaluma zinazohusu filamu. Maana ya istilahi 'itikadi' kiasilia inatokana na maandishi ya mwanafalsafa wa Kijerumani, Karl Marx na mwenzake Friedrich Engels (Abdulla, Mansur na wenzake, 2014). Katika uchanganuzi wao wa kimsingi wa jamii, walifafanua itikadi kama dhana na imani za tabaka tawala katika kipindi maalumu. Dhana na imani za tabaka tawala ndizo hutamalaki taratibu za kuunda fikra, mawazo na mielekeo ya wanajamii kwa ujumla. Kwa hivyo, mfumo wote wa fikra za tabaka tawala ndio unajenga itikadi ya jamii fulani ndiposa tukaona Waswahili wana itikadi na mila tofauti tofauti.
  • 2. 2 Kama tulivyosema hapo awali kuwa itikadi ni taasisi iliyo hai katika tamaduni za jamii zote za wanadamu huku zikiwa zimegawanyika aina kuu mbili za itikadi: itikadi za kisiasa, na itikadi za kiepistemolojia (ni sehemu ya falsafa ambayo inahusu utafiti wa jinsi tunavyojua mambo). Itikadi ya kisiasa ni upangiliaji unaohusu mawazo ya kimaadili na vipi nchi itaendeshwa. Itikadi za kiepistemolojia ni upangiliaji unaohusu mawazo ya kifalsafa, ulimwengu, na jinsi gani watu wanapaswa kufanya maamuzi.Kuna aina nyingi za itikadi. Moja kati ya hizo ni pamoja na Ukomunisti, Usoshalisti, na ubepari ni itikadi kubwa sana za kiuchumi na kisiasa kwa ujumla. Kwa sasa tutaangalia itikadi za Waswahili pekee yake. Waswahili wana itikadi nyingi sana na mifano ni kama : kula gizani ni kula na shetani. Hivyo basi walijiepusha na kula gizani kwani waliamini sana. Mtu yeyote akila gizani basi akaumwa na tumbo au akawa mgonjwa kisa na maana alikula na shetani yaani alikula gizani. Mtu hafai kula ovyo ovyo bila kujali mazingira. Waswahili itikadi yao hueleza kuwa kula kitu kitamu kinjia njia mtu atasibiwa na shetani yaani ni tabia mbaya na chafu kula wakati unatembea. Ama mwenye kula miguu ya kuku atakuwa daima katika mwendo tu kwa sababu ni nyama moto inayojaza hisia kama ngisi ndiposa Waswahili wakaeka itikadi mtu kama huyo atakuwa na tabia ya kurangaranga. Ni lazima ja ya ibada kwa kila jambo kumtanguliza Maulana. Waswahili waliamini kutomtanguliza Jalali katika maakuli basi ni kosa adhimu. Wao huamini mtu akila bila ya kupiga Bismillahi basi baraka itaondoka na mtu hataweza kushiba.Na isitoshe hata mgeni akija ghafla wakati wa chakula na hakuna aliyepija Bismillahi basi chakula hakitatosha na italeta izara baada yake.
  • 3. 3 Sote tunaamini ubadhirifu kwa jambo lolote lile halifai. Waswahili walikuwa na itikadi ya kuukomesha ubadhirifu na israfu kwa kuwa na itikadi ya ukikanyaga chakula makusudi utasibika na maradhi ya matende (elephantiasis). Ni ada kukataza watoto haswa kula sufuriani kwa sababu hudhihakiwa kuwa harusi yakoitanyesha. Maneno haya yamesadikishwa na Waswahili na wakaamini kwamba mwenye kuzowea kula ndani ya chungu basi atapata mvua kubwa siku ya harusi yake. Lingine ni kunywa maji msalani mtu huwa mwongo. Iwapo mtu ana mazoea ya kudangaya basi Waswahili huamini mtu huyo amekunywa maji msalani kwa sababu wakaazi msalani ni ma jini. Wao majini ndiyo husababisha mtu kudangaya akinywa maji msalani. Eti wamekunywesha maji hayo ndiposa ukawa na tabia ya kudanganya. Aidha, Kwa mwanadamu kuwa na afya bora ni lazima achunge usafi. Hii ni kwa sababu maradhi mengi husababishwa na kutotilia maanani usafi wa vyakula na vinywaji ndiposa Waswahili wakakataza kunywa maji ndani ya kata pasi na kuikung’uta. Hii ni kwa sababu huenda maji yale yakawa na wadudu na kusababisha maradhi yasiyo na tiba. Bundi ni ndege mweusi anayeonkana sana sana wakati wa usiku.Waswahili wanaamini bundi akilia juu ya nyumba anatangaza kifo cha mtu katika nyumba hio. Pindi mtu anapomwona bundi basi ni bora kujiepusha na pahali hapo ili asije akafa yeye. Aidha watu wazima katika jamii ya waswahili ni watu wanaopenda mavazi ya kikoi ambamo ndani ya kikoi ni aghalabu kwa mtu kuvaa suruali ya ndani ndiposa wakatoa ilani kali kwa wenye tabia ya macho makali kwa kuashiria kuwa kumchungulia mtu mzima aliyekaa uchi kunaleta upofu.Hapa si ule upofu wa macho bali ni kukosa nuru ya macho kama kuto ona vizuri.
  • 4. 4 Kushona nguo mwilini kunaleta ufukara; tabiahii aidha inajongeza kifo, maana inakuwa kama mtu anajishonea sanda yake mwenyewe.Na ni kupitia kwa itikadi kama hizi Waswahili waliepuka sana hata kushona nguo kwa cherehani kwa sababu waliamini hio ndio sababu mwafaka ya kujitafutia jongomeo. Ulishuhudia wapi binadamu akitembea kwa kiatu kimoja kama sio kurukwa na akili? Waswahili katika itikadi zao waliamini kutembea hali ya kuwa mtu amevaa kiatu kimoja tu kunavimbisha ziwa la mama wake. Je ni nani leo atakaetaka kumwadhibu Mama mlezi wake? Ni jambo adhimu ambalo ni itikadi ya Waswahili. Karne hii ya sasa twanywa maji kwa kutumia mageleni huku tukisahau mitungi na vyungu. Basi kuanzia leo fahamu kuwa mtu akinywa maji usiku pasi na kuufunika mtungi wa maji, usiku roho yake itaingia ndani ya mtungi na iwapo atatokea mtu akaufunika huo mtungi wakati uo huo, basi atakufa papo hapo.Hii ni itikadi kali iliyo na msingi wa mtu kuwa mwangilifu wakati wowote anapotumia kifaa chake. Wageni ni Baraka kama tujuavyo. Iwapo leo utafikwa na sisimizi wengi nyumbani kwako basi fahamu kuwa utabahatika na wageni kwako. Waswahili wana itikadi kuwa iwapo mtu ataona chunguchungu ama sisimizi ukutani basi atafikiwa na wageni wa ghafla.Hii ni ishara kwa mwanadamu apate kujitayarisha kuwalaki wageni hao. Ni watu wengi ulimwenguni hukoga kabla ya kulala. Je, ushawahi kujiuliza kwa nini? Kwa sababu Waswahili wanaamini Kwenda kulala pasi na kuosha miguu, basi hiyo miguu italazwa katika moto wa Jahannam. Mtu akilala pasipo kuosha miguu, nyayo zake zitarambwa na shetani.Na hii ni ishara mtu huyo ni mchafu na shetani anapenda uchafu.
  • 5. 5 Pia mtu akifagia usiku ati anafukuza baraka katika nyumba yao. Je kitu cha sukari kikimwagika hatutasafisha ili tusifukuze baraka? Lakini cha kustaajabisha sana ni kuwa itikadi za Waswahili hutokea kweli kwa kila anayeamini kwa sababu ni taasisi ilyokokotezwa katika jamii yao. Kuchanganya mikasa katika jamii ni jambo lianloepukwa sana na Waswahili katika itikadi zao wakakataza watu kukusanya taka za chumba kimoja na kupeleke chumba kingine hii ni kwa sababu huko ni miongoni mwa sababu zitakazo changia kuongeza na kuleta matatizo wakati mmoja. Vilevile, Kuuza chumvi usiku ni nuksi kwa mwenye duka.Hii ni itikadi iliyo nzito kufahamika katika fahamu zetu za kileo. Aidha, watoto wamehusishwa sana katika itikadi za Waswahili. Nilipokuwa mdogo nilikanywa kuchezea moto wa koroboi na wala sikufahamu maana yake na la kustaajabisha usiku wake nilijipata nimeamka huku nikiwa nimelowa mikojo. Waswahili waliamini katika itikadi zao kuwa mtoto mwenye kuchezea kivuli chake cha taa atakojoa kitandani na hili mimi nakubaliana nalo mia kwa mia. Isitoshe, mtoto mchanga akiachwa peke yake, atageuzwa na shetani. Inaaminika na jamii ya Waswahili kuwa Shetani yupo kila sehemu haswa sehemu ambazo hazina watu ndiposa tunakanywa tusiwaache watoto wachanga pekee yao. Si ajabu ukaona watoto wengi wa karne hii na majivuno mengi kwa sababu Waswahili wanaamini itikadi zao kuwa kumbusu mtoto usingizini kunasabibisha mtoto huyo kuwa na majivuno ukubwani mwake. Hizo ni baadhi za itikadi zinazohusishwa na watoto. Aidha, kuna sehemu ya nyumba ijulikanayo kama Kizingiti. Sehemu hii ina athari kubwa katika itikadi za waswahili kwani wao huamini kwamba Mwenye kufanya mazowea ya kukaa kizingitini atakawia kuoa. Hii ina maana kuwa mtu huyo anawaza zaidi ya yanayotarajiwa na atapoteza muda tele hao kizingitini bila kunufaika. Isitoshe ya kuoa, mja mzito pia atakapokukaa
  • 6. 6 kizingitini basi kutasababisha mwanae kuzaliwa kuchelewa kuliko ule muda uliyotarajiwa na Wauguzi.Mbali na hayo, Kula wima kizingitini, mtu atapigwa dafrau na shetani. Hii ni kwa sababu kizingiti sio mahali sahihi kupata chakula. Hitimisho Waswahili wana itikadi na mila nyingi sana tofauti. Katika kitabu cha Mbaabu anamalizia sura ya mwisho wa kitabu chake na maneno haya: `Itikadi ... zina mafunzo mengi yanayostahili kuhifadhiwa na kuzingatiwa ' (uk.49).
  • 7. 7 MAREJELEO  Abeid K.A. 1965. Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri. Dar es Salaam: East African Literature Bureau.  Akida H. 1977. Utamaduni,matumizi na misingi ya lugha ya Kiswahili. MULIKA 11, kur. 9-18.  Chiraghdin S. 1974. Kiswahili na Wenyewe. Kiswahili 44:1, kur. 48-53.  Chum H. Utamaduni wa Watu wa Wilaya ya Kusini-Unguja. (Mswada unaotayarishwa kutolewa kitabu, Mhariri Dkt. T.S.Y. Sengo).  Mbaabu I. (Mhar.) 1985. Utamaduni wa Waswahili. Nairobi: Kenya Publishing & Book Marketing Co. Ltd.  Mwinyihaji, Esha Faki (2001). “The Contribution of Islam Towards women Emancipation: A case Study of the Swahili Muslims in Mombasa District”, Unpublished M.Phil Thesis, Moi University,2001.  Ndzovu, Hassan Juma (2001). “The impact of Islam on witchcraft and sorcery among the Adigo community”, Unpublished M.Phil Thesis, Moi University, pp. 98-99  Sengo T.S.Y. 1985. The Indian Ocean Complex and the Kiswahili folklore: The case of Zanzibarian Tale-Performance. Unpublished Ph.D thesis. Khartoum University