2. Nami ninayo sauti, bali hawanisikizi,
Hawaruhusu ongea, hata hawaniulizi,
ataka kutoa wazo, na wamenifumba domo,
ami ninayo sauti, bali hawanisikizi.
3. Nikimanisha mi nani, lakini wanidharau,
Sauti yakumba anga, yalia herufi tatu,
Ambayo haimdhuru mtu, wala kumkwaza mtu,
Nami ninayo sauti, bali hawanisikizi.
4. P- bendera yapepea, A- ni mnara wa furaha,
Z- njia inayokuja, inayoenda hewani,
Kutoka nyumbani kwako, hadi kwangukukutana,
Nami ninayo sauti, bali hawanisikizi.
5. Amani imetoweka, sababu ya dharau,
Hili nimelifikiri, nipeni muda nisema ,
Na sasa nalihubiri, alifahamu kila mtu,
Nami ninayo sauti, bali hawanisikizi.
6. Dharau imekithiri, tufumbue macho yetu,
Shairi limeshamiri, name nawaambia watu,
Wale wenye kudharau, si wanyama au watu,
Nami ninayo sauti, bali hawanisikizi.
7. Kalamu twaweka chini, wino umetuishia ,
Shukrani zetu pokea, kwa uchache wa shairi,
Nami nawaambieni, kosa sauti hatari,
Nami ninayo sauti, bali hawanisikizi.