Kongamano

905 views

Published on

0 Comments
0 Likes
Statistics
Notes
 • Be the first to comment

 • Be the first to like this

No Downloads
Views
Total views
905
On SlideShare
0
From Embeds
0
Number of Embeds
1
Actions
Shares
0
Downloads
3
Comments
0
Likes
0
Embeds 0
No embeds

No notes for slide

Kongamano

 1. 1. Mwanza Press Club MDAHALO WA WADAU WA HABARI KUHUSU KATIBA Hali ya sasa kimaadili katika tasnia ya habari Na Denis MpagazeTR. 14. 1. 2012Denis Mpagaze (denis_mpagaze@yahoo.com, +255753665484 ) ni mhadhili na mharirimsaidizi wa jarida la kitaaluma liitwalo African Communication Research katika Chuo Kikuucha Mtakatifu Agustino. Pia anafundisha na kufanya utafiti katika mambo ya maadili yauandishi wa habari
 2. 2. UtanguliziUkweli unabaki palepale kwamba tasnia ya habari ni tasnia yenye umuhimusana kuliko tasnia nyingine zote hapa Duniani na Mbinguni. Ni tasniaambayo inamchango mkubwa katika kumsaidia mwanadamu kuyatawalamazingira yake kwa sababu mtu hawezi kupanga mipango pasipokuwa nahabari. Na anayetegemewa kutoa habari makini ni mwandishi wa habari.Ndiyomaana leo hii wasomi kwa wasiosoma, walimu kwa wanafunzi,wafanyabiashara kwa wakulima, vijana kwa wazee, wakubwa kwa wadogo,mapadri kwa masista hutegemea tasnia ya habari kufahamu nini kimejirindani na nje ya nchi yao. Ukitaka kuamini ninachokiongea hapa piga pichaleo hii unaamka asubuhi hakuna gazeti, televisheni na redio. Nini kitatokea?Patakuwa hapatoshi kama wasemavyo waswahili. Napenda kutumia nukuuya mtaalam mmoja kutoka kitivo cha sayansi ya jamii katika chuo kikuu chaColumbia, bwana Walter Williams katika kuelezea umuhimu wa Tasnia yahabari: Mbinguni hakutakuwa na uhitaji wa mwanasheria au wakili kwa sababu huko hakutakuwa na kesi yoyote, wala hakutakuwa na uhitaji wa madaktari kwa sababu hakuna kuugua. Pia Mbinguni hakutakuwa na polisi wala askari kwa sababu huko ni amani na upendo. Hakutakuwa na maafisa uhamiaji kwa sababu watu watakuwa na viza za kudumu. Lakini mbinguni kutakuwa na uhitaji wa Mwandishi wa habari kwa sababu upande mmoja wa Mbinguni watahitaji kujua nini kinaendelea katika upande mwingine wa Dunia1 1 In heaven there will be no need for lawyers or magistrates, for the people will not be involved in any court cases - there will be no need for doctors because the people will not be sick. Also, in heaven, there will be no need for policemen because the people will be peaceful and orderly. In heaven there will be no need for immigration and customs officers because each resident of heaven will have permanent and multiple visas for free movement of goods and people. In heaven there will not be any need for the politician because there will be no politics…But in heaven there will be need for journalists and the press because the people living in the Western part of heaven will want to know what happens to their counterparts in the Easter part of heaven. So also will the people living in the Southern part of heaven want to know what happens to their counterparts in both the North, East or Western parts of heaven.
 3. 3. Pamoja na umuhimu mkubwa wa tasnia ya habaria kwa jamii bado imebakikukosa heshima miiongoni mwa wanajamii waliowengi kama ilivyo tasniaya sheria na nyinginezo. Kwa kweli ni taaluma ambayo ukijatambulisha kwawanajamii leo wataonesha kila aina ya kutokuwa na imani na wewe.Kunamsemo wa kwamba count your words before journalists. Maana yamsemo huu ni kwamba unatakiwa kuwaa makini na mwandishi wa habarikwani anaweza kubadilisha yale uliyoyaongea na kuripoti ya kwake.Vijana wengi hawanamvuto wa kwenda hata kusomea taaluma hii ya habarina hata wale wanaoisomea wengi wanaishia kufanya kazi katika tasnianyingine. Utafiti uliofanywa kwa mara ya mwisho na profesa wamawawasiliano, Robert White ulionesha kwamba wanafunzi waliokuwawanafanya vizuri darasani katika uandishi wa habari wameishia kuajiriwakama bank tellers. Leo hii wanafunzi wengi katika tasnia hii hawana ndotoya kuwa waandishi kabisa, wengi wanafikiria kuwa maafisa uhusiano(PublicRelations Officials).Kwa nini?Ni ukweli usiofichika kuwa tasnia ya habari imekuwa ikilaumiwa kwa kilakitu kibaya kinachotokea katika jamii. Wanasiasa wanalalamika kwambawaandishi wa habari wanawachafua, kwamaana kwamba wanawaandikakinyume cha matakwa yao. Vile vile wasamii ndio kabisa kila siku wanaliana waandishi wa habari kwamba wanawadhalilisha. Serikali ya Tanzaniaimefikia hata hatua ya kutumia nguvu ya dora kuwaadhibu waandishiwanaoonekana kukiuka matakwa ya serikali.
 4. 4. Madhumuni mahsusi ya kazi hiiSasabasi lengo la kazi hii nikuripoti utafiti mfupi juu hali ya sasa kimaadilikatika tasnia ya habari Tanzania. Kama tunavyofahamu walio wengi maadiliya uandishi wa habari ni vigezo na mwenendo mzima katika utekelezaji wawa kazi ya taaluma ya uandishi wa habari. Mtaalamu wa mambo ya habarihayati Francis Kasoma anasema kwamba, maadili ya uandishi wa habarilazima yaambatane na maadili ya jamii husika. Kwa maana hiyo basi katikanchi zetu za Kiafrika Kasoma anasema maadili yajikite katika Afri-ethics.Msingi mkubwa wa maadili ya kiafrika ni kumthamini mtu ndani ya jamii (Iam because we are). Tanzania kama moja ya nchi za Afrika hainabudi kuwana tasnia ya habari ianayoendeleza mazuri yaliyomo katika jamii.Kwahiyo mwandishi yeyote atakayekwenda kinyume na maadili ya kiafrikabasi atakuwa amekiuka misingi ya taaluma yake, hivyo ni jukumu lawanajamii kumkanya na kujirekebisha. Kwa sababu mtu mmoja anauwezowa kuchafua familia nzima (SAMAKI MMOJA AKIOZA WOTE WAMEOZA) nifalsafa ambayo inaongoza maadili ya kiafrika.Tathmini kutoka kwa mlaji wa habari TanzaniaKimsingi ili ujue tabia yako unatakiwa kuwauliza wanaokufahamu na siyokujiuliza mwenyewe. Leo hii ukimfuata mwandishi yeyote wa habari naukamuuliza aseme juu ya maadili ya habari haitakuwa rahisi kukupa ukweli.Sana atavutia upande wake kwamba anafanya vizuri. Sasa mimi kamamwanataluma ili kuondoa vionjo vyangu binafsi suala hili niliwaanchiawalaji wa habari wafanye tathmini hii. Kutokana na ufinyu wa muda wakuandaa mada hii (nimepewa siku tatu) niliamua kutumia moja ya mitandaoya kijamii yaani Face Book katika kukusanya maoni ya wanajamii juu ya hali
 5. 5. ya sasa kimaadili katika tasnia ya habari. Ilikuwa rahisi kutumia Face Bookkwa sababu inarahisisha kufahamu nani yuko hewani kwa wakati huo nakumuomba atoe maoni yake. Mpaka asubuhi ya leo washiriki 55wamejitokeza katika kutoa maaoni juu ya maadili ya tasnia hii kwa sasa.Wachangiaji wote wameoneshwa kutofurahishwa na mwenendo mzima wavyombo vya habari Tanzania kwa kukiuka maadili yao. Sifaeli E. Muddyanasema: Wengi wa waandaji wa habari,wameingiza hisia binafsi katika uandaaji wa vipindi, hasa hasa hisia za ushabiki wa kisiasa.. ikiwepo na ushabiki wa wamiliki.. utakuta kama chombo kinamilikiwa na serikali ,siku zote habari zitakuwa zinakipamba chama tawala na kuficha yale mabaya, mfano mzuri juu ya hilo, ni miezi kadhaa iliyopita, chombo kimoja kikubwa cha habari kilimtimua kazi mkurugenzi kisa kurusha habari ambazo zinaponda wamiliki wake.. kwa maana hiyo maadili ya habari yanakiukwa sana ndani ya nchi yetu.Omar Suleiman yeye anasema kwamba maadili yakochini hasa ukizingatiavyombo vingi vya habari viko kiushabiki, kwa maana ya kwamba kama kunakitu au mtu anapendwa na mwandishi au chombo cha habari fulaniataandikwa au atatangazwa kwa kupambwa hata kama hafanyi mema.Kwa kawaida maadili katika tasnia hii yanajieleza wazi kwamba mwandishihatakiwi kuonesha aina yoyote ya ushabiki wala kuegemea katika upandewowote.Mwandishi mzuri ni yule asiyeonesha chembe hata moja ya hisiazake anapokuwa kazini.Utafiti wangu pia unaonesha jinsi gani wanajamii wamefikia hatua hata yakuwanawasiwasi kama kweli Tanzania tunawaandishi wa habari au la.Bryan Majenga anasema: Mie naona hivi kuna waandishi na watangajazi katika taaluma ya habari ... Lakini Tanzania kwetu kuna wadaku na wazungumzaji !
 6. 6. news values hazizingatiwi ! Mapresenters badala ya Kupresent wana zungumza nonsense.Hapa Bryan anafahamu kabisa mwandishi bora atajikita katika maadili yakena anapopotoka anashindwa kuamini kama kweli amepitia taaluma hii yauandishi wa habari ingawa kujua sio kutenda. Mtu anaweza kuwa amesomavizuri kabisa lakini sababu ya mazingira flani anashindwa kufuata yalealiyofundishwa.Kutokana na utendaji kazi usioiridhisha jamii, utafiti wangu anaoneshakwamba waandishi wa habari kubatizwa majina mengi ya kuudhi kama vilekanjanja, mdaku, mmbeya, tapeli, muongo na mengine mengi. FredrickStanley anasema: maadili ya vyombo vya habari sio mazuri sana we fikiriampaka kuna magazeti yanaitwa ya udaku,unafikiria nini kitachoandwikwahapo?.Utafiti pia unaonesha kwamba tasnia ya habari imekosa dira baada ya kuwaimeacha kufuata maadili yake. Pius Maro anasema: Vyombo vya habari havina dira kwani vinakwenda na matukio.Wanatupa kile wanachotaka wao na sicho tunachotaka sisi. Hakuna uchambuzi wa kina juu ya uchumi bali vimebaki kuwa vyombo vya habari vya matukio. Unaweza kupata kichaa ukiendelea kufuatilia vyombo vya habari vya Tanzania.Mdashiru anasema tatizo la vyombo vyetu vya habari vimekuwa vikilindamaslahi ya wamiliki badala ya kujikita katika kuisaidia jamii kwa ujumla.Swali la msingiHivi, kunauhalali wowote kwa tasnia ya habari kubeba tuhuma hizo? Kamajibu ni ndiyo Je, mambo hayo waandishi wa habari wanayafanya kwamakusudi au ni kutokujua maadaili ya habari? Inafamika kabisa maadili yawaandishi wa habari ni kutekeleza yale ambayo tasnia yake humtaka
 7. 7. kutekeleza. Kama tunavyojua bila kujali mwandishi anatokea chombo gani,Duniani pote msingi wa maadili ya uandishi wa habari ni kumsaidiamwananchi kupata taarifa muhimu ili aweze kuyatawala maisha yake. Sasabasi mwandishi anapoonekana kushindwa kutekeleza hayo anakuwakinyume na taaluma yake na matokeo yake ni kudharauliwa na jamiiinayomzunguka. Kwa mfano unategemea nini pale chombo cha habarikutetea maslahi ya watu wachache na kusahau ya watu wengi? Mchangiajimmoja, David Secha anasema vyombo vya habari sasa vimekuwa na tabia ya kuhubiri yale yaliyo mazuri hususani mjini na kusahau vijijini ambako asilimia 80 ni wakulima duni wasio na jinsi ya kujikwamua kiuchumi.Prosper Mwitinda anasema waandishi wamekosa ubunifu katika kufanyakazi yao, na badala yake wanakaa tu mijini wakisubiria wapate habaribadala ya kuzunguka maeneo mbalimbali kutafuta habari ambazo jamiiinatakiwa kupata.Ni jambo la kushangaza kwa baadhi ya vyombo vya habari kugeuka nakuwa wasemaji wa wanasiasa wachache tena wale wanaopatikana mijini tu.Mbaya zaidi ni pale ambapo baadhi ya vyombo vya habari kugeuka na kuwauwanja wa mapambano ya wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa. Leo hiikunamajina ya watu haipiti siku hujayasikia katika vyombo vyetu vya habariwakioneshwa ubaya wao. Hapa mchangiaji mmoja anasema. “medianyingine zinaandika habari kwa kuchafua tu bila hoja za msingi”. ProsperMwitinda anasema: The journalists of nowadays write news which are beneficial to particular people or group of people BUT not for the whole majority. Utakuta mwandishi anapewa kifuta jasho sisi wasomi tunaita "Brown Envelope ili andike story fulani kwa ajili ya watu fulani, this is UNETHICAL.
 8. 8. Chukizo kwa jamii?Pengine wananchi wanatuhumu vyombo vya habari kwa kuchafua maadiliya kitanzania. Kwa mfano ni ukweli usiopingika kwamba hivi karibunikunavituo vya redio na television vimekuwa vikitangaza matangazo yakikundi kimoja cha taarabu kijulikanacho kama KANGA MOKONDEMBENDEMBE-LAKI SI PESA. Sio utamaduni kabisa wa mtanzania kuvaanguo zinazooenesha viungo vya ndani. Utafiti wangu unaonesha watuhawajafurahishwa kabisa na mwenendo huu na kutupa lawama kwa tasniaya habari kwa kueneza utamaduni huu. Neema Emmanuel Sway kuhusukikundi hiki anasema: Sometimes media ziwe zinachuja vitu vya kupresent kwa audience. Leo wadogo zetu wanajifunza nini kwao? Kwani wana tofauti gani na wanao cheza uchi? Alafu wanahitaji kuheshimiwa eti wapo kazini nani atakueshimu ikiwa mwenyewe haujieshimu? Media hazifikirii watoto wanajifunza nini wao wanawaza kupata hela tu..hawatambui kama wanaharibu society yao? Ingekuwa amri yangu hawa kanga moko ningewafunga miaka 30 kwa kuharibu jamii kwa makusudi. kumbuka media zina power zaidi ya kuharibu na kutengeneza zingekuwa zina wakritisaizi wasingefika mbali lakini siku hizi kanga moko imekuwa slogan Tanzania. Eti laki si pesa kama ingekuwa si pesa wange cheza uchi?Picha tunayoipata hapa ni kwamba baadhi ya vyombo vya habari vimekuwavikihabarisha umma kama vile vyenyewe siyo sehemu ya umma.Vinashindwa kuelewa leo jamii inapoharibika navyo vitaathirika. Kwamfano Kikundi hiki kwa namna moja au nyingine kineweza kuchochea hamuya kufanya ngono miongoni mwa wanajamii na watu wengi kuishiakuathirika na gonjwa la UKIMWI. Sasa basi serikali itajikuta ikitumia pesanyingi kwa kuwahudumia waathirika amabazo zingetumika kujengabarabara. Katika taaluma ya Management tunasema waandishi wa habariwanaongozwa na kanuni ya WIN-LOSE GAME badala ya WIN-WIN.
 9. 9. Wachangiaji, Bunigini Willy na David Secha wanasema kwamba maadili yavyombo vya habari hushuka siku hadi siku kutokana na kuweka masilahimbele kuliko utu hii inatokana na vyombo vingi kumilikiwa na tabakatawala kwani wao ndio wana amua kipi kisikike na kipi kisisikike.Deogratias Konyani anasema: kwa upande wa maadili, hasa kwa upande wa print media! Wanafikiria sana kuuza kuliko uzito wa yale wanayoyatoa kwa jamii wakisahau kuwa hata watoto wao wanaathirika na habari hizo maarufu kama "udaku" hatukatai, kuburudika kupo lakini si kuonyesha kwa picha wazi watu waliofumaniwa, walio kwenye kumbi za burudani, fukwe za mahoteli nk. mfano, itaburudisha na kusisimua kwa wapenda udaku kuona msanii/kiongozi au mtu maarufu kafumaniwa gest na mke wa mtu tena na picha wazi zikiwaonesha wapo kwenye mikao ya aibu lakini ki mantiki haijengi na ukizingatia ni nchi yenye matatizo lukuki ya kuzungumziwa!Kinachowashangaza zaidi wanajamii ni pale ambapo hata chombo chahabari cha Taifa kinapokuwa katika mrorongo wa kuharibu maadili ya jamii.Yacny Senge anasema: Leo hii hata TBC1 wanarusha sebene linalooneshamdada akidansi nusu uchi mchana tunakula...! Tv ya taifa haichuji maadili?Bwana Fredrick Stanley anasema: kuna television nyingine zinaoneshamovie au miziki ambayo kama umekaa na wazazi wako au dada zakoutaondoka mwenyewe. Sio utamaduni wetu bwana lazima tutunzeutamaduni wetu.HitimishoPamoja na utafiti wangu kuonesha kwamba hali ya maadili ya sasa katikatasnia ya habari hairidhishi bado nabaki kuamini kwamba maadili yauandishi kwa sasa ni mazuri isipokuwa wapo waandishi wachache tena sanatu wanaoipaka matope tasnia hii. Hili halikwepeki kwani falsafa yetu yawatu wa Afrika tunaamini kabisa SAMAKI MMOJA AKIOZA WOTEWAMEOZA. Ndiyomaana hata katika familia zetu mtu mmoja akifanya
 10. 10. mambo ya aibu katika jamii familia yote itachafuka. Sasa basi tasnia yahabari kama familia tunatakiwa tuwe kitu kimoja, tupendane na tuhakikishepale mwenzetu anapokosea tunarekebisha. Kwa kufanya hivyo tutarejeshaheshima ya taaluma yetu ya habari kwa jamii. Rafiki mzuri ni akuoneshaye mapungufu yako Asnteni kunisikiliza

×