HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDARISALA ILIYOSOMWA NA ENG TANU DEULE, MHANDISI WA MAJI WA WILAYA YABUNDA KWENYE SIKU YA KILEL...
Mh. Mgeni RasmiTarehe 22 Machi kila mwaka ni siku ya Maji Duniani. Maji ni uhai, na upatikanaji wamaji ni chachu ya maende...
utekelezaji wa malengo ya MKUKUTA, Malengo ya Milenia (MDGs) na Dira ya Taifaya Maendeleo (Development Vision 2025)Mh. Mge...
•  Mapato kwa mwaka yamekuwa kutoka 20,246,311(2006) hadi 74,184,663 (2010)•  Mamlaka imepunguza maji yanayopotea Unacco...
iii. Nyumba ya kufunga pampu (Pump House)      iv. Nyumba ya wahudumu wa pamp (pump attendant house) na choo yake  ...
Musoma kwaniaba ya Wizara ya Maji na kwa upande wa Halmashauri wapo Mamlakaya Maji ya Bunda.Mh. Mgeni Rasmichangamoto zina...
•  Ofisi ya Mkuu wa wilaya kusaidia namna ya kudhibiti hujuma na kwa Kutumia  vyombo vya dola kama vile Mahakama, Polis...
Mh mgeni RasmiKabla ya kumaliza napenda kuzungumzia jambo la UKIMWI. Tukumbuke ukimwihaubagui mtu mwenye maji wala yule as...
Upcoming SlideShare
Loading in …5
×

Risala kilele wiki ya maji by Eng Deule, tanu

784 views

Published on

Speech ready by Eng Deule, Tanu at the Climax of Water Week, the World Water day on 22nd March 2011 at Tairo Primary school grounds in Bunda Township

Published in: Education
0 Comments
0 Likes
Statistics
Notes
 • Be the first to comment

 • Be the first to like this

No Downloads
Views
Total views
784
On SlideShare
0
From Embeds
0
Number of Embeds
2
Actions
Shares
0
Downloads
3
Comments
0
Likes
0
Embeds 0
No embeds

No notes for slide

Risala kilele wiki ya maji by Eng Deule, tanu

 1. 1. HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDARISALA ILIYOSOMWA NA ENG TANU DEULE, MHANDISI WA MAJI WA WILAYA YABUNDA KWENYE SIKU YA KILELE CHA WIKI YA MAJI KATIKA KIJIJI CHA TAIRO TAREHE 22-MACHI-2011Mh. Mgeni RasmiWah. Viongozi mliofika hapa wa chama na serikaliKaimu Meneja wa Mamlaka ya Maji Bunda Mr Jumanne TurbetWafanyakazi wa Mamlaka ya Maji BundaWafanyakazi wenzangu wa Idara ya Maji ya Halmashauri ya wilaya ya BundaWafanyakazi wenzetu wa Halmashauri mliofika hapa kutuunga mkonoUongozi mzima wa Shule ya Msingi TairoNdugu zetu waandishi wa habariWananchi Mabibi na mabwanaTumsifu Yesu KristuAsalam aleykumAwali ya yote naomba kumshukuru mwenyezi Mungu, kwa kutujalia pumzi, afya nanguvu ya kusherehekea kilele cha wiki ya maji hapa Wilayani kwetu. Siku ya leo nimhimu kwasababu ni siku ya maji duniani kote yaani “World Water day”.Ninayofuraha kubwa kupata fursa ya kuadhimisha wiki ya maji katika kijiji hiki kwanini nafasi nzuri ya kuzidi kufahamiana na wanajamii ambao ndio wadau mhimu wausalama na uendelevu wa miundombinu yetu ya maji ya Mjini Bunda.
 2. 2. Mh. Mgeni RasmiTarehe 22 Machi kila mwaka ni siku ya Maji Duniani. Maji ni uhai, na upatikanaji wamaji ni chachu ya maendeleo kwa kila mwanajamii.Hii ndiyo sababu kuu taifa letukuadhimisha wiki ya maji kwa nia ya kutathimini hali ya upatikanaji wa huduma yamaji na usafi wa mazingira na kujiwekea mikakati ya kuboresha upatikanaji wa majisafi na salama.Wananchi wa Wilaya ya Bunda leo wanaungaana na taifa zima kuadhimisha kilele chawiki ya maji. Wiki iliyozinduliwa tarehe16/3/2011 Jijini Mwanza na Waziri wa Maji,Prof Mark Mwandosya (MB). Tangu mwaka 1988, maadhimisho haya ya wiki ya maji niya 23 na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Maji kwaajili ya Miji: kukabiliana nachangamoto mbalimbali Mijini”Kauli mbiu ya mwaka huu inagusa maji mijini na changamoto zake. Miji inayotajwakatika kauli mbiu hii ni pamoja na mji wa Bunda. Na hapa utaona maadhimisho yawiki ya maji mwaka huu yamezinduliwa kwenye viunga vya mjini na yanahitimishwakwenye viunga vya mjini pia.Mh. Mgeni Rasmi,Kuhusu malengo ya MKUKUTA na MILENIA kuhusu utoaji wa huduma ya MajiSera ya Maji ya Taifa ya mwaka 2002 iliweka madhumuni ya kuongeza na kuimarishahali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama toka asilimia 54(2005) hadiasilimia 65 kwa wakazi waishio vijijini, na kutoka asilimia 74 (2005) hadi asilimia 90kwa wakazi waishio mijini ifikapo mwaka 2010. Lengo kuu ilikuwa ni kupunguzaumasikini na kuwa na maisha bora kwa watu wote. Malengo haya yameshindwakufikiwa kwa wilaya ya Bunda kwa sababu mbalimbali na hivyo kuwa nyuma ya 2
 3. 3. utekelezaji wa malengo ya MKUKUTA, Malengo ya Milenia (MDGs) na Dira ya Taifaya Maendeleo (Development Vision 2025)Mh. Mgeni RasmiHali ya huduma ya maji kiwilayaAsilimia 47.7 ya wakazi wa vijijini wanapata maji safi na salama. Vyanzo vikuu vyahuduma ya maji vijinini ni Visima virefu na vifupi, ziwa Victoria, matanki ya kuvunamaji ya mvua, visima vya asili na malambo. Kiwango cha utoaji huduma ya majiwilayani Bunda ni cha chini ukilinganisha na wastani wa kitaifa wa utoaji wa hudumaya maji ambao ni asilimia 58 (2010). Hali hii ni changamoto kwetu kama wilaya na jamiizetu kuhakikisha tunaongeza upatikanaji wa huduma ya maji wilayani Bunda.Mh. Mgeni RasmiKuhusu chombo chenye mamlaka ya kutoa huduma ya maji Bunda mjiniJukumu la utoaji wa huduma ya maji Mjini Bunda lipo chini ya Mamlaka ya MajiBunda yaani Bunda Water Supply Authority. Hii ni Mamlaka kamili iliyoanzishwatarehe 21/6/2002 baada ya kutangazwa kwenye gazeti la serikali. Bodi yake ya kwanzailiteuliwa tarehe 1Juni 2003 na hivi sasa kuna Bodi ya tatu iliyoteuliwa rasmi tarehe 10januari mwaka huu wa 2011.Mh. Mgeni RasmiKuhusu mafanikio ya Mamlaka ya Maji kwa miaka5 iliyopita (2006-2010)• Kiwango cha maji yanayozalishwa kwa siku yameongezeka kutoka lita 720,000 mwaka 2006 hadi liata 1,260,000 mwaka 2010• Wateja wameongezeka kutoka 650 mwaka 2006 hadi wateja1,227 mwaka 2010• Wastani wa watu wenye maji ya bomba wameongezeka kutoka asilimia 22 mwaka 2006 hadi asilimia 27.4 mwaka 2010 3
 4. 4. • Mapato kwa mwaka yamekuwa kutoka 20,246,311(2006) hadi 74,184,663 (2010)• Mamlaka imepunguza maji yanayopotea Unaccountable for Water) toka 75% (2006) hadi 42(2010)• Mamlaka imepata pikipiki 3 na Laptop 1• Kituo cha ushahi kimejengewa Uzio• Tangi la Mgaja limekarabatiwa na Maji sasa yanasukumwa hadi hospitali ya Manyamanyama• Mtandao wa mabomba umeongezwa kutoka 49km 73km hivi sasa• Nyumba ya pampu imekarabatiwa na kujengwa chumba cha wahudumu MgajaMh. Mgeni RasmiKuhusu mradi Mpya wa Maji Bunda MjiniTakwimu iliyoonyeshwa hapo juu kwamba katika watu 100 ni watu 27 tu ndowanapata maji ya bomba inadhihirisha ukubwa wa tatizo lililopo na kwambachangamoto hii ni kubwa sana kwetu. Hivyo basi, Halmashauri kwa kushirikiana naWizara ya Maji na kwa Msukumo wa pekee wa mheshimiwa Mbunge wa jimbo laBunda, Mh. Stephen M. Wasira (MB) na Waziri wa nchi ofisi ya raisi –Mawasiliano naUratibu, tumeanza kutekeleza mradi mpya wa maji hapa Bunda mjini utakaokuwa nachanzo chake kwenye kijiji cha Nyabehu kilichopo umbali wa kilomita 26 kutoka mjini.Mradi huu ni mkubwa na una gharimu fedha nyingi. Mradi umekuwa unatekelezwakadiri fedha zilivyokuwa zinapatikana kama ifuatavyo;Awamu ya I: Zimenunuliwa pampu mpya 9 za kusukuma maji na tayari zipo hapa Wilayani Bunda zimetunzwa kwenye Bohari yetuAwamu ya II: Umefanyika ujenzi wa i. Tengi la maji Migungani lenye ujazo wa lita 225,000 ii. Tengi la kwenye Mlima Kaswaka lenye ujazo wa lita 675,000 4
 5. 5. iii. Nyumba ya kufunga pampu (Pump House) iv. Nyumba ya wahudumu wa pamp (pump attendant house) na choo yake v. Barabara ya kwenda kwenye tengi la maji kwenye Mlima KaswakaAwamu ya II: Awamu hii bado haijatekelezwa lakini itahusisha kazi zifuatazo • Ujenzi wa chujio (treatment plant) • Kununua na kulaza mabomba ya bomba kuu kilometa 26 • Kusimika pampu • Kuingiza umeme wenye msongo mkubwa, na • Kusuka mtandao mpya wa usambazaji maji hapa mjiniMh. Mgeni RasmiAwamu hii ya tatu ndiyo awamu inayohitaji fedha nyingi zaidi kuliko awamuzilizopita. Makisio ya awali yanaonesha kuwa zitahitajika zaidi ya shilingi billion kumi(10Billions) kukamilisha mradi huu kiasi ambacho ni kikubwa ukilinganisha natakribani billion moja ambayo imekwishatumika kwa awamu ya I na awamu ya II.Habari njema ni kwamba, mradi huu sasa utatengewa bajeti kubwa kwenye mwaka wafedha wa 2011/2012 ili ukamilike. Hii pia ilipewa uzito na kauli ya Mh Waziri wa Majitarehe 16/3/2011 kwenye uzinduzi wa wiki ya maji pale alipo thibitishia umma kwakusema, nanukuu “sasa tumedhamiria kuukamilisha mradi wa Bunda natutaukamilisha” mwisho wa kunukuu.Hata hivyo mheshimiwa mgeni rasmi kazi za awali za maandalizi ya awamu hii ya tatuzimeshaanza kufanyika kwani mhandisi mshauri ameshapatikana na anafanya kazi yakuandaa zabuni za ujenzi wa chujio, zabuni za ununuzi na utandazaji wa mabomba yamaji, na anaandaa zabuni za uwekaji umeme wa msongo mkubwa na usimikaji wamitambo. Mradi huu kwa ujumla unasimamiwa na Mamlaka ya Maji taka na Maji Safi 5
 6. 6. Musoma kwaniaba ya Wizara ya Maji na kwa upande wa Halmashauri wapo Mamlakaya Maji ya Bunda.Mh. Mgeni Rasmichangamoto zinazoikabili Mamlaka ya Maji Bunda Mjini; i. Miundimbinu ya maji inahujumiwa kwa bomba kutobolewa na wafugaji wa vijiji vya njiani kwenye bomba kuu ambavyo ni Guta, Tairo na Migungani ii. Uchakavu wa miundombinu ya maji hasa mabomba na mitambo iii. Mamlaka inapoteza maji kiasi cha asilimia 46% kwa mwaka 2010 iv. Kukatika nishati ya umeme mara kwa mara kumesababisha kuunguza pampu zetu za maji na vifaa vyake v. Watumiaji maji kutolipa Ankara zao za maji kwa wakati vi. Maji yanayosukumwa kutokidhi mahitaji ya jamii vii. Ukosefu wa fedha za kulipia Billi ya Umeme kwani ruzuku mara inakuja kidogo au miezi mingine ruzuku haiji kabisa na TANESCO hutishia kukata umeme mara kwa mara. viii. Mwaka 2006 tulikwisha fanya mategenezo ya mabomba mara 253 na hivi sasa tumefikia mara 1,085 kwa mwaka 2010 hali ambayo inaonesha kuwa uhujumu wa miundombinu yetu unazidi kuongezeka badala ya kupunguza.Mikakati inayotumika kukabiliana na changamoto hizi ni kama ifuatavyo;• Ukamilishaji wa mradi mpya wa maji wenye chanzo chake Nyabehu• Kuendelea ukarabati wa miundombinu ya maji kwa kutumia fedha kidogo tunazokusanya kwa wateja kila mwezi 6
 7. 7. • Ofisi ya Mkuu wa wilaya kusaidia namna ya kudhibiti hujuma na kwa Kutumia vyombo vya dola kama vile Mahakama, Polisi na serikali za Vijiji kusaidia kudhibiti hujuma dhidi ya miundombinu yetu• Kuendelea kuiomba serikali kutoa fedha za ruzuku kwa wakati kama ilivyo kwenye bajeti ili shughuli zisikwameTunapenda kutoa rai kwa watumiaji maji kulipia Ankara zao za maji kwa wakati nakuwaasa waepukane na utumiaji wa maji salama kwa Bustani, kuoshea magari n.k Piawasikubali kuchepusha maji yasipite kwenye mita kwani kwa kufanya hivyo ni kosa lajinai na wanaweza kushitakiwa kwa mjibu wa sheria. Wananchi waisaidie Mamlakayao kufichua waovu wanaoihujumu Mamlaka isisonge mbeleAidha tunawaomba Wananchi waendelee kushirikiana na Mamlaka kwa kuwafichuawahalifu wanaotoboa mabomba ili watiwe nguvuni mara moja kwa maana serikaliinaweka nguvu nyingi katika kujenga miundo mbinu hii na sisi hatuna budi kuitunzakwa faida yetu na vizazi vijavyo.Tusipobadili tabia na mazoea yetu kwa hili, sheria sasaitaanza kuchukua mkondo wake.Mh. Mgeni RasmiWazo mbadala juu ya maji safi kwa Mji wa BundaKwakuwa mji wa Bunda unazungukwa na miamba ya mawe kwa eneo kubwa(Impermeable Rocks) ambayo inaweza kutumika kuhifadhi maji hivyo tunafikiriauwezekano wa kuvuna maji ya mvua kwa kuweka uzio wa mifereji ya siment juumilimani ili kukusanya maji ya mvua ya mwaka mzima na kutumiwa na watu kwakunywa n.k kwa njia ya mtiririko bila kutumia nishati ya umeme. Ninayo imani kuwabaadhi ya eneo la mji wa Bunda litaweza kuhudumiwa kwa njia hii. 7
 8. 8. Mh mgeni RasmiKabla ya kumaliza napenda kuzungumzia jambo la UKIMWI. Tukumbuke ukimwihaubagui mtu mwenye maji wala yule asiye na maji,tajiri wala masikini, mnene wala,mwembamba, mrefu au mfupi, sura nzuri au mbaya. Ndugu zangu mimi na wewe“Tubadilike tabia, ukimwi unaua napengine njia ya kujikinga na ukimwi ni kuaminikuwa kila mtu anao na tujiepushe na ukimwi, hauna dawa. Ukiwa mbishi dhambizako mwenyewe.Mh. Mgeni RasmiMwisho naomba kwa ridhaa yako nitumie fursa hii kukushukuru wewe binafsi kwakukubali mwaliko wetu. Pili niwashukuru kwa namna ya pekee wenzetu wa Mamlakaya Maji Bunda kwa kufanikisha shughuli hii ya kilele cha wiki ya Maji hapa wilayanikwetu Bunda. Niwashukuru watumishi wa idara ya maji kwa ushirikiano waokufanikisha shughui hii na pia niwashukuru kwa namna pekee waandishi wa habariwa televisheni, Magazeti na redio waliofika hapa.Maji ni Uhai na Usafi wa Mazingira ni UtuSiku ya Maji Duniani HoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeAksanteni kwa kunisikiliza 8

×